Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1490 | 1491 | (Page 1492) | 1493 | 1494 | .... | 3353 | newer

  0 0
  0 0

  NA HASSAN SILAYO-MAELEZO 
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bi.Sihaba Nkinga amekemea vitendo vya Ukeketaji kwa watoto nchini na kuahidi kuwachukulia hatua kali za kisheria wale watakaobainika. 
   Akiongea wakati wa Mahafali ya watoto 46 waliokimbia kukeketwa na kujiunga na Kituo cha kulea watoto hao cha ATFGM Kilichopo Masanga Tarime Vijijini Bi.Sihaba alisema kuwa suala la ukeketaji ni kinyume na sheria za nchi na haki za binadamu na ni suala lenye madhara kwa maisha ya watoto. 
   “Hatukubaliani na suala hili kwani linarudisha maendeleo ya nchi yetu,suala hili pia linachangia kurudisha fikra za vijana wetu na kubatilisha ndoto za vijana wetu, tunao muda wa kujirekebisha na kama tulikuwa tunaendelea basi turudi nyuma”Alisema Bi. Sihaba. 
  Katibu Mkuu huyo amesema kuwa jamii inayo wajibu wa kulinda na kuendeleza mila zenye kuleta maendeleo na kuacha kulinda na kukumbatia mila zinathoathiri maisha ya binadamu kwani sio suala sahihi kwani mila nyingine zinagharimu maisha ya vijana wetu.

   Mkurugenzi wa Kituo cha Kulea Watoto waliokimbia Kukeketwa cha ATFGM-Massanga Sister Stella Mgaya akimuonesha Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga kifaa cha asili cha muziki kilichotengenezwa na mangariba wastaafu.
   Mkurugenzi wa Kituo cha Kulea Watoto waliokimbia Kukeketwa cha ATFGM-Massanga Sister Stella Mgaya akiongea wakati wa  mahafali ya wasichana 46 waliokimbia ukeketaji na kushukuru juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na uongozi wa wilaya ya Tarime kukabiliana na tatizo hilo, ambapo ameomba wadau kujitokeza kuwaendeleza watoto wanaohitimu kituoni hapo.
   Mkuu wa Wilaya ya Bunda Bi.Lydia Bupilipili akiongea wakati wa mahafali ya wasichana 46 waliokimbia ukeketaji na kuwasisitiza wazazi na walezi kubadilika na kuachana na imani potofu ya ukeketaji ili kuwawezesha wasichana kutimiza malengo yao.
   Mkuu wa Wilaya ya Tarime Mhe. Glorious Luoga akiongea wakati wa mahafali ya watoto waliokimbia kukeketwa na kujiunga katika kituo Watoto waliokimbia Kukeketwa cha ATFGM-Massanga ambapo aliwataka wazazi wanaowatenga na kulazimisha kukeketa watoto wa kike waliohitumu mafunzo kuacha tabia hiyo kwani watachukuliwa hatua kali za kisheria.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga akiongea wakati wa mahafali ya watoto waliokimbia kukeketwa na kujiunga katika kituo Watoto waliokimbia Kukeketwa cha ATFGM-Massanga, ambapo alisisitiza kuwa serikali itaendelea kuwachukulia hatua kali wazazi na jamii inayoendelea na kitendo kiovu cha ukeketaji kwa watoto wa kike. 

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama ngombe wa kisasa wakati alipotembelea  shamba la ng'ombe wa maziwa  la MILKCOM  TANZANIA LIMITED  lililopo Kigamboni  jijini Dar es salaam akiwa katika ziara ya wilaya ya Kigamboni  leo Januari 4, 2017. 
   Waziri Mkuu  Kassim Majaliwa akieleza jambo wakati alipotembelea  shamba la ng'ombe wa maziwa  la MILKCOM  TANZANIA LIMITED  lililopo Kigamboni  jijini Dar es salaam akiwa katika ziara ya wilaya ya Kigamboni  leo Januari 4, 2017. 
   Wananchi wa eneo la Kisarawe Two wilayani Kigamboni wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao baada ya kukagua wodi ya wazazi iliyojengwa na kampuni ya mafuta ya OILCOM kijijini hapo. Waziri Mkuu alikuwa katika ziara ya wilaya hiyo Januari 4, 2017.
  Waziri Mkuu  Mhe. Kassim Majaliwa akitazama kitanda wakati alipotembelea wodi ya wazazi iliyojengwa na kampuni ya mafuta ya OILCOM katika  ENEO la  Kisarawe Two wilayani Kigamboni, Januari 4, 2017. Kushoto kwake ni Mkuu wa wilaya ya Kigamboni, Mhe. Hashim Mgandilwa.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

  0 0

   Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama-IJA-Lushoto, Mhe. Jaji Dkt. Paul Kihwelo akifungua rasmi Mafunzo ya Utunzaji wa Kumbukumbu kwa njia za kisasa “Training on Modern Record Keeping and Document Management” yanayoshirikisha Wasaidizi wa Kumbukumbu na Maafisa TEHAMA wa Mahakama ya Tanzania. Kulia ni Mkurugenzi wa Utawala, Bw. Edward Nkembo.
   Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu- Mahakama ya Tanzania, Bw. Edward akieleza jambo kwa washiriki wa Mafunzo.
   Baadhi ya washiriki wa Mafunzo
   Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama, Mhe. Jaji. Dkt. Paul Kihwelo, (wa pili kulia), Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu-Mahakama ya Tanzania, Bw. Edward Nkembo (wa pili kushoto), Mkurugenzi-Msaidizi-Mafunzo, Mahakama ya Tanzania, Bi. Patricia Ngungulu, wa kwanza kushoto na Mratibu wa Mafunzo ya Mahakama toka  Chuo cha Uongozi wa Mahakama-IJA, Bw. Lameck Samson (wa kwanza kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa TEHAMA na Wasaidizi wa Kumbukumbu wanaoshiriki katika mafunzo hayo.
  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na  Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa  Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Deusdedit Mpazi wakati alipotembelea  maghala ya NFRA, Chang'ombe jijini Dar es salaam Januari 4, 2017.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mhahindi wakati alipotembelea magahala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) , Chang'ombe jijini Dar es salaam Januari  4, 2017.  Kulia kwake ni  Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa  Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Deusdedit Mpazi. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mhahindi wakati alipotembelea magahala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) , Chang'ombe jijini Dar es salaam Januari  4, 2017.  Kulia kwake ni  Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa  Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Deusdedit Mpazi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Arusha  Mhe. Mrisho Gambo akifungua kikao cha Wadau wa Elimu Mkoa wa Arusha

   Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akishirikiana na wataalamu kuweka mitambo sawa kwa ajili ya wadau wa Elimu kuwasilisha taarifa.

   Viongozi wa Halmashauri ya Ngorongoro wakifuatilia Kikao cha Wadau wa Elimu

   Wadau wa Elimu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

       Kaimu Afisa Elimu Mkoa Ndg. Emmanuel Mahondo akiwasilisha taarifa ya Elimu Mkoa wakati wa Kikao cha wadau wa Elimu kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.


  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  MWANAMUZIKI nguli wa muziki wa bongofleva nchini, Judith Wambura "Lady Jaydee" (Binti Komando) amesema kuwa wanamuziki wa kike wanatakiwa kuongeza nguvu na kutokata tamaa katika kazi zao.

  Jaydee ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na ripota wa globu ya jamii juu ya nini wasanii wakike wanatakiwa kufanya ili kufikia mafanikio ambayo yeye ameyafikia katika muziki huu ndani na nje ya nchi.

  “Muziki wa sasa unazidi kukua na wasanii wa kike wanajitahidi  ila wanatakiwa kuongeza juhudi zaidi ya hapo, hivyo sisi tulio tangulia tunatakiwa kuwatia moyo pia wasikate tamaa kwani vipaji wanavyo na wameonyesha na jamii imewakubali”Amesema  Jaydee.

  Amesema kuwa kuna kipaji na kufahamika ni jambo jingine na kutunza kipaji chako kutokana na misukosuko ni jambo jipya ambalo linaweza kukukatisha tama katika muziki wa leo.

  Amesisitiza kuwa katika kipindi hiki kumekuwa na wanamuziki wengi wa kike tofauti na miaka yetu ambayo tulikuwa tukiesabika lakini wingi huo bado hauwezi kulinganishwa na wingi wa wanamuziki wa kiume jambo ambalo linawapa ushindani mkubwa wanamuziki wa kike.

  Ametaja kuwa licha ya kupata nafsi lakini bado wanamuziki hao wanapitia changamoto kubwa sana ya kujikwamua kiuchumi kutokana na muziki.

  UNAWEZA ANGALIA HAPA CHINI VIDEO YAKE MPYA

  0 0

  Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Longido umetembelea kituo cha Watoto yatima na Wanaoishi katika mazingira magumu cha Masai Foundation kilichopo mji mdogo wa Namanga na kutoa msaada wa vyakula pamoja na vifaa mbalimbali.  Mjumbe Baraza Kuu  UVCCM Mkoa wa Arusha Robert Kaseko Amesema kuwa wameamua kushirikiana na jamii katika kusaidia watoto ikiwa ni moja kati ya michango wanayoitoa ili kutosheleza mahitaji muhimu yanayohitajika katika kituo hicho.  Robert Amesema kuwa jukumu la kuwasaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu ni la kila mwanajamii hivyo jamii inapaswa kujitoa kusaidia watoto hao.  Katibu Hamasa wa CCM mkoa wa Arusha Neema Emmanuel amesema kuwa vijana hao wameamua kujitoa kutoa msaada kwa jamii ili kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu hivyo ameiomba jamii kujitokeza kwa wingi kuwasaidia watoto hao.  “Hawa ni watoto wetu sote kila mtu anapaswa kuona kuwa ana jukumu la kuwasaidia hawa watoto ili waweze kufanikisha ndoto zao”  Neema  Katibu  wa UVCCM wilaya ya Londigo Isaya Karakara na Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya Tulli Lemanga aliyejitolea kuwakatia bima ya afya watoto wanaolelewa katika kituo hicho wamesema  kuwa vijana hao wataendelea na utamaduni huo mara kwa mara katika kuunga mkono juhudi za serikali katika kutatua changamoto za watoto.  Mmiliki wa kituo hicho Joyce Kabati amewashukuru vijana hao kwa kutembelea watoto hao jambo ambalo linaleta faraja kwa watoto hao ambao na wanamahitaji mbalimbali ambayo yamewasilishwa na vijana hao.
   Kushoto ni Katibu  wa UVCCM wilaya ya Longido Isaya Karakara, Katibu Hamasa wa UVCCM mkoa wa Arusha Neema Emmanuel  na Mjumbe Baraza Kuu  UVCCM Mkoa wa Arusha Robert Kaseko w akikabidhi msaada kwa Mmiliki wa kituo cha kulelea Watoto yatima cha Masai Foundation  Joyce Kabati

   Kushoto ni Katibu  wa UVCCM wilaya ya Longido Isaya Karakara, Katibu Hamasa wa UVCCM mkoa wa Arusha Neema Emmanuel  na Mjumbe Baraza Kuu  UVCCM Mkoa wa Arusha Robert Kaseko w akikabidhi msaada kwa Mmiliki wa kituo cha kulelea Watoto yatima cha Masai Foundation  Joyce Kabati.Habari picha na Woinde Shizza,Arusha.  0 0

  Msemaji wa Polisi, Advera Bulimba – ACP

  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu ametuma timu ya Maofisa  wa Polisi ikiongozwa na Kamishna wa Polisi Jamii Mussa Alli Mussa kwenda Zanzibar kushughulikia kero na malalamiko ya wananchi juu ya vitendo vya udhalilishaji na ukatili kwa watoto/wanawake ambavyo vimekuwa vikiripotiwa mara kwa mara.


  Timu hiyo imepewa jukumu la kuchunguza vitendo hivyo vya udhalilishaji na kiini chake na hatimaye kuja na mpango mkakati wa kuzuia vitendo hivyo ikiwemo kuwakamata  wahusika na kuwafikisha mahakamani.


  IGP Mangu amewataka wananchi wa Zanzibar, Taasisi za kiserikali na Taasisi za kiraia zilizopo Zanzibar kutoa ushirikiano kwa timu hiyo ili kukomesha vitendo hivyo ambavyo ni kinyume na maadili ya Watanzania.


  Imetolewa na:

  Advera John Bulimba - ACP

  Msemaji wa Jeshi la Polisi.


  Makao Makuu ya Polisi. 

  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Tanga(CUF)Mussa Mbaruku akimuelekeza namna ya kuitumia Baiskeli ya kutembelea mkazi wa Mtaa wa Tongoni Jijini Tanga,Mwinchumu Ally jana mara baada ya kumkabidhi ikiwa ni ahadi aliyemuahidi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka juzi .
  Mbunge wa Jimbo la Tanga(CUF) Mussa Mbaruku kulia akimkabidhi baikeli mkazi wa Mtaa wa Tongoni Jijini Tanga,Mwinchumu Ally jana ambaye anamatatizo ya ulemavu wa miguu kwa ajili ya kutembelea ikiwa ni kutimiza ahada aliyomuahaidi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka
  juzi,Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

  0 0

  1
  Nasieku Kisambu Mkurugenzi wa Mipango Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA) akizungumza katika mafunzo ya Haki za Wanawake na Jinsi ya kufanya utetezi katika ngazi ya Kitaifa, Kikanda na Kimataifa yakiwa na lengo la kuongeza uelewa wa misingi ya kulinda na kutetea haki za wanawake na watoto Kitaifa , Kikanda na Kimataifa.

  Kuelewa mifano iliyopo katika Kanda, Kikanda na kimataifa inayolinda haki za wanawake , Haya ni mafunzo yanayolenga kujenga uwezo wa Taasisi zinazotetea haki za wanawake kutumia fursa zilizopo katika mikataba, Taasisi na mifumo ili kuweza kubadilisha sera na sheria kandamizi na kutetea haki za wanawake. 

  Mafunzo hayo yanayofanyika kwenye hoteli ya Courtyard Upanga jijini Dar es salaam yameandaliwa na Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) na kwa ushirikiano na mashirika mengine yanayotetea haki za wanawake na watoto ambapo wadau mbalimbali kutoka katika taasisi hizo wameshiriki katika mafunzo hayo
  2
  Maria Matui Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake Wanasheria Tanzania (TAWLA) akifungua mafunzo hayo ya siku mbili yanayofanyika kwenye hoteli ya Courtyard Upanga jijini Dar es salaam.
  3
  Mkufunzi wa Mafunzo hayo Dk. Clemence Mashamba akitoa mada wakati wa mafunzo hayo yanayoendelea kwenye hoteli ya Courtyard Upanga jijini Dar es salaam.
  8
  Washiriki wa Mafunzo hayo wakiwa katika picha ya pamoja.


  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala (mwenye miwani) akizungumza na mwananchi wa kata Mabale aliyefika kuchota maji katika bwawa la maji la Akashwa lililo kata Mabale. Bwawa hilo limekauka kwa kiasi kikubwa kutokana na kukosekana mvua kwa muda mrefu. Balozi Kamala ametembelea pia mabwaya ya Nyankere na Lwoga ambayo yako hatarini kukauka kama mvua hazitanyesha ndani ya kipindi kifupi kijacho.
  Mkazi wa Kata Kilimilile akichota maji baada ya mradi wa kata Kilimilile kuanza kutoa maji. Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala ameshuhudia kuanza kazi kwa mradi huo na amewaomba wananchi kutunza mradi huo. Balozi Kamala anaendelea na ziara ya kukagua miradi ya maji Wilayani Missenyi.

  0 0

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na mkuu wa mkoa wa ruvuma Mhandisi Binilis Mahenge mara alipowasili katika uwanja wa ndege wa Ruvuma kwa ziara ya kikazi kulia ni mke wa mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mama Mahenge
  Waziri mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Kaimu Jaji Mfawidhi wa Songea Mh Salima Chikoyo ambaye alikuwepo katika uwanja wa ndege wa Ruvuma katika mapokezi ya waziri mkuu Kushoto ni Naibu waziri wa maliasili na utali Mhandisi Ramo Makani na kushoto ni katibu tawala wa mkoa wa Ruvuma Hassani Bndeheko Waziri mkuu amewasili mkoani Ruvuma kwa ziara ya kikazi. Picha na Chris Mfinanga

  0 0

   Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

  WATU watatu wamenusurika kufa Mkoani Kigoma katika tukio la Unyang'anyi wa kutumia silaha lililotokea katika eneo la Zuru Manispaa ya kigoma ujijj ambapo Majambazi sita wasio julikana wakiwa na silaha aina ya SMG/SAR 01 walivamia Duka la Mpesa la Mfanya biashara ,Hussen Issa  na Kuiba Kiasi cha shilingi 250,000 pamoja na simu tatu .

  Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa Wa Kigoma, alisema mnamo tarehe 3 Januari mwaka huu majira ya saa 20:30 usiku Huko zuru Gungu  Watu sita wasio faamika waliingia dukani kwa mfanya biashara huyo kama wateja huku wakiwa wameficha siraha zao kwenye makoti baada ya Wizi huo kufanyika waliwapiga Risasi watu wa tatu katika vurugu za kufanya Wizi huo.

  Mtui aliwataja walio jeruhiwa na Risasi hizo ni Hamad Kharid (36) alipigwa ubavuni ,Hussen Ndoroma (42) amejeruhiwa maeneo ya makalio na Sifa  Salimu (65)  amejeruhiwa na risasi miguuni ambapo risasi hiyo ilimkuta Nyumbani kwake ambapo ni jirani na wafanya biashara hao.

  Aidha Mtui alisema Mpaka sasa majeruhi wanaendelea na matibabu katika hospital ya Mkoa Maweni na Jeshi la polisi linawashikilia watu wawili kwa mahojiano zaidi juu ya tukio hilo na msako mkari unaendelea kuwasaka majambazi hao wanaofanya matukio hayo ya Unyang'anyi kwa kutumia siraha.

  "Niwaombe Wananchi  kuendelea kutoa taarifa kwa Jeshi la polisi dhidi ya  uhalifu ilikuunga mkono jitihada za kuondoa uhalifu kwa kutoa taarifa za waalifu wanao jihusisha na vitendo vya kiuhalifu ilihatua za kisheria ziwe zinachukuliwa dhidi yao", alisema Mtui.

  Kwa Upande wake Majeruhi wa tukio hilo, Hussen Ndoroma alisema jana majira ya saa moja usiku kuna watu ambao walifika dukani kwake wakiwa waneshika panga na wengine siraha ya SMG baada ya kubishana nao ndipo walipo amua kumpiga Risasi ya Mguuni iliyotokea  kwenye makalio ndipo ilipoenda kumpiga  Mwanamke mmoja aliekuwa Nyumba kwake.

  Alisema majambazi hao walifanikiwa kuchukua kisasi cha shilingi 250,000  pamoja na simu tatu na kuingia duka la Mwenzake  Ahmadi Kharid aliekuwa akiomba msaada mwenzake asaidiwe ndipo walipo mpiga risasi eneo la ubavu wa Kushoto.

  Hata hivyo Sifa Salim ambae pia nae ni miongoni mwa majeruhi hao alisema Yeye akiwa Nyumbani kwake maeneo ya zuru akiendelea na Shughuli zake za nyumbani alishtukia kitu kinakuja na kumpiga maeneo ya miguuni na kushtukia damu zikiendelea kitoka hakujua tatizo ninini.

  Nae Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Kigoma Maweni Fadhiri Kibaya  alikili kupokea majeruhi hao wakiwa katika hali mbaya na majeraha yao yaki vuja damu kwa Wingi ndipo walipo wachukua na kuanza kuwafanyia matibabu , mpaka sasa hili zao ni nzuri na wagonjwa wanaendelea na mayibabu.

  0 0


  Kampuni na Taasisi mbalimbali hapa nchini zimeaswa  kuiga mfano wa Kampuni ya simu za mkononi ya  Airtel Tanzania kwa kuwawezesha vijana mbalimbali  kujiajiri wenyewe kupitia   mradi wa Airtel Fursa, ili kupunguza tatizo la Ajira hapa nchini.
  Hayo yamebainishwa na mmoja kati ya waliofaidika na mradi wa Airtel Fursa kijana mjasiriamali anayejihusisha na  fani ya ufundi seremala  Fikiri Chinji aishie katika kijiji cha Ng'ong'ona manispaa ya Dodoma wakati alipotembelewa na Airtel ili kutadhimini maendeleo yake.
  Fikiri alisema wapo vijana wengi ambao wapo mtaani wakitafuta ajira na wengine wakikumbwa na changamoto za mitaji ili kuendesha biashara zao, program kama hii ya Airtel Fursa ni vyema ikafanywa na makampuni mengi ili kuinua uchumi wa vijana  jamii nan chi kwa ujumla
  Mpaka sasa nawashukuru sana Airtel kwa kuniwezesha mtaji ambao umeweza kuinua biashara yangu, kupitia program hii nimeweza kutanua biashara yangu ya ufundi selemala na kuanzisha biashara ya welding. Sambamba na kutanua biashara pia nimeweza kuajiri vijana  saba na kuongeza vifaa vingine zaidi, nawashukuru Airtel kwa kunishika mkono.”
   Akizungumza katika eneo hilo Afisa Airtel kanda ya kati, Hendrick  Werner amesema kijana Fikiri Chinji ameweza kupiga hatua kwa kuongeza vifaa vingine toka alipowezeshwa na Airtel Fursa, kukuza biashara pamoja na kutengeneza ajira kwa vijana wengine na  kuwataka vijana wengine kuiga mfano wa fikiri kwa  kuanzisha vikundi mbalimbali na kuwatafuta wadau  watakao wawezesha kupita program mbalimbali ikiwemo hii ya Airtel Fursa.
  Airtel Fursa ni mradi wa kijamii wenye dhumuni la kuhamasisha vijana, kuwapa nafasi ya kujiendeleza kibiashara na ujuzi utakoawawezesha kuimarisha biashara zao. Pambana group ni kikundi kingine kilichonufaika na mradi wa Airtel Fursa Dodoma ambacho kina vijana zaidi ya 15.
   Meneja mauzo Airtel mkoa wa Dodoma, Hendrick Bruno (kushoto) akiongea na Fikiri Chinji (kulia) anayejishughulisha na ufundi seremala  juu ya maendeleo na changamoto za biashara baada ya kuwezeshwa na Airtel kupitia mpango wake wa Airtel FURSA “Tunakuwezesha”, wakati Airtel ilipotembelea kwenye karakana yake katika Mtaa wa Ng’ong’ona manispaa ya Dodoma ili kujionea maendeleo yake pamoja kupanga jinsi ya kuboresha zaidi biashara yake.
  Meneja mauzo Airtel mkoa wa Dodoma, Hendrick Bruno (kulia) akishuhudia matumizi ya moja ya vifaa alivyowezeshwa kijana Fikiri Chinji anayejishughulisha na ufundi seremala kwa kupitia mpango wa Airtel


  FURSA “Tunakuwezesha” miezi tisa iliyopita, wakati Airtel ilipotembelea kwenye karakana yake katika Mtaa wa Ng’ong’ona manispaa ya Dodoma ili kujionea maendeleo yake pamoja kupanga jinsi ya kuboresha zaidi biashara yake.

  0 0

  Na Stella Kalinga, Simiyu.

  Serikali Mkoani Simiyu  imewashauri wakulima wote wilayani Busega  wenye mashamba yaliyo karibu na ziwa Victoria kuorodhesha jumla ya ekari za mashamba waliyonayo ili waweze kusajiliwa na kuingizwa katika mpango wa  kilimo cha umwagiliaji kinachotarajiwa kuanza mapema mwaka huu.


  Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka katika ziara yake maalum ya kuwatembelea wananchi wa vijiji vilivyopo  kandokando ya ziwa Victoria Wilayani Busega, ambapo ameanza na vijiji vya Nyamikoma na Nyakaboja  kata ya Kabita.


  Mtaka alisema endapo wakulima watakuwa tayari kufanya  kilimo cha umwagiliaji  kwa kufuata ushauri wa kitaalamu na kutumia mbegu bora watapata mazao mengi yatakayokubalika katika soko la ndani na nje ya Mkoa ikiwa sambamba na  na kujikwamua kiuchumi.


  Alieleza kuwa  lengo la serikali  ya Mkoa ni kuhakikisha dhana ya mapinduzi ya kilimo kwa mfumo wa umwagiliaji inatekelezwa kwa vitendo kwa kuwapatia elimu ya kitaalamu wakulima ili waweze kuzalisha mazao bora na mengi yanayotosheleza soko la ndani ya nchi na kupunguza uagiziaji mazao nje ya Mkoa.


   “Tumekuja kama mkoa kuzungumza na wananchi ili wale watakaokuwa tayari waanze kutekeleza. Ni lazima tufanye maamuzi ya kufanya mapinduzi ya kilimo kama watu tulio kandokando ya ziwa Victoria ili uwepo ziwa utunufaishe” amesema Mtaka.


  Aidha alifafanua kuwa kilimo hicho katika maeneo ya  Wilaya ya Busega  kitahusisha mazao ya Mpunga,  mboga mboga, mahindi na mazao jamii ya mikunde, hivyo wakulima kwa kushirikiana na Serikali wanatakiwa kuendelea kubuni mbinu  mbalimbali za uzalilishaji mazao hayo kwa wingi ili kwenda sambamba na fursa ya masoko ya ndani na nje ya nchi hasa kwa mazao ya mikunde.
    Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nyakaboja wilayani Busega katika Mkutano wa hadhara kwa lengo la kuwahamasisha kuanza kutekeleza mpango wa kilimo cha umwagiiaji wilayani humo.
   Mkuu wa Wilaya ya Busega Tano Mwera akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Nyakaboja wilayani humo katika Mkutano wa hadhara kwa lengo la kuwahamasisha wananchi kuanza kutekeleza mpango wa kilimo cha umwagiiaji wilayani humo.
  Afisa Ardhi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Simiyu, Bibi.Grace Mgombera akitoa  ufafanuzi wa juu masuala ya ardhi yaliyowasilishwa na wananchi wa Kijiji cha Nyamikoma B wilayani Busega  kama kero kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka katika mkutano wa hadhara uliofanyik kjijini hapo.
   Diwani wa Kata ya Kabita wilayani Busega akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Nyakaboja wilayani humo katika Mkutano wa hadhara kwa lengo la kuwahamasisha wananchi kuanza kutekeleza mpango wa kilimo cha umwagiiaji wilayani humo.
  Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Nyamikoma B Kata ya Kabita, wilayani Busega wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka katika Mkutano wa hadhara kuwahamasisha kuingia na kuanza kutekeleza mpango wa kilimo cha umwagiiaji wilayani humo.
   Baadhi ya Maafisa wa Sekretarieti ya Mkoa walioambatana na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka katika ziara yake ya kuwahamasisha wananchi wa Busega kutekeleza mpango wa kilimo cha umwagiliaji.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

   Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhan akitoa ufafanuzi kuhusu uwekaji wa kituturi cha kupigia kura wakati wa mafunzo ya Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo na Kata watakaosimamia uchaguzi mdogo wa Madiwani utakaofanyika katika kata 20 za Tanzania Bara na Ubunge katika jimbo la Dimani  Januari 22, 2017 leo mjini Dodoma.
  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhan akionyesha mfano wa namna ya kuweka vituturi vya kupigia kura vituoni ili kuwawezesha wananchi kupiga kura kwa wakati wa mafunzo ya Wasimamizi wa Uchaguzi mdogo wa Madiwani utakaofanyika katika kata 20 za Tanzania Bara na Ubunge katika jimbo la Dimani  Januari 22, 2017.
   Kaimu Naibu –Uendeshaji wa Uchaguzi, Bi. Irene Kadushi Tutah  akiwasilisha mada kuhusu Kujumlisha na Kutangaza Matokeo ya Ubunge na Madiwani wakati wa mafunzo ya Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo na Kata watakaosimamia uchaguzi mdogo utakaofanyika Januari 22, 2017.
   Washiriki wa mafunzo ya Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo na Kata kutoka Kanda ya Kaskazini na Pwani wakiendelea na mafunzo ya kuwajengea uwezo wasimamizi hao wakati uchaguzi mdogo wa Madiwani utakaofanyika katika kata 20 za Tanzania Bara na Ubunge katika jimbo la Dimani  Januari 22, 2017.
    Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo wakiwemo Wakurugenzi wa Halmashauri wakifuatilia kwa makini mafunzo ya Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo na Kata watakaosimamia uchaguzi mdogo Januari 22, 2017 mjini Dodoma. Picha na Aron Msigwa - NEC 

  0 0

  Na Angella Msangi,Dar Es Salaam

  WAKAZI wa jiji la DAR ES SALAAM wamepongeza huduma mbali mbali za matibabu zinazotolewa kwenye Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo kwenye hospitali ya TAIFA ya MUHIMBILI,ambapo wamesema kuwa kwa sasa matibabu ya moyo yamepata ufumbuzi tofauti na miaka mingine ilivyokuwa hapa nchini.

  Wakizungumza hospitalini hapo, baadhi ya wananchi hao waliokuwa katika nyuso za furaha mara  baada ya kupata huduma nzuri, wameeleza kuwa hospitali hiyo inafaa kuwa mfano wa kuigwa kutokana na namna ya huduma zinavtolewa kuanzia madaktari mpaka wauguzi na watoa huduma wa kawaida.

  REUBEN MTAITA (79) mkazi wa KONGOWE nje kidogo ya jiji la DAR ES SALAAM amesema tangu ameanza kutibiwa katika hospitali hiyo ameweza kupata nafuu kwa matatizo ya moyo yanayomsumbua, huku akibainisha kuwa huduma ziko katika viwango na hujutii kupata matibabu katika hospitali hiyo.

  “Ni kweli na wazi hospitali hii inatoa huduma bora kabisa , hata namna madaktari wanavyokuhudumia inatia moyo, na kwamba wako karibu na wagonjwa kuhakikisha unapata matibabu sahihi”alisema MTAITA

  Kwa upande wake mkazi wa TEMEKE KHADIJA OMARY(30) amesema anafuraha huduma za hospitali hiyo na kwamba tangu aanze kutibiwa ameona unafuu mkubwa na kwamba hali yake inazidi kuimirika.

  “Huduma zipo kwenye ubora na wagonjwa tuna hudumiwa bila ubaguzi hili jambo limenifurahisha kabisa”alisema KHADIJA.

  Baadhi ya madaktari, BASHIR NYANGASA na GEORGE LONGOPA wamesema kwamba wanajitahidi kwa uwezo wao kuhakiksha wagonjwa wanapata matibabu ya uhakika na yenye viwango vya juu ili kuhakikisha wagonjwa wa moyo wanakuwa salama .

  “Tunajitahidi kwa uwezo wetu kuwahudumia wagonjwa wote wanaofika katika taasisi yetu katika kiwango cha hali ya juu na kama ulivyoona mwenyewe, wagonjwa wanaridhika na matibabu wanayopata” alisema Dkt.NYANGASA alipokuwa akizungumza na Mwandishi wa habari hii

  Naye mkurugenzi mkuu wa taasisi hiyo ya MOYO YA JAKAYA KIKWETE Professa Mohamed Janabi, amesema kwamba ,katika hospitali hiyo wanaendelea kutoa huduma zilizo bora na kuwashauri wananchi nchini kujiuga na huduma za bima afya ili kuweza kumudu gharama za ugonjwa wa moyo katika matibabu na vipimo vyake.

  “Mwananchi akiwa kwenye mpango wa bima ya afya ni rahisi sana ana unafuu katika kutibwa kwani ni gharama kubwa , lakini mtu anapokuwa amejiunga katika mfuko wa bima ya taifa unaweza kugharimia “ alisema Dkt.Janabi.

  Amesema kwa sasa hospitai hiyo iamdelea na maboresho mbali mbali hasa katikaeneo la huduma kwa wateja ambapo amesema wafanyakazi waliopo katika idara hiyo wanapataiwa mafunzo mbali mbali ya kuweza kuhudumia wagnjwa wanaokuja katuka taasisi hhiyo.

  Kwa mujibu wa Dkt.Janabi mpaka sasa taasisi hiyo iliyoanzishwa mwaka 2015 mwaka jana iliweza kufanya upasuaji wa moyo kwa wagonjwa wenye jumla ya 973 ambapo ameongeza kuwa hospitali hiyo imepunguza kwa asilimia 80 kwa wagonjwa kwenda nje ya nchi kutibiwa na badala yake hutibiwa hapa nchini katka hospitali hiyo kutokana na wataalamu waliopo . 

  Hata hivyo amesema mbali na wagonjwa wa hapa nchin kutibiwa katika hosptali hiyo pia wagonjwa kutoka nchini za Comoro,Burundi,Congo na Uganda wamekuwa wakitibiwa katika taasisi hiyo.

  0 0

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba  Serikali zote Mbili Tanzania ile ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Mapinduzi ya Zanzibar zitaendelea  kujenga mazingira ya kuwapatia makaazi bora wafanyakazi wa Umma ili kuwapunguzia ukali za maisha wanayokabiliana nao kila siku.

  Alisema Serikali hizo zinatambua  wazi kuwa watumishi wa Umma wanapopatiwa makaazi bora ya kuishi hata utekelezaji wa majukumu yao katika maeneo ya kazi unaimarika  mara dufu.

  Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo katika hafla ya ufunguzi wa Nyumba za kuishi Maafisa na Askari wa Uhamiaji hapo Mtaa wa Ndugukitu Chake Chake Kisiwani Pemba ikiwa ni muendelezo wa shamra shamra za maadhimisho ya sherehe za kutimia Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.
  Alisema  ujenzi wa nyumba za watumishi nchini unatiliwa mkazo hasa wale wa Idara  ya Uhamiaji ambao ni macho ya Taifa kwa vile muda wao wote wamekuwa wakiutumia kusimamia usalama wa Taifa kwa kuwatambua  na kuwagundua wageni wote wanaoingia Nchini kinyumecha Sheria  na utaratibu zilizowekwa.

  Balozi Seif  alisema Makubaliano ya pamoja yaliyofikiwa hapo nyuma kati ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Mapinduzi ya Zanzibar  kuhusu kufunguliwa kwa Ofisi ndogo za SMT Visiwani Zanzibar ni vyema yakatekelezwa haraka iwezekanavyo hasa kwa zile Taasisi za Muungano ambazo hadi wakati huu hazijaitumia fursa hiyo.

  Akizungumzia hali ya Amani na Usalama  iliyopo Nchini inayowapa Fursa Wananchi kufanya shughuli zao kama kawaida Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliliagiza Jeshi la Polisi na Idara ya Uhamiaji Tanzania kuendelea kusimamia vyema hali hiyo.

  Balozi Seif alisema  wapo baadhi ya Watu hasa wale wenye asili ya Tanzania ambao tayari wameshaukataa na kubadilisha Uraia wao wamekuwa na tabia mbovu zinazowashawishi pia kujihusisha na masuala ya Kisiasa jambo ambalo wanaelewa vyema kuwa wanavunja sheria na Taratibu za Nchi.
  Akitoa Salamu katika hafla hiyo fupi Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani Tanzania Meja General Projestus Rwegasira  alisema Idara ya Uhamiaji imekuwa na  Mkakati wa muda mrefu katika azma yake ya kuimarisha mazingira bora ya Jeshi hillo.

  Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Mambo ya Ndani alisisitiza kwamba lengo la Idara ya Uhamiaji pamoja na masuala mengine iliyopangiwa kutekeleza, lakini pia imekusudia kujenga Ofisi sambamba na Nyumba za Kuishi Watendaji wa Jeshi hilo katika Wilaya zote Nchini Tanzania.

  Othman Khamis Ame
  Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
  4/1/2017.
   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akilikagua Jengo la Gorofa Mbili litakalobeba Familia Sita za Maafisa na Askari wa Uhamiaji  baada ya kulizindua rasmi hapo Mtaa wa Mtukitu  Chake  chake Kisiwani  Pemba ikiwa ni sherehe za kutimia Miaka 53 ya Mapinduzi Zanzibar.
   Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi, Maafisa wa Uhamiaji na Wizara ya Mambo ya Ndani walioshuhudia ufunguzi wa Jengo la Makaazi ya Maafisa na Askari wa Uhamiaji chake chake Pemba.Kuluia ya Balozi Seif ni Kamishna wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar Johari Msoud Sururu,Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani Meja Gneral Projestus Rwegasira na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh., Mohamed Aboud Mohamed. Kushoto ya Balozi Seif ni Mkuu wa Mkoa Kusini Pemba Mh. Mwnajuma Majid,Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiam Iddi na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mihayo Juma N’hunga.
   Muonekano wa Haiba ya Jengo Jipya la Makaazi ya  Maafisa na Askari wa Uhamiaji liliopo katika Mtaa wa Mtukitu Chake Chake Kisiwani Pemba.
   Kamishna wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar Johari Masoud Sururu akitoa Taarifa ya ujenzi wa jengo la Makaazi ya Maafisa na Askari wa Uhamiaji wakati wa hafla ya kulizindua rasmi.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Meja General Projestus Rwegasira akitoa salamu katika hafla ya uzinduzi wa jengo la Makaazi ya Askari wa Uhamiaji Chake chake Pemba.

  ndi cha Utamaduni cha Mkuta Ngoma cha Mkoa wa Kusini Pemba kikitumbuiza kwenye hafla ya ufunguzi wa Jengo la Makaazi ya Maafisa na Askari wa Uhamiaji Chake Chakle Pemba. Picha na – OMPR – ZNZ.


  0 0


older | 1 | .... | 1490 | 1491 | (Page 1492) | 1493 | 1494 | .... | 3353 | newer