Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1496 | 1497 | (Page 1498) | 1499 | 1500 | .... | 3278 | newer

  0 0
  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  MWANAMUZIKI mahiri wa miondoko ya bongofleva, Mwasiti Almas "Chiti" amesema kuwa haoni sababu ya wanamuziki wa hapa nchini kwenda kufanya Video nchini Afrika Kusini wakati  hapa nchini bado tuna maandhari mazuri.

  Mwasiti amesema hayo wakati alipokuwa akizungumza na ripota wa Globu ya Jamii juu ya maandalizi ya uandaaji wa video ya wimbo wake mpya ambao anataraji kuufanya hivi karibuni.

  “nataka kufanya video wiki ijayo lakini nitafanya na mtayarishaji wa hapa ndani ambaye ni Msafiri wengi wamezoea kumwita Traveler hivyo kila mtu akae mkao wa kula kupokea nyimbo nzuri kutoka kwa Mwasiti” amema

  Amesema kuwa watu wengi wamekuwa wakimuambia kuwa amekaa kimya kwa muda mrefu hivyo anawaeleza kuwa amerudi na ladha ile ile ambayo imekuwa ikiishi kwa miaka mingi.

  Ametaja kuwa wanamuziki wengi hapa nchini wamekuwa wakifanya muziki wa Bigijii ambao uishi kwa muda mfupi, lakini mwasiti ni habari nyingine kwani yeye asipokuwepo muziki wake bado utaishi.

  0 0

  Mwanamuziki mkongwe ambaye alipotea katika fani ya muziki kwa kipindi kirefu kutokana na matatizo ya dawa za kulevya, Rehema Chalamila “Ray C” ameibuka na kusema yupo fiti na ameachana na uteja.

  Ray C ambaye amezungumza na ripota wa Globu ya Jamii katika studio za THT ambako yupo katika maandalizi ya kurekodi nyimbo ambazo zitamtambulisha upya katika ramani ya muziki wa bongo fleva.

  “nakwambia niko fiti na tayari nimesharekodi nyimbo tano kwa mtayarishaji Johban John a nyingine nafanyia hapa THT kwa Imma the boy ambapo moja ya kazi yangu nimemshirikisha bushoke” amesema Ray C

  Ray C amesema kuwa kwa sasa yeye ameamua kufanya muziki kama zamani na kamwe hawezi rudia kutumia dawa za kulevya kwani anajua zilivyomtesa kwa kipindi kirefu kiasi cha kushusha utu wake.

  Amesema kuwa kwa sasa anachohitaji ni sapoti ya wadau wa muziki ambao wanaweza kumsaidia kuutoa muziki wake hapa ulipo na kuupeleka katika soko la kimataifa kwa kumsaidia kufanya video na mahitaji madogo madogo.

  Ray C amewashukuru wadau mbalimbali ambao wamemsaidia mpaka kufikia hapo na kumtaja Ruge Mutahaba kuwa ni miongoni mwa watu waliopo katika mstari wa mbele kuakikisha yeye amekuwa sawa.

  0 0  0 0  0 0

  UPDATES: Marehemu mpendwa wetu Eyshe Max amezikwa jana  katika makaburi ya Geneva, mazishi yaliyohudhuriwa na watu wengi ikiwemo jumuiya ya Watanzania waishio huko, ndugu, jamaa na marafiki. 
  Marehemu Eyshe atakumbukwa daima kwa ucheshi na upendo wake na zaidi  zaidi kwa ucha Mungu wake. Tunamuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi, na aifariji familia yake aliyoiacha nyuma. 
  Amin.🙏🏾

  0 0

  Na JOHN KITIME wa 
  www.johnkitime.co.tz
  Januari 2013, niliandika makala kuhusu nilivyouona muziki mwaka 2012. Naona nirudie makala ile kama nilivyoiandika, na kukuachia msomaji kulinganisha na hali ilivyokuwa 2016.
  Mwaka 2012 ndio huoo umetokomea, ni vizuri kuangalia yaliyopita ili kujitayarisha na yajayo. 

  Muziki wa nchi yetu ulitawaliwa na muziki wa Bongoflava, Taarab, muziki wa bendi, matarumbeta, muziki wa enjili, na muziki wa kiasili. Si siri kuwa muziki wa Bongoflava ndio uliokuwa ukitawala katika vyombo vya habari na sehemu nyingi za maonyesho. Muziki huu ulikuwa  ukifuatiliwa na muziki wa Taarab na muziki wa enjili.  Katika muziki wote huu jambo lililokuwa wazi ni kuwa waimbaji ndio waliokuwa wakipewa kipaumbele katika tasnia hii.  
  Waimbaji katika aina zote za muziki uliotajwa hapo juu ndio waliotajwa sana na kupewa sifa kwa ubora wa muziki. Kumekuweko na mashindano kadhaa ambayo yote yamejikita katika kutafuta vipawa vya waimbaji japo mara nyingi yamejitambulisha kama mashindano ya kusaka vipaji mbalimbali.
  Hakuna ubishi muziki wa dansi na muziki wa asili ndio muziki uliopewa muda mchache sana katika vyombo vya habari. Na hata katika muziki huo, bendi ambazo zimejikita kufuata mipigo ya Kikongo zilipewa nafasi zaidi kuliko bendi ambazo zimejichagulia njia nyingine za muziki wao.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Mjumbe wa Halimashauri Kuu ya CCM na MNEC Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (MB) akingalia burudani ya ngoma ya Mganda ambayo ilikuwa imeandaliwa kwa ajili ya kumkaribisha katika ofisi ya CCM Mkoa wa Ruvuma kwa ajili ya kuzungumza na Viongozi wa CCM Mkoa wa Ruvuma
  Mjumbe wa Halimashauri Kuu ya CCMna MNEC Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (MB)amemkabidhi kadi ya CCM Bwana Musa Ndomba ambaye amerudi CCM mwanzo alikuwa mwana chama wa Chadema na Diwani wa Kata ya Tanga manispa ya songea na mwenyekiti wa wawanafunzi katika chuo kikuu cha mtakatifu John kilichopo Songea shughuli hiyo imefanyika katika ukumbi wa ccm mkoa wa Ruvuma
  Mjumbe wa Halimashauri Kuu ya CCMna MNEC Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (MB)akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya CCM Mkoa wa Ruvuma wakatialipofika hapo kwa ajili ya kuongea na viongozi wa ccm mkoa wa Ruvuma kushoto ni Mwenyekiti CCM mkoa wa Ruvuma Bwana Oddo Mwisho na anaye fuatia ni katibu wa CCM Mkoa wa Ruvuma Verena Shumbusho.
  Mjumbe wa Halimashauri Kuu ya CCM na MNEC Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (MB)akizungzumza na viongozi wa CCM mkoa wa Ruvuma katika ukumbi wa CCM Mkoani Ruvuma
  Waziri Mkuu yupo mkoani Ruvuma kwa ziara ya kikazi.

  Picha na Chris Mfinanga

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewaagiza Majaji na Mahakimu wanawake kote nchini kupambana ipasavyo katika kukabiliana vitendo vya rushwa,unyanyasaji kijinsia na rushwa ya ngono ili kusaidia wanawake kupata haki zao za msingi bila kubaguliwa katika jamii.

  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa agizo hilo jijini Dar es Salaam wakati anafungua Mkutano Mkuu wa NANE wa Chama cha Majaji na Mahakimu wanawake Tanzania (TAWJA).

  Makamu wa Rais pia ameonya kuhusu vitendo vya rushwa ya ngono inayofanywa na baadhi ya watendaji wenye madaraka na kusema tabia hiyo ni mbaya na lazima ikomeshwa mara moja katika jamii.

  Amesema kuwa vitendo hivyo vya rushwa ya ngono huzuia na kukwamisha juhudi za wanawake kufikia huduma za kijamii na za kiserikali ipasavyo ikiwemo elimu, ajira na haki kwa ajili ya ustawi wa wanawake.

  Aidha Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amekishukuru Chama cha Dunia cha Majaji Wanawake (IAWJ) kwa mchango na msaada wake kwa TAWJA katika programu ya miaka mitatu ya kupambana na matumizi mabaya ya madaraka na rushwa ya ngono.

  Makamu wa Rais pia ameipongeza Wizara ya Katiba na Sheria, Shirika la UN Women na wadau wengine wa TAWJA kwa kuunga mkono mapambano ya aina zote za ubaguzi na ukatili dhidi ya wanawake na watoto nchini.

  Amesema elimu ya haki za Binadamu iliyotolewa na Chama hicho imeleta badiliko kwa wengi kwa njia ya mafunzo na machapisho na jitihada hivyo lazima ziongezwe ili huduma hiyo iweze kuwafikia wananchi wengi zaidi kote nchini.

  Amesisitiza wanachama wa Chama cha TAWJA waendelee kutoa msaada katika kuwasaidia wanawake na watoto ambao wanakandamizwa kwa kunyimwa haki zao katika jamii ili waweze kupata haki zao nchini.

  Kwa upande wake, Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mohamed Chande Othman amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa mkakati wa uimarishaji wa shughuli za mahakama nchini unaendelea vyema lengo likiwa ni kutenda haki kwa wananchi kote nchini bila ubaguzi.Kauli mbiu ya Mkutano Mkuu wa NANE wa Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania (TAWJA) “Kuongoza njia kufikia hitajio la upatikanaji wa haki kwa wote na kwa wakati”.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa nane wa Majaji Wanawake ulioandaliwa na Chama Cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) unaofanyika kila baada ya miaka miwili na mkutano wa mwaka huu ulikuwa na kauli mbiu isemayo Kuongoza njia kufikia hitajio la upatikanaji wa haki kwa wote na kwa wakati.

  Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akihutubia wakati wa mkutano wa nane wa chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania uliofanyika kwenye ukumbi wa PSPF Golden Jubilee jijini Dar es Salaam.

  Mhe. Othman Makungu, Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Zanzibar,Mhe. Othman Makungu,akitoa nasaha zake wakati wa uzinduzi wa mkutano wa nane wa chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA)

  Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania Jaji Imani Aboud akitoa salaam za ufunguzi wa mkutano wa nane wa chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA)

  Sehemu ya waliohudhuria wakiwa makini katika kuchukua yale yaliosemwa na Mhe. Makamu wa Rais wakati wa uzinduzi wa mkutano wa nane wa Chama Cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA)


  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0  0 0

  BMGHabari
  Bodi ya Filamu nchini imewahamasisha watanzania kuongera ari ya kuzipigia kura filamu za kitanzania zinazowania tuzo za Africa Magic Viewers Awards (AMVA 2017) za nchini Nigeria.
  Katibu Mtendaji wa bodi hiyo, Bi Joyce Fissoo (pichani juu) ametoa hamasa hiyo hii leo, wakati akihojiwa kwenye kipindi cha Power Break Fast On Saturday kinachoendeshwa na watangazaji Philip Mwihava na Godfrey Kusolwa.
  “Filamu hizo ni Naomba Niseme, Aisha na Home Coming ambazo zinawania tuzo za filamu bora na Siri ya Mtungi ambayo inagombea filamu bora ya lugha ya Kiswahili. Niwaase Wanzania, ushindi wa filamu hizi ni sisi kuwapigia kura hawa vijana wetu ambao wameshika bendera yetu kwenda kutuwakilisha kule Nigeria, niwasihi waweze kuzipigia kura na wahakikishe wanahamasisha marafiki zao pia kuzipigia kura ili nafasi zote tuzo zije Tanzania”. Amesisitiza Fissoo.
  Naye Mtayarishaji wa filamu nchini, Staphord Kihole (pichani) ambaye pia alikuwa kwenye kipindi hicho, ametumia fursa hiyo kuwaomba watanzania kuzipigia kura filamu za kitanzania ili zishinde tuzo za Africa Magic Viewers Choice Awards ikiwemo filamu yake ya "Naomba Niseme" inayowania vipengele viwili, kikiwemo kipendele cha Best East Africa na Best All Africa kinachoamuliwa na majaji.
  Ili kuzipigia kura filamu za Tanzania ambazo ni Naomba Niseme, Aisha na Home Coming, unapakua Application ya We Chat, unajisajiri kwenye Africa Magic kwa kutumia nambari ya simu na kisha unatafuta kipengele cha AMVCA na utaweza kupiga kura kadri upendavyo ambapo mtu mmoja anaweza kupiga kura hadi 100 kwenye filamu tofauti tofauti.
  Bonyeza Hapa  Au play hapo chini kusikiliza sauti Credit: Clouds Fm

  0 0
 • 01/07/17--03:36: save the date...

 • 0 0

  Mratibu wa mpambano wa ngumi Jocktan Masasi katikati akiwainuwa mikono juu mabondia Mfaume Mfaume kushoto na Mohamed Matumla Baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga feb 2 katika ukumbi wa uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es salaam.

  Mmoja wa Viongozi wa TPBC Joe Anena  katikati akiwainuwa juu mikono mabondia Mfaume Mfaume kulia na Mo0hamed Matumla wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika Feb 5 katika uwanja wa ndani wa Taifa. kulia kabisa ni mmoja wa wajumbe wa TPBC Chese Masanja 

  Bondia Mfaume Mfaume akisaini mbele ya mwanasheria Hussein Mlinga wanaoshuhudia ni  wajumbe wa kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBC Chese Masanja (kushoto) na mmoja wa Viongozi wa TPBC Joe Anena 
  Bondia Mohamed Matumla akisaini mbele ya mwanasheria Hussein Mlinga anaeshughudia ni mmoja wa wajumbe wa kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBC Chese Masanja na Mmoja wa Viongozi wa TPBC Joe Anena.
  Picha na Super Boxing News 

  0 0

  Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Dkt. Juma Ally Malewa(pichani) amefanya Mabadiliko ya Uongozi kwa baadhi ya Wakuu wa Magereza Mikoa na vituo mbalimbali hapa nchini.

  Mabadiliko hayo ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza SACP Katos Rugainunura amehamishiwa Makao Makuu ya Magereza sehemu ya Utawala na nafasi yake inakaimiwa na Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Mzee Nyamka aliyekuwa Mkuu wa Utawala Magereza Mkoani Morogoro. 

  Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza SACP Antonino Kilumbi aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma amehamishwa kwenda Makao Makuu ya Magereza kuwa Mkuu wa Kikosi cha Ujenzi na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza SACP Julius Sang’udi aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mbeya.

  Aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kilimanjaro Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Anderson Kamtiaro anaenda kuwa Afisa Mnadhimu Magereza Mkoani Arusha na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Hassan Mkwiche ambaye alikuwa ni Mkuu wa Gereza Kuu Karanga, Moshi. 
  Aliyekuwa Mkuu wa Gereza Same Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Evarist Katego anakwenda kuwa Mkuu wa Gereza Kuu Karanga, Moshi. Aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mwanza Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza SACP Uwesu Ngarama amehamishiwa Makao Makuu kuwa Boharia Mkuu wa Jeshi na nafasi yake inachukuliwa na aliyekuwa Afisa Mipango wa Jeshi ACP Athuman Kitiku.

  Aidha, aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoani Mtwara, Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Musa Kaswaka anakwenda Makao Makuu Kitengo cha Ukaguzi na nafasi yake kuchukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Ismail Mlawa aliyekuwa Mkuu wa Kiwanda cha Samani Gereza Kuu Ukonga. Aliyekuwa Afisa Mdhibiti wa Fedha wa Jeshi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza SACP Gideon Nkana anakwenda kuwa Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga, Dar es Salaam na nafasi yake kuchukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Chacha Jakson.

  Wengine ni pamoja na aliyekuwa Afisa Mnadhimu wa Magereza Mkoa wa Mbeya ACP Kijida Mwakingi anakaimu nafasi ya Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Abdalah Misanga anayetoka Gereza Mgumu kwenda kuwa Mkuu wa Gereza Msalato, Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP John Itambu anayetoka Gereza Kilosa kwenda kuwa Mkuu wa Kiwanda cha Samani Gereza Kuu Ukonga.

  Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Erasmus Kundy anayetoka Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Ukonga kwenda Makao Makuu Kitengo cha Habari, Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Julius Ntambala aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Ujenzi Makao Makuu anabakia Makao Makuu Kitengo cha ujenzi kuwa Msaidizi wa Mkuu wa Kitengo, Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Sylivester Mrema anayetoka Gereza Idete kwenda Gereza Ubena kuwa Mkuu wa Gereza.
  Aliyekuwa Mkuu wa Gereza Ubena Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Shaba Zephania anakwenda Magereza Mkoa wa Pwani kuwa Afisa Mnadhimu, Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Solomon Urio anayetoka Makao Makuu kwenda Magereza Mkoa wa Dar es Salaam kuwa Afisa Mnadhimu pamoja na aliyekuwa Boharia Mkuu wa Jeshi la Magereza Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza SACP George Kiria amehamishiwa Makao Makuu Kitengo cha Uhasibu .

  Mabadiliko hayo ni ya kawaida na yanalenga kuboresha utendaji kazi na ufanisi wa Jeshi la Magereza.

  Imetolewa na:
  Lucas Mboje - ASP
  Ofisa Habari wa Jeshi la Magereza
  Makao Makuu ya Magereza Tanzania Bara
  07 Januari, 2017.

  0 0

   Makamu wa Pili a Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiweka jiwe la Msingi la Ujenzi wa Ukuta wa kuzuia maji ya Bahari hapo Mizingani Forodhani Mjini Zanzibar ikiwa ni shamra shamra za kusherehekea miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Wa kwanza kushoto ni Waziri wa Fedha na Mipango wa SMZ Dr. Khalid Salum Mohamed ambapo wa nyuma yake ni Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mh. Zubeir Ali Maulid.
  Mandhari nzuri ya kuvutia ya muonekano wa Ukuta wa kuzuia maji ya Bahari hapo Mizingani Forodhani Mjini Zanzibar  ambapo ujenzi wake umewekwa jiwe la Msingi  na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Utunzaji na Uhifadhi wa Mji Mkongwe wa Zanzibar Nd. Issa Sarboko Makaran akimpatia maelezo Balozi Seif jinsi ya wajenzi wa Ukuta wa Kuzuia Maji ya Bahari Mizingani wanavyozingatia  uhifadhi wa urithi wa Dunia uliomo ndani ya Mji Mkonhgwe.
   Balozi Seif akizungumza na Wananchi katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Ukuta wa kuzuia maji ya Bahari hapo Mizingani Forodhani Mjini Zanzibar.
  Kikundi cha Utamaduni cha Mkoa wa Mjini Mgharibi kikifanya vitu vyake wakati wa kutoa burdani kwenye hafla ya ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Ukuta wa kuzuia maji ya Bahari hapo Mizingani Forodhani Mjini Zanzibar. Picha na OMPR - ZNZ. 

  0 0

  Taja jina la Bitebo popote ulipo tanzania, na hata dunia nzima kwa jumla, na dhana ya utaalamu wa kunyoa nywele inamjia yeyote anayelisikia. Unajiuliza, je ni kwa nini jina hilo limekuwa maarufu hivyo hadi inashangaza? 
  Globu ya Jamii ilitembelea kiwanda cha kutengeneza mitindo ya nywele cha New Bitebo Hair Designer maeneo ya Magomeni Mikumi, jirani na ukumbi maarufu wa Lango la Jiji jijini Dar es salaam na kukutana na Mkurugenzi Mtendaji na mmiliki wa kiwanda hicho – Abdallah Bitebo ambaye badala ya kutuambia ni nini siri ya mafanikio yake akaamua kututembeza kiwandani humo ili kujionea wenyewe. 
  "Sera ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli ni ya viwanda. Nasi hapa tunamuunga mkono kwa kuwa na kiwanda cha kutengeneza mitindo ya nywele na ndevu za watu kwa weledi wa kimataifa. 
  "Mzee Magufuli kila siku unamsikia kiwanda sio lazima kikwe kikuuubwa, bali hata cha chumba kimoja ni kiwanda. Sembuse ya sisi hapa ambapo tuna nyumba nzima", amesema Bitebo ambaye kiwanda chake hutembelewa sana na nyota wa tasnia mbalimbali ikiwemo filamu, soka na muziki na hata wa dini na siasa. 
   Hakika anastahili sifa zote hizo na zaidi. Na si ajabu kiwanda hicho kikachaguliwa kwa kura nyingi mno na kutwaa tuzo ya kuwa Best Hair Designer wa Tanzania mwaka 2016. Jionee mwenyewe…
  Bango lililopo nje ya kiwanda cha kutengeneza mitindo ya nywele cha New Bitebo Hair Designer maeneo ya Magomeni Mikumi, jirani na ukumbi maarufu wa Lango la Jiji jijini Dar es salaam 
  Mkurugenzi Mtendaji na mmiliki wa kiwanda hicho Abdallah Bitebo (kati) akiwa na jeshi lake la kazi
  Mkurugenzi Mtendaji na mmiliki wa kiwanda hicho Abdallah Bitebo (kati) akiwa na jeshi lake la kazi
  Mteja akipigwa scrub ya nguvu katika kiwanda cha kutengeneza mitindo ya nywele cha New Bitebo Hair Designer. Wenyewe wanakwambia unaingia mzee unatoka kijana. Ukiwa kijana unatoka mtoto...

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye Mkutano wa Nane wa mwaka wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) kwa ajili ya kuufunga leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman na kulia ni Mwenyekiti wa TAWJA ambaye pia ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Tanga Mhe. Iman Abood.  
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akimsikiliza Mwenyekiti wa TAWJA Mhe. Jaji Iman Abood (hayupo pichani) akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Nane wa mwaka wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA). Katikati ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman na kushoto ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifungua  Mkutano wa Nane wa mwaka wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA leo jijini Dar es salaam.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyekiti wa TAWJA Mhe. Jaji Iman Abood wakati wa Mkutano wa Nane wa mwaka wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA leo jijini Dar es salaam

    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea risala toka kwa Mwenyekiti wa TAWJA Mhe. Jaji Iman Abood wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Nane wa mwaka wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA)  leo jijini Dar es salaam
  Sehemu ya wageni na wajumbe wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Nane wa mwaka wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA)  leo jijini Dar es salaam.

  0 0


  Dk. Senkoro aliyegombea urais mwaka 2005 kupitia Chama cha TPP –Maendeleo alifariki dunia ghafla Januari 4, mwaka huu wakati akipelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa ajili ya matibabu.

  Shughuli ya kumuaga Dk. Senkoro ilianzia leo nyumbani kwake, Tabata Segerea, kisha mwili wake ulihamishiwa katika Kanisa la Winners Chapel International, Banana, Ukonga kwa ibada fupi, ambapo viongozi walitoa salamu za rambirambi. 

  Mbali na Makinda, viongozi wengine waliohudhuria ni; Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM,  Humphrey Polepole na Mwnyekiti wa Chadema Wilaya ya Ilala, Dk. Makongoro Mahanga.Akizungumza baada ya ibada hiyo, Makinda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), alisema alipokea kwa mshtuko mkubwa kifo cha rafiki yake na mdogo wake huyo katika siasa.

  Alisema Dk. Senkoro alijaribu kuwa rais mwaka 2005, lakini Mungu akamwambia anaweza kuwatumikia wananchi kwa njia nyingine kama alivyofanya.“Tumemuamini Kristo hivyo hatuwezi kufika kwake bila kulala na Anna amefariki dunia katika Ukristo, swali, jiulize wewe kama ungekuwa Senkoro ungekwenda wapi?” alihoji Makinda.

  Alisema familia yake ikae kwa amani na kwamba waamini Anna yuko kwa Mungu amekwenda kutuandalia makao.Naye Dk. Mahanga akitoa salamu za Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na rafiki yake, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, alisema wamesikitishwa na kifo hicho na kuwapa pole ndugu, jamaa na marafiki walioondokewa na kipenzi chao.

  "Sisi kama chama tumempoteza kamanda mwenzetu na mpambanaji toka alipojiunga na chama mwaka juzi Julai, yote ni mapenzi ya Mungu," alisema Dk. Mahanga.Kwa upande wake, Polepole akitoa salamu kwa niaba ya Mwenyekiti wa chama hicho, Rais John Magufuli pamoja na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana alisema:

  "Tuishi maisha mema na yenye kutenda haki kwa sababu Biblia inasema taifa linalotenda haki Mungu uliinua pamoja na kuwa waaminifu kwa uajibikaji na kutenda haki."Dk. Senkoro wakati wa uhai wake aliwahi kufanya kazi katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika Gereza la Ukonga, ameacha watoto watu na wajukuu wawili.

  Msemaji wa Taasisi ya JKCI, Maulid Kikondo, alisema mara ya mwisho kabla ya kufikwa na mauti, Dk. Senkoro alifika hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu na kufanyiwa vipimo kadhaa ambavyo madaktari waligundua tatizo lililokuwa likimsumbua.

  Alisema jopo la madaktari bingwa wa taasisi hiyo walikuwa na nafasi ya kuokoa maisha ya Senkoro iwapo angekubali kulazwa kwa ajili ya matibabu katika kitengo hicho.Alisema baada ya vipimo alishauriwa kulazwa kutokana na hali yake, lakini Dk. Senkoro alikataa na kutaka kurudi nyumbani. 
  Spika mstaafu wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lililokuwa na mwili wa aliyekuwa mgombea wa Urais wa Kwanza Mwanamke marehemu Anna Senkoro katika Kanisa la Wninner Chapels International jijini Dar es Salaam jana, Marehemu alizikwa katika makaburi ya Kinondoni. 
   Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza la marehemu Anna Senkoro.
   Ndugu wa marehemu.
   Wafiwa.
   Wafiwa. 

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii


  MWANAMUZIKI wa muziki wa kizazi kipya Benard Paul 'Ben Pol, ameachia wimbo mpya unaoitwa 'Phone' akimshirikisha  mwanamuziki kutoka nchini Nigeria Mr. Eazi. 

  Akizungumza kuhusiana na kuachiia wimbo huo mwanzoni mwa mwaka Ben Pol amesema kuwa wimbo huo ameutengeneza katika studio ya One love records, iliyopo jijini Dar es Salaam chini ya mtayarishaji Tiddy Hotter. 

  Ben Pol alisema ujio wa wimbo huo ni moja ya mipango yake ya mwaka 2017 na ameanza kwa kutoa wimbo huo wa 'Phone'. na tayari wimbo huo umeanza kusikika kupitia vituo mbalimbali vya radio, huku ujio wa video yake ukiwa njiani. 

  "Wimbo wa Phone ni moja ya malengo yangu ya mwaka huu na ndiyo ujio wangu wa 2017, naomba wapenzi waupokee na kuusikiliza kila mtu ataelewa nini nimejipanga kupitia mwaka huu"alisema Pol. 

  Mwanamuziki huyo anayetamba na nyimbo mbalimbali ikiwemo pamoja na, Moyo Mashine, Maneno, Sofia, Pete, Maumivu, Samboira na ameshirikishwa kwenye wimbo wa Darasa unaotamba kwa sasa nchini unaitwa muziki.

  0 0

  Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ally Hapi leo ametembelea kituo cha Polisi cha Msimbazi jijini Dar es salaam ambacho kilipatwa na ajali ya moto siku za hivi karibuni na kutoa msaada wa mifuko 100 ya saruji sawa na tani 5.
  Katika ziara yake kwenye kituo hicho, Hapi ametembelea kambi ya makazi ya askari na familia zao iliyoko nyuma ya kituo hicho ambapo amekabidhi mifuko hiyo ya Saruji kwa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala Ernest Matiku na kuagiza kuwa saruji hiyo itumike kwa ukarabati wa jengo zima la kambi hiyo ambayo inakaliwa na familia 72 za askari.

  Kaimu Mkuu wa Mkoa ameeleza kuwa Polisi wanafanya kazi kubwa ya kulinda amani na usalama na hivyo jamii haina budi kuwaunga mkono.
  Kwa upande wake Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi Ilala Ernest Matiku ameeleza kuwa wanamshukuru Kaimu Mkuu wa Mkoa kwa msaada huo kwani jengo lao limechakaa sana hali inayohatarisha usalama wa askari na familia zao.Hivyo wataanza ukarabati mara moja vifaa vitakapo kamilika na kila kitu kitafanyika kama ilivyo kusudiwa.

older | 1 | .... | 1496 | 1497 | (Page 1498) | 1499 | 1500 | .... | 3278 | newer