Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1479 | 1480 | (Page 1481) | 1482 | 1483 | .... | 3282 | newer

  0 0

  Pichani ni akina mama wa kinyakyusa wakiserebuka kwa wimbo wao wa kinyakyusa kwenye moja ya hafla yao huko jijini mbeya.
  Mama wa Kinyakwusa akiwa amezama ndani ya hisia zake kucheza wimbo wao wa kinyakyusaa kwa staili ya aina yake huko jijini mbeya.
  Wimbo huo ukiendelea kuteka hisia za Akina mama hao katika moja ya kumbi za sherehe Jijini Mbeya.
  Rahaa kweli kweli.


  0 0

   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye ni mbunge wa Ruangwa akisalimiana na baadhi ya wananchi wa kijiji cha Manokwe katika wilaya ya Ruangwa ambao walijitokeza kumsikiliza mbunge wao alipokuwa anawahimiza kufanya kazi ilikujileta maendelo katika wilaya ya ruangwa Waziri mkuu yupo Jimboni Ruangwa kwa ziara ya kikazi.
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye ni mbunge wa Ruangwa akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Manokwe katika wilaya ya Ruangwa ambao walijitokeza kumsikiliza mbunge wao alipokuwa anawahimiza kufanya kazi ilikujileta maendelo katika wilaya ya ruangwa Waziri mkuu yupo Jimboni Ruangwa kwa ziara ya kikazi
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye ni mbunge wa Ruangwa akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Manokwe katika wilaya ya Ruangwa ambao walijitokeza kumsikiliza mbunge wao alipokuwa anawahimiza kufanya kazi ilikujileta maendelo katika wilaya ya ruangwa Waziri mkuu yupo Jimboni Ruangwa kwa ziara ya kikazi .
   Wananchi wa kijiji cha Nga’u kilichopo wilaya ya Ruangwa wakiwa wamejikinga  mvua kwakutumia viti wakati wakimsikiliza mbungewao Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipokuwa akiwahutubia kwa ajili yakuhimiza shughuli za maendeleo jimboni Ruangwa Mkoani Lindi.Picha na Chris Mfinanga


  0 0

  Watanzania wametakiwa kuongeza hamasa ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini ikiwemo hifadhi za Taifa ili kufurahia rasilimali walizotunukiwa na Mwenyezi Mungu.

  Mchungaji Josephine Miller kutoka nchini Marekani aliyasema hayo jana wakati wa ziara yake ya kutembelea hifadhi ya Taifa ya Serengeti ili kujionea vivutio mbalimbali vya wanyama katika hifadhi hiyo.

  Alisema alipokuwa katika hifadhi mbalimbali barani Afrika ikiwemo za Afrika Kusini na Zimbabwe, alikuwa akisikia kuhusu uzuri wa hifadhi ya Serengeti hivyo amefurahia kutembelea hifadhi hiyo akisema kwamba hilo lilikuwa ni chaguo lake la pili baada ya kuonana na watu wa bara la Afrika.

  Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya, Dkt.Daniel Kulola, alisema ni vyema Mamlaka ya Hifadhi za Taifa TANAPA ikaongeza hamasa kwa Watanzania kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini ili kuukuza zaidi utalii wa ndani huku akiomba suala la miundombinu ya barabara kuboreshwa ili watalii.

  Kumbuka Mtanzania hulipa Tsh.11,800 pamoja na VAT kwa mtu mzima ili kuingia katika hifadhi ya Serengeti. Wageni hulipa dolla 70 ikikadiliwa kuwa Tsh, laki moja na elfu hamsini na nne. Hakika watanzania wanayo furusa kubwa kutembelea vivutio vya vya utalii.
  Waumini wa EAGT Lumala Mpya wakifurahia uwepo wao ndani ya hifadhi
  Mchungaji Josephine Miller kutoka Marekani (kulia) akifurahia uwepo wake ndani ya hifadhi ya Serengeti. Kushoto ni Mwanahabari na Blogger wa Lake Fm Mwanza, George Binagi
  Pundamilia, nyumbu na nyati wakiwa kwenye makundi ndani ya hifadhi ya Serengeti
  Twiga na upendo wao, hawaachani
  Ni muda wa chakula ndani ya hifadhi ya Serengeti huku pia Watalii wa Ndani na Watalii wa Nje, wakifurahia pamoja uzuri wa hifadhi ya Serengeti.


  0 0

  Inline image 1
  TWIGA WA KIPEKEE DUNIANI

  Twiga huyu mwenye ulemavu wa ngozi ambae kisayansi anajulikana kwa jina la 'OMO' akifananishwa na SABUNI YA OMO, aligunduliwa na Dk.Derek Lee katika mbuga ya TARANGIRE,Mkoani Arusha wakati dokta huyo akifanya uchunguzi na utafiti wa wanyama mbalimbali.

  Dk.Lee 'alimgundua' twiga huyu mwenye ulemavu wa ngozi kutokana na utofauti wake na twiga wenzake ambao wanapatikana katika mbuga hiyo.Twiga huyu alioneakana akiongozana na twiga wenzake sehemu mbalimbali za mbuga hiyo bila ya twiga wenzake kumshangaa wala kumtenga twiga huyu.
  Inline image 2
  Mnyama huyu ni mnyama aliyetofauti sana na wanyama wenzake katika kipengele cha rangi kwani rangi yake ni ile nyeupe ya kukolea inayofanana kabisa na rangi ya binadamu mwenye ulemavu wa ngozi ingawa hali hii kitaaluma inaitwa inaitwa leuscism na siyo albinism per se
  Gazeti moja la kimarekani lilitoa ripoti kwamba twiga wa aina hii yani mwenye ulemavu wa ngozi ni wachache sana hapa duniani na kama twiga huyu atatunzwa vizuri basi atakuja kuwa moja ya kivutio kikubwa sana cha utalii hapa duniani.

  0 0

  Na Is-haka Omar, Zanzibar.

  MADIWANI wa Manispaa ya Mjini, wamempitisha Khatib Abdulrahman Khatib , kugombea nafasi ya umeya wa manispaa hiyo.

  Uchaguzi huo ulimpendekeza meya huyo na kumpitisha baada ya kupata kura 27 za madiwani wote, hatua ambayo itamfanya kuwania nafasi hiyo katika uchaguzi wa Meya kupitia Chama Cha Mapinduzi.

  Khatib alipitishwa kuwania nafasi hiyo katika Mkutano uliofanyika  Ukumbi wa CCM Mkoa Mjini Amani Unguja ambapo mgombea huyo atachaguliwa kwa kuwa hakuna chama kingine chenye Madiwani ukiachia CCM na inatarajiwa atashika nafasi hiyo kwa mara ya pili. Kwa sasa Khatib ndie Meya wa Manispaa ya Mjini.

  Madiwani hao pia walipitisha majina ya Naibu Meya ambaye ni Bimkubwa Said Sukwa aliepata kura 15, akimshinda mpinzani wake , Saleh Fasihi Saleh aliepata kura 12.

  Kwa mujibu wa miongozo ya uchaguzi huo Majina hayo ya Meya na Naibu Meya yatapigiwa kura na wajumbe wa Baraza la Madiwani la Mjini.

  Kupitia Uchaguzi huo nafasi nyingine zilipigiwa kura ni Mwenyekiti wa Madiwani wa CCM katika manispaa hiyo na kupatikana Omar Mwalimu Juma , aliepata kura 13 na nafasi ya Katibu wa Kamati ya Madiwani iliyochukuliwa na Makame Khamis aliepata kura 27.

  Mapema Akifungua Mkutano huo Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai aliwataka Madiwani hao kuwachagua viongozi makini na wenye sifa za kujituma  kiutendaji.

  “ Endelelezeni utamaduni wa Chama Chetu katika kufanya uchaguzi huru na wa haki ili kupata viongozi watakaoweza kusimamia shughuli za manispaa yetu kwa ufanisi.

  Pia epukeni makundi na badala yake kuweni wamoja katika kufanya kazi za maendeleo ili wananchi waweze kunufaika na uwepo wenu katika Manispaa ya Mjini.”, aliwasihi Vuai na kuongeza kuwa Manispaa ya Mjini ndiyo kioo cha Mjini wa Zanzibar hivyo lazima pafanyike kazi ya ziada kuhakikisha panakuwa safi na kung’ara muda wote kama ilivyo Miji mingine Duniani.

  Naibu Katibu Mkuu huyo aliwasisitiza Madiwani hao kuwa Chachu ya kuleta maendeleo katika Wadi zao na kubuni miradi inayoendana na matakwa halisi ya wananchi ili kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho kwa vitendo.

  Akizungumza na Gazeti hili mara baada ya Uchaguzi huo Meya Mteule wa Manispaa hiyo Khatib Abdulrahman Khatib aliwashukru Madiwani hao kwa kumuamini na kumpitisha tena ili aweze kuendelea kuongoza Manispaa hiyo kwa awamu ya pili.

  Aliahidi kuendeleza mikakati ya kimaendeleo ndani ya Manispaa hiyo ikiwemo kushirikiana na viongozi wengine na wananchi kwa ujumla kuhakikisha Manispaa hiyo inakuwa na hadhi inayoendana na historia ya Zanzibar kimataifa.

  Aliwakumbusha wananchi kudumisha usafi na utunzaji wa miundombinu mbali mbali iliyomo katika Manispaa hiyo ili kuepuka kuingia katika mikono ya kisheria.

  0 0

  MEYA wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita anatarajia kuwa mgeni rasmi katika fainali za kuwania Kombe la Diwani wa Tabata yanayotarajia kuanza Januari nane mwakani kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Tabata.

  Akizungumza juzi, Diwani wa Kata ya Tabata, Patrick Assenga alisema ufunguzi wa mashindano hayo mgeni rasmi anatarajia kuwa Meya wa Ilala Charles Kuyeko.

  Assenga alisema kabla ya kuanza kwa mashindano hayo, Januari 3 anatarajia kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu shiriki 16 vikiwemo jezi na mipira kwa washiriki.

  Aseenga alisema mashindano hayo yatashirikisha timu mbili za mitaa nane ambako mitaa yenyewe ni pamoja na Tabata, Kisiwani, Msimbazi, Msimbazi Magharibi, Mtambani, Mandela, Matumbi na Tenge.

  Assenga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mipango miji wa jiji la Dar es Salaam alitaja zawadi kwa mshindi wa kwanza ni ng’ombe mkubwa na mpira, mshindi wa pili atazawadiwa ng’ombe na mpira na mshindi wa tatu atazawadiwa mipira na jezi.

  Aidha Assenga alisema katika ufunguzi wa mashindano hayo atawashirikisha wachezaji wa zamani kama akina Jella Mtagwa, Peter Tino na wengineo kwa lengo la kuwapa heshima kwa waliyoifanyia Tanzania miaka iliyopita.

  Assenga alisema hamasa hiyo itasaidia wachezaji wa sasa kuongeza hamasa kwa akina Mbwana Samatta ili wasijutie mchezo huo.

  0 0


  Na.Vero Ignatus Arusha.

  Mahakama kuu kanda ya Arusha imesikiliza maombi ya rufaa yayaliyowasilishwa na upande wa jamhuri na ule wa mshtakiwa Godbless Lema ambapo pande zote mbili wamekubaliana kusikilizwa rufaa ya upande wa jamhuri ambapo upande wa serikali wameiomba mahakama kuwasilisha kwa hati ya maandishi hapo kesho tarehe 30 disemba 2016 

  Aidha rufaa hizo ni pamoja na ile ya upande wa Jamhuri kutoridhika na maamuzi ya Jaji Dkt. Modesta Opiyo la kuwapa siku kumi (10) upande wa mshtakiwa Lema kufaili notisi ya rufaa ,na upande wa mshtakiwa ni ile ya kupinga uamuzi wa mahakama ya chini kushindwa kumpa Lema masharti ya dhamana

  Jaji aliyekuwa anasikiliza kesi ya rufaa hizo Salma Magimbi amesema kuwa mara baada ya upande wa jamhuri kuleta rufaa kwa njia ya maandishi upande wa mshtakiwa Lema wataijibu tarehe 30 desemba 2016 ambapo tarehe 2 januari watakutana pande zote kwa ajili ya kufanya majumuisho na maamuzi ya rufaa hiyo yatatolewa tarehe 4 januari 2017

  Hata hivyo baada ya kusikiliza rufaa hizo mahakama imeibua hoja yenyewe na kuwapa kazi mawakili wa pande zote mbili kuangalia kuwa notisi iliyowasilishwa na mahakama ya chini imekidhi matakwa ya kisheria?

  Kwa upande wa wakili wa mshtakiwa Peter Kibatala amesema kuwa kwa upande wao wameiomba mahakama kusubirisha rufaa yao ili wasikilize kwanza rufaa ya upande wa jamhuri kwani rufaa zote zimegongana na zinaelekea sehemu moja 

  "Unajua leo rufaa mbili zimegongana ile ya upande wa jamhuri na ile ya kwetu sisi,hivyo basi sisis tumeiomba mahakama kusitisha rufaa yetui isikilizwe ile ya serikali kwanza,kwani rufaa zote zinaelekea upandemmoja ,wandege apande ndege na wa basi apande basi "alisema Kibatala.

  Hata hivyo mbunge huyo wa Arusha mjini Godbless lema amerudishwa rumande hadi hapo maamuzi yatakapotolewa na mahakama. 


  0 0

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Wawekezaji na wananchi wa Jamuhuri ya Cuba wana nafasi nzuri ya kutumia mlango wa uwekezaji uliofunguliwa na Zanzibar katika kuanzisha miradi mipya kwenye Sekta ya Utalii hapa Nchini.

  Alisema mpango huo ambao licha ya kuimarisha uhusiano wa muda mrefu uliopo kati ya Zanzibar na Cuba tokea Uhuru wa Mataifa hayo Mawili lakini pia utaongeza ushirikiano wa pande hizo zinazofanana katika Historia zake.

  Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar wakati wa mazungumzo yake na Balozi wa Jamuhuri ya Cuba Nchini Tanzania Bwana Jorge Luis Lopez aliyefika kumuaga rasmi baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa Nchini.Alieleza kwamba Cuba imekuwa mshirika mkubwa wa harakati za maendeleo ya Wananchi wa Zanzibar hasa katika kusaidia Taaluma ya Sekta za Afya na Kilimo chini ya Muasisi wa Taifa hilo Marehemu Fidel Castro.

  Balozi Seif alisema mafungamano hayo kwa sasa yanapaswa kuelezwa nguvu zake katika Sekta ya Utalii inayoonekana kushamiri zaidi hivi sasa Ulimwenguni na kuleta mapato makubwa yanayochangia Mataifa mbali mbali ambayo tayari yamekwisha wekeza kwenye miradi hiyo.

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimuomba Balozi Jorge Luis licha ya kumaliza muda wake wa Kidiplomasia hapa Tanzania lakini bado ana nafasi ya kuisaidia Tanzania na Zanzibar kwa ujumla katika kuzitangaza Kiutalii kwa wawekezaji wa Nchi yake wakati atakaporejea nyumbani.

  Aliishukuru Serikali ya Cuba kwa juhudi kubwa iliyochukuwa katika kusaidia maendeleo ya Wananchi wa Zanzibar ambao katika maisha yao yote ya baadaye wataendelea kuzikumbuka juhudi hizo.Balozi Seif alifahamisha kwamba wataalamu wengi wa Cuba hasa wale wa Sekta ya Afya waliowahi kutoa Taaluma kwa vijana na Wananchi tofauti wa Zanzibar ni mfano halisi wa juhudi hizo.

  Mapema Balozi wa Jamuhuri ya Cuba Nchini Tanzania Bwana Jorge Luis Lopez alisema kwamba uhusiano wa Kihistoria uliopo kati ya Zanzibar na Cuba utaendelea kama kawaida licha ya mabadiliko ya watendaji wanaosimamia uhusiano huo.Balozi Lopez alimuhakikishia Balozi Seif kuwa mrithi wa kuchukuwa nafasi yake anayetarajiwa kuingia Nchini Tanzania wakati wowote kuanzia sasa ni Mwanadiplomasia mzoefu mwenye upeo wa kuzifahamu Siasa na mazingira ya Mataifa ya Bara la Afrika.

  Bwana Lopez alimuahidi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba wazo lake la kumuomba kuitangaza Zanzibar atakaporejea nyumbani kwake atalifanyia kazi ipasavyo ili kuweka kumbu kumbu nzuri wa uwepo wake wa kazi Nchini Tanzania.

  Balozi wa Cuba Nchini Tanzania Bwana Jorge Luis Lopez ambae mapema alikutana kwa Mazungumzo na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mh. Zubeir Ali Maulidi anarejea Nyumbani baada ya kumaliza muda wake wa kazi wa Miaka Minne hapa Tanzania.

  Othman Khamis Ame
  Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Balozi wa Cuba Nchini Tanzania Bwana Jorge Luis Lopez aliyefika Ofisini kwake Vuga kumuaga rasmi baada ya kumaliza muda wake wa kazi Nchini Tanzania.
  Balozi Seif akibadilishana mawazo na Balozi wa Cuba Nchini Tanzania Bwana Jorge Luis Lopez aliyefika kuaga rasmi akimalizia utumishi wake wa Kidiplomasia Nchini Tanzania.
  Nakukabidhi Picha hii tuliyopiga siku ya kwanza wakati nakukaribisha Zanzibar ulipoanza kazi yako ya Ubalozi. Picha hiyo walipiga pamoja miaka Minne iliyopita.
  Balozi Seif akimkabidhi Mlango Balozi wa Cuba Bwana Jorge Lopez kama kumbu kumbu ya kukaribishwa tena Zanzibar wakati wowote atakapopenda.
  Picha na – OMPR – ZNZ.


  0 0


  Na Anthony John- Glob ya Jamii.

  TAKWIMU zinaonyesha kuwa maambukizi mapya ya ukimwi yamepungua ikiwemo kwa watoto kwa asilimia 50% japokuwa bado ni janga kubwa kwa Dunia,Afrika na Tanzania hivyo nguvu zaidi inahitajika kupambana na ugonjwa huo.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo hii Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania Leonard Maboko amesema kuwa mapambano dhidi ya virusi vya Ukimwi yanatakiwa kuwa endelevu haswa katika maeneo yanayoonyesha kuathirika zaidi ili kutokomeza maambukizi mapya.

  " wakati maambukizo mapya yameshuka kwa asilimia 50 miongoni mwa watoto duniani 290,000 wapya waliambukizwa mwaka 2010 na watoto wapya 150,000 waliambukizwa Mwaka 2015 maambukizo mapya kwa watu wazima hayajashuka tangu 2010 duniani" amesema Maboko.

  Aidha maboko ameongeza kuwa Dunia imejiweke lengo la kutokomeza Ukimwi kama janga ifikapo mwaka 2030 kupitia Shirika la umoja wa mataifa linalo ratibu mapambano dhidi ya Ukimwi (UNAIDS) kwakuanza kutoa dawa za kufubaza virusi vya ukimwi mara tu mgonjwa anapogundulika kuwa na Ugonjwa huo.

  Wakati Huo Huo Mkurugenzi huyo alitumia fursa hiyo kuwaasa watanzania kutokubweteka na mafanikio ya takwimu kushuka kwa maambukizi ya virusi vya Ukimwi na badala yake kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa huo.
   
   Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Dkt Leonard Maboko (Katikati)akiwa na Mkuu wa kitengo cha Sheria Bi Elizabeth Kaganda(Kushoto)Pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Uraghibishi Bw Jumanne Issango(Kulia)Wakiongea na Waandishi wa Habari Kuhusu Takwimu za Hali ya Virusi vya  Ukimwi na Ukimwi kwa Tanzania kwa Kulinganisha na hali ya Dunia na ya Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika.
   Akizngumza na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Mikutano wa TACAIDS leo jijini Dar es salaam.Picha na Yasir Adam Blog ya Jamii⁠⁠⁠⁠

  0 0

   Watoto wakichota maji katika bomba la maji linalovuja katika kata ya Tabata Kimanga, kama walivyokutwa na kamera yetu mtaani.Picha na Humphrey Shao.  0 0  0 0  MWANAMUZIKI wa Hip Hop anayefanya poa kwa sasa hapa Bongo, Shariff Thabeet ‘Darassa’, leo amefanikiwa kuisimamisha Ilala alipokutana na mashabiki wake kabla ya Jumamosi hii hajapanda kwenye Jukwaa la Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam.

  Darassa na Roma, kwa pamoja watapanda katika Jukwaa la Dar Live kwenye Mkesha wa Mwaka Mpya ili kumaliza ubishi wa nani mkali wa michano katika pambano la Nichane Nikuchane.

  Akiwa kwenye Viwanja vya Karume jijini Dar, leo, Darassa aliisimamisha Ilala pale alipotoa burudani fupi ikiwa ni kionjo kabla ya shoo yenyewe kamili ya siku hiyo.

  Akizungumza na mashabiki wake, Darassa alisema: “Mashabiki zangu, siku hiyo ya Mkesha wa Mwaka Mpya mnachotakiwa kufanya ni kuja kwa wingi pale Dar Live kushuhudia miujiza nitakayoifanya kwani siku zote naamini huwa nafanya miujiza kila ninapopanda jukwaani.”

  Naye Meneja wa Mkuu wa Kampuni ya Global Publishers ambao ni waandaaji wa pambano hilo, Abdallah Mrisho, alisema: “Shoo hii inayoenda kufanyika ni ya tofauti, kama tujuavyo R.O.M.A na Darassa kwa sasa ndiyo habari ya mjini hasa kwenye Muziki wa Hip Hop, hii ni mara ya kwanza kwa Darassa kupanda kwenye Jukwaa la Dar Live, hivyo mashabiki ni fursa yenu kujumuika naye siku hiyo."

  Katika hatua nyingine, Meneja wa Dar Live na mratibu wa mpambano huo, Juma Mbizo, alisema: “Kwa kiingilio cha Sh 5,000, mashabiki watapata fursa ya kuingia na kushuhudia mpambano huo mkali ambao rasmi utaanza saa 7 mchana mpaka majogoo.”

  Mbali na wakali hao kupanda jukwaani siku hiyo, pia wengine watakaotoa burudani ni pamoja na Kundi la Muziki wa Taarab la Jahazi, Juma Nature, Makhirikhiri, MC Darada, Topido, ID Classic, H-Mbizo na wengine wengi.

  darassa-dar-live-10
  Darassa akigonga shoo ya bure Viwanja vya Karume leo.
  darassa-dar-live-17
  darassa-dar-live-18
  Mashabiki wakisukuma gari la Darassa.
  darassa-dar-live-1
  Meneja Mkuu wa Kampuni ya Global Publishers ambao ni waandaaji wa shoo ya R.O.M.A na Darassa, Abdallah Mrisho akitoa ufafanuzi kwa wanahabari waliokuwepo Viwanja vya Karume jijini Dar, leo kuhusu shoo hiyo.


  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na vikongwe wa kijiji cha Nandandala wilayani Ruangwa baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara kijijini hapo akiwa katika ziara ya jimbo lake la uchaguzi la Ruangwa , Desemba 28, 2016.


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Namilema wilayani Ruangwa akiwa katika ziara ya jimbo lake la uchaguzi, Desemba28, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Nandandala wilayani Ruangwa akiwa katika ziara ya jimbo lake la uchaguzi la Ruangwa Desemba 28, 2016.

  Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Namilema wialyani Ruangwa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao akiwa katika ziara ya jimbo lake la uchaguzi la Ruangwa Desemba 28, 2016.

  Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Namkunjera wilayani Ruangwa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kijijini hapo akiwa katika ziara ya jimbo lake la Ruangwa Desemba 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  (Tamisemi), Selemani Jafo, amefanya ziara katika halmashauri mpya ya
  Itigi na Manyoni huku akibaini uwepo wa changamoto mbalimbali hususan
  upungufu wa dawa katika Kituo cha Afya Itigi na Hospitali ya wilaya ya
  Manyoni mkoani Singida.

  Akizungumza katika ziara hiyo, Jafo amesema mara baada ya kutembelea
  Halmashauri hizo amebaini changamoto za dawa katika kituo cha afya
  Itigi pamoja na vifaa katika chumba cha mama huku akisema zipo
  changamoto ambazo zinazotakiwa kutatuliwa ndani ya halmashauri hiyo.

  Jafo akizungumza kuhusu suala la upatikanaji wa dawa, amesema tatizo
  hilo linaonekana ni kikwazo kutokana na watendaji kushindwa kutumia
  fedha za dharura wanazopewa na serikali kununulia dawa na vifaa tiba.

  “Naziagiza Halmashauri hizi kuhakikisha zinaweka kipaumbele uboreshaji
  wa vituo vya afya kwa kununua dawa nyingi na vifaa vingine tofauti na
  kusubiri zinazotoka Bohari ya Madawa (MSD),”amesema Naibu Waziri huyo

  Amewaagiza watendaji wa idara mbalimbali kuhakikisha wanashirikiana na
  mkurugenzi wa Itigi ili kutimiza wajibu wao na kuifanya halmashauri
  hiyo kuwa bora na kuwaonya kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo akiangalia
  kitanda ambacho kinatumiwa na akina mama wajawazito wakati wa
  kujifungua katika Hospitali ya wilaya ya Itigi mkoani singida wakati
  alipofanya ziara ya kushtukiza. Kulia kwake ni Dkt. Mary Rume Kaimu
  Mganga Mkuu wa Wilaya Itigi na anayefuatia ni Mkuu wa wilaya Manyoni
  Geoffrey Mwambe.
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo akipata
  maelezo toka kwa Agnesi Katumbo juu ya kusitishwa kwa kutolewa kwa
  risiti za kielectroniki ambayo ni kinyume na utaratibu wa Serikali na
  kutoa wiki moja kurudisha huduma hiyo ambayo ni chanzo cha kupotea kwa
  fedha za Serikali.
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo akipata
  maelezo toka Mkuu wa wilaya Manyoni Geoffrey Mwambe wakati wa ziara
  yake aliyoifanya wilayani humo Manyoni na Halmashauri ya Itigi,
  alieleza juu ya changamoto za wahamiaji, uharibifu wa mazingira na
  tatizo la utoro wa wanafunzi ambalo linasababishwa na wazazi zaidi
  katika wilaya hiyo, walio kaa kulia kwake ni Mkurugenzi wa Halmashauri
  ya Manyoni Edward C. Fussi na anayefuata ni Mwenyekiti wa Halmashauri
  ya Manyoni Moses Matonya.
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo
  akimpima uzito mmoja wa watoto katika hospitali ya wilaya ya Manyoni
  alipotembelea hospitali hiyo wilayani manyoni leo hii.


  0 0
  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Kinondoni ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Ally Hapi amezungumza na vyombo vya habari leo na kueleza umma kuwa kampuni ya Zantel imetii agizo alilotoa la kulipa mapato ya zaidi ya milioni 687 yatokanayo na mkataba ulioingiwa na manispaa ya Kinondoni mwaka 2009 uliogubikwa na harufu ya ufisadi katika utekelezaji wake.

  Mkataba huo ambao tangu usainiwe mwaka 2009 kati ya manispaa ya Kinondoni na kampuni ya Zantel, kampuni hiyo haikuwahi kulipa mapato husika kwa manispaa hiyo kwa mujibu wa mkataba.Aidha, mkataba husika uliibwa katika nyaraka za manispaa hiyo na hivyo mapato hayo kutokuwa na ushahidi wa kuyadai.

  Mapema wiki iliyopita, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi alitinga ofisi za kampuni hiyo akiwa na mkataba husika huku akiambatana na Kamati ya ulinzi na usalama na Mkurugenzi wa manispaa hiyo Aron Kagurumjuli na kuutaka uongozi wa Zantel kulipa mapato hayo ya kimkataba ndani ya siku 7.Kampuni ya Zantel imelipa fedha hizo tarehe 21 Disemba 2016 ndani ya wakati waliopewa kiasi cha zaidi ya milioni 687.

  Baada ya kulipwa fedha hizo Hapi ameeleza kuwa ametoa maelekezo na manispaa imeanza kujipanga kwa mujibu wa taratibu zake kuzipeleka fedha hizo katika ujenzi wa vyumba vya madarasa ya sekondari ambapo wilaya hiyo inakabiliwa na upungufu wa Madarasa 79 ya sekondari, hali inayowafanya wanafunzi zaidi ya 3169 waliofaulu kwenda kidato cha kwanza kukosa nafasi.Fedha hizo zitawezesha jumla ya madarasa mapya 40 kujengwa Kinondoni.

  “Tutahakikisha tunawabaini wote waliohusika kula njama za kuhujumu serikali na kuuficha mkataba huo kwa muda wa miaka saba..."alisema.Hapi alisema kutokana na ulipaji huo Manispaa ya Kinondoni kwa sasa tayari imeshawapa risiti ya malipo ya fedha hizo ambapo zililipwa Disemba 21, mwaka huu.

  Kaimu Mkuu wa Mkoa ametoa rai kwa kampuni zilizoingia mkataba na manispaa zote za mkoa wa Dar es Salaam miaka ya nyuma kuhakikisha wanalipa mapato yote ya serikali na kwamba wahusika watasakwa popote walipo hata kama mikataba husika wameiiba kifisadi katika mafaili ya manispaa kwa kushirikiana na watumishi wasio waadilifu.

  Katika hatua nyingine, Hapi amelipongeza jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam kwa kufanya kazi nzuri ya kudhibiti na kuhakikisha kunakua na usalama wa kutosha wakati wa sikukuu za Christmas. Amewatakia wananchi wote wa Dar es Salaam kwa niaba ya serikali ya Mkoa sherehe njema za mwaka mpya zenye amani na baraka na kwamba vyombo vya dola jijini Dar es Salaam vimejipanga vema kuhakikisha usalama wa kutosha unakuwepo.


  0 0


  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewahimiza wakazi wa vijiji saba wilayani Ruangwa waharakishe kufyatua matofali ili waanze ujenzi wa zahanati na yeye atawachangia mabati.

  Ametoa ahadi hizo leo (Jumatano, Desemba 28, 2016) wakati akizungumza na wananchi wa vijiji vya Namilema, Mbuyuni, Nandandara, Namkonjera, Muhuru, Chikundi na Chibula na viongozi wa wilaya ya Ruangwa, mkoa wa Lindi ambako anapita kuwasalimia wananchi wa jimbo lake na kuhimiza kazi za maendeleo. Waziri Mkuu yuko Ruangwa kwa siku nne kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka.Amesema sera ya Serikali ni kuwa na zahanati kwa kila kijiji na kituo cha afya kwa kila kata na kwamba umefika wakati wa kuanza kutekeleza kaulimbiu ya jimbo hilo inayosema “Ruangwa kwa maendeleo, inawezekana.”

  Katika kuhimiza ujenzi wa zahanati hizo, amechangia mabati kati ya 50 na 150 kwa kila kijiji na akawahimiza wahakikishe wanakamilisha mapema ujenzi wa maboma ili aweze kutimiza ahadi yake ya mabati.

  Amesema katika awamu iliyopita, alikazania sana suala la elimu kwa kusimamia ujenzi wa nyumba za walimu na madarasa kwenye shule ambazo hazikuwa na madarasa ya kutosha. Pia alisimamia ukarabati wa majengo chakavu katika baadhi ya shule.

  “Kuanzia awamu hii na miaka minne iliyobakia, mkakati wangu ni kusimamia upatikanaji wa maji safi na suala la kuboresha sekta ya afya katika jimbo zima nikishirikiana na uongozi wa Halmashauri yetu,” amesema.Pia amemwagiza Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, Dk. Japhet Simeo ahakikishe anawasiliana na viongozi wa vijiji hivyo ili wapatiwe michoro ya ramani zilizoidhinishwa na Wizara ya Afya.

  Wakati huohuo, Mkurugenzi wa kampuni ya Umemejua ya Baraka Solar Specialist, Bw. Ansi Mmasi amesema atajitolea kuweka mfumo wa umemejua wa watts 300 pamoja na nyaya zake kwenye zahanati inayotaka kujengwa kwenye kijiji cha Namilema.Alisema anaishukuru kwa kuwapa kazi makandarasi wazawa na akawataka wakandarasi wenzake watumie vifaa bora na imara pindi wanapopewa kazi ya kutoa huduma na taasisi mbalimbali ikiwemo halmashauri na idara za Serikali.

  “Tujitahidi kufanya kazi hizi kwa weledi na tutumie vifaa bora na imara ili watu wanaotarajia huduma zetu waweze kuridhika na kuendelea kuwa na umani na wakandarasi wazawa kwamba tunaweza kufanya kazi nzuri na zenye ubora unaotakiwa,” amesema.

  Naye Mkurugenzi wa kampuni ya ujenzi ya Wanyumbani Construction, Bw. Fakihi J. Bakili alisema atachangia mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa zahanati hiyo ya kijiji cha Namilema. Pia alichangia mifuko 100 kwenye zahanati ya kijiji cha Manokwe na mifuko mingine 50 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Chikundi.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMATANO, DESEMBA 28, 2016.

  0 0  Mkuu wa wilaya ya Kinondoni ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Ally Hapi amezungumza na vyombo vya habari leo na kueleza umma kuwa kampuni ya Zantel imetii agizo alilotoa la kulipa mapato ya zaidi ya milioni 687 yatokanayo na mkataba ulioingiwa na manispaa ya Kinondoni mwaka 2009 uliogubikwa na harufu ya ufisadi katika utekelezaji wake.
  Mkataba huo ambao tangu usainiwe mwaka 2009 kati ya manispaa ya Kinondoni na kampuni ya Zantel, kampuni hiyo haikuwahi kulipa mapato husika kwa manispaa hiyo kwa mujibu wa mkataba.
  Aidha, mkataba husika uliibwa katika nyaraka za manispaa hiyo na hivyo mapato hayo kutokuwa na ushahidi wa kuyadai.
  Mapema wiki iliyopita, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi alitinga ofisi za kampuni hiyo akiwa na mkataba husika huku akiambatana na Kamati ya ulinzi na usalama na Mkurugenzi wa manispaa hiyo Aron Kagurumjuli na kuutaka uongozi wa Zantel kulipa mapato hayo ya kimkataba ndani ya siku 7.
  Kampuni ya Zantel imelipa fedha hizo tarehe 21 Disemba 2016 ndani ya wakati waliopewa kiasi cha zaidi ya milioni 687.
  Baada ya kulipwa fedha hizo Hapi ameeleza kuwa ametoa maelekezo na manispaa imeanza kujipanga kwa mujibu wa taratibu zake kuzipeleka fedha hizo katika ujenzi wa vyumba vya madarasa ya sekondari ambapo wilaya hiyo inakabiliwa na upungufu wa Madarasa 79 ya sekondari, hali inayowafanya wanafunzi zaidi ya 3169 waliofaulu kwenda kidato cha kwanza kukosa nafasi.
  Fedha hizo zitawezesha jumla ya  madarasa mapya 40 kujengwa Kinondoni.
  “Tutahakikisha tunawabaini wote waliohusika kula njama za kuhujumu serikali na kuuficha mkataba huo kwa muda wa miaka saba..." alisema.
  Hapi  alisema kutokana  na ulipaji huo Manispaa ya Kinondoni kwa  sasa tayari imeshawapa  risiti ya malipo   ya fedha hizo ambapo zililipwa Disemba  21, mwaka huu.
  Kaimu Mkuu wa Mkoa ametoa rai kwa kampuni zilizoingia mkataba na manispaa zote za mkoa wa Dar es Salaam miaka ya nyuma kuhakikisha wanalipa mapato yote ya serikali na kwamba wahusika watasakwa popote walipo hata kama mikataba husika wameiiba kifisadi katika mafaili ya manispaa kwa kushirikiana na watumishi wasio waadilifu.
  Katika hatua nyingine, Hapi amelipongeza jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam kwa kufanya kazi nzuri ya kudhibiti na kuhakikisha kunakua na usalama wa kutosha wakati wa sikukuu za Christmas. Amewatakia wananchi wote wa Dar es Salaam kwa niaba ya serikali ya Mkoa sherehe njema za mwaka mpya zenye amani na baraka na kwamba vyombo vya dola jijini Dar es Salaam vimejipanga vema kuhakikisha usalama wa kutosha unakuwepo.

  0 0

  Waliosimama toka kushoto. Ahmed Amasha, Rishard Adolph, Dotto Rutta  Mokili, Salim Omar, chini toka kushoto Abdullah Shamuni, Hilal Hemed na Yussuf Abeid. 

  0 0

  Na Asteria Muhozya, Muleba

  Imeelezwa kuwa, Serikali imepanga kutumia Nguzo za Zege katika utekelezaji wa Mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini Awamu ya Tatu, unaotarajia kuanza kutekelezwa kuanzia mwezi Januari, 2017 chini ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

  Hayo yamebainishwa kwa nyakati tofauti na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa mradi wa REA Awamu ya Pili katika Kata za Ngenge na Ngwanseri, Wilayani Muleba Mkoani Kagera, pamoja na kueleza mipango ya Serikali katika utekelezaji wa mradi husika Awamu ya Tatu.

  Dkt. Kalemani amesema kuwa, lengo la kutumia nguzo hizo za zege ni kutokana na uimara wake utakaowezesha upatikanaji umeme wa uhakika na kuepuka kuchomwa na kuongeza kuwa, tayari nguzo hizo zimeanza kutumika katika Mkoa wa Kilimanjaro.

  Akizungumzia utekelezaji wa REA Awamu ya Pili, amesema Serikali imetekeleza mradi huo kwa kasi kubwa kutokana na dhamira yake ya kuhakikisha kuwa, ifikapo mwaka 2025 asilimia 75 ya Watanzania wawe wameunganishwa na nishati hiyo ambayo ni kichocheo cha shughuli za kiuchumi.

  “ REA awamu ya pili imekamilika kwa kiwango kikubwa. Vipo baadhi ya vijiji havijafikiwa kutokana na dosari ndogo ndogo lakini tutavikamilisha kuwezesha utekelezaji wa Awamu ya Tatu. Hata katika Wilaya hii vipo na tayari nimemwelekeza Mkandarasi kukamilisha kazi hiyo haraka,”amesisitiza Dkt. Kalemani.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt.Medard Kalemani, akizungumza jambo wakati wa Mkutano wake na wananchi wa Kata ya Ngwanseri,wilaya ya Muleba, wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Mradi wa REA Awamu ya Pili.
  Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhandisi Richard Ruyango,akizungumza jambo wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt.Medard Kalema ni kukagua utekelezaji wa Mradi wa REA Awamu ya Pili.Wengine katika picha ni baadhi ya Viongozi wa Halmashauri hiyo,Wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, REA,TANESCO, na Wakandarasi wanaotekeleza mradi husika.
  Wananchi wa Kata za Ngwanseri na Ngenge wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Dkt.Medard Kalemani na ujumbe wake wakati wa ziara yake a kukagua utekelezaji wa Mradi wa REA Awamu ya Pili wilayani Muleba.


  Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini Prof.Anna Tibaijuka (kulia) akiteta jambo na Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Dkt.Medard Kalemani ( katikati) mara baada ya kumaliza mkutano wake na wananchi wa Kijiji cha Kishuro. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhandisi Richard Ruyango.


older | 1 | .... | 1479 | 1480 | (Page 1481) | 1482 | 1483 | .... | 3282 | newer