Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

LUKUVI AWAPA WAHADZABE HATI ZA KUMILIKI ARDHI

0
0
Na Kitengo cha Mawasiliano - Wizara ya Ardhi
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amewapatia hati miliki za Ardhi kwa jamii ya wa Hadzabe wanaoishi wilayani Karatu Mkoani Arusha.
Waziri Lukuvi amefika katika maeneo yao na kuwapa hati miliki za kimila kwa vijiji na wanayoishi jamii ya wa Hadzabe na jamii nyingine za kifugaji ili kulinda maeneo yao ya malisho na maeneo wanayotumia kuwinda wanyama.
Jamii ya wa Hadzabe ni watu ambao huishi kwa mfumo wa maisha ya kuwinda, kufuga wanyama pori na kula mimea na matunda ya miti inayowazunguka. Jamii hii kwa miaka mingi imekuwa ikiishi bila kufuata mipaka ya maeneo yao na hivyo kusababisha migogoro ya ardhi kwa jamii nyingine zinazoishi karibu na maeneo yao.

Pamoja na ziara hiyo Mhe. William Lukuvi amtatua migogoro ya Ardhi ya wananchi wa wilayani Karatu Mkoani Arusha na wananchi walio na kero za migogoro ya ardhi na kuzipatia ufumbuzi pamoja na kupokea vielelezo vya kero za wananchi walizoziwasilisha kwa Waziri ili azitolee maamuzi.
Wananchi wa vijiji vya Mang’ola juu na Midabini wilayani Karatu Mkoani Arusha walisimamisha msafara wa Mhe. Lukuvi ili awasikilize kero zao za ardhi, ambapo Waziri Lukuvi alisimama na kuzitatua pamoja na kumuagiza Mkuu wa wilaya ya karatu Bibi Therezia Mahongo kutafutia ufumbuzi baadhi ya migogoro hiyo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi anaendelea na Ziara zake za utatuzi wa Migogoro ya Ardhi nchini, ambayo imejikita zaidi katika kutatua migogoro ya ardhi ya Mikoa ya kanda ya Magharibi, Kaskazini na ile ya Kanda ya Ziwa hapa nchini.
Hadi sasa Mhe. Lukuvi ndani ya mwezi huu wa Desemba ameishatatua migogoro ya ardhi ya Mkoa wa Kigoma na wilaya zake za Kigoma mjini, Kasulu na Kibondo na katika Mkoa wa Shinyanga na wilaya zake za Kishapu na Shinyanga mjini na katika mkoa wa Geita amefanya ziara katika wilayani Chato.
Pia Mhe. Lukuvi ametatua migogoro ya ardhi ya Mkoa wa Mara katika wilaya za Musoma na Bunda ambapo kwa Arusha ametatua migogoro ya wilaya ya Arumeru na Karatu.
 Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (wa nne kulia mbele) akiwasili wilayani Karatu kwa ajili ya kuwapatia hati miliki za Ardhi jamii ya wa Hadzabe.
 Wa Hadzabe wakimkaribisha Waziri wa ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi kwa kumvusha taji.
  Waziri wa ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiwapatia hati miliki za Ardhi kwa jamii ya wa Hadzabe wanaoishi wilayani Karatu Mkoani Arusha.
  Wa Hadzabe wakifurahi na Waziri wa ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi baada ya kuwapa hati miliki za Ardhi.
 Wakazi wa kijiji cha Midabini wilayani Karatu Mkoani Arusha wakisimamisha msafara wa Mhe. Lukuvi ili awasikilize kero zao za ardhi, ambapo Waziri Lukuvi alisimama na kuzitatua.
Wakazi wa kijiji cha Mang’ola juu wilayani Karatu Mkoani Arusha waliosimamisha msafara wa Mhe. Lukuvi wakimsikiliza wakati akitatua mgogoro wao wa Ardhi.

MAGIC FM BAMIZA TOP 20 COUNTDOWN

MAMA MAJALIWA ATEMBELEA KITUO CHA YATIMA NA KUTOA MSAADA

0
0
 Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akiwa amewabeba watoto, Editha  (kushoto) na Edina wa Kituo cha kulea watoto yatima cha CHAKUWAMA kilichopo Sinza jijini Dae es salaam jijini Dar es salaam  wakati alipotembelea kituo hicho na kutoa misaada mbalimbali leo  Desemba 24, 201
MKE wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa ametoa msaada wa vitu mbalimbali kwa makundi ya watoto yatima jijini Dar es Salaam ili kuwawezesha kufurahia sikukuu za mwisho wa mwaka. 
Mama Majaliwa ametoa msaada huo leo (Jumamosi, Desemba 24, 2016) katika vituo vitatu vya CHAKUWAMA kilichopo Sinza, HISANI kilichopo Kigamboni na CHAMAZI kilichopo Mbagala. 
Akikabidhi msaada huo ikiwemo mchele, sabuni, mbuzi, juisi na soda, Mama Majaliwa amesema ameona ni vema atoe msaada huo kwa watoto hao ili na wao waweze kufurahia sikukuu za mwisho wa mwaka kama ilivyo kwa watoto wengine. 
Pia ametoa wito kwa makundi mbalimbali yenye uwezo katika jamii wawe na moyo wa kusaidia makundi yenye uhitaji. 
Kwa upande wao, walezi wa vituo vya kulelea watoto yatima vya CHAKUWAMA na HISANI wamemshukuru mke wa Waziri Mkuu kwa msaada huo huku baadhi ya watoto wakisema msaada huo umewapa faraja kubwa. 
Mlezi wa kituo cha CHAKUWAMA, Bibi Saida Hassan mbali ya kushukuru kwa msaada huo, amewaombea kwa Mwenyezi Mungu awape afya na nguvu za kuendelea kuwatumikia vizuri Watanzania. 
Naye Mlezi wa kituo cha HISANI, Bi. Hidaya Mutalemwa ameiomba jamii iendelee kuyakumbuka makundi yenye uhitaji kwani bado yanakabiliwa na changamoto nyingi za kufanikisha ndoto zao ikiwemo kupata elimu.

BONDIA FRANCIS CHEKA AGOMA KUPIMA UZITO MPAKA APEWE FEDHA ZA KIANZIO

0
0
Na Humphrey Shao, 
Globu ya Jamii
Bondia wa mchezo wa ngumi za Kulipwa nchini,Francis Cheka amegoma kupima uzito kwa ajili ya pambano lake dhidi ya Dula Mbabe mpaka hapo atakapopewa shilingi 3000,000/- kama kianzio kabla ya kupanda ulingoni.
Cheka amegoma kupima uzito  katika ukumbi wa Mango Garden ambapo mpinzani wake tayari alikuwa ameshawasili tayari kwa ajili ya kupima.
“Nimetoka Morogoro kwa nauli yangu na nimelala hoteli kwa fedha yangu na nimejaribu kumpigia promota wangu Kaike mara kdhaa toka jana hakupokea simu. Nilivyofika hapa nikamuomba anipatiea fedha yangu bado akagoma. Hivyo mimi nimeamua kutopima uzito wala kucheza mpaka hapo nitakapopewa fedha yangu”amesema Cheka.
Baada ya kushindwa kuelewana bondia Francis Cheka aliamua kuondoka ukumbini hapo na kurudi hotelini alipofikia kujiandaa na safari ya kurejea Morogoro kuendelea na mambo mengine. 
Kwa upande wake promota wa mchezo huo Siraju Kaike alisistiza kuwa pambano hilo lipo licha ya bondia huyo kugoma kupima uzito kutokana na kutokubaliana katika masuala ya kifedha. Hakufafanua.
  Bondia Abdallah Pazi "Dula Mbabe" akipima uzito kwa ajili ya kupambana na Francis Cheka hapo kesho katika ukumbi wa Mango Garden jijini Dar es salaam leo
 Bondia Francis Cheka akitoka nje ya ukumbi wa Mango Garden baada ya kugoma kupima uzito 
 Mdogo wake Francis Cheka, Cosmas Cheka,  akiongea a baadhi ya wadu wa ngumi juu ya swala la Kaka yake kutopewa pesa ya kianzio kabla ya kupima uzito
 Mashabikiwa mchezo wa ngumi wakiwasili katika ukumbi wa Mango Garden Kinondoni kushuhudia jinsi mabondia hao wanavyopima uzito
 Baadhi ya wadau wakijaribu kuzungumza na Cheka baada ya kugoma kupima uzito mpaka atakapopewa pesa yake

FAMILIA YA WATU SABA WASIOONA WAPATIWA MISAADA WILAYANI KIBAHA

0
0
Na John Gagarini, Kibaha
JUMUIYA ya Maili Moja A ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Maili Moja imetoa misaada ya nguo na vyakula kwa familia yenye wasioona saba inayoishi kwenye Mtaa wa Simbani wilayani Kibaha mkoani Pwani.
Akizungumza na gazeti hili mara baada ya kukabidhi misaada hiyo ambayo ilipelekwa na Jumuiya hiyo mwenyekiti Jacob Samson alisema kuwa waliamua kupeleka misaada hiyo baada ya kupata taarifa za familia hiyo.
Samson alisema kuwa wametoa misaada hiyo pia ni katika kuwafanya nao waweze kusherehekea siku kuu ya X- Mass na wenzao wakiwa na furaha hasa ikizingatiwa wao ni wahitaji na wanahitaji misaada mbalimbali.
“Tunaamini kusaidia jamii zenye mahitaji ni ibaada kamili na inawatia moyo na kujiona kuwa hawako peke yao kwani kuna watu wanawaunga mkono na kushiriki nao kwa pamoja,” alisema Samson.
Alisema kuwa Jumiya yao hufanya ibaada za nyumba kwa nyumba ambapo hutembeleana na kushirikiana kwenye masuala mbalimbali ya kijamii pamoja na ya kiimani.
“Jumuiya yetu iko kwa ajili ya kusaidiana kwenya matatizo na furaha hivyo wanajumuiya walisema kuwa twende kwenye hiyo familia iwe sehemu ya ibaada ya yetu ya kila Jumamosi ili kuwafariji na wamejitolea sana ili kuhakikisha familia ile nayo inafurahia kipindi hichi cha mwisho wa mwaka,” alisema Samson.
Aidha alisema kuwa wanaomba watu wengine nao wajitokeze kuisaidia familia hiyo ambayo ina hitaji misaada mbalimbali kutokana na kuwa kwenye mazingira magumu.
“Kutoa ni moyo na si utajiri kwani watu wenye moyo wanapaswa kwenda kuwasaidia kwa jambo lolote la kijamii hasa ikizingatiwa familia hiyo inasimamiwa na mwanamke ambaye alitengana na mumewe,” alisema Samson.
Kwa upande wake mama wa familia hiyo Mwajuma Maulid alisema kuwa anaishukuru Jumuiya ya maili Moja kwa kuwapatia misaada hiyo ambayo wameitoa kwani wameonyesha moyo wa kipekee.
Maulid alisema kuwa vyakula vilivyotolewa vitawasaidia katika kusherehekea sikukuu ya X-Mass kwa furaha kama wanavyofurahia watu wengine na kuwataka watu wengine waendelee kuwasaidia.
“Tuko kwenye mazingira magumu sana kwani hali yetu si nzuri ambapo tunaishi maisha ya kubahatisha kwa hiyo wanapokuja watu kama hawa na kutupa misaada tunashukuru sana,” alisema Maulid.
Familia hiyo inaishi mtaa wa Simbani kata ya Kibaha ina watu saba ambao hawaoni ambapo wasioona ni mume wake ambaye walitengana,watoto wanne wasioona na  wajukuu wawili wote hawaoni na inaishi kwa kutegemea kuchoma mkaa na kusuka mikeka.
 Valeria Mfuse mmoja wa Wanajumuiya ya Maili Moja A ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT Usharika wa Maili Moja akimkabidhi mafuta ya kupikia Mwajuma Maulid kwa ajili ya familia yake ambayo ina watu saba wasioona  baada ya kuitembelea
 Mzee wa Kanisa kutoka Jumuiya ya Maili Moja A ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT Usharika wa Maili Moja, Samwel Luhembe kushoto akikabidhi sabuni kwa ajili ya familia ya watu saba wasioona Mwajuma Maulid.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maili Moja A ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT usharika wa Maili Moja Jacob Samson kushoto akimkabidhi moja ya msaada uliotolewa na Jumuiya hiyo kwa family ya watu saba wasioona anayepokea ni Mwajuma Maulid ambaye ndiye mama anayeihudumia familia hiyo
 Mzee wa Kanisa kutoka Jumuiya ya Maili Moja A Samwel Luhembe kushoto akikabidhi nguo zilizotolewa  na jumuiya hiyo ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT usharika wa Maili Moja anayepokea ni mama wa familia ya watu wasioona saba Mwajuma Maulid kulia.
  
Familia ya watu wasioona wakiwa katika picha ya pamoja

Yaliyojiri Katika Vituo Mbalimbali vya Televisheni

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ziarani China

0
0

 Ujumbe wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ukiogozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif ulioko upande wa ulia ukifanya mazungumzo na Uongozi wa Shirika la Kimataifa linalotoa huduma za Kijamii la Nchini China la AVIC.
 Balozi Seif  wa Tatu kutoka Kulia na Ujumbe wake akiwa pamoja na Uongozi wa Avic International wa Nchini China ukiongozwa na Makamu wa Rais wa Shirika  hilo Bw. Lin Jun kulia ya Balozi Seif mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Mjini Beijing.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya Kimataifa ya Uvuvi ya China  ya Hongdon Bw. Lan Ping Yong Sheraton Hoteli Mjini Beijing China.
 Balozi Seif akisalimiana na Makamu wa Rais wa Kampuni kubwa  ya Miradi ya Umeme Duniani ya China  Bwana Wang Pinshan kabla ya kuanza kwa mazungumzo yao kwenye Hoteli ya Kimataifa ya Sheraton Mjini Beijing.
 Makamu wa Rais wa Kampuni kubwa  ya Miradi ya Umeme Duniani ya China  Bwana Wang Pinshan wa pili kutoka Kulia akikiongoza kikao cha mazungumzo ya pamoja na Ujumbe wa Zanzibar ulioongozwa na Balozi Seif  wa Tatu kutoka Kushoto. Wa kwanza kutoka  kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utawala Bora na Utumishi wa Umma Bibi Asha Ali Abdulla na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Mh. Mohamed Ahmed Salum. Kushoto ya Balozi Seif  ni Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dr. Khalid Salum Mohamed na Katibu Mkuu wake Nd. Khamis Mussa.

KUTOKA MAKTABA: MWALIMU NA WAPIGA PICHA WA VYOMBO VYA HABARI

0
0
Mwalimu Nyerere akiwa katika picha ya pamoja na wapiga picha wa vyombo mbalimbali habari Ikulu Dar es salaam. Waliosimama kutoka kushoto ni Max Madebe (Mfanyakazi), Sam Mmbando (Shihata), Vicent Urio (Daily News), Mzee Makwaia (Maelezo), Mwalimu, Mzee wa AVI, Juma Dihule (Shihata) Adinani Mihanji (Shihata) Moshi Kiyungi (Maelezo). 
Waliochuchumaa toka kushoto ni Mzee Kassange wa Ikulu, Mzee Charles Kagonji (Maelezo), Mzee wa Shihata, Mwanakombo Jumaa (Maelezo), Khatibu Ally (Uhuru na Mzalendo) na Raphael Hokororo.

LEO NI HAPPY BIRTHDAY YA MAMA WA MITINDO ASYA IDAROUS-KHAMSIN, SANAA FASHION SHOW KUPAMBA SIKU

0
0
Happy Birthday Mama wa Mitindo Tanzania Asya Idarous-Khamsin

SAMIA AWATAKA WANA CCM MKOA WA KASKAZINI UNGUJA KUIMARISHA USHIRIKIANO

0
0
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi-CCM- Taifa ambaye pia Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka wanachama na viongozi wa CCM katika mkoa Kaskazini Unguja wadumishe na kuimarisha ushirikiano miongoni mwao kama hatua ya kujenga chama imara.

Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ametoa kauli hiyo katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kaskazini (B) Unguja wakati akizungumza kwenye kikao kilichojumuisha viongozi wa ngazi mbalimbali wa chama hicho kwa ajili ya kujadili mipango na mikakati ya kuimarisha chama hicho.

Mjumbe huo amesisitiza kuwa kama viongozi wa chama hicho watadumisha ushirikiano na kuondoa tofauti zao watakijenga chama na kuongeza idadi kubwa ya wanachama wapya ikilinganishwa na hali ilivyo kwa sasa katika eneo hilo.Amesema baada ya kumalizika kwa uchaguzi Mkuu kazi iliyopo kwa sasa kwa viongozi wa CCM katika ngazi zote ni kuweka wanaweka mipango na mikakati madhubuti itakayoweza chama hicho kuendelea kushika dola.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi-CCM-Taifa SAMIA SULUHU HASSAN ambaye pia ni Mlezi wa CCM katika mkoa wa Kaskazini Unguja amesema anaimani kubwa kuwa kuanzia sasa viongozi hao watajipanga ili kuhakikisha chama hicho kinapata ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020.

Kuhusu uimarishaji wa jumuiya za Chama hicho, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wa CCM katika mkoa wa Kaskazini Unguja waimarishe jumuiya hizo ili ziweze kutekeleza majukumu ya kichama katika kila ngazi.

Mjumbe huyo ameonya viongozi hao waache tabia ya kugombania madaraka kwenye chama bali washirikiane katika kuongeza idadi ya wanachama hasa vijana ndani ya Chama hicho.


Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Mlezi wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wabunge, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka mkoa wa Kaskazini ,Wenyeviti na Makatibu wa Majimbo CCM Mkoa wa Kaskazini pamoja na Wenyeviti na Makatibu wa Jumuiya kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini B Kinduni. 
Wabunge, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka mkoa wa Kaskazini ,Wenyeviti na Makatibu wa Majimbo CCM Mkoa wa Kaskazini pamoja na Wenyeviti na Makatibu wa Jumuiya wakimsikiliza Mlezi wa CCM mkoa wa Kaskazini na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini B Kinduni.
Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Mhe. Vuai Ali Vuai akihimiza Umoja na Mshikamano kwa Viongozi wa CCM mkoa wa Kaskazini Unguja wakati wa kikao cha kupokea tathmini ya uchaguzi wa mwaka 2015 kikao ambacho mgeni rasmi alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini B Kinduni.


WAZIRI NAPE AOMBOLEZA VIFO VYA MPOKI BUKUKU NA MODEST MFUTAKAMBA

0
0
Mhe. Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ametuma salamu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa, wapiga picha pamoja na Wanahabari wote nchini kufuatia kifo cha mwanahabari na mpiga picha Mpoki Bukuku (kushoto) kilichotokea jana tarehe 23 Desemba, 2016 katika Taasisi ya Mifupa (MOI) Jijini Dar es Salaam. 
Mhe. Nape Nnauye pamoja na watendaji wa Wizara wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha mwanahabari huyo kwani ni pigo katika tasnia ya habari nchini. 
Mhe. Waziri Nape amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha mwanahabari huyo na ameeleza kuwa, kifo chake ni pigo katika tasnia ya habari hususani katika picha kwasababu Marehemu wakati wa uhai wake ametoa mchango mkubwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo magazeti ya Majira, Business Times, The Guardian, Nipashe na Mwananchi na The Citizen.


Wakati huo huo Mhe. Waziri ametuma salamu za rambirambi kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel pamoja na familia kufuatia kifo cha mtumishi wake Bw. Modest Mfutakamba Mfilinge (kulia) kilichotokea usiku wa kuamkia leo 24 Desemba, 2016. 
Mungu azilaze roho za Marehemu mahali pema peponi. Amina.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,
Dar es Salaam.


24 Desemba, 2016.

WAZIRI MKUU AKAGUA ENEO LA UJENZI WA MAKAZI YA ASKARI MAGEREZA JIJINI DAR, AMPONGEZA KAIMU KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NAMNA ALIVYOJIPANGA KUSIMAMIA UJENZI

0
0
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa(Mb)  akisalimiana na Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa kabla ya kuongea na Maafisa na askari wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Dar es Salaam alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua maandalizi ya ujenzi wa nyumba 320 za makazi ya Maafisa na askari wa Jeshi hilo katika eneo la Gereza Kuu Ukonga, Jiji la Dar es Salaam Disemba 24, 2016(wa kwanza kushoto) ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni.
 Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akitoa maelezo mafupi kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim(hayupo pichani) namna Jeshi hilo lilivyojipanga katika kuhakikisha kuwa ujenzi wa nyumba hizo ambazo zinatarajiwa kujengwa katika eneo la Gereza Kuu Ukonga, Jijini Dar es Salaam unakamilika ipasavyo.
 Meneja Ujenzi wa Mamlaka ya Majengo nchini – TBA, Arch. Humphrey Killo akitoa maelezo ya kitalaamu kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua maandalizi ya ujenzi wa nyumba 320 za makazi ya askari katika eneo la Gereza Kuu Ukonga, Jiji la Dar es Salaam Disemba 24, 2016.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akikagua eneo la ujenzi wa nyumba hizo za makazi ya askari.

RAIS DKT. MAGUFULI AWASILI MKOANI SINGIDA, ANATARAJIWA KUSHIRIKI KATIKA IBADA YA KRISMASI SIKU YA KESHO MKOANI HUMO

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi mara baada ya kuwasili mkoani humo. Pia Rais Dkt. Magufuli anatarajiwa kushiriki katika Ibada ya Krismasi mkoani humo hapo Kesho
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili mkoani Singida na kupokelewa na Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akielezea ujio wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mkoani humo ambapo pamoja na mambo mengine atashiriki katika Ibada ya Siku ya Krismasi katika Kanisa mojawapo mkoani Singida. PICHA NA IKULU



ngoma azipendazo ankal: Baba Gaston - Kakolele Viva Christmas

THE HOME GOING CELEBRATION


MAGAZETI YA LEO JUMAPILI DEC 25

PENGO AWAASA WAUMINI WAO KANISA KATOLIKI KUTUNZA AMANI

0
0
Na  Humphrey Shao, Globu ya jamii.

Askofu mkuu wa Kanisa katoliki jimbo kuu la Dar es Salaam ,Mwadhama Polycarp Cardinali Pengo amewaasa watanzania kutunza amani iliyopo, licha ya kutajwa kuwa maskini na kuachana na tamaa za utajiri ambazo mara zote huvuruga amani.

Pengo amesema hayo katika ibada ya mkesha wa mwaka mpya iliyofanyika katika kanisa kuu la Mtakatifu Joseph lilipo jijini Dar es Salaam.

“Maskini wasiwe chimbuko la ukosefu wa Amani kwa tamaa ya utajiri, kwani katika Dunia ya leo watu wengi wamekuwa wakitegemea mali ili wapate amani, jambo ambalo baadae huwa kinyume chake, kwani amani ya kweli huanzia moyoni mpaka kwa Taifa zima”amesema Pengo.

Amesema kuwa amani ya kweli inapatikana kwa kila mmoja kutekeleza wajibu wake wa kufanya ambayo Mungu ametuagiza kufanya ili tuweze kuwa na furaha ya nchi.

Ametaja kuwa asiwepo mtu yoyote ambaye atasema mimi maskini siwezi kuwa chimbuko la Amani, hivyo kuwaomba kila mmoja amuweke Mungu nafasi ya juu ili aweze kuwa na maamuzi sahihi katika maisha yake.

Ameweka wazi kuwa ni vyema viongozi wakawa watu wa kwanza kumuweka Mungu mbele ili wanaowaongoza wawe wakiiga kutoka kwao hivyo hapo amani itapatikana. 
 Askofu mkuu wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama ,Polycarp Cardnali  Pengo akihubiri katika ibada ya usiku wa mkesha wa Xmass katika kanisa la mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam.



Waumini wa Kanisa Katoliki wakiwa wamepiga magoti kumuomba Mungu wakati wa ibada hiyo y mkesha wa Xmass 
Kikundi cha kwaya kikitumbuiza katika kanisa hilo wakati ibada ya mkesha ikiendelea

ILIVYOKUWA KWENYE USIKU WA WADAU GODFREY SINYANGWE NA ESTHER KILUMA JIJINI MWANZA.

0
0
Jana Disemba 24, 2016 ilikuwa siku ya furaha kwa Bwana Godfrey Sinyangwe (kushoto) pamoja na Bi.Esther Kiluma (kulia), baada ya kufunga ndoa takatifu katika Kanisa la Saint Nicholas Jimbo Kuu la Mwanza chini ya Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo, Lazaro Manjelenga aliyesaidiana na Mchungaji Joseph Samwel.

 Zifuatazo ni baadhi ya picha zikionesha matukio katika hafla ya ndoa hiyo iliyofanyika usiku wa kuamkia leo, ukumbi uliopo Bugando Jijini Mwanza.
#BMG
Maharusi wakikata keki
Maharusi wakilishana keki, kwa upendo kabisa.

DC ILALA AWAAGIZA POLISI KUACHA KUWANYANYASA WAENDESHA BODABODA

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

MKUU wa Wilaya Ilala, Sophia Mjema ameagiza polisi kuacha mara moja kuwanyanyasa waendesha bodaboda na kutaka polisi kutumia mashine ya EFD pale wanapotoa faini kwa bodaboda hao.

Kutumia mashine za EFD kutawafanya waendesha bodaboda kulipa ndani ya siku saba kama wanavyofanya kwa wenye bodaboda.

Hata hivyo amesema maagizo ya mkuu wa Mkoa ya askari mgambo na ulinzi shirikishi wafanye kazi na watendaji wa kata na kuhoji kuwa mgambo na ulinzi shirikishi wanapenda kazi ya kukamata bodaboda.

Mkuu wa Wilaya ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa bonanza la bodaboda jana lililofanyika Pugu, Jijini Dar es Salaam, Sophia amesema kunyanyasika kwa bodaboda kunatokana na baadhi yao kutotambua umuhimu wa kazi zao.Alifafanua kuwa “Ulinzi shirikishi na mgambo ni marufuku kuwasumbua bodäboda, kwani wanayo haki ya kufanya kazi na kuishi kwa amani kama ilivyo”.

Sophia amesema licha ya kuwepo kero za bodaboda kukamatwa inatokana na baadhi yao kutopewa elimu ya usalama barabarani hivyo lazima wapewe elimu hata wakikosea watajua.Amesema wakati umefika wa kazi za bodaboda kuheshimika kudharau kazi hiyo inafanya wafanye kazi bila uhakika.

Hata hivyo amesema kutokana na kupata malalamiko atafanya mkutano kati ya bodaboda na jeshi la polisi kwa ajili ya kutoa elimu ya pamoja na kutatua sintofahamu zinazojitokeza kwa bodaboda.
.Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akiwa katika pikipiki kabla ya uzinduzi wa bonanza la Bodaboda Pugu jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akizungumza na waendesha bodaboda katika uzinduzi wa bonanza Pugu, jijini Dar es Salaam.Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
Mrakibu Msaidizi wa Jeshi Polisi (ASP),Charle’s Kanyunyu akizungumza katika uzinduzi wa bonanza jana Pugu, jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Bodaboda wa Kituo cha Mombasa, Athuman Omary, akitoa kero wanazokutana nazo katika madereva wa bodaboda katika uzinduzi wa bonanza jana Pugu, jijini Dar es Salaam.

SALAMU ZA SIKUKUU YA CHRISTMAS KWA WANANCHI WA MKOA WA DAR ES SALAAM

0
0

DC Kinondoni Ally Hapi

Ndugu wana Dar es Salaam,

Kwa niaba ya serikali ya Mkoa wetu, napenda kuchukua fursa hii kwa dhati kabisa kuwatakia waumini wote wa kikristo na wana Dar es salaam kwa ujumla sikukuu njema ya Christmas yenye furaha, upendo, amani na utulivu.

Ni muhimu wana familia kuchukua tahadhari za kiusalama katika siku hii ikiwemo kuongeza umakini na uangalizi wa watoto maeneo ya fukwe (beach) ili kuondoa uwezekano wa maafa, kutoondoka nyumbani bila kuacha angalau mtu mmoja mzima wa kubaki kutazama usalama wa nyumba na kuzidisha umakini katika matumizi ya barabara.

Tusisite kutoa taarifa kwa jeshi letu la polisi pindi tunapoona viashiria vya uhalifu au kuvunjika amani katika maeneo tuliyopo.

Nawasihi tutumie siku hii kuiombea nchi yetu iendelee kuwa ya amani na utulivu, na tuwaombee viongozi wetu akiwemo Rais wetu mpendwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli na wasaidizi wake wote ili waendelee kuitumikia nchi yetu vema. 

Aidha tuwajali wagonjwa, walemavu, yatima na watu wasiojiweza katika maeneo yetu tunayoishi ili nao waweze kusherehekea siku hii kwa furaha.

Mwisho nawatakia heri, furaha na amani katika sikukuu hii ya Christmas.

ALLY HAPI
KAIMU MKUU WA MKOA
DAR ES SALAAM
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live


Latest Images