Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1489 | 1490 | (Page 1491) | 1492 | 1493 | .... | 3353 | newer

  0 0

  Kamanda wa bendi ya Ngoma Africa aka FFU ya kule nchini Ujerumani, mwanamuziki Ebrahim Makunja aka Ras Makunja mapema leo ametembelea ofisi ya Michuzi Media Group jijini Dar es Salaam na kukutana na Ankal Issa Michuzi  pichani kulia pamoja na Ahmad Michuzi (Michuzi Jr) kushoto.
  Kamanda wa bendi ya Ngoma Africa aka FFU ya kule nchini Ujerumani, mwanamuziki Ebrahim Makunja aka Ras Makunja mapema leo ametembelea ofisi ya Michuzi Media Group jijini Dar es Salaam na kukutana na Ankal Issa Michuzi  pichani kulia pamoja na Ahmad Michuzi (Michuzi Jr) kushoto,pamoja na Cathbeth Kajuna

  0 0


  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, (kulia), akipeana mikono na Katibu Tawala Msaidizi (anayeshughulikia masuala ya serikali za mitaa), jijini Dar es Salaam, Bi. Merry Assey, baada ya kufungua semina ya mafunzo kwa watumishi wa Ofisi ya Katibu Tawala mkoa wa Dar es Salaam, iliyoandaliwa na Mfuko huo na kufanyika Januari 3, 2017 kwenye makao makuu ya PSPF Golden Jubilee Towers jijini.


  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said.

  MFUKO wa Pensheni wa PSPF, umeendesha semina ya mafunzo kwa watumishi wa Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, ili kuwajengea uwezo wa kushughulikia matatizo ya wananchi ambao ni wanachama wa Mfuko huo.

  Mafunzo hayo ya siku mbili, yameanza leo Januari 3, 2017, na kufunguliwa na Katibu Tawala Msaidizi (sehemu ya serikali za mitaa), Bi. Merry Assey kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa ea Dar es Salaam, Paul Makonda.

  “Niipongeze PSPF kwa kuandaa semina hii ambayo inatoa fursa ya watumishi hawa waliohudhuria katika mafunzo haya kuelewa huduma na shughuli zinazofanywa na Mfuko huu na kwa maana hiyo iwe rahisi kwenu kutatua kero za wananchi wanaofika pale Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa kutafuta ufumbuzi hususan kwa wanachama wa Mfuko huu,.” Alisema Bi. Assey, wakati akifungua semina hiyo.

  Akimkaribisha mgeni rasmi, Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, alisema, PSPF ilifikia uamuzi wa kuandaa semina hiyo kufuatia wazo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye alitaka kujengewa uwezo kwa watumishi wa Ofisi yake ili waweze kuwahudumia vema wananchi wakiwemo wanachama wa PSPF.

  “Nililipokea wazo hilo na sisi PSPF tukaona ni fursa nzuri kwa kuwaelimisha watumishi hawa ambao, ninahakika baada ya mafunzo haya, watakuwa mabalozi wetu wazuri lakini pia na wao watajiunga na Mfuko huu.” Alisema Bw. Mayingu.

  Mada mbalimbali zilitolewa kwa wanasemina hao ikiwa ni pamoja na ile ya shughuli za Mfuko iliyotolewa na Mkurugenzi wa Huduma wa Mfuko huo, Bi. Neema Muro, Kaimu Meneja Mafao, Bw. Haji Moshi na Maafisa wengine wa Mfujko huo.
   Bi. Merry Assey, akifungua semina hiyo
   Kaimu Meneja Mafao wa PSPF, Bw.Haji Moshi, akitoa mada ya namna mwanachama wa Mfuko huo anavyoweza kupata mafao yake.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Na Dotto Mwaibale.

  CHAMA cha Wahudumu wa Baa Tanzania (Chawabata) kimepinga zoezi linalofanywa na Manispaa ya Ilala la kukagua leseni za wauza vileo usiku.

  Akizungumza Dar es Salaam  jana Mwenyekiti wa chama hicho,  Ali Hussein alisema zoezi hilo linawatisha wateja wanapokuwa wakipata vinywaji katika baa mbalimbali.Hussein alisema chama hicho kimepokea malalamiko kutoka kwa wamiliki wa baa ambao ni wanachama wao.

  Alisema wiki moja kabla ya kuanza kwa sikukuu za mwishoni mwaka maofisa biashara wa Manispaa ya Ilala walikuwa wakipita katika baa mbalimbali maeneo ya Ukonga na vitongoji vyake kuanzia saa mbili usiku kukagua leseni.Alisema maofisa hao walikuwa wameongoza na askari polisi waliokuwa na bunduki jambo ambalo kiusalama sio zuri.

  "Huu utaratibu wa kukagua leseni usiku na mtutu wa bunduki unaweza kutoa fursa kwa wahalifu nao kwenda kwenye mabaa na kujifanya ni maofisa biashara na kufanya uporaji tunaomba serikali kuliangalia jambo hili" alisema Hussein.

  Alisema hali hiyo imejitokeza baada ya serikali kuzuia baa kufunguliwa asubuhi kama ilivyokuwa awali ambapo chama hicho oktoba mwaka jana kiliiomba serikali kupitia mtandao huu na katika vyombo vya habari  kuruhusu kufunguliwa kwa baa wakati wote ili kutoa nafasi ya wauza vileo kufanya biashara na kuweza kukusanya fedha za kulipa kodi ya serikali.

  Alisema kwa nyakati za mchana ni vigumu kukuta baa zikiwa wazi na ndio maana maofisa hao wameamua kwenda usiku kukagua leseni hizo jambo ambalo ni hatari kwa wateja na maofisa hao

  "Muda wa kufungua baa kuanzia saa 10 jioni unawaathiri wateja wetu kwani kwa masaa matano ya kufanyabiashara ya vileo na vinywaji vingine ni mchache mno" alisema Hussein.

  Alisema hatua hiyo ya serikali ya kuamuru baa kufunguliwa kuanzia saa 10 imeathiri wahudumu wa baa ambao wengi wao wamepunguzwa kazi ambapo wanaiomba serikali kuangalia jambo hilo.

  Meneja wa Baa ya Serengeti iliyopo eneo la mabaa Banana katika manispaa hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Emanuel alisema kitendo cha maofisa hao kukagua leseni za biashara usiku ni kigeni kwao na kinawatisha wateja wao ambapo ameomba manispaa kuangalia upya muda wa kufanya ukaguzi huo.

   Ofisa Habari wa Manispaa ya Ilala, Neema Njau alisema zoezi hilo lipo kisheria na linafanywa na kamati maalumu iliundwa na manispaa hiyo ambayo ipo chini ya wakuu wa polisi wa wilaya hiyo.

  "Ukaguzi wa leseni hizo hauwezi kufanyika mchana kwa kuwa baa nyingi zinakuwa zimefungwa lakini wasiliana na ofisa biashara wa manispaa atakupa maelezo mazuri zaidi" alisema Njau. 
   Mwenyekiti wa Chama cha Wahudumu wa Baa Tanzania (Chawabata), Ali Hussein (kulia), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, wakati akipinga zoezi linalofanywa na Manispaa ya Ilala la kukagua leseni za wauza vileo usiku. Kushoto ni Katibu wa chama hicho, Boniface Lameck.
  Katibu wa chama hicho, Boniface Lameck akitoa ufafanuzi 

  katika mkutano huo.

  0 0

  Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu ambaye pia ni Mkurugenzi wa huduma ya Upasuaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Bashir Nyangasa na Dk. Sun Long wakimfunga bandeji mgonjwa leo baada ya kumaliza kumfanyia upasuaji wa kuunganisha mishipa ya damu (AVF- Arterio Venous Fistula) kwa ajili ya kusafishia damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo (Hemodialysis).
  Daktari bingwa wa upasuaji wa kifua, moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Wambura Wandwi (Kulia) na Dkt. Bingwa wa Upasuaji Hussein Hassan wakimfanyia mgonjwa leo upasuaji wa kuunganisha mishipa ya damu (AVF- Arterio Venous Fistula) kwa ajili ya kusafishia damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo (Hemodialysis). Kushoto ni Afisa Muuguzi wa chumba cha upasuaji Sr. Elina Mulenda.
  Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu ambaye pia ni Mkurugenzi wa huduma ya Upasuaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Bashir Nyangasa (aliyevaa kofia ya pinki) akiwaonyesha kitu Dkt. bingwa wa upasuaji wa kifua, moyo na mishipa ya damu Wambura Wandwi (Kulia) na Dkt. Bingwa wa Upasuaji Hussein Hassan wakati wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kuunganisha mishipa ya damu (AVF- Arterio Venous Fistula) kwa ajili ya kusafishia damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo (Hemodialysis). Picha na Anna Nkinda - JKCI

  0 0

  Katibu Mkuu wa wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Mbogo Futakamba amewataka wafanyakazi wa Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (Dawasco) kufanya kazi kwa ushirikiano, nidhamu pamoja na kuwa wabunifu katika kazi, ili kufanikisha utoaji wa huduma bora ya Majisafi na Majitaka katika jiji la Dar es salaam pamoja na Miji ya Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani.

  Hayo yalizungumzwa katika kikao cha pamoja kilichoandaliwa na menejimenti ya Dawasco cha kumuaga Katibu Mkuu huyo ambaye anamaliza muda wake wa utumishi katika umma kisheria, kikao ambacho  kilichofanyika makao makuu ya shirika hilo, jijini Dar es Salaam.

  “Nawashukuru sana kwa ushirikiano wenu mzuri ambao umenipa heshima na kuniondolea aibu katika suala zima la Maji, ninawasihi muendelee kuwa na nidhamu pamoja na ubunifu katika kazi kwani mimi mwenyewe nilikuwa mbunifu”.

  Aidha, ameipongeza Dawasco kwa kazi nzuri ambayo wamekuwa wakifanya ikiwemo ya kudhibiti upotevu wa Maji kwa kiwango kikubwa kwa kuzuia mivujo kwa wakati na wizi wa maji katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam na Pwani.

  Naye, Afisa Mtendaji mkuu wa Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (Dawasco), Mhandisi Cyprian Luhemeja amempongeza katibu mkuu huyo kwa ushirikiano na uaminifu mkubwa alionyesha kipindi chote cha utumishi wake, amemtakia heri na mafanikio katika maisha yake mapya anayokwenda kuyaanza. 

  “Kwa niaba ya wafanyakazi wote, tunakushukuru sana mzee wetu kwa mchango wako mkubwa katika shirika kipindi chote cha utumishi wako, tumejifunza mengi kutoka kwako, sisi wafanyakazi wa Dawasco tunakuombea Baraka na mafanikio makubwa katika maisha yako mapya ya ustaafu”.
  Katibu Mkuu wa wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Mbogo Futakamba (Katikati kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Menejimenti ya DAWASCO, baada yakumaliza kikao cha kumuaga katibu mkuu huyo (katikati kulia ) ni Afisa mtendaji mkuu wa Dawasco.

  0 0

  Na. Aron Msigwa - NEC.

  TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI imewataka Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi wa Uchaguzi mdogo wa Udiwani utakaofanyika katika Kata 20 za Tanzania Bara na Ubunge katika jimbo la Dimani Visiwani Zanzibar Januari 22, 2017 kuzingatia Sheria, Kanuni na Maadili ili Uchaguzi huo uwe Huru na wa Haki.

  Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhan wakati akifungua mafunzo ya siku 3 ya Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya jimbo na Kata na Maafisa wa Uchaguzi leo mjini Dodoma.

  Mkurugenzi Kailima amewataka Wasimamizi hao kuzingatia matakwa ya Katiba, Sheria, Kanuni na miongozo mbalimbali katika kushughulikia mambo yatakayojitokeza wakati wa uchaguzi huo.

  Katika kutimiza majukumu yao wawe tayari kutoa ufafanuzi juu masuala mbalimbali kwa kuzingatia sheria na kutokuwa tayari kukubali kuyumbishwa na mtu yeyote atakayekiuka miongozo, sheria na kanuni za Uchaguzi.

  Amewataka Wasimamizi hao watende mambo yote kwa kuzingatia kanuni na Sheria na kutoa maamuzi sahihi kwa mustakabali wa Taifa na kuwasisitiza kuepuka kutoa upendeleo katika maamuzi wanayoyafanya na wasikubali kuyumbishwa na matakwa ya baadhi ya watu.
   Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw.kailima Ramadhani akifungua mafunzo ya siku 3 ya Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya jimbo na Kata na Maafisa wa Uchaguzi leo mjini Dodoma. 


  Baadhi ya Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya jimbo na Kata na Maafisa wa Uchaguzi wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kutekeleza majukumu yao wakati wa Uchaguzi mdogo utakaofanyika Januari 22, 2017 leo mjini Dodoma. Picha na Aron Msigwa - NEC.  0 0

  Duru la Pili la Ligi Kuu soka ya Wanawake ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linatarajiwa kuanza kesho Jumatano Januari 4, 2017 kwa michezo minne itakayofanyika kwenye viwanja mbalimbali.

  Kwa mujibu wa ratiba, katika kundi ‘A’ pekee litakuwa na mchezo mmoja wakati kundi ‘B’ litakuwa na michezo mitatu kwa siku ya kesho Jumatano.

  Mchezo pekee wa kesho wa kundi ‘A’ utakuwa kati ya Mburahati Queens ya Kinondoni, Dar es Salaam na Viva Queens ya Mtwara – mchezo utakaofanyika Uwanja wa Karume jijini katika mzunguko wa sita wa ligi hiyo.

  Michezo mingine mitatu itakuwa ni ya Kundi B ambako Mejengo FC itacheza na Marsh Academy ya Mwanza kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida wakati Panama ya Iringa inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Sisterz ya Kigoma kwenye Uwanja wa Samora huku Victoria Queens ikiikaribisha Baobab ya Dodoma kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Kagera.

  Kabla ya michezo ya juma lijalo, upande wa Kundi A michezo yake miwili ya mzunguko wa sita itafanyika Alhamisi Januari 5, mwaka huu ambako Evergreen ya Temeke, Dar es Salaam itacheza na Fair Play ya Tanga kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.

  Mlandizi ya Pwani inatarajiwa kuikaribisha JKT Queens ya Dar es Salaam, katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Mabatini.

  0 0


  0 0
 • 01/03/17--06:58: Article 4


 • 0 0

  Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa atawasili mkoani Ruvuma kesho kwa ziara ya siku tano ambapo katika ziara hiyo atapita kukagua miradi mbalimbali ndani katika wilaya ya Mbinga na wilaya ya Songea Halmashauri ya Madaba. Kwa undani wa habari hii hii hapa video yake. 


  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga akiwakabidhi Mangariba wastaafu(Kina Mama na Kinababa Wakisasa) vitendea kazi watakavyotumia katika shughuli zao mpya baada ya kuachana na ukeketaji na kuamua kujiwekeza katika ujasiriamali.
  Mkurugenzi wa Kituo cha Kulea Watoto waliokimbia Kukeketwa cha (ATFGM-Massanga) Sister Stella Mgaya akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Watoto kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi.Margareth Mussai.
  Mkuu wa Wilaya ya Tarime Bw. Glorious Luoga akiongea wakati wa mahafali ya watoto waliokimbia kukeketwa na kujiunga katika kituo Watoto waliokimbia Kukeketwa cha (ATFGM-Massanga) ambapo aliwataka wazazi wanaowatenga na kuwalazimisha kuwakeketa watoto waliohitumu mafunzo kuacha tabia hiyo kwani watachukuliwa hatua kali za kisheria.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga akiongea wakati wa mahafali ya watoto waliokimbia kukeketwa na kujiunga katika kituo Watoto waliokimbia Kukeketwa cha (ATFGM-Massanga) ambapo alisisitiza kuwa serikali itaendelea kuwachukulia hatua wazazi na jamii inayoendelea na kitendo kiovu cha ukeketaji kwa watoto wa kike.PICHA NA IDARA YA HABARI .
  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi amepiga marufuku kufanyika kwa shughuli zozote zile za kimila zinazotumia chakula kuanzia mwezi wa huu wa Disemba mpaka Mei 2017.

  Shughuli hizo ni pamoja na Unyago, Ndoa na Ngoma za Majini. Alisema shughuli hizo zinazofanywa na Wananchi zimekuwa zinatumia chakula kingi hali hii inaweza kupelekea kutokea kwa janga la njaa mkoani hapo.
  Mkuu huyo wa Mkoa wa Lindi aliwataka Wananchi kuwa wavumilivu na waelewa kwani janga la njaa halichagui Mkoa bali matumizi mabovu ya chakula yanaweza kuleta janga hilo kwa Wananchi wote.

  “Sitaki kuwa Mkuu wa Mkoa ambaye Mkoa wangu umekutwa na janga la njaa kwani hii ni aibu kubwa hivyo Watu wawe makini katika matumizi ya chakula hata kama chakula wanalima kwa nguvu zao wenyewe“.

  Wakati huo huo Mhe. Zambi aliwataka Wananchi wa Ruangwa wajenge vyoo imara na vya matumizi ya muda mrefu, ili kuweza kujiepusha na maradhi ya Kipindupindu kama ambavyo yanaikabili Wilaya ya Kilwa.

  Aidha, Mkuu wa Mkoa aliwataka Watendaji wa vijiji kusimamia zoezi la kila Mwananchi wa eneo lake anakuwa na choo imara na Mtu atakaekaidi kufanya ujenzi wa choo cha nyumbani kwake basi achukuliwe hatua za kisheria.

  Vilevile aliwasa Wananchi kuwa na matumizi mazuri ya pesa wanazoipata za kuuza korosho au fidia wanazolipwa na kuacha matumizi mabovu ya pesa hizo kama ambaVyo inafanywa na baadhi ya Watu.

  Mhe. Zambi aliwakata Wananchi kutumia pesa wanazozipata katika kutengeneza maisha yao kama katika kusomesha Vijana wao na kujenga nyumba imara kwa ajili ya familia zao.

  Mkuu wa Mkoa Godfrey Zambi akiwa anaongea na wanakijiji wa Kijiji cha Makanjiro

  Mkuu Wa Wilaya ya Ruangwa Joseph Mkirikiti akiwa anaongea na wananchi wa kijiji cha Mandawa(Na: Mwanakheri Ahmed wa Ruvumatv.com)

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya posho mbalimbali zisizokuwa za kisheria zinaelekezwa katika miradi ya maendeleo.

  Ametia agizo hilo leo (Jumanne, Januari 3, 20017) wakati akizungumza na watumishi wa Manispaa ya Kigamboni akiwa katika ziara yake ya kikazi.

  “Kuanzia sasa marufuku Wakurugenzi kutoa posho zisizotambulika kisheria zikiwemo za mazingira magumu, kujenga uwezo na vitafunwa katika halmashauri zenu na badala yake fedha hizo zitumike kwenye miradi ya maendeleo,” amesema.Agizo hilo litawezesha Jiji la Dar es Salaam kuokoa sh bilioni 130 zilizokuwa zitumike na Halmashauri na Manispaa za jiji hilo, ambazo kwa sasa zitaingizwa kwenye miradi na shughuli za maendeleo.

  Aidha, Waziri Mkuu amewataka watumishi wa umma nchini kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na kuacha kutumia fedha kinyume cha utaratibu na watakaobainika Serikali haitosita kuwachukulia hatua kali za kisheria.

  “Katika halmashauri zetu kila mtumishi anashiriki katika ukusanyaji wa mapato hadi walinzi, lakini mwisho wa siku vitafunwa huliwa na wachache wanaojiita wakubwa huku wengine wakisikilizia kwa nje. Jambo hili haliwezekani,” amesisitiza.Waziri Mkuu amesisitiza kwamba Mkurugenzi yeyote atakayebainika kulipa posho hizo baada ya siku ya leo atakuwa amejifukuzisha kazi.

  Aidha, ameagiza fedha zilizokuwa zikitolewa kwa madiwani kwa ajili ya kuhamasisha maendeleo zisitolewe moja kwa moja kwa madiwani na badala yake zipelekwe kwenye kata husika na zifuatiliwe matumizi yake.

  Hata hivyo, Waziri Mkuu amezionya halmashauri zote nchini kuhakikisha kuwa kila fedha zinayopelekwa kwenye halmashauri hizo inatumika kama ilivyokusudiwa na atakayebainika kutumia kinyume hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.Pia amewataka watumishi wote wa umma nchini kuwajibika ipasavyo na kuhakikisha wanawatumikia vyema mwananchi ikiwa ni pamoja na kuepuka vishawishi na kujiingiza kwenye vitendo vya rushwa na ufisadi.

  Wakati huo huo, Waziri Mkuu ametoa siku tatu kwa watumishi 10 wa halmashauri hiyo ambao wamehamishiwa kutoka wilaya ya Temeke wawe wameripoti katika Manispaa hiyo, vinginevyo watakuwa wamejifukuzisha kazi.

  Awali Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Bw. Hashim Mgandilwa wakati akiwasilisha taarifa ya wilaya hiyo kwa Waziri Mkuu, alisema hadi sasa asilimia 98 ya watumishi waliotakiwa kuhamia kwenye halmashauri hiyo wameripoti isipokuwa 10 na hakuna taarifa zozote juu yao.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  L. P. 3021,
  JUMANNE, JANUARI 3, 2017

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifungua pazia kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa VERDE-MARINE HOTEL Mtoni Mjini Magharibi,hoteli ya kisasa yenye hadhi ya nyota 5 inayojengwa na kampunui ya ujenzi ya Bakhresa Group of Companies,ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar,(kulia) Mwenyekiti wa Bakhresa Group of Companies Bw.Said Salim Bakhresa.[Picha na Ikulu.]

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Manispaa ya Kigamboni jijini Dar es salaam akiwa katika ziara ya wialaya ya Kigamboni Januari 3, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa wialya ya Kigamboni baada ya kuwasili wilayani humo kwa ziara ya siku moja. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0  Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akiongoza waombolezaji kuaga mwili wa marehemu Kenan Mhaiki Rubani Mstaafu wa ndege za marais wa Tanzania wakati wa shughuli ya kuaga mwili wake iliyofanyika Kunduchi, jijini Dar es Salaam Januari 2 2017. Mwili wa marehemu umesafirishwa leo kwenda Songea Mjini Mkoani Ruvuma kwa mazishi yanayotayarajiwa kufanyika Januari 4, Makaburi ya Matogoro. (Imeandaliwa na Robert Okanda blogspot)
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Leonard Chamriho akitoa salamu kwa niaba ya serikali wakati wa ibada ya misa na shughuli ya kumuaga marehemu Kenan Paul Mhaiki.

  Katibu Mkuu Kiongozi wa zamani, Balozi Ombeni Sefue akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Kenani Mhaiki Rubani Mstaafu wa ndege za marais wa Tanzania wakati wa shughuli ya kuaga mwili wake iliyofanyika Kunduchi, jijini Dar es Salaam jana. Mwili wa marehemu umesafirishwa jana kwenda Mkoani Ruvuma kwa mazishi yanayotayarajiwa kufanyika Januari 4 2017. soma zaidi hapa

  0 0


  Na Omary Mngindo, Ruvu

  MBUNGE wa Jimbo la Chalinze Mkoa wa Pwani Mwanasheria Ridhiwani Kikwete Jan 3 amewatembelea wafanyabiashara katika kijiji cha Ruvu Darajani, Kata ya Vigwaza Halmashauri ya Chalinze Mkoa wa Pwani huku akiwaomba wawe wanahudhulia mikutano inayoitishwa na viongozi wao.

  Ridhiwani amefika kwenye kijiji hicho kwa lengo la kushuhudia utekelezaji wa agizo lililotolewa na Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Alhaj Hemed Mwanga linalowataka wenyeviti wa vijiji na vitongoji wilayani humo kuitumia siku ya Jan 3 kuwa maalumu kwa ajili ya kuwasomea wananchi wao mapato na matumizi ili wananchi wao watambue makusanyo na matumizi yake.

  Hata hivyo Ridhiwani alipofika mweAnye Makao ya ofisi ya kijiji hicho kinachongoza na Kambona Kwalo na ofisa Mtendaji wake Williamu Jeuli, mkutano haukufanyika kwa madai ya wananchi hao kugoma kusomewa wakidai kwanza lizungumzwe suala la mgongano unaohusha ardhi kati ya wananchi haona mmoja wa wakazi anateishi jijini Dar es Salaam wakidai ni la muda mrefu huku kukiwa hakuna utekelezaji wake.

  Baada ya kushindikana kufanyika kwa mkutano huo, Mwanasheria huyo aliamua kufanya ziara ya papohapo ya kuwatembelea wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao katupika soko la Ruvu Darajani ambapo pia alitumia fursa hiyo kuwaomba vijana kuwa na utamaduni wa kuhudhulia mikutano ya setikali ya kijiji kwani ndipo sehemu ya kuibua miradi kwenye eneo lao.

  Akizungumza na vijana hao Ridhiwani alisema kwamba kwa utaratibu ambao vijana na baaddhi ya wakazi hao ya kutohudhulia mikutano kwenye eneo lao kutawafanya kukikosesha maendeleo kwa sababu kila jambo la maendeleo linaibuliwa kwenye mikutano hivyo ni vema wakaweka itikadi zao pembeni katika masuala yanayohusu maendeleo.

  “Vijana wenzangu katika suala linalohusu maendeleo tuweke pembeni itikadi zetu binafsi, kwani katika maeneo yeyote ambayo mnayaona au kuyasikia yana mafanikio makubwa, chanzo kikuu ni watu wake kuitikia wito wa kuhudhuria mikutano kwani hapo ndipo wanapokaa na kukubalia jambo gani lifanyike au la, kwa utaratibu ambao mnauendeleza wa kutohudhulia mikutano mtaendelea kukidhohofisha kijiji chetu,” alisema Mwanasheria huyo.

  Alimalizia kwa kuwaomba wajitokeze kwa wingi siku ya Alhamisi katika mkutano utaofanyika kwenye ofisi ya kijiji chao ili waweze kuibua miradi yakimaendeleo badala ya kukaa vijiweni na kuendeleza migomo ya kutofika kwenye mikutano kwani hatua hiyo isiyo na yija itaendelea kukikosesha maendeleo kijiji chao.
  Mbunge wa jimbo la Chalinze, Halmashauri ya Chalinze Mkoa wa Pwani Mwanasheria Ridhiwani Kikwete akizungumza na baadhi ya wakaazi wa kijiji cha Ruvu Darajani alipokwenda kwa ajili kusikiliza mkutano wa kusomwa mwa mapato na matumizi ya kijiji ikiwa ni utekelezji wa agizo lililotolewa na Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Alhaj Hemed Majid la kuwataka viongozi wote wa vijiji vinavyounda wilaya hiyo kuitumia siku ya Jan 3 kuwasomea mapato na matumizi wannchi wao, hata hivyo mkutano huo umesogezwa mpaka Alhamisi ya Jan 5.
  Mbunge wa jimbo la Chalinze, Halmashauri ya Chalinze Mkoa wa Pwani Mwanasheria Ridhiwani Kikwete akiwaunga mkono wafanyabiashara wa samaki wa kukaanga wanaofanya biashara zao katika eneo la Ruvu Darajani pembezoni kidogo mwa barabara Kuu ya Dar es Salaam- Chalinze, Morogoro- Segera, alipowatembelea kushuhudia wanavyofanya shughuli zao hizo. 
  Mbunge Ridhiwani Kikwete akiwasikiliza wafanyabiashara waaouza bidhaa mbalimbali hapa wauza bidhaa jamiyambogamboga wakizungumza na mbunge wao.

  0 0

  Shukran

  0 0

  Usiku wa kuamkia mwaka mpya wa 2017 wadau Wasia na Laila waliandaa mnuso wa nguvu wa  Harusi yao kwenye Ukumbi wa Taj Hall ulioko Savoy Drive jijini Houston, Texas, Marekani.  Pata taswira  za tukio hilo hapa chini.
  Wadau Wasia na Laila wakimeremeta kwenye mnuso walioandaa
  Newly Wed Mr. Wasia akiwa na Mkewe Bi. Laila na kijana wao Zion.
  Kwa taswira zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Kamati ya Mpito TZUK kwa masikitiko makubwa imepokea taarifa za msiba wa baba mzazi wa Ndugu yetu na mwanajumuiya mwenzetu Chris Lukosi, Marehemu Mzee BONIFACE PANGAWE LUKOSI ambaye amefariki jana  tarehe 3/01/2017, nyumbani Tanzania.

  Taratibu za msiba zinaendelea kufanywa na watoto wa marehemu hapa U.K. wanatazamia kusafiri kesho alfajiri kuelekea Tanzania.Tunaomba kuwaombea safari njema na Mungu awape Faraja katika kipindi hiki kigumu. Wanajumuiya, Watanzania, Ndugu, Jamaa, na marafiki tunawaomba sana tujitoe kwa hali na mali kuwafariji watoto wa marehemu katika kipindi hiki kigumu na cha majonzi.

  Michango yote ielekezwe moja kwa moja 

  kwa mtoto wa marehemu Ndugu Chris Lukosi kupitia;
  Account name - Chris Lukosi
  Account No. 47710160
  Sort Code.  60-17-31
  Natwest Bank
  Kamati ya Mpito TZUK Itaendelea kuwapa taarifa zaidi za msiba na mahitaji nyumbani Tanzania, Mungu awabariki kwa kujitoa kwenu kuwafariji na kuwa pamoja na familia ya Marehemu 🙏🏾🙏🏾

older | 1 | .... | 1489 | 1490 | (Page 1491) | 1492 | 1493 | .... | 3353 | newer