Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel Catalog



Channel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1497 | 1498 | (Page 1499) | 1500 | 1501 | .... | 3278 | newer

  0 0




  dar-1
  Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (MAZINGIRA) na mwenyekiti wa kikao hicho   Januari Makamba akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu mkakati wa Serikali katika kupambana na uvuvi haramu nchini mara baada ya kumalizika kwa kikao kilichohusisha Wizara Saba kushoto ni  Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Charels Tizeba.dar-2
  Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Charels Tizeba akiwaeleza waandishi wa habari (Hawapo Pichani) athari za  uvuvi haramu na jinsi unavyoathiri uchumi wa nchi kushoto ni Naibu Waziri aOfisi ya Rais TAMISEMI Suleiman Jaffo.dar-2
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Suleiman Jaffo akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) na kutoa maagizo ya Serikali kwa wakurugenzi nchini hasa kwenye maeneo wanayojishughulisha na uvuvi kuwachukulia hatua maafisa uvuvi wanaoshindwa kutimiza wajibu wao wa kupambana na uvuvi haramu, kushoto ni Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na mwenyekiti wa kamati hiyo.
  PICHA NA BEATRICE LYIMO-MAELEZO.
  ………….
  Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
  Serikali imewaagiza wakurugenzi nchini hasa kwenye maeneo wanayojishughulisha na uvuvi kuwachukulia hatua maafisa uvuvi wanaoshindwa kutimiza wajibu kwa kushindwa kuzuia uvuvi haramu.
  Akizungumza baada ya kikao cha kamati kilichohusisha Wizara saba za Maliasili, Ulinzi, Nishati na Madini Tamisemi, Kilimo, Mifugo na Uvivi pamoja na Mambo ya Ndani Naibu Waziri TAMISEMI Suleiman Jaffo aliwataka watendaji hao kutumia agenda ya kupambana na uvuvi haramu kuwa agenda ya kudumu  katika vikao vyao.
  Alisema kuwa maafisa uvuvi hao wanatakiwa kupimwa wajibu na utendaji kazi kwa kuangalia ni kiasi gani wanajihusisha na masuala mazima ya kupambana na uvuvi wa kutumia mabomu.
  “Kuna baadhi ya mafisa uvuvi wanahusika na vitendo vya uvuvi haramu nchini hivyo kuanzia kesho wataanza kupimwa wajibu wao na kwa atakayeshindwa kutimiza wajibu atatolewa katika nyazifa hiyo”.
  Kwa upande wake Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Januari Makamba alisema kuwa nchi yetu inaeneo kubwa la bahari na kwa miaka kadhaa nchi yetu imekuwa na changamoto ya uvuvi haramu, hivyo tumeona kuna haja ya kuchukua hatua ya haraka katika kupambana na uharamia huo.
  Akifafanua zaidi kuhusu hilo Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Charels Tizeba alisema kuwa jambo la uvuvi haramu lisipochukuliwa kwa umakini litapelekea kuathiri uchumi wa nchi hivyo lengo la Serikali ni kukomesha uharibifu unaojitokeza sasa.
  Alisema ni aibu kwa taifa letu la Tanzania kuendelea kuvua kwa njia haramu kwani nchi nyingi kwa sasa zimeondoka katika uvuvi wa namna hiyo.Naye Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba alitoa wito kwa watanzania wote kushirikiana na Serikali katika kufichuwa wale wanaohusika na uvuvi haramu.Mwigulu Nchemba alisisitiza kuwa “kila mtanzania anawajibu wa kuwa makini katika kulinda rasilimali za majini tulizo nazo”.
  Kikao hicho ni utekelezaji wa agizo la Makamu wa Rais la kupambana na uvuvi haramu ambapo maazimio hayo yatafanyiwa kazi na kuahidi kukutana baada ya miezi sita kwa ajili ya kutafakari hatua zilizochukuliwa pamoja na kurekebisha pale patakapoonekana pana changamoto

  0 0


  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akizungumza kabla ya kuzindua matembezi ya UVCCM ya miaka 52 ya CCM, kwenye Viwanja vya Donge, Vijibeni, Wilaya ya Kaskazini Jimbo la Donge, mkoa wa Kaskazini Unguja.

  Vijana wakihamasika na kuonyesha kuwa tayari kuanza matembezi ya UVCCM ya miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibara, baada ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, kutoa maneno yaliyoshiba nasaha, wakati wa hotuba yake ya kuzindua matembezi hayo leo.

  Mpogolo akikabidhi picha ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere kwa mmoja wa viongozi wa matembezi hayo
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Lodrick Mpogolo (wanne kushoto-mstari wa mbele), akizindua matembezi ya UVCCM ya Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar, kwa kutembea na vijana hao kutoka kwenye Viwanja vya Donge, Vijibeni, Wilaya ya Kaskazini Jimbo la Donge, mkoa wa Kaskazini Unguja. Picha zote na Bashir Nkoromo. 


  Matembezi yakaanza 
  .


  0 0

  BMGHabari
  Bodi ya Filamu nchini imewahamasisha watanzania kuongera ari ya kuzipigia kura filamu za kitanzania zinazowania tuzo za Africa Magic Viewers Awards (AMVA 2017) za nchini Nigeria.

  Katibu Mtendaji wa bodi hiyo, Bi Joyce Fissoo (pichani juu) ametoa hamasa hiyo hii leo, wakati akihojiwa kwenye kipindi cha Power Break Fast On Saturday kinachoendeshwa na watangazaji Philip Mwihava na Godfrey Kusolwa.

  “Filamu hizo ni Naomba Niseme, Aisha na Home Coming ambazo zinawania tuzo za filamu bora na Siri ya Mtungi ambayo inagombea filamu bora ya lugha ya Kiswahili. Niwaase Wanzania, ushindi wa filamu hizi ni sisi kuwapigia kura hawa vijana wetu ambao wameshika bendera yetu kwenda kutuwakilisha kule Nigeria, niwasihi waweze kuzipigia kura na wahakikishe wanahamasisha marafiki zao pia kuzipigia kura ili nafasi zote tuzo zije Tanzania”. Amesisitiza Fissoo.
  Naye Mtayarishaji wa filamu nchini, Staphord Kihole (pichani) ambaye pia alikuwa kwenye kipindi hicho, ametumia fursa hiyo kuwaomba watanzania kuzipigia kura filamu za kitanzania ili zishinde tuzo za Africa Magic Viewers Choice Awards ikiwemo filamu yake ya "Naomba Niseme" inayowania vipengele viwili, kikiwemo kipendele cha Best East Africa na Best All Africa kinachoamuliwa na majaji.

  Ili kuzipigia kura filamu za Tanzania ambazo ni Naomba Niseme, Aisha na Home Coming, unapakua Application ya We Chat, unajisajiri kwenye Africa Magic kwa kutumia nambari ya simu na kisha unatafuta kipengele cha AMVCA na utaweza kupiga kura kadri upendavyo ambapo mtu mmoja anaweza kupiga kura hadi 100 kwenye filamu tofauti tofauti.

  0 0

   WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameitaka kampuni ya TANCOAL Energy inayochimba makaa ya mawe kwenye mgodi wa Ngaka itimize masharti ya mkataba iliouingia na Serikali mwaka 2008.

  Kampuni ya TANCOAL iliundwa Aprili 3, 2008 na kampuni tanzu ya Atomic Resources Limited ambayo wakati huo ilikuwa ikijulikana kama Pacific Corporation East Africa (PCEA) na kwa sasa inaitwa Intra Energy (T) Limited ambayo hisa zake ni asilimia 70 na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) lenye asilimia 30 ya hisa.

  Ametoa kauli hiyo jana mchana (Ijumaa, Januari 6, 2017) mara baada ya kutembelea mgodi huo na kukagua shughuli za uzalishaji. Mgodi wa Ngaka uko wilaya ya Mbinga, mkoani Ruvuma na unamilikiwa na kampuni ya TANCOAL kwa ubia baina ya Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) na kampuni ya Intra Energy Corporation ya Australia.

  Kwa mujibu wa mkataba huo, ilikubaliwa kwamba mbali ya kuzalisha makaa ya mawe, kampuni hiyo ilipaswa kuzalisha umeme wa megawati 400 kutokana na makaa hayo. TANCOAL ina migodi miwili; Mbalawala na Mbuyura ambao umetengwa mahsusi kwa ajili ya kuzalisha umeme.

  “Kwenye mkataba tulikubaliana kuwa mtazalisha umeme lakini hadi hadi leo hamjaanza mnadai kuwa TANESCO wanawachelewesha. Nitafuatilia nione kama ni wao au la ili tujue ukweli,” alisema.

  Kwa mujibu wa mikataba huo, TANCOAL ilipaswa kugharamia dola za Marekani milioni 14.49 kwa ajili ya ujenzi wa barabara na madaraja ili kuwezesha malori makubwa na madogo yaweze kufika mgodini na kusomba makaa hayo.

  “Mlisema mngetengeneza barabara lakini hadi sasa bado hamjafanya hivyo na ndiyo maana malori yanaishia kule. Yangefika hapa moja kwa moja, mngeweza kubaini kwa urahisi mahitaji ya makaa ya mawe ni kiasi gani,” alisema Waziri Mkuu.

  Hivi sasa, malori ya kutoka mgodini yanashusha makaa yaliyochimbwa kwenye eneo lililokodishwa na TANCOAL la Amani Makolo ambalo liko umbali wa km.55 kutoka mgodini na malori makubwa yanapakia makaa hayo kutoka kwenye eneo hilo jambo ambalo linazidisha gharama za usafirishaji.

  Kwa mujibu wa mkataba huo, TANCOAL ilipaswa kuwekeza mtaji wa Dola za Marekani milioni 82 lakini hadi sasa imewekeza kiasi cha dola milioni 14 ambazo ni sawa na asilimia 12 tu ya ahadi iliyotolewa.

  “Makubaliano yalikuwa ninyi mtawekeza Dola za Marekani milioni 81.69 lakini hadi sasa mmetumia dola za Marekani milioni 14, hamjafikia hata nusu,” alisema Waziri Mkuu.

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemtaka Mwenyekiti wa Bodi ya NDC, Dk. Samuel Nyantahe afuatilie kwa makini mambo yanayoendelea ndani ya shirika hilo. “Wewe unaendesha vikao lakini haya ndiyo mambo yanayoendelea kwenye taasisi unayoiongoza,” alisema.

  Alimtaka afuatilie pia uwasilishaji wa mkataba huo kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili vipengele vinavyoibana NDC kiuendeshaji na kupata gawio viweze kuangaliwa upya.

  Wakati huo huo, Waziri Mkuu amewapongeza viongozi wa kampuni ya TANCOAL kwa kuwashirikisha wajasiriamali wadogo kupata teknolojia ambayo itasaidia kupunguza tatizo la ukataji miti kwa matumizi ya kuni na mkaa.

  Alisema mgodi huo umeanza kuwanufaisha wenyeji kwani ameona kazi nzuri inayofanywa na kikundi cha akinamama cha Mbalawala (mbalawala Women Group) ambacho kinatumia vumbi la makaa hayo (ambayo ni mabaki) kutengeneza mkaa wa kupikia majumbani (briquettes).

  “Hii teknolojia ikisambazwa kwenye shule, mahospitali na kwenye magereza itasaidia kupunguza matumizi makubwa ya kuni yanayofanywa na taasisi hizi,” alisema.

  Meneja wa kikundi hicho, Bibi Leah Kayombo alisema wanatumia chengachenga na vumbi la makaa hayo kwa kuchanganya na kemikali nyingine ili kupunguza joto halisi la makaa hayo, jambo linalowezesha mkaa huo kutumika majumbani bila kuharibu masufuria.


  IMETOLEWA NA
  OFISI YA WAZIRI MKUU
  JUMAMOSI, JANUARI 7, 2017.

  0 0


  Aliyekuwa mwana chama wa Chadema na Diwani wa Kata ya Tanga Manispa ya Songea na Mwenyekiti wa Wawanafunzi katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu John kilichopo Songea, Musa Ndomba arudi CCM. Kufuatia maamuzi hayo, mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemkabidhi Ndomba kadi ya CCM na shughuli hiyo imefanyika katika ukumbi wa CCM mkoani Ruvuma.

  0 0

  Rais a Zanzibar na Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia kuashiria uzinduzi wa Skuli mpya ya Sekondari Mkanyageni Mkoa wa Kusini Pemba,iitwayo Mohamed Juma Pindua, ikiwa ni shamara shamara za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar(kushoto) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe,Riziki Pembe Juma,[Picha na Ikulu.] 07Jan 2017.
  Rais a Zanzibar na Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikata Utepe kuashiria uzinduzi wa Skuli Sekondari Mkanyageni Mkoa wa Kusini Pemba, ikiwa ni shamara shamara za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar (kushoto) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe,Riziki Pembe Juma, (kulia) Mama Mwanamwema Shein,
  Rais a Zanzibar na Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe,Riziki Pembe Juma pamoja na Viongozi mbali mbali walipotembelea chumba cha Kompyuta mara baada ya kuizindua Skuli Mpya ya Sekondari ya Mkanyageni,iliyopewa jina la Mohamed Juma Pindua,katika Kijiji cha Mkanyageni Mkoa wa Kusini Pemba, ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
  Rais a Zanzibar na Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiangalia Vitabu mbali mbali wakati alipotembelea madarasa mbali mbali na maabara baada kuizindua Skuli Mpya ya Sekondari ya Mkanyageni,iliyopewa jina la Mohamed Juma Pindua,katika Kijiji cha Mkanyageni Mkoa wa Kusini Pemba, ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar (kushoto) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe,Riziki Pembe Juma.


  0 0

  Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Maudline Castico akifungua pazia kuashiria uwekaji wa Jiwe la msingi la nyumba za wafanyakazi wa Hospitali ya Makunduchi, Mkoa Kusini Unguja ikiwa ni miongoni mwa maadhimisho ya miaka 53 ya Mpinduzi ya Zanzibar.
  Mkuu wa Mkoa Kusini Unguja Idrissa Muslim Hija akizungumza na wananchi wa Makunduchi baada ya uwekaji wa jiwe la msingi la katika la nyumba za wafanyanyakazi wa Hospitali hiyo, wa tatu (kushoto) Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman.
  Baadhi ya wananchi wa Makunduchi na vijiji jirani waliohudhuria uwekaji wa jiwe la msingi la nyumba za wafanyakazi wa Hospitali ya kijiji hicho wakimshangiria mgeni rasmi katika sherehe hiyo.
  Picha ya pamoja Waziri Maudline Castico na baadhi ya viongozi wa Mkoa Kusini Unguja na Wizara ya Afya baada ya sherehe za kuweka jiwe la msingi la nyumba zawafanyakazi wa Hospitali ya Makunduchi.

  Picha na Makame Mshenga/Maelezo Znz.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesifia huduma za tiba zinazotolewa kwenye kituo cha afya Mabada katika wilaya ya Songea licha ya kuwa ni kidogo.

  Akizungumza na watumishi wa kituo hicho, mwishoni mwa wiki, Waziri Mkuu alisema licha ya kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba ni mpya, bado huduma zinazotolewa ni za kuridhisha na amepata uthibitisho huo kwa baadhi ya wagonjwa waliolazwa kwenye kituo hicho.

  “Hali ya usafi ni nzuri, huduma zilizopo zinaridhisha… nimewadadisi baadhi ya wagonjwa wamesema huduma ziko vizuri. Mara nyingi huwa naongea nao kutaka kujua kama kuna rushwa, lugha kali kutoka kwa wauguzi au ukosefu wa dawa, lakini hapa wamenithibitishia kuwa huduma ziko vizuri, hongereni sana,” alisema.

  Alisema amelazimika kuyasema hayo mbele ya watumishi wote kwa sababu katika upya wa halmashauri, lazima kungekuwa na mizengwe na usumbufu katika upatikanaji wa huduma hali ambayo huwa inachosha wagonjwa hadi wanalazimika kutoa kitu kidogo ili wapatiwe huduma kwa haraka.

  Akizungumzia upatikanaji wa huduma za bima ya afya, Waziri Mkuu aliupongeza Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kusogeza huduma zake kwa jamii na kusaidia kuwapatia dawa, vifaa tiba na mashuka pea 25.

  Akitoa maelezo wakati akikagua majengo hayo, Meneja wa NHIF mkoa wa Ruvuma, Bw. Abdiel Mkaro alimweleza Waziri Mkuu kwamba taasisi hiyo imekisaidia kituo hicho kupata dawa na vifaa tiba vyenye thamani ya sh. milioni 27.

  “Tunashukuru sana kwa msaada wenu na ninaomba ufikishe salamu hizi kwa Mkurugenzi Mkuu wa NHIF. Nimeona pia mashuka mliyotoa, tunawashukuru sana.”

  Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kwa kuwapongeza viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba kwa kuwasajili wakazi wengi kwenye Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) jambo ambalo alisema linawapunguzia usumbufu wa kupata huduma za afya wakazi hao. 

  “Nimewauliza kule mawodini kama wamejiunga na kila niliyeongea naye alikuwa akinionyesha kadi yake. Ninawapongeza Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi wa Halmashauri, Baraza zima la madiwani pamoja na timu yenu kwa hii nzuri ya kuwashawishi wananchi wajiunge na mfuko huu,” alisema.

  Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba, Dk. Mustafa Waziri alisema wamekwishasajili kaya zaidi ya 3,000 kwenye Mfuko wa Afya ya Jamii. “Tunaishukuru NHIF ambayo pia ina wanachama 527 ambao ni watumishi wa Halmashauri lakini wana mpango wa kusajili wengine 500 ambao ni wajasiriamali na wanachama wa SACCOS,” alisema Dk. Waziri.

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alisema Serikali itaangalia uwezekano wa kukipandisha hadhi kituo hicho cha afya kiweze kutoa huduma za hospitali ya wilaya ili tiba zote za muhimu zipatikane hapo badala ya kuwalazimisha wagonjwa waende Songea mjini ambako ni umbali wa zaidi ya km.120 kutoka Madaba.

  “Kituo hiki kipo karibu sana na njia kuu iendayo Dar es Salaam, ikitokea ajali hapa kama hakuna huduma stahiki itakuwa shida kuwahudumia majeruhi; ndiyo maana tunaona ni vema kipandishwe hadhi ili kiweze kutoa huduma zote hapa hapa. Na kama ni kwenda Songea mjni basi iwe kwa dharura haswa,” alisema huku akishangiliwa.

  Hata hivyo, Waziri Mkuu aliitaka Halmashauri hiyo iangalie uwezekano wa kuongeza jengo la la ‘Grade A’ ili yawe mawili tofauti kwa ajili ya wanawake na wanaume. “Hali ilivyo hivi sasa, akilazwa mwanaume katika hiyo wodi, mwanamke hawezi kulazwa huko. Angalieni wa kuboresha na kuongeza jengo jingine ili kutoa huduma zote kwa wakati mmoja,” alisisitiza.

  0 0

   Rais mpya wa Ghana ambaye aliwahi kuwa wakili wa haki za kibinaadamu hapo zamani, Nana Akufo-Addo, ameapishwa rasmi leo kuwa kuwa rais mpya wa nchi hiyo, katika sherehe iliyofanyika katika uwanja wa Independence Square Jijini Accra, Ghana na kuhudhuriwa na viongozi kadha wa Afrika.

  Katika hotuba yake ya kwanza, Nana Akufo-Addo, alimsifu rais aliyemaliza muda wake madarakani, John Dramani Mahama, kwa namna alivyokiri kushindwa katika uchaguzi wa mwezi uliopita.

  Viongozi zaidi ya 14 kutoka nchi za Afrika walikusanyika katika mji mkuu wa Ghana, Accra, kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa rais huyo mpya, Nana Akufo Addo.
  Rais Akufo Addo, alimshinda Rais John Dramani Mahama, katika uchaguzi wa mwezi uliopita.

  Baada ya kuapishwa kwa rais, sasa viongozi waliohudhuria sherehe hiyo, watajadili namna ya kuhakikisha kuwa Rais wa Gambia, Yahya Jammeh, anaondoka madarakani.

  Kiongozi huyo amekataa kustaafu ingawa alishindwa katika uchaguzi wa Mwezi Disemba.

  0 0


  0 0

   Katibu tawala Mkoa wa Kagera Kamishina, Diwani Athumani akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe, Adeodata Agustine juu ya janga la moto katika soko kuu la Kayanga alipotembelea soko hilo kujionea athari za moto tarehe 7 Januari 2017.
  Katibu tawala Mkoa wa Kagera Kamishina, Diwani Athumani (katikati) akipata maelezo ya uratibu wa majanga kutoka kwa  Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brg. Jen. Mbazi Msuya wakati alipotembelea soko hilo kujionea athari za moto tarehe 7 Januari 2017 (kushoto) ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe, Adeodata Agustine.(PICHA ZOTE NA OFFISI YA WAZIRI MKUU)
   Baadhi ya Wafanyabiashara wa mazao ya nafaka wakipakia mabaki ya mazao  yao baada ya vibanda vyao vya biashara kuungua moto kufuatia moto uliozuka usiku wa saa 9:00 usiku wa tarehe 7Januari, 2017,  na kuteketeza sehemu ya soko kuu la Kayanga wilayani Karagwe kwa mara ya pili ikiwa limewahi kuungua tarehe 11 Machi 2016.

  0 0

  HUAWEI Technologies Co. Ltd offered the fund support to the State University of Zanzibar (SUZA) so as to help the operation of “remote TV-learning” programmes which aim to foster digital education material training and knowledge transfer for middle school students being part of their “Seeds for the Future” programme in Zanzibar. 
  The handing over ceremony of US $ 30,000 took place at Tunguu campus on Wednesday 4th January, 2017 in which His Excellency Mr. Xie Xiuouwu, the People’s Republic of China Consul General in Zanzibar on behalf of HUAWEI Technologies Co. Ltd handed over a cheque of the said amount.

  The event was also witnessed by Honourable Riziki Pembe Juma, the Zanzibar Minister of Education and Vocational Training who in her welcome speech to H.E. Mr. Xiuouwu informed that the government of Zanzibar is very much thankful for a number of notable contributions in many sectors offered by the government of the People’s Republic of China to Zanzibar. 
  “China has been a good friend and partner of Zanzibar since a long time ago, you cannot talk of Zanzibar’s development without mentioning China,” she said. “We welcome HUAWEI to share its global ICT experience to us, give their advice and participate in Zanzibar ICT innovation,” Hon. Riziki continued to say. 
  Hon. Riziki (2ndleft) and H.E. Mr. Xie Xiuouwu (centre) watch one of the lessons in the TV studio.

   The Chinese Consul General in Zanzibar, H.E. Mr. Xie Xiuouwu delivers his speech during the fund handing over ceremony.

  A group photo of the participants who witnessed the ceremony.


  0 0

   Amisi Tambwe akipambana na beki wa Azam Yahaya Mohamed  wakati wa mchezo wa hatua ya makundi wa kombe la Mapinduzi uliomalizika kwa Azam kutoka na ushindi wa goli 4-0.

  Na Zainab Nyamka,
   Globu ya Jamii, Zanzibar
  Timu ya Azam Fc imefanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali kwa kuipa kipigo cha mbwa mwizi cha bao 4-0  timu ya Yanga huku wakikalia usukani mwa kundi B katika kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar usiku huu.

  Mpira ulianza kwa kasi ikionekana Azam FC wamepania kupata bao la mapema Dakika ya kwanza ya mchezo na katika dakika ya 2 Azam wanapata bao kupitia kwa mfungaji wao John Bocco baada ya  kutokuwa na maelewano baina ya mabeki wa Yanga kwenye kuuokoa mpira uliookolewa na golikipa wa Yanga, Deogratius Munish "Dida".

  Katika dakika ya 9 Yanga wanafanya shambulizi langoni mwa Azam lakini Saimon Msuva anashindwa kumalizia kazi nzuri iliyofanywa na mrundi Amisi Tambwe.

  Baada ya kuonekana kutokuwa na maelewano katika safu ya ushambuliaji Kocha George Lwandamina anafanya mabadiliko kwa kumtoa  Juma Mahadhi na nafasi yake inachukuliwa na Emmanuel Martin katika dakika ya 36. Mpaka Mapumziko Azam 1 Yanga 0.
  Kipindi cha pili kinaanza kwa kila mmoja kumsoma mwenzake lakini katika dakika ya 54, Yahaya Mohamed  anaipatia Azam goli la pili baada ya kuunganisha krosi safi Abubakar Salum " Sure Boy".


  Wakiwa bado hawaamini Dk 81, Joseph Mahundi anaiandikia Azam goli la tatu baada ya kuachia shuti kali nje ya 18 na kuacha mashabiki wa Yanga wakiduwaa wakiwa hawaamini wanachokiona.
  Dk 84, Atta aliyeingia kipindi cha pili anaifungia timu yake bao safi akiunganisha  pasi ya Afful baada ya Mwashiuya kuukosa mpira, na mpaka mpira unamalizika Azam wanatoka kifua mbele wakiwa na alama 7 wakifuatiwa na Yanga wenye alama 6.  
  Timu hizi zinasubiri washindi wa mechi za kesho kwenye kundi A ili kupambana nazo kwenye hatua ya nusu fainali.

  Kikosi cha Yanga kilichopambana usiku huu.


  Kikosi cha Azam kilichopambana usiku huu.
   Timu zikiingia uwanjani wakati wa mchezo wa hatua ya makundi kati ya Yanga na Azam 
   Saimon Msuva akimtoka beki wa Azam wakati wa mchezo wa hatua ya makundi wa kombe la Mpoinduzi uliomalizika kwa Azam kutoka na ushindi wa goli 4-0.
   Juma Mahadhi akipambana katikati ya mabeki wa Azam wakati wa mchezo wa hatua ya makundi wa kombe la Mpoinduzi uliomalizika kwa Azam kutoka na ushindi wa goli 4-0.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0

   Jumuiya ya Watanzania Seattle, Marekani, wakiwa katika picha ya kumbukumbu baada ya kufanya hitma ya mwenzao marehemu Ubwa Jaha Ubwa aliyefariki dunia Desemba 30, 2015 na kuzikwa siku ya pili. Hitma hiyo imefanyika Itafanyika katika jengo Boys and Girls club. Spiritwood Manor Apartments jana Jumamosi.


  0 0

   Watoto  wakicheza mpira  katika  kiwanja  cha  kijiji  cha Mkaranga   wilaya ya  Kilolo  mkoani  Iringa  huku  wakitumia  vyandarua  kama  nyavu za  goli  jambo  ambalo  halikuwa  ni lengo  la  serikali  kugawa vyandarua   hivyo  kwa matumizi kama  haya ya viwanjani
  Mchezaji  akijiandaa kupiga  mpira  uliotengenezwa kienyeji  kwa karatasi

  0 0

  Tukianza na mtiririko mzima kwa wanasoka wa Tanzania, wapo wachezaji ambao waliuchukulia mpira wa miguu ni kama moja ya starehe, iwe labda kwa kupunguza vitambi, Pia wachezaji ambao walijitahidi kucheza mpira wakiwa na dhamira kubwa siku moja wapate angalu bahati waweze kucheza Simba au Yanga kwakuwa ndio vilabu vilikuwa vinaonekana angalau unaweza kuvaa vizuri na ukapata offer kuingia mziki bure na mambo Mengine ya hanasa.

  Labda kwa wale wenzangu wa miaka ya 70, 80 mpaka 90, wanaweza kujitetea kwamba miaka ile soka walikuwa wanacheza kama mapenzi tu hakukuwa na motisha ya kumfanya mchezaji aone kwamba pale uwanjani ndio kazini na soccer ndio maisha yake yote.

  Wadau wenzangu lazima mjue Mpira wa miguu ni Hazina kubwa sana, wachezaji wa ki Tanzania wanatakiwa walitambue hilo, Kwa mfano leo hii Mchezaji wa Tanzania anataka  nimlete Marekani aje kucheza Soccer, kutakuwa na changamoto kubwa  sana,

  Kwanza hautopata market nzuri, sisemi hivyo kwa kuwaponda wa Tanzania wenzangu la hasha, Kila kitu kipo wazi, ukiangalia katika Link ya FIFA, Tanzania wapo katika nafasi ya 156, na Marekani wapo katika nafasi ya 28, ki soccer,  wakati ukiangalia majirani zetu Rwanda na Burundi ni nchi ambazo zimekumbwa katika mikasa ya kivita kwa muda mrefu, lakini leo hii wametuzidi katika Link ya FIFA na wako mbali sana, Sasa utategemea vipi mchezaji wa Tanzania achukuliwe kama mchezaji wa kulipwa nchini Marekani, kwa kwenda kubadilisha kitu gani hasa katika soccer?

  Mimi binafsi nawakubali wachezaji wetu wapo wazuri na ningependa kuwasaidia wakafika mbali sana, Lakini mimi binafsi nakuwa na hofu kubwa sana hawatopata kile ambacho mimi nafikiria, Mshahara mzuri, Marupurupu ya kutosha, Malazi, Chakula na Usafiri. Kwakuwa mimi ndio naweza kuwa mdhamini wake, Gharama zote hizo zitakuwa ni juu yangu.

  Sasa Klabu itakayo mchukuwa wataamuwa wamlipe Dolla 500, kwa mfano, Mimi binafsi kama mfadhili wake sinto kubaliana na malipo hayo, matokeo yake Itabidi mcheza arudi nyumbani,
  Sina uhakika kama mchezaji huyo atalizungumza jina langu kwa wema, kwa kuwa waandishi wa habari za michezo watapenda kujua safari yake tangu ilipokuwa mwanzo mpaka ilipo fikia, siamini kama atakuwa mkweli 100% na hapo ndipo atakapo lichafua jina langu kwenye magazeti na vyombo vingine vya habari.

  Ushahuri wangu tu kwa chama cha Mpira cha Tanzania kwanza kithamin mchango wa wachezaji kwani watambue bila wachezaji, wao kama viongozi wasingekuwa pale walipo.

  Wawaondolee wachezaji vikwazo, Na chama cha mpira kizingatie zile sheria 17 za FIFA,Wakifanikiwa hilo basi watambue mpira wa Tanzania utafika mbali sana na watatambulika kwenye  medani ya soccer kimataifa.

  Pia jambo kubwa ambalo mimi linanishangaza hasa kwa Vilabu vikubwa vya Tanzania kuchukua wachezazaji kutoka nje ya Tanzania kama wachezaji wa kulipwa,

  Tujiulize wadau wenzangu, Chama cha mpra kilitumia vigezo gani na kuwapa nafasi wao ya kuja Tanzania kucheza soka la kulipwa?

  Leo mchezaji wa Tanzania kupata timu ya nje ya Tanzania kuna  vigezo vingi vina hitajika, Kwanza awe na muonekano mzuri wa kimaumbile, Na kama ni mfungaji basi ajue idadi ya magoli mangapi amesha funga, iwe kwa mechi za kitaifa au kimataifa, itakuwa vizuri zaidi angalau awe ameshafanya chezea timu ya Taifa lake " National Team" 
  kwa umri wake je utamruhusu?

  Kwa sababu timu inapo mchukuwa inakuwa inafanya biashara watategemea kwamba watafanya mauzo ya Jezi kupitia mchezaji walio mnunua na sio kuja kucheza tu, 

  Natumaini wadau wenzangu mpo na mmepitia Kila mstari katika haya niliyo jaribu kuwaletea.

  Nawaombeni na nyinyi mchango wenu wa  mawazo  nini kifanyike ili niweze kusaidia wana Soccer wa Tanzania?
  KAJU SPORTS BLOG.

  0 0

  Rais wa zamani wa nchi ya Ureno, Mario Soares ambaye anaheshimika kama baba wa demokrasia nchini humo amefariki dunia hapo jana akiwa na umri wa miaka 92. 

  Rais huyo wa zamani ndiye mwanzilishi wa chama cha kisoshalisiti nchini humo na katika kipindi cha uhai wake alitumia miongo kadhaa katika masuala ya siasa ikiwa ni pamoja na kuwa mstari wa mbele wakati wa mchakato wa nchi hiyo kujiunga kwenye Umoja wa Ulaya. 

  Soares alikuwa rais wa nchi hiyo katika kipindi cha kuanzia mwaka 1986 hadi mwaka 1996 baada ya kuwa tayari amelitumikia taifa hilo katika nyadhifa za uwaziri wa mambo ya nchi za nje na Waziri Mkuu. 

  Ureno imetangaza siku tatu za maombolezo kuanzia Jumatatu kwa ajili ya kuomboleza kifo cha kiongozi huyo.

  0 0

  Ripoti mpya iliyotolewa na mashirika ya kijasusi nchini Marekani Ijumaa wiki hii imedaiwa kumtaja Rais Vladimir Putin wa Urusi kuwa aliagiza kufanyika kampeni maalumu kupitia katika vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na kufanya udukuzi kwa lengo la kuingilia uchaguzi wa Rais wa Marekani uliofanyika Novemba mwaka jana. 

  Ripoti hiyo pia imeeleza kuwa Rais Putin alifanya hivyo kwa makusudi akilenga kumdhoofisha kisiasa mgombea wa chama cha Democratic Hillary Clinton katika kampeni zake za kuwania kuchaguliwa kuwa Rais wa Marekani. 

  Maafisa wa mashirika hayo ya kijasusi ya Marekani walitoa kurasa 25 za ripoti hiyo kwa umma Ijumaa wiki hii baada ya kuwa tayari wamewasilisha ripoti ndefu kuhusiana na uchunguzi huo kwa Rais Barack Obama, Rais Mteule Donald Trump pamoja na wabunge waandamizi nchini humo. 

  Aidha ripoti hiyo inaeleza kuwa Rais Putin na serikali ya Urusi walionyesha upendeleo maalumu kwa Rais Mteule Donald Trump. Hata hivyo licha ya ripoti hiyo kuwekwa wazi Trump bado ameendelea kutetea uhalali wa kuchaguliwa kwake.

  0 0

  Dotto Charles Heka (13) aliyekuwa Mwanafunzi wa shule ya msingi Lupungu wilayani Malinyi hatimaye amefufua ndoto zake za kuendelea na elimu ya sekondari.

  Awali baada ya kuhitimu elimu ya msingi tu wazazi wake walimshinikiza na kumlazimisha aolewe pasipo yeye mwenyewe kuridhia kuishi na mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Masenga, kama mme na mke, akielezea kwa uchungu mbele ya Mkurugenzi wa wilaya ya Malinyi ndugu Marcelin Ndimbwa, Afisa elimu wa wilaya Kalagila Silivesta na mwanasheria Sospeter Kalekwa, mwanafunzi Doto Charles Heka anasema,kwakuwa hakupata kuungwa mkono na hata mmoja wa wazazi na ndugu zake alikubali kuoelewa hivyo hivyo. 

  Baada ya matokeo kutoka baadhi ya wasamaria wema waligundua kwamba amefaulu na amechaguliwa kujiunga na shule ya sekondari ya kutwa ya Ngoheranga na kuamua kutoa taarifa wilayani iliyopelekea mkurugenzi kulivalia njuga jambo hilo na baada ya kujiridhisha aliweka mtego na jeshi la polisi lilifanikiwa kumkamata baba wa mtoto na kumchukua mtoto huyo ambaye mpaka sasa bado yupo chini ya uangalizi wake mkurugenzi na mtoto anaishi kwa mwalimu, akisubilia kufunguliwa kwa shule . 

  Mbali na hayo yote pia Mkurugenzi ameamua kujitolea kumsomesha mwanafunzi huyo kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita na amemwomba afisa elimu mkoa amtafutie nafasi ya shule ya bweni huku Ndugu Masenga aliyetoroka akiendelea kutafutwa na jeshi la polisi na kuhakikisha anatiwa nguvuni na sheria kuchukua mkondo wake na kuwa onyo na somo kwa wengine wote wenye mawazo na tabia za namna hizo ndani ya halmashauri yake. Aidha mkurugenzi amewapongeza maafisa elimu, watumishi wa halmashauri hiyo pamoja na wasamaria wema waliotoa ushirikiano na kumnusuru binti huyo. Mungu atawalipa kwa haya mliyomtendea malaika wake Dotto.

  0 0

older | 1 | .... | 1497 | 1498 | (Page 1499) | 1500 | 1501 | .... | 3278 | newer