Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110105 articles
Browse latest View live

WANASHERIA OFISI YA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM WAJIUNGA NA PSPF

$
0
0
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said.

WATUMISHI wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kitengo cha sheria, wamejiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF baada ya kuhudhuria semina ya mafunzo ya siku mbili iliyomalizika leo Januari 4, 2017.

Semina hiyo iliandaliwa na Mfuko huo kufuatia ombi la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makodna, kutaka wanasheria wa ofisi yake, wapewe semina ili kuwajengea uwezo wa kutatua kero za wananchi ambao ni wanachama wa Mfuko huo watakaofika Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa kwa shida zinazohusiana na masuala ya Mafao na Pensheni.

Katika senmina hiyo iliyoanza Januari 3, 2017, wanasheria hao walipatiwa ufafanuzi wa kina kuhusu shughuli namajukumu yanayotekelezwa na PSPF.

Meneja wa PSPF huduma kwa wateja, Bi.Leila Magimbi, alitaja majukumu hayo kuwa ni pamoja na kutambua na kusajili wanachama wapya, kukusanyan michango na kutunza taarifa za michango ya wanachama, kuwekeza michango katika vitegauchumi mbalimbali na kulipa mafao.

Shughuli nyingine zinazotekelezwa na Mfuko huo ni kulipa mafao kwa wanaostahili kwa mujibu wa sheria, kutunza kumbukumbu za wanachama na wastaafu, kuangalia upya ubora wa mafao na kufanya tathmini ya Mfuko na kuweka mikakati endelevu, aliongeza Bi. Magimbi.

Pia wanasheria hao walipata fursa ya kuelezwa aina za wanachama wa PSPF ambao ni Watumishi wa Umma, sekta binafsi ambao hawa watachangia katika mfumo wa uchangiaji wa lazima na watu wote walio katika sekta isiyo rasmi, ambao wao watachangia katika Mfumo wa uchangiaji wa Hiari.

Aidha faina apatazo mwanachama wa PSPF, kwa mujibu wa Kaimu Meneja Mafao, Bw.Haji Moshi, ni pamoja na Fao la uzazi, mkopo wa elimu, mkopo kwa mwajiriwa mpya, mikopo ya viwanja, mikopo ya nyumba, mkopo wa fedha taslimu, mikopo kwa wastaafu yenye masharti nafuu, mafao ya muda mrefu, fao la ulemavu, fao la mirathi, fao la kufukuzwa au kuachishwa kazi, na bima ya afya.

Akifunga semina hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, amewataka wanasheria hao kutumia busara wanapohudumia wananchi kwani kwa kufanya hivyo itawasaidia kurahisisha utoaji huduma kwa wananchi kama ilivyokusudiwa.

“Huko mtakutana na watu wa aina mbalimbali, wengine wamesoma zaidi yenu, wengine hawakupata fursa ya kusoma kama nyinyi, kwa hivyo mnao wajibu wa kutunmia busara katika kuhudumia wananchi wa kada tofauti tofauti.” Aliwaasa Bw. Mayingu.

Aidha mwakilishi wa wanasheria hao, Bi.Georgia Ephraim Kamina, amesema semina hiyo imekuwa na manufaa makubwa kwao, na kuishukuru PSPF kwa kuandaa semina hiyo na kuuomba uongozi wa Mfuko, kujenga mahusiano ya kudumu baina ya Mfuko na wanasheria hao katika utendaji kazi wao wa kuhudumia wananchi.
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu akitoa nasaha zake wakati wa kufunga semina hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma na uendeshaji, Bi. Neema Muro
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu akitoa nasaha zake mbele ya wanasemina hao wakati wa kufunga semina hiyo
Wanasemina wakitembelea kitengo cha kutunza kumbukumbu cha PSPF.
Sehemu ya utunzaji nyaraka kwenye mfumo wa makabati yanayoendeshwa kielektroniki
Afisa Uendeshaji wa PSPF, Hadji Hamisi Jamadari, akitoa ufafanuaiz kuhusu kazi zifanywazo na Mfuko huo, hususan uchangiaji wa hiari, (PSS), mwishoni mwa seina ya mafunzo ya siku mbili, kwa watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kitengo cha sheria, iliyomalizika leo Januari 4, 2017. Baada ya semina hiyo wanasheria hao zaidi ya 35 walijiunga na Mfuko huo kupitia mpangio huo wa PSS.
Afisa Masoko Mwandamizi wa PSPF, Bw. Magira Werema, akifafanua masuala kadhaa yahusuyo shughuli za Mfuko na faida zake kwa wanachama.





MASAUNI ATEMBELEA MAGEREZA UKONGA,AJIONEA SHUGHULI MBALIMBALI ZINAZOFANYWA NA JESHI HILO

$
0
0
  Na Anthony John Glob Jamii.

NAIBU Waziri  mambo ya Ndani  Mhandisi Hamad Masauni amelitaka jeshi la zimamoto na  Uhamiaji kutoshona sare zao za uraiani, badala yake wakashone katika jeshi  la Magereza ili kubana matumizi ya serikali.

Masauni ameyasema hayo  leo katika  ziara yake ya kutembelea  Magereza Ukonga,jijini Dar, ambapo amekagua  Kiwanda  cha Magereza kinachojishughulisha na ushonaji wa nguo za wafungwa na nguo za askari Magereza.

Sanjari na hayo Mhandisi Masauni ametoa wito  kwa Watanzania kwa kununua  bidhaa mbali mbali zinazo tengenezwa na jesi la Magereza ili kuunga mkono kwa kazi nzuri wanazozifanya.
 
Aidha amewapongeza askari wa jeshi la  Magereza kwa kujitolea kujenga nyumba zao bila kusubiri serikali kuwajengea na kuwaahidi kuwa Serikali itaandaa bajeti Mwakani ili kumalizia maeneo machache yaliyo baki.

Naye   kaimu Mkuu wa Magereza  Kamishina Msaidizi . Juma Malewa amesema Jeshi hilo linakabiliwa na uhaba wa vitendea kazi  kama mashine za  kushonea nguo, na mashine za za ufundi selemala , ukosefu wa mtaji wa kuendesha shughuli za kilimo,  hivyo amesema pindi serikali itakapo wawezesha watajitosheleza kwa chakula na mahitaji mengine. 
 Naibu waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Masauni akiwa na Mkuu wa Magereza kamishna Juma Malewa wakizungumza  na Waandishi  wa Habari leo katika gereza la Ukonga Jijini Dar es salaam.
 .Naibu Waziri  wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Masauni akizungumza jambo na  Mratibu wa Ujenzi wa Nyumba za Askari Magereza Bw. Julious Chege  katika gereza hilo la Ukonga,jijini Dar.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Masauni akizungumza jambo na Kaimu kamishna wa Jeshi la Magereza Juma Malewa,mara baada ya kukagua Kiwanda cha kutengeneza Samani Katika gereza la Ukonga.

BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 04/01/2017

MHASIBU WA KIJIJI TUNDURU MBARONI KWA KUKATAA KUSOMA MAPATO NA MATUMIZI

$
0
0

Mhasibu wa kijiji cha Huria mkoani wilaya ya Tunduru atiwa mbaroni kwa kukataa kusoma mapato na matumizi ya kijiji. Kwa undani wa habari angalia video yake.

BEI YA MAZAO - MCHELE NA VIAZI JIJINI MBEYA

UZINDUZI WA VIFAA VIPYA VYA KUFANYIA KAZI BANDARINI ZANZIBAR

$
0
0
 Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji Mhe,Ali Abeid Amani Karume,alipokuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) katika hafla ya Uzinduzi wa  Vifaa vipya vya kufanyia kazi Bandarini ikiwemo Makontena na Mizigo mizito leo,ikiwa ni shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akitoa hutuba yake ya Uzinduzi wa Vifaa vipya vya kufanyia kazi katika Bandari ya Malindi Mjini Unguja leo ikiwemo  Makontena ya mizigo mizito,ikiwa ni shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kulia) Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji Mhe,Ali Abeid Amani Karume,(kushoto) Makamo wa Pili wa  Rais wa Zanzibar Mhe,Balozi Seif Ali Iddi na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Bandari Bw.Salmin Senga.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Vifaa vipya vya kufanyia kazi katika Bandari ya Malindi Mjini Unguja leo ikiwemo  Makontena ya mizigo mizito wakiwepo na Viongozi mbali mbali,  ikiwa ni shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Mashine ya 
 ​Reach
  
 ​Stacker ​
 yenye uwezo wa kunyanyua Tani 
 ​45
  ikionesha namna inavyoweza kufanya 
 ​kutoa huduma 
 Makontena 
 ​baada ya kushushwa ​
 katika Meli 
 ​ 
 na kupanga sehemu ya kuhifadhia (Container Yard) mara baada ya Uzinduzi wa 
Vifaa vipya vya kufanyia kazi katika Bandari ya Malindi Mjini Unguja

 Mashine ya Mobile Harbour Crane LHM 280 yenye uwezo wa kunyanyua Tani 64 ikionesha namna inavyoweza kufanya kazi katika kushusha Makontena katika Meli pia na kupanga sehemu ya kuhifadhia (Container Yard) mara baada ya Uzinduzi wa Vifaa vipya vya kufanyia kazi katika Bandari ya Malindi Mjini Unguja. Picha zaidi BOFYA HAPA


AMSHA KIPAJI CHAKO NA MICHUZI TV...GOLIATH WA MBEYA KAPENYA

Mwanamuziki Janet Jackson apata mtoto akiwa kagonga Fifte

$
0
0
Mwanamuziki maarufu nchini Marekani na Duniani kwa ujumla, Janet Jackson amejifungua mtoto wa kwanza (mtoto wa kiume) akiwa na umri wa miaka 50.

Taarifa hiyo iliyothibitishwa na afisa wake wa mawasiliano imesema mwanamuziki huyo na mumewe Wissam Al Mana, ambaye ni mfanyabiashara kutoka Qatar, wana furaha kumpata mtoto wa kiume ambaye wamempa jina la Eissa Al Mana.

"Janet alijifungua bila matatizo yoyote na kwa sasa anapumzika," alisema afisa wake huyo.
Janet Jackson ndiye mwanamke maarufu wa pekee aliyejifungua mtoto akiwa na umri mkubwa, wakati Mshindi wa tuzo ya Oscar, Halle Berry alijifungua mtoto wake wa pili akiwa na miaka 47 miaka mitatu iliyopita, wakati mke wa Mcheza filamu John Travolta, Kelly Preston, alijifungua mtoto wake wa tatu akiwa na miaka 48. ambapo huko nchini India nako kuna wanawake watatu ambao wamedaiwa kujifungua watoto wakiwa na umri wa zaidi ya miaka 70.
Janet Jackson na hazbendi wake Wissam Al Mana waliponaswa wakipiga misele katika mitaa ya Jiji la London, Nchini Uingeleza, miezi michache iliyopita.

MKUU WA MAJESHI NCHINI GAMBIA ATANGAZA KUMUUNGA MKONO RAIS ALIYOPO MADARAKANI SASA

$
0
0
Mkuu wa jeshi la taifa la Gambia, Jenerali Ousman Badjie ametangaza kumuunga mkono rais wa taifa hilo Yahya Jammeh licha ya mgogoro unaondelea nchini humo, kufuatia matokea ya Uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana.

Rais Jammeh alishindwa katika uchaguzi mkuu wa urais wa nchi hiyo na mpinzania Adama Barrow. Awali alikubali matokeo ya uchaguzi huo lakini alibadili uamuzi siku kadhaa baadaye akitaja kuwepo kwa udanganyifu wa matokeo ya kura katika uchaguzi huo.

Katika taarifa iliyotolewa na magazeti yanayounga mkono serikali, Jenerali Ousman Badjie aliahidi kwamba jeshi litaendelea kumtii rais huyo ambaye bado yuko madarakani sasa.

Uingiliaji wa kati wa Jenerali Badjie unafuatia vitisho vya kijeshi vya jamii ya kiuchumi ya mataifa ya Magharibi ECOWAS iwapo Jammeh atakataa kuondoka madarakani ifikiapo Januari 19.

Rais Jammeh amesema kuwa hatua yoyote kama hiyo itasababisha vita.

Kundi la bwana Barrow awali lilikuwa limedai kuungwa mkono na Jenerali Badjie.
Hatua hiyo ya Jeshi inaonekana kuleta utata katika kuanzisha serikai mpya baada ya Jammeh iliyokuwa madarakani kwa miaka 22.

Taifa hilo dogo la Afrika magharibi halijawahi kuwa na ukabidhi wa mamlaka kutoka uongozi mmoja hadi mwengine kwa njia ya amani tangu taifa hilo lijipatie Uhuru wake kutoka kwa Uingereza mwaka 1965.

Mzozo kuhusiana na matokeo ya uchaguzi umesababisha wasiwasi, huku mataifa jirani na jamii ya kimataifa yakimtaka rais Jammeh kuondoka mamlakani. chanzo: BBC Swahili

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS JANUARI 5, 2016

INTRODUCING RAMA DEE - MAZOEA

MAAGIZO MATATU YA WAZIRI MKUU KWA SERIKALI YA MKOA WA RUVUMA

$
0
0
Baada ya kusomewa taarifa ya mkoa wa Ruvuma na mkuu wa mkoa huo Dokta Binilith Mahenge katika ikulu ndogo ya Songea , Waziri mkuu wa Jamhuri ya Tanzania Kassim Majaliwa akatoa maagizo matatu ambayo ambayo mkoa huo unatakiwa kuyatekeleza.

SENDOFF YA MUNIRA BAWAZIRI NA AMIRI MONGI ILIVYONOGA JIJINI ARUSHA.

$
0
0
Wakwanza kushoto ni ndugu Amin Mongi,akifuatia na  pili kushoto ni Katibu wa Arusha Press Club(APC) ndugu Amir Mongi (bwana harusi mtarajiwa)akiwa na mkewe mtarajiwa ,Wa kwanza kulia  bi Millen Amin ,siku ya sendof Jijini Arusha.Picha na Vero Ignatus Blog

LEO NI SIKU YA KUZALIWA KWA MTOTO BRAYDEN MOSES MWANGENDE

$
0
0
Leo Tarehe 05/01/2017,familia ya Bwana na Bibi Moses Mwangende wa Dar es salam wanapenda   kumtakia  kheri mtoto wao mpendwa Brayden kwa kutimiza miaka 5. Tunakuombea kwa Mwenyezi Mungu akukuze na kukupa  afya njema. Tunakupenda 

NAIBU WAZIRI JAFFO AAGIZA KUUNDWA TUME YA KUCHUNGUZA MAMILIONI YA FEDHA YALIY0TOLEWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MKURANGA

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Seleman Jaffo amemuagiza Katibu Tawala Mkoa wa Pwani kuunda Tume ya kuchunguza upotevu wa fedha za dawa katika Hospitali ya Mkuranga, Mfumo wa ukusanyasaji wa mapato kwa kutumia stakabadhi.

Jaffo ametoa agizo hilo wakati alipokutana na watendaji wa Halmashauri ya Mkuranga mapema jana, amesema serikali ilitoa sh. milioni 258 kwa ajili ukarabati wa Hospitali kati ya hizo Sh. milioni 86 ni za kununulia dawa, lakini dawa zilizonunuliwa katika Hospitali hiyo ni za sh. Milioni 22 na fedha iliyobaki haina majibu

Amsema wananchi wanahitaji dawa kutokana na fedha wanayochangia katika huduma ya afya, kukosa dawa kwao suala ambalo sio matarajio yao.
Jaffo amesema ukusanyaji mapato katika hospitali ya Mkuranga sio mzuri kutokana na kutumia mfumo wa makaratasi ikilinganishwa na sehemu nyingine kutokana na kutumia mashine za Kieletroniki.

Amesema Hospitali ya Mkuranga inakusanya mapato ya sh. Milioni 2.7 kwa mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana sh. milioni 2.1 ambapo ongezeko lake ni sh. 600, 000 wakati Hospitali zingine zinakusanya zaidi ya sh. milioni 20.

Mwitikio wa kufika kwa Naibu Waziri Jaffo kulitokana na ombi la Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega ambaye alifanya ziara katika vijiji 90 na malalamiko ya wananchi ni ukosefu wa dawa katika Hospiali ya Wilaya, Vituo vya Afya pamoja na Zahanati.

Hata hivyo, Jaffo ametoa agizo la Kisima cha Mwarusembe ndani ya siku tatu awe amepata majibu ya kuridhisha kutokana wananchi kukosa maji kwa muda mrefu. Nae Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega amesema wananchi wanaweza kuondokana na tatizo la kukosa dawa kutokakana watendaji kufuata taratibu za uombaji.

.Naibu Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Seleman Jaffo akizungumza na watumishi wa afya katika Hospitali ya Mkuranga mapema jana alipofanya ziara katika Wilaya hiyo .
Naibu Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Seleman Jaffo akipata maelezo ya Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega juu ya wananchi kulalamikia upatikanaji wa dawa katika Hospitali ya Mkuranga katika Mkutano wa hadhara uliofanyika hivi karibuni.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

Muonekano wa Wodi ya Wazazi Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga ambapo Naibu Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Seleman Jaffo alifanya ziara mapema jana .

Naibu Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Seleman Jaffo akielezwa na mgonjwa, Emiliana shila aliyefika katika Hospitali Mkuranga akiwa na vifaa Tiba na Dawa alizoambiwa akanunue nje .
Naibu Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Seleman Jaffo akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga mapema jana alipofanya ziara katika Wilaya hiyo.


Article 3

KANISA LA POOL OF SLOAM LATOA MSAADA WA MATAILI MATANO KWA KITUO CHA POLISI NGURUKA MKOANI KIGOMA

$
0
0

Na Abel Daud,KIGOMA 

Kupitia jitihada za zinazofanywa na Asasi,taasisi,makampuni na watu binafsi,kwa kuunga mkono juhudi za Serikali kwa lengo la kukamilisha huduma mbalimbali kwa Umma ,Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma amepokea jumla ya mataili 05 yenye thamani ya shilingi millioni mbili na laki nane ili kuboresha gari la polisi la kituo cha Nguruka kata ya Nguruka wilayani Uvinza.

Akipokea mataili hayo yaliyotolewa na kanisa la Pool of Sloam,kwa niaba ya Naibu kamishina wa polisi Mkoani Kigoma,Ferdinand Mtui,mkuu wa polisi wilaya ya Uvinza Amedeus Malenge amesema kuwa kitendo kilichofanywa na kanisa hilo kitasaidia kuifikia jamii kwa wakati hasa wahalifu.

Kwa upande wake Kuhani UFAHAMU HAKIKAZI ambaye alimwakilisha kiongozi mkuu wa kanisa hilo hapa nchini,amesema kuwa baada ya kupata taarifa ya uhitaji wa mataili hayo,kanisa limechukua hatua hiyo kwa kuwa kanisa na Serikali hufanya kazi pamoja katika kukamilisha huduma za kijamii.

Aidha kuhani.HAKIKAZI ameongeza kuwa ,kupitia mahitaji ya kuboreshwa kituo cha polisi kilichopo kijijini humo,amesema kuwa amelichukua na atalifikisha kwa uongozi wa kanisa ili kuona namna linavyoweza kufanyiwa ufumbuzi wa kuboresha kituo hicho.

Nao viongozi wa kijijini humo akiwemo mwenyekiti wa kijiji cha nguruka Bw.Mosha Mohamed na mwenyekiti wa kitongoji cha nguruka kusini Hamis Kiliza,wamesema kuwa kwa kuwa huduma ya polisi inauhitaji mkubwa kwa jamii,mataili hayo yatasaidia kupunguza uhalifu kwa kuwa kazi sasa zitafanyika kwa wakati huku wakiomba kuboreshwa tena kwa kituo hicho cha polisi kwa kuwa sasa hakitoshi kutoa huduma kulingana na wingi wa wahalifu wanaowekwa ndani ya kituo hicho.
 Kuhani Ufahamu akipeana mkona na Mkuu wa Polisi wilaya ya Uvinza mara baada ya kumkabidhi mataili hayo.
  Wakijadili.jambo nje ya kituo hicho cha polisi Nguruka
Matairi hayo yaliyokabidhiwa katika kituo hicho cha polisi Nguruka.

WAZIRI MKUU AONGOZA MAMIA KUMZIKA KAPTENI MHAIKI, SONGEA

$
0
0
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  na mkewe Mery Majaliwa wakiweka shada la maua katika kaburi la aliye kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali Kapteni  Kenan Mhaiki  aliyefariki tarehe 31/12/2016 na kuzikwa tarehe 4/1/2017 kijijini kwao Matogoro Mkoani Ruvuma
 
 Waziri mkuu Kassim Majaliwa  akitoa salamu za serikali katika misa ya kumuombea marehemu Kapteni Kenan Mhaiki iliyofanyika katika kanisa la Jimbo kuu Katoliki la Songea  Parokia ya Mtoto Yesu  Matogoro, Songea
 
 Mjane wa Marehemu  Kapteni Kenan Mhaiki  akiweka shada la maua katika kaburi la mume wake
 Watoto wa Marehemu Kapteni Kenan Mhaiki wakiweka Mashada ya maua katika kaburi la Baba yao

Jeneza lenye mwili wa marehemu Kapteni Kenan Mhaiki wakati wa misa ya kumuombea katika kanisa la Jimbo kuu Katoliki la Songea  Parokia ya Mtoto Yesu  Matogoro, Songea. Picha na Chris Mfinanga

BEI YA MADAFU LEO

zaidi ya watumishi wa serikali 2000 wameshanufaika na mikopo yenye riba nafuu - Mwalukasa

$
0
0
 Mkurugenzi wa Idara ya Nyumba Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Michael Mwalukasa akizungumza na Waandishi wa Habari Leo Jijini Dar es salaam kuhusu mfuko wa kuwawezesha watumishi wa Serikali kumiliki Nyumba ambapo zaidi ya watumishi 2000 wameshanufaika na mikopo yenye riba nafuu ya asilimia 3 ili kuwawezesha kumiliki nyumba bora. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Mikopo ya Nyumba Bi Lucy Kabyemera na Kushoto ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Bi Fatma Salum.
Mkurugenzi Msaidizi Mikopo ya Nyumba,Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi Lucy Kabyemera akifafanua kwa waandishi wa habari kuhusu faida wanazopata watumishi wa Umma kutokana na mikopo inayotolewa na Serikali ili kuwawezesha kumiliki makazi bora.  Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Nyumba Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Michael Mwalukasa. Picha na Frank Mvungi-Maelezo

Viewing all 110105 articles
Browse latest View live




Latest Images