Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA

$
0
0
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, SACP Ahmed Msangi

WANAFUNZI WAWILI KURUKA NA PIPA KUSHUHUDIA MASHINDANO YA TAFITI ZA SAYANSI NCHINI IRELAND

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

TAASISI ya Karimjee Jevanjee imetoa ufadhili kwa wanafunzi wawili wanaokwenda kushuhudia tafiti mbalimbaliza kisayansi zinazofanywa na wanafunzi wa Dublin nchini Ireland.

Wanafunzi wawili hao walishinda katika mashindano ya wanasayansi chipukizi yaliyofanyika Agasti mwaka jana ambayo yaliratibiwa na Young Scientist Tanzania (YST).Walioshinda mashindano hayo ni  wasichana wa Shule ya  Sekondari ya Wasichana ya  Mtwara ambao ni Diana Sosoka pamoja na Nadhira Mresa.

Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Karimjee Jivanjee Foundation, Yusuf Karimjee amesema wanatoa ufadhili huo kwa kutambua mapinduzi ya uchumi yanahitaji wanasayansi.

Amesema kushuhudia mashindano ya tafiti za Sayansi itawaongezea kuboresha miradi yao walioifanya katika mashindano walioyafanya Agasti mwaka jana.Yusuf amesema wanafunzi hao watapata ufadhili wa masomo ya elimu ya juu pindi watakapohitimu kidato cha sita.

Nae Mkurugenzi wa Young Scientist Tanzania (YST) Dk. Gosbert Kamugisha amesema mashindano hayo ambayo yamekuwa kichocheo kwa wanafunzi kusoma masomo ya Sayansi na kuonyesha kwa vitendo.Kamugisha amesema wanafunzi hao wataporudi watakuwa wameongeza ujunzi kupitia kwa wanasayansi wataokutana nao.
Mkurugenzi wa Young Scientist Tanzania (YST) Dk. Gosbert Kamugisha akizungumza na waandishi wa habari wakati utoaji wa zawadi na Ufadhili wa masomo kwa wanafunzi walioshinada mashindano ya Young Scientist iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya jamii.
Mkurugenzi Mtendaji wa Karimjee Jivanjee Foundation, Yusuf Karimjee akimkabidhi zawadi Nadhira Mresa iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wakiwa na zawadi zao walizokabidhiwa kw ajili ya safari nchini Ireland iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Rais Dkt. Magufuli awasalimia wakazi wa Chato Mjini, pia atembelea Shule ya Msingi aliyosoma Chato

$
0
0
 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika benchi la kibanda cha kupigia kiwi (Shoe Shine) pamoja na wakazi wengine wa Chato katika eneo maarufu kama Stendi za zamani Chato mkoani Geita. Kibanda hicho cha Kiwi ndicho Rais Dkt. Magufuli alichokuwa akisafishiwa viatu  vyake kabla ya kuwa Rais, pia ni sehemu ambayo alikuwa akipenda kukaa na  kubadilishana mawazo na wakazi wa Chato wakati akiwa mapumzikoni kipindi cha Nyuma.

 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Chato mkoani Geita. Shule hiyo ya Msingi Chato ndiyo Rais Dkt. Magufuli alisoma kuanzia darasa la kwanza mpaka Darasa la Saba. Rais Dkt. Magufuli amewaasa Wanafunzi hao kusoma kwa bidii kwasababu yeye pia alisoma shuleni hapo. Picha na Mpigapicha Maalum

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Chato mkoani Geita. Shule hiyo ya Msingi Chato ndiyo Rais Dkt. Magufuli alisoma kuanzia darasa la kwanza mpaka Darasa la Saba. Rais Dkt. Magufuli amewaasa Wanafunzi hao kusoma kwa bidii kwasababu yeye pia alisoma shuleni hapo. Picha na Mpigapicha Maalum.

TIZA YA JOTO LA ASUBUHI LA REDIO 93.7 EFM JANUARY10

KARIMJEE JIVANJEE FOUNDATION REWARDS YOUNG SCIENTISTS 2016

$
0
0
By Daniel Mbega of MaendeleoVijijini Blog
THE Karimjee Jivanjee Foundation (KJF) has rewarded Diana Sosoka and Nadhra Mresa from Mtwara Girls Secondary School for being overall winners of the Young Scientists Tanzania (YST) Awards in 2016.
Speaking at a press event to send off the winners to Dublin, Ireland, the KJF Team said the winners would receive scholarship from the foundation to study at any local university when they complete their high school education.
They both take a combination of Chemistry, Biology and Geography and aspire to be medical doctors.
The students are travelling to Dublin today to attend the BT Young Scientists and Technology Exhibition, an Irish annual school students’ science competition, which aims at encouraging interest in science in primary, and secondary schools.
Speaking at the event, the students thanked their school teacher, Mr. Rashid Namila their Biology teacher, whom they said has been a fundamental to their success.
They also thanked the YST, led by Dr. Gozbrt Kamugisha, and the KJF for making their dreams come true.
Winners Diana Sosoka and Nadhra Mresa

BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU 09.01.2017

AMSHA KIPAJI CHAKO NA MICHUZI TV - PETRONIA WA MBEYA KAPENYA

Rais mpya wa Ghana amtumbua mkurugenzi wake wa mawasiliano kwa kuiba hotuba za watu

$
0
0
Rais wa Ghana Mhe. Nana Addo Dankwa Akufo-Addo  amemtumbua Mkurugenzi wake wa mawasiliano Eugene Arhin kutokana na  udukuzi wa hotuba yake wakati wa kuapishwa na kusababisha fedheha kubwa na aibu kimataifa kwa kiongozi huyo wa nchi.
Video zikimuonesha Rais  Addo akisoma hotuba yake mara tu baada ya kula kiapo jijini Kumasi ilionesha kuwa ni ya kuiga neno kwa neno toka katika hotuba za marais wawili wa marekani, na imekuwa gumzo mitandaoni dunia nzima.
Taarifa iliyotolewa mara baada ya hayo ilisema kwamba Mkurugenzi wa Mawasilianio Bw. Eugene Arhin amefutwa kazi.
Hotuba ya Rais huyo wa Ghana imekuwa chachu ya utani kwenye tasnia ya habari duniani kote, hasa baada ya video hiyo kumuonesha Rais Addo akitamka neno kwa neno maneno ya Marais George W. Bush na Bill Clinton.
Mapema Bw. Eugene Arhin  alitoa taarifa kupitia ukurasa wake katika mtandao wa Facebook akijaribu kufuta soo kwa kusema alichokosea ni kusahau kuweka chanzo cha maneno hayo.
"Nia yangu ilikuwa ni kuweka bayana vyanzo vya maneno katika hotuba ya Rais wa Jamhuri (ya Ghana) Nana Mhe Addo Dankwa Akufo-Addo, wakati wa kuapishwa kweke Jumamosi, January 7, 2017.
"Naomba radhi kewa kutotaja chanzo cha maneno hayo. Ilikuwa ni kujisahau na sio kwa makusudi. Ikumbukwe kwamba katika hotuba hiyo hiyo nilitaja vyanzo toka kwa  J.B Danquah, Dr. K.A. Busia, Dr. Kwame Nkrumah na Biblia", alisema. Lakini siko la kufa halisikii dawa. Akajikuta yeye ndiye mtu wa kwanza kutumbuliwa. 
Hiyo haikuwa mara ya kwanza kwa kituko kama hicho kutokea barani Afrika. Mwaka jana baada ya kutoa hotuba yake ya kuapishwa, Rais Muhamadu Buhari alikiri baadaye kwamba sehemu ya hotuba yake ilidukuliwa toka katika hotuba ya Rais Obama wa Marekani ya mwaka 2008.

USIRI WATAWALA YANGA NA SIMBA, KUVAANA LEO USIKU UWANJA WA AMAAN, ZANZIBAr

$
0
0

Na Zainab Nyamka, 
Globu ya Jamii, Zanzibar
IKIWA imebakia masaa machache kufikia mtanange wa watani wa jadi kuelekea nusu fainali ya kombe Mapinduzi, viongozi wa timu hizo mbili wamegoma kuzungumza na vyombo vya habari na zaidi wakisema mpira ni dakika 90.
Wakati  Simba wakiingia msituni wakitoka pale walipokuwa wanakaa toka kuanza kwa mashindano haya, Yanga wameendelea kusalia pale pale huku wakiwaficha wachezaji wao na kuamua kufanya mazoezi usiku kwenye Uwanja wa Amani.
Mashabiki wa pande zote mbili wamejinadi kuweza kuondoka na ushindi katika mchezo huo huku kwa upande wa Simba wakijiamini zaidi wakiwa na imani na kikosi chao kwa kuweza kupata matokeo mazuri zaidi, Yanga wakiwa na uchungu wa kupoteza katika mchezo wao wa hatua ya makundi dhidi ya Azam.
Mechi hiyo ya nusu fainali ya watani wa jadi itapigwa leo majira ya saa 2:15 katika uwanja wa Amaan. Kabla ya mchezo huo kutakuwa na nusu fainali ya kwanza kati ya Azam na Taifa Jang'ombe. 

Jang’ombe inakutana na Azam FC katika mchezo leo  Jumanne saa 10.15 jioni, hapo hapo Amaan, baada ya kumvua taji bingwa mtetezi wa michuano hiyo, URA ya Uganda kwa kuifunga bao 1-0 katika mchezo wake wa mwisho wa Kundi A.
Mara ya mwisho Azam FC kukipiga na Jang’ombe ilikuwa ni Julai 31 mwaka jana kwenye mchezo wa kirafiki wa maandalizi ya msimu huu, ambapo mabingwa hao wa Ngao ya Jamii walishinda bao 1-0 lililowekwa kimiani kiufundi na mshambuliaji aliyekuwa katika majaribio Mburundi Fuadi Ndayisenga.


JPM ATEMBELEA KIJIWENI NA KUJICHANGANYA NA WANANCHI CHATO

RC MAKALLA AKUTANA NA VIONGOZI NA WANAFUNZI WA CHUO CHA ULINZI WA TAIFA, VIONGOZI NA WADAU WA SOKA MKOA WA MBEYA

$
0
0
Image may contain: 20 people, people standing

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla  amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi na wanafunzi wa Chuo cha Ulinzi na kuwaeleza mambo mbalimbali ikiwemo hali ya usalama, shughuli za kiuchumi na kijamii katika Mkoa wa Mbeya.
Amewaeleza kwa takwimu za kiuchumi Mkoa wa Mbeya ni Mkoa wa Tatu kwa kuchangia pato la Taifa baada ya Dar es salaam na Mwanza 

Viongozi wa Chuo na wanafunzi wamefurahishwa na jitihada za serikali ya Mkoa kudumisha amani na kwa kufanya hivyo wananchi kushiriki kikamilifu ktk shughuli za maendeleo.
Mkuu wa Mkoa amewaeleza kuwa Siri ya mafanikio ni ushirikiano ulipo kati ya serikali na wananchi na kwamba ni matumaini yake kuwa Mkoa wa Mbeya utapiga hatua katika maendeleo.
Image may contain: 15 people, people smiling, people standing
Mkuu wa Mkoa wa Meya Mh.Amos Makalla atangaza kuunda Kamati ya kusaidia timu za Mbeya 
- Achangia sh 3,000,000( milioni Tatu) kwa timu ya Mbeya Kwanza iliopo Daraja la kwanza na Mbarali United iliopo Daraja la pili 
- Awataka WADAU kushirikiana na kuepuka Makundi na Siasa katika Soka 
- Awagiza wakuu wa wilaya ,wakurugenzi na madiwani kutenga maeneo ya michezo
- Awakaribisha wadau na wawekezaji kuwekeza katika sport academy.

DROO YA BORESHA MAISHA NA DCB YAFANYIKA MWISHONI MWA WIKI

$
0
0
 Kaimu Mkurugenzi wa DCB, Steven Dede akizungumza na waandishi wa habari mwishoni wa wiki hii wakati wa droo ya promosheni ya Boresha maisha na DCB mwishoni mwa wiki hii, kulia ni Mkuu wa uendeshaji wa matawi wa DCB Haika Machaku.
Kaimu Mkurugenzi wa DCB, Steven Dede akiwa anabonyeza kuanza kwa droo hiyo akishuhudiwa na mkaguzi wa bodi ya michezo ya kubahatisha (Bahati Nasibu) Bakari Maggid (kushoto).

Two Tanzanian firms among Finalists for the Africa Finance & Investment Forum (AFIF) Entrepreneurship Award 2017

$
0
0
Six African projects with big economic and social impact will be presented during the AFIF 2017, convened by EMRC in Nairobi, Kenya
BRUSSELS, Belgium, January 9, 2017/ -- Six African SMEs have been nominated as finalists for the AFIF Entrepreneurship Award 2017, supported by the Rabobank Foundation. Out of the 51 projects from around the continent and following a few rounds of selection, the jury has selected these innovative projects from Ethiopia, Kenya, Nigeria and Tanzania for their social, economic and ecological impact, and their potential for growth and job creation nationally and regionally. The winner will be announced during the Africa Finance & Investment Forum (AFIF) 2017 (http://APO.af/y28Bux), which will be held in Nairobi from 13-16 February.

HABARI KUTOKA TELEVISHENI

ANGALIA GWARIDE LA HESHIMA LA RAIS BARAK OBAMA WA MAREKANI


magoli bora ya mwaka 2016 kuwania tuzo ya fifa ya puskas, mshindi ni....

UZINDUZI WA MRADI WA UJENZI WA MIUNDOMBINU MAENEO HURU YA UCHUMI FUMBA

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Group Bw.Said Salim Bakhresa wakati alipofika  kuzindua  Mradi wa Ujenzi wa Miundombinu katika maeneo huru ya Uchumi huko Fumba Wilaya ya Magharibi "A" Mkoa Mjini Magharibi leo, sambamba na uwekaji wa jiwe la msingi nyumba za kuishi katika shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Group Bw.Said Salim Bakhresa wakati alipofika  kuzindua  Mradi wa Ujenzi wa Miundombinu katika maeneo huru ya Uchumi huko Fumba Wilaya ya Magharibi "A" Mkoa Mjini Magharibi leo, sambamba na uwekaji wa jiwe la msingi nyumba za kuishi katika shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
 Miongoni mwa nyumba za kisasa zinazoendelea kujengwa katika mradi wa Ujenzi wa Miundombinu katika maeneo huru ya Uchumi huko Fumba Wilaya ya Magharibi "A" Mkoa Mjini Magharibi , sambamba na uwekaji wa jiwe la msingi nyumba za kuishi zilizozinduliwa leo na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) ikiwa ni  shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  akiangalia majarida yenye michoro inayohusiana na  Mradi wa Ujenzi wa Miundombinu katika maeneo huru ya Uchumi huko Fumba Wilaya ya Magharibi "A" Mkoa Mjini Magharibi leo, sambamba na uwekaji wa jiwe la msingi nyumba za kuishi baada ya kuzindua mradi huo rasmi ikiwa ni   katika shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA





UMEME CHANZO CHA KUZOROTESHA HUDUMA BORA ZA AFYA KATIKA JIMBO LA MAFINGA MJINI - MBUNGE COSATO CHUMI

$
0
0
 Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini Mhe. Cosato Chumi (kulia)  akisikiliza kilio cha wafanyakazi wa zahanati na vituo vya afya alipotembelea kujionea na kusikiliza changamoto za huduma za afya katika jimbo lake ili kuzitafutia ufumbuzi na kuboresha huduma hiyo.

Na Fredy Mgunda, Iringa
MBUNGE wa jimbo la Mafinga Mjini Mhe. Cosato Chumi alifanya ziara ya kuzitembelea zahati,vituo vya afya na hospitali za jimbo hilo kwa lengo la kujionea changamoto za kiafya. 
Akiwa katika ziara hiyo alikumbana na changamoto ya kukosekana kwa umeme katika baadhi zahati za jimbo hilo na kuahidi kulipeleka tatizo hilo bungeni ili litafutiwe ufumbuzi mapema.
Akizungumza na blog hii Chumi alisema tatizo la umeme katika vituo na zahati ni kubwa hivyo inahitajika nguvu ya ziada kutatua tatizo la umeme ili kuboresha afya za wananchi wake pamoja na huduma ya mama na mtoto.

Baridi kali yayakumba maeneo mengi barani Ulaya, wasio na makazi waathirika zaidi

$
0
0
Kiwango cha joto kimeshuka hadi nyuzi 23 chini ya sifuri katika baadhi ya maeneo ya Ulaya. Hali hii imesababisha maafa na hata watu kufa. maisha ya wakimbizi na watu wasiokuwa na mahala pa kuishi yako hatarini

Bara zima la Ulaya linatetemeka kwa baridi kali kutokana na kushuka kwa viwango vya nyuzi joto katika msimu huu wa baridi.  Watu kadhaa wameripotiwa kufa kutokana na baridi kali.  Hali hii ya baridi ya kupindukia imesababisha pia mtafaruku katika utaratibu wa usafiri na wakati huohuo wakimbizi waliokwama katika kisiwa cha Chios nchini Ugiriki wanakabiliwa na hali mbaya. 

Hali hii mbaya ya baridi kali inawakumba pia wakimbizi walioko katika kisiwa cha Lesbos ambapo inaripotiwa kuwa hawana maji wala umeme. Takriban watu elfu 15 wanasubiri kurudishwa nchini Uturuki kufuatia makubaliano yaliyofikiwa baina ya Umoja wa Ulaya na serikalri ya Ankara.
Huko Ujerumani dereva mmoja ambaye anajishughulisha na kuwasafirisha watu kinyume cha sheria aliwatelekeza abiria wake 19 ndani ya gari alilokuwa akiwasafirishia.  Dereva huyo aliliacha gari hilo katika maegesho na kuamua kutoweka bila kuwajulisha abiria wake hao katika jimbo la Bavaria na wakati huo kulikuwa na baridi ya kiwango kilichoshuka zaidi cha nyuzi 20 chini ya sifuri. 

Polisi wameeleza kuwa watu hao 14 na watoto watano walikuwa wamemlipa dereva huyo kiasi cha Euro 500 hadi 800 na kwamba huenda dereva huyo aliamua kuwaacha baada ya kutambua kuwa gari lake lina matatizo ya kimitambo.  

Hali ya baridi kali na kuanguka kwa theluji katika maeneo mbalimbali katika siku za hivi karibuni imesabaisha madhila katika maeneo mengi barani Ulaya. 

Kwingineko takriban watu 9 wamekufa nchini Poland watatu katika Jamuhuri ya Czech na wawili nchini Holand. Taarifa zilizoandikwa na Mtandao wa DW zinaeleza kuwa wengi wa watu wanaokumbwa na umauti ni wale ambao hawana mahala pa kuishi.  Polisi nchini Poland wamesema kuwa wanatarajia idadi ya vifo kuongezeka.
Nchini Ufaransa abiria wanne raia wa Ureno walikufa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kuteleza na kuacha njia katika eneo la mji wa Lyon taarifa kutoka wizara ya mambo ya ndani ya Ufaransa zinaeeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo huenda kilitokana na mtelezo katika barabara uliosababishwa na barafu inayoteleza. 

Ujerumani, Italia, Ugiriki, Poland na Uturuki ni miongoni mwa nchi ambazo zinakabiliwa na kumwagika kwa theluji nyingi na kushuka kwa viwango vya joto huku Ujerumani ikijiandaa kwa hali mbaya ya hewa kutokana na dhoruba inayotazamiwa kutokea maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo.
Wataalamu wa hali ya hewa nchini Ujerumani wametahadharisha juu ya hatari za barafu nyeusi ambayo inateleza mno.

MABULA AFIKA IROLE KILOLO KUSHUGULIKIA SITOFAHAMU YA MIPAKA KATI YA IROLE NA ILAMBILOLE, IRINGA

$
0
0
Naibu waziri  wa ardhi na maendeleo ya makazi Angelina Mabula katikati  wa  tano akiwa  na  viongozi  wa  wilaya ya  kilolo na wajumbe  wa  baraza la ardhi la kata ya Mtitu  Kilolo wa  pili  kulia ni  mbunge  wa  Kilolo  Venance  Mwamoto na wa  pili  kulia ni mwenyekiti wa  Halmashauri ya  Kilolo akifuatiwa  na  Dc  kilolo Asia Abdalah
Dc  Kilolo Asiah Abdalah  akifungua  kikao
Naibu  waziri Bi Mabula  akitoa  maelekezo kwa mwenyekiti  wa  kijiji  cha   Irole jana  kulia ni Dc wa Iringa Richard  Kasesela, mbunge  Venance  Mwamoto na Dc  Kilolo Asia Abdallah
Mwenyekiti  wa  baraza  la ardhi kata ya  Mtitu  Veronica Salangwa  akitoa  maelezo mbele ya  naibu  waziri  kulia  ni mbunge  Mwamoto. Kushoto ni Dc  wa Kilolo Asia Abdalah na naibu  waziri  Mabula
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images