Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

Article 11


Mashindano ya Kimataifa ya Chess yaja

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Spicenet Tanzania Ltd, Vinay Choudary (wa pili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu mashindano ya Kimataifa ya mchezo wa Chess yatakayoanza Juni 14 mwaka huu jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni Ofisa Michezo katika Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Benson Chacha, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Chess Tanzania, Joe Anea na mjumbe wa kamati ya chama cha chess, Emmanuel Mwaisumbe.
Raisi wa Chama cha Chess Tanzania (TACA), Geoffrey Mwanyika (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu mashindano ya Kimataifa ya mchezo wa Chess yatakayoanza Juni 14 mwaka huu jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni Ofisa Michezo katika Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Benson Chacha, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Chess Tanzania, Joe Anea na mjumbe wa kamati ya chama cha chess, Emmanuel Mwaisumbe.
Baadhi ya wapiga picha za habari wakirekodi tukio hilo jijini Dar es Salaam leo.

NBC wamwaga misaada Taasisi ya Saratani ya Ocean Road

$
0
0
Muuguzi  wa  Taasisi ya Saratani  ya Ocean Road  (ORCI) Sr.  Felista John (katikati aliyevaa gauni jeupe) akipokea msaada wa vyakula mbalimbali  kutoka Meneja Uendeshaji Mikopo wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Mwanaisha Ayosi, iliyotolewa na benki hiyo kitengo cha Operesheni ikiwa ni moja ya mikakati ya benki hiyo kusaidia shughuli za kijamii hospitalini hapo. Wengine ni wafanyakazi katika kitengo hicho.
Mmoja wa wafanyakazi wa maofisa wa benki ya NBC, Lioba Massao (kushoto) akifanya maombezi kwa baadhi ya wagonjwa waliolazwa katika wodi ya  Taasisi ya Saratani ya Ocean Road  (ORCI) katika hafla ambayo benki hiyo kitengo cha operesheni kilikabidhi  msaada wa vyakula mbalimbali ikiwa ni moja ya mikakati ya benki hiyo kusaidia shughuli za kijamii hospitalini hapo.
Baadhi ya wafanyakazi wa NBC wakimjulia hali mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika taasisi hiyo mara baada ya kukabidhi msaada wa aina mbalimbali za vyakula.
Baadhi ya wafanyakazi wa NBC wakimjulia hali mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika taasisi hiyo na pia kumkabidhi msaada wa sabuni ya kufulia.
Baadhi ya wafanyakazi wa NBC wakibeba mizigo ya vyakula na mafuta ya kupikia tayari kuwakabidhi wagonjwa waliolazwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road ya jijini Dar es Salaam kama sehemu ya juhudi za NBC katika kusaidia shughuli za jamii.

DKT SALIM AHMED SALIM AONGELEA MAFANIKIO NA CHANGAMOTO ZA UMOJA WA AFRIKA

Breaking Nyuzzzz: Msanii wa Bongo Fleva,Mangwea afariki dunia

$
0
0
TAARIFA ILIYOTUFIJIA HIVI PUNDE,INAELEZA KUWA MSANII WA MUZIKI WA BONGO FLEVA,ALBERT MANGWEA (PICHANI) AMEFARIKI DUNIA HUKO NCHINI AFRIKA YA KUSINI.

CHANZO CHA KIFO CHA MSANII HUYO BADO HAKIJAFAHAMIKA.

GLOBU YA JAMII INAENDELEA KUFUATILIA TUKIO HILO LA KIFO CHA MANGWEA NA TAARIFA KAMILI ITAKUJA BAADAE KIDOGO. HEBU JIKUMBUSHE HAPA CHINI NA KIBAO CHAKE CHA 'MIKASI'

Katibu mkuu wa ccm,ndugu kinana awakuna wakazi wa ludewa mkoani njombe,amfagilia Filikunjombe kwa kazi nzuri.!

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara wa CCM, kwenye Uwanja wa mpira mjini Ludewa mkoni Njombe, leo Mei 28, 2013. Kinana ambaye yupo katika ziara ya siku saba, kukagua utekelezaji wa ilani ya chama na kuzungumza na wananchi mkoani Njombe, amefuatana na Katiobu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.

Baadhi ya maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika Mei 28, 2013 katika Uwanja wa mpira mjini Ludewa mkoani Njombe.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na ujumbe wake wakiwasili kwenye mkutano wa hadhara wa CCM, katika Uwanja wa mpira mjini Ludewa mkoni Njombe, leo May 28, 2013. Kinana ambaye yupo katika ziara ya siku saba, kukagua utekelezaji wa ilani ya chama na kuzungumza na wananchi mkoani Njombe, amefuatana na Katiobu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
Baadhi ya wakazi wa Wilaya ya Ludewa na Vitongoji vyake wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara wa CCM, uliofanyika  katika Uwanja wa mpira mjini Ludewa mkoni Njombe, leo Mei 28, 2013. 
Sehemu ya umati wa watu wakishangilia jambo wakati Nduhu Kinana alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa CCM, katika Uwanja wa mpira mjini Ludewa mkoni Njombe, leo Mei 28, 2013.
Mbunge wa Jimbo la Ludewa Mh.Deo Filikujombe akizungumza na wananchi  wa Ludewa na vitongoji vyake waliofika kwenye mkutano wa hadhara wa CCM, katika Uwanja wa mpira mjini Ludewa mkoni Njombe, leo May 28, 2013.
3Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM Ndugu Nape Nnauye akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo kwenye uwanja wa mpira wa mjini Ludewa .
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wanachama wa shina la CCM tawi la Itunda kata ya Malangali mapema leo,alipotembelea mashina kadhaa kwa kuzungumza nao mambo mbalimbali ya kuimarisha chama.

Article 5

TRA MBEYA YATEKETEZA BIDHAA FEKI - ITV


sisi tutashiriki, wewe je??

$
0
0
Kuna mambo kusimamiwa kwake kidete ni kukaa chini, mengine ni kulala na mengine ni kusimama wima. Kukiwa na jambo au hali haulidhiki nayo, machaguo yako mengi kuonyesha hisia na hata msimamo wako. Yote haya lazima yafanyike maadamu tu ujumbe ufike kwa ufasaha mahala husika wakati hatua sahihi zikiendelea na utekelezwaji. Haiwezekani kwenye nchi yenye tatizo la ajira linaloongezeka kila uchao vijana wenye vipaji wafe na njaa kisa tu ugomvi na madalali wa sanaa! 
Wasanii wanapaswa kufa na njaa pale tu kama kazi zao hazikubaliki na hadhira na hivyo hazinunuliki. Lakini suala la kufichwa na kufunikwa kwa jitahada za nguvu ya uwezo wa kifedha, mali na mtandao mpana ni la kupingwa kwa nguvu zote na hadhira. Lazima hadhira iwe ndiyo hakimu pekee wa kazi, maslahi na mafanikio ya wasanii. Haiwezekani hadhira ionekane ni ya muhimu tu katika kauli mbiu za kuteka masoko kibiashara lakini linapokuja suala la mahitaji, hadhira ichaguliwe na fanani nini inastahili kusikia, kuona, au kula. Hili kamwe haliwezi kuwa chaguo langu wala la hadhira au Watu. 
Ni chaguo la fanani na la stahili kusikilizwa, kuonwa au kuliwa na huyo huyo fanani na mafanani wenzake. Dhihaka inakuwa kubwa zaidi pale jambazi linapoongoza jitihada ya kutokomeza kazi za vibaka! Kweli mwenye nacho hujitwalia zaidi na sheria ni kipofu kwa mwenye nacho. Pamoja na yote haya, umma unayo silaha nzito na mahsusi yenye uwezo wa kuwaangamiza majambazi na kuwatokomeza vibaka. Silaha yetu ni umoja katika kupinga ufedhuri wa mafanani uchwara na dhihaka ya majambazi. Anayejitenga na umoja huu, anajindalia upweke msibani zamu yake ikifika. 
Ni masikitiko kwamba wanaodhurumiwa na kuibiwa wameanguka katika tego la kale la majambazi na wadhurumaji. Wametegwa wajitenge na umoja na wao kwa kujua ama kwa kutokujua wakategeka! Wamekubali kuutumikia mkate wa siku wa kafiri wasijue kwamba kesho safari ya dhuluma yaendelea! Na hawa watadumu katika safari ya kudhulumiwa milele na hawachomoki ng’o! Tunaochukizwa na yote yaliyosimuliwa hapo juu, tuungane na waliokwisha jitambua katika kujinasua na ufedhuri wa madalali uchwara wa sanaa. 
Tuwasaidie kupaza sauti za umoja katika kuwashambulia majambazi. Tuwaonyeshe mafanani uchwara na majambazi kwamba nguvu haziko kwao bali kwetu (hadhira). Tulidhirishe kwamba sisi ndiyo tunapaswa kuchagua tukipendacho maana twalipia muda, huduma na bidhaa. 
Tukatae kuchagulia nini kisikilizwe na masikio yetu, macho yetu yaone nini au vinywa vile nini na kisha watupigie kauli mbiu za “Chaguo la Watu” Ijumaa ya Tarehe 31 mwezi huu, tuliowengi hatuendi na kipaumbele cha kucheza disco, kuangalia wacheza disco au kusikiliza music live bali tunakwenda kusema hapana: “Unyonyaji haukubaliki na Kufanyiwa machaguo hakukubaliki”. Tutafanya hivyo kwa sauti kubwa na ya umoja. Tunakwenda kuthibitisha kuwa ni Sisi ndiyo hadhira na siyo wao.

HOJA YA MDAU: Kwanini Adam Nditi asiitwe national team?

$
0
0

Nimesoma hoja hii kwenye blog moja kwamba Adam Nditi mchezaji wa Chelsea yuko tayari kucheza national team lakini hajawahi kuitwa na kuna baadhi ya wapenzi wanatoa lawama nzito kwa chama cha Mpira na viongozi wandamizi wa TFF. Mimi kama muumini wa soka la bongo naomba nitaharishe chama cha mpira ili tusifanye yale ya zamani ya kumleta Kally Ongala huku tukijua ana uraia wa Uingereza na huku Tanzania sheria zetu zikiwa haziruhusu mtu kuwa na uraia wa Nchi mbili (Dual citizenship).

Adam Nditi yuko Uingereza toka akiwa  mtoto mdogo kabisa hivyo sidhani kama kweli kijana huyu anaecheza Chelsea akawa anatumia passport ya Tanzania, ni na wasiwasi hatuna taarifa Za kutosha kuhusu huyu kijana. Ni kwasababu hiyo hatuwezi kukurupuka na kuwaandama viongozi wa TFF wakati hatujui status ya mchezaji mwenyewe.

Naomba kutoa hoja,

Onesmo Waziri

CCM YAFUNIKA MKUTANO WA LUDWA,NJOMBE

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara wa CCM, kwenye Uwanja wa mpira mjini Ludewa mkoni Njombe, leo May 28, 2013. Kinana ambaye yupo katika ziara ya siku saba, kukagua utekelezaji wa ilani ya chama na kuzungumza na wananchi mkoani Njombe, amefuatana na Katiobu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
Baadhi ya maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika Mei 28, 2013 katika Uwanja wa mpira mjini Ludewa mkoani Njombe. (Picha na Bashir Nkoromo).

DK.SHEIN AANZA RASMI ZIARA YAKE NCHINI CHINA

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(wa nne kushoto)akiwa na ujumbe wake katika mazungumzo na Rais wa China Xi Jinping,(wane kulia) katika Ikulu ya Mjini Beijing Nchini China leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Makamo wa Rais wa China Li Yuanchao,katika makaazi yake Mjini Beijing nchini China akiwa katika ziara ya mualiko wa Kiserikali wa Nchi hiyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwatambulisha Viongozi katika ujumbe aliofuatana nao kwa Rais wa Jamhuri ya watu wa China Xi jinping, walipofika Ikulu ya Mjini Beijing Nchini China akiwa katika ziara ya mualiko wa Serikali wa Jamhuri hiyo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Article 24

katibu wa bunge atoa pole kwa familia ya marehemu ernest zulu, ratiba ya mazishi yatolewa

$
0
0
 Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilila akimpa pole Theresia Mlekani ambaye ni mke wa Ofisa Habari Mwandamizi wa Bunge, Ernest Zulu wakati alipokwenda kuwapa pole wafiwa nyumbani kwao Ubungo Kibangu, Dar es Salaam.

Kupata  ratiba ya mazishi ya 

KUKANUSHA TAARIFA YA GAZETI LA JAMHURI

$
0
0

TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI

Jeshi la Polisi nchini linapenda kutoa ufafanuzi juu ya taarifa ambayo imekuwa ikiripotiwa katika gazeti la Jamhuri la siku ya Jumanne tarehe 21 – 27 Mei, 2013 toleo No. 81 na la tarehe 28 Mei -Juni 3, 2013 toleo No. 83, yenye kichwa cha habari “MTANDAO WA MAUAJI YA BARLOW WATAJWA NA IGP MWEMA AMPA HIFADHI MUUAJI WA BARLOW”.
Taarifa hiyo siyo sahihi, kwa sababu mtu aliyehojiwa na gazeti hilo anayejulikana kwa jina la Mohamed Edward Malele ni mgonjwa wa akili ambaye mpaka hivi sasa amelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu. Mara kadhaa mtu huyo amekuwa na tabia ya kuwatuhumu viongozi na watu mbalimbali juu ya tuhuma zisizo na ukweli wowote kutokana na ugonjwa wake wa akili.
Jeshi la Polisi nchini linatoa rai kwa gazeti la Jamhuri kuwa makini na habari wananzoziandika ambazo hazijafanyiwa uchunguzi wa kutosha zenye lengo la kupotosha jamii.

Imetolewa na:-
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.

CHAGONJA AWAFARIJI ASKARI WALIOCHOMEWA NYUMBA MTWARA

$
0
0


Na Frank GeofrayJeshi la Polisi, Mtwara.


Kamishana wa Operesheni na Mafunzo Paul Chagonja (pichani) amefika mkoani Mtwara na kuwafariji Askari wote waliochomewa nyumba zao na wahalifu wakati wa vurugu zilizotokea hivi karibuni wakati wa uwasilishaji wa bajati ya Wizara ya Nishati na Madini na kuwahakikishia kuwa Jeshi la Polisi litawakamata wale wote waliohusika katika vurugu hizo.
Vurugu hizo zilisababishwa na baadhi ya wananchi ambao walikuwa wanapinga kujengwa kwa bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam ambapo walifanya uharibifu wa miundominu mbalimbali ikiwemo kuchoma nyumba zaAskari Polisi.
Akizungumza katika kikao cha Maofisa na Askari polisi mkoani hapa Kamishna Chagonja alisema Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Said Mwema amesikitishishwa sana na vitendo vya uchomaji wa nyumba hizo na amewataka kutovunjika moyo katika kufanya kazi.
Alisema kilichowapata Askari hao ni changamoto katika kazi na wanapaswa kuzikabili ili kuhakikisha wanaendelea kulinda usalama wa raia na mali zao na raia wachache wasiopenda amani wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
“Raia wema ni wengi na wahalifu ni wachache hivyo lazima tuhakikishe wale wote wanaofadhili na kuhamasisha vurugu hapa mkoani mtwara tunawakamata na kuwafikisha mahakamani ili sheria iweze kuchukua mkondo wake kwa kuwa vitendo wanavyovifanya sio vizuri hasa kuchoma makazi ya watu”Alisema Chagonja.
Wakati huohuo Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya rufaa ya Ligula Dk Mohamed Kodi amesema katika kipindi chote cha vurugu zilizotokea mkoani hapa hakuna mgonjwa yeyote aliyefika hospittalini hapo na kulalamika kufanyiwa vitendo vya ubakaji kama taarifa zilivyoenea katika vyombo mbalimbali vya habari.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoani Mtwara Kamishna Msaidizi wa Polisi Linus Sinzumwa alisema mpaka hivi sasa hawajapokea malalamiko yoyote kuhusiana na vitendo hivyo na amewataka kama wapo watu waliofanyiwa vitendo hivyo wapeleke malalamiko yao katika kamati iliyoundwa inayojumuisha vyombo vyote vya ulinzi na usalama.
“Naomba malalamiko hayo yawe ya msingi na siyo ya uzushi na uongo na pindi ikigundulika kuwa maneno hayo ni ya uzushi na uongo sheria itachukua mkondo wake dhidi ya wahusika” Alisema Sinzumwa.
Amewataka wakazi wa Mtwara kuendelea na shughuli zao kwa amani na utulivu na kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili wahusika wote wa vurugu hizo waweze kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya dola.

Brasilian Portuguese Teacher wanted

$
0
0
Hello Michuzi.
 I'm looking for a Brasilian Portuguese teacher. He/She'll be responsible for a class size of minimum 20 students in Dar es Salaam. The venue will be arranged. He is needed as soon as possible.

For interested ones please contact spoi2002@gmail.com.

Kamati ya Maridhiano Six: Kongamano la Kitaifa la Mwongozo wa Katiba ya Tanzania Part 1

Nine acres, land Plot for sale Location: Kibaha Misugusugu

$
0
0

Ningependa kuwatangazia fursa hii hapa chini wadau wa maendeleo kutoka pande zote za dunia:


Size: Nine acres
Purpose: Industrial development & suitable for warehouses
Clean Land Title available
Water & Electricity: within good reach & good road
Semi-developed
Price: US$ 155000

SIKIA HII...

$
0
0
Walevi wa3 walikodi Bajaji, dereva aliwasha bajaji kutaka kuwapeleka wanapokwenda alafu akaizima alipoona wamelewa sana na moyo wake kusita kwamba hatolipwa pesa yake na kutakuwa na utata baadae. 

Mlevi wa kwanza alisema asante kwa kutufikisha, Wa pili alimpa hela, Watatu alimpiga kofi dereva akamwambia "siku nyingine usiendeshe kwa kasi!!" 

 So nani aliyekuwa amelewa sana hapo? Wadau tupeni majibu
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images