Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live

Waigama, Matinyi, Kiboko waelezea maana ya Kichuri

$
0
0
 Mubelwa Bandio wa Changamoto Yetu Blog akifanya mahojiano na Mwenyekiti wa kamati ya Kichuri Day Bwn. Waigama siku ya Jumamosi May 25, 2013 Ellicott City, Marylnd.
 Mubelwa Bandio akifanya mahojiano na Kiboko (T-shirt nyekundu) na Mobhare Matinyi.
Wakurya wakicheza Ritungu

Wakurya waishio maeneo ya Washington DC na vitongozi vyake, jumamosi ya Mei 25 mwaka huu walikutana na kwa mara ya kwanza ya kujuana, kujadiliana kuhusu kabila lao na pia kula chakula cha kikwao.

Katika siku hiyo waliyoiita Kichuri Day, kulikuwa na mambo mengi yaliyoakisi maisha yao ya nyumbani Tanzania ikiwemo chakula, muziki wa kikwao n.

Mubelwa Bandio anayo taarifa kamili; bofya mshale hapo...

Article 5

kinana na ujumbe wake wa ccm awasili mkoani njombe leo,kufanya ziara ya siku saba mkoani humo, awaonya wanaojipitishapitisha kutaka urais

$
0
0
NA BASHIIR NKOROMO, IRINGA 
 KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana amesisitiza kwamba Chama kitamwadhibu bila huruma mwanachama yeyote anayejipitisha-pitisha katika maeneo mbalimbali na kufanya kampeni za kuwania urais kabla ya wakati.
 Kinana alisema hayo leo wakati akizungumza na Kamati ya Siasa na mkoa wa Iringa, katika kikao maalum, kilichofanyika kabla ya kwenda mkoani Njombe ambako ameanza ziara ya siku saba mkoani humo. 
 Kinana alisema, katazo la wanachama kujipitisha-pitisha na kupiga kampeni za kuwania urais au nafasi yoyote kabla ya muda halitoki midomoni mwa viongozi bali ni kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Chama. "Ndugu zanguni, nawakumbusha kwamba kwa hili hatuna mzaha nalo, hivyo hakikisheni kila mmoja wenu kama kiongozi hajihusishi kwa namna yoyote kushiriki katika kutumiwa na wanachama hao wanaojipitishajiptisha", alisema Kinana na kuongeza; 
 "Ni lazima Chama kiwe kikali kwenye jambo hili, kwa sababu kama kitawaacha watu hawa kukiuka taratibu na kanunzi za Chama wanazidi kukifanya chama kuwa na makundi mengi ambayo yatakipeleka pabaya," alisema Kinana Kinana alisema, kazi walioyonayo wale wote wanaokitakia mema Chama, ni kumuunga mkono Mwenyekiti, Rais Jakaya katika kazi ya kuhakikisha CCM inakamilisha utekelezaji ilani yake ya Uchaguzi kwa kiwango kinachostahili na siyo muda kujipitisha pitisha mtu binaafsi kwa wanachama huku utekelezaji wa ilani ukisinzia. 
 Alisema kuwa hivi sasa kazi ya CCM ni kuhakikisha inatekeleza ilani ya uchaguzi kwa kipindi kilichobaki cha miaka miwili ya nusu kabla ya kumalizi kwa awamu ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete.
 "Ni wazi kazi yatu CCM ni kuhakikisha tunatekeleza ilani ya uchaguzi kwa vitendo na si mamneno kama wanavyofanya wengine. ni kazi kubwa imefanyika chini ya uongozi wa Rais Kikwete na katika kipindi cha miaka miwili iliyobaki tumedhamiria kuifanya zaidi"
Alisema moja ya maeneo ambayo licha ya kuwepo changamoto za hapa na pele lakini yamefanikisha sana utekelezaji wa ilani ya CCM, ni kwenye Halmashauri mbalimbali nchini ambapo watendaji walio wengi wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kasi. 
 "Kwa kweli CCM lazima hawa tuwapongeze maana kuna wengine kazi yao imebaki kuwashambulia huku wakijua watendaji hao hawana fursa ya kujitete mbele ya jamii. chapeni kazi nasi tupo nyuma yenu, na kila wakati tutakuwa tukitambua juhudi na kazi kubwa mnayoifanya kwa jamii," alisema Kinana. 
 Akizungumzia uchaguzi mdogo wa madini unaofanyika katika kata mbalimbali nchini Kinana, alisema CCM itashinda uchaguzi huo kwenye kata zote 25 kutokana na mtandao wa chama chake na imani inayoonekana kuwepo kwa wananchi juu ya CCM.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akilakiwa na Mbunge wa Njombe Kaskazini,Mh Deo Sanga a.k.a Jah People mara baada ya kuwasili jioni ya leo mpakani mwa Mkoa wa Iringa na Njombe katika kijiji cha Idofi,kata ya Mlowa,ambapo pia alipokelewa na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Njombe akitokea Mkoani Iringa ambaka aliwasili leo Asubuhi akitokea jijini Dar akiwa ameambatana na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Ndugu Nape Nnauye.

Ndugu Kinana na ujumbe wake watakuwa na ziara ya siku saba mkoani Njombe ambapo watatembele Wilaya zote za Njombe,Makete, Ludewa na Wanging'ombe  wakiimarisha chama na kusikiliza matatizo ya Wananchi,huku wakikagua miradi ya maendeleo mbalimbali katika kusimamia serikali ili kutekeleza Ilani uchaguzi ya CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akivalishwa skafu .
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Ludewa,Mh.Deo Filikunjombe,kushoto shati la drafti ni Mbunge wa jimbo la Mwibara,Mh Kange Rugora


Pichani kulia ni Mjumbe wa kamati kuu na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Njombe,Pindi Chana akicheza na akina mama wakati wa mapokezi ya katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana 
 Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Ndugu Nape Nnauye  akishirikiana na  mmoja wa wapiga ngoma za asili wakati walipowasili leo mapema mchana wakiongozwa na  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana
 Ndugu Kinana na ujumbe wake wakipokelewa kwa shangwe mapema jionu ya leo,mpakani mwa Mkoa wa Iringa na Njombe katika kijiji cha Idofi,kata ya Mlowa,ambapo pia alipokelewa na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Njombe akitokea Mkoani Iringa ambaka aliwasili leo Asubuhi akitokea jijini Dar akiwa ameambatana na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Ndugu Nape Nnauye .
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akitazama moja ya kikundi cha ngoma kilichofika kumlaki,mara baada ya kuwasili jioni ya leo mpakani mwa Mkoa wa Iringa na Njombe katika kijiji cha Idofi,kata ya Mlowa,ambapo pia alipokelewa na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Njombe akitokea Mkoani Iringa ambaka aliwasili leo Asubuhi akitokea jijini Dar akiwa ameambatana na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Ndugu Nape Nnauye.

Ndugu Kinana na ujumbe wake watakuwa na ziara ya siku saba mkoani Njombe ambapo watatembele Wilaya zote za Njombe,Makete, Ludewa na Wanging'ombe  wakiimarisha chama na kusikiliza matatizo ya Wananchi,huku wakikagua miradi ya maendeleo mbalimbali katika kusimamia serikali ili kutekeleza Ilani uchaguzi ya CCM.

adakwa akiiba nyaya za mkongo wa taifa

$
0
0
Mwizi wa mkongo wa mawasiliano amekamatwa akiwa na vipande vya mkongo maeneo ya boko darajani jijini Dar es salaam. Matukio kama haya yamekuwa ni vipingamizi katika kutoa huduma bora kwa wateja wetu.Kutokana na hali hiyo, sisi kama wadau wa mawasiliano, tunapenda kuwaasa Watanzania kwa ujumla, kama kweli tuna uzalendo wa kweli na mapenzi ya dhati na kampuni yetu ya mawasiliano inabidi  kujitoa zaidi katika kufanikisha usalama wa miundombinu ya kampuni yetu. Kwa matukio yeyote kama haya naomba msisite kutoa taarifa polisi au toa taarifa kwa namba zifuatazo:- 0737206622 , 07372066230737206624 ,07372066250737206626.

MSEMAJI
OFISI ZA MKONGO WA TAIFA

makamu wa pili wa rais wa zanzibar ziarani pemba

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesisitiza umuhimu wa wakulima wa mashamba ya Mikarafuu kukubali kuzingatia ushauri unaotolewa na wataalamu wa Kilimo hicho ili kujenga nguvu za uzalishaji wa uhakika wa zao Karafuu Nchini. 
 Balozi Seif alitoa sisitizo hilo wakati wa ziara yake ya kukagua baadhi ya Mashamba ya Serikali ya Miti ya Mikarafuu ambayo yako chini ya usimamizi wa baadhi ya wakulima ndani ya Mkoa wa Kusini Pemba. Alisema bado ipo dhana kwa baadhi ya wakulima wa Mikarafuu kujilimbikizia miti mingi ya zao hilo wakiwa na mawazo na fikra za kupata uzalishaji mkubwa zaidi jambo ambalo ni ndodo Kitaalamu. 
 Balozi Seif ambae amekuwa na utaratibu wa kutembelea mara kwa mara mashamba ya Mikarafuu hasa Kisiwani Pemba alieleza kwa kuwa Serikali Kuu inaendelea na Mikakati ya kuimarisha zao hilo Wananchi pamoja na Wakulima wa Kilimo hicho wanapaswa kuunga mkono juhudi hizo za Serikali.
 “ Hivi sasa tunapaswa kuwa makini katika uzalishaji wa zao la Karafuu kitaalamu kwani wakati wa kuvuna karafuu mpeta umepitwa na wakati kulingana na mazingira yaliyopo ya soko la Dunia “ Alisisitiza Balozi Seif. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza wakulima Abdulla Masoud Abdulla wa Kijiji cha Shungi na Mkulima Ali Othman Ali wa Kijiji cha Minazini kwa uamuzi wao wa kujikubalisha kuyahuisha mashamba ya Mikarafuu ya Serikali yaliyomo katika maeneo yao. 
 Balozi Seif alisema juhudi hizo zimeleta faraja kwa Serikali na kuwaahidi kwamba wao ndio wanaostahiki kupewa upendeleo wa kukodishwa wakati unapofikia msimu wa zao la karafuu. Naye Mkulima Ali Othman Ali wa Kijiji cha Minazini alimueleza Balozi Seif kwamba shamba hilo la Serikali lilikuwa pori tupu kwa muda mrefu na kulazimika kuliomba kulihuisha kutoka kwa Taasisi husika ili kulirejesha katika hali yake. 
 Mkulima Ali Othman alifahamisha kwamba alilazimika kutumia nguvu za ziada katika kulihuisha shamba hilo lenye ukubwa unaokadiriwa kufikia ukubwa wa Eka moja.
 Alisema hatua hiyo hivi sasa imempa faraja kwa vile tayari mazao ya Mihogo na Migomba aliyoiotesha ndani ya miti ya Mikarafuu iliyomo ndani ya shamba hilo imeanza kumpatia faida cha chakula sambamba na fedha za kujikimu kwa mambo mengine ya maisha. Naye Mkulima Abdulla Masoud Abdulla wa Kijiji cha Shungi amemuahidi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuzingatia ushauri wa wataalamu katika harakati za kuendesha kilimo hicho.  
Othman khamis Ame
 Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar 
 27/5/2013.
Shamba la Mikarafuu la Serikali lililo chini ya uangalizi wa Mkulima Ali Othman Ali wa Kijiji cha Minazini Wilaya ya Mkoani ambalo liko katika hali nzuri ya kupendeza baada ya kuhuishwa kwake.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisisitiza Umuhimu wa Mashamba ya Mikarafuu kulimwa kwa Kitaalamu ili kukidhi mahitaji halisi ya soko la Kimataifa.
Mkamu Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifurahia mazingira bora ya baadhi ya mashamba ya Serikali ambayo yamekuwa yakihuishwa na baadhi ya wakulima katika maeneo mbali mbali ya Kisiwa cha Pemba.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

KADA wa CCM Mustapha Jaffer Sabodo asaidia upatikanaji wa visima korogwe

$
0
0
Na Mashaka Mhando, Korogwe

KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mustapha Jaffer Sabodo ameipatia wilaya ya Korogwe visima vitatu vitakavyogharimu kiasi cha shilingi milioni 60 ambavyo vitachimbwa katika maeneo ya Korogwe Mjini na Korogwe Vijijini. 
 Akizungumza na waandishi wa habari mjini Korogwe juzi Sabodo ambaye hadi kufikia jana tayari amechimba visima 245 katika maeneo mbalimbali nchini, atachimba visima hivyo kupitia taasisi yake mpya ya Sabodo Water Wells Faundition inayoongozwa na mwenyekiti wake Profesa Mark Mwandosya.
 Alisema ameamua kuisadia wilaya ya Korogwe kutokana na adhima yake aliyoiweka ya kusaidia jamii ya Watanzania nchini kutokana na suala la maji kuwa kero katika maeneo mengi hivyo kusaidiana na serikali katika kutatua kero hiyo. 
 "Nitatoa visima vitatu viwili katika jimbo la Profesa Majimarefu na kimoja nimepa Mama mary Chatanda Korogwe mjini, lakini vingine 15 nitawachimbia mwenzi Desemba mwaka huu, vitano Korogwe mjini na kumi korogwe vijijini," alisema Sabodo. 
 Akizungumza katika eneo la Kwasemangube ambalo litachimbwa kisima kimoja, Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani 'almaarufu Profesa Majimarefu, alimshukuru Sabodo kwa msaada wake wa kusaidia visima hivyo ambavyo vitaondopa kero ya maji katika maeneo ambayo vitachimbwa. 
 Alisema katika visima viwili atakavyowapa Sabodo, kimoja kitachimbwa katika Kijiji cha Magamba kwalukonge na kingine kitachimbwa katika kijiji cha Kijango kilichopo kata ya Magoma ambako kumekuwepo na tatizo la maji kwa muda mrefu. 
 Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo, aliyeongozana na Wakurugenzi wa mji Lewis kalinjuna wa Korogwe Vijijini Lucas Mweri wakati wakimuonesdha eneo litakalochimbwa kisima katika kijiji cha Kwasemangube, alisema walimfuata Sabodo kuomba msaada wa visima kutatua kero ya maji katika maeneo ya wilaya hiyo. 
 "Tulimfuata sabodo nikiwa na Mbunge wa Korogwe Vijijini, Mbunge wa viti Maalumu mkoa wa Tanga Mary Chatanda ambaye alimuomba visima hivyo ili kusaidia katika jimbo la Korogwe mjini kama unavyojua mama Chatanda, anaishi Korogwe mjini," alisema Gambo.
 Viongozi mbalimbali wa wilaya ya Korogwe wakizungumza na Sabodo kuhusu ufadhili wa visima katika wilaya ya Korogwe tukio lililofanyika jana kwenye hoteli ya White house mjini Korogwe. (picha na mashaka Mhando).

Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo (Kushoto) akiwa na Kada wa CCM Mustapha Jaffer Sabodo wakati wakizungumza kuhusu ufadhili wa visima katika wilaya ya Korogwe.

wadhamini wazidi kujitokeza Matembezi ya Hisani ya ‘Barclays Step Ahead’

$
0
0
Meneja wa Mawasiliano na Huduma za Jamii wa Benki ya Barclays Tanzania, Tunu Kavishe (kushoto) akizungumza na waandishi wakati wa kutangaza wadhamini wa Matembezi ya Hisani ya ‘Step Ahead’ ambayo yamelenga kukusanya fedha kwaajili ya kusaidia afya ya mama na mtoto na yanataraji kufanyika Juni 8 mwaka huu jijini Dar es salaam. Pamoja na ni Meneja masoko wa benki hiyo, Sara Munema.(Picha na Mpigapicha wetu).

===============    ==============    =============

Every year, Barclays Bank Tanzania organises a fund-raising walk christened ‘Step-Ahead’. Barclays Tanzania held its first Step-Ahead event in the year 2008 through which funds were raised and donated towards cancer treatment for children at the Ocean Road Cancer Institute (ORCI). Introduced globally in 2004, Step-Ahead is a signature Barclays initiative which aims to create awareness and resources in support of community needs.

Speaking at the press conference today, Ms. Tunu Kavishe, the Barclays Tanzania Communications and Community Investment Manager said “Barclays Bank takes its Citizenship role seriously and recognizes it as one of our key business deliverables. Taking on maternal and infant health as our flagship cause in Tanzania springs from our need to play a role in addressing the march towards achieving the 2015 MDG goals on maternal and infant health.

We are pleased that our partners CCBRT and AMREF have joined us once again in this initiative. This exciting event will be held on the 8th June, 2013 at the Golden Tulip Hotel and will include a 5km walk in which all members of the public are invited to participate. Step Ahead Walk 2013 welcomes the support of all partners and the community at large.

Today we are pleased to announce our sponsors for this year’s Event and these are Montage Ltd, ITV/Radio One and Capital TV, Clouds Media Group, Cocacola, Golden Tulip, Mwananchi Communications, Serena Hotels and Ultimate Security she added…

The funds raised will go towards supporting the Capacity building for midwives, Fistula treatment and Reconstructive surgery for children born with correctible birth defects

Tickets cost Tshs 5,000/- each and will be available at any Barclays Bank branch, Montage Limited offices – Ada Estate, Golden Tulip, Serena Hotels and Slipways

Uhuru Marathon 2013 Yafungua Milango kwa Wadhamini

$
0
0
Katibu mkuu wa chama cha Riadha Taifa,Suleyman Nyambui (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza kufunguliwa rasmi milango kwa makampuni, mashirika na taasisi mbalimbali zitakazopenda kudhamini mbio za Uhuru Marathon ambazo ni za aina yake nchini zitakazokuwa zikifanyika kila mwezi Desemba zikiambatana na maadhimisho ya sherehe za Uhuru wa Tanzania.Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Intellectuals Ltd ambao ndio Waratibu wa Mbio hizo,Innocent Melleck.
Mkurugenzi Mkuu wa Intellectuals Ltd ambao ndio Waratibu wa Mbio hizo,Innocent Melleck akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza kufunguliwa rasmi milango kwa makampuni, mashirika na taasisi mbalimbali zitakazopenda kudhamini mbio za Uhuru Marathon ambazo ni za aina yake nchini zitakazokuwa zikifanyika kila mwezi Desemba zikiambatana na maadhimisho ya sherehe za Uhuru wa Tanzania.Kushoto ni Katibu Mkuu wa chama cha Riadha Taifa,Suleyman Nyambui.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakichukua tukio hilo.

BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI

UJUMBE TOKA CHINA WAFANYA MAZUNGUMZO NA UONGOZI WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI JIJINI DAR LEO

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akiukaribisha Ujumbe toka Wizara ya Usalama wa Raia China katika Kikao cha pamoja na Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi jijini Dar es Salaam.
Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika kikao na Ujumbe wa Wizara ya Usalama wa Raia toka China.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi na mgeni wake, Naibu Waziri wa Usalama wa Raia wa China, Mhe. Yang Huanning, wakisaini Hati ya Ushirikiano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Tanzania na Wizara ya Usalama wa Raia, China.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi na Naibu Waziri wa Usalama wa Raia wa China wakibadilishana Hati ya Ushirikiano wa Wizara zao.
Picha ya pamoja ya Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Ujumbe wa Wizara ya Usalama wa Raia toka China.

Alliance One trains for a stronger Management Team

$
0
0
MARK MASON the Managing Director sharing with event participant’s the company overview strategy 2013
Wheel borrow race from Left is MARK MASON pushing ROB PAGE representing KFC Team, next KHASSIM NGATOLUWA pushing MUSTANSIR MUSAJI representing Kali Team.
Event participants sitting in a circle to hear Heads of Department share their departmental concerns. (Head of departments - ALEX TAIT Leaf and Sales Director, THOM BENADE Operation’s Director, GUY MCDONALD Factory Director, BLASIUS LUPENZA Human Resources Director and CHIZA JERE Finance Director

Alliance One Tobacco Tanzania Limited (AOTTL) held a management team building exercise on 10th May 2013 at White Sands resort. The Team building was organised so management could enhance their skills as well as share challenges from their departments then workshop solutions.

During the exercise, AOTTL’s Managing Director, Mark Mason took the opportunity to address is management team of 20 professionals about the strategy for AOTTL in 2013/14. The highlights of the strategy included the growth of the Company; Farmers’ sustainability; enhancing Safety Health and Environment policies as well as improving Customer Relations further. “At Alliance One our strategies are geared towards growth for the company through positive relationships.

We aim to return value to our shareholders and partners as well as our stakeholders. We are very excited to be recognised as one of the significant contributors to Tanzania’s GDP, as well as a proactive developer of Tanzania’s agricultural sector. This is what we will be the key focus of our initiatives going forward,” said Mason.

The 2013/14 Strategy for AOTTL will aim to optimise processes in the value chain by improving on efficiencies. Top line measures that include; agronomy up-skilling for tobacco farmers; technological innovation in the industry; as well as a robust reforestation programme; will all be implemented in the current financial year. 

 Sustainable CSI programmes are also part of the strategy as AOTTL aims to assist Tanzanian communities where it operates. During the presentation Mason also pointed out that Management were the bridge between the theory of a strategy and its practical application on the ground. The strategy presentation led into the Team Building that the Management team had assembled for.

Speaking on the team building Mason said, “It is not every day that we take time out to assess our performance as Alliance One’s management team outside of our daily routines. We took this opportunity to leave our desks and get together to share our challenges. There after we also had an opportunity to use our broad collective experience to find solutions.” Carl Bosse, the training facilitator also added that the management team building exercise needed to be a regular part of a company calendar to ensure that the lessons learnt in the sessions become a culture.”

The exercises which included ‘Building the emotional intelligence of a team’; as well as ‘Strengthening interdepartmental understanding’, were conducted at White Sands Resort.

Article 21

wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro yapewa Msaada wa T-shirt 500 kwa ajili ya Mbio za Mwenge wa Uhuru

$
0
0
Kampuni ya nguo ya A to Z ya Arusha imetoa msaada wa fulana mia tano kwa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro ajili ya mbio za mwenge wa Uhuru mwaka huu.

Mkurugenzi mkuu wa A to Z,Bwana Anuj Shah amekabidhi rasmi fulana hizo kwa mkuu wa wilaya ya Hai,Bwana Novatus Makunga.

Shah ameeleza kuwa kwa kutambua umuhimu wa mbio za mwengi kwa ajili ya mustakabari wa taifa,ndiyo maana ameamua kutoa mchango wake wa fulana.

"Sisi ni wafanyabiashara ambao kuwepo kwa mazingira mazuri ndani ya taifa kunatupa fursa ya kufanya vizuri na mwenge kwa miaka yote umekuwa nyenzo muhimu ya kuwaunganisha Watanzania bila la kujali dini,kabila ama vipato,"alifafanua.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Hai,Bwana Makunga ameeleza kuwa mwenge wa Uhuru utakuwa wilayani humo kesho Jumatano.

Amesema kuwa katika wilaya ya Hai utapitia miradi nane,ambapo kati ya hiyo mitatu itazinduliwa na miwili itafunguliwa wakati mingine mitatu itawekewa mawe ya msingi.

Amesema kuwa miradi hiyo ina thamani ya shilingi 1,165,781,250 ambapo mchango wa serikali kuu ni shilingi 666,466,000,halmashauri ya wilaya 15,551,450 na nguvu za wananchi ni shilingi 11,033,800 na wahisani shilingi 472,700,000.

Amesema kuwa mbio za mwenge za mwaka huu zimebeba ujumbe unaosema "watanzania ni wamoja" wenye kauli mbiu "Tusigawanywe kwa misingi ya tofauti zetu za dini,itikadi,rangi na rasilimali"

Makunga ameeleza kuwa mwenge huo utapokelewa katika eneo la Maili sita ukitokea wilayani Moshi.

Amesema kuwa baada ya kuwa wilayani Ha kwa siku nzima siku inayofuata wataukabidhi mwenge katika wilaya ya Siha katika eneo la Lawate.

Picha: Mkuu wa wilaya ya Hai akipokea fulana kwa ajili ya mwenge wa Uhuru kutoka kwa mkurugenzi wa kampuni ya nguo ya A to Z ya jijini Arusha,Anuj Shah

MKUU WA JESHI LA MAGEREZA AENDESHA ZOEZI LA UVALISHAJI NISHANI KANDA YA KASKAZINI LEO

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Magereza, Kamishna Jenerali, John Minja akikagua Guard ya Heshima iliyoandaliwa kwa ajili yake kabla ya kuanza zoezi la Uvalisha Nishani kwa Maafisa na Askari wa Magereza toka Mikoa ya Kanda ya Kaskazini leo Mei 28, 2013 katika viwanja vya Gereza Kuu Karanga, Moshi, Kilimanjaro.
Mkuu wa Jeshi la Magereza, Kamishna Jenerali, John Minja (kulia) akimvalisha Nishani ya Utumishi Uliotukuka Kazini, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kilimanjaro, ACP Hamis Nkubasi. Jumla ya Maafisa na Askari 30 kutoka Mikoa ya Kanda ya Kaskazini wamevalishwa Nishani mbalimbali leo, Mei 28, 2013 katika viwanja vya Gereza Kuu Karanga, Moshi, Kilimanjaro.
Guard Maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya kutoa heshima kwa Mkuu wa Jeshi la Magereza, Kamishna Jenerali John Minja (hayupo pichani) ikitoa heshima kabla ya zoezi la Uvalishaji Nishani kwa Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza wa Mikoa ya Kanda ya Kaskazini lililofanyika leo Mei 28, 2013 katika viwanja vya Gereza Kuu Karanga, Moshi, Kilimanjaro.
Mkuu wa Jeshi la Magereza, Kamishna Jenerali, John Minja (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na watunukiwa Nishani mara baada ya zoezi la Uvalishaji Nishani kwa Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza kutoka Mikoa ya Kanda ya Kaskazini leo Mei 28, 2013 katika viwanja vya Gereza Kuu Karanga, Moshi, Kilimanjaro. Picha na Felix Mwagara.

Vimwana wa Redd's Miss Tanga 2013 haya hapa

$
0
0
Washiriki wa shindano la Redd's Miss Tanga 2013 wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mazoezi ya kujiandaa na shindano hilo, litakalofanyika Juni 22 kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

CHUO CHA MUCCOBS-Moshi na IAA-Arusha mabingwa wa Safari Pool

$
0
0
  Mchezaji wa Pool wa Chuo cha KCMC, Kim Kunthea akicheza dhidi ya mpinzani wake Idrisa Juma wa Chuo cha KCMC wakati wa fainali za mashindano ya Safavri Lager Higher Learning Pool Compitition 2013 mchezaji mmoja mmoja (Singles) Mkoa wa Kilimanjaro.
Wachezaji wa timu ya Chuo cha Institute of Accountant of Arusha (IAA) wakishangilia na kitita cha sh.500,000/= ikiwa ni zawadi  mara baada ya kuibuka mabingwa wa mashindano ya Safari Lager Higher Learning Pool Compitition 2013 Mkoa wa Arusha.
  Wachezaji wa Mchezo wa Pool,Winfrida Mponzi kutoka Chuo cha MUCCOBS na Aluiya Herode kutoka Chuo cha SMMUCO wakishindana kulagi wakati wa mashindano ya Safari Lager Higher Learning  Pool Comitition 2013 Mkoa wa Kilimanjaro.

NANI KAMA TANZANIA?

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Marais wastaafu, Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mzee Benjamin William Mkapa, na Waziri Mkuu Mstaafu ambaye pia ni Katibu Mkuu Mstaafu wa OAU Dkt. Salim Ahmed Salim, huko Addis Ababa ambako viongozi hao walialikwa kuhudhuria sherehe za miaka 50 ya Umoja wa Afrika. Ni nadra sana katika bara la Afrika na kwengineko duniani kuona Marais walioko madarakani na waliostaafu kuwa pamoja kwa amani na furaha namna hii. Tanzania Oye!

MTANDAO WA KIMATAIFA WA WABUNGE WANAOPIGANIA DEMOKRASIA, AMANI,UTAWALA WA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU DUNIANI KUKUTANA JIJINI DAR

$
0
0
Mtaalam wa sheria za kimataifa na Haki za Binadamu kutoka mtandao wa kimataifa wa wabunge wanaotetea Haki za Binadamu, Amani na Utawala wa Sheria duniani Bw. Peter Barcroft (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mkutano wa wabunge walio kwenye mtandao huo jijini Dar es salaam kujadili namna watakavyounganisha nguvu zao katika kuzihamasisha na kuzishawishi nchi mbalimbali duniani kupinga na kuzuia silaha kuangukia mikononi mwa makundi ya wahalifu kwa kusaini mikataba inayozuia hali hiyo.
Mbunge kutoka Ghana Bw. Alban Bagbin akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa mkutano wa wabunge walio katika mtandao wa Kimataifa wa kutetea amani, maendeleo, utawala wa sheria na Haki za Binadamu duniani watakavyopanga mikakati mbalimbali ya kuzishawishi nchi wanazotoka kusaini mikataba inayozuia uagizaji , uingizaji na usambazaji wa silaha katika nchi zao kuyafikia makundi yasiyohusika ambayo yamekuwa chanzo cha uvunjifu wa amani duniani. Takribani wabunge 22 kutoka nchi za Afrika wanashiriki mkutano huo.
Mbunge kutoka Sierra Leone Bernadette LAHAI akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) athari zinazosababishwa na silaha kuangukia katika mikono ya wahalifu hasa katika bara la Afrika na kuwa chanzo cha machafuko na kukwamisha maendeleo ya wananchi. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

TAIFA STARS YAANZA KUJINOA ADDIS ABABA

$
0
0
Taifa Stars imetua jijini Addis Ababa, Ethiopia leo (Mei 28 mwaka huu) alfajiri kwa ndege ya EgyptAir ambapo itaweka kambi ya wiki moja kujiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco (Lions of the Atlas) itakayochezwa Juni 8 mwaka huu jijini Marrakech.

Stars iliyotua na kikosi cha wachezaji 21 imefikia hoteli ya Hilton, na imeanza mazoezi leo (Mei 28 mwaka huu) saa 12 jioni kwenye Uwanja wa Addis.

Kwa mujibu wa Kocha Kim Poulsen, Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itakuwa na vipindi (sessions) vinne vya mazoezi kabla ya kucheza mechi ya kirafiki na Sudan (Nile Crocodile). Mechi dhidi yan Sudan itachezwa Jumapili kuanzia saa 11 jioni kwenye Uwanja wa Addis.

Sudan ambayo pia imeweka kambi yake Addis Ababa kujiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia ilicheza mechi yake ya kwanza jana (Mei 27 mwaka huu) dhidi ya wenyeji Ethiopia na kulala mabao 2-0.

Wachezaji wanaounda Stars ni nahodha Juma Kaseja, nahodha msaidizi Aggrey Morris, Mwadini Ally, Ally Mustafa, Shomari Kapombe, Kevin Yondani, Erasto Nyoni, Haroub Nadir, Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Khamis Mchana, Amri Kiemba, Salum Abubakar, Simon Msuva, John Bocco, Vicent Barnabas, Mudathiri Yahya, Athuman Idd, Haruni Chanongo na Zahoro Pazi.

Kikosi hicho kinatarajiwa kuondoka Addis Ababa kwenda Marrakech alfajiri ya Juni 3 mwaka huu kwa ndege ya EgyptAir. Stars itatua siku hiyo hiyo Casabalanca na kuunganisha moja kwa moja kwenda Marrakech.

Shimozzz Kinondoni Mkwajuni

$
0
0
Kama ni mpitaji mzuri wa barabara Kawawa jijini Dar,basi ni lazima utakuwa umekutana na hadha ya shimo hili lililopo pale Kinondoni Mkwajuni.Kiukweli shimo hilo ambalo ni la kudumu,limekuwa ni kero kubwa sana kwa watumiaji wa njia hiyo hasa kwa wenye magari madogo.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI AAHIDI SERIKALI KUIMARISHA ULINZI NA USALAMA NCHINI

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Emmanuel Nchimbi akiongoza Kikao na Wawakilishi wa Nchi za Umoja wa Ulaya waliomtembelea Wizarani. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil.Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP, Said Mwema pia alihudhuria Kikao hicho akiwa na Wakuu wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam (Kushoto).
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) akizungumza na mmojawapo wa Wawakilishi wa nchi za Umoja wa Ulaya waliofanya kikao naye jijini Dar es Salaam leo.Katikati ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini,IGP Said Mwema. (Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel nchimbi amesema Serikali imeimarisha shughuli za ulinzi hapa nchini ili kuhakikisha kuwa wananchi na wageni wanaishi na kufanya shughuli zao kwa amani. 

 Dk. Nchimbi ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokutana na Ujumbe wa wawakilishi wa nchi za Umoja wa Ulaya (EU) na baadhi ya mabalozi wa Nchi hizo waliopo hapa nchini. 

 Aliuambia ujumbe huo ulioongozwa na Balozi Filberto Cerani Sebregondi kuwa Jeshi la Polisi limeweka mikakati mbalimbali ya kukabiliana na vitendo vya uhalifu katika jiji la Dar es Salaam na maeneo mengine ya nchi.

 Amesema kwa upande wa raia wa kigeni, Jeshi hilo limeanzisha Dawati Maalumu litakalohudumia raia hao pale wanapopata matatizo ili waweze kupata huduma za haraka.

 Kwa upande wake, Kiongozi wa Ujumbe huo amesema Umoja huo utaendelea kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na ameishukuru Wizara hiyo kwa jitihada inazoendelea kuchukua kuhakikisha ulinzi na usalama unaimarishwa kwa wageni na raia.
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live




Latest Images