Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1501 | 1502 | (Page 1503) | 1504 | 1505 | .... | 3270 | newer

  0 0
 • 01/09/17--22:30: WAREHOUSE GODOWN FOR RENT
 • Kimara stop over Meter 50 kutoka Morogoro Road Parking ipo kwa magari makubwa .

  Mawasiliano 0713 882 800

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 
  WIZARA YA NISHATI NA MADINI
  Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, kwa kushirikiana na Benki ya Dunia (WB) itatoa Ruzuku ya  jumla ya Shilingi Bilioni 7.481 kwa Wachimbaji Madini Wadogo 59 ambapo kiwango cha juu cha Ruzuku kwa Kikundi/Mtu binafsi ni  Shilingi Milioni 210.

  Hafla ya utoaji wa Ruzuku hiyo itafanyika siku ya Jumanne,  tarehe 17  Januari 2017, Mjini Mpanda mkoani Katavi, Mgeni Rasmi atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim  M. Majaliwa (Mb.).

  Fedha za Ruzuku kwa kila Mnufaika, zitatumika kununua vifaa vya kuchimbia au kuchenjulia madini ambapo kabla ya kukabidhiwa vifaa hivyo, wanufaika hao watapata mafunzo kuhusu matumizi sahihi ya ruzuku yatakayotolewa na Wizara ya Nishati na Madini tarehe 16 Januari, 2017 Mjini Mpanda.

  Miradi 59 itakayopata ruzuku hiyo, ndiyo iliyoshinda kati ya miradi 592 ya uchimbaji madini mdogo iliyokuwa kwenye ushindani.. Waombaji wengine ambao maombi yao hayakushinda watajulishwa kwa Barua.

  Wizara ya Nishati na Madini ilianza mchujo wa kuwapata Washindi tangu Mwezi Julai 2016, kwa kuwashirikisha Viongozi wa Wachimbaji Madini Wadogo wa mikoani (REMA’s),Viongozi wa Kitaifa  (FEMATA) pamoja na Viongozi wa Wachimbaji Madini Wanawake (TAWOMA).

  Majina ya wanufaika wa Ruzuku awamu ya tatu  pia yanapatikana kwenye Tovuti ya Wizara: www.mem.go.tz pamoja na Ofisi Za Madini Za Kanda.
  Imetolewa na,

  Prof. Justin W. Ntalikwa
  KATIBU MKUU

  0 0


  Shirikisho la Soka Duniani Fifa leo linatarajiwa kupiga kura  kuamua kuhusu mpango wa kupanua Kombe la Dunia liwe linashirikisha mataifa 48. Mpango huo ukiidhinishwa, basi utaanza kutekelezwa Kombe la Dunia la 2026, na utakuwa na faida kwa nchi za Afrika na Asia.
  Rais wa shirikisho hilo Gianni Infantino (pichani) ambaye amekuwa akipigia upatu  mpango huo na amekuwa na uungwaji mkono mkubwa, pia anataka michuano hiyo iwe na makundi 16 ya mataifa matatu kila kundi na klabu mbili kutoka kila kundi zitafuzu kwa hatua ya mtoano na iwapo mpango huo utaidhinishwa, basi itakuwa mara ya kwanza kwa Kombe la Dunia kupanuliwa tangu mwaka 1998.
  Kuna mapendekezo matano ambayo baraza kuu la Fifa lenye wanachama 37 litaangazia ikiwemo timu 48 na zikiwa kwenye makundi 16 na timu tatu kila kundi ambapo timu mbili bora zitasonga kwa hatua ya mtoano na kuingia timu 32 (mechi 80 kwa jumla).
  Mapendekezo mengine ni kuwa na timu 40 na makundi 10 ya timu nne kila kundi ambapo mshindi, na timu sita pekee zinazomaliza nambari mbili kundini ndizo zinafuzu (mechi 76) nyingine ni kuwa na timu 40 na  makundi manane ya timu tano kila kundi (mechi 88) kusalia na kuendelea kusalia na timu 32 .
  Infantino, 46, ambaye alimrithi raia mwenzake Sepp Blatter kama rais wa Fifa mwezi Februari 2016 alifanya kampeni akiahidi kupanua michuano hiyo. Awali alipendekeza michuano ya timu 40, wazo lililowasilishwa na rais wa wakati huo wa Uefa Michel Platini 2013, kabla ya kubadilisha msimamo na kuunga mkono michuano ya timu 48.
  Chini ya mpango wa Infantino anaoupendekeza kwa sasa, mechi zinaongezeka kutoka 64 hadi 80, lakini fainali bado zinaweza kuchezwa kwa kipindi sawa na cha sasa cha siku 32. Taifa halitatakiwa kucheza zaidi ya mechi saba, sawa na ilivyo chini ya mpango wa sasa na dhaifu pekee ni kwamba huenda mikwaju ya penalti ikatakiwa kutenganisha klabu zinazotoka sare kwenye makundi.
  Historia ya Mabadiliko Kombe la Dunia

  Kombe la Dunia Timu
  1930 Uruguay 13
  1934 Italy 16
  1950 Brazil 13
  1954 Switzerland 16
  1958 Sweden 16
  1974 West Germany 16
  1982 Spain 24
  1986 Mexico 24
  1998 France 32

  Kwa msaada wa BBC.

  0 0

  Na Othman Khamis Ame, OMPR
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Taifa linawategemea Vijana  wakati wowote katika dhana nzima itakayothibitisha kwamba wanasimamia kwa vitendo Mapinduzi katika kuondoa maovu yote yanayolikabili Taifa.
  Alisema Serikali zote mbili ile na Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na iIe ya Mapinduzi ya Zanzibar zinataka kuona  Vijana wake wanakuwa chem chem ya Maendeleo badala ya kuwa dimbwi la matatizo mitaani.
  Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati akiyafunga Matembezi ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) kuunga mkono maadhimisho ya sherehe za kutimia miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964  hapo Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akivishwa Skafu na Vijana wa Chipukizi kabla ya kuyafunga matembelezi wa UVCCM yaliyohitimishwa hapo Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.

   Vijana wa UVCCM wapatao 400 wakihitimisha matembezi yao ya kuadhimisha miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyopokelewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hayupo pichani.
   Balozi Seif akipokea Picha ya Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Aman Karume iliyotumiwa na Vijana hao katika matembezi yao. Wa kwanza kutoka kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM Tanzania Ndugu Shaka Hamdu Shaka na Makamu Mwenyekiti wa Umoja huo  Bibi Mboni Muhita.
   alozi Seif akipokea Picha ya Muasisi wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar  Hayati Mwalimu Julius K. Nyerere iliyotumika kwenye matembezi hayo.
   Vijana wa UVCCM wakimkabidhi Bendere ya Zanzibar Balozi Seif waliyoitumia kama kielelezo kwenye matembezi yao ya kuunga mkono sherehe za kutimia miaka 53 ya Mapinduzi ya  
  Sehemu ya Vijana wa UVCCM wapatao 400 wakiimba wimbo wa Taifa bada ya matembezi yao ya kuadhimisha miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Picha na OMPR, ZNZ. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

  0 0
 • 01/09/17--23:53: Article 2


 • 0 0


  Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi,Mh.Saleh Mbwana Mhando leo amefanya ziara ya kutembelea na kukagua shughuli mbalimbali za uvuvi wa samaki aina ya Sangara na Dagaa katika mwambao wa ziwa Tanganyika mkoani humo.Dc Mhando amesema kuwa ziara hiyo imelenga kuangalia fursa mbalimbali zilizopo na kuwawezesha wavuvi hao wadogo wadogo.Pichani Dc Mhando (pili kulia) akipata maelezo mafupi kuhusiana na mradi huo wa kukausha dagaa pembezoni mwa ziwa Tanganyika,mkoani Katavi.

  Samaki aina Sangala kama aonekanavyo pichani mara baada kuvuliwa kwenye ziwa Tanganyika.
  Mmoja wa akina mama wanaojishughulisha na ukaushaji wa dagaa pembezoni mwa ziwa Tanganyika,akimuelezea Dc Mhando changamoto mbalimbali wazipatazo kuhusiana na suala zima la soko na usafirishaji

  0 0
  0 0

  Amir Mongi akimvisha pete mewe Munirah Bawaziri siku ya ndoa yao ,katika sherehe iliyofayika kwenye ukumbi wa Mamba Complex Marangu Kilimanjaro januari 2017.
  Maharusi wakiwa wanapata chakula pamoja na waandishi wa habari kuroka Jiji la Arusha.
  Sherehe inaendelea.
  Baadhi ya waandishi wa habari kutoka Jijini Arusha wakiwa wamesimama na mmoja wao aliyevaa gauni la njano Pamella Mollel akiwa anazungumza kwa niaba yao.Picha na Vero Ignatus Blog.


  0 0

   Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospter Muhongo (wa tatu kushoto) na Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda Mhandisi Irene Muloni (wanne kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa   Hafla ya Uzinduzi wa Usanifu wa Awali wa michoro ya mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Uganda Hadi Bandari ya Tanga Tanzania mjini Kampala Uganda.
  Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo akisaini kitabu cha Wageni katika Ubalozi wa Tanzania nchini Uganda baada ya kuhudhuria Hafla ya Uzinduzi wa Usanifu wa Awali wa Michoro ya Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Uganda hadi Bandari ya Tanga, Tanzania.  Wengine wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa, Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mhandisi Kapuulya Musomba na Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Marwa Petro.


  Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo tarehe 9/1/2017 aliongoza Ujumbe wa Tanzania jijini Kampala nchini Uganda katika hafla ya Uzinduzi wa Usanifu wa Awali (Front End Engineering Design -FEED) wa mradi wa Bomba la kusafirisha Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga, Tanzania.   Uzinduzi huo ulifanyika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini ya Uganda na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri wa nchi zote mbili za Uganda na Tanzania, Makatibu Wakuu wa nchi zote mbili, Wakurugenzi wa mashirika ya mafuta na gesi, Kampuni zilizogundua mafuta nchini Uganda za Total (Ufaransa), CNOOC (China), TULLOW (Uingereza), Kampuni ya Mafuta ya Uganda National Oil Co. (UNOC), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na wawakilishi wa vyombo vya habari.  Wakati wa uzinduzi huo ilielezwa   kuwa, FEED ni moja ya hatua muhimu katika kuhakikisha mradi huo unatekelezwa katika viwango vinavyozingatia usalama wa kimazingira na ustawi wa jamii.  Vilevile, ilielezwa kuwa, hatua hiyo itajumuisha pia upatikanaji wa njia ya gharama nafuu ya kupitisha bomba la mafuta ambapo pia Wataalamu wa taaluma mbalimbali watahusika katika kuhakikisha mradi huo unafuata viwango na ubora wa kimataifa.  Pia , imeelezwa  kuwa bomba hilo litakuwa la kwanza kwa urefu duniani kuwa bomba linalopashwa joto muda wote kutokana na asili ya mafuta yanayosafirishwa.  Mradi huo mkubwa utatekelezwa kwa ushirikiano wa Serikali za Uganda na Tanzania na pia utahusisha kampuni za TOTAL, CNOOC na TULLOW.

  0 0

  Na. Aron Msigwa – NEC
  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewataka wagombea na Vyama vya Siasa vinavyoendelea na kampeni za Uchaguzi mdogo wa Ubunge na Madiwani kufanya kampeni za kistaarabu zinazozingatia maadili ya Uchaguzi ya mwaka 2015 na kwamba Chama au mgombea atakayekiuka maadili hayo atachukuliwa hatua.

  Kauli hiyo imetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mkuu (Mst. Znz.) Hamid M. Hamid zikiwa zimebaki siku chache kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi huo Januari 22, 2017 kufuatia baadhi Vyama na Wagombea kuanza kukiuka Maadili na taratibu za Kampeni  kwa kutoa matamko yaliyo nje ya Sera za Vyama vyao.

  Amesema kipengele cha 2.1 (m) cha Maadili ya Uchaguzi kinachoeleza  Wajibu wa Vyama vya Siasa na Wagombea katika kuendesha shughuli za Siasa wakati wa Kampeni kinavitaka Vyama vya Siasa, Wagombea na Wafuasi wao kufanya kampeni kwa kuzingatia misingi inayolenga kutangaza Sera ambazo hazijengi chuki, mafarakano na kuleta mgawanyiko katika jamii.

  “Katika Kampeni zinazoendelea, baadhi ya vyama vya Siasa vimeanza kukiuka taratibu za kampeni na maadili na kutumia fursa ya kampeni vibaya, vinawasema viongozi wa Kitaifa , kutoa matamko ambayo kihalisia siyo ya kumnadi mgombea na kufanya kampeni zisizo za kistaarabu,” Amesema Jaji Hamid.

  Amesema kuwa vyama Vyama au Wagombea watakaoendelea kukiuka Maadili ya Uchaguzi katika Mikutano ya kampeni inayoendelea katika maeneo mbalimbali ya Tanzania pamoja na Jimbo la Dimani, Zanzibar watachukuliwa hatua.

  Jaji Hamid ameeleza kuwa kipengele cha 5.3 cha Maadili ya Uchaguzi kinaeleza wazi kuwa Chama au Mgombea atakayekiuka Maadili ya uchaguzi katika jimbo au Kata yenye uchaguzi mdogo atafikishwa katika kamati ya maadili ya ngazi husika na kuchukuliwa hatua stahiki.

  Aidha, kipengele cha 5.10 cha Maadili ya Uchaguzi yaliyokubaliwa na Vyama vyote vya Siasa kinafafanua kuwa Kamati za Maadili ya uchaguzi ngazi ya Taifa, Jimbo na Kata katika kushughulikia malalamiko na kutoa adhabu zinaweza kuchukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukitaka Chama au Mgombea kusahihisha kosa au makosa au kuomba msamaha hadharani.

  Hatua nyingine ni Kukisimamisha Chama au Mgombea kuendelea kufanya kampeni za Uchaguzi, kutoza Faini, Kutangaza jina la Chama au Mgombea aliyekiuka Maadili kwa kueleza kosa au Makosa yake kupitia redio, televisheni, magazeti na njia nyingine za mawasiliano.

  0 0


  Na Mwandishi wetu
  NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, ameitaka Taasisi ya Utoaji mikopo na huduma za kifedha ya 'UTT Microfinance' kuandaa mpango mkakati wa kuwafikia wakulima vijijini na kuwapa mikopo itakayowasaidia kuzalisha mazao kwa wingi.

  Akizungumza jana kwenye hafla fupi ya kuzindua rasmi bodi ya wakurugenzi ya Taasisi hiyo, Kijaji, alisema Tanzania ya viwanda inayotajwa pia itawategemea wakulima kufikia malengo hayo.

  "naipongeza sana UTT kwa utendaji wake wa kazi na hasa kwa bodi hii iliyomaliza muda wake, kwa bodi mpya ninayoizindua leo iangalie namna ya kuwfikiwa wakulima vijijini na kuwapa mikopo nafuu ili kuborosha uzalishaji wake," alisema Kijaji.
  Aidha, alisema viwanda vitakavyoanzishwa nchini vingi vitategemea malighafi kutoka ndani ya nchi yakiwemo mazao ya wananchi vijijini.
  "Serikali inataka kuona taasisi zake zoye za kifedha zilizoanzishwa zinatoa mikopo yenye masharti nafuu kwa wananchi, hii itasaidia kuboresha maisha kwa mwananchi mmoja mmoja," aliongezea kusema.
  Alisema pamoja na mafanikio waliyoyapata UTT Microfinance kwa kipindi cha miaka mitatu, taasisi hiyo ijipange kutoa elimu kwa wajasiriamali na kuwaibua.
  Awali akimkaribisha Naibu waziri huyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo, James Washima, alisema Serikali haikufanya makosa kuanzisha taasisi hiyo kwa kuwa katika kipindi cha miaka miatatu tangu kuanzishwa kwake imewafikia zaidi ya wajasiriamali 23,513 huku kiasi cha shilingi bilioni 29.13 kilitolewa kama mikopo kwa wananchi hao. Alisema katika kipindi hicho matawi 12 yalifunguliwa katika mikoa ya Arusha, Mwanza, Dodoma, Mbeya, Zanzibar na Dar es Salaam.
  Bodi iliyozinduliwa na Naibu waziri Kijaji, inaongozwa yenye wajumbe wa nne inaongozwa na Mwenyekiti wa bodi Godwin Mjema, ambayo itakaa madarakani kwa kipindi cha miaka mitatu.
   .Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Ashatu Kijaji (katikati)ambaye alikuwa mgeni rasmi akifafanua jambo katika  hafla ya Uzinduzi wa Bodi  Mpya ya  wakurugenzi wa  Taasisi ya Huduma za Fedha na Mikopo –UTT Microfinance PLC (UTT MFI) iliyofanyika makao makuu ya taasisi hiyo  leo  jijijni Dar es Salaam,Kushoto ni Mwenyekiti wa bodi hiyo Prof. Godwin Mjema na kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo, James Washima.
    Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Ashatu Kijaji (wapili kutoka kulia) akimkabidhi vitendea kazi Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Huduma za Fedha na Mikopo –UTT Microfinance PLC (UTT MFI) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi  Mpya ya  wakurugenzi wa  Taasisi ya Huduma za Fedha na Mikopo –UTT Microfinance PLC (UTT MFI)   Profesa Godwin Mjema   wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Mpya ya Wakurugenzi  wa taasisi hiyo iliyofanyika leo  makao makuu ya ofisi hiyo Upanga jijini Dar es Salaam.
   Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Huduma za Fedha na Mikopo –UTT Microginance PLC (UTT MFI) wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashuta Kijaji wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi Mpya ya Wakurugenzi iliyofanyika leo Upanga jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushrikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.Balozi Dkt. Augustine Mahiga akijadili jambo na mgeni wake Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Mhe. Wang Yi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Nyerere Jijini Dar es Salaam, wakati akijiandaa kuondoka baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi nchini. Wa kwanza kulia ni Balozi wa China nchini Tanzania Mhe. Lu Younqing 
  Waziri Mahiga akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje wa China Mhe. Wang Yi 
  Waziri Mahiga na Waziri Wang Yi wakifurahia jambo wakati wa mazungumzo 
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Mhe.Wang Yi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Nyerere wakati akiondoka nchini mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi 
  Waziri Mhe. Balozi Dkt. Mahiga Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia Balozi Mbelwa Kairuki (katikati kulia) na Makuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara Bi. Mindi Kasiga wakipunga mikono kumuaga Warizi Mhe. Wang wa China. 

  0 0  0 0

  Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii mapema leo, inaeleza kuwa chombo (Jahazi) cha nahodha Badru Said kilichoondoka Mkoani Tanga jana usiku kuelekea wete Kisiwani Pemba kimepatwa na dhoruba ya bahari na kuzama umbali mfupi kutokea bandari ya Tanga, na kudaiwa kuwa watu zaidi ya 13 wamepoteza maisha huku wengine wakiwa wamejeruhiwa na kupoteza fahamu na baadae kuwahishwa hospitali ya Rufaa ya Bombo Mkoani Tanga kwa matibabu ya haraka.

  Kwa mujibu wa mmoja wa abiria katika chombo hicho, Mahfoudh Khamis ambaye yupo katika hospitali ya Bombo akipatiwa matibabu, amesema kuwa jumla ya maiti 13 zilipatikana akiwemo Nahodha mwenyewe wa Chombo hicho, Badru Said na majeruhi zaidi ya 30  wameokolewa na kulazwa hospitalini hapo.

  Inaelezwa kuwa kuna wengine waliokoka na kurudi makwao ambao idadi yao haikufahamika kwa haraka, Wengi waliokuwamo kwenye chombo hicho inadaiwa ni wanawake na watoto ambao walikuwa wanarudi likizo zao za Mwezi Disemba.

  Mungu azilaze peponi roho za Marehemu wote na awajaalie kupona kwa haraka majeruhi wote.

  Amin .

  0 0


  0 0  Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Dkt. Hassan Abbas (Pichani kati) akizungumza na waandishi wa habari mara baada kukamatwa kwa watu wanaodaiwa kutaka kusajili gazeti kwa nyaraka za kughushi leo jijini Dar es Salaam, Kulia ni Kaimu Msajili wa Idara ya Habari Maelezo, Patrick Chipangula na kushoto ni Afisa Habari wa Idara ya Habari MAELEZO,Lilian Lundo. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
  watuhumiwa waliotaka kusajili gazeti kwa nyaraka za kugushi wakiwa chini ya ulinzi leo jijini Dar es Salaam.
  watuhumiwa waliotaka kusajili gazeti kwa nyaraka za kugushi wakiwa chini ya ulinzi leo jijini Dar es Salaam,tayari kuelekea kituo cha polisi kati.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

  0 0

  KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, mchana huu imemtangaza, Aristica Cioaba, kuwa Kocha Mkuu wa kikosi hicho.

  Cioaba, 45, anakuja Azam FC kurithi mikoba ya Mhispania Zeben Hernandez, aliyesitishiwa mkataba pamoja na benchi lake zima la ufundi.

  Kocha huyo atasaidiana na makocha wazawa, Idd Nassor Cheche na Kocha wa Makipa Idd Abubakar, walioiongoza timu hiyo kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi, ambapo saa 10.15 jioni ya leo itasaka fainali kwa kukipiga na Taifa ya Jang’ombe.

  Akizungumza na mtandao rasmi wa klabu Azam, Ofisa Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Saad Kawemba, tayari amefanikiwa kumpata kocha huyo na wameingia naye mkataba wa muda wa miezi sita wenye kipengele cha kuongezwa.
  Kocha mpya wa Azam FC, Aristica Cioaba kutoka nchini Romania, akimwaga wino wa kukinoa kikosi hicho, mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Saad Kawemba, huko visiwani Zanzibar leo.

  Alisema Cioaba ana uzoefu mkubwa wa soka la Afrika na ataiongoza Azam FC kwa kipindi hiki hadi mwishoni mwa mwa msimu, ambapo baada ya kuisha watakaa tena mezani kufanya tathimini ya mafanikio yake na wapi wanaweza kuendelea kutokana na kazi iliyofanyika.

  “Bodi ya Wakurugenzi ya Azam FC inapenda wadau wote wa mpira na wapenzi na mashabiki wa Azam kwamba klabu imempata mwalimu, ambaye ndiye ataiongoza klabu kwa kipindi hiki hadi mwishoni mwa msimu.

  “Kwa hiyo kwa mashabiki wetu maana yake ni kwamba tukiingia kwenye mechi inayofuata ya ligi, kocha atakuwa ameanza kazi na Cheche (Idd Nassor) atakuwa msaidizi wake na benchi lake zima alilokuwa nalo hivi sasa litaendelea,” alisema.

  Kawemba aliongeza kuwa hivi sasa kocha huyo atakuwa na kikosi visiwani Zanzibar kufuatilia mwenendo wa timu ulivyo na ataendelea kutoa ushauri panapohitajika na ataanza rasmi kukaa kwenye benchi mpaka pale vibali vyake vya kufanya kazi nchini vitakapokamilika.

  “Taratibu hizo zitakwenda kwa mujibu wa sheria za nchi, ambapo tutaziheshimu na kuona ya kwamba tutazifanya kwa haraka zaidi ili mwalimu aweze kupata kibali cha kufanya kazi hapa nchini, kwa hayo machache tunawaomba mashabiki wetu wawe watulivu wampe sapoti kocha na wadau wote wa mpira waone ya kwamba tumefanya jambo la kheri,” alisema.
  Kauli ya kwanza ya Cioaba

  Kwa upande wake Cioaba, alisema kuwa anafuraha kubwa leo hii kusaini mkataba wa kuifundisha timu hiyo huku akiahidi kazi nzuri na kuifanya timu hiyo kuwa bora.

  “Najua Azam FC hapa Tanzania ni moja ya timu kubwa yenye historia huko nyuma, napenda kuushukuru uongozi kwa kuniamini na kunipa nafasi kuja kufundisha soka kwenye nchi hii, kwa mashabiki napenda kuwaambia kuwa nalijua soka la Afrika, nimewahi kufundisha Ghana na kupata matokeo mazuri.

  “Kuhusu wakati ujao, nina furaha sana kuhusu uongozi walipoongea na mimi wakati tunaweka mipango ya timu ya hapo baadaye na hili ni jambo zuri kwa kocha, kitaaluma nawaahidi mashabiki na watu wote wanaoipenda Azam FC, niko hapa kuwapa mambo mazuri katika kazi yangu kwenye klabu,” alisema.

  Msimu uliopita, Cioaba aliiongoza Aduana Stars ya Ghana kushika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu ya Ghana, ambapo anafahamiana kwa ukaribu na nyota wawili wa Azam FC, Yakubu Mohammed na Yahaya Mohammed, waliosajiliwa kutoka timu hiyo katika usajili wa dirisha dogo.

  Mbali na kufundisha soka nchini Ghana pia amewahi kufanya kazi kwenye miamba ya Morocco, Raja Casablanca, Al Masry ya Misri na katika nchi za Romania, Kuwait, Oman na Jordan.

  0 0

  On January 9, 2017, the Executive Board of the International Monetary Fund (IMF) completed the fifth review of Tanzania’s economic performance under the program supported by a three-year Policy Support Instrument (PSI). The Board’s decision was taken on a lapse of time basis.

  In completing the review, the Board also granted waivers for the non-observance of the end-June 2016 assessment criteria on the overall fiscal deficit and the non-accumulation of domestic expenditure arrears on the grounds that the slippages were minor. The PSI for Tanzania was approved by the Board on July 16, 2014 (see Press Release No. 14/350).
  Tanzania’s macroeconomic performance remains strong. Economic growth was robust during the first half of 2016 and is projected to remain at about 7 percent this fiscal year. Inflation came down below the authorities’ target of 5 percent and is expected to remain close to the target, while the external current account deficit was revised down on account of lower imports of capital goods. Nevertheless, there are risks that could adversely affect economic growth going forward, arising from the currently tight stance of macroeconomic policies, the slow pace of credit growth that may become protracted, slow implementation of public investment, and private sector uncertainty about the government’s new economic strategies.

  Program performance was broadly satisfactory and most assessment criteria for June 2016 and all indicative targets for September 2016 were met. While progress in structural reforms identified under the program has been generally slow, the authorities have recently stepped up efforts to advance them. These include measures taken to strengthen public financial and debt management, modernize the monetary policy framework, and improve monitoring of parastatal enterprises. The authorities have committed to further reforms in these areas.

  The current tight macroeconomic conditions should be addressed by loosening the short-term policy stance, in line with program targets. After recording a small fiscal surplus in July-September, the government is committed to stepping up budget implementation, particularly in public investment, including by mobilizing external financing. Monetary policy should be eased to address the tight liquidity situation and support credit to the private sector. The Bank of Tanzania’s steps in this regard are appropriate, but will need to be fine-tuned when the planned fiscal spending materializes. The increase in international reserves recorded since the beginning of the fiscal year is a welcome step to gradually rebuild buffers.

  The authorities are implementing an ambitious development and reform agenda over the medium term, as described in their recently-released second Five-Year Development Plan. The strong drive against corruption and tax evasion has led to higher fiscal revenues, which, if sustained, will provide a good foundation for the envisaged scaling up of infrastructure investment, starting with the 2016/17 budget. The Plan also envisages a significant structural transformation of the economy by nurturing human development. Full involvement of all stakeholders in policy design and implementation—including importantly the private sector—will be crucial.

  0 0

  Na Bashir Nkoromo

  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo, ameongoza umati wanachama wa CCM na nawananchi kwa jumla, katika mazishi ya aliyekuwa Katibu wa CCM wilaya ya Kilindi mkoani Tanga, Hawa Nangaju, yaliyofanyika leo Januari 10, 2017, Mbagala, Dar es Salaam.

  Katika mazishi hayo, walihudhuria pia viongozi kadhaa akiwemo Katibu wa Halmashauri Kuu Taifa(NEC) ya CCM, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinza na Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na baadhi ya viongozi kutoka Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba.

  Akizungumza kwenye mazishi hayo, Mpogolo alisema, Chama Cha Mapinduzi kimeondokewa na kiongozi ambaye alikuwa mwadilifu, mchapakazi na anayekipenda kwa dhati Chama, hivyo kimebakiwa na majozi makubwa kutokana na kifo cha katibu wake huyo.

  "Ni kutokana na Chama kilivyomfahamu na kumwamini Hawa Omari Nangajau, ndiyo sababu sisi viongozi tuliobaki pamoja na wanachama wenzetu wa CCM, tumepokea msiba huu kwa majonzi makubwa, hivyo ili kumuenzi ni sisi kufanyakazi kwa uadilifu, kujituma na kukipenda Chama kama alivyokuwa akifanya", alisema Mpogolo.

  Akisoma, wasifu, Mkuu wa Utawala Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Bakari Khamis Hamadi alisema, Marehemu Hawa Nanganjau aliyezaliwa Novemba 27, 1962 katika Kijiji cha Mkaramo Wilayani Kilwa mkoani Lindi alihitimu elimu yake ya sekondari katika shule ya Sekondari Kibasila, Temeke, Dar es Salaam mwaka 2004.

  Khamis alisema, amekuwa akifanya kazi mbalimbali katika CCM tangu mwaka 1981 akiwa katibu wa Tawi na kupita katika nafasi mbalimbali za ukatibu hadi nanafasi yake ya mwisho ya Ukatibu wa CCM wilaya ya Kilindi mkoani Tanga, tangu mwaka 2013 hadi mauti yalipomfika, Januari 8, 2017, kutokana na maradhi ya tumbo.
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo,amkimfariji mtoto aliyekuwa Katibu wa CCM,Wilaya ya Kilindi mkoa wa Tanga,hawa Omari Nanganjau,Said Mbaraka,Wakati wa masishi ya Katibu huyo,yaliyofanyika leo,Mbagala jijini Dar.Picha na Bashir Nkoromo.
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo (wapili kushoto), akiwa msibani wakati wa mazishi ya aliyekuwa Katibu wa CCM wilaya ya Kilindi Hawa Omari Nanganjau, yaliyofanyika leo nyumbani kwa marehemu, Mbagala, Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ngemela Lubinza
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo akisalimiana na Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na WatotoUmmy Mwalimu, wakati wa mazishi ya aliyekuwa Katibu wa CCM wilaya ya Kilindi Hawa Omari Nanganjau, yaliyofanyika leonyumbani kwa marehemu, Mbagala, Dar es Salaam. 
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinza wakiwapa pole waombolezaji, wakati wa mazishi ya aliyekuwa Katibu wa CCM wilaya ya Kilindi Hawa Omari Nanganjau, yaliyofanyika leo nyumbani kwa marehemu, Mbagala, Dar es Salaam.

  0 0

  Taasisi ya Flaviana Matata Foundation (FMF) leo imezindua rasmi msimu wa muhula/mwaka mpya wa masomo 2017 #BackToSchool2017 kwa kutoa msaada wa vifaa vya kujifunzia kwa wanafunzi 317 wanaosoma Shule ya Msingi Msinune iliyopo kata ya Kiwangwa wilayani Bagamoyo mkoani Pwani. Msaada huo umekabidhiwa moja kwa moja kwa wanafunzi ikiwa ni moja ya juhudi za Taasisi kuinua kiwango cha elimu kwa kuwahamasisha wanafunzi mashuleni. Katika harakati zake za kuinua kiwango cha elimu shuleni Msinune na kurahisisha upatikanaji wake, pamoja na kugawa vifaa vya kujifunzia na kufundishia kwa wanafunzi na walimu; Taasisi ya Flaviana Matata imefanikiwa kujenga na kukarabati madarasa, kujenga vyoo kwa ajili ya walimu na wanafunzi na kutoa msaada wa madawati. 


  Akizungumza wakati wa kupokea msaada Kaimu Mkuu wa Shule ya Msinune alisema kwamba tangu taasisi ya Flaviana Matata ianze kutoa misaada shuleni hapo kumekuwa na upungufu wa utoro kwa wanafunzi na pia idadi ya wanafunzi waliomaliza darasa saba imeongezeka kutoka 18 waliomaliza mwaka 2015 mpaka 46 kwa mwaka 2016. Pia ufaulu wa wanafunzi umeongezeka kwa asilimia 2.64; mwaka 2015 wanafunzi 5 walichaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari na kwa 2016 wanafunzi 14 walichaguliwa. Akielezea changamoto zinazowakabili, Kaimu Mkuu wa Shule amezielezea kwamba ni pamoja na Elimu kukosa kipaumbele wilayani Bagamoyo, upungufu wa vyumba vya madarasa, uhaba wa walimu (shule ina walimu 6), ukosefu wa nyumba za walimu na mila na desturi za wakazi wa eneo hilo ambao wanafanya jitihada kuzuia watoto wa kike wasiendelee na elimu ya sekondari ili waweze kuolewa, hii hupelekea wazazi wa watoto wa kike kuwalazimisha wajifelishe wakati wa mitihani ya kumaliza darasa la saba. 
  Akiongea wakati wa kukabidhi misaada hiyo, mwanzilishi wa Taasisi na Mlezi wa shule ya Msinune Flaviana Matata alisema kwamba Taasisi yake itaendelea kuisimamia na kujitahidi kuiboresha shule hiyo kwa kumalizia kujenga madarasa yaliyobaki na kuangalia namna ya kuwashirikisha wadau wengine wa elimu na serikali kushughulikia nyumba za walimu.


older | 1 | .... | 1501 | 1502 | (Page 1503) | 1504 | 1505 | .... | 3270 | newer