Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1480 | 1481 | (Page 1482) | 1483 | 1484 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Mbunge wa Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesikitishwa na wizi wa dawa na uharibifu wa baadhi ya vifaa katika Kituo cha Afya cha Murangi, Musoma Vijijini na kuagiza wahusika wachukuliwe hatua.

  Agizo hilo alilitoa hivi karibuni wakati akikabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vya afya ikiwemo vitanda maalum 10, baisikeli za wagonjwa na vifaa vingine kutoka kwa wafadhili wa Australia kwa ajili ya Kituo hicho na kushuhudiwa na wananchi mbalimbali kutoka maeneo tofauti ya jimbo hilo.

  Awali kabla ya makabidhiano ya vifaa hivyo, alipokea taarifa kutoka kwa wananchi kuhusiana na wizi wa dawa uliomhusisha mlinzi wa Kituo hicho pamoja na tukio la kuharibiwa kwa gari la wagonjwa alilokabidhi mwezi Machi mwaka huu.

  Taarifa husika ilimkasirisha Profesa Muhongo na hivyo kuagiza wahusika wote wachukuliwe hatua za kisheria haraka iwezekanavyo ili iwe fundisho kwa wenye tabia za namna hiyo.Akizungumzia gari hilo, Profesa Muhongo alisema lilitolewa na Serikali ya Japan kwa ajili ya wananchi wa jimbo la Musoma Vijijini lengo likiwa ni kusaidia wananchi hao kuondokana na usumbufu waliokuwa wakiupata.

  Aliongeza kuwa Serikali hiyo ya Japan ilimuahidi magari mengine zaidi ikiwa gari hilo litatunzwa vizuri na kutumika kwa shughuli iliyokusudiwa.“Hii ni aibu kubwa, hata wafadhili watatushangaa na kutucheka, dawa nyingi tulipewa na wafadhili na gari ile tulikabidhiwa ikiwa bado mpya na kwa Tanzania gari za namna hiyo zipo mbili tu, ni hapa na Muhimbili,” alisema.

  Mbali na hilo aliongeza kuwa Serikali ya Japan ilitoa kiasi cha shilingi milioni 170 kwa ajili ya kuboresha Kituo hicho na kuongeza kuwa atamuomba Balozi wa Japan nchini kufanya ukaguzi wa matumizi ya fedha hiyo.Aliwaagiza Madiwani kufuatilia kubaini hatua iliyofikiwa ya matumizi ya fedha hiyo na alisema endapo itadhihirika kuna ubadhirifu wa aina yoyote hatua za kisheria zichukuliwe ikiwa ni pamoja na kurejesha fedha hizo.

  Profesa Muhongo alisema anashangazwa kupewa taarifa hiyo na wananchi huku viongozi wakiwa kimya bila kuonesha hatua walizochukua na hivyo aliwataka Madiwani kutokuwa waoga katika kuwachukulia hatua wanaofanya ubadhirifu.Aidha, Profesa Muhongo aliwaagiza Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Thadeus Makwanda na Kaimu Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Murangi, Dkt. Josephat Karambo kuhakikisha hadi kufikia Tarehe 15 mwezi ujao gari hilo liwe limetengemaa.
  Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akizungumza kabla ya kukabidhi vifaa. Wa kwanza kushoto ni Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Thadeus Makwanda na katikati ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Murangi, Dkt. Josephat Karambo. 
  Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akiwasili katika Kituo cha Afya cha Murangi kwa ajili ya kukabidhi vifaa mbalimbali. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Vicent Naane.
  Baadhi ya Vitanda ikiwa ni miongoni mwa vifaa vilivyokabidhiwa katika Kituo cha Afya cha Murangi.
  Matroni wa Kituo cha Afya cha Murangi, Sabina Daudi akitoa shukrani kwa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) baada ya kupokea vifaa kwa ajili ya kituo hicho.

  0 0

  JINA: DEUSDEDITI M. GOGADI. 

  Ni siku, miezi hatimaye mwaka mmoja sasa tangu ulipotangulia mbele za haki mpendwa baba yetu DEUSDEDITI M. GOGADI.

  Hatutasahau upendo, ucheshi na busara zako daima pengo lako halitazibika kamwe. Unakumbukwa  sana na mke wako Tecla Gogadi, watoto wako Jacqueline, Neema na Monica Gogadi, mkwe wako, mashemeji zako, ndugu, jamaa na marafiki.

  Mkesha wa kumuombea baba yetu utafanyika Nyumbani kijitonyama tarehe 30/12/2016 nyumbani kwake Kijitonyama kuanzia saa 2 usiku ukifuatiwa na ibada takatifu itakayofanyika tarehe 31/12/2016 saa 12.30 asubuhi katika kanisa la Katoliki la Mwenge maximilian Kolbe  RAHA YA MILELE UMPE EE BWANA 
  NA NURU YA DAIMA IMWANGAZIE 
  APUMZIKE KWA AMANI. 
  AMEEN.


  0 0


   Golikipa wa Ndanda FC, Jeremiah Kisubi akiokoa moja ya hatari langoni mwake wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara dhidi ya Yanga. Yanga imeshinda 4-0. (Picha na Francis Dande).
  Wachezaji wa Yanga wakipongezana baada ya Amis Tambwe kuipatia timu yake bao.
  Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma akimtoka beki wa Ndanda FC, Nassoro Kapama katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Yanga ilishinda 4-0.
   Wachezaji Juma Abdul, Vicent Bossou na Simon Msuva wakishangilia bao la 4 la timu hiyo lililofungwa na Bossou.
  Beki wa Yanga, Vicent Bossou akipiga kichwa mpira uliozaa bao la 4 la timu hiyo wakati ilipopambana na Ndanda FC kwenye Uwanja wa Uhuru.

  0 0


  Ziara ya Meya wa jiji la Dar es SalaamIsaya Mwita, imebaini kuwepo kwa wizi wa fedha katika vizimba vya soko la kariakoo jambo ambalo limeonyesha kulinyima jiji mapato kwa kipindi kirefu.

  Hatua hiyo imekuja baada ya wajumbe wa kamati ya Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam kufanya ziara ya kukagua mali za jiji ambapo ikiwa ni mwendelezo wa ziara zilizowahi kufanyika hapo awali.

  Katika kikao hicho ambacho kilifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa soko la kariakoo, Meneja Mkuu wa shirika la soko la Kariakoo Hetson Kips shirika hilo likabaliwa na tatizo la uwezo mdogo wa kifedha jambo linalofanya kushindwa kumudu kuendesha shirika hilo.

  Akizungumza katika kikao hicho, Meya wa Jiji Isaya Mwita licha kuonyesha kukerwa na hali aliyoiona katika soko hilo alimueleza mejena huyo kwamba asifanye mchezo na ujio huo kwani atafanya kwa vitendo nasio kupita tu.

  Isaya alisema anachotaka kukiona ni kwamba wafanye kila njia ili kuhakikisha kwamba jiji linapata fedha badala ya wizi ambao wanaufanya kwani kila kitu kinachoendelea ndani ya soko hilo anafahamu.

  “ Leo tunaongea kirafiki, sitaki kuongea sana, sitawawajibisha hata mmoja, ila kunasiku mtajikuta hampo hapa , narudia tena tukienda mbali zaidi kwa wizi huu ambao mnaufanya hali itakuwa mbaya” alisema Meya Isaya.
    Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akisikiliza taarifa ya soko iliyokuwa ikisomwa Mbele ya wajumbe wa halmashauri hiyo. 
   Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita a kizungumza na wajumbe wa halmashauri ya jiji na menejiment ya soko la kariakoo baada ya kufanya ziara yake Jana. 
  Mjumbe wa halmashauri ya jiji ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Kawe Halima Mdee akichangia jambo mara baada ya kuwasilishwa kwa taarifa ya soko hilo.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Ufuatao ni muktasari  wa thamani na faida ya kutuliza mawazo ya fikra kuleta amani ya nafsi kupitia mafunzo ya” Meditation” ama  kutafakari katika jamii zetu.

  Ulimwengu wa leo wa karne ya 21 unakabiliwa na changa moto nyingi sana kimawazo na maendeleo ya teknolojia kupitia sayansi na njia ya mitandao na kuwawezesha wanaadam kuwa karibu sana ya mitandao kulikoni jinsi ya karne zilizopita.

  Uijio huo wa maendeleo ya sayansi, pia umeleta mchanganyiko mkubwa kwenye ubongo wa jamii ya kizazi cha leo na hata kile kilichopita pia, hasa ukizingatia kwamba urahisi wa teknolojia na kuwa na uwezo wa habari na matukio dunia kupitia mitandawazi na hatimae, pia kujenga mazingira magumu kwa wale wasioitumia jinsi inavyostahili.
  Yoga Instructor Rumadha Fundi  Katika mkao wa "Gomukhasana" zoezi la Yoga na kutafakari.  Dunia ya kizazi kipya , kina kadiriwa na changa moto za kifra na mawazo, tamaa, nia ya kuwa kama wenzao na taabu ya mawazo katika jamii yetu inayoshawishiwa na hayo maendeleo tuliyonayo sasa. Mambo  kama vile “Stress” na shinikizo la kutaka kuwa  na ushindani katika jamii kumaendeleo  ni moja ya vikwazo vikubwa vinavyo sababisha hata jamii yetu iwe na msingi dhaifu kulinganisha na vizazi vya karne zilizopita, japokuwa kuna mabadiliko makubwa ya sayansi na teknolojia, lakini fikra za wengi katika jamii hazina uvumilivu na amani ya mawazo mema katika jamii zetu kutokana na vishawishi vya hayo maendeleo ya nayoletwa na mitandawazi katika viganja vyetu kila sekunde.


  Hivyo basi, kutokana na muktasari huu, hapo ndipo haja ya kutuliza mawazo na fikra za ubongo wa mwanaadam ni nguzo muhimu sana katika jamii zetu. Hivyo umadhubuti wa fikra na akili ndio njia pekee inayoweza kutoyumbishwa na vishawishi vinavyo shambulia akili ya mwanaadam mitandaoni kwa nia isiyo elimisha, bali kuujaza ubongo na hali inayo sababisha udhaifu wa mawazo,  kutokuwa na utulivu itumiwapo kwa nia isiyojenga na kuimarisha manufao ya akili na fikra. 

  SOMA ZAIDI HAPA

  0 0


  0 0


  Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Antony Mavunde (katikati), akikabidhi pikipiki zilizotolewa na mbunge wa viti maalum mkoa wa mara, Agnes Marwa kwa waendesha Bodaboda wa mjini Musoma na kudhaminiwa na NSSF, wakati wa Semina juu ya kujiunga na mfuko huo. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, James Oigo. jumla ya pikipiki 5 zilitolewa kwa waendesha bodaboda hao.
  Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Antony Mavunde(katikati), akikabidhi pikipiki zilizotolewa na Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Mara, Agnes Marwa, kwa waendesha Bodaboda mjini Musoma na kudhaminiwa na NSSF, jumla ya waendesha bodaboda 108 walijiunga na NSSF, Mbunge huyo alitoa pikipiki 5 kwa waendesha bodaboda hao.
  Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Antony Mavunde akizungumza wakati wa Semina iliyoandaliwa na Mbunge wa Viti Maalimu Mkoa wa Mara, Agnes Marwa kwa waendesha Bodaboda mjini Musoma na kudhaminiwa na NSSF, jumla ya waendesha bodaboda 108 walijiunga na NSSF, Mbunge huyo alitoa pikipiki 5 kwa waendesha bodaboda hao.
  Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Antony Mavunde akimkabidhi kadi ya uanachama wa NSSF kwa mmoja wa waendesha bodaboda wa mjini Musoma.

  0 0


  0 0
  0 0

  Profesa Mark Mwandosya jana alitimiza umri wa miaka 67. Yeye na familia yake walisherehekea siku hiyo ya kuzaliwa kwake kiaina kijijini Matema Beach,  ukingoni mwa Ziwa Nyasa. 
  Akiongea na Globu ya Jamii kwa njiaya mtandao Profesa Mwandosya alisema: "Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa zawaidi ya uhai. Nawashukuru ndugu, marafiki, na Watanzania wengi sana walionitumia salaam za hongera na kunitakia afya njema na maisha marefu." 
  Timu nzima ya  Globu ya Jamii pia inamtakia afya na maisha marefu zaidi na kumtaka aendelea kuwa mshauri wetu wa ufundi, kazi ambayo amekuwa akiifanya muda wote toka tumeanza Libeneke. Hongera sana Prof na hongera zake Mama Lucy Mwandosya kwa kukutunza vyema.
   Profesa Mwandosya na mkewe Mama Lucy Mwandosya na watoto wao wakisherehekea Happy Birthday kiaina Matema Beach
    Profesa Mwandosya na familia yake wakisherehekea Happy Birthday kiaina Matema Beach
    Profesa Mwandosya akilishwa keki na mjukuu 
   Profesa Mwandosya na mkewe Mama Lucy Mwandosya na wanafamilia wakisherehekea mnuso wa Happy Birthday hiyo huko Matema Beach.

  0 0
 • 12/29/16--00:13: YALE YALEEEE......


 • 0 0

  Msimamizi wa Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha kuzalisha Umeme cha Kinyerezi II, Mhandisi Bernd Siegemund akiweka bayana mipango na mikakati ya kumalizika kwa ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi II katika muda uliopangwa. Wengine ni wataalam kutoka Tume ya Mipango, wataalam kutoka TANESCO pamoja na wahandisi wanaotekeleza mradi huo.


  Na Adili Mhina, Dar

  Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Tume ya Mipango imetembelea mradi wa ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi II kwa lengo la kuangalia maendeleo ya kituo hicho ambacho kinatarajiwa kuzalisha kiasi cha megawati 240 pale kitakapokamilika.


  Akizungumzia juu ya maendeleo ya mradi huo, msimamizi wa shughuli za ujenzi katika kituo hicho, Mhandisi Bernd Siegemund kutoka Ujermani alieleza kuwa ujenzi wa kinyerezi II unaendelea vizuri na unatarajia kukamilika kwa muda uliopangwa.  Ujenzi huo ulianza tarehe 13 Machi, 2015 na kutokana na kasi yake, Mhandisi Siegemund alieleza kuwa matarajio ni kwamba hadi kufikia mwezi Novemba mwaka 2017 mtambo wa kwanza utaanza kuzalisha umeme huku mitambo mingine ikiendelea kuwashwa kadiri itakavyokuwa inakamilika.  Kuhusu vifaa vya ujenzi vinavyohitajika, Mhandisi Siegemund alisema kuwa wanajitahidi kununulia ndani ya nchi vifaa vyote vinavyopatikana na vinavyokidhi mahitaji katika mradi huo na pale inapobidi hulazimika kuagiza kutoka nje.   Aliongeza kuwa pamoja na nondo kuzalishwa ndani ya nchi wamelazimika kuagiza kutoka nje kwa kuwa viwanda vya ndani bado havijazalisha aina ya nondo wanayohitaji katika ujenzi wa kituo hicho.    “Vifaa kama saruji na vingine tunaagiza kutoka kwa wazalishaji wa ndani ili kusaidia kukua kwa uchumi wa nchi. Tulitaka kuagiza nondo hapa nchini lakini hatukupata kiwango tunachohitaji kwa kuwa ujenzi huu hautumii nondo tulizozizoea katika ujenzi wa kawaida,”alieleza Siegemund.  Aliongeza kuwa mradi  huo utakapokamilika utakabidhiwa na kuendeshwa na Shirika la Umeme nchini (TANESCO) ambapo wataalam wa shirika hilo wanaendelea kupata elimu na uzoefu katika kutumia mitambo ya kisasa zaidi na wanashirikishwa katika kila hatua ya ujenzi wa kituo hicho.   Wataalam kutoka Tume ya Mipango walipata fursa ya kukagua maeneo mbalimbali ya mradi huo ambao umesaidia kupatikana kwa ajira takriban 400 katika ngazi mbalimbali na kumshauri mkandarasi huyo kuendelea na kasi hiyo ili malengo ya Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016/17-2020/21) pamoja na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 yafikiwe kwa haraka.

  Msimamizi wa Mradi wa ujenzi wa Kituo cha kuzalisha Umeme cha Kinyerezi II, Mhandisi Bernd Siegemund akitoa maelezo ya historia ya mradi huo kwa maofisa wa ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Tume ya Mipango wakati wataalam hao walipofanya ziara kukagua maendeleo ya ujezi wa kituo hicho.
  Mhandisi Omari Athuman (aliyeshika notebook) kutoka Tume ya Mipango akitoa ushauri kwa mkandarasi wa mradi wa ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme cha kinyerezi II.


  0 0


  Baada ya kufanya onyesho la kwanza Jijini Tanga lililowapagawisha Mashabiki wa Dansi Mkoani Tanga ndani ya Nyumbani Hotel (Pool side) sasa ni zamu ya Kanda ya Kusini...(KUSINI KUCHELEEE)

  Mashujaa Band Tanzania mkesha wa Mwaka mpya Jumamosi 31/12/2016 itakuwa Mkoani Lindi ndani ya Bwalo la Polisi kuanzia saa mbili usiku.

  Siku ya Mwaka mpya 01/01/2017 ni zamu ya wakazi wa Masasi..ukumbi wa Iwawa

  0 0
 • 12/29/16--01:12: Article 6


 • 0 0

  Mkaazi wa Singida Mjini, Mrisho Joseph mwenye umri wa miaka 23 ameibuka mshindi baada ya kubashiri vyema matokeo ya mechi kupitia Kampuni ya m-Bet na kujishindia zaidi ya Shilingi Milioni 50/-. 
  Mrisho amekabidhiwa fedha zake leo katika hafla  fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam kwenye ofisi za m-Bet 
  Kwa upande wake, Mkurugenzi wa m-Bet, Dhiresh Kabba alisema kuwa Kaungame alifanikiwa kuzoa kitita hich baada ya kufanikiwa kutabiri matokeo ya mechi 15 za ligi ya Ulaya kwa mtindo wa kucheza kawaida.
  “Tunafarijika kumkabidhi Mrisho Joseph kitita hicho cha Sh milioni 50/- akiwa ndiye mshindi wa m-Bet ambapo amesema atawekeza katika biashara zake ili aweze kusaidia wakazi mbalimbali wa mji wa singida wanaomzunguka,” alisema Kabba.
  Aliwataka watanzania kuchangamkia kutumia mtandao wa intaneti kuonyesha ushabiki halisi wa soka akisema kuwa Perfect 12 ni mchezo wa ziada unaoruhusu kutabiri mechi 12 kwa Tsh 1,000 tu ambapo ukipatia zote  unaondoka na kitita chako mchana kweupe na ndicho Mrisho alichofanya. 
  Naye Mshindi huyo, Mrisho Joseph amewashauri watanzania wote hasa wakazi wa Singida wenye umri unaoruhusiwa kisheria kujitokeza kubashiri matokeo ya mechi mbalimbali kupitia Kampuni ya m-Bet . 
  "Nashukuru sana m-Bet kwa kuniwezesha kujikwamua kimaisha, nitatumia fedha hizi kutimiza ndoto yangu ya kununua kiwanja na kuanza ujenzi", alisema Mrisho.
   Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abbas Tarimab (kushoto) akikamkabidhi mfano wa hundi  yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 50/- mshindi wa M-bet, Mkazi wa Mkoa wa Singida,Mrisho Joseph(kulia)kwenye hafla fupi ya makabidhiano hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo,Katikati ni Mkurugenzi wa M-bet, Dhiresh Kaba.

   Mkurugenzi Mkuu wa  Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, Abbas Tarimba(kushoto)na Mkurugenzi wa M-bet, Dhiresh Kaba,wakimpongeza kwa kumpigia makofi mshindi wa M-bet, Mkazi wa Mkoa wa Singida,Mrisho Joseph(kulia)wakati wa  hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam ya kumkabidhi hundi yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 50/- mshindi huyo leo.
  Mkurugenzi wa M-bet, Dhiresh Kaba(kushoto)na mshindi wa M-bet, Mkazi wa Mkoa wa Singida,Mrisho Joseph(kulia) wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa  Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, Abbas Tarimba,akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa  hafla fupi ya kumkabidhi hundi yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 50/- mshindi huyo jijini Dar es Salaam leo.

  0 0

  Na Fredy Mgunda,Iringa .

  MAKUNDI maalumu yanayohusisha vijana, walemavu na wanawake wa mjini Iringa walioingia katika mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa 2015 wakitoa masikitiko yao ya namna vyombo vya habari vilivyowapa nafasi finyu katika mchakato huo.

  Makundi hayo yalikuwa yakijadili ripoti ya tathmini ya jinsi vyombo vya habari (televisheni, magazeti na redio) vilivyoripoti habari zao wakati wakitia nia na kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo iliyofanywa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA).

  Dora Nziku anatoa malalamiko yake kwa kuvilaumu vyombo vya habari mkoani iringa kwa kutowapa nafasi wanawake,walemavu hata wale wasio na kipato kwa kuwa waandishi wengi walikuwa wanajali maslai kuliko ukubwa wa habari.“Naona kama wanawake tuliathiriwa zaidi katika mchakato huo kwani habari zetu hazikupata nafasi kama ilivyo kwa wagombea wengine hasa wanawake,” alisema Diwani wa Viti Maalumu Iringa Mjini, Dora Nziku (CCM).

  Nziku alisema imekuwa ni jambo la kawaida kwa baadhi ya wanahabari kuomba hela kwa wagombea na viongozi wa kisiasa ili waweze kutoa habari zao.“Pamoja na kuwapa hela wakati mwingine habari hizo hazitoki na mimi ni mmoja wa wahanga wa hilo, nimewahi kuita wanahabari, wakaniomba hela lakini hawakutoa habari zangu na nadhani hazikutoka kwasababu mimi ni mwanamke,” alisema diwani huyo bila kutaja wanahabari hao.

  Naye Agusta Mtemi aliyekuwa mgombea udiwani viti maalumu mjini Iringa (CCM) alisema katika kinyang’anyiro hicho aliwashinda kwa kura 266 wagombea wenzake zaidi ya 10 lakini katika mazingira tata alionekana kama mshindi namba mbili na kukosa nafasi ya kuwawakilishi wanawake wenzake katika Baraza la Madiwani la Jimbo la Iringa Mjini.
  Baadhi ya washiriki walikuwa wakijadili ripoti ya tathmini ya jinsi vyombo vya habari (televisheni, magazeti na redio) vilivyoripoti habari zao wakati wakitia nia na kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi Mkuu wa 2015 na mjadala huo uliongozwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA).

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (Kushoto) akimpatia Zawadi ya Ramani ya Tanzania Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayemaliza muda wake, Dkt. Tonia Kandiero (Kulia).
  Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayemaliza muda wake, Dkt. Tonia Kandiero (Kulia aliyesimama) akizungumza wakati alipotembelea TADB. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga.
  Afisa anayeshughulikia masuala ya kijinsia katika Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania, Bibi Beatrice Mrema akitoa neno la Shukrani kwa Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayemaliza muda wake, Dkt. Tonia Kandiero.
  Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayemaliza muda wake, Dkt. Tonia Kandiero (Wapili kulia mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti na maafisa waandamizi wa TADB.


  0 0  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Morogoro

  Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk. Kebwe Stevene Kebwe, amesema watu 13 akiweno aliyehusika kumchoma mkuki mkulima mmoja katika eneo la Mikumi, wamekamatwa na kutiwa mbaroni.

  Kebwe amesema hayo ailipokuwa akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari ambao wapo mjini hapa kwa jili ya mafunzo ya siku moja kuhusu masuala ya utoaji wa hati za kimila katika Wilaya tatu za mkoa huo.

  “Serikali imekamata watu 13 mmoja wao akiwa ndiye aliyehusika kumchoma mkuki mkulima huyo huku wengine wakiwa ni wale waliokuwa wakishabikia kitendo hicho. Hivi sasa watu hao wapo katika kituo cha polisi na wanasubiri kufunguliwa mashitaka kwa ajili ya kufikishwa mahakamani”amesema Kebwe.

  Aidha, Kebwe alimshukuru Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kwa kusimamia vema upimaji wa ardhi katika mkoa wa Morogoro.Alisema upimaji huo wa ardhi ndio mwarobaini wa migogoro ya ardhi.

  Amesema ni vyema serikali na wadau kuendelea kutoa elimu kwa wafugaji ili wananchi waweze kutambua mipaka ya maeneo yao hatua itakayosaidia kuepusha migogoro ya ardhi hususani baina ya wafugaji na wakulima.
  Mkuu wa mkoa wa Morogoro Kebwe Stevene Kebwe akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari.
  Baadhi ya washiriki wa warsha ya masula ya ardhi wakimsikiliza mkuu huyo wa mkoa


  0 0


  Mpendwa Mteja,
  YAH: KUFUNGWA KWA BENKI SIKU YA JUMAMOSI, 31/12/2016
  Tunapenda kukujulisha kwamba benki itafungwa siku ya Jumamosi, tarehe 31/12/2016. kwaajili ya kupisha uboreshaji wa mfumo wa kiufundi wa benki na huduma zitarejea kama kawaida siku ya jumatatu, tarehe 2/01/2017.
  Ijumaa, 30 Desemba 2016
  Tutakuwa wazi kuanzia saa                           2: 30 Asubuhi -10:00 Jioni
  Jumamosi, 31 Desemba 2016
  Tutafunga kupisha uboreshaji wa mfumo wa kiufundi wa Benki
  Jumatatu , 2 Januari 2017
  Kurejea kwa Huduma
  Unashauriwa kufanya miamala yote ya muhimu kabla ya siku tajwa hapo juu, ili kuepusha ucheleweshaji usio wa lazima.
  Huduma za kibenki kwa njia ya mtandao (Internet Banking), ATMs na Visa cards zitaendela kupatikana kama kawaida katika kipindi tajwa hapo juu.
  Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza na tunawahakikishia dhamira yetu ya kuendelea kuwahudumia ipasavyo. Kwa maelezo Zaidi tafadhali tembelea tawi letu lolote lililo karibu nawe au piga 0782 262 291.
  Tunakutakia Heri ya Mwaka Mpya wa 2017.
  Imetolewa na Utawala
  28.12.2016

  0 0


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole   Bi Mugwe Mbabe ambaye ni Mke mkubwa wa Marehemu Mzee Maarufu Admirabilis Mbabe Manyama(82) mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Chato mkoani Geita.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Bi. Regina Mbabe mke mdogo wa Marehemu Mzee Maarufu Admirabilis Mbabe (82) Manyama mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Chato mkoani Geita.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Deodatus Manyama wakwanza (kushoto) ambaye ni mdogo wa marehemu Marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama(82) mara baada ya kuwasili nyumbani kwa Marehemu Chato mkoani Geita.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Bi. Mugwe Mbabe mke mkubwa wa Marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Chato mkoani Geita.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini daftari la maombolezo mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama (82) Chato mkoani Geita
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na kutoa pole katika msiba huo wa Marehemu MzeeAdmirabilis Mbabe Manyama mara baada ya kuwasili nyumbani kwake.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
older | 1 | .... | 1480 | 1481 | (Page 1482) | 1483 | 1484 | .... | 3270 | newer