Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

Vyuo India vyaeleza vinavyoweka ulinzi vyuoni

$
0
0
BAADHI ya maofisa kutoka vyuo vikuu vya India ambao wamekuwa wakishirikishi maonyesho ya vyuo vya nje yaliyofanyika tarehe 14 hadi 15 Desemba Dodoma, wameeleza namna vyuo nchini mwao vinavyoweka kipaumbele katika ulinzi wa wanafunzi wao.

Ofisa kutoka Chuo Kikuu cha Lovely (LPU), Love Kumar alisema, katika maonyesho hayo yaliyoandaliwa na Kampuni ya wakala wa vyuo vya nje, Global Education Link (GEL) kuwa kwa mfano katika chuo chake kuna kamera nyingi zilizofungwa katika maeneo mbalimbali kuchunguza kila kinachoendelea.

“Tunatamani kuona watu wanakuja kwetu na kusoma kwa amani, India ni nchi ya amani. Hata hivyo tumeweka zaidi ya kamera 4000 kuhakikisha kila kitu kinaangaliwa kwa ufasaha” aliongeza Kumar.

Naye Mratibu wa wanafunzi wanaotoka nje kutoka Chuo Kikuu cha Maharishi Markandeshwar, Rashmi Garg alisema hali ni hivyo pia katika chuo hicho. Alifafanua kwamba sababu ya kufunga vifaa vya ulinzi ni kuendelea kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa.
Mojawapo ya majengo ya Chuo Kikuu cha Lovely nchini India. Global Education Link (GEL) ni mwakilishi rasmi wa chuo hiki hapa nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel, aliwahakikisha Watanzania kwamba kampuni yake inafanya inaloweza kuhakikisha Watanzania wengi zaidi wanakwenda nje ya nchi kupata ujuzi ambao watarudi nao nchini kwa ajili ya kusaidia kukuza maendeleo.

MHANDISI NGONYANI AMUAGIZA MKANDARASI KUMALIZA UJENZI MAPEMA

$
0
0
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani (Wa tatu kulia) akijadiliana jambo na Mkandarasi wa kampuni ya Rv associates India& AES Tanzania anayejenga Daraja la Kilombero. Daraja hilo lipo katika barabara kuu ya Ifakara –Mahenge Mkoani Morogoro.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani amemuagiza Mkandarasi wa kampuni ya Rv associates India & AES Tanzania  anayejenga daraja la Kilombero lenye urefu wa mita 384 kukamilisha ujenzi huo mapema ifikapo januari mwakani  ili daraja hilo lianze kutumiwa na wananchi wa Mkoa wa Morogoro.

Mhandisi Ngonyani ametoa agizo mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo lenye urefu wa mita 384 linalounganisha  barabara kuu ya Ifakara –Mahenge mkoni Morogoro.

“Wananchi wa Ifakara wanahamu ya kuona daraja hili linakamilika na kuanza kutumika mapema, hivyo ongezeni kasi ya ujenzi wa daraja hili ili likamilike haraka na kwa ubora uliokusudiwa ili liweze kudumu na kutumika kwa muda mrefu”. amesisitiza Mhandisi Ngonyani.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani (Wa kwanza kushoto) akipata maelezo Ujenzi wa Daraja la Kilombero kutoka kwa Mkandarasi wa kampuni ya Rv associates India& AES Tanzania. Daraja hilo lipo katika barabara kuu ya Ifakara –Mahenge Mkoani Morogoro.

Ameongeza kuwa kukamilka kwa daraja hilo kutawafanya wananchi kuachana na usafiri wa kutumia kivuko cha Mv. Kilombero ambacho wakati wa mvua kubwa hushindwa kutoa huduma za usafiri kwa wananchi hao na hivyo kukwamisha shughuli zao za kimaendeleo.

Katika hatua nyingine Mhandisi Ngonyani amekagua barabara ya kuu ya kitaifa (Trunk roads) ya kutoka Mikumi-Mahenge, Kilosa kwa mpepo-Londo ambopo amesema kuwa Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya Kidatu –Ifakara(KM 67) kwa kiwango cha lami ifikapo machi mwakani wakati barabara ya Lupilo hadi Lumecha upembuzi yakinifu unaendelea.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya mji Ifakara Bw. Mashaka Mbilinyi ameelezea umuhimu wa barabara hiyo kuwa itakuwa kichocheo cha mendeleo ya kiuchumi kwa majimbo manne ya Mlimba, Malinyi, Ulanga na Kilombero.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani (Wa pili kulia), akiendelea na ukaguzi wa sehemu ya juu ya daraja la Kilombero.

“Barabara hii itakapokamilika itawawezesha wananchi kupata huduma katika sehemu mbalimbali za majimbo yetu na pia kusafirisha kusafirisha mizigo ya nafaka kwenda katika masoko mbalimbali na hivyo kukuza kipato cha mwananchi na taifa kwa ujumla”. amesema Bw. Mbilinyi.

KUTOKA TELEVISHENI LEO

$
0
0

SIMU.tv: Rais Magufuli amemteua rasmi Prof. Yunus Mgaya kuwa mkurugenzi mkuu wa NIMR kufuatia utenguzi wa mkurugenzi wa awali.  https://youtu.be/D71HdEO1l3U

SIMU.tv: Mwanafunzi wa shule ya Sekondari mkoani Mbeya amefariki dunia baada ya kugongwa na gari  la mbunge wa Mbeya mjini Mhe. Joseph Mbilinyi. https://youtu.be/eVfHRdZ9erE

SIMU.tv: Mtu mmoja amabye jina lake halikufahamika ameuawa na mwili wake kutupwa kwenye boma ambalo halijaisha huko mkoani Geita. https://youtu.be/79SXghJzLjM

SIMU.tv: Mkuu wa mkoa wa Geita amesema hatasita kuwasaka na kuwakamata waganga wote wa jadi wanaopiga ramli chonganishi na kusababisha mauaji ya vikongwe. https://youtu.be/6KsJZEPzFZ8

SIMU.tv: Mchezaji Rish Vipul Somaiya amesema maendeleo ya mchezo kitaifa na kimataifa hutegemea uendelezaji wa vipaji toka ngazi za chini. https://youtu.be/-zDmJysIM10

SIMU.tv: Ligi ya kandanda Tanzania bara msimu wa pili imeanza kutimua vumbi hii leo  kwa mechi kadhaa kuchezwa huku Yanga ikianza kwa ushindi mnono. https://youtu.be/mV7A-X-7v-I

SIMU.tv: Mganga mkuu wa serikali ametoa wito kwa watafiti nchini wametakiwa kutumia lugha inayoeleweka kwa jamii; https://youtu.be/Lz0ux3jXid0

SIMU.tv: Chama Cha Mapinduzi CCM kimeibuka kidedea katika uchaguzi wa Umeya wa Manispaa ya Kigamboni katika uchaguzi uliofanyika hii leo; https://youtu.be/JIYS_CFdsos

SIMU.tv: Waziri mkuu Kassim Majaliwa ametoa wito kwa idara zinazosimamia mipaka ya nchi kudhibiti wahamiaji haramu; https://youtu.be/wanvzWtVuMo

SIMU.tv: Mkuu wa wilaya ya Kisarawe amewakamata na kuwaweka ndani wenyeviti na maafisa wendaji wa vijiji vitatu kwa kusababisha migogoro ya ardhi; https://youtu.be/8Oo4PWDuttA

SIMU.tv: Serikali imesema itatoa kipaumbele kwa wakandarasi wazawa katika ujenzi wa reli mpya ya kisasa; https://youtu.be/9AC9VFiA-GM

PROF. MBARAWA AAGIZA BARABARA YA MAKUTANO-NATA YA KM50 IKAMILISHWE

$
0
0
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maagizo kwa Mhandisi Mshauri Eng. Domicus Mapunda wa Kampuni ya Ujenzi ya Mbutu Bridge JV inayojenga barabara ya Makutano-Nata KM 50 kwa kiwango cha lami mkoani Mara wakati alipokagua mradi huo.

 Ujenzi wabarabara ya Makutano-Nata KM 50 inayojengwa kwa kiwango cha lami, wilaya ya Butiama, mkoani Mara ukiendelea.

 Kaimu Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Musoma Bi. Faraja akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto), ramani ya eneo la kiwanja cha ndege hicho, alipokagua kiwanja hicho mkoani Mara.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Musoma Bi. Faraja kuhusu eneo litaloongezwa kiwanja hicho, mkoani Mara. 

SUZA 12th GRADUATION CEREMONY

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI DESEMBA 18, 2016

WAZIRI MKUU AZUNGUMZIA KUHUSU FARU JOHN KATIKA MAJUMUISHO YA ZIARA MKOA WA ARUSHA

TIMU YA KIJITONYAMA VETERANS WAFANYA MKUTANO WA KUPATA VIONGOZI WAPYA

$
0
0
 TIMU ya Kijitonyama Veterans yenye maskani yake Kijitonyama, leo imefanya uchaguzi mkuu na kupata viongozi wapya wa kuingoza timu hiyo kwa kipindi cha miaka mitano.

Nafasi zilizokuwa zikigombewa ni tisa, ambapo katika nafasi ya Mwenyekiti aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo muda uliopita, Lupyana Michael, ameendelea kubaki katika nafasi hiyo baada ya kupigiwa kura na wajumbe na kuongoza dhidi ya mpinzani wake, Petro Malima .

Pia aliyekuwa Katibu Mkuu wa Timu hiyo Amon Petro, naye ameendelea kubaki katika nafasi hiyo baada ya kuibuka na kura nyingi zaidi ya mpinzani wake, Evodius Mtawala

Naye Mratibu wa timu hiyo, Majuto Omary,pia ameendelea kubaki katika nafasi hiyo baada ya kuibuka kidedea dhidi ya mpinzani wake Evans Malla, 

Kwa mujibu ya utaratibu wa Timu hiyo, kutokana na mapendekezo ya Wajumbe, katika uchaguzi, majina mawili yanayopigiwa kura na mmoja kati yao anayepata kura nyingi ndiye anapaswa kuwa kuwa kiongozi katika nafasi husika na anayefuatia kwa kura anakuwa msaidizi.

VIONGOZI WALIOCHAGULIWA:-

MWENYEKITI:  Lupyana Michael
MAKAMU MWENYEKITI: Malima Petro

KATIBU MKUU: Amon Petro
KATIBU MSAIDIZI: Evodius Mtawala

MRATIBU MKUU: Majuto Omary
MTARIBU MSAIDIZI: Evans Malla

MWEKAHAZINA MKUU: Othaman Hussein 
MWEKA HAZINA MSAIDIZI: Sweetbert Mwombeki

MSEMAJI WA TIMU: Muhidin Sufiani (Mafoto)

 Baadhi ya wajumbe wakipitia vifungu vya katiba wakati wa uchaguzi huo.


Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli aungana na wana Parokia wenzake kusali ibada ya Jumapili

$
0
0

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli leo Jumapili ameungana na Wakristo wenzake wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Petro iliyopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam ikiwa ni wiki kadhaa tangu alipougua na kulazwa hospitali.

Akiwa mwenye afya njema na furaha Mama Magufuli aliyekuwa pamoja na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wamesali ibada ya asubuhi katika kanisa hilo na baadaye kusalimiana na waumini nje ya kanisa.

Baada ya kumalizika kwa Ibada, baadhi ya Waumini wa Kanisa hilo wameelezea furaha yao ya kumuona Muumini mwenzao akiungana nao katika ibada na wamemuombea afya njema. "Nimejisikia furaha sana kumuona Mama Magufuli amekuja Kanisani akiwa na afya njema na uso wa bashasha, na ninamuombea kwa Mungu aendelee kumsimamia" amesema Mama Mabula.

"Nimeshukuru sana kumuona Mama yangu Mama Magufuli, Mwanajumuiya mwenzangu leo Kanisani, huku afya yake ikiwa imetengemaa zaidi, tunamshukuru sana Mwenyezi Mungu na tunamuombea aendelee kumpigania afya yake izidi kuwa imara" amesema Thomas Simon.

"Kwa kweli siku ya leo kwangu mimi ninafuraha sana kwa kumuona Mama akiwa kanisani, na zaidi Mama wote wawili kwa sababu pia amekuja Mke wa Mhe. Waziri Mkuu, kwa hiyo kwetu sisi ni furaha sana kama Parokia, tunafurahi sana tunaposhirikiana na viongozi wetu" ameongeza Epifania Ngonyani.

Mwezi uliopita Mama Janeth Magufuli aliugua na kulazwa katika wodi ya Sewahaji iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako alipata matibabu kwa siku mbili na kisha kuruhusiwa.

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipokea komuniyo kutoka kwa Padre Paul Haule wa Kanisa la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam. 
1Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa katika Ibada ya Jumapili katika Kanisa la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam. wa kwanza kulia kwake ni Dada yake Ester Enock na anayefuata ni Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa. 

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akifuatilia Mahubiri yaliyotolewa na Padre Paul Haule wa Kanisa la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akifuatilia Mahubiri yaliyotolewa na Padre Paul Haule wa Kanisa la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akizungumza na baadhi ya waumini akiwemo muuza magazeti maarufu Bw. Bonge nje ya Kanisa la Mtakatifu Petro, Oysterbay Jijini Dar es Salaam.

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa nje ya Kanisa la Mtakatifu Petro, Oysterbay Jijini Dar es Salaam.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWAKUNA WAPINZANI KIKAO CHA MAJUMUISHO ZIARA YA ARUSHA

$
0
0
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika kikao cha majukmuisho ya ziara yake ya mkoa wa Arusha kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha, Desemaba 18, 2016. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo  na kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Arusha, Lekule Laiza.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
  Baadhi ya Wenyeviti wa halmashauri  za mkoa wa Arusha wakisikiliza kwa makini hotuba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ya majumuisho ya ziara yake ya mkoa  huo  kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha Desemba 18, 2016. 
 Wabunge wa Arusha wakifuhia hotuba ya majumuisho ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ya kuhitimisha ziara yake ya mkoa huo kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha , Desemba 27, 2016. Kutoka kushoto ni  Mbunge wa Arumeru Magharibi, Gipson Mesiek, Mbunge wa Viti Maalum Amina Mollel na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Baadhi ya Wenyeviti wa halmashauri  za mkoa wa Arusha wakisikiliza kwa makini hotuba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ya majumuisho ya ziara yake ya mkoa  huo  kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha Desemba 18, 2016. 9Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari, akionyesha ishara ya kukubaliana na maneno ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipotoa hotuba ya majumuisho ya ziara yake mkoani Arusha kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Desemba 28, 2016. Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum, Amina Mollel.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (kushoto) wakizungumza na Mbunge wa Monduli, Julius Kalanga (wapili kulia) na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Monduli, Isaac Joseph (kulia) baada ya Waziri Mkuu kumaliza kikao cha majumuisho ya ziara yake mkoani Arusha kwenye ukumbi wa Mkuu wa mkoa huo, Desemba 18, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)​.

HII NDIO RATIBA RASMI YA MAPINDUZI CUP INAYOANZA DESEMBA 30, 2016

$
0
0
30/12/2016  
Taifa ya Jang'ombe vs Jang'ombe boys saa 2:30 usiku.

1/1/2017 
KVZ VS URA Saa 10:00 alasiri, 
Simba vs Taifa ya Jang'ombe saa 2:30 usiku
.
2/1/2017 
Azam vs Zimamoto saa 10:00 alasiri,
Yanga vs Jamhuri saa 2:30 usiku.

3/1/2017 
Jang'ombe Boys vs URA saa 10:00 alasiri,
KVZ vs Simba saa 2:30 usiku.

4/1/2017 
Zimamoto vs Yanga saa 10:00 alasiri, 
Jamhuri vs Azam saa 2:30 usiku.

5/1/2017 
KVZ vs Jang'ombe boys saa 10:00 alasiri,
 Simba vs URA saa 2:30 usiku.

6/1/2017  
Taifa ya jang'ombe vs KVZ saa 2:30 usiku.

7/1/2017  
Jamhuri vs Zimamoto saa 10:00 alasiri, 
Yanga vs Azam saa 2:30 usiku.

8/1/2017 
Simba vs Jang'ombe boys saa 10:00 alasiri ,
Taifa ya jang'ombe vs URA 2:30 usiku.

10/1/2017  
  Saa 10: 00 nusu fainali ya kwanza ,  
Saa 2:30 nusu fainal ya pili.

13/1/2017         
FAINALI
   saa 2: 30 usiku.

WAZIRI MKUU AUNDA TUME YA KUCHUNGUZA TAARIFA ZA UHAMISHO WA FARU JOHN,AAGIZA KABURI LAKE LITAFUTWE.

$
0
0
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imeunda tume kuchunguza taarifa inayoelezea utaratibu uliotumika kumhamisha faru John kutoka Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Sasakwa Black Rhino Sanctuary iliyoko kwenye Hifadhi ya Grumeti Serengeti pamoja na kutafuta kaburi la faru huyo.

Amesema timu hiyo ya wataalamu tayari imeshafika Sasakwa  VIP Grumet kwa ajili ya kutafuta kaburi na kuchukua vinasaba vya masalia ya faru John na kisha watakwenda kwenye Hifadhi ya Ngorongoro kuchukua vinasaba vya watoto wake  na kuvilinganisha na pembe hiyo ili  kubaini kama kweli pembe aliyopelekewa ni  ya faru John au la.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumapili, Desemba 18, 2016) wakati wa majumuisho ya ziara yake ya kikazi mkoani Arusha. Ziara hiyo ililenga kukagua utekelezaji wa shughuli za maendeleo na kuona utoaji wa huduma kwa wananchi. 

"Tume niliyounda kwa ajili ya uchunguzi wa faru John imetua VIP  Grumet Serengeti kujiridhisha kama kuna kaburi la faru John na kama lipo wachukue vinasaba na baada ya hapo watakwenda Creter na kuchukua vinasaba vya watoto wa faru John na kuvipima kwa pamoja. Lengo ni kutaka kubaini kama pembe iliyowasilishwa kwangu Disemba 9 mwaka huu ni ya faru John,” amesema.

Waziri Mkuu amesema wakati faru John akiwa V I P Grumet taarifa zilisema ni mgonjwa na daktari alipompima mara ya kwanza akabaini faru huyo hakuna na ugonjwa wowote.”Daktari alimpima tena kwa mara ya pili taarifa zikasema tena si mgonjwa  ghafla wakasema amekufa. Hili  haliwezekani,”.

Waziri Mkuu amesema ameiagiza timu hiyo kufanya kazi ya uchunguzi wa taarifa hizo kikamilifu kwa sababu Serikali imetumia fedha nyingi kuwaleta faru hao kutoka nchini Afrika Kusini. Ni lazima nyara hizo za Serikali zilindwe kwa manufaa Taifa. 

Waziri Mkuu alipokea taarifa inayoelezea utaratibu uliotumika kumhamisha faru John kutoka Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Sasakwa Black Rhino Sanctuary iliyoko kwenye Hifadhi ya Grumeti Desemba 9, 2016 katika kikao kilichofanyika kwenye makazi ya Waziri Mkuu Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe na baadhi ya watendaji wa wizara yake, Baada ya kupokea taarifa hiyo Waziri Mkuu alisema taarifa hiyo itafanyiwa kazi na wataalamu wa ofisi yake.Akisoma taarifa hiyo mbele ya Waziri Mkuu, Prof. Maghembe alisema hadi kufikia Desemba 2015 wakati faru John anahamishwa alikuwa na watoto 26 (sawa na asilimia 70.2) ya faru wote waliokuwepo ndani ya kreta. 

“Kati ya faru 37 waliokuwepo ndani ya kreta, watoto wake walikuwa 26 sawa na asilimia 70.2. Uamuzi wa kumuondoa John ulikuwa ni muhimu ili kuwezesha kuongezeka kwa faru weusi na kupunguza tatizo la ‘inbreeding’ ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro,” alisema Waziri Maghembe. 

Baada ya kuhamishiwa Sasakwa, Waziri Maghembe alisema Julai 10, 2016 afya ya faru John ilianza kudorora na alikufa tarehe 18 Agosti, mwaka huu.
 Taarifa hiyo iliandaliwa na Kamati ya Taifa ya Kuwalinda Tembo na Faru. Kamati hiyo inaundwa na Mkurugenzi Mkuu wa TAWIRI, Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Mkurugenzi Mkuu wa NCAA na Mhifadhi Mkuu wa Ngorongoro.
 Akikabidhi pembe za faru huyo mbele ya Waziri Mkuu, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Kupambana na Ujangili wa Wanyamapori, Bw. Robert Mande alimweleza kwamba pembe kubwa ya faru John ilikuwa na uzito wa kilo 3.6 na pembe ndogo ilikuwa na uzito wa kilo 2.3.

Desemba 6, mwaka huu, akiwa ziarani mkoani Arusha, Waziri Mkuu aliuagiza uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), umletee nyaraka zote zilizotumika kumhamisha faru maarufu kwa jina la ‘John’ kutoka kwenye hifadhi hiyo ifikapo Alhamisi, Desemba 8.

Alitoa agizo hilo alipotembelea ofisi za makao makuu ya NCAA zilizoko wilayani Ngorongoro, mkoani Arusha na kuzungumza na watumishi wa mamlaka hiyo pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wafugaji ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani humo.

                                                  IMETOLEWA NA:                                                         
OFISI YA WAZIRI MKUU,

JUMAPILI, DESEMBA 18, 2016.   

wawekezaji kutoka Uingereza waonesha nia kuwekeza katika usafiri wa majini kisiwani mafia

$
0
0
Mbunge wa Mafia Mhe Mbaraka Dau akiwa na wawekezaji kutoka Oxford, Uingereza, leo asubuhi wakiwa katika gati la Kilindini huko Mafia, mkoa wa Pwani. Wawekezaji hao, kwa mujiu wa Mhe dau,  wameonesha nia ya kuwekeza katika usafiriwa majini, ambapo wana mpango wa kuleta boat ya kisasa kurahisisha usafiri kutoka Kilindoni  hadi  Nyamisati katika mkoa wa pwani



uzinduzi wa duka la Mikono Fair trade lililopo jijini Dar es salaam

$
0
0
Wajasiriamali wadogo na wakati(SME) nchini wametakiwa kuboresha huduma zao ikiwa pamoja na kuzalisha bidhaa zinazoweza kushindana katika soko la ndani na nje ya nchini. 
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw.Charles Mwijage amesema dawa pekee kwa wajasiriamlai kushinda masoko ni kutengeneza bidhaa zenye ubora wa hali ya juu. 
“Nchi yeyote duniani ambayo imepiga hatua ya viwanda na maendeleo , mchango mkubwa umetoka kwa wajasiriamali,” alisema Bw.Mwijage

Akifungua duka la Mikono fair trade Shop linalomilikiwa na Mikono Cultural Heritage Ltd ambalo linauza bidhaa zinazotengenezwa na wajasiriamali wadogo wa hapa nchini, Waziri Mwijage alielezwa kulidhishwa na bidhaa zilizokuwa dukani hapo. 
Alisema Serikali itatoa ushirikiano kwa wajasiriamali katika kuwakuza kwa kuwatafutia masoko ya bidhaa zao na pia kuwapatia elimu zaidi ya namna ya kuboresha bidhaa ili kuwendana ushidano wa soko.

“kazi kubwa iliyopo ni kuhakikisha bidhaa hasa za kitamaduni nchini zinapatikana katika duka hili,” alisema Waziri Mwijage na kuongezea kuwa hivyo ndivyo yanavyofanya maduka trade fair duniani kote.

Alisema kampuni hii inashirikiana vizuri na UTT microfinance hivyo wanaweza kukopeshwa na kukuza uzalishaji wa bidhaa ili kwendana na mahitaji ya soko. 
Alisema tufikirie zaidi katika kuuza bidhaa zetu nje ya nchini kwani soko bado ni kubwa tatizo ni uzalishaji na viwango. 
Aliwapongeza kwa kubuni jiko ambalo limekuwa na soko  kubwa hapa nchini na kuwataka waongeze uzalishaji wa majiko hayo na kutoa wito kwa watanzania kupenda kutumia bidhaa zinazozalishwa nchini badala.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mikono Cultural Heritage, Bw.Henry Clemens alisema uwepo wa duka hili utasaidia kukuza soko la ndani la bidhaa za kitamaduni zinazozalishwa na wajasiriamaliv nchini. 
“dhana ya serikali ya viwanda itatusaidia kulinda soko la bidhaa za ndani na wajasiriamali kunufaika,” alisema Bw.Clemens

Alisema tunaishukuru Serikali kwa kuwa na dhamira ya dhati ya kukuza viwanda hasa vidogo kwani ndio msingi wa maendeleo ya viwanda, tutajitahidi kuhakikisha bidhaa zetu zinakuwa na ubora na kukidhi ushindano wa soko ndani na nje ya nchi. 
Naye Mkurugenzi wa Shirika la Maonyesho la Dunia kwa upande wa Afrika (World Fair Trade Organisation- AFRICA (WFTO-AFRICA), Bw.Bernard Outah kutoka Kenya alisema uzinduzi wa duka hili ni mwanzo nzuri wa kukuza biashara kwa wajasiriamali toka Tanzania.

“jambo kubwa ni kukuza uzalishaji wa bidhaa zenye viwango vya kimataifa ili ziweze kuuzika katika mataifa mengine” alisema Bw.Outah 
Aliongezea kuwa masoko yapo mengi changamoto ni upatikanaji wa bidhaa bora na kwa idadi kubwa, hivyo tukiweza haya viwanda vyetu vitakuwa na kufanya uchumi wa nchi kukua. 
Robino Ntila ni Msanii - uchoraji na uchapaji alisema kwa uwepo wa duka hili bidhaa zao zitakwenda kuuzika kwa bei halali yenye manufaa kwako kuliko ilivyokuwa zamani kwani wamekuwa wakiranguliwa na wait wa kati. 
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw.Charles Mwijage (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka la Mikono Fair trade lililopo jijini Dar es salaam. duka hilo linalomilikiwa na Mikono Cultural Heritage Ltd litakuwa likiuza bidhaa za kitamaduni za wajasiriamali ikiwa ni moja ya njia ya kukuza sekta ya viwanda nchini. kulia ni Mwenyekiti wa Bodi wa kampuni hiyo,Bw.Henry Clemens, wapili kulia ni Mkurugenzi wa  Shirika la Maonyesho Duniani kwa upande wa Afrika (World Fair Trade Organisation- AFRICA (WFTO-AFRICA), Bw.Bernard Outah. kushoto kwake ni Mkurugenizi wa kampuni hiyo Bw.Deo kafwa na wapili kushoto ni Mbunge wa Temeke Bw.Abdala Mtolea.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw.Charles Mwijage akipokea zawadi ya jiko toka kwa Mwenyekiti wa Bodi wa kampuni ya Mikono Cultural Haeritage,Bw.Henry Clemens mara baada ya kuzindua duka la mikono fair tradelitakalouza bidhaa mbalimbali za kitamaduni za wajasiriamali ikiwa ni moja ya njia ya kukuza sekta ya viwanda nchini. katikati ni Mkurugenzi wa viwanda vidogo na biashara ndogo wa Wizara ya viwanda,biashara na uwekezaji, Dkt. Consolata Ishebabi

AZAM, AFRICAN LYON ZAVUTANA SHATI UWANJA WA UHURU JIJINI DAR LEO, ZAGAWANA POINT MOJA MOJA KWA SULUHU YA 0-0

$
0
0
Mshambuliaji wa Timu ya Azam Fc, Yahaya Mohamed akiutulisha mpira mbele ya Mabeki wa Timu ya African Lyon, katika Mchezo wa muendelezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa ni Mzunguko wa pili, uliochezwa jioni ya leo katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Mechi hiyo imemalizika kwa suluhu ya ya bila kufungana 0-0.
Beki wa Azam Fc, Aggrey Moris akijaribu kutaka kuuzuia mpira uliokuwa umeelekezwa langoni kwao, katika Mchezo wa muendelezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa ni Mzunguko wa pili, uliochezwa jioni ya leo katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Mechi hiyo imemalizika kwa suluhu ya ya bila kufungana 0-0.
Beki wa Timu ya African Lyon, Bakari Jaffary akiruka juu na kuchukua mpira mbele ya Mshambuliaji wa Timu ya Azam Fc, John Bocco, katika Mchezo wa muendelezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa ni Mzunguko wa pili, uliochezwa jioni ya leo katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Mechi hiyo imemalizika kwa suluhu ya ya bila kufungana 0-0.
Kipa wa Timu ya African Lyon, Rostand Youth akipitwa na mpira ulioelekezwa langoni mwake na Mshambuliaji wa Timu ya Azam Fc, Yahaya Mohamed, goli ambalo lilikataliwa na Mwamuzi kutokana mchezi huyo kuwa ameotea.
Kipa wa Timu ya African Lyon, Rostand Youth akionekana ni mwenye maumivu makali baada ya kuumia alipokuwa akijaribu kuokoa moja ya hatari zilizoelekwa langoni kwake na kupelekea kujigonga kwenye moja ya nguzo za goli sehemu za mbavu na kupelekea kushindwa kabisa kuendelea na mchezo huo.


JAMII YATAKIWA KUHESHIMU HAKI ZA WATU WENYE ULEMAVU - DKT. POSSI

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu, Mhe. Dkt. Abdallah Possi ameitaka jamii kuzingatia haki na usawa kwa watu wenye ulemavu nakuondokana na imani potofu za kuona watu wenye ulemavu hawana uwezo wa kufanya shughuli za maendeleo.

Mhe. Possi ameyasema hayo kwa nyakati tofauti alipotembelea Vituo na Shule zinazohudumia watu wenye mahitaji maalum vya Nandanga, Rasi Bula, Shule ya msingi Nyangao mkoani Lindi pamoja na makazi ya wenye ulemavu na Ukoma ya Mkaseka, Chuo cha wenye Ulemavu cha Mtapika, shule ya Lulindi na Masasi mkoani Mtwara.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mhe. Selemani Mzee (wa kwanza kulia) wakati wa ziara yake katika shule ya Masasi yenye kuhudumia wenye ulemavu Mkoani Mtwara.

Katika ziara hiyo Mhe.Possi alisisitiza jamii zibadili mitazamo hasi juu ya masuala ya haki na usawa kwa watu wenye ulemavu kwa kuwashirikisha katika shughuli zote na kuwapa vipaumbele vya fursa sawa.

“Ninasisitiza jamii ibadili mitazamo dhaifu juu ya haki na usawa wa kuwashirikisha watu wenye ulemavu kwani wana uwezo wa uzalishaji endapo tutawapa fursa sawa kama ilivyokuwa kwa wakina mama walipoachwa nyuma muda mrefu ila jamii imeona fursa ndani yao, iwe hivyo hivyo kwa watu wenye ulemavu” alisema.

Aidha Waziri Possi ameweka mkazo juu ya kuwahusisha na kutokuwaona kuwa ni kundi la kuachwa nyuma na kama tegemezi.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akionesha namna ya kutumia Kurunzi ya mwanga wa jua kwa baadhi ya wazee wenye ukoma wanaoishi katika Kambi ya Mkaseka Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara na kuwapatia wazee hao kurunzi 20 kwa kila nyumba.

“sheria zipo wazi kabisa zinazotuelekeza juu ya haki na usawa kwa watu wenye ulemavu kwa mujibu wa matakwa ya Sheria ya watu wenye Ulemavu namba 9 ya mwaka 2010 inayoeleza haki za watu wenye Ulemavu kuwahudumia kwa haki na usawa na kuboresha maeneo muhimu ikiwemo fursa za kielimu, ajira, kiuchumi na kijamii,” alieleza.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe. Joseph Mkirikiti alikiri kuyapokea yote aliyoeleza Mhe.Waziri katika ziara yake na kuipongeza Serikali kwa juhudi za kuisaidia jamii bila kujali hali zao na tofauti zao.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi (wa kwanza kushoto) akiwa katika ziara ya kuangalia maeneo ya shule ya Masasi inayohudumia wanafunzi wa mahitaji maalum wakati wa ziara yake mkoani Mtwara.

“Ninaipongeza Serikali ya Awamu ya Tano inayowajali wanyonge na kujali haki zao pamoja na mhe. Waziri kwa kuona umuhimu wa kututembelea wana Ruangwa na tunaahidi kukuweka katika kumbukumbu zetu maana umewagusa wakazi wa Mtwara hususani wazee na watu wenye ulemavu.”Alisisitiza Mkuu wa Wilaya hiyo.

LUKUVI AZUNGUMZA NA WANANCHI MKOANI MARA, ATATUA MIGOGORO YA ARDHI

$
0
0
Na. Hassan Mabuye (Kitengo cha Mawasiliano - Wizara ya Ardhi)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi anaendelea na Ziara zake za utatuzi wa Migogoro ya Ardhi nchini, ambayo imejikita zaidi katika kutatua migogoro ya ardhi ya Mikoa ya kanda ya Magharibi, Kaskazini na ile ya Kanda ya Ziwa hapa nchini.

Mhe. Lukuvi kwa siku ya jumatatu tarehe 19 Desemba 2016 atatua migogoro ya ardhi ya wilaya ya Musoma mkoani Mara na siku ya jumanne tarehe 19 Desemba 2016 atatua migogoro ya ardhi ya wilaya ya Bunda mkoani Mara.

Katika ziara hiyo Waziri Lukuvi atakutana na wananchi wa Musoma mjini na wananchi wa Bunda walio na kero za migogoro ya ardhi na kuzitatua pamoja na kutembelea miradi inayosimamiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika wilaya ya Musoma.

Aidha, Mhe. Lukuvi baada ya ziara hiyo anatarajiwa kuwasili mkoani Arusha ambapo pia atatua migogoro ya ardhi inayoukabili mkoa huo.

Hadi sasa Mhe. Lukuvi ndani ya mwezi huu wa Desesmba ameishatatua migogoro ya ardhi ya Mkoa wa Kigoma na wilaya zake za Kigoma mjini, Kasulu na Kibondo na katika Mkoa wa Shinyanga na wilaya zake za Kishapu na Shinyanga mjini na katika mkoa wa Geita amefanya ziara katika wilayani Chato.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiongea na wananchi walio na migogoro ya ardhi wakati wa ziara zake mikoani.
Muonekano wa Halmashauri ya Musoma Mjini.

BARABARA YA LOLIONDO-MTO WA MBU KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI

$
0
0
Serikali imesema ipo katika hatua za mwisho za kuanza ujenzi wa Barabara ya Loliondo- Mto wa Mbu yenye urefu wa KM 218 itakayojegwa kwa kiwango cha lami ili kurahishisha usafiri na usafirishaji wa mizigo kwa wananchi wa  mikoa ya Mara, Manyara, Arusha na Mwanza.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa katika kijiji cha Sale, wilayani Ngorongoro mara baada ya kukagua barabara hiyo ambayo ni kiungo kati ya mikoa hiyo minne na nchi jirani ya Kenya.

"Tumeshatangaza Zabuni kwa ajili ya ujenzi wa barabara hii, mapema mwakani zitafunguliwa ili kumpata mkandarasi ambae atajenga barabara hii kwa kiwango kilichobora", amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Aidha,Waziri huyo amefafanua kuwa ujenzi wa barabara hiyo utatekelezwa kwa awamu mbalimbali ambapo awamu ya kwanza itahusisha ujenzi wa barabara ya kutoka katika kijiji cha Waso -  Sale  yenye urefu wa KM 49.

Ameongeza kuwa barabara hiyo ikikamilika itaungana na ile ya Makutano-Nata yenye urefu wa KM 50 iliyopo Wilaya ya Butiama, mkoani Mara na itasaidia kupunguza kero ya usafiri na kufungua mikoa hiyo  kibiashara kwa wakazi wa maeneo hayo.

Amewataka wananchi wa maeneo hayo kutoa ushirikiano kwa mkandarasi atakayepata zabuni hiyo ili kumrahisishia kumaliza mradi huo kwa wakati na viwango vinavyokubalika.

Kwa upande wao wakazi wa Kijiji cha Sale wamemuelezea Waziri Changamoto wanazozipata katika barabara hiyo na kuiomba Serikali kuharakisha mradi huo kwani utasaidia kuongeza pato katika Sekta ya Utalii na kurahisisha huduma za kijamii.

“Barabara hii ni ya muhimu sana kwani tumeteseka kwa muda mrefu, huduma za kijamii kama kumsafirisha kutoka nyumbani mpaka kwenye kituo cha afya ilikuwa ikituchukua muda mrefu kutokna na ubovu wa miundombinu”, amesema Bw. Elias Badiani.

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro kuhusu utekelezaji wa miradi ya miundombinu alipowatembelea ofisini kwao.


 Muonekano wa barabara ya Changarawe ya Loliondo – Mto wa Mbu KM 218 inayotarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Manyara

Mkazi wa Kijiji cha Sale, Bw. Michael Nagwianye mkoani Manyara akitoa maoni kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa mara baada ya kukagua barabara ya Loliondo – Mto wa Mbu KM 218 inayotarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami.

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

$
0
0

SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, amemshukuru waziri mkuu  kwa kufanya ziara mkoani mwake ambapo alisikiliza na kutatua kero za wananchi; https://youtu.be/XWZ_p7shDyc

SIMU.TV: Vitendo vya uvuvi haramu katika ziwa Rukwa vimezidi kushamiri na kupelekea kuhatarisha kwa uwepo wa samaki katika ziwa hilo; https://youtu.be/zOpA81NdJCc

SIMU.TV: Serikali iko katika hatua za mwisho kuanza ujenzi wa barabara ya Loliondo mpaka Mto wa mbu huku lengo likiwa ni kuharakisha sekta ya mawasiliano; https://youtu.be/qfSVxi0awuE

SIMU.TV: Mkuu wa wilaya ya Muleba mkoani Kagera Richard Ruyango amelitaka jeshi la polisi wilayani humo kuwachukulia hatua bodaboda uchwara; https://youtu.be/xvQpHeolBJk

SIMU.TV: Serikali imezishauri taasisi za kidini kuweka taratibu ambazo zitawawezesha wananchi wenye uhitaji kufaidika na taasisi hizo; https://youtu.be/M5HuqXSjbd0

SIMU.TV: Mke wa rais mama Janeth Magufuli ameungana na waumini wenzake na kushiriki ibada katika kanisa la mtakatifu Petro lililopo Oysterbay jijini Dar Es salaam; https://youtu.be/dpYwA0SSeMY

SIMU.TV: Mjumbe wa kamati kuu ya CCM Taifa Steven Wassira amewataka wazazi nchini kuwafundisha watoto historia ya nchi ili kuwajengea uzalendo; https://youtu.be/3b4ZjNNrxac

SIMU.TV: Timu ya soka ya Simba imerejea kileleni mwa ligi kuu Tanzania bara baada ya kufanikiwa kuifunga timu ya Ndanda Fc kwa jumla ya mabao 2-0; https://youtu.be/2mG7zrwHuBI  

SIMU.TV: Watanzania wamehimizwa kuendeleza soka la mchangani kwani linasaidia kuibua kwa vipaji vinavyoweza kusaidia taifa hapo baadae; https://youtu.be/tc9gKLU3F4k
SIMU.TV: Watanzania wameshauriwa kulichangamkia soko la Kiswahili kwa Afrika mashariki ili kujiletea maendeleo; https://youtu.be/3MV_-7InvRU

Zanzibar na kampuni ya ZTE ya China zimetiliana saini Mkataba wa ushirikiano katika uendelezaji wa miradi

$
0
0
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Kampuni ya Kimataifa ya Mitandao ya Kisasa ya Mawasiliano ya ZTE ya Mji wa Shengzhen Nchini Jamuhuri ya Watu wa China zimetiliana saini Mkataba wa ushirikiano katika uendelezaji wa miradi itakayotumia mfumo unaokubalika Kimataifa kwa hivi sasa.
Miradi hiyo itakayotumia  mfumo waTeknolojia ya Kisasa { TEHAMA } ni pamoja na Mradi wa Mawasiliano Serikalini { E Goverment } huduma za umeme, usafiri, miji mipya, afya pamoja na huduma za Kijamii ikiwemo utaratibu wa udhibiti wa ukusanyaji wa Mapato ya Serikalini.
Saini ya Mkataba huo imetiwa na Rais wa Kampuni ya ZTE Bwana Zhang Rejun wakati upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ambaye yuko Nchini China kwa ziara rasmi ya Kiserikali ya siku Tano.
Akizungumza na Uongozi wa Kampuni hiyo ya ZTE kwenye Makao Makuu yake Mjini Shengzhen Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Zanzibar inaendelea kuipa fursa zaidi Kampuni ya ZTE katika mtazamo wake wa miradi ya maendeleo inayotarajia kuanzisha hapo baadaye.
Balozi Seif alisema hatua hiyo ya Serikali imekuja kutokana na Uongozi wa juu wa Kampuni ya ZTE kuonyesha juhudi kubwa za kuendelea kuunga mkono harakati za kuimarisha miradi ya Maendeleo zinazotekelezwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliishukuru na kuipongeza Kampuni ya ZTE kwa kasi kubwa ya uwajibikaji wa watendaji wake  katika mfumo wa Teknolojia ya kisasa ya mawasiliano unaoonekana kukubalika na Mataifa mengi Duniani zikiwemo pia Nchi za Bara la Afrika.
Balozi Seif aliutolea mfano mradi Mkubwa  wa mawasiliano Serikalini                      {E Goverment } ambao ulisimamiwa na Kampuni hiyo kwa upande wa Zanzibar ukikamilika katika awamu ya kwanza.

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi (kushoto)  na Rais wa Kampuni ya ZTE ya Mji wa Shengzhen Nchini China Bwana Zhang Rejun kulia wakitia saini Mkataba wa ushirikiano katika uendelezaji wa miradi itakayotumia mfumo wa Teknolojia ya Kisasa ya Mawasiliano  Makao Makuu wa ZTE Mjini Shengzhen China.
 Balozi Seif kushoto akibadilishana hati na Rais wa ZTE Bwana Zhang Rejun baada ya kutia saini Mkataba wa Ushirikiano wa uendelezaji wa miradi itakayotumia mfumo wa Teknolojia ya Kisasa ya Mawasiliano.
Mtaalamu wa Ufundi wa Kampuni ya ZTE Bibi Radhika Devi wa kwanza kutoka Kushoto akimkaguza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif na Ujumbe wake katika vitengo mbali mbali ndani ya Makao Makuu ya  Kampuni hiyo Mjini Shengzheng. Kushoto ya Balozi Seif ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Mh. Mohamed Ahmed Salum na Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bibi Asha Ali Abdulla
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images