Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

MAKAMBA ATEUA WAJUMBE BODI YA NETFUND.

$
0
0
Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (anayeshughulikia Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba ameteua wajumbe wa Bodi ya wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Dhamana ya Hifadhi ya Mazingira Nchini (National Environmental Trust Fund - NETFUND).

Waziri huyo amefanya uteuzi huo leo jijini Dar es salaam kufuatia uamuzi wa Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kumteua Ali Mafuruki kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko huo.

Mh. Waziri Makamba amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa Sheria ya mazingira Sura ya 191 ya mwaka 2004, kifungu cha 215 (2).

Uteuzi huo ni kufuatia mabadiliko madogo yaliyofanyika hivi karibuni kwenye Sheria ya mazingira ambapo Bodi itakuwa na uwezo na mamlaka ya kualika mtu yeyote ambaye siyo mjumbe kushiriki katika maamuzi pale inapoona inafaa

Amewataja wajumbe walioteuliwa kuwa ni Mwajuma Mbogoyo, Emelda Teikwa, Profesa Razak Bakari Lokina na Hatibu Senkoro.Wengine ni Alesia Mbuya, Baraka Juma Kalangahe,Dkt. Andrew Komba na Profesa Yunus Mgaya.

Mhe. Makamba amesema kuwa uteuzi huo unaanza mara moja na kuwatakia kila la heri wajumbe wapya wa Bodi hiyo katika kutekeleza majukumu yao kama yalivyoainishwa katika Sheria.

WAZIRI MKUU AONYA VITA YA MADIWANI NA WATUMISHI

$
0
0
*Ataka Wakuu wa Idara watoe ushauri wa kitaalamu bila woga   

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Wakuu wa Idara kwenye Halmashauri za Wilaya na Manispaa wasaidie kutoa utaalamu badala ya kupingana na madiwani ili wawezeshe kuleta maendeleo kwa wananchi.

Pia amewataka madiwani wasikilize ushauri wa kitaalamu unaotolewa na Wakuu wa Idara katika utekelezaji wa miradi iliyotengwa na Halmashauri.

Ametoa wito huo leo mchana (Alhamisi, Januari 5, 2017) wakati akizungumza na watumishi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Mabada na viongozi na watendaji wa mkoa wa Ruvuma akiwa katika siku ya pili ya ziara yake mkoani humo.

“Wakuu wa Idara nyie ni washauri. Tumieni taaluma zenu kutoa ushauri, semeni bila woga pale inapodidi. Ninawasihi waheshimiwa madiwani wasitumie fursa yao ya ‘kuazimia’ pale inapotokea kuna watumishi wenye msimamo,” amesema.

Akizungumzia kuhsu ukusanyaji wa mapato, Waziri Mkuu amesema Serikali iko makini kwenye matumizi kwa kila senti inayokusanywa na akawataka watumishi hao kila mmoja aongeze mapato ya Serikali kupitia sekta aliyopo. Pia amepiga marufuku matumizi holela ya fedha za umma.

“Kuanzia leo, marufuku kwa fedha iliyokusanya kwa mapato ya ndani kutumika bila utaratibu. Serikali hii haina mzaha na miradi inayotekelezwa chini ya viwango. Mtumishi ukiharibu hapa Madaba, usidhani utahamishwa, tunamalizana na wewe hapahapa. Wala usiombe ndugu yako akuombee uhamisho, tutakufuata hukohuko,” amesisitiza.

Amewataka watumishi wa umma wote watumie Ilani ya Chaguzi ya CCM katika kutekeleza majukumu kwani inaeleza kila kitu ambacho Serikali inatakiwa kukifanya katika kipindi ca miaka mitano.

“Zaidi ya hayo, ninawasihi kila Mkurugenzi atoe nakala ya hotuba ya Mheshimiwa Rais ambayo aliitoa Novemba 20, 2015 wakati akizindua Bunge la 11, awape watendaji wake waisome na kufanyia kazi maeneo yote aliyoyaainisha kwani ilitoa dira ya nini anataka kufanya katika Serikali hii,” amesema.

Waziri Mkuu amesema Serikali kwa upande wake inaendelea kuboresha maslahi ya watumishi na imeanza kulipa madeni yaliyokuwa yamelimbikizwa. “Serikali imedhamiria kupunguza madeni ya watumishi na hadi kufikia Novemba 30, 2015 jumala ya sh. bilioni 28.9 zilikuwa zimekwishlipwa kwa watumishi 31,032 wenye madai katika sekta mbalimbali. Zoezi hili linaendelea.”

Alitumia fursa hiyo kuwakumbusha watumishi wa wilaya hiyo wajibu wao wa kuwahudumia Watanzania bila kujali dini, itikadi, kabila au hali zao na akasisitiza kuwa Serikali haitamuonea mtumishi yeyote ambaye anatimiza wajibu wake.

Akifafanua kuhusu upandishaji madaraja ya watumishi, Waziri Mkuu amesema Serikali imeondoa utaratibu wa mtumishi kulazimika kuandika barua ya kukiri kupandishwa daraja/cheo ndipo aanze kupata stahili zake mpya.

"Hii imeondoa ucheleweshaji wa kufanyika marekebisho ya mshahara na pili imeondoa tofauti za mishahara kwa watumishi wenye ngazi moja (sifa sawa za kitaaluma, tarehe moja ya kuajiriwa) ambao walikuwa wakilipwa tofauti kwa sababu mmoja aliwahi kuandika barua ya kukiri na mwingine alichelewa kuandika barua kama hiyo hiyo, " amesema.

 IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU
ALHAMISI, JANUARI 5, 2017.

KINANA AZINDUA KAMPENI ZA CCM, DIMANI ZANZIBAR

$
0
0
  Katibu Mkuu wa CCM,Andulrahman Kinana akimnadi Mgombea wa Ubunge jimbo la Dimani Juma Ali Juma, katika uzinduzi wa kampeni za Uchaguzi mdogo wa Ubunge katika jimbo hilo, mjini Zanzibar, leo, Januari 5, 2017. (Picha na Bashir Nkoromo).
 Katibu Mkuu wa CCM akihutubia wananchi katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM za uchaguzi mdogo jimbo la Dimani, Zanzibar, uliofanyika leo. 
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenez, Humphrey Polepole, akisalimia wananchi alipotambulishwa naKatibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM za uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Dimani, Zanzibar, leo. 
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo, akisalimia wananchi alipotambulishwa naKatibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM za uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Dimani, Zanzibar, leo. (Picha na Bashir Nkoromo).
 Wananchi wakishangilia wakati wa mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM za uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Dimani, Zanzibar leo.

BENCHI LAMCHOSHA MANYIKA, KUANZA LEO KWENYE MECHI YAO NA URA

$
0
0
Peter Manyika.


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Baada ya kukalia benchi kwa kipindi kirefu bila kudaka hatimaye benchi la ufundi la timu ya Simba limeamua kumuamini na kumpatia nafasi golikipa kijana Peter Manyika aliyewika msimu wa 2014/2015 na timu hyo.

Hii inakuwa ni mechi yake ya kwanza toka kusajiliwa kwa golikipa Vicent Angban aliedaka nusu msimu 205/2016 aliyebwagiwa manyanga  na nafasi yake kuchukuliwa na mghana Daniel Aggey

1. Manyika Peter
2. Javier Bokungu
3. Mohammed Zimbwe
4. Abdi Hassan Banda
5. Method Mwanjale
6. Jonas G Mkude
7. Shiza R Kichuya
8. Muzamir Yasini
9. Laudit Mavugo
10. Juma Luzio
11. Pastory Athanas

Sub

1. Denis Richard
2. Vicent Costa
3. Novart Lufunga
4. Said H Ndemla
5. Hijja Ugando
6. Jamal Mnyate
7. Mosses Kitandu.

RIDHIWANI KIKWETE AMJULIA HALI PRO. MAJI MAREFU HOSPITALINI

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akimjulia hali Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Steven Hillary Ngonyani "Prof. Maji Marefu" ambaye amelazwa katika Hospitali ya Kairuki, Jijini Dar es salaam akisumbuliawa na Mguu wake kwa kipindi kirefu. 
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akizungumza jambo na Mama mzazi wa Prof. Maji Marefu ambaye ndie anaemuuguza hospitalini hapo.

KIKAO KAZI NGAZI YA MAKATIBU WAKUU CHAFANYIKA ZANZIBAR KUJADILI CHANGAMOTO ZA MUUNGANO

$
0
0
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais - Zanzibar Bw. Joseph Meza (wa kwanza kulia) akiongoza kikao kazi cha Makatibu Wakuu kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katikati ni Mwenyekiti Mwenza Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Muungano kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Dar es Salaam Bw. Baraka Rajab. Kikao kazi hicho kimefanyika leo tarehe 05/01/2017 katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar na kwa pamoja wamejadili changamoto za Muungano.
Baadhi ya Makatibu Wakuu kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakifuatilia kikao kazi kilichojadili changamoto za Muungano. Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Bw. Shomari Omar Shomari Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, Bi. Fatma Gharib Bilal Katibu Mkuu Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto na Bi. Khadija Bakari Juma Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya amali kwa pamoja wakifuatilia kikao kazi kilichojadili changamoto za Muungano na namna bora ya kuzipatia ufumbuzi.

Gambo apania kutokomeza vifo vya mama na Mtoto Mkoani Arusha

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akizungumza katika mkutano wa Wadau wa Afya uliofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya Meru,kushoto ni Mganga Mkuu wa mkoa,Dk frida Mokiti.

Nteghenjwa Hosseah, Arusha

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Dokta Frida Mokiti amesema kuwa uhaba wa vituo vya afya katika maeneo ya pembezoni mwa miji umekua ukichangia vifo vya mama wajawazito na watoto kutokana na kutembea umbali mrefu kutafuta huduma hiyo.

 Akizungumza katika Kikao kazi cha Mkoa kinachojadili hali ya afya ya mkoa, Dr. Mokiti amesema kuwa juhudi za makusudi zinahitajika kuhakikisha kuwa huduma za afya kwa mama na mtoto zinapatikana kwa urahisi ili kupunguza tatizo hilo ambalo limekua likirudisha nyuma afya ya wakina mama pamoja na kukatisha maisha yao.

 Akizungumza katika Kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kuhakikisha kuwa wanajenga Kituo cha Afya katika kila tarafa ili kusogeza karibu huduma za afya kwa wananchi pia amewataka viongozi kuweka mipaka katika maeneo ya zahanati ili kuepuka uvamizi wa maeneo hayo yanayowahudumia watu.

“Wakati sasa umefika wa kuhakikisha tunatokomeza kabisa changamoto hii ya vifo vya mama na mtoto, inasikitisha sana kuona mama anafariki wakati wa kujifungua kwa sababu tu amekosa huduma ya afya karibu na makazi yake,lazima tuwalinde na kuwajali wananwake, kwa sababu bila ya wao kujifungua hata sisi tusingekuwepo” Alisema Gambo.

Aliongeza kuwa Kila Halmashauri ihakikishe inatenga Fedha kwenye mapato yake ya ndani halkadhalika Ruzuku toka Serikali Kuu ielekezwe kwenye Miradi ya Afya na tuendelee kutafuta wadau watakaotusaidia katika utekelezaji wa miradi hii bila kusahau uhamasishaji wa nguvu za wananchi kwa Pamoja tutatokomeza tatizo hili.

 Kwa upande wake Mkazi wa Arusha   Hussein Igunge na Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe. Daniel Chongolo  wameitaka serikali iboreshe huduma za afya ikiwemo upatikanaji wa madawa kwa wale waliokata bima ili waweze kunufaika na bima zao pamoja na uhaba wa watumishi katika sekta ya afya.
Mganga Mkuu wa mkoa wa Arusha,Dk Frida Mokiti akizungumza katika mkutano wa Wadau wa Afya uliofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya Meru,kulia ni Mkuu wa mkoa,Mrisho Gambo akimsikiliza kwa makini,kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Karatu na Katibu Tawala mkoa wa Arusha,Richard Kwitega.
Baadhi ya Watalaam wa sekta ya afya wakiwa kwenye mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya Meru mkoa wa Arusha.
Baadhi ya viongozi wa dini walioshiriki mkutano huo wakisikiliza kwa makini pia waliahidi kushirikiana na mfuko wa Bima ya Afya(NHIF)kuhamasisha waumini wao kujiunga na mfuko wa CHF.
Wakuu wa wilaya za mkoa wa Arusha wakiwa kwenye mkutano huo uliojadili kwa kina mikakati ya kuinua sekta ya Afya kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Arusha,Gabriel Daqarro,Mkuu wa wilaya ya Monduli,Idd Kimanta na Mkuu wa wilaya ya Karatu,Theresia Mahongo.

ASHA BARAKA ANG’AKA SWALA LA CHOKI KUVUNJA MKATABA TWANGA PEPETA

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Mkurugenzi wa kampuni ya Aset Entertiment inayomiliki bendi ya Twanga Pepeta, Asha Baraka, amekuja juu mara baada ya kusikia mwanamuziki kinara wa bendi hiyo Ally Choki anataka kuondoka.

Asha Baraka ambaye amempigia simu ripota wa globu ya jamii mara baada ya kuandikwa  habari za choki kuhamia moja ya bendi zilizopo mkoani Songea na kuvunja mkataba na Twanga Pepeta.

“nasema hivi choki awezi kuondoka Twanga Pepeta kwakua alisaini mwenyewe mkataba wa miaka mitatu na mkataba huo unamalizika mwaka 2018 sasa huyo anayemtaka choki asubiri wakati ufike ndio aanze kumshawishi choki” amesema Asha Baraka.

Hata hivyo asha Baraka alipoulizwa juu ya mtu anayehitaji kuvunja mkataba anatakiwa kulipa kiasi gani cha fedha aligoma kuzungumzia swala la kuvunja mkataba na kusema yeye anachojua yupo na mwanamuziki kwa miaka mitatu.

Amesema mimi nipo na mwanamuziki kwa mkataba wa miaka mitatu sasa huyo anayetaka kuvunja mkataba wangu na choki mwambie siko tayari kuzungumzia swala la kuvunja mkataba kwa sasa mimi nipo kwa ajili ya kuimarisha bendi sio kubomoa bendi.

BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI JANUARI 5, 2017

MGOGORO WA WAFUGAJI NA MWEKEZAJI WA SHAMBA LA MKONGE MARUNGU MKOANI TANGA WAONGILIWA KATI NA DC

$
0
0
 Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa mkutano wa wananchi wa Kijiji cha Marungu ambao ni sehemu ya waathirka na mgogoro huo sambamba na muwekezaji wa shamba hilo na kusema kuwa makubaliano yaliyofikiwa baina ya serikali na wafugaji hao lazima yatekelezwe kwa wakati ili kuepusha vurugu za uvunjifu wa amani uliokuwa ukijitokeza mara kwa mara.
 Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga(DAS),Faidha Salim akizungumza katika mkutano huo
 Diwani wa Kata ya Marungu (CCM) Mohamed Mambea akizungumza wakati wa mkutano huo

BOFYA HAPA KUSOMA HABARI KAMILI

Obama awataka Democrat waikingie kifua sheria ya Obamacare

$
0
0
 Rais wa Marekani, Barack Obama amewahimiza wanachama wa chama cha Democratic kupigania sheria yake ya bima ya afya ambayo utawala wa Rais Mteule, Donald Trump umeahidi kuubatilisha baada ya kuingia madarakani.

Akizungumza katika mkutano wa faragha wa saa mbili, Obama aliwahimiza wabunge wa chama hicho kuitetea sheria hiyo, huku wanachama wa Republican nao wakichukua hatua ya kufuta sheria hiyo.

Makamu wa rais mteule wa nchi hiyo, Mike Pence pia alikuwa katika bunge la Congress, ambapo alisema chama chake kitafuta sheria hiyo ambayo hufahamika sana kama Obamacare. Sheria hiyo iliwezesha takriban Wamarekani milioni 20 na zaidi kupokea huduma ya afya.

Hata hivyo, sheria hiyo imekabiliwa na changamoto za kupanda kwa malipo ya wanaopokea huduma ya bima na pia kampuni nyingi za bima zimejitoa kutokana na mpango huo. Hilo limewaacha Wamarekani wakiwa hawana njia nyingine mbadala za kujipatia bima ya afya.

Baada ya Rais Obama kufanya ziara hiyo ya nadra sana makao makuu ya bunge la Marekani Capitol Hill siku ya Jumatano, mbunge wa chama cha Democratic, Elijah Cummings aliwaambia wanahabari kwamba Obama aliwahimiza kupigana kulinda sera hiyo kuu iliyotimizwa na utawala wake.
Baadhi ya waliokuwepo waliwaambia wanahabari Marekani kwamba rais huyo anayeondoka pia aliwahimiza "kuwa na nguvu" huku Republican wakijiandaa kuchukua udhibiti wa ikulu ya White House na mabunge yote mawili ya Congress - Bunge la Wawakilishi na Bunge la Seneti - kwa mara ya kwanza katika mwongo mmoja.

Alisema hayo huku bunge la Seneti likichukua hatua ya kwanza ya kufuta sheria hiyo ya Obamacare.
Walipiga kura 51 dhidi ya 48 kujadili azimio la bajeti ambalo lengo lake ni kunyima ufadhili kwa mpango huo wa Obama.BBCSwahili

MAGAZETI YA LEO JANUARI 6, 2017

introducing Panga by Wakazi

2017 New Year Message from Tausi Suedi, CSI CEO

$
0
0
Picture

Health. Peace. Love - wishes for my family, friends and humanity; with health being number one. Whenever I speak with my mother-in-law and share with her the different projects I am doing, she always reminds me, "as long as you have good health, everything else is possible" and I agree. Health is the ultimate wealth through which great achievements and discoveries stem from for individuals, societies and nations. While good health is desired by everyone, globally millions are marginalized particularly women, children and youth especially in developing countries limiting their timely access to quality health services and information. 
For more CLICK HERE

SERIKALI KUENDESHA MPANGO WA KUTATHMINI NA KURASIMISHA UJUZI ULIOPATIKANA NJE YA MFUMO RASMI WA MAFUNZO.


WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII,PROFESA JUMANNE MAGHEMBE AZINDUA BODI MPYA YA TANAPA.

$
0
0
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA),Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali George Waitara (kushoto) akizungumza jambo na Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof ,Jumanne Maghembe mara baada ya kuzinduliwa kwa Bodi hiyo. Katikati yao ni Mkurugenzi wa TANAPA Bw. Allan Kijazi.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa  Jumanne Maghembe akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) muda mfupi baada ya bodi hiyo kuzinduliwa.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa  Jumanne Maghembe pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa idara mbalimbali katika shirika hilo.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakiwa katika picha ya pamoja na mameneja katika shirika hilo. 
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kasazini.

Mahubiri ya Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola

$
0
0
Usikose kufuatilia maombezi na ibada ya neno la Mungu kutoka kwa Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Jijini Mwanza, mubashara (live) kupitia ukurasa wake wa facebook.
Ni kila siku ya Alhamisi kuanzia saa nane kamili mchana kupitia ukurasa wake wa facebook wa DANIEL KULOLA ambapo mahubiri na maombezi yatarushwa moja kwa moja (mubashara) kwa njia ya video.

WEEKLY MEM BULLETIN ISSUE NO.153

UZINDUZI WA KIWANDA CHA AZAM DAIRY PRODUCTS LIMITED FUMBA

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) na Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Group Bw.Said Salim Bakhresa wakikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Mradi wa kiwanda cha uzalishaji wa Maziwa (Azam Dairy Products Ltd.) huko Fumba wilaya ya Magharibi "A" Unguja, ikiwa ni katika shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kushoto)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifungua pazia kuashiria Uzinduzi wa Mradi wa kiwanda cha uzalishaji wa Maziwa (Azam Dairy Products Ltd.) huko Fumba wilaya ya Magharibi "A" Unguja, ikiwa ni katika shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kushoto) Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Group Bw.Said Salim Bakhresa
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Meneja Uzalishaji katika Kiwanda cha Maziwa cha AZAM DAIRY PRODUCTS LTD ADILSON FAGUNDES (kushoto) wakati alipotembelea Kiwanda hicho huko Fumba Kororo Wilaya ya Magharibi "A" Unguja kuona harakati za uzalishaji baada ya kukizindua leo,ikiwa ni katika shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Meneja Uzalishaji katika Kiwanda cha Maziwa cha AZAM DAIRY PRODUCTS LTD ADILSON FAGUNDES (kushoto) wakati alipotembelea Kiwanda hicho huko Fumba Kororo Wilaya ya Magharibi "A" Unguja kuona harakati za uzalishaji baada ya kukizindua leo,ikiwa ni katika shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

MIAKA 53 YA MAPINDUZI: MAPINDUZI YAMEONDOA MATESO KWA WAAFRIKA WA BARA NA VISIWANI - DKT. MOHAMMED SEIF KHATIBU

$
0
0
Na Judith Mhina - MAELEZO

Waziri katika Serikali ya Awamu ya Kwanza, Pili na ya Tatu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mtaalamu wa lugha ya Kiswahili, Dkt Mohammed Seif Khatibu (pichani) amesema Mapinduzi ya Zanzubar ya mwaka 1964 yalimaliza mateso ya muda mrefu waliyoyapata Waafrika wa Tanzania Bara na Visiwani.


Dkt.  Mohammed Seif Khatibu amesema hayo alipohojiwa na Idara ya Habari - MAELEZO leo kuhusiana na mafanikio yaliyopatikana tangu mapinduzi ya Zanzibar yalipofanyika miaka 53 iliyopita. 
Amesema, Mapinduzi yameondoa madhila ya utumwa, masuria, kubaguliwa, kufanyishwa kazi, kudhalilishwa, kunyanyaswa, kudharauliwa na kuuzwa kama samaki:


“Inashangaza kuona Watanzania hawasheherekei ipasavyo Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwa kama si Mapinduzi hayo mateso na madhila kwa Waafrika wa Bara na Visiwani yangeendelea”. “Madhila ya Zanzibar hayawagusi Waafrika wa Zanzibar peke yake, bali pia Waafrika wa Tanzania Bara”. Kusoma zaidi BOFYA HAPA
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images