Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1495 | 1496 | (Page 1497) | 1498 | 1499 | .... | 3272 | newer

  0 0  Mchezaji wa timu ya Taifa ya kuogelea,Dennis Khamis Mhina akipokea shada la maua kutoka kwa baba yake mzazi mzee Khamis Hussein Mhina wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere leo alasili akitokea nchini Canada ambako alishinda na kushika nafasi ya nne katika mashindano ya vijana ya Dunia ya kuogelea yaliyofanyika nchini humo hivi karibuni.
  Mchezaji wa timu ya taifa ya kuogelea ya vijana Kijana Dennis Khamis Mhina akipokewa na ndugu jamaa na marafiki wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere leo alasili akitokea nchini Canada ambako alishinda na kushika nafasi ya nne katika mashindano ya vijana ya dunia ya kuogelea yaliyofanyika nchini humo hivi karibuni.
  Mchezaji wa timu ya taifa ya vijana ya kuogelea Kijana Dennis Khamis Mhina akitoka nje na mama yake mzazi Bhoke Mukoji Mhina kulia wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa
  Kimataifa wa JK Nyerere leo arasili akitokea nchini Canada ambako alishinda na kushika nafasi ya nne katika mashindano ya vijana ya dunia ya kuogelea yaliyofanyika nchini humo hivi karibuni.
  Katibu Mkuu wa Chama Cha Kuogelea nchini, Ramadhan Namkoveka akizungumza wakati walipompokea mchezaji wa timu ya taifa ya vijana ya kuogelea Kijana Dennis Khamis Mhina wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa
  Kimataifa wa JK Nyerere leo alasili akitokea nchini Canada ambako alishinda na kushika nafasi ya nne katika mashindano ya vijana ya dunia yaliyofanyika nchini humo hivi karibuni, Kulia ni mama mzazi wa kijana Dennis Mhina Bi Bhoke Mukoji Mhina.
  Mchezaji wa timu ya taifa ya vijana ya kuogelea Mchezaji wa timu ya taifa ya vijana ya kuogelea Kijana Dennis Khamis Mhina akizungumza mara baada ya kuwasili nchini kwenye uwanja wa ndege wa
  Kimataifa wa JK Nyerere leo alasili akitokea nchini Canada ambako alishinda na kushika nafasi ya nne katika mashindano ya vijana ya dunia yaliyofanyika nchini humo hivi karibuni kulia ni mama mzazi Dennis Mhina Bi. Bhoke Mukoji Mhina, kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Kuogelea nchini, Ramadhan Namkoveka na baba yake Khamis Hussein Mhina.


  0 0

  Na Zainab Nyamka, 
  Globu ya Jamii
  Hii itakuwa mechi ya tatu kwa Yanga na Azam kukutana kwenye Kombe la Mapinduzi ikiwa ni mechi ya kwanza kwa benchi la Yanga linalokuwa chini ya George Lwandamina na Azam ikiwa chini ya Abubakari Cheche.

  Jumla timu hizi zimekutana mara 27 kwenye mashindano yote. Yanga imeshinda mara 10, Azam imeshinda mara 9 na zimetoka sare mara 8. Yanga wamefunga mabao 37 na Azam wamefunga mabao 34.
  Kupata rekodi mbalimbali za timu hizi BOFYA HAPA

  0 0

  Zaidi ya wakazi elfu tano wa vijiji viwili vya MAGINGO na MKONGOTEMA , vilivyopo kata ya MKONGOTEMA, Halmashauri ya Madaba Wilaya ya SONGEA Mkoani RUVUMA, Wameishukuru serikali kwa kuwaletea mradi wa maji na kuondokana na hadha waliyokuwa wakiipata ya kutafuta maji umbali wa kilomita moja hadi mbili , Shukrani hizo wamezitoa baada ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, KASSIM MAJALIWA kuzindua Mradi wa maji ulipo katika kijiji cha MAGINGO uliogharimu kiasi cha shilingi Bilioni Moja. Tizama video yake. 


  0 0

                 
  (1)Mchezaji bora wa mwaka wa Afrika  Riyad MAHREZ (Algeria & Leicester City). nafasi ya pili ni Pierre-Emerick AUBAMEYANG (Gabon & Borussia Dortmund),na Sadio MANE (Senegal & Liverpool) anashika nafasi ya tatu.

  (2)Mchezaji bora wa mwaka wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza barani Afrika ni Denis ONYANGO (Uganda & Mamelodi Sundowns).

  (3)Mchezaji bora wa mwaka wa Afrika upande wa wanawake ni Asisat OSHOALA (Nigeria & Arsenal Ladies)
  (4)Mchezaji bora kijana  anayechipukia.
  Kelechi IHEANACHO (Nigeria & Manchester City)
  (5)Mchezaji bora kijana Alex IWOBI (Nigeria na Arsenal)
  (6)Kocha bora wa mwaka Pitso MOSIMANE (Mamelodi Sundowns)
  (7)Club bora ya mwaka ni Mamelodi Sundowns.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji (WVBU) Prof. Adolf Mkenda amehitimisha mafunzo ya ukusanyaji wa taarifa za bei za mazao ya kilimo na bidhaa nyingine kwa kukabidhi simu za Mkononi Washiriki wa Mafunzo hayo kutoka mikoa mbalimbali Tanzania bara. Mafunzo hayo yaliyofanyika mkoani Dodoma kwa siku nne mfululizo na kuwashirikisha wakusanya taarifa wapatao 113 ngazi ya wilaya na mikoa.

  Katika Hotuba yake ya ufunguzi alieleza malengo ya Mafunzo hayo kuwa ni kuwajengea uwezo wa kufanya kazi kwa weledi zaidi kwa kuzingatia maendeleo ya kiteknologia na Habari kadiri mahitaji ya taarifa yanavyoongezeka.

  “mafunzo haya mnayopatiwa yanalenga kuwawezesha kukusanya na kutuma taarifa za masoko ya mazao ya Kilimo pamoja na bidhaa nyingine kwa wakati na usahihi Zaidi”.

  Alisisitiza kuwa taarifa sahihi zitasaidia wakulima,wafanyabiashara, watunga sera na Taasisi nyingine kufanya mamuzi ili kuleta mageuzi ya kiuchumi yatakayoongozwa na uchumi wa Viwanda.

  “Ni matumani yangu kuwa mtatumia weledi wenu na uzalendo kuwapatia wakulima, wasindikaji au wenye viwanda na walaji taarifa sahihi watakazozitumia katika kuendesha shughuli za kibiashara”. Aliongeza kuwa taarifa sahihi na kwa wakati utasaidia kuondoa utitiri wa madalali ambao hutumia mwanya wa ukosefu wa taarifa kuwanyonya wakulima kwa kutumia mbinu mbalimbali kama vile kwenda moja kwa moja kwa wakulima na kununua mazao kwa wakulima badala ya kusubiri mazao yafike sokoni.

  Mafunzo haya yaliandaliwa na Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kupitia Mradi wa SECO UN TRADE, pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) .
  Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf Mkenda akimkabidhi Simu ya Mkononi mmoja wa Washiriki wa Mafunzo ya wakusanya taarifa za Bei za Mazao ya kilimo na Bidhaa Nyingine ikiwa ni kitendea kazi kitakachowasaidia wakusanya taarifa.
  Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf Mkenda (wa tatu kulia) walioketi kwenye viti akiwa na picha ya pamoja na wahitimu wa mafunzo ya Ukusanyaji wa Taarifa za Bei za Mazao ya Kilimo na Bidhaa Nyingine yanayofanyika Mkoani Dodoma.Wa Pili (Kulia) walioketi ni Bw. Odilo Majengo Mkurugenzi Idara ya Uhamasishaji Biashara na Bi. Hilda Mwampeta Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Uhamasishaji Biashara na Masoko Wizara ya Viwanda ,Biashara na Uwekezaji.

  0 0

  Na Nteghenjwa Hossea, Arusha

  Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Arusha wameagizwa kusimamia Halmashauri zao kujibu hoja zote zilizowasilishwa na  Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa  Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016 kabla ya kufika mwisho wa juma lijalo.

  Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo  wakati wa Kikao  cha maandalizi ya Bajeti ya mwaka 2017/2018 na mapitio ya bajeti ya nusu mwaka wa Fedha 2016/2017 kilichohusisha Halmashauri zote za Mkoa wa Arusha  na wataalam toka Ofisi ya Mkaguzi wa hesabu za Serikali.

  Akitoa Agizo hilo Mhe. Gambo alisema “Nataka kila Halmashauri ikamilishe ujibuji wa Hoja kwa wakati na kwa majibu sahihi sio kufanya majibu ambayo yanaibua hoja zaidi au hayajitoshelezi na kwa Halmashauri ambayo ilipata Hati Chafu au Hati ya Mashaka kwa mwaka uliopita ianishe wataalamu waliopelekea Halmashauri kupata Hati hizo ili waweze kuchukuliwa hatua Stahiki”.

   Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(kwanza kulia) akizungumza katika kikao cha maandalizi ya Bajeti 2017/2017 na mapitio ya Bajeti 2015/2016.

   Baadhi ya Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Arusha pamoja na wadau wengine wakifuatilia Kikao cha maandalizi na mapitio ya Bajeti.

   Katibu Tawala Msaidizi huduma za Mipango  Mkoa wa Arusha Bi. Grace Mbaruku akiwasilisha mpango wa bajeti ya 2017/2018.

   Katibu Tawala Msaidizi Serikali za Mitaa Bi. Susane Mnafe akiwasilisha taarifa ya changamoto za usimamizi wa Halmashauri za Mkoa wa Arusha

  1.     Viongozi wa Mkoa na Wilaya ya Arusha wakifuatilia mawasilisho ya mpango wa Bajeti ya mwaka 2017/2018. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA


  0 0


  0 0

  Na Ofisa habari Mufindi

  Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imeendelea kustawi katika sekta ya elimu  ambapo tathimini ya  matokeo  ya darasa la saba ya Halmshauri hiyo   yanaonesha kupanda kutoka asilimia 80.39 mwaka 2015  hadi  asilimia 84.90% mapema mwaka jana, ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 4.51.


  Akisoma taarifa wakati wa kikao cha thathmini ambacho huwakutanisha wakuu wa shule zote za msingi na maaofisa elimu kata, Ofisa elimu taaluma wa Halmshauri ya Wilaya ya Mufindi Miriamu Ngala amebainisha kuwa tathimini ya ufaulu huo umejumuisha shule 143, watahiniwa elfu 05 mianne 38 ambapo wavulana ni elfu 02 miatatu 84 na wasichana ni elfu 03 na 54 huku wanafunzi waliofaulu na kuchaguliwa kuendelea na elimu ya Sekondari  wakiwa ni 4,617 sawa na asilimia 84.9.

   Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William katika picha ya pamoja na  na waalimu wakuu wa shule zilizofanya vizuri na kutunukiwa vyet na Fedha 
   Mkuu wa wilya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William (kushoto) akitunuku chet na Fedha kwa mmoja kati ya waalimu wakuu ambao shule zao zimefanya vizuri.
  Walimu wakuu na maofisa elimu kata wakiimba wimbo wakati wakimlaki mgeni rasmi kwenye ukumbi wa Halmshauri  ya Wilaya ya Mufindi.

  0 0

  Na Chalila Kibuda, 
  Globu ya Jamii
  ‘’KABLA hujafa hujaumbika ni maneno ya wahenga kuwa unaweza ukawa mzima lakini mwisho wa siku ukapata ulemavu wa kudumu katika maisha’’.

  Haya ni maneno ya Fundi wa Kushona Nguo Asiyeona, Abdallah Nyangalilo alipoambiwa afanyiwe oparesheni ya macho katika Hospitali ya Taifa Muhimbili mwaka 1989, akaambiwa kuwa hataona isipokuwa maumivu ya kichwa yatakuwa yamepungua.
  Akizungumza na Michuzi Blog katika darasa la wanafunzi wasiyeona, Nyangalilo amesema kuwa wakati alipokuwa amefanyiwa oparesheni Daktari wa Macho Raia wa Urusi alimuambia kuwa amfundishe kushona ambayo ndio itakuwa kazi yake, alikataa na baadae kukubali na kuanza kufundishwa.
  Amesema Daktari huyo alikuwa ana cherehani yake akiwa nje ya kazi hutumia cherehani kushona nguo na ndio cherehani aliofundishwa Nyangalilo
  Nyangalilo amesema 1994 alianza kazi ya kushona kwa kutumia ujuzi wa Daktari wake na fundi kufundisha wasiyeona na kuongeza kuwa maisha yalikuwa magumu na baadhi ya watu walikuwa hawamini kazi ya kushona ya mtu asiyeona.
  Amesema katika kufanya kazi hiyo ameweza kuendesha maisha yake,licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali kutokana na hali aliyokuwa nayo ya kuona.Nyangalilo amesema katika kufanya hivyo anaweza kushona nguo kwa kuchukua kipimo cha kushika kiganja cha mkono na kujua saizi zote na kusababisha kuitwa, Dk. Abdallah Nyangalilo.
  Amesema Mkurugenzi wa Tan Trade alianza kumwita Daktari kutokana na kazi hiyo wakafika madaktari wa kutoka Norway, Uganda, Kenya na Tanzania na kushauri Mkurugenzi wa Tantrade kuomba kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kumtunuku Udaktari wa Heshima, Abdallah Nyangalilo.
  Abdallah amesema kwa sasa anafundisha wasio ona wa Manispaa ya Temeke ikiwa ni wasio ona wote wa Jiji la Dar es Salaam na matarajio yake ni kuona anamiliki huo cha kushona cha wasio Ona .
   .Fundi wa Kushona Nguo Asiyeona, Dk. Abdallah Nyangalilo akizungumza na mwandishi wa michuzi Blog hayupo pichani leo jijini Dar es Salaam.
   Fundi wa Kushona Nguo Asiyeona, Dk. Abdallah Nyangalilo akimpa Maelezo Diwani wa Viti Maalum wa Manispaa ya Ilala (siyeona) , Nuru Awadhi alipotembelea  darasa la  Dk. Abdallah Nyangalillo. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii. 
   Mwanafunzi wa Kushona asiyeona, Seif Mdumbe akimpa maalezo Diwani wa Viti Maalum wa Manispaa ya Ilala asiyeona , Nuru Awadhi alipotembelea  darasa la  Dk. Abdallah Nyangalillo.
    Fundi wa Kushona Nguo asiyeona, Dk. Abdallah Nyangalilo akionesha nguo anazoshona  kwa Diwani wa Viti Maalum wa Manispaa ya Ilala asiyeona , Nuru Awadhi alipotembelea  darasa la  Dk. Abdallah Nyangalillo.
  Sehemu ya wasiyeona wakiwa katika mafunzo ya ushonaji nguo. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.


  0 0


  *Aahidi kutuma Gavana, CAG, Msajili wa Hazina kufanya ukaguzi
  *Asema Serikali haitaruhusu uagizaji wa makaa hayo kutoka nje ya nchi
  *Autaka uongozi wa kampuni uimarishe teknolojia ili kuongeza uzalushaji

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa atamtuma mara moja Msajili wa Hazina aende kufanya uchunguzi wa kina na wa kijinai (forensic investigation) ili kijiridhisha kama mapato na matumizi ya kampuni ya TANCOAL ni halali.

  Ametoa kauli hiyo leo mchana (Ijumaa, Januari 6, 2017) mara baada baada ya kupokea taarfa na kutembelea mgodi huo ili kuona shughuli za uzalishaji zikoje.

  Waziri Mkuu amesema atamwagiza pia mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ili apitie mahesabu ya kampuni tangu mwaka 2011 walipoanza uzalishaji. “Mbali CAG, itabidi Gavana wa Benki Kuu naye aangalie utumaji wa fedha uliokuwa ukifanywa kama ulifanyika kwa halali,” amesema.
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia shughuli za uchimbaji wa makaa ya mawe unavyofanywa nakampuni ya Tancoul katika mgodi wa Ngaka uliopo wilayani Mbinga  kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la maendeleo la taifa NDC Dr Samuel Nyantahe.
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia mkaa wa mawe ulivyo
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa ameongozana na mkuu wa mkoa wa Ruvama Mhandisi Mahenge pamoja naviongozi mbalimbali walipokuwa wanatemmbelea mgodi wa Ngaka. Picha na Chris Mfinanga,

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ( wa pili kulia) akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais Mhe, Balozi Seif Ali Iddi wakati alipowasili Mazizini Mkoa wa Mjini Magharibi kuweka jiwe la msingi ujenzi wa jengo jipya la Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Zanzibar leo, ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kushoto) Waziri wa Fedha na Mipamgo Zanzibar Dkt.Khalid Salum Mohamed

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ( katikati) na Mwakilishi wa Benki ya Dunia Bibi.Elizabe Ann Talbert (kulia) wakifungua pazia kuashiria Uwekaji wa jiwe la Msingi  jengo jipya la Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Zanzibar huko   Mazizini Mkoa wa Mjini Magharibi leo ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
   Baadhi ya Viongozi waliohudhuria katika hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi Ujenzi wa jengo jipya la Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Zanzibar,uliowekwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein huko Mazizini Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja,ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
   Mkandarasi wa Ujenzi wa jengo jipya la Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Zanzibar  Nd,Edwin Shitindi kutoka alipokuwa akitoa maelezo ya Kitaalam kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupi pichani) baada ya kuliweka jiwe la msingi jengo hilo leo, ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akitoa hutuba yake baada ya kuliweka jiwe la msingi jengo jipya la Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Zanzibar leo, ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kulia) Waziri wa Fedha na Mipamgo Zanzibar Dkt.Khalid Salum Mohamed. Picha na IKULU. Taarifa kamili BOFYA HAPA

  0 0

  Wakuu wa mashirika ya upelelezi nchini Marekani wanatarajiwa kukutana na Rais mteule wa nchi hiyo, Donald Trump na kumwonyesha ushahidi kuwa Urusi ilifanya jaribio lisilokifani kuvuruga uchaguzi wa Marekani kwa kufanya udukuzi katika chama cha wapinzani wake cha Democratic.

  Mkutano huo unakuja wakati kukiwa na mvutano mkubwa kati ya viongozi wa mashirika ya ujasusi ya Marekani na rais huyo ajaye, ambaye anapinga vikali madai yoyote kuwa Urusi ilimsaidia kushinda uchaguzi wa rais. 

  Baada ya Trump kuonyesha wasiwasi kwa mara ya kwanza mapema mwezi uliopita, Rais Barack Obama aliyaamuru mashirika ya upelelezi kutoa ripoti ya kina kuhusu mashambulizi ya mtandaoni na uingiliaji wa Urusi katika uchaguzi wa rais. 
  Obama alifahamishwa kuhusu ripoti hiyo jana na wakuu wa ujasusi na wanatarajiwa kuzungumza na Trump hii leo.

  0 0


  0 0


  0 0

  The United Republic of Tanzania

  MINISTRY OF NATURAL RESOURCES AND TOURISM

  NOTICE FOR GRADING OR RE-GRADING OF ACCOMMODATION 
  FACILITIES IN DAR ES SALAAM REGION (PHASE I)


  All owners and operators of accommodation facilities in Dar es Salaam Region are hereby notified that the Ministry of Natural Resources and Tourism shall conduct Grading/Re-grading of all designated accommodation facilities in Dar es Salaam Region. To this effect, the Ministry gives thirty (30) days notice, from the date of issuance of this notice, for the owners and operators of accommodation facilities in Dar es Salaam Region to make the necessary preparations for a smooth and efficient run of the ensuing exercise.


  The Criteria for Grading, and the list of accommodation facilities scheduled for grading/re-grading in this Phase 1 for 2017, are available HERE also available at www.tanzaniatourism.go.tz and www.tourismcollege.go.tz. 
  .

  This notice is given in consideration of Sections 10 (3), 17, 53 (1) (b) and (c), 46 (1) (a) and (f) of the Tourism Act, No. 29 of 2008; and Regulation 5 of the Tourism (Fees and Charges) of 2015 (GN.267).

  Issued by:

  PERMANENT SECRETARY

  MINISTRY OF NATURAL RESOURCES AND TOURISM

  MPINGO HOUSE – 40 JULIUS NYERERE ROAD

  15472 – DAR ES SALAAM

  TEL: +255 22 2864271/ 2864230

  6 JANUARY, 2017


  To  access the Criteria and List of accomodation click the link FOLLOW ME below;

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wenyeviti wa TPSF, CTi, TCCIA na ZNCCIA juu ya mpango wa kibiashara unaojulikana kama China One Belt, One Road ulioasisiwa na serikali ya China na unajumuisha bara la Asia, Mashariki ya Kati,Ulaya na Afrika, Ikulu jijini Dar es Salaam.
   
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Wenyeviti wa TPSF,CTi,TCCIA na ZNCCIA juu ya mpango wa kibiashara unaojulikana kama China One Belt, One Road ulio asisiwa na serikali ya China na unajumuisha bara la Asia, Mashariki ya Kati,Ulaya na Afrika.

  0 0


  0 0

  Mwili wa marehemu mze Boniface Pangawe Lukosi umesafirishwa jana Ijumaa Januari 6, 2017 kuelekea kijijini kwake Kalenga mkoani Iringa baada ya misa na kuagwa katika kanisa la Mtakatifu Yohana lililopo Yombo Vituka jijini Dar es salaam. 
  Marehemu mzee Lukosi, aliyefariki Januari 3, 2017 akiwa na umri wa miaka 95, anatarajiwa kuzikwa leo Jumamosi Januari 7, 2017 kwenye makaburi ya familia hapo Kalenga. Ndugu, jamaa, marafiki na majirani walijitokeza kwa wingi kuaga mwili wa marehemu, kabla ya jeneza lake kuingizwa kwenye basi na kuanza safari majira ya saa kumi jioni. Mola aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi - AMINA
   Sehemu ya ndugu, jamaa, marafiki na majirani waliojitokeza kwa wingi kwenye misa na kuaga mwili wa marehemu. Aliyebeba mtoto ni mdau Chef Issa wa Sweden ambaye yuko mapumziko mafupi na nyuma yake mwenye fulana ya pundamilia ni mdau Dr. D. Ruhwago
   Wafiwa wakiongozwa na mdau Chris Lukosi wakiwa kanisani hapo
   Baba Paroko akiombea mwili na wafiwa safari njema
   Jeneza lenye mwili wa marehemu likiingizwa garini tayari kwa safari
   Mdau Chris Lukosi katika majonzi
  Mdau Chris Lukosi akitambulishwa kwa Chef Issa na mdau Seraphin na Dr. D, Ruhwago ambao ni baadhi ya wadau waliofika kumfariji mwanagrupu mwenzao anayeishi Uingereza.

  0 0
 • 01/06/17--19:00: SHUKURANI NA KUMBUKUMBU
 • Captain  Denis Mshami wa wakala wa ndege za serikali napenda kuwashukuru wote kwa upendo na faraja mlioonesha wakati wa msiba pamoja na arobaini ya mke wangu mpenzi Husna Kiluvia Mshami.

  Kwa moyo wa dhati kabisa mimi na familia yangu tunapenda kusema asante sana na Mwenyezi Mungu atawajazia pale patapopungua.

  Ni watu wengi sana wa kuwashukuru lakini baadhi ya hawa wachache iwe ni uwakilisho wa wengi waliotufariji pamoja na kumuuguza Husna.

  Nao ni madaktari ya Hindu Mandal, Dar Group Hospital, Dr Mvungi, Ofisi ya Rais Tume ya Utumishi, Wakala wa Ndege za serikali chini ya Capt. Raymond Musingi, Michuzi blog, majirani pamoja na ndugu jamaa na marafiki. Tunapenda kusema tena asante sana.
  Husna, leo ni tarehe 7.01.2017 umetimiza miezi miwili toka uondoke. Nilikupenda sana na nitakupenda siku zote. Mwenyezi Mungu akupe pumziko la amani. Amina.
  "Wote wamwaminio Mungu watatambua ukweli wake;wote walio waaminifu watakaa upande wake kwa upendo, maana huwajalia neema na huruma watakatifu wake. Na huwaangalia kwa wema hao aliowateua".
  (Hekima ya Sulemani 3:9)

older | 1 | .... | 1495 | 1496 | (Page 1497) | 1498 | 1499 | .... | 3272 | newer