Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1481 | 1482 | (Page 1483) | 1484 | 1485 | .... | 3278 | newer

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

     Simu:255-22-2114615, 211906-12
  Barua pepe: nje@nje.go.tz
  Barua pepe: gcu@nje.go.tz
  Tovuti : www.foreign.go.tz

  Nukushi: 255-22-2116600

                

   

   

                  20 KIVUKONI           FRONT,
                 P.O. BOX 9000,
     11466 DAR ES SALAAM, 
                                      Tanzania.

   


  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


  Baadhi ya Vyombo vya habari vya hapa nchini hivi karibuni vilitoa taarifa kuwa, Watanzania 8 wanaodaiwa kuwa ni majasusi wa Serikali ya Tanzania wamekamatwa nchini Malawi kwa tuhuma za kuingia kwenye mgodi wa urani wa Kayerekera uliopo nchini Malawi kinyume cha sheria. 

  Taarifa hiyo kwa mara ya kwanza ilitolewa na chombo cha habari cha Malawi ambacho kilidai kuwa watu hao wametumwa na Serikali ya Tanzania ili kuchunguza kama Serikali ya Malawi inatengeneza silaha za nyuklia kwa kutumia madini ya urani ya kutoka mgodi huo.

  Kufuatia taarifa hizo, Wizara kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini Malawi ulifuatilia ili kubaini ukweli wa tukio hilo. Baada ya kufuatilia ilibainika kuwa ni kweli Watanzania 8 kutoka taasisi ya CARTAS iliyo chini ya Kanisa Katoliki Songea mkoani Ruvuma walikamatwa na vyombo vya usalama katika Wilaya ya Karonga ambayo inapakana na Wilaya ya Kyela.  Watanzania hao mara moja walifunguliwa kesi kwa kutuhumiwa kufanya kosa la jinai la kuingia eneo la mgodi bila kibali (criminal trespass).

  Ubalozi uliwasiliana na Taasisi ya CARTAS kutaka kufahamu madhumuni ya watu hao kufanya ziara nchini Malawi. Ubalozi ulielezwa kuwa ziara hiyo ilikuwa ni ya mafunzo ambapo walitaka kufahamu juu ya madhara yatokanayo na machimbo ya madini ya urani. Watanzania hao kwa sasa wapo katika gereza kuu la Mzuzu hadi kesi yao itakapotajwa tena tarehe 04 Januari 2017.

  Ubalozi unaendelea kufanya mawasiliano na Kanisa Katoliki Songea ili kupata maelezo zaidi kuhusu ziara ya watu hao kwa madhumuni ya kuyawasilisha mamlaka husika ili watuhumiwa waweze kutolewa.

  Aidha, Wizara kupitia Ubalozi umebaini kuwa CARTAS iliruhusu watu hao kufanya ziara nchini Malawi bila kupata kibali kutoka mamlaka husika na bila kutoa taarifa Ofisi ya Ubalozi kuhusu ziara hiyo.

  Aidha, kipindi cha kufanya ziara hiyo nchini Malawi hakikuwa muafaka kwa kuwa watumishi wa Serikali ya Malawi wanakuwa katika likizo ya mwaka kuanzia tarehe 22 Desemba hadi 03 Januari 2017. Hii inakwamisha juhudi za kuwafuatilia watu hao ikiwa ni pamoja na kukwama kwa maombi ya kibali cha kuwatembelea watu hao tarehe 28 Desemba 2016.

  Wizara inatoa wito kwa mara nyingine kwa taasisi za dini, vyuo vya elimu na watu binafsi kuomba vibali na kufuata sheria za nchi nyingine wanapofanya ziara za mafunzo au ziara nyinginezo ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na ofisi za Balozi zetu kwa madhumuni ya kufahamishwa taratibu zinazotakiwa kufuatwa kabla ya kufanya ziara husika ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza.

  Wizara, kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini Malawi unaendelea na jitihada za kuhakikisha kuwa suala hilo linapatiwa ufumbuzi kwa haraka.

  Imetolewa na:

  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki


  Dar es Salaam, 29 Desemba  2016.


  0 0


  0 0

  Katika gazeti la Mwananchi toleo la Desemba 16 mwaka huu, ukurasa wa 11, kulichapishwa barua ya Afisa Mifugo mstaafu wilayani  Mpwapwa, Dododma, Bw. Edward Chedego Uledi. Katika barua yake iliyosomeka “Rais Magufuli nisaidie nilipwe stahiki zangu,” mstaafu huyo alilalamikia kupunjwa mafao yake.


  Mtumishi huyo aliyestaafu tangu 2008, alilalamikia kitendo cha maafisa utumishi   kuchelewa kurekebisha taarifa zake kwa kuzingatia cheo chake cha mwisho na hivyo kusababisha apunjwe mafao na akalipwa kwa mujibu wa cheo cha zamani.


  Serikali imefuatilia kwa kina na kuona kuna ukweli katika sehemu ya madai ya mstaafu huyo. Tunapenda kuutaarifu umma kuwa malalamiko ya mwananchi huyo sasa yameshughulikiwa haraka na Bw. Uledi amejulishwa na kuridhika na hatua zilizochukuliwa. Akiishukuru Serikali kwa hatua hizo alisema:


  Nimeeleweshwa vizuri, nimeelewa na naishukuru sana Serikali ya Awamu ya Tano kwa kasi hii. Namshukuru sana Rais na nawapongeza watendaji wote waliojitoa kufuatilia na kutatua malalamiko ya mimi mwananchi wa kawaida.” 


  Serikali inatumia nafasi hii kuvipongeza vyombo vya habari nchini vinavyojitoa na kujikita katika kusaidia kutatua changamoto za kweli za wananchi. Aidha tunawakumbusha watendaji wa Serikali kuendelea kufanyakazi kwa bidii, ubunifu, kasi na kujituma katika kufuatilia na kutatua kero mbalimbali za wananchi.


  Imetolewa na:
  Dkt. Hassan Abbasi,


  Mkurugenzi Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali.  


  0 0

  Baadhi ya wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), leo wametoa zawadi mbalimbali kwa wagonjwa waliolazwa katika hospitali hiyo.

  Akizungumza katika hafla hiyo fupi, Mkurugenzi wa Uuguzi katika hospitali hiyo, Bi. Agnes Mtawa amewashukuru wauguzi hao kwa kuonyesha ushirikiano katika kazi na kutoa huduma nzuri kwa wagonjwa.

  Mtawa aliwaasa wauguzi kuendelea na upendo huo waliouonyesha katika kipindi chote cha mwaka 2016 kwa kuwa ndio upendo ambao Mungu anataka wauonyeshe kwa wagonjwa.

   Pia, aliwapongeza kwa kukabiliana na changamoto mbalimbali katika mwaka huu na kuwataka kutumia changamoto hizo kama sehemu ya mikakati ya mwaka 2017.

  Naye Meneja wa Jengo la Watoto, NPC One, Bi. Anna Mponeja aliwashukuru wauguzi kwa kutoa huduma nzuri kwa wagonjwa katika kipindi chote cha mwaka 2016. Hafla hiyo imeudhuriwa na zaidi ya wauguzi 70. 
   Mkurugenzi wa Uuguzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Agnes Mtawa akizungumza na wauguzi baada ya wauguzi hao kutoa zawadi kwa wagonjwa waliolazwa katika hospitali hiyo. Zawadi hizo zimepokelewa na mtoto Neema Selemani kwa niaba ya wagonjwa wengine. Kutoka Kushoto ni Mkuu wa Jengo la watoto, NPC One,  Bi. Anna Mponeja na Katibu wa Tughe Tawi La Muhimbili, Bw. Faustine Fidelis.
   Mkuu wa Jengo la Watoto, NPC One, Bi. Anna Mponeja akimkabidhi Mkurugenzi wa Uuguzi katika hospitali hiyo, Bi. Agnes Mtawa zawadi maalamu.
   Bi. Anna Mponeja akimlisha keki mtoto Neema Seleman Leo katika hospitali hiyo.
  Ni wakati wa kufungua Champainge..Picha zote na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


  0 0

  Na Humphrey Shao, 
  Globu ya Jamii Morogoro
   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema kuwa licha ya nchi yetu kuwa na ardhi kubwa na yenye rutuba ya kutosha na hali ya hewa nzuri amesema serikali bado inachangamoto ya uwepo ya ardhi kidogo iliyopimwa na kupatiwa hati hali inayosababisha migogoro. 
  Amesema hayo kwa  waandishi wa habari leo mjini Morogoro wakati wa ufunguzi wa warsha ya kuhusu jukumu la vyombo vya habari katika kutoa elimu juu ya sheria ,kanuni na taratibu katika utawala wa ardhi ili kusaidia kutatua migogoro ya ardhi. 
  “Bado kuna changamoto kadhaa zinazotukabili changamoto hizo ni pamoja na kiasi kidogo kilichopimwa na kupatiwa hati hivyo kuleta migogoro inayohusu umiliki halali wa ardhi baina ya watumiaji mbalimbali wa ardhi” amesema Waziri Lukuvi. 
  Amesema uelewa duni wamatumizi bora ya ardhi kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi na ongezeko kubwa la ardhi kwa ajili ya kuendeleza makazi mijini pamoja na uvamizi wa ardhi katika maeneo yaliyohifadhiwa. 
  Amesema serikali ya Tanzania inakusudia kutumia fursa ya ukuaji wa uchumi kwa wastani wa asilimia 7 kwa mwaka kama ilivyoonekana katika miaka iliyopita katika kuhakikisha maendeleo yanakuwa endelevu na yenye usawa na fursa kwa wananchi wote. 
  Ameweka wazi kuwa miongoni mwa jitihada zinazoendelea katika kurasimisha sekta ya ardhi na kutekeleza program ya kuwezesha umilikishaji wa ardhi kwa majaribio ya miaka mitatu ambayo inalenga kuleta hati miliki katika wilaya za Kilombero, Ulanga na Malinyi katika mkoa wa Morogoro.
  Amesema pia program hii itawezesha kufanya mapitio na maboresho ya masula ya kisera, kisheria na kitasisi hili kuharakisha urasimkishaji wa sekta ya ardhi nchini.
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi, akizungumza wakati wa uzinduzi wa warsha hiyo mkoani morogoro.
  Sehemu ya washiriki wa warsha hiyo wakifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri lukuvi
  Washiriki wa warsha hiyo wakifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri Lukuvi

  0 0

  Wananchi  wa kijiji cha Muhuru wilayani Ruangwa wakifanya kila linalowezekana ili wamwone Mbunge wao, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kijijini hapo Desemba 28, 2016. 
  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Na Pascal Mayalla 
   Tanzania imeanza kutumia vizuri Mabilioni ya Taasisi ya TradeMark East Africa, kuwajengea uwezo wafanyabiashara wanawake wa Tanzania, kwa kugharimia mafunzo ya kuwajengea uwezo Wafanyabiashara Wanawake wa Tanzania, walio chini ya mwamvuli wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania , (Tanzania Women Chamber of Commerce, TWCC), ili kuweza kuvuka mipaka na kuwezesha bidhaa za Tanzania, kuyafikia masoko ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na hata nje ya bara la Afrika. 
   Akizungumzia kuanza kwa mafunzo hayo, Mkurugenzi wa TradeMark Tawi la Tanzania, Bw. John Ulanga, aliyewakilishwa na Program Manager wa TradeMark East Africa, Tawi la Tanzania, Bi Monica Hangi, amesema, mafunzo hayo ni sehemu ya utakelezaji wa mradi mkubwa wa Taasisi ya Trademark East Africa ujulikanao kama “Women in Trade” unaolenga kuwajengea uwezo wafanyabiashara wanawake wa Tanzania, kuhimili ushindani wa kibiashara na kukabiliana na vikwazo vya kibiashara kwa wafanyabiasha wanawake Tanzania kuwawezesha kufanya biashara ya kimataifa ikiwemo kuwezesha bidhaa zao kuyafikia masoko ya nchi za Afrika Mashariki na masoko ya kimataifa.
  Taasisi ya TradeMark imetenga Dola za Marekani Milioni 5,300,000 ambazo ni zaidi ya Shilingi Bilioni 12 za Kitanzania kugharimia mpango huo. Bi Hangi amesema, “Ukimuwezesha mwanamke, ni kuiwezesha familia nzima, familia zikiwezeshwa ni kuwezesha jamii nzima na jamii zikiwezeshwa na kuwezesha taifa kwa ujumla, hivyo uwezeshaji huo kwa wanawake ni uwezeshaji kwa taifa kupata maendeleo” 
   Program Manager wa TradeMark East Africa, Tawi la Tanzania, Bi Monica Hangi, akitunuku cheti cha kuhitimu mafunzo ya kuvuka mipaka, kwa mjasiliamali wa Mavazi, Bi. Daria Gwao Makaramba kwenye hafla fupi  ya kufunga mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kuvuka mipaka kwa wafanyabiashara wanawake  wa Tanzania yaliyoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC) ili kuwezesha bidhaa za Tanzania, kuyafikia masoko ya Afrika Mashariki . Mafunzo hayo, yameendeshwa taasisi ya mafunzo ya CABO Consult na kufadhiliwa na TradeMark East Africa.
   Program Manager wa TradeMark East Africa, Tawi la Tanzania, Bi Monica Hangi, akitunuku cheti cha kuhitimu mafunzo ya kuvuka mipaka, kwa mjasiliamali wa kusindika vyakula, Mwal. Rose Romanus kwenye hafla fupi  ya kufunga mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kuvuka mipaka kwa wafanyabiashara wanawake  wa Tanzania yaliyoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC) ili kuwezesha bidhaa za Tanzania, kuyafikia masoko ya Afrika Mashariki . Mafunzo hayo, yameendeshwa taasisi ya mafunzo ya CABO Consult na kufadhiliwa na TradeMark East Africa.
   Program Manager wa TradeMark East Africa, Tawi la Tanzania, Bi Monica Hangi, akitunuku cheti cha kuhitimu mafunzo ya kuvuka mipaka, kwa mjasiliamali kijana, Hadija Ahmed, kwenye hafla fupi  ya kufunga mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kuvuka mipaka kwa wafanyabiashara wanawake  wa Tanzania yaliyoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC) ili kuwezesha bidhaa za Tanzania, kuyafikia masoko ya Afrika Mashariki . Mafunzo hayo, yameendeshwa taasisi ya mafunzo ya CABO Consult na kufadhiliwa na TradeMark East Africa.
   Washiriki wa mafunzo ya kuvuka mipaka, kwenye hafla fupi  ya kufunga mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kuvuka mipaka kwa wafanyabiashara wanawake  wa Tanzania yaliyoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC) ili kuwezesha bidhaa za Tanzania, kuyafikia masoko ya Afrika Mashariki . Mafunzo hayo, yameendeshwa taasisi ya mafunzo ya CABO Consult na kufadhiliwa na TradeMark East Africa.
  Washiriki wa mafunzo ya kuvuka mipaka, kwenye picha ya pamoja na vyeti vyao baada ya kuhitimu mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kuvuka mipaka kwa wafanyabiashara wanawake  wa Tanzania yaliyoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC) ili kuwezesha bidhaa za Tanzania, kuyafikia masoko ya Afrika Mashariki . Mafunzo hayo, yameendeshwa taasisi ya mafunzo ya CABO Consult na kufadhiliwa na TradeMark East Africa.

  0 0

  Na Lulu Mussa

  Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora ameuagiza ungozi wa Dezo  Civil Constractors Co. Ltd kuhakikisha ujenzi wa Miundombinu ya maji taka katika Manispaa za Ilala na Temeke unakamilika kwa muda uliopangwa na kwa ubora wa hali ya juu kwa kuzingatia makubaliano yaliyopo katika mkataba.

  Akikagua ujenzi unaoendelea wa miundombinu hiyo, katika Wilaya ya Ilala eneo la Bungoni, Prof. Kamuzora amemtaka Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw. Palela Msongera kuhakikisha changamoto zinazojitokeza katika ujenzi huo zinatatuliwa mara moja ikiwa ni pamoja na utupaji wa taka maji na taka ngumu katika mfereji huo unaojengwa.

  Awali Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw. Palela Msongela alimueleza Katibu Mkuu kuhusu changamoto zinazohusu mazingira hususan uhaba wa miundombinu ya mifumo ya maji taka na ujenzi wa makazi holela unaosababisha udhibiti hafifu wa taka.

  Aidha, Prof. Kamuzora amewataka watendaji wa Manispaa ya Ilala kuwaelimisha wananchi juu ya athari zinazoweza kujitokeza kwa kutiririsha maji machafu kuwa ni pamoja na milipuko ya magonjwa hususan kipindupindu na kuhatarisha afya za wakazi hao.

  Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Buguruni Bw. Adam Fugame amemhakikishia Prof Kamuzora kuwa ataongea na wananchi katika Kata yake na kusisitiza matumizi sahihi ya sheria ndogondogo za mitaa walizojiwekea ikiwa ni pamoja na kuwatoza faini wananchi wanaokiuka taratibu hizo.

  “Nikuhakikishie, kwa kupitia mikutano na vikao na wananchi katika Kata yangu, tutazidi kusisitiza juu ya jambo hili na kuweka sheria kali zaidi kwa watakao kaidi”. Alisisitiza Mhe. Diwani Fugame

  Ujenzi huo wa  Ukuta wa (Obama/Ocean Road na Kigamboni) na Miundombinu ya maji taka katika Manispaa za Ilala na Temeke unatekelezwa chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais chini ya Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi. Mradi huu unafadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira (UNEP). Kampuni ya Dezo Civil Contractors ndio inafanya ujenzi huu na unatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni na kazi zinatarajiwa kukamilika mwezi Julai 2017.

    Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora (kulia) akimsikiliza Diwani wa Kata ya Buguruni Mhe.  Adam Fugame (Kushoto)  wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua ujenzi wa mfereji wa maji taka katika eneo la Ilala Bungoni, Jijini Dar es Salaam.

   Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw. Palela Msongela  (kushoto) akiongea na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora mara baada ya kukagua ujenzi unaoendelea katika mfereji wa kupitisha maji taka eneo la Ilala Bungoni

   Bw. Gervas wa Kampuni ya Dezo Civil Contractors Co. Ltd akifanunua jambo kwa Prof Kamuzora, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, katika eneo la Temeke ambapo Kampuni hiyo imepewa kazi ya kusafisha na kujenga mfumo wa maji taka. Katikati ni Bw. Motongori Chacha, Afisa Mazingira Manispaa ya Temeke.

   Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora (kushoto) akimsikiliza Bi. Ukende Mkumbo kutoka Taasisi ya Mwalimu Nyerere Kigamboni akifafanua hatua za ujenzi wa ukuta katika eneo lao. Katikati ni mwakilishi kutoka Kampuni ya Dezo Civil Contractors Co. Ltd

              Sehemu ya Ukuta wa barabara ya  Obama/Ocean Road jijini Dar es salaam ukarabati ukiendelea.(Picha na Habari na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Ofisi ya Makamu wa Rais.)  0 0

   Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania,Mosi Nasoro(kulia)akishuhudia Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo,Matina Nkurlu akiwaonesha waandishi wa habari(hawapo pichani)namba ya mmoja ya washindi kati ya 50 wa mtandao huo waliojishindia shilingi Milioni 1/-kila mmoja na 26 kujishindia shilingi laki 1 kila mmoja  wakati wa droo ya wiki ya tatu(3)ya Promosheni ya”Nogesha Upendo”jijini Dar es Salaam leo.Ili ushinde mteja anatakiwa kujiunga na kifurushi chochote cha mtandao wa Vodacom na kujishindia muda wa maongezi,Vifurushi vya intaneti pamoja na  fedha taslimu.
  Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kushoto)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa kuchezesha droo ya wiki ya tatu(3)ya Promosheni ya”Nogesha Upendo”jijini Dar es Salaam leo iliyowafanya wateja 50 wa mtandao huo kujishindia shilingi Milioni 1/-kila mmoja na 26 kujishindia shilingi laki 1 kila mmoja ili kushinda mteja anatakiwa kujiunga na kifurushi chochote cha mtandao wa Vodacom na kujishindia muda wa maongezi,Vifurushi vya intaneti pamoja na  fedha taslimu.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini,Godfrey Simbeye akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya ushiriki wa Sekta Binafsi na Sekta ya Umma leo Jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo(TCCIA), Gotfrid Muganda

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 
  Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (TPSF) imesema ni vigumu kwa nchi inayoendelea kama Tanzania kupata maendeleo pasipo kupata mitaji kutoka kwa wawekezaji wa nchi nyingine zenye mitaji.
  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo juu maoni ya TPSF, kuhusu umuhimu wa majadiliano kati ya sekta binafsi na sekta ya Umma katika kuleta mazingira wezeshi ya uwekezaji hapa nchini kwa mwaka 2016.
   Mkurugenzi Mkuu wa TPSF, Godfrey Simbeye amesema mitaji ikipatikana inaweza kuwekezwa katika maeneo mbalimbali na nchi ikaweza kupata maendeleo tunayoyataka hususani katika sekta ya Viwanda. Amesema serikali aanzishe utaratibu wa kila Wizara kuwa na kitengo kitachokuwa kinaratibu maboresho au mazingira ya biashara katika maeneo kazi yao.

  Simbeye amesema serikali imetenga fedha nyingi za maendeleo katika bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017 ili ziweze kutumika katika miundombinu ya barabara, reli, uboreshaji wa viwanja vya ndege, uboreshaji wa bandari, miradi ya umeme pamoja Kilimo cha umwagiliaji. Aidha amesema katika kuyafikia maendeleo hayo kunahitajika kuwepo kwa kamati ya kitaifa ya kusimamia maboresho ya mifumo ya usimamizi wa leseni kwa kuwa na wajumbe wa sekta binafsi na serikali.

  0 0

  Timu ya ya Soka ya Simba ya Jijini Dar es salaam imeendelea kujikita kileleni kwa tofauti ya alama nne baada ya Kuwabugiza Maafande wa Ruvu Shooting goli 1-0.

  Mpira ulianza kwa kasi kwa upande wa Simba kutaka kupata goli la mapema lakini jitihada za mlinda mlango na mabeki ziliweza kuzaa matunda.
  Mpaka kufika Dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza Simba wanaandika goli la kwanza kupitia kwa Mohamed Ibrahim baada ya kupokea pasi kutoka kwa Shiza Kichuya.

  Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa Ruvu Shooting kutaka kusawazisha lakini safu ya ushambuliaji ilikuwa butu na haikuweza kuzaa matunda.

  Kwa upande wa Simba bahati haikuwa yao baada ya kushindwa kutumia nafasi walizozipata ingawa walifanya mabadiliko.

  Mpaka dakika 90 za mwamuzi Alex Mahagi zinamalizika Simba wanatoka kifua mbele kwa ushindi wa goli 1-0.⁠⁠⁠⁠
  Mshambuliaji wa Timu ya Simba, James Kotei akiinchambua ngome ya Timu ya Ruvu Shooting, katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara duru la lala salama, uliopogwa jioni ya leo katika Uwanja wa kwenye Uwanja wa Uhuru, Jijini Dar es salaam. Simba imeshinda bao 1-0.
  Beki wa Timu ya Simba, Abdi Banda akiwania mpira wa juu huku akimdhibiti vilivyo Mshambuliaji wa Timu ya Ruvu Shooting, Full Maganga katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara duru la lala salama, uliopogwa jioni ya leo katika Uwanja wa kwenye Uwanja wa Uhuru, Jijini Dar es salaam. Simba imeshinda bao 1-0.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0

  Iddi Cheche (kushoto) sasa ndiye atakaimu ukocha wa Azam wakati timu ikitafuta kocha mwingine.

  Kwa hisani ya Bin Zubeiry
  AZAM FC imetangaza rasmi kuachana na makocha wake kutoka Hispania chini ya Zeben Hernandez Rodriguez leo na kwamba kocha wa vijana, Iddi Nassor 'Cheche' ataiongoza timu kwa muda akisaidiwa na Iddi Abubakar. 
  Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba amesema leo kwamba kwamba wamefikia makubaliano na makocha hao kutoka Hispania kuvunja mikataba. 
  Jopo hilo la makocha linaundwa na Kocha Mkuu Zeben Hernandez, Msaidizi wake, Yeray Romero, Kocha wa Makipa Jose Garcia, Kocha wa Viungo, Pablo Borges na Mtaalamu wa tiba za Viungo, Sergio Perez. 
   Kawemba amesema kwamba uamuzi huo umefikiwa na Bodi ya Wakurugenzi wa timu hiyo jana, na umetokana na mwenendo mbaya wa Azam FC kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ambayo imefikia raundi ya pili hivi sasa. 
  "Azam FC inawatakia kila la kheri na mafanikio mema makocha hao huko waendako na inawashukuru kwa mchango wao wote walioutoa kwenye timu kwa kipindi chote walichokaa, ikiwemo kuwapa taji la kwanza la Ngao ya Jamii mwaka huu kwa kuifunga Yanga kwa mikwaju ya penalti 4-1 kufuatia sare ya mabao 2-2,"amesema Kawemba. 
  Amesema wakati uongozi ukiwa katika mchakato wa kusaka kocha mpya, kikosi hicho kitakuwa chini ya makocha wa timu ya vijana ya timu hiyo, Idd Cheche na Kocha wa Makipa, Idd Abubakar, ambao walianza kazi jana jioni kukiandaa kikosi kuelekea mchezo wa leo dhidi ya Tanzania Prisons. 
  "Azam FC inapenda kuwaambia mashabiki wake kuwa wawe watulivu katika kipindi hiki kwani uongozi umefanya uamuzi sahihi kwa ajili ya kuinyanyua timu juu ili hatimaye ushiriki wetu wa michuano mbalimbali uweze kuwa ni wa kiwango cha juu tofauti na hali ilivyokuwa sasa," amesema Kawemba. 
  Hernandez anaondoka Azam FC akiwa ameingoza timu hiyo kwenye mechi 18 rasmi ambazo ni za mashindano, 17 za ligi na moja ya Ngao ya Jamii, amefanikiwa kushinda mechi nane, sare sita na kufungwa mara nne.

  0 0

  Leo Disemba 29, 2016 ni siku ya furaha kwa ndugu, jamaa na marafiki wa kijana Jackson John Binagi, wa Kenyamanyori Tarime mkoani Mara (wa tatu kushoto),aliyefunga ndoa na Bi.Monica Syaga wa Mogabiri Tarime, Mara.
  Maharusi na wapambe wao, pamoja na ndugu, jamaa na marafiki
  Maharusi na wapambe wao
  Maharusi katika ubora wao
  Wazazi wa bibi harusi wakiongozwa na baba, wakimpa baraka bibi harusi
  Ni furaha kwa ndugu, jamaa na marafiki kucheza ngoma ya asili ya Kikurya (Ritungu) kwenye harusi hiyo. TAZAMA PICHA ZAIDI HAPA

  0 0

   Na Baraka Chibiriti
  Barabara yetu mpya yaanza ajali, gari ndogo limeparamia  kwenye lori, na kusababisha lori kuchochora nje ya barabara maeneo ya Msalato, nje kidogo ya mji wa Dodoma hii leo. Wa gari ndogo ameumia sana na kukimbizwa hospitali ya Mkoa wa Dodoma. Inasemekana ni Gwamaka Bukuku ambaye ni kaka yake  na Marehemu Mpoki Bukuku ambaye amezikwa juzi tu, nyumbani kwao Msalato - Dodoma. 
   Gari dogo lililoparamia lori 
  Majeruhi akiopolewa kabla ya kukimbizwa hospitali
   Lori lililohusika na ajali hiyo
   Eneo la tukio
  Majeruhi baada ya kupata matibabu hospitali ya mkoa Dodoma. Hali yake inaendelea vyema ingawa ana maumivu makali baada ya kuvunjika mkono wa kuume na mguu wa upande huo umeumia sana. Pia ana maumivu makali kiunoni.

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
  MBUNGE wa Mkuranga Mhe.  Abdallah Ulega amefanya ziara katika vijiji vya Kisayani na Msorwa ili kujua changamoto mbalimbali zinazowakabiliwa wananchi na kuweza kuzishughulikia kupitia Halmashauri pamoja Ofisi yake.
  Akizungumza na wananchi waVijiji hivyo amesema wakati wa sasa ni kufanya wa maendeleo ya kweli bila kuangalia itikadi za vyama.
  Amesema kwa kutambua umuhimu wananchi kuwa watu wako katika mapumziko ya sikukuu za mwisho wa mwaka lakini ameona bora kutembelea wananchi waliompigia kura. Ulega amesema Mkuranga inahitaji maendeleo kutokana na kukaa muda mrefu bila kuwa na mabadiliko ya wananchi katika huduma za jamii kutokana na viongozi
  Amesema kazi yake ni kuhamasisha wananchi katika masuala ya maendeleo pamoja na kupokea na kusikiliza kero na changamoto mbalimbali za wanachi wa vijiji hivyo katika ziara hiyo, amepokea changamoto mbalimbali ikiwemo ubovu wa miundominu ya barabara, Afya,Elimu, Umeme pamoja na Maji ambapo amewahakikishia wananchi hao kuzishughulikia changamoto hizo zinazo wakabili ili kuchochea maendeleo ya vijiji hivyo.
  Ulega amesema ameweza kufanya ziara katika vijiji 90 kati ya vijiji 125 katika Jimbo la Mkuranga ambapo kati ya vijiji hivyo asilimia 50 changamoto zimetatuliwa.
   Mbunge wa Mkuranga, Mhe. Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kisayani alipokwenda kuwatembelea pamoja na kuangalia maendeleo ya kijiji hicho leo 
  Sehemu ya wananchi wa kijiji cha Kisiyani wakimsikiliza  Mbunge wa Mkuranga , Abdallah Ulega 
   Diwani wa Kata ya Mbezi, Mkuranga, Rashid Selungwi akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Msorwa katika ziara ya Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega leo.
   Mkazi wa Kijiji cha Kisiyani Kata ya Mbezi, Joel Kianga akichangia mada katika ziara ya Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega leo.
  0 0

  Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa

  *Asema wanaotaka fedha wataipata shambani

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wakazi wa Ruangwa na mkoa mzima wa Lindi wachangamkie fursa ya kulima mihogo na alizeti kwa sababu mazao hayo yana uhakika wa soko.

  Alitoa wito huo wakati akizungumza na wananchi wa vijiji mbalimbali vya wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi ambako anapita kuwasalimia wananchi wa jimbo lake na kuhimiza kazi za maendeleo. Waziri Mkuu yuko Ruangwa kwa siku nne kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka.

  “Nimekuja na fedha, wangapi wanataka kupata fedha?” alihoji Waziri Mkuu katika mikutano yake na kuitikiwa “Sisi” na umati wa watu walionyoosha mikono juu kuonesha kuwa wako tayari kupokea fedha hizo. Mikutano hiyo ilifanyika kwenye vijiji vya Namilema, Mbuyuni, Nandandara, Namkonjera, Muhuru, Chikundi, Chibula na Matumbu.

  “Mnataka fedha siyo? Fedha iko shambani! Nimewaletea fursa ya mwekezaji anayetaka kununua mihogo yote katika mkoa huu,” alisema Waziri Mkuu na kusababisha kicheko kwa watu waliokuwa wakinyoosha mikono yao.

  “Limeni mtu mmoja mmoja au jiungeni kwenye vikundi ili mpate ekari tatu hadi nne kwa sababu mna uhakika wa soko. Mwekezaji huyu anataka kununua mihogo yote na ya wilaya hii peke yake haitoshi kiasi ambacho anataka. Kwa hiyo tumekubaliana na wabunge wenzangu kwamba kiwanda hiki kitajengwa Nanjilinji ambako ni katikati ya mkoa ili iwe rahisi kusomba na kupeleka mazao hayo,” alisema.

  Waziri Mkuu alisema eneo la Nanjilinji lililoko wilayani Kilwa, linafikiwa kwa urahisi na wakazi wote kutoka Kilwa, Nachingwea, Ruangwa, Lindi Vijijini na Liwale.

  Akifafanua zaidi, alisema mwekezaji aliyepatikana (bado ni mapema kumtaja) yuko tayari kufuata mazao waliko wakulima na atakuwa akiwalipa hukohuko. “Yeye anachotaka ni mihogo ya kutosha, ndiyo maana nawasisitizia muanze kulima zao hili kwa wingi cha msingi mfuate kanuni bora za kilimo,” aliongeza.

  Wakati huohuo, Waziri Mkuu amewataka wakazi hao walime zao la alizeti kwa wingi kwa sababu amekwishapatikana mwekezaji wa kununua zao hilo na kwa bei nzuri.

  “Nilipokwenda Singida nilikutana na mmiliki mmoja wa kiwanda cha kusindika mafuta ya alizeti akasema anahitaji kununua zao hilo kwa wingi kwa sababu inayozalishwa kule haitoshi. Ameshakuja hapa na kuangalia ardhi ya hapa amesema inafaa kwa zao hilo,” alisema.

  “Yeye atawaletea mbegu na kila ekari moja inahitaji kilo tano. Ukivuna kila ekari unapata magunia 20 na kila gunia lina uwezo wa kutoa lita 20. Bei ya dumu mojala lita 20 ni sh. 60,000 kwa hiyo katika ekari yako moja una uhakika wa kupata sh. milioni 1.2. Hata ukitoa gharama ya kulima na palizi, bado huwezi kukosa walau sh. milioni moja kwa kila ekari.”

  Alimwagiza Mkuu wa Idara ya Kilimo (Umwagiliaji na Ushirika) wa wilaya hiyo, Bi. Violeth Byanjweli afanye kazi ya kuratibu ni wakazi wangapi wana mashamba ya alizeti na wangapi wako tayari kuanzisha kilimo hicho ili mbegu zitakapoletwa iwe ni rahisi kuwasambazia huko waliko.

  “Hiki kilimo ni cha miezi mitatu tu na palizi yake ni mara moja tu. Kwa hiyo mvua za Januari zikianza, changamkieni hiyo fursa na baada ya miezi mitatu kila mtu atakuwa na hela yake badala ya kusubiria korosho ambazo mnavuna mara moja kwa mwaka,” alisisitiza.

                              
  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  ALHAMISI, DESEMBA 29, 2016.

  0 0


  Na Lulu Mussa

  Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora ameuagiza ungozi wa Dezo Civil Constractors Co. Ltd kuhakikisha ujenzi wa Miundombinu ya maji taka katika Manispaa za Ilala na Temeke unakamilika kwa muda uliopangwa na kwa ubora wa hali ya juu kwa kuzingatia makubaliano yaliyopo katika mkataba.

  Akikagua ujenzi unaoendelea wa miundombinu hiyo, katika Wilaya ya Ilala eneo la Bungoni, Prof. Kamuzora amemtaka Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw. Palela Msongera kuhakikisha changamoto zinazojitokeza katika ujenzi huo zinatatuliwa mara moja ikiwa ni pamoja na utupaji wa taka maji na taka ngumu katika mfereji huo unaojengwa.

  Awali Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw. Palela Msongela alimueleza Katibu Mkuu kuhusu changamoto zinazohusu mazingira hususan uhaba wa miundombinu ya mifumo ya maji taka na ujenzi wa makazi holela unaosababisha udhibiti hafifu wa taka.

  Aidha, Prof. Kamuzora amewataka watendaji wa Manispaa ya Ilala kuwaelimisha wananchi juu ya athari zinazoweza kujitokeza kwa kutiririsha maji machafu kuwa ni pamoja na milipuko ya magonjwa hususan kipindupindu na kuhatarisha afya za wakazi hao.

  Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Buguruni Bw. Adam Fugame amemhakikishia Prof Kamuzora kuwa ataongea na wananchi katika Kata yake na kusisitiza matumizi sahihi ya sheria ndogondogo za mitaa walizojiwekea ikiwa ni pamoja na kuwatoza faini wananchi wanaokiuka taratibu hizo.

  “Nikuhakikishie, kwa kupitia mikutano na vikao na wananchi katika Kata yangu, tutazidi kusisitiza juu ya jambo hili na kuweka sheria kali zaidi kwa watakao kaidi”. Alisisitiza Mhe. Diwani Fugame

  Ujenzi huo wa Ukuta wa (Obama/Ocean Road na Kigamboni) na Miundombinu ya maji taka katika Manispaa za Ilala na Temeke unatekelezwa chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais chini ya Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi. Mradi huu unafadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira (UNEP). Kampuni ya Dezo Civil Contractors ndio inafanya ujenzi huu na unatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni na kazi zinatarajiwa kukamilika mwezi Julai 2017.

  (Picha na Habari na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Ofisi ya Makamu wa Rais.)
  Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora (kulia) akimsikiliza Diwani wa Kata ya Buguruni Mhe. Adam Fugame (Kushoto) wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua ujenzi wa mfereji wa maji taka katika eneo la Ilala Bungoni, Jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw. Palela Msongela (kushoto) akiongea na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora mara baada ya kukagua ujenzi unaoendelea katika mfereji wa kupitisha maji taka eneo la Ilala Bungoni.
  Gervas wa Kampuni ya Dezo Civil Contractors Co. Ltd akifanunua jambo kwa Prof Kamuzora, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, katika eneo la Temeke ambapo Kampuni hiyo imepewa kazi ya kusafisha na kujenga mfumo wa maji taka. Katikati ni Bw. Motongori Chacha, Afisa Mazingira Manispaa ya Temeke.
  Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora (kushoto) akimsikiliza Bi. Ukende Mkumbo kutoka Taasisi ya Mwalimu Nyerere Kigamboni akifafanua hatua za ujenzi wa ukuta katika eneo lao. Katikati ni mwakilishi kutoka Kampuni ya Dezo Civil Contractors Co. Lt
  Sehemu ya Ukuta wa Obama/Ocean Road ukarabati ukiendelea

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
  WAKALA wa Vipimo (WMA) inatarajia kuweka Sticker katika vipimo mbalimbali ili kuweza kumlinda mlaji kwa huduma inayoendana na thamani fedha yake.

  Akizungumza na waandishi wa habari  leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Meneja Sehemu ya Elimu , Habari na Mawasiliano, Irene John amesema uwekaji Sticker utaanza rasmi mwaka ujao kwa kubandika sticker hiyo kwa kila kipimo ambacho kinatambulika na Wakala Vipimo. Amesema sticker hizo zitawekwa katika pampu zinazotumika katika vituo vya vya mafuta ambavyo vitakuwa vimehakikiwa ili mteja ajue uhalali wa kipimo hicho na mafuta.

  Irene amesema mlaji akiona sticker katika kituo cha mafuta afahamu kituo hicho kimehakikiwa na wakala wa vipimo. Amesema katika uwekaji wa sticker huo ni pamoja bohari za Mafuta kwa kuweka sticker maalumu katika kipimo cha mafuta 'flow Meters' zitakazotumika kujaza mafuta katika magari ya kubebea mafuta itafanya wabebaji wa mafuta kwa magari wataweza kutambua kipimo hicho kilivyohakikiwa.

  Hata hivyo amesema katika jitihada hizo hufanya uhakiki wa mizani yote kuhakikisha inapima kwa usahihi ikiwa ni pamoja na kuweka sticker maalumu. Irene amesema mizani yote inayotumiwa na wafanyabiashara itahakikiwa ili kujua usahihi wake na uhakiki wake utakuwa ni kugonga mhuri na kuweka sticker.

  Amesema mazao yote watahakiki mizani ya wafanyabiashara na mizani ambayo itakuwa haina sticker wakulima wasitumie na wanatakiwa kutoa taarifa.
  Kaimu Meneja sehemu ya Elimu, Habari na Mawasiliano wa Wakala wa Vipimo, Irene John akizungumza na waandishi wa habari juu ya Uwekaji wa Sticker mpya zitazoanza kutumika mwakani. 


  Mkurugenzi wa Ufundi Bi. Stella Kahwa akionyesha kwa Waandishi wa Habari Sticker zitakazoanza kutumika hapo mwakani

  0 0

  Dereva boda boda Kasian Haule ambaye
  alimpakia Denis Komba na nyoka wake.

  Tukio lililozua taharuki kwa wakazi wa mji wa Songea mkoani Ruvuma na kupewa nafasi kubwa katika vyombo vya habari vya Tanzania na nje ya Tanzania pamoja na mitandao ya kijamii, huku likiacha gumzo midomoni mwa watu, kuhusiana na kifo cha DENIS KOMBA kufariki dunia baada ya nyoka wake aliyekuwa anasadikiwa kummiliki, kuuawa na wananchi DESEMBA 26 MWAKA HUU, majira ya saa 4 na nusu usiku , katika maeneo ya hospital ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma. Ruvuma TV imezungumza na KASIANI HAULE, ambaye ndiye dereva boda boda  aliyekuwa kakodiwa na marehe DENISI KOMBA Bonyeza hiyo Video upate ukweli wa tukio.


  0 0


older | 1 | .... | 1481 | 1482 | (Page 1483) | 1484 | 1485 | .... | 3278 | newer