Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1492 | 1493 | (Page 1494) | 1495 | 1496 | .... | 3272 | newer

  0 0


  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa na viongozi waandamizi wa CCM katika boti ya wakati wakiwa safarin kwenda Zanzibar kwenye uznduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Dmani, mkoa wa mjini Magharibi, leo. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole na kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstafu Lubinza na Katibu wa NEC Oganaizesheni Muhammed Seif khatib
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa na viongozi waandamizi wa CCM katika boti wakati wakiwa safarin kwenda Zanzibar kwenye uznduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Dmani, mkoa wa mjini Magharibi, leo. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole na kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstafu Lubinza na Katibu wa NEC Oganaizesheni Muhammed Seif khatib
  Msaidizi wa Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Msami akiwa na Msimamizi Mkuu wa Blog ya Taifa ya CCM, Ndugu Nkoromo, katika boti wakati wakienda Zanzibar na Viongozi hao.

  0 0

  Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii Malinyi.

  Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi ni moja ya Wilaya mpya hapa nchini zilizoundwa kutokana na ukubwa wa mkoa wa Morogoro kwa lengo la kuzidi kuongeza huduma za kiserikali kwa wananchi walio pembezoni hili kupunguza gharama za wananchi kutembea umbali mrefu.

  Malinyi ambayo imezaliwa kutoka katika Wilaya Mama ya Halamashauri ya Wilaya ya Ulanga ambayo ilionekana kubwa kuliko kawaida na kushindwa kukidhi kuwahudumia wakazi wa malinyi kutokana na umbali wa kijiografia.
  Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Malinyi ,Marcelin Ndimbwa, akikagua ujenzi wa madarasa ambayo yamejengwa kwa ajli ya watoto wa wafugaji Rumbanga.

  Marceline Ndimbwa ni Mkurugenzi wa kwanza katika halmashauri hiyo mpya kuteuliwa na Rais wa awamu ya tano Daktari John Pombe Magufuli ili kuhakikisha maendeleo ya wilaya hiyo yanafanana na sehemu nyingine.

  Ndimbwa amekuwa ni mkurugenzi wa halamashauri hiyo huku akikabiliana na changamoto kubwa ya mgogoro wa ardhi baina ya wakulima na wafugaji na changamoto ya miundombinu ya elimu katika jamii kubwa ya wafugaji.

  Ndimbwa anasema kuwa Rumbanga ni moja ya maeneo ambayo hayapo mbali na mji wa Malinyi lakini yamekuwa na jamii kubwa ya wafugaji wa kabila la kisukuma huku wakiwa na changamoto ya kutokuwa na shule ya msingi, Sekondari na huduma za afya.

  Ndimbwa anasema kuwa mbali na changamoto zote hizo lakini ameamua kuanza na changamoto kubwa ya kutokuwepo na shule ya msingi katika eneo hilo la Rumbanga.

  “kiukweli hali sio nzuri katika eneo la Rumbanga kwani shule iliyopo ni ya nyasi ambayo imejengwa na wanakijiji wenyewe na haina walimu wa kufundisha zaidi ya vijana wawili ambao wamemaliza kidato cha nne na kuamua kujitolea katika kuwafundisha wadogo zao ambao wapo kuanzia darasa la kwanza mpaka la nne”amesema Ndimbwa.

   Ndimbwa anasema kuwa mara baada ya kuona mazingira hayo wakaona ni lazima wa kuamua kujenga shule hiyo kuwa ya kisasa kutokana changamoto ya umbali kufata shule ambayo ipo kilometa 34 kutoka hapo Rumbanga na wanafunzi hao kutakiwa kutembea kwenda na kurudi katika shule ya msingi Mwembeni hali iliyochangia watoto wengi kuacha masomo na watoto wa kike kupata ujauzito katikati ya masomo na kulazimika kuacha shule.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0

  GWIJI wa muziki dansi nchini 'Kamarade' Ally Choki yuko mbioni kuitosa bendi yake ya The African Stars 'Twanga Pepeta' baada kutengewa 'mkwanja' mnene na bendi ya Extra Peramiho ya Mjini Songea Mkoani Ruvuma. 

  Habari za uhakika kutoka mjini Songea zinaeleza, Choki akiwa mjini humo wiki iliyopita alikokwenda kutumbuiza na Twanga Pepeta wakati wa sikukuu ya Krisimasi aliitwa mezani na tajiri wa Extra Peramiho mfanyabiashara John Floyd Ngonyani ili kuweka mambo sawa. 

  Taarifa zinaeleza,katika kikao hicho cha siri kilichofanyika katika moja ya hoteli za Kitalii mjini humo Choki, alimueleza Ngonyani kuwa bado ana mkataba na Twanga Pepeta unaofikia ukomo mwakani hivyo itakuwa ngumu kwake kuitosa bendi hiyo kutokana na kubanwa kisheria. 

  Inaelezwa mfanyabiashara huyo alimueleza Choki yuko tayari kuvunja mkataba huo kwa gharama yoyote kwani amepanga kuiimarisha Extra Peramiho kuwa moja ya bendi kubwa za muziki wa dansi nchini. Tayari bendi hiyo imeshawanyakuwa baadhi ya wanamuziki waliowahi kufanya kazi na Choki enzi ya Extra Bongo wakiongozwa na kiongozi Greyson Semsekwa na Bob Kisa ambapo wako mbioni kuwanasa mpiga dramu Sunday Mashine na mpiga solo mahiri Ephraim Joshua,Mfaume Solo na mpiga Tumba wa Tanzania One Theatre (TOT) Salum Chakuku 'Kuku Tumba'. 

  MTANDAO huu ulimtafuta Ngonyani kupata ukweli wa taarifa hizo ambapo alikiri kuteta na Choki na kusema kila kitu kitawekwa wazi mambo yatakapoiva. Kwa upande wake Choki alisema,aliitwa na mfanyabiashara huyo kutoa ushauri wa namna ya kuiboresha bendi hiyo ila hafahamu habari za kuondoka Twanga

  0 0

  Na Woinde Shizza,Arusha

  Jumla ya shilingi  4,708,680,000 zimekusanya na jeshi la polisi mkoa wa Arusha kikosi cha usalama barabarani kutokana na faini zilizolipwa na watumiaji wa vyombo vya  moto  kwa kipindi cha January 2016 hadi December 2016 hiii ikiwa ni ongezeko kubwa tofauti na miaka iliopita

  Hayo yamebainishwa na kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Charles   Mkumbo wakati akiongea na waandishi wa habari  kwa ajili ya kutoa taarifa ya hali ya usalama kwa kipindi chote cha mwaka 2016 kuanzia Januari hadi Disemba  ambapo alisema kuwa kwa upande wa ukusanyaji wa notification  fedha zimeongezeka kwa kiasi kikubwa.

  Alisema kuwa  tozo hizo za notificationi katika kipindi cha mwaka 2016 ziliongezeka hadi kufikia shilingi 4,708,680,000/=  tofauti na mwaka 2015 ambapo jumla ya shilingi 3,227,640,00/= zilikusanywa kwa  hivyo kutokana na takwimu hizo kikosi cha usalama barabarani kimekusanya ongezeko la zaidi ya shilingi 1,481,040,000/=.

  “fedha hizi zimeongezeka kutokana na makosa mbalimbali yanayofanywa na madereva mbalimbali wa vyombo vya moto kwa kujua wanavunja sheria ,na wengine wakiwa wanafanya kwa kutokujua sasa sisi kama jeshi la polisi tunatumia njia ya kuwaonya kwa kuwatoza faini ili waweze kujirekebisha  kwa haraka kwa sababu tusipo fanya hivyo na kuwaonya bila kuwapiga faini watakuwa wanarudia makosa kila siku ,na pia ongezeko hilo limetokana na kuwepo na ongezeko kubwa la watu wanaotumia vyombo vya moto ,mfano ukiangalia  magari mjini uwezi kufananisha magari yaliyokuwepo mwaka jana na mwaka huu mwaka huu yameongezeka kwa kasi na hata pikipiki pia ni hivyo hivyo”alisema Mkumbo.

  0 0

  Na Amina Kibwana,Globu ya Jamii.

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt.Augustine Mahiga anatarajia kumpokea Waziri wa mambo ya nje wa Jamuhuri ya watu wa china Mh.Wang Yi anayetarajia kufanya ziara ya kikazi nchini Tanzania  Januari 9 Kwa lengo la kukuza  mahusiano mazuri baina ya china na Tanzania na kuangalia maeneo mapya ya ushirikiano wa kiuchumi.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam  msemaji wa Wizara ya mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mindi Kasiga amesema kuwa wakati wa ziara hiyo Waziri Wang Yi atakutana na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dkt. John Pombe Joseph Magufuli pamoja na kufanya mazungumzo na Dkt Mahiga kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano wa Kimataifa baina ya Tanzania na China.

  "Kwakuwa china iliichagua Tanzania kuwa miongoni mwa nchi nne barani Afrika zitakazo wezeshwa kupiga hatua kwenye maendeleo ya viwanda hivyo kupitia mpango huo tunatarajia viwanda takruban 200 vitajengwa au kuwekezwa nchini."

  Amesema kuwa mbali na uendeshaji wa viwanda viongozi hawa watazungumzia miradi mingine ya miundombinu ambapo china imeahidi kuisaidia Tanzania ikiwa ni pamoja na maboresho makubwa ya Reli ya Tazara, Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo pamoja na ujenzi wa Reli ya Kati.

  Aidha Mh. Yi anatarajiwa kuzungumza na mwenyeji wake kuhusu masuala ya ushirikiano wa Kimataifa ikiwa ni pamoja mageuzi ya Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ambapo china inaunga mkono msimamo wa Afrika na  wa Tanzania kutaka Afrika ipewe viti viwili vya kudumu kwenye barala hilo na kepewa kura ya turufu, Masuala ya amani na usalama katika eneo la Afrika Mashariki pamoja na eneo la Bahari ya kusini mwa china.

  Ameongeza kuwa mpango huo unaenda sambamba na mpango wa Taifa wa maendeleo wa mwaka  2016/2020 kupitia ahadi za Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh.John Pombe Joseph Magufuli wa kujenga Tanzania ya viwanda ifikapo mwaka 2020.

  0 0

  Peter Tino
  WACHEZAJI nembo ya Tanzania Kimataifa wanatarajia kuzindua mashindano ya kuwania kombe la Diwani wa Kata ya Tabata, Patrick Assenga (Chadema) yanayotarajia kuanza mwishoni mwa wiki kwenye uwanja wa Shule ya msingi Tabata.

  Akizungumza jana kwenye hafla ya kukabidhi vifaa kwa timu shiriki za mashindano hayo, Assenga alisema wachezaji wanaotarajia kuwa sehemu ya uzinduzi wa mashindano hayo ni pamopja na Jellah Mtagwa, Peter Tino, Dua Said, Moses Mkandawile na wengineo waliowahi kuitangaza nchi nje ya mipaka yake.

  “Tumepanga wachezaji wa zamani watacheza kwa dakika chache katika uzinduzi wa mashindano hayo na baadaye tutawakabidhi zawadi maalum kwa lengo la kuthamini mchango wao katika soka la Tanzania,” alisema Assenga.

  Assenga alisema katika mashindano yake yanayotarajia kushirikisha timu 16 za mitaa nane iliyoko katika kata hiyo, ameguswa na wachezaji waliowahi kutamba katika soka la Tanzania ambao hawathaminiwi kama mashujaa waliofanya makubwa katika nchi hii.

  Assenga alisema uandaaji wa mashindano hayo ni ahadi aliyowahi kuitoa wakati wa kampeni za kuwania uongozi huo  kwamba atajikita zaidi kwenye kusaidia vijana hasa katika upande wa michezo na maendeleo mengine yanayowahusu vijana.

  Diwani huyo alisema pamoja na kuwa na lengo la kuwasaidia vijana pia kuwapa thamani waliokuwa wachezaji waliowahi kuitangaza Tanzania katika nchi nyingine kama Nigeria, Liberia na kwingineko.

  Aidha Diwani huyo alisema mashindano hayo yatakuwa yakifanyika kila mwaka hadi atakapomaliza uongozi wake katika Kata  hiyo ambako katika uzinduzi huo, Meya wa Ilala Charles Kuyeko anatarajia kuwa mgeni rasmi.
  Jellah Mtagwa

  “Nimepanga pia kabla ya kuanza mashindano, Jumamosi nitashirikiana na na wananchi wa Tabata kufanya usafi  kwa kushirikiana na wananchi wa Kata hiyo, hivyo nawaomba wakazi wa Tabata kujitokeza kufanya usafi katika maeneo yao,” alisema Assenga.

  Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya mashindano hayo, Rogers Peter alisema  wamejipanga vilivyo kufanikisha mashindano hayo ambayo yanabeba taswira ya Tanzania kwa sababu wamekumbuka wachezaji  wa zamani na  kuwalinganisha na vijana  wa sasa lengo likiwa ni kutoa elimu kwa vijana na kuwatengenezea fursa zaidi kwa ajira.

  Hata hivyo, Peter alitumia fursa hiyo kumuomba Diwani kutupia macho fursa nyingine za mchezo kkwa upande wa soka la ufukweni na wanawake akiwa na dhamira ya kutaka Tabata kuwa kisima cha vipajia nchini.
  Naye Mkuu wa Nidhamu wa mashindano hayo, aliyekuwa golikipa wa Simba, Moses Mkandawile alisema katika historia ya Tabata haijawahi kutokea kiongozi mwenye maono kama Assenga ambaye ameguswa zaidi  na vijana ambao  mara nyingi wanashinda vijiweni.

  0 0

  Na Hassan Silayo-MAELEZO

  Wazee wa Kimila kutoka Koo Tano Mkoani Mara wamemuomba Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga kuwawezesha kutembea Koo hadi Koo kwa ajili ya kuelimisha jamii kuhusu madhara ya ukeketaji.

  Akiongea wakati walipokutana na Katibu Mkuu aliyepo Wilayani Tarime Mzee wa Koo ya Bukenye Mzee Elias Maganya alisema kuwa walishapata elimu kutoka kwenye Jukwaa la Kulinda Utu wa watoto(CDF) na changamoto ni jinsi ya kuzifikia koo nyingine Mkoani huko ili kuwezesha kuondoa kabisa mila hiyo.

  “Tumechoka vitendo vya ukatili kwa watoto na vitendo visivyoturishisha sisi kama wazee, tutafanya kila jitihada kuweza kuondokana na vitendo hivi, tunahitaji ushiriki zaidi wa serikali na asasi nyingine zishirikiane na CDF ili kwa pamoja tuweze kufikia lengo tuliloliweka” Alisema Mzee Elias

  Akitolea ufafanuzi suala hilo Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga amesema kweli upo umuhimu wa kutekeleza suala hilo la kupeleka elimu juu ya madhara ya ukeketaji ili kuweza kuwasaidia watoto wakike.

  Naye Mzee wa Kimila kutoka Koo ya Bukira Mzee Sinda Nyangore ameishauri serikali na mashirika mengine kutoa elimu katika vipindi vyote vya mwaka na kuacha utaratibu wa kutoa elimu katika msimu wa ukeketaji kwenye koo mbalimbali.

  Katika Ziara hiyo Katibu Mkuu Sihaba Nkinga alitembelea maeneo mbalimbali ikiwemo Dawati la Jinsia katika wilaya hiyo na kujionea namna wanavyofanya kazi na jinsi wanavyokabiliana na changamoto mablimbali.

  Aidha Bi. Sihaba aliwatembelea watoto wa kike waliopo katika mpango wa uendelezwaji kijasiriamali unaotekelezwa na Jukwaa la Kulinda Utu wa watoto(CDF) katika kata ya Manga Wilayani Tarime Mkoani Mara.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akiongea na wazee wa kimila kutoka koo tano mkoani Mara ambapo amewapongeza kwa kazi ya kuelimisha jamii inayowazunguka juu ya madhara ya ukeketaji kwa watoto wa kike na tohara mara mbili kwa watoto wakiume, Katikati ni Mtumishi Jukwaa la Utu wa Mtoto(CDF) Bi. Kambibi Kamugisha, kushoto ni Katibu Tawala Tarime Bw. John Marwa na Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Watoto kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi.Margareth Mussai.
  Mzee wa Kimila kutoka Koo ya Bukira Mzee Sinda Nyangore akiongea na na Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga ambapo alishauri serikali na mashirika mengine kutoa elimu katika vipindi vyote vya mwaka na kuacha utaratibu wa kutoa elimu katika msimu wa ukeketaji kwenye koo mbalimbali.
  Mzee wa Koo ya Bukenye Mzee Elias Maganya akiongea na Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga ambapo alimuomba Katibu Mkuu kuangalia uwezekano wa kuwezeshwa kutembea Koo hadi Koo kwa ajili ya kuelimisha jamii kuhusu madhara ya ukeketaji.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akiwa katika picha ya pamoja na wazee wa kimila kutoka koo tano za Bukenye,Nyabasi,Bukira,Butimbaru na Buhunyaga leo Mjini Tarime.


  0 0

  Rais wa Mexico, Enrique Pena Nieto, amemteua waziri wa zamani wa fedha, Luis Videgaray kuwa waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo.

  Awali Luis alifutwa kazi kufuatia ziara yake nchini Marekani muda mfupi baada ya kuteuliwa kwa Donald Trump.

  Akizungumzia uteuzi huo wa waziri aliyekuwa amemfukuza kazi, Rais Nieto anasema amechukua hatua hiyo ili kupitia waziri huyo mpya wa mambo ya nje kuweza kuimarisha mahusiano na ujao wa Rais wa Marekani Donald Trump. Chanzo: BBC Swahili

  0 0


  Na Daudi Manongi-MAELEZO

  SERIKALI kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu,Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu kwa kushirikiana na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi – VETA wanaendesha mpango wa kutathmini na kurasimisha ujuzi uliopatikana nje ya Mfumo rasmi wa Mafunzo.

  Kwa mujibu wa Taarifa ya Katibu Mkuu wa Kazi, Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Eric Shitindi, imesema kuwa mpango huo unatoa fursa ya kufanyiwa tathmini ya ujuzi, kupewa mafunzo, kuziba upungufu na kisha kutunukiwa cheti.

  Taarifa hiyo inaeleza kuwa sifa za mwombaji wa mafunzo hayo ni pamoja na uzoefu usiopungua miaka mitano na umri usiozidi miaka 45. Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa fani mbalimbali zitakazohusika ni Uashi, Useremala, Ufundi Magari (makenika), upishi, uhudumu wa hoteli, Bar na Migahawa.

  Ili kufanya maombi waombaji wanatakiwa kufika katika ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa, Mji au Wilaya iliyoko karibu ili kuchukua fomu za kujaza maombi bila malipo yeyote na maombi hayo kuwasilishwa kuanzia tarehe 5 hadi 25 Januari 2017.

  Taarifa hiyo imeongeza kuwa mchakato wote wa tathmini na urasimishaji wa ujuzi utagharamiwa na Serikali na pia watakaokidhi sifa, vigezo na masharti watajulishwa kwa ajili ya usaili kuanzia Tarehe 10 Februari 2017.

  0 0

  Mtu mmoja mwenye umri wa miaka 54 nchini Vietnam, Man Van Nhat ameondolewa kifaa cha upasuaji kilichosahahulika wakati wa kufanyiwa operesheni tumboni mwake kwa miaka 18 iliyopita.

  Madaktari nchini Vietnam wamekiondoa kifaa hicho cha upasuaji kwa mtu ambae amedumu nacho katika mwili wake pasipo kufahamu kwa miaka 18. Televisheni ya taifa VTV imeripoti kuwa Man Van Nhat, mwenye umri wa miaka 54 amesema kifaa hicho kilisahaulika tumboni mwake mwaka 1998 wakati alipofanyiwa upasuaji wa dharura, uliotokana na ajali ya barabarani.

   Kwa mara kadhaa Nnat alikuwa akihisi maumivu ya tumbo na alipokwenda hospitali alipewa dawa za kutuliza vidonda vya tumbo. 

  Lakini baada ya uchunguzi wa X-ray, ambao ulifanyika mwaka jana ikabainika kuwa mzizi wa maumivu yake kuwa ni kifaa hicho kilichosahaulika tumboni. Kifaa cha urefu wa sentimita 15 kikiwa kimegawanyika baada ya kumeguka kilikuwa kikimsababishia maumivu mtu huyo. 

  Mkurugenzi wa hospitali ya Back Kan, Trinh Thi Luong, amekiambia kituo cha televisheni cha VTV, kwamba maafisa wapo katika jitihada za kumsaka yule aliyekiacha kifaa hicho katika tumbo la Nhat. Amesema hata kama tayari wamestaafu watawaeleza ili iwe funzo kwa madaktari wengine.

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Rodrick Mpogolo akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mjini Magharibi, Aziza Mapuri baada ya msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kuwasili Bandari ya Zanzibar leo .
  "NAAM TUMEWASILI KWA MUDA SAHIHI" Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimwambia Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Zanzibar Vuai Ali Vuai baada ya kuwasili Bandari ya Zanzibar leo
  Katibu Mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole (kushoto) baada ya kuwasili Bandari ya Zanzibar
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo (kushoto) alipowasili Bandari ya Zanzibar leo .
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiagwa na viongozi wakati akitoka Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar kwenda kwenye mapumziko kabla ya kwenda kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la Dimani leo jioni. Picha zote na Bashir Nkoromo .


  0 0

  Na Mwamvua Mwinyi,Chalinze

  HALMASHAURI ya mji mdogo wa Chalinze,mkoani Pwani,imetenga kiasi cha sh.mil 36 katika kipindi cha mwaka 2016/2017 kwa ajili ya kuwalipa posho wenyeviti wa vijiji na vitongoji katika halmashauri hiyo.

  Kati ya fedha hiyo wenyeviti hao wanalipwa kila mmoja sh.30,000 kwa mwezi hadi mwezi july mwaka huu itakapokoma bajeti hiyo.

  Akizungumzia kuhusiana na mpango huo,kwa waandishi wa habari mjini hapo,mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Chalinze ,Said Zikatimu ,alisema halmashauri hiyo imeamua kuwalipa posho wenyeviti hao kwani wanafanyakazi kubwa ndani ya miaka mitano bila kuambulia chochote.

  Alisema wameshirikiana na mbunge wa jimbo la Chalinze,Ridhiwani Kikwete,kuona namna ya kuwatupia jicho wenyeviti hao wa vijiji na vitongoji .

  Aidha Zikatimu alieleza kwamba ,fedha hizo zitawawezesha wenyeviti hao kujikimu na kuondokana na hali ya kuuza ardhi za vijiji kwa visingizio vya kukosa posho ama mishahara.Alibainisha ,fedha hiyo pia itaweza kuwasaidia wenyeviti hao kuwa na morali na ari ya kuchapakazi kwenye maeneo yao na wamejipanga kila mwaka watakuwa wakitenga fedha hizo.

  “Kiasi hiki cha sh.mil.36 ni fedha watakazolipwa hadi july 2017 na bajeti inayofuata tutaangalia kama kuna uwezekanao wa kuongeza kiasi kilichopangwa katika bajeti hii ama ibakie kiasi kilichotengwa kwenye bajeti hii”alifafanua Zikatimu.Hata hivyo Zikatimu alisema ,wanachotarajia ni wenyeviti hao kuendelea kuwa wasimamizi wazuri katika vyanzo vya mapato na kuachana na tabia ya kuuza maeneo ya vijiji kinyume na taratibu.

  Alisema wanawahamasisha kusimamia vyanzo vya mapato ili kuinua makusanyo hasa ya vyanzo vya ndani ikiwemo vizuizi mbalimbali vya pembezoni na ndani ya mji huo.Mwenyekiti huyo alitoa wito kwa halmashauri nyingine nchini kuwaangalia wenyeviti hao kwani kwa Chalinze imeshaleta tija ndani ya miezi sita tangu kuanza kwa mpango huo.

  Aliiomba serikali na halmashauri hizo ziangalie namna ya kuwatengea fedha wenyeviti wa vijiji na vitongoji kama ilivyo kwa madiwani na wabunge wanavyotengewa posho wakimaliza muda wao,ili waweze kuwa na moyo wa kufanya kazi pasipo kukosa chochote.“Halmashauri ni sehemu ya kwanza na serikali kuu ni sehemu ya pili,hivyo halmashauri zionyeshe nia ili serikali ilione hili,kwa kuwapa kipaombele ya kuwatengea fedha bila kuwaacha”

  Zikatimu alisema wenyeviti hao wanasimamia chaguzi mbalimbali na ilani ya CCM hivyo waangaliwe katika suala hilo ili waweze kujiona ni viongozi wanaoaminika kwenye maeneo yao.
  Mwenyekiti wa halmashauri ya Chalinze, Saidi Zikatimu, akizungumzia mikakati waliyojiwekea kuwalipa posho wenyeviti wa vijiji na vitongoji sanjali na kuinua mapato ya ndani (Picha na Mwamvua Mwinyi).

  0 0  Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limetoa ratiba ya kombe la mataifa Afrika AFCON yanayotarajiwa kuanza  Januari 14  zikiwa zimesalia siku tisa kufikia kuanza kwa mashindano hayo.


  AFCON  2017 


  14 January 2017
  18:00PM  

  Gabon v Guinea-Bissau
  21:00PM  Burkina Faso v Cameroon
  15 January 2017
  18:00PM  

  Algeria v Zimbabwe
  21:00PM 

  Tunisia v Senegal
  16 January 2017
  18:00PM  

  Cote d'Ivoire v Togo
  21:00PM  

  DR Congo v Morocco
  17 January 2017
  18:00PM  

  Ghana v Uganda
  21:00PM  

  Mali v Egypt
  18 January 2017
  18:00PM  

  Gabon v Burkina Faso
  21:00PM  

  Cameroon v Guinea-Bissau


  19 January 2017
  18:00PM 

  Algeria v Tunisia
  21:00PM  

  Senegal v Zimbabwe
  20 January 2017
  18:00PM 
  Cote d'Ivoire v DR Congo
  21:00PM  
  Morocco v Togo
  21 January 2017
  18:00PM  

  Ghana v Mali
  21:00PM  

  Egypt v Uganda
  22 January 2017
  21:00PM 

  Guinea-Bissau v Burkina Faso
  21:00PM  

  Cameroon v Gabon
  23 January 2017

  21:00PM 

  Senegal v Algeria
  21:00PM 

  Zimbabwe v Tunisia
  24 January 2017
  21:00PM  

  Togo v DR Congo
  21:00PM 

  Morocco v Cote d'Ivoire
  25 January 2017
  21:00PM 

  Egypt v Ghana
  21:00PM  

  Uganda v Mali

  0 0

    Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipata maelezo ya mradi wa maji  kutoka kwa mkurugenzi wa Halimashauri ya  Madaba Bwana Safi Mpenda Waziri Mkuu ameuzindua mradi huo ambao umejengwa katika kijiji cha Magingi wilaya ya Songea,  Mradi ambao una uwezo wa kutoa lita 200000 (laki mbili) na kuhudumia zaidi ya watu 5000 (Elfu tano) katika Halmashauri ya madaba, Songea


   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimtwisha ndoo ya maji Bibi Leonara Kibuno ikiwa ni ishara ya uzinduzi  wa mradi huo ambao umejengwa katika kijiji cha Magingi wilaya ya Songea,Mradi ambao una uwezo wa kutoa lita 200000 (laki mbili) na kuhudumia zaidi ya watu 5000 (Elfu tano) katika Halmashauri ya madaba, Songea

  Waziri mkuu Kassim Majaliwa akiwa hutubia wananchi wa halimashauri ya Madaba.Picha na Chris Mfinanga


  0 0

  Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Askari wa Wanyamapori wa Pori la Akiba la Selous, Kanda ya Kaskazini Mashariki Kingupira imewaokoa wafugaji 50 waliokuwa wakiwapitisha jumla ya ng’ombe 1780, kondoo 200 na punda 6 baada ya kutelekezwa kwa muda wa siku tano na mtu mmoja aliyetajwa kwa jina la Mzigua aliyewarubuni kwa kuwaonyesha njia za mkato ndani ya Pori hilo wao bila kujua na kuamua kuwakimbia. 

  Bw. Lisasi Cherehani ambaye ni mmoja wa wafugaji hao alisema ‘’tulimpa Mzigua kiasi cha zaidi ya shilingi 5,000,000 kutoka kwa wafugaji kama malipo ya kutufikisha eneo la Ilonga mkoani Morogoro tukitokea vijiji vya Ndundunyekanza, Kipungila na Chumbi vilivyopo wilayani Rufiji mkoani Pwani kwa makubaliano kuwa atatupitisha njia fupi ya mkato tutakayotembea kwa muda wa siku tano tu, hatukujua anatutupitisha ndani ya pori hili. ‘’

  Baada ya kutelekezwa, wafugaji hao ambao walikuwa katika hali mbaya waliomba msaada kwa ndugu zao ambao waliwasiliana na Uongozi wa Pori la Akiba la Selous ambao kwa haraka walifanya jitihada za kuokoa maisha yao ikiwa ni kuwapa huduma ya kwanza, maji, uji pamoja na kuwakimbiza hospitalini kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi aliwatembelea wafugaji hao jana kwa ajili ya kuwapa pole na kuwapelekea chakula yakiwemo maji pamoja na unga.

  Aidha, Milanzi aliagiza Wafugaji hao waachiwe huku akitoa wito kwa wananchi kuacha kupita maeneo ya Hifadhi kwa vile ni kosa kisheria na wale wote watakaobainika watachukuliwa hatua za kisheria na kuahidi kuwa mtu huyo aliyewa danganya kwa kuwapitisha ndani ya Hifadhi hiyo ni lazima akamatwe kwa udi na uvumba.

  ‘’Sisi kama Serikali kitu cha kwanza ni ubinadamu tumewahudumia na hivyo natoa tamko la kuwaachia wafugaji wote waliopotea ndani ya Pori hili kwa vile mateso waliyoyapata na mali waliyoipoteza ni kubwa sana baada ya kudanganywa kwa na kupitishwa ndani ya Pori la Akiba la Selous.’’ Alisema Milanzi
     Baadhi wa Wafugaji wakiwa wanakunywa maji na juisi walizopelekewa kama msaada baada ya kuokolewa na Askari wanyamapori wa Pori la Akiba la Selous,  Kanda ya Kaskazini Mashariki  Kingupira  baada ya kutelekezwa kwa muda wa  siku tano na mtu mmoja waliyemtaja kwa  jina maarufu la Mzigua aliyewarubuni kwa kuwaonyesha njia za mkato ndani ya Pori hilo ( Picha na Lusungu Helela-Wizara ya Maliasili na Utalii) 
    Baadhi ya Mzoga wa ngombe uliopatikana ndani ya Pori la Akiba la Selous,  Kanda ya Kaskazini Mashariki  Kingupira  baada ya Wafugaji 50  waliotelekezwa kwa muda wa  siku tano na mtu mmoja waliyemtaja kwa  jina maarufu la Mzigua aliyewarubuni kwa kuwaonyesha njia za mkato ndani ya Pori hilo na kisha kuwakimbia( Picha na Lusungu Helela-Wizara ya Maliasili na Utalii)

     Mmoja wa  wafugaji aliyepotea na  kutelekezwa ndani ya Pori la Akiba la Selous,  Bw. Lisesi Cherehani aliyekuwa na ng’ombe 180 na punda mmoja akiangalia mmoja wa ng'ombe wake aliyekufa kwa kukosa  maji ya kunywa kwa muda  wa siku tano kwenye Kanda ya Kaskazini Mashariki katika Pori la Akiba la Selous ( Picha na Lusungu Helela-Wizara ya Maliasili na Utalii)

   Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence  Milanzi (katikati) akipata taarifa kutoka kwa  Meneja wa Mradi wa Pori la Akiba la Selous    Bw. Enock Msocha (wa tatu kushoto)  mara baada ya  kuwasili kwa ajili ya kuwatembelea  Wafugaji 50 waliokolewa na Askari wanyamapori baada ya kutelekezwa  na mtu mmoja waliyemtaja kwa  jina maarufu la Mzigua aliyewarubuni kwa kuwaonyesha njia ya mkato ndani ya Pori hilo na kisha kuwakimbia ( Picha na Lusungu Helela-Wizara ya Maliasili na Utalii)

  0 0

  Na Amina Kibwana-Globu ya Jamii.
   
  Wizara ya ardhi,nyumba na maendeleo ya Makazi kupitia idara ya nyumba imepewa jukumu la kusimamia mfuko wa mikopo ya Nyumba kwa watumishi wa serikari kwa lengo la kuwawezesha watumishi wake kujenga,kununua au kukarabati nyumba kupitia mkopo huo mwenye masharti nafuu.

  Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Idara ya nyumba Michael Mwalukasa amesema kuwa mfuko huu ulianzishwa kwa ajili ya kusaidia na kuwawawwzesha watumishi wa serikali wanaoishi mjini na vijijini kupata mkopo wa nyumba wenye masharti nafuu kwa ajili ya kujenga au kununua nyumba.

  Ameongeza kuwa mfuko huo unatoa mikopo kuanzia milioni 20 kwa riba ya asilimia tatu ambao muda wa juu wa kurejesha mkopo huo ni miaka thelasini(30) katika kipindi cha utumishi kabla ya kustaafu au anapoacha utumishi kwa sababu zozote zile.

  Mwalusaka amesema kuwa kuna sifa mbalimbali  za kupata mkopo huu ikiwa ni pamoja na mkopaji ni lazima awe mtumishi wa serikali, raia wa Tanzania,aliyeajiriwa kwa masharti ya kudumu na kuthibitishwa kazini pamoja na kuwa na hati ya kiwanja ambacho kitamuwezesha kupata mkopo kwa ajili ya kujenga.

  Kwa upande wake Mkurugenzi msaidizi mikopo ya nyumba Lucy Kabyemera ameeleza faida za mikopo hiyo kwa watumishi wa  serikali ikiwa ni pamoja na kuwawezesha watumishi kupata mikopp yenye riba nafuu, kuweza kumiliki nyumba kwenye maeneo yenye hadhi,kuchochea kasi ya maendeleo kwenye miji na wilaya mbalimbali pamoja na kutoa fursa kwa watumishi kumiliki nyumba kwa kadri ya matakwa yao.

  "Faida zipo nyingi sana kwani pamoja na kunufaika na mikopo baadhi ya wakopaji pia wameendelea kunufaika na ushauri wa kutumia technologia ya bei nafuu ya ujenzi kutokana na tafiti zilizofanywa na taasisi iliyopo chini ya Wizara (NHBRA)."

  Kabyemera ameongeza kwa kusema kuwa ujenzi wa nyumba unahitaji gharama nyingi hivyo ndio maana wameamua kutoa mikopo hasa kwa watumishi wa serikali ili iweze kuwasaidia kwa kuwapa fedha taslimu ya shilingi milioni 20.

  Mfuko wa Mikopo ya Nyumba ni moja wapo ya vyombo vilivyoanzishwa na serikali mara baada ya nchi kupata uhuru mnamo mwaka 1963 kupitia waraka wa watumishi wa serikali na.8 na badae kuendeshwa kupitia waraka wa watumishi wa serikali na.4 wa mwaka 1965.
  Mkurugenzi wa Idara ya Nyumba Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Michael Mwalukasa akizungumza na Waandishi wa Habari Leo Jijini Dar es salaam kuhusu mfuko wa kuwawezesha watumishi wa Serikali kumiliki Nyumba ambapo zaidi ya watumishi 2000 wameshanufaika na mikopo yenye riba nafuu ya asilimia 3 ili kuwawezesha kumiliki nyumba bora. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Mikopo ya Nyumba Bi Lucy Kabyemera na Kushoto
  Mkurugenzi Msaidizi Mikopo ya Nyumba,Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi Lucy Kabyemera akifafanua kwa waandishi wa habari kuhusu faida wanazopata watumishi wa Umma kutokana na mikopo inayotolewa na Serikali ili kuwawezesha kumiliki makazi bora. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Nyumba Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Michael Mwalukasa.Picha na Frank Mvungi-Maelezo.


  0 0

  Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa za kiuhalifu zilizotokea hivi karibuni katika maeneo mbalimbali, ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.
  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  WATU watatu wanaodaiwa kuwa ni majambazi wameuawa katika shambulio la kutupiana risasi na Askari Polisi walipokuwa wakitaka kufanya tukio la ujambazi maeneo ya Mikocheni, Jijini Dar es salaam jana.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro, amesema watu hao wanaodaiwa kuwa majambazi inadaiwa walifanya tukio la unyanganyi juzi maeneo ya Tazara ambapo waliondoka na sh.milioni 26.

  Kamanda Sirro, amesema watu hao walikuwa wanne ambapo watatu waliuawa wakati wakirushiana risasi na polisi.

  Amesema watu hao walikuwa wakifanya tukio la ujambazi kwa kutumia pikipiki ambapo katika tukio hilo mmoja alitoweka na usafiri huo.

  Sirro amesema ndugu zao kama wanawatafuta polisi watatoa msaada wa kupeleka miili yao ili waweze kuhifadhi.

  Katika matukio mengine, Jeshi la Polisi limewakamata vijana wanne wanadaiwa kufanya wizi wa vitu mbalimbali ikiwe  Computa, ving'amuzi katika ofisi ya mpiga chapa mkuu wa serikali, walikamatwa na hakuna mahusiano ya wafanyakazi wa ofisi hiyo kuhusika katika tukio hilo.

  Wakati huo huo jeshi la Polisi linamshikilia Mlinzi wa Kampuni ya Ulinzi ya Amadori, Anwaz Ally (45) aliyekutwa na silaha ya moto katika sehemu ya maungo ya mwili wake aina ya berretta na risasi 23 huku akiwa hana kibali cha umiliki wa silaha hiyo.

  Aidha Polisi inamshikilia mtu mmoja anayedaiwa  kufanya uhalifu kwa watalii waliokuwepo Wilaya ya Mkuranga na kuchukua vitu mbalimbali na upelelezi unaendelea kutafuta mtandao huo.
  Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akionyesha silaha iliyokutwa na mlizi huko kigamboni leo jijini Dar es Salaam.
  Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro akionyesha magari yaliyokuwa yameibiwa katika sehemu mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam leo.Pich na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

  0 0

  Na Anthony John, Globu ya Jamii 

  MWILI wa aliyekuwa Mgombea wa Urais Mwanamke kupitia Chama Cha PPT Maendeleo Dkt, Anna Senkoro unatarajiwa kuagwa Jumamosi katika kanisa la Winner Chaapel International lililopo Ukonga Jijini Dar es salaam majira ya saa saba mchana na ibada itakayoongozwa na Mchungaji Samuel Adeyemi. 

  Akizungumza leo na waandishi wa habari katika makazi ya marehemu huyo Tabata jijini Dar es Salaam ,Mdogo wa Marehemu George Nathaniel amesema baada ya kumaliza ibada ya kuagwa mwili huo utaapelekwa katika Makaburi ya Kinondoni kwa ajili ya mazishi. 

  Nae Mbunge wa Zamani wa Jimbo la Ukonga, Dkt Makongoro Mahanga amesema ameupokea msiba huo kwa masikitiko makubwa ya kuondokewa na mwanaharakati wa siasa na kuwaomba wana familia kushirikiana katika kipindi hiki kigumu cha majonzi. 

  Makongoro, amesema marehemu Dkt. Anna alikuwa mfano wa kuigwa katika jamii kwa uhodari wake.Aidha mtoto wa pili wa marehemu Joan Senkoro amesema bado wataendelea kumuombea mama yao kwa Mungu na amejifunza mengi ikiwemo msimamo aliokuwa nao mama yake. 
  Aliyekuwa Mbunge wa Ukonga, Dkt. Makongoro Mahaga akizungumza katika Msiba wa aliyekuwa Mgombea wa Uraisi wa Chama cha PPT Maendeleo,Dkt.Anna Senkoro leo jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya waombolezaji waliofika katika Msiba wa aliyekuwa Mgombea wa Uraisi wa Chama cha PPT Maendeleo, Dkt.Anna Senkoro, leo jijini Dar es Salaam. Picha na Bakari Madjeshi wa Globu ya Jamii. 


  0 0

  LakeFmHabari

  Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, ameonya juu ya suala la uchafu kukithiri kwenye wodi za wagonjwa katika vituo vya kutolea huduma za afya ikiwemo hospitali ya rufaa ya Sekour Toure.

  Mongella ametoa onyo hilo hii leo wakati akikabidhi msaada wa vitanda, magodoro, mashuka pamoja na vyandarua, uliotolewa na mbunge wa Viti maalumu kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Mkoani Mwanza, Kemirembe Lwota.

  Ameeleza kusikitishwa na hali ya uchafu katika wodi za wagonjwa hususani akina mama katika Vituo vya Afya, Zahanati pamoja na Hospitali huku akikuta mashuka mpya yamehifadhiwa stoo kwenye baadhi ya vituo hivyo.

  “Na siyo hapa Sekour Toure tu, hata maeneo mengine, huwa nasikitika sana ninapokuta shuka chafu kitandani. Bahati mbaya nimewahi kwenda mahali nikakuta shuka mpya stoo, mimi nasema hizi shuka zitumike, zichakae, tutafute zingine”. Amesisitiza Mongella na kutaka suala la usafi kupewa kipaumbele zaidi.

  Mganga Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Dkt.Leonard Subi, amesema huduma za afya zinaendelea kuboreshwa licha ya kuwepo uhitaji mkubwa wa vitendea kazi ambapo kwa siku yanahitajika mashuka manane kwa kila kitanda.

  Mbunge wa Viti Maalumu CCM Mkoani Mwanza, Kemirembe Lwota, amewahimiza wadau wengine kujitokeza ili kusaidia kutatua kero za huduma za afya, huku akiishukuru taasisi ya Mo Dewji kwa kusaidia upatikanaji wa msaada huo ambao ni mashuka 100, vitanda 20, magodoro 20 pamoja na vyandarua 20 wenye thamani ya shilingi Milioni 25.

  Mkuu wa Taasisi ya Mo Dewji, Barbara Gonzales, amesema taasisi hiyo imedhamiria kusaidia uboreshaji wa huduma mbalimbali katika nyanza za elimu, afya pamoja na maendeleo ya jamii ili kuboresha zaidi maisha ya wananchi.

  Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, akizungumza hii leo, kabla ya kukabidhi msaada wa vitanda 20, magodoro 20, vyandarua 20 pamoja na mashuka 100, uliotolewa na mbunge wa Viti Maalumu kupitia Chama cha Mapinduzi CCM mkoani Mwanza, Kemirembe Lwota.

  Ameonya juu ya suala la uchafu kukithiri kwenye wodi za wagonjwa katika vituo vya kutolea huduma za afya ikiwemo hospitali ya rufaa ya Sekour Toure.

  Na BMG

  Mganga Mkuu mkoani Mwanza, Dkt.Leonard Subi, akizungumza kwenye utoaji wa msaada huo
  Mbunge wa Viti Maalumu CCM mkoani Mwanza, Kemirembe Lwota, akizungumza wakati wa utoaji wa msaada huo
  Mkuu wa Taasisi ya Mo Dewji, Barbara Gonzales, akizungumza wakati wa utoaji wa msaada huo
  Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella (kushoto), akimpongeza Mbunge wa Viti Maalumu CCM mkoani Mwanza, Kemirembe Lwota, baada ya kufanikisha upatikanaji wa msaada 

  0 0

  Familia ya marehemu Hamadi Kiluvia inapenda kutoa shukrani zao za dhati kwa ndugu jamaa na marafiki kwa ushirikiano wenu mkubwa mliouonyesha katika msiba wa baba Yao mpendwa Hamadi Kiluvia ambaye alifariki dunia mnamo tarehe 23/11/2016

  Familia inapenda kuwashukuru kwa ushirikiano wao Raisi Mstaafu Dr Jakaya Kikeete,Waziri MKuu mstaafu Cleopa Msuya,Naibu Speaker Dr Tulia Ackson,Mbunge wa Chalinze muheshimiwa Ridhiwani Kikwete viongozi wengine wa mbalimbali wa seri Kali walioweza kufika na kushirikiana Nao katika msiba WA baba yao

  Tunapenda pia kuwashukuru IPP media,redio clouds na groove back entertainment,pia tunapenda kuwashukuru Misokia catering 
  Tunapenda kuushukuru uongozi wa Yanga na TFFA 
  Familia inapenda kutoa shukrani zao kutoka Moyoni kwa wote mlioshiriki katika msiba huu

  Dua;

  Famila ya marehemu mzee Hamadi Kiluvia inapenda kuwakaribisha Kwenye hitmah Dua ya kumaliza msiba itayofanyika nyumbani kwa marehemu no93 Regent Estate migombani road Siku ya tarehe 07/01/2017 kwa kuelekezwa piga no 0768768284 or 0657755555

  Asanteni sana Mungu awabiriki.

older | 1 | .... | 1492 | 1493 | (Page 1494) | 1495 | 1496 | .... | 3272 | newer