Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109611 articles
Browse latest View live

Article 17

0
0
Mbali ya kuwa Sikukuu ya Krismasi kwa Wakristo duniani, pia jana Disemba 25,2016 ilikuwa siku ya furaha kwa ndugu, jamaa na marafiki wa Bwana harusi Mathew Akrama Rwekila na Bibi harusi Agnes Martine (wawili katikati), baada ya kufunga pingu za maisha katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza.

Bibi harusi ni mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili Jijini Mwanza, akifahamika zaidi kwa jina la Agnes Akrama, wote wakimtumikia Mungu katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza.
Picha na Craty Cleophace
Maharusi na wasaidizi wao, wakimsikiliza Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la EAGT Lumala Mpywa, Dkt.Daniel Moses Kulola, wakati wa ibada yao
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya, Dkt.Daniel Moses Kulola, akisisitiza jambo wakati wa ibada ya ndoa
Bwana harusi Mathew Akrama Rwekila na Bibi harusi Agnes Martine, wakila kiapo cha ndoa."Mungu akasema, Si vyema mtu huyu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye". Mwanzo 02:18
BMG inawatakia maisha mema, Amen!
Tazama picha zaidi HAPA

introducing "Moyo sukuma damu" by lameck ditto

0
0
Moyo Sukuma Damu is composed by Lameck Ditto himself and produced by Emma the Boy of Epiq Studios based in Dar es Salaam, Tanzania.The released video, directed by Traveller of Kwetu Studios, is set to achieve massive appeal based on the concept as well as level of detail focused on the project.
Shot in Dar es Salaam, the video will showcase the lifestyle and appeal of the city as a frontier market for music and tourism.Speaking of the release of his video, the talented and well-versed Lameck Ditto said ‘I want to give my fans something they will enjoy to watch as they have enjoyed listening by taking a unique approach to the shootig of the video’.
Follow
Instagram: @lameckditto
Twitter @lameckditto

Yaliyojiri Katika Vituo Mbalimbali vya Televisheni

MAGAZETI YA LEO DEC 26

Magazeti ya leo Desemba 26, 2016

tamasha la sikukuu ya krismasi la”Nogesha Upendo” la WCB Wasafi lanoga Dar es salaam na Iringa

0
0
Sehemu ya umati ya wakazi wa manispaa ya Iringa waliojitokeza katika”Nogesha Upendo” lililoandaliwa na WCB Wasafi na kudhaminiwa Vodacom Tanzania  lilifanyika katika uwanja wa Samora mjini Iringa jana..
 Msanii kutoka WCB, Harmonize akitumbuiza katika”Nogesha Upendo”lililoandaliwa na WCB Wasafi na kudhaminiwa Vodacom Tanzania  lilifanyika katika uwanja wa Samora mjini Iringa jana..
Msanii wa kimataifa Diamond Platinumz akitumbuiza katika”Nogesha Upendo” lililoandaliwa na WCB Wasafi na kudhaminiwa Vodacom Tanzania  lilifanyika katika uwanja wa Samora mjini Iringa jana..
  Wasanii wa muziki wa kundi la Navy Kenzo wakiwapagawisha mashabiki wakati wa tamasha la mkesha wa sikukuu ya krismasi la”Nogesha Upendo” lililoandaliwa na WCB Wasafi na kudhaminiwa Vodacom Tanzania  lilifanyika katika ufukwe wa bahari ya hindi  Jangwani Seabreez jijini Dar es Salaam.
 Mwanamuziki nguli wa muziki wa bongo fleva Diamond Platinumz akikonga nyoyo za  mashabiki wake wakati wa tamasha la mkesha wa sikukuu ya krismasi la”Nogesha Upendo” lililoandaliwa na WCB Wasafi na kudhaminiwa Vodacom Tanzania  lililofanyika katika ufukwe wa bahari ya hindi  Jangwani Seabreez jijini Dar es Salaam. Picha zaidi BOFYA HAPA


TAARIFA KWA UMMA KUHUSU GHARAMA ZA MATIBABU YA DAWA YA SUMU YA NYOKA NCHINI

0
0
Kama tunavyofahamu, nchi yetu ina aina mbalimbali za nyoka ambao pindi wakimuuma mtu huleta madhara mbalimbali ya kiafya. Aidha tunafahamu kwamba tatizo hili lipo zaidi katika maeneo ya vijijini ambako uwezo wa wananchi kumudu gharama za matibabu ni mdogo.
Dawa za kutibu sumu ya nyoka huagizwa kutoka nje ya nchi. Dawa hizo siyo tu hazipatikani kwa urahisi, bali pia zinapatikana kwa gharama kubwa. Bei ya kununulia dawa hizi ni kati ya dola za kimarekani 55 hadi 85 (yaani shilingi za kiTanzania 118,250 hadi 182,750) kwa kichupa kidogo (vial) kimoja. Kichupa hicho huweza kutumika kwa wagonjwa wanne, lakini mara tu baada ya kufunguliwa dawa hiyo huwa haifai tena kutumika ndani ya mwezi mmoja tu.
Pamoja na changamoto hizo, Serikali kupitia MSD kila mwaka huagiza dawa hizi kwa ajili ya mahitaji hayo ya kutibu wagonjwa walioumwa na nyoka, ambapo bei ya kuinunua kutoka MSD ni TZS 200,000/= kwa kichupa kimoja. Hospitali zetu mbalimbali zimekuwa zikiagiza dawa hizi kutoka MSD na kwa washitiri wengine kwa bei hii au zaidi na kuwatibu waathirika wanaohitaji dawa za sumu za nyoka mara zinapohitajika. 
Napenda kuwakumbusha kwamba kwa mujibu wa Sera ya Afya ya mwaka 2007, huduma za tiba hutolewa bure kwa makundi maalum, au kwa kuchangiwa kwa sehemu ya gharama, au kwa kupitia mfumo wa Bima mbalimbali za Afya kama vile CHF. Kwa wale wasio na uwezo na wanaothibitishwa kuwa hawana uwezo, utaratibu wa msamaha hutumika.
Katika kuhakikisha kwamba wananchi wanaohitaji dawa ya  sumu ya nyoka wanahudumiwa ipasavyo, Mhe. Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anatoa maelekezo yafuatayo:- BOFYA HAPA

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi arejea kutoka ziarani China

0
0
Na Othman Khamis Ame, OMPR
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kukamilika kwa ujenzi wa miradi mitatu inayotekelezwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutafungua fursa pana ya ajira hasa kwa Vijana pamoja na kuimarika kwa ufanisi wa kazi katika Taasisi za Umma na hata zile Binafsi.
Akizungumza na Waandishi wa Vyombo mbali mbali vya Habari hapa Nchini mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar akitokea Nchini China kwa ziara ya siku Tano ya Kiserikali Balozi Seif  aliitaja miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa Bandari ya Mpiga Duri, kukamilika kwa eneo la maegesho ya ndege pamoja na Mawasialiano  Serikalini { E. Government }.
Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea kukamilisha taratibu zilizobakia katika hatua za mwisho  kwa ajili ya kukamilisha mradi wa ujenzi wa eneo la maegesho ya Ndege kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar.
Balozi Seif alisema Zanzibar kupitia miradi hiyo itaongeza mapato yake kupitia Sekta ya Utalii, harakati za Kibiashara nah ii itatokana na ongezeko kubwa la idadi ya watalii na wageni watakaoamua kutumia huduma hizo za usafiri wa uhakika.
Akizungumzia Mradi wa Mawasiliano Serikalini { E - Government } Balozi Seif alisema kukamilika kwa mradi huo  awamu ya Pili kwa hatua ya kuunganishwa na mfumo wa Mtandao wa Kisasa utawawezesha Wananchi kupata huduma kwa njia ya mawasiliano.
Alisema Wananchi watapata kuhudumiwa moja kwa moja kwa mfumo wa Internet kwenye sekta za Afya, Elimu pamoja na urahisishaji wa ukusanyaji wa  Mapato ya Serikali Kuu.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akipokewa na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar akitoa nchini China baada ya kumaliza ziara ya siku Tano ya Kiserikali. Kulia ya Mh. Ayoub ni Meya wa Manispaa ya Mjini Mstahiki Khatib Abdulrahman Khatib na Waziri wa  Kazi Uwezeshaji, Wazee, Vijhana na Watoto Mh. Maudlin Cyrus Castico.
  Balozi Seif akisalimiana na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Joseph Abdulla Meza.
 Balozi Seif akisalimiana na Timu ya Wazee waasisi wa Chama cha Mapinduzi.
Balozi Seif  kulia akiwa makini kusikiliza Maswali mbali mbali aliyoiulizwa na Wana Habari mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar akitokea Nchini China. Kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar Dr. Khalid Salum Mohamed aliyembatana naye katika ziara hiyo ya Kiserikali ya siku Tano. Picha na – OPMR – ZNZ.

BOT yakanusha Uvumi juu ya Noti ya Shilingi 500

0
0
Benki kuu ya Tanzania inapenda kuwafahamisha wananchi wote kuwa,habari inayoenea katika mitandao mbalimbali ya kijamii kwamba noti ya shilingi mia tano  haitatumika tena kuanzia Desemba 31,2016; sio taarifa ya kweli na ni uvumi unaopaswa kupuuzwa. 
Ukweli ni kwamba noti ya shilingi 500 itaendelea kuwepo katika mzunguko sambamba na ile sarafu ya shilingi 500 hadi pale noti hiyo itakapotoweka mikononi mwa wananchi. Tafadhali mpuuze taarifa hizo sio za ukweli.

Marcian Kobello. 
Mkurugenzi wa Huduma za kibenki- BoT .

TAARIFA YA KUSIKITISHA KUTOKA KATA YA MASANZE JIMBO LA MIKUMI.

0
0
OFISI YA MBUNGE Jimbo La Mikumi inalaani sana kitendo cha kinyama kilichofanywa na Ndugu zetu wa jamii ya wafugaji kwa kujichukulia sheria mkononi na kumjeruhi vibaya Ndugu Augustino Mtitu mkulima wa kitongoji cha Upangwani, Kijiji cha Dodoma Isanga, Kata Ya Masanze Jimbo la Mikumi ambapo leo tarehe 25 Desemba majira ya Mchana amechomwa mkuki mdomoni na kutokezea nyuma ya shingo yake, ambapo alipelekwa hospitali ya wilayani Kilosa na baadae amekimbizwa hospitali ya mkoa Morogoro  ili kufanyiwa operesheni ya kuondoa mkuki huo na kwa matibabu zaidi.

Augustino Mtitu alishambuliwa na wafugaji wa kimasai alipokuwa akimsaidia jirani yake kufukuza Ng'ombe wasiharibu mazao shambani kwake, Kipande cha mti kinachoonekana hapo mdomoni ndiyo mkuki uliokatwa ili kupunguza urefu wa mkuki huo wakati wakimkimbiza hospitali,  Inasemekana MwenyeKiti wa kijiji na MwenyeKiti wa kitongoji hicho nao wamejeruhiwa.
WITO KWA SERIKALI.
Ofisi Ya Mbunge Mikumi inatoa wito kwa Serikali  kuwabaini wale wote waliofanya kitendo hiki cha kinyama kuhakikisha wanachukuliwa hatua kali za kisheria  ili kuweza kukomesha vitendo hivi vya kujichukulia sheria mkononi inayopelekea kuongezeka kwa uvunjifu mkubwa wa Amani na migogoro isiyokwisha kati ya wakulima na wafugaji wilayani KILOSA.



Imetolewa na:-
Robert A. Galamona
Katibu Ofisi Ya Mbunge
Mikumi.




Kompyuta za Bayport zaifuta machozi Halmashauri ya Same

0
0
Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Mercy Mgongolwa (kulia), akimkabidhi Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Mheshimiwa Said Mecky Sadick moja ya kompyuta sita zilizotolewa na taasisi yao kwa mkoa huo kama msaada wa kuweza kuongeza utendaji kazi mzuri kwa watumishi wa umma, hususan kwa Manispaa ya Moshi, Halmashauri ya Mwanga na Halmashauri ya Same, huku kila moja ikipewa kompyuta mbili. Kushoto kwa RC Sadick ni Katibu Tawala wa Mkoa huo wa Kilimanjaro, Mheshimiwa Aisha Amour. Picha zote na Mpiga Picha Wetu.


Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro.

HALMASHAURI ya Wilaya Same imeanza kupokea faraja za msaada wa kompyuta mbili kati ya sita zilizofikishwa mkoani Kilimanjaro, ikiwa ni siku chache baada ya ofisi yao kuungua moto na kutekeza vifaa mbalimbali vya kiofisi.


Kompyuta hizo zilipokewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mheshimiwa Said Mecky Sadick, akiambatana na wakuu wa idara wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na watumishi mbalimbali kutoka kwenye halmashauri za Same na Mwanga.
Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Mheshimiwa Said Mecky Sadick wa pili kutoka kushoto, akimkabidhi kompyuta hizo alizopokea kwa Taasisi ya Bayport Financial Services, Katibu Tawala wake wa Mkoa, Mheshimiwa Aisha Amour.

Akizungumza mwishoni mwa wiki katika hafla ya kupokea kompyuta hizo, Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Mercy Mgongolwa, alisema wamekabidhi kompyuta hizo, ikiwa ni siku chache baada ya ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Same kuungua moto.


Alisema ingawa msaada wao umekuja kabla ya ofisi hizo kuungua moto, lakini wanaamini kuwa kompyuta hizo zinaweza kupunguza adha ya watumishi wa umma kufanya kazi kwa wakati mgumu, huku zikilengwa kwa Halmashauri ya Same, Mwanga na Manispaa ya Moshi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mheshimiwa Said Mecky Sadick katikati akizungumza jambo na Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Mercy Mgongolwa kulia bada ya kukabidhiana kompyuta sita za msaada kwa Mkoa huo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mheshimiwa Said Mecky Sadick kushoto akimkabidhi kompyuta mwakilishi wa Halmashauri ya Same.

“Taasisi yetu inatoa pole kubwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na watumishi wote wa Same, ila tunaamini kwa kiasi kidogo kompyuta tulizotoa zitawafuta machozi wadau wenzetu wa Same na Serikali yote kwa ujumla hapa nchini,” alisema Mercy.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mheshimiwa Mecky Sadick, aliwashukuru sana Bayport kwa msaada wao wa kompyuta na kuwataka waendelee kuwasaidia watumishi wa Same kwa kuongeza idadi ya kompyuta zao.


“Tunapokea kompyuta hizi kwa mikono miwili lakini tunawaomba wenztu wa Bayport muongeze idadi ya kompyuta kwa Halmashauri ya Same kwa sababu kule kuna uhitaji mkubwa zaidi baada ya ofisi kuungua moto.


“Ofisi yetu imepata pigo kubwa mno hivyo mtusaidie kwa hilo kwa sababu tunafahamu msaada wenu ni muhimu kwetu na taasisi yenu imekuwa karibu sana na jamii kwa kusaidia mambo mbalimbali ya kijamii ambayo yana tija kwetu sote,” alisema RC Sadick.


Utaratibu wa utoaji wa kompyuta 205 kwa ofisi za serikali zenye thamani ya Sh Milioni 500 umeanzishwa ili kuwafanya watumishi wa serikali wafanye kazi zao kwa ufanisi ili kuhamasisha masuala ya kimaendeleo hapa nchini.

MBUNGE WA JIMBO LA NYASA AMBAYE PIA NI NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA, ENG. STELLA MANYANYA ANAWAKARIBISHA WANANCHI KWENYE UZINDUZI WA TAMASHA LA UTALII (NYASA TOURISM FESTIVAL)

Safari ya Mwisho ya Mpiganaji katika tasnia ya Habari, Marehemu Mpoki Bukuku

0
0

Na Humphrey Shao ,Globu ya Jamii

Waziri wa habari, utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye amesema amejifunza mengi kupitia kazi za mwandishi na mpiga picha wa kampuni ya TheGurdianLtd marehemu Mpoki Bukuku kutokana na mchango wake mkubwa katika tasnia ya habari.

"Bukuku ameacha pengo kubwa hivyo hatosahaulika... wanahabari hatuna cha kufanya ila tunamshukuru Mungu na kupitia kazi zake tujifunze yale yote aliyoyafanya," alisema.

Akisoma historia ya Bukuku, kaka wa marehemu, Alfred Mwakaposa alisema marehemu alizaliwa 15/3/1972 katika Hospitali ya Mount Meru mkoani Arusha, akiwa mtoto wa tano kwenye familia ya Bukuku.

Alisema alianza elimu ya msingi katika Shule ya Forodhani, Mlimwa Dodoma na baadae kuhamia Kisarawe, elimu ya sekondari alisoma Canon Andrea mkoani Dodoma na kidato cha tano na sita katika Shule ya Makumira Arusha.

"Baadaye marehemu alijiunga na elimu ya chuo cha uandishi wa habari TSJ ngazi ya cheti na Diploma... Amewahi kufanya kazi katika gazeti la Majira, Mwananchi na kuhamia Guardian mpaka mauti yalipomfika," alisema.

Akizungumza kwa niaba ya wasanii wa filamu, Muigizaji maarufu Steve Nyerere alisema tasnia ya filamu imepata pigo kubwa kumpoteza Bukuku hivyo wanaamini anapoenda ni sehemu nzuri.

"Nimemjua Mpoki wakati tupo Singida, tunaamini anapoenda Mpoki ni sehemu nzuri, tuko pamoja na familia yake, " alisema
Sehemu ya umati wa watu mbalimbali waliojitokeza kutoa heshima zao mwisho kwa mwili wa Marehemu Mpoki Bukuku.
Jeneza lenye mwili wa mpiga picha maarufu Marehemu Mpoki Bukuku likiwa katika eneo la uwanja wa Shule ya Wazazi, Tabata Kimanga jijini Dar mchana huu tayari kwa kutoa heshima za mwisho 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza jambo wakati wa kuagwa kwa mwili wa mpiga picha maarufu Mpoki Bukuku katika eneo la uwanja wa Shule ya Wazazi, Tabata Kimanga jijini Dar mchana huu.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akizungumza jambo wakati wa kuagwa kwa mwili wa mpiga picha maarufu  Mpoki Bukuku.
Mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akitoa salamu za pole kwa familia ya Marehemu Mpoki Bukuku wakati wa kuagwa kwa mwili huo.
Mpigapicha Mkuu wa gazeti la Jambo Lelo pamoja na Muwakilishi wa Bloggers, Richard Mwaikenda akitoa salamu za rambirambi katika Msiba wa Mpoki Bukuku, viwanja vya Shule ya Wazazi, Tabata Kimanga jijini Dar.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

HAJI MANARA AMUOMBEA MSAMAHA JERRY MURO KWA RAIS WA TFF

0
0
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba Haji Sunday Manara amejitokeza kwa mara ya kwanza kumuombea msamaha mtani wake Jerry Muro ili kuifufua upya hamasa na kuongeza ushindani katika ulimwengu wa soka la Bongo.
Jerry Muro ambaye ni Mkuu wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga amefungiwa na TFF kwa muda wa mwaka mmoja kutojihusisha na soka kutokana na matumizi mabaya ya kauli zake kupitia vyombo vya habari mwezi Julai mwaka huu.
Manara katika ujumbe aliouweka kwenye mtandao wake wa Instagram akiuelekeza kwa Rais wa TFF Jamal Malinzi, amesema katika kuadhimisha sikukuu ya Krismasi anaona ni wakati muafaka sasa kwa Rais wa TFF Jamal Malinzi kutumia mamlaka yake kumfungulia Jerry kwa kuwa amekwishatumikia takriban nusu ya kifungo chake na kwamba soka la Bongo linamuhitaji sana kwa sasa.
"Nimekaa nimetafakari sana,nimeamua kumuombea msamaha mtani wangu Jerry Muro ambaye TFF mlimfungia mwaka mmoja kujihusisha na mpira wa miguu, ninafanya hivi nikijua kabisa Jerry alikosea na tayari ameshatumikia karibia nusu ya kifungo chake, ninajua kwa kufanya hivyo atakuwa keshajifunza lugha za kutumia na pia itakuwa fundisho kwetu sisi wasemaji na viongozi wa vilabu kwa ujumla,"ameandika Manara.

Manara pia hakusita kukumbushia jinsi ambavyo Jerry Muro amewahi kumtolea hata yeye mwenye lugha za kuudhi "
"Nnafahamu pia Jerry aliwahi kunitolea lugha zisizostahili mimi bnafsi. Lakini yale yashapita na binafasi amenihakikishia kutorudia tena, na nnaamini viongozi na washabiki wa Simba watanielewa dhamira yangu hii njema, ambayo inathibitisha uungwana tulio nao wanaSimba".
Manara amemaliza kwa kusema kuwa soka la Tanzania linammiss sana Jerry Muro na kuomuomba Rais Malinzi kutumia mamlaka yake kumfungulia kwa kuwa Jerry bado alikuwa hajawa na uzoefu wa kutosha katika siasa za mpira.
Kwa upande wake Jerry Muro amefurahi na kushukuru kuona mtani wake Haji Manara anamkumbuka na kutumia fursa hiyo kuomba msamaha kwa shirikisho la soka Tanzania ili aendeleze hamasa ya soka aliyokuwa ameiweka nchini yeye na Haji Manara.

RAIS WA TFF JAMAL MALINZI AMLILIA MAREHEMU MPOKOI BUKUKU

0
0

Wakati mwili wa Mwanahabari, Mpoki Bukuku ukiagwa leo jijini Dar es Salaam, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi (pichani) ametuma salamu za rambirambi kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Theophil Makunga kutokana na kifo hicho. 

 Mpoki Bukuku alifariki dunia Ijumaa iliyopita, alipokuwa akipatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa vibaya kwa kugongwa na gari eneo la ITV Barabara ya Bagamoyo jijini. 
 Hadi mauti yanamkuta akiwa na umri wa miaka 44, Mpoki alikuwa Mpigapicha wa magazeti ya The Guardian ambako kabla aliwahi kufanya kazi kwa mafanikio makubwa katika kampuni za Mwananchi Communications na Business Times – zote za Dar es Salaam. 
 Rais Malinzi alipokea taarifa za kifo cha mwanahabari huyo kwa masikitiko makubwa na katika salamu za rambirambi pia zimekwenda kwa familia ya marehemu Mpoki Bukuku, ndugu, jamaa na marafiki na kuwataka kuwa na moyo wa subira wakati huu mgumu wa msiba wa mpendwa wao. 
 Rais Malinzi alimwelezea Mpoki Bukuku, wakati wa uhai wake alikuwa na mchango mkubwa katika tasnia ya habari za michezo akitoa mawazo yake hivyo ameacha alama ya ucheshi, kujituma na uwajibikaji katika kufanikisha kazi zake katika vyombo vya habari alivyofanyia kazi. 
 Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya marehemu Mpiki Bukuku mahala pema peponi. 
 Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina la Bwana lihimidiwe - AMINA

ngoma azipendazo ankal: Jim Reeves - This World is not my home

MAGAZETI YA LEO JUMANNE DESEMBA 27, 2016

Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW) kuwanufaisha wanawake wengi nchini Tanzania

0
0
Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani "WOMAN ON WHEEL" (WOW) umelenga kuwapa fursa wanawake kujiajiri na kuajiriwa katika sekta ya usafirishaji kwa kuendesha vyombo vya moto vya abiria na mizigo.
Mradi wa WOW kwa sasa unasajili wanawake kwa ajili ya kuwapatia fursa ya kufundishwa udereva bure katika viwango mbalimbali na baadae kuwatafutia ajira na wengine kuwawezesha ili waweze kujiajiri.
Mradi wa WOW umelenga katika kipindi cha mwezi Disemba hadi Februari uwe umesajili wanawake 600 nchi nzima ili waweze kupatiwa mafunzo.
Lengo kubwa la mradi ni kuondoa mila potofu za mfumo dume wa uwepo wa kazi za kiume na kike.
Mradi wa WOW utawezesha wanawake kushiriki kikamilifu kuchangia pato la taifa kwa kujiwezesha kulipa kodi mbalmbali za serikali kupitia sekta ya usafirishaji.
1
Martin Gabone-Mkurugenzi Mkuu Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW) akizungumza na washiriki wa semina hiyo ya siku moja hawapo pichani, iliyolenga kuwapa fursa wanawake kujiajiri na kuajiriwa katika sekta ya usafirishaji kwa kuendesha vyombo vya moto vya abiria na mizigo kupitia mradi huo.
2
Martin Gabone-Mkurugenzi Mkuu Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW) akizungumza na washiriki wa semina hiyo ya siku moja , iliyolenga kuwapa fursa wanawake kujiajiri na kuajiriwa katika sekta ya usafirishaji kwa kuendesha vyombo vya moto vya abiria na mizigo kupitia mradi huo.
3
Baadhi ya wanawake washiriki wa semina hiyo ya siku moja wakifurahia maelezo na umuhimu wa Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW).
4
Baadhi ya wanawake washiriki wa semina hiyo ya siku moja wakifuuatilia maelezo ya umuhimu wa Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW).
5
Victor Francis-Meneja Mafunzo wa Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW) akielezea jambo wakati alipotoa mafunzo kwa wanawake washiriki wa semina hiyo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Article 1

0
0
 Albam ya Nyuma ya Mlima (DVD) imeingia sokoni ikiwa na nyimbo 6 ambazo ni 

1., Nyuma ya Mlima
2. Tamaa Mbele
3. Penda unapopendwa
4. Yesu wa thamani
5.,Mitihani ya kausha
6. Nawashukuru adui (Ku
 mpiga teke chura)

MSAMA AVIKUMBUKA VITUO VYA WATOTO YATIMA JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
Bw. Alex Msama akikabidhi msaada wa chakula kwa Bi.Zainab Bakari mlezi wa kituo cha kulea watoto yatima cha Maunga Yatima Centre kilichopo Kinondoni jijini Dar es salaam wakati alipotembelea kituoni hapo na kuzungumza na watoto, Msama aligawa chakula pia katika vituo vya Honorata Temeke, Shifaa Bunju na Mwandalio kilichopo Temeke Vetenary vyote vya jijini Dar es salaam. 
Msama ametoa wito kwa watu mbalimbali wenye uwezo kwa namna yoyote wajitokeze kuwasaidia watoto yatima na wasiojiweza kwa kutoa misaada mbalimbali ili jamii hiyo nayo ifurahie msimu wa sikukuu kwa furaha kama wengine.
 Bw. Alex Msama akikabidhi msaada wa 
chakula kwa kituo cha Shifaa -Bunju.

  Bw. Alex Msama akiwaasa watoto wa kituo cha Honorata kutoka Temeke,wakasherehekee sikukuu kwa upendo na amani na kwa umoja wao wakamshukuru Mungu kwa kila jambo.
Bw. Alex Msama akikabidhi msaada wa chakula kwakituo cha Mwandalio cha Vetenary Temeke.
Viewing all 109611 articles
Browse latest View live




Latest Images