Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

Kampuni ya TTCL yanogesha sherehe za Chrismass vituo vya watoto yatima Dar

$
0
0


Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Mushi (kushoto) akimkabidhi mmoja wa watoto wa kituo cha yatima 'Yatima Group Trust Fund Mbagala Chamazi mfuko wa unga, . TTCL imekabidhi msaada wa bidhaa mbalimbali vikiwemo mchele, sukari, mafuta ya kupikia, soda, maji ya kunywa na mbuzi kwa ajili ya sherehe za Siku Kuu ya Chrismass. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Kituo cha Yatima Group Trust Fund Mbagala Chamazi.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Mushi (wa pili kushoto) akimkabidhi mbuzi Mkurugenzi Msaidizi wa Kituo cha Yatima Group Trust Fund Mbagala Chamazi. TTCL imekabidhi msaada wa bidhaa mbalimbali vikiwemo mchele, sukari, mafuta ya kupikia, soda, maji ya kunywa na mbuzi kwa ajili ya sherehe za Siku Kuu ya Chrismass.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Mushi (wa tatu kulia) akimkabidhi mmoja wa watoto wa kituo cha watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi cha Kimara SUCA maji ikiwa ni moja ya bidhaa zilizotolewa. TTCL imekabidhi msaada wa bidhaa mbalimbali vikiwemo mchele, sukari, mafuta ya kupikia, soda, maji ya kunywa na mbuzi kwa ajili ya sherehe za Siku Kuu ya Chrismass.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Mushi (kushoto) akimkabidhi mfuko wa unga Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi cha Kimara SUCA, Evans Tegete ikiwa ni baadhi ya msaada uliotolewa na kampuni hiyo. TTCL imekabidhi msaada wa bidhaa mbalimbali vikiwemo mchele, sukari, mafuta ya kupikia, soda, maji ya kunywa na mbuzi kwa ajili ya sherehe za Siku Kuu ya Chrismass.


IBADA YA MKESHA WA KRISMASI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Na Dotto Mwaibale
AMANI Duniani na hapa nchini haiwezi kuletwa na matajiri bali italetwa na maskini wenye kumcha Mungu, amesema Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo wakati akiongoza ibada ya mkesha wa Krismasi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Dar es Salaam jana.
"Amani duniani na hapa nchini haiwezi kuletwa na matajiri bali italetwa na maskini wamchao kristo" alisema Pengo.
Alisema kila mmoja wetu mahali alipo akitekeleza wajibu wake ipasavyo atambue anakuwa anatekeleza amani.
Askofu mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dk. Alex Malasusa alisema Sikukuu ya Krismasi inamaanisha ni amani na ndio maana watu mbalimbali wamekuwa wakipeana zawadi kuashiria amani hivyo akawaomba wakristo na watu wote kuendeleza amani nchini. 
Katika ibada hiyo ya mkesha wa Krismasi waumini walimiminika kwenye makanisa ya Anglikana la Mtakatifu Albano, Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam la Mtakatifu Joseph na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Azania Front huku wakiburudishwa na nyimbo za kumsifu Mungu za kuzaliwa Yesu Kristo.
 Askofu mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa, akisalimiana na muumini wa kanisa hilo Usahrika wa Azania Front, Mama  Violet Muro baada ya kumpatia zawadi ya ibada mkesha wa Krismasi iliyofanyika jana usiku jijini Dar es Salaam.
 Kwaya ya Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Akbano ikitumbuiza katika ibada iliyofanyika katika kanisa hilo jijini Dar es Salaam.
 Waumini wa Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano wakiwa kwenye ibada ya mkesha wa krismasi.
 Vijana wa Kanisa la KKKT la Azania Front wakiigiza igizo la kumbukumbu ya kuzaliwa Yesu Kristo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

DIAMOND APAGAWISHA USIKU WA WASAFI JANGWANI SEA BREEZE DAR ES SALAAM

$
0
0
 Naseeb Abdul aka Diamond Platinumz akitumbuiza katika Tamasha la Vodacom Wasafi lililofanyika Jangwani Sea Breeze  jijini Dar es Salaam
 Diamond  akisalimia mashabiki  wakati wa Tamasha hilo

Viongozi wa Vijiji watakiwa kujiridhisha na Miradi ya Umeme Vijijini

$
0
0
Mkandarasi wa Kampuni ya Derm Electric Limited anayetekeleza Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Pili (REA II) Mkoani Mara ameagizwa kukutana na Uongozi wa Shirika la Umeme (TANESCO) Mkoani humo pamoja na Viongozi wa Vijiji vinavyopitiwa na mradi huo ili wajiridhishe kabla hajaukabidhi. 
Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alipofanya ziara ya Kikazi ya kukagua utekelezaji wa Miradi umeme Vijijini katika Kijiji cha Kwikuba Kata ya Busambala, Wilaya ya Musoma Vijijini.
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akizungumza jambo wakati wa ziara yake ya utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini (REA II). Kulia kwake ni Mhandisi wa mradi kwa Mkoa wa Mara kutoka kampuni ya Derm Electric Limited, Mhandisi Hussein Ayubu.
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa pili kulia) akisaini kitabu cha wageni katika Kijiji cha Kwikuba baada ya kuwasili kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa Mradi wa umeme na kuzungumza na wananchi.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kwikuba waliofika kuzungumza na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani). 

IBADA YA KRISTMASI YAFANYIKA KITAIFA MJINI BUKOBA KATIKA KANISA LA MWOKOZI KKKT LEO

$
0
0
Ibada ya Krismasi Kitaifa imefanyika katika kanisa la Mwokozi KKKT Mjini Bukoba huku viongozi wa dini wakitoa wito wa kudumishwa kwa amani na kuepuka vitendo vyovyote vya ubaguzi vinavyoweza kuwatenga wananchi.

Katika mahubiri hayo Askofu wa Dayosisi ya Ksikazini Magharibi Dokta Abednego Keshomshahara pia aliwataka wananchi kufanya kazi kwa bidii badala ya kutegemea mafanikio yanayotokana na miujiza badala ya kufanya kazi.


Ibada hiyo ilianza kwa maandamano yaliyoongozwa na Askofu huyo ambapo Jumuiya ya Kikristo Nchini iliwakilishwa na Moses Matonya aliyetoa wito wa kuendelea kudumisha amani na kusisitiza upendo miongoni mwa wananchi

Askofu Abedinego Keshomshahara wa Kanisa hilo la kirutherli Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Magharibiakiwasalimu na kuwapa Neno Waumini leo hii.





Mkuu wa Mkoa mpya wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salim Mustafa Kijuu akiwasalimia waumini katika kanisa la Mwokozi KKKT Mjini Bukoba mara baada ya kushiriki Misa ya Krismasi katika kanisa hilo
Waumini wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Yaliyojiri Katika Vituo Mbalimbali vya Televisheni

KANISA LA KKKT KIVULE DAR WAMPIGIA SALUTI YESU KRISTO IBADA YA KRISMASI

$
0
0
 Wanakwaya wa Vijana ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Mtaa wa Kivule, wakimpigia saluti Yesu Kristo walipokuwa wakiimba wimbo wa kumsifu Yesu wakati wa Ibada ya Krismasi.
 Mchungaji wa Kanisa la KKKT Mtaa wa Kivule, Dar es Salaam, Michael Mgaya akitoa mahubiri wakati wa Ibada ya Kuzaliwa Yesu Kristo ya Krismasi asubuhi
 Waumini wakimwimbia Yesu Kristo
 Waumini wakiimba wimbo wa kumsifu Yesu Kristo

WATENDAJI IDARA YA UJENZI NATUMBO WANUSURIKA KUTUMBULIWA

$
0
0

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Suleiman Said Jaffo akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Namtumbo Mkoani Ruvuma ambao hawaonekani katika picha.Picha na www.ruvumatv.com


HIGHLIGHTS MAJIMAJI VS AZAM FC SONGEA

Profesa Muhongo asheherekea Krismasi kwa kufanya makubwa Musoma Vijijini

$
0
0
Mbunge wa Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ametoa mifuko 300 ya saruji kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa Zahanati ya Kigeraetuma iliyopo Kijiji cha Kamuguruki, Musoma Vijijini ikiwa ni zawadi ya sikukuu ya Krismasi.

Zawadi hiyo imetolewa leo kijijini humo katika hafla ya chakula aliyoiandaa kwa ajili ya wananchi wa Kijiji hicho pamoja na vijiji vingine mara baada ya ibada iliyofanyika katika kanisa la Menonite lililopo kijiji cha Nyakatende, Musoma Vijijini..

Katika hafla hiyo Profesa Muhongo aliongozana na familia yake pamoja na rafiki zake kutoka Ujerumani ambao kwa pamoja walijumuika na wananchi wa Musoma vijijini kusherehekea.
 Kanisa la Menonite la kijiji cha Nyakatende ambapo Mbunge wa Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, familia yake na rafiki zake kutoka Ujerumani walishiriki ibada ambapo aliahidi kuchangia ujenzi wake. 
 Mbunge wa Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa tatu kutoka kushoto waliokaa katika viti) katika picha ya pamoja na waumini wa Kanisa la Menonite mara baada ya kumalizika ibada.
Diwani wa Kata ya Nyakatende, Rufumbo Rufumbo (katikati) akionesha vifaa vya umeme jua alivyokabidhiwa na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) . 
 Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (aliyeshika kipaza sauti) akiwa amepanga foleni na wananchi wa jimboni mwake kwa ajili ya kuchukua chakula.
 Wananchi wa Kata ya Nyakatende wakichukua chakula
Mbunge wa Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa pili kulia) akionesha vifaa vya umeme jua ambavyo Balozi wa Korea nchini anatarajiwa kupeleka mtaalamu jimboni humo ili kuwafundisha vijana namna ya utengenezwaji wake ili kujipatia kipato

ULEGA ATOA SALAM ZA SIKUKUU KATIKA KANISA LA KIGANGO CHA MWANAMBAYA WILAYANI MKURANGA

$
0
0
 Mbunge wa Mkuranga Bw Hamisi Abdala Ulega Akisalimiana na Mmoja wa Waumini Bw Alfred John Kanisani hapo
 Akiwa Katika Dua ya Pamoja na waumini wa Kanisa hilo la Kigango cha Mwanambaya Wilayani Mkuranga.
Mbunge wa Mkuranga Bw Hamis Abdala Ulega Akiongea na Waumini wa Kanisa la Kigango cha Mwanambaya lililopo Mwanambaya Wilayani Mkuranga na Kuwataka kumkumbuka Muumba katika kila Jambo Katika Maisha yao kila siku.Picha na Yasir Adam Globu ya Jamii

AMSHA KIPAJI CHAKO NA MICHUZI TV

MAONESHO KAHAWA NA UTALII YAFANYIKA MJINI RIYADH, SAUDI ARABIA

$
0
0


Na Mwandishi Wetu, Riyadh Saudi Arabia

Maonesho makubwa ya kahawa na chocolate (coffee and Chocolate) yamemalizika kwa mafanikio jijini Riyadh Saudi Arabia, huku kwa mara ya kwanza maonyesho hayo yakishirikisha Ubalozi wa Tanzania, nchini Saudi Arabia. 
Katika maonyesho hayo yaliyoanza Desemba 20 hadi 23 mwaka huu, yalihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwamo wafanyabiashara wa Tanzania kwa nia ya kutangaza bidhaa za mazao ya kilimo na viwanda kutoka Tanzania.

Akizungumza katika maonyesho hayo, Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Mhe. Hemed Mgaza, aliyasifu maonyesho hayo akisema kuwa yamekuwa na tija kwa nchi ya Tanzania pamoja na wafanyabiashara waliohudhuria. Alisema ofisi yake ilidhamilia kuyatumia maonyesho hayo kwa ajili ya kutangaza bidhaa za Tanzania pamoja na wafanyabiashara wake ili kufanikisha maendeleo yao kwa ujumla kwa ajili ya kukuza uchumi wa nchi yao.
“Tumeweka historia nchini Saudi Arabia kwa kuhakikisha kwamba tunashiriki kwa mara ya kwanza kwa ajili ya kuitangza nchi yetu, wafanyabiashara wetu pamoja na bidhaa zetu ili kila mmoja afahamua mazuri tuliyokuwa nayo. 
“Tulichofanya ni kuandaa banda letu lenye kila aina ya zuri letu hususan katika mazao ya kilimo ambayo kwa kawaida kila mtu alionyesha kuvutiwa na maonyesho hayo,” alisema Balozi Mgaza.
Mazao mengine yaliyoonyeshwa katika maonyesho hayo ni pamoja na kahawa, chai, asali, katani, viungo, maziwa, mchele, karafuu, ufuta na nyinginezo huku mfanyabiashara Bi Khadija Naif akialikwa na Ubalozi ili kuwawakilisha wafanyabiashara kadhaa wa Tanzania kwa kubeba jukumu la kuleta bidhaa mbalimbali zilizooneshwa kwa siku hizo 4.
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemed Mgaza (kushoto) akifanya mazungumzo na wadau mbalimbali wa biashara katika maonyesho yaliyofanyika mjini Riyadh, Saudi Arabia.
Mazungumzo yanaendelea kwenye banda hilo.
Balozi Hemed Mgaza akizungumza na wawekezaji wa Saudi Arabia waliohudhuria katika maonyesho hayo.
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemedi Mgaza mwenye suti nyeusi alipata fursa ya kukutana na wawekezaji mbambali waliotembelea banda la Tanzania wakati wa maonesho hayo.

Mfanyabiashara wa Tanzania aliyehudhuria maonyesho ya biashara ya Saudi Arabia, Bi Khadija Naif, akiwa na wasaidizi wake wakitoa maelekezo kwa watembeleaji wa banda lao.

Introducing "Penzi laua" by Saidi Tumba

KRISMAS ILIVYOSHEREHEKEWA KATIKA UFUKWE WA COCO BEACH JIJINI DAR LEO

$
0
0
 Mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es salaam na maeneo ya jirani, wakiwa wamefurika kwa wingi wao katika Ufukwe wa Coco Beach ikiwa ni sehemu ya kusherehekea sikukuu ya Krismas leo. Hili ni moja ya maeneo ambayo wakazi wengi wa jiji la Dar hutembelea katika kusherehekea sikukuu.




USIKU WA ZUBEIR IMANI NA ZAWADI MOHAMED WAFANA

$
0
0
  Bw. Harusi Zubeir Imani na mkewe, Bi. Zawadi Mohamed wakiyarudi magoma wakati walipokuwa wakiingia ukumbini katika tafrija maalum ya kuwapongeza kwa kuungana kwao, iliyofanyika katika ukumbi wa Kilimanjaro uliopo Viwanja vya Sabasaba, Jijini Dar es salaam jana Desemba 24, 2016.
 Bw. Harusi Zubeir Imani na mkewe, Bi. Zawadi Mohamed wakiyarudi magoma.

RAIS DKT. MAGUFULI PAMOJA NA MKEWE MAMA JANETH WASHIRIKI IBADA YA KRISMASI KATIKA KANISA KATOLIKI (KANISA KUU LA MOYO MTAKATIFU WA YESU) MKOANI SINGIDA

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Baba Askofu wa Jimbo la Singida Askofu Edward Mapunda mara baada ya Ibada ya Krismasi katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.

Baba Askofu wa Jimbo la Singida Askofu Edward Mapunda akimuombea na kumbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya Ibada ya Krismasi katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mke wake Mama Janeth Magufuli wakiwa katika Misa ya Krismasi katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia waumini wa Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida mara baada ya kushiriki Misa ya Krismasi katika kanisa hilo mkoani Singida. 

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwasalimia waumini wa Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida mara baada ya kushiriki Misa ya  Krismasi katika kanisa hilo mkoani Singida 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakisalimiana na waumini wa Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida mara baada ya ibada ya Krismasi. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


ngoma azipendazo ankal: Orchestre Veve, Nakomitunaka

Article 0

WANAUME WASINDIKIZENI WAKE ZENU KILINIKI-Father Festus

$
0
0

Na,Vero Ignatus.Arusha.

Wito umetolewa kwa wanaume kuwa makini na kuwasindikiza wake zao kiliniki wakati wakiwa wajawazito kwani yapo mambo muhimu watakayojifunza wakiwa pamoja yatakayomsaidia mama na mtoto kuwa salama hadi wakati wa kujifungua.

Hayo yamesemwa na father Festus Makwame wa kanisa katoliki Sent Treza jimbo la Arusha alipokuwa kwenye ibada ya mkesha wa sikukuu ya krismas na kusema kuwa wanaume wengi hawana tabia ya kuwa na wake zao pindi wanapokuwa wajawazito jambo ambalo ni kosa kubwa

“Wanaume wasindikizeni wake zenu kiliniki huoni kwamba anashirikiana na Mungu katika uumbaji tena anakujengea heshima yawewe kuitwa baba Fulani?nenda nae yapo mambo mengi mtakayoelekezwa hata namna ya vyakula anavyotakiwa kula akisahau kwa vile ulikuwepo utamkumbusha?hebu igeni mfano wa Joseph na Maria hadi Yesu Kristo anazaliwa walikuwa pamoja.”alisisitiza

Amewataka waumini waliohudhuria ibada hiyo ya mkesha wa christmas waamue kubadilika waruhusu Kristo azaliwe mioyoni mwao ili mambo yao yawe mapya ,huku akisisitiza msamaha wa kweli pale mmoja anapomkosea mwingine kwani ni jambo ambalo Mungu analifurahia

“Wacha tuwe wakweli hakuna jambo gumu kama kumsamehe mtu aliyekukosea tena kwa makusudi,lakini kwa vile Mungu ameagiza tusameheane ni lazima tufanye hivyo na ukweli utabakia kuwa hivi Msamaha wa kweli ni ule ambao unautoa huku Unauma umekosewa lakini unasamehe kwa faida yako mwenyewe pia.”Alisisitiza father Festus.

Aidha amesema kuwa katika ibada hiyo ya mkesha wa krismas amewataka waumini kuachana mila na desturi potofu ambazo hazimpendezi Mungu kwani ni uvuli wa mauti. 

“Wacheni michanganyo michanganyo kwani haimpendezi Mungu jamani kama umeamua kuwa kwa Mungu ,basi mfuate ili upate uzima wa milele ,na kama mwenzetu umeamua kumfuata shetani basi mfuate uangamie kwaani mambo haya ya michanganyiko michanganyiko mkiiendekeza huwa inaleta balaa na mikosi katika familia zenu”alisema father Festus.

Festus Makwame wa Kanisa la Katoliki Sent Treza Jimbo la Arusha akiwa anafurahiajambo wakati akiwa anaendesha ibadaya mkesha wa sikukuu ya christimas hapo jana usiku Jijini Arusha.Picha naVero Ignatus Blog.
Baadhi ya waumini waliohudhuria katika ibada hiyo ya mkesha wa sikukuu ya Christmass ni pamoja na maharusi hawa .Picha na Vero Ignatus Blog 
fFather Festus Makwame akiwa anahubiri katika mkesha wa sikukuu ya christimasiliyofanyika katika kanisa la Katoliki Sent Treza Jimbo laArusha.

Maharusi Denis na bi Joviety wakiwa ibadani muda mfupi kabla ya kufunggishwa ndoa kanisani hapo.Picha na Vero Igantus Blog

Maharusi hawa bwana Charles na bi Sabilina waliweza kufunga ndoa katika mkesha huo wa sikukuu ya christma katika kanisa la Katoliki Sent Treza Jimbo la Arusha .Picha na Vero Ignatus Blog.
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live


Latest Images