Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1465 | 1466 | (Page 1467) | 1468 | 1469 | .... | 3283 | newer

  0 0

  Na Chalila Kibuda , Globu ya  Jamii.

  MAKAMU wa Rais, Samia  Hassan Suluhu amewaagiza Wakuu wa Mikoa nchini pamoja na Wakuu  kutangaza siku ya Jumamosi ya pili ya mwanzo wa mwezi kuwa siku maalum ya  kufanya mazoezi ya kukimbia kwa lengo la kuondokana na magonjwa yasiyo ya kuambukizwa ambayo yanatokana na mtu kutofanya mazoezi.

  Hata hivyo,  Makamu wa Rais, amewaagiza pia viongozi hao wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha ndani ya miezi mitatu  wanavirudisha viwanja vyote vya michezo walivyoviuza ili viweze kuwasaidia wananchi katika kufanyia mazoezi au kutafuta maeneo mengine ya wananchi kufanyia mazoezi.

  Makamu wa Rais ametoa maagizo hayo  leo, Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa  kampeni ya kufanya mazoezi nchini ili kujikinga na magonjwa yasiyo ya kuambikizwa katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.

  Amesema kwa sasa serikali imebaini kuwa magonjwa mengi yasiyo ya  kuamuikizwa yamechangiwa na watu kutofanya mazoezi hivyo ameagiza  viongozi hao kuhakikisha wanatenga siku hiyo hali ambayo inaweza kupunguza magonjwa hayo.

  "Nawataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha kila Jumamosi ya pili ya mwenzi iwe siku ya kufanya mazoezi katika wilaya na vitongoji kwa kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwenye maeneo yao kufanya mazoezi ya mbalimbali  ili iweze kuwasadia’’amesema Makamu wa Rais Samia Hassan  Suluhu.

  Amesema anafahamu kuna tatizo kwenye Halmashauri mbalimbali kuwa  wameuza   viwanja vya wazi na kuwaagiza  watendaji wa Halmashauri  ndani ya miezi mitatu kuvirudisha viwanja hivyo kwa ajili ya mazoezi hata kama wakishindwa wametakiwa kutangaza maeneo mengie ili wananchi wayatumie kufanya  mazoezi.

  Kwa upande wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Dk. Ali Hassan Mwinyi, amewataka watanzania kupenda kufanya mazoezi kwani njia hiyo itawasaidia katika kuongeza siku za kuishi na kufanikiwa kujikinga na magonjwa mbali  mbali. "Nawaambia siri ya umri wangu  ufanyaji mazoezi kwani mimi kila siku natenga dakiki 90 za kufanya mazoezi kila nikiamka’amesema Rais Mstaafu". Mzee Mwinyi.

  Nae Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia  Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kwa sasa hali inatisha kwani magonjwa mengi yasiyo ya kuambukizwa yameongezeka na yanasababishwa na kutofanya mazoezi jambo analodai limewasukuma kuandaa kampeni hiyo ya kuwahamasisha wananchi kufanya mazoezi ili waweze kujikinga na magonjwa.
  Makamu wa Rais, Mh. Samia Hassan Suluhu (katikati), Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi (wa tatu kushoto), Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia  Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na Naibu wake, Dkt. Hamis Kigwangala (kulia) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakiwa katika kampeni ya kufanya mazoezi katika viwanj vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, pamoja na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia  Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga wakati wa kampeni ya kufanya mazoezi leo katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyanyakazi wa mfuko huo katika uzinduzi wa kampeni ya kufanya mazoezi leo katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Duru la Pili la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara linalotarajiwa kuanza leo Jumamosi Desemba 17 kwa michezo minne kabla ya michezo mingine minne kufanyika siku ya Jumapili Desemba 18, mwaka huu.

  Katika mechi za leo, Mabingwa watetezi wa taji hilo, Young Africans SC ya Dar es Salaam itakuwa mgeni wa JKT Ruvu ya Pwani kwenye mchezo utakaofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

  Licha ya kwamba mwenyeji wa mchezo huo ni JKT Ruvu ambayo uwanja wake wa nyumbani mara nyingi huwa ni Mabatini ulioko Mlandizi, lakini kwa mujibu wa Kanuni ya 6 (5) na (6) ya Ligi Kuu Bara, mechi zake za nyumbani dhidi ya Simba, Young Africans na Azam FC, hufanyika Uwanja wa Uhuru.

  Michezo mingine ya kesho ni Kagera Sugar kuwa mgeni wa Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya wakati Ruvu Shooting ya Pwani itakuwa mwenyeji wa Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye Uwanja wa Mabatini, Pwani ilihali Mwadui ya Shinyanga itaikaribisha Toto Africans ya Mwanza kwenye Uwanja wa Mwadui Complex.

  Jumapili, Desemba 18, mwaka huu Mbao FC ya Mwanza itacheza na Stand United ya Shinyanga kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza wakati Ndanda itakuwa mwenyeji wa Vinara wa Msimamo katika Ligi Kuu ya Vodacom, Simba kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.

  African Lyon ya Dar es Salaam itaikaribisha Azam FC pia ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Uhuru jijijini siku hiyo ya Jumapili wakati Majimaji ya Songea itakuwa Mbeya kucheza na Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine.

  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, limetoa masharti kadhaa likitaka klabu za Ligi Kuu ya Vodacom kufuata. 

  Masharti hayo, ni kwa klabu kutumia makocha wenye sifa kwa mujibu wa kanuni ya 72 ya Ligi Kuu ya Vodacom. Kwa mujibu wa Bodi ya Ligi Kuu ya Shirikisho la Mpira wa Tanzania (TFF) na kwa mujibu wa kanuni hiyo, makocha wanaopaswa kukaa kwenye benchi la Ligi kuu kwa msimu huu wasipungue sifa ya kuwa na leseni B ya CAF.

  Pia kwa timu za Ligi Daraja la Kwanza na Pili, masharti ni lazima makocha wawe na sifa za kuzinoa timu hizo ambazo zimeanishwa kwenye kanuni za ligi husika.

  Kadhalika, tunaagiza klabu kutotumia wachezaji wa kigeni au makocha kama hawana vibali vya ukaazi na kufanya kazi kutoka Idara ya Uhamiaji nchini iliyoko chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani. 

  0 0

  Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii

  Imeelezwa watoto wengi wa kike wanakosa muda wa kuzungumza na wazazi wao wa kiume juu ya masuala ya mabadiliko ya kimaumbile hali inayochangia kwa kiasi kikubwa kwa watoto wa kike kujiingiza katika vishawishi mbalimbali.

  Hayo yamesemwa na mkuunzi wa masuala ya kijinsi na jinsia kutoka tasisi isiyo ya kiserikali ya TGNP,Liliani Liundi katika warsha kuhusu kupigania usawa wa kijinsia kwa mtoto wa kike haswa katika kuangalia vipaumbele vya sekta ya Afya ,Maji , Elimu , Kilimo na Viwanda.

  "Ifike muda sasa kwa wazazi wa kiume waanze kuanza kuzungumza na watoto wao juu ya masuala ya mabadiliko ya kimaumbile na kuweka bajeti kwa watoto wa kike katika familia na kutenga vyombo maalum vya kuhifadhia taka zinazotokana na matumizi ya vifaa vya kimaumbile ya mtoto wa kike kisha kuzichoma"amesema.Liliani Lihundi.

  Kwa upande wake muwezashaji mwingine kutoka TGNP ,Deo Temba amesema kuwa ukosefu wa elimu salama ya uzazi wa mpango umechangia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa mimba za utoto kwa watoto waliopo chini ya miaka 18 nchini hali inayohatarisha kuwepo na nguvu kazi ya usawa kwa vijana wetu.

  Katika mjadala huo amesema ni vyema jamii ikajipanga upya na kufikiria kuboresha mfumo wa utoaji elimu ya afya ya uzazi katika jamii  na kuvunja mfumo dume unaobebwa na mila na desturi hasa kwa kutumia sanaa na kutumia vyombo mbalimbali vya habari.
  Mkufunzi wa masuala ya kijinsia kutoka TGNP, Lilian Liundi akizungumza na wadau walioshiriki katika warsha hiyo.
  Muwezeshaji kutoka TGNP, Deo Temba akitoa mada katika warsha hiyo ya wadu wa sanaa na waandishi wa habari iliyofanyika ofisi za tasisi hiyo Mabibo.
  Washiriki wa semina hiyo wakifatilia kwa makini mafunzo hayo.
  Washiriki wakisikiliza kwa makini mafunzo hayo.

  0 0

   Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akipiga baruti juu kuashiria ufunguzi rasmi wa mashindano ya michezo mbalimbali yanayofanyika Wilayani Karatu (Karatu Sports Festival).
   Wanariadha wanaoshiriki mashindano ya michezo mbalimbali yanayofanyika Wilayani Karatu wakijandaa kuanza kukimbia wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo uliofanywa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye Disemba 17/2016.
   Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimiana na baadhi ya washiriki wa mashindano ya michezo mbalimbali yanayofanyika Wilayani Karatu.
   Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimiana na baadhi ya washiriki wa mashindano ya michezo mbalimbali yanayofanyika Wilayani Karatu.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimiana na baadhi ya washiriki wa mashindano ya michezo mbalimbali yanayofanyika Wilayani Karatu.

  0 0  0 0

   Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akimpa maelezo Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo, kuhusu jengo la mikutano la CCM, lililopo Kilimani mjini Dodoma wakati Naibu Katibu Mkuu huyo mpya alipotembelea jengo hilo akiwa katika ziara ya kukagua mali za CCM, leo. Kushoto ni Mkuu wa Utawala Makao Makuu ya CCM, Innocent Msena na kulia ni Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Utumishi na Uendeshaji Makao Makuu ya CCM Filbert Mdaki..
   Mafara wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo ukiwa mbele ya jengo hilo la mikutano la CCM
   Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akimpa maelezo Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo wakati wakiizunguka kuikagua nyumba ya CCM ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Mpogolo alipokuwa katika ziara ya kukagua mali za Chama mjini Dodoma, leo.
   Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akionyeshwa gari lililofunguliwa boneti, kupata uthibisho wa gari tatizo la gari, alipokuwa akikagua magari mabovu ya Chama, akiwa katika ziara ya kukagua mali za Chama, leo mjini Dodoma.


  0 0

  Na JamiiMojaBlog, Mbeya.
  Mkazi wa Iyunga jijini Mbeya ambaye amefahamika kwa jina moja la Rachel (13) amefariki dunia mara baada ya kugongwa na gari  namba T161 CPP Toyota LandCruiser inayodaiwa kumilikiwa na Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi maharufu kwa jina la (SUGU), kwenye kivuko cha barabara (ZEBRA) na kumsababishia kifo chake papo hapo.

  Tukio hilo limetokea leo Desemba 17  majira ya saa mbili asubuhi huko katika eneo la Iyunga Jijini hapa, wakati gari ya Mbunge huyo ikiwa njiani kuelekea uwanja wa ndege wa Songwe kwa ajili ya mapokezi ya kiongozi wa kitaifa Freeman Mbowe.
  Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wakizungumza , kwa nyakati tofauti , wamesema mtoto huyo akiwa na mama yake walikuwa wakivuka barabara baada ya magari ya upande wa  pili kusimama na kuwaruhusu watembea kwa miguu hao kuvuka.
  Amesema, wakiwa katikati ya kivuko hicho mama wa marehemu alishangaa kuliona gari ya Mbunge hiyo ikija kwa kasi hivyo kumuachia mtoto wake aliyekuwa amemshika mkono na yeye kutafuta njia ya kujiokoa.
  Wameeleza kuwa  licha ya dereva wa gari ya Mbunge kuona madereva wenzie wa magari yaliyokuwa yakitokea Mbalizi wakisimama kwa ajili ya kuwaruhusu watembea hao kuvuka lakini yeye akitokea mjini Mbeya alishindwa kutii sheria hiyo na kupita akiwa katika mwendo kasi.
  “Madereva wenzie tumesimama ili mama na mtoto wavuke lakini yeye akiwa na haraka alipita tu, kwa kweli hii inauma sana, nasikia mtoto amepoteza maisha lakini mama amejeruhiwa na kwamba amekimbizwa hospitali Teule ya Ifisi kwa matibabu,”alisema mmoja wa mashuhuda hao.
  Gari la Mbunge wa Mbeya mjini Mheshimiwa Joseph Mbilinyi (Sugu) Toyota Land Cruser T.161 CPP likiwa ofisi za Usalama barabarani jijini Mbeya baada ya kugonga mtembea kwa miguu na kusababisha kifo .

  Kamanda wa  Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Dhahiri Kidavashari akizungumza kwa njia ya simu amekiri kutokea kwa tukio hilo na kuthibitisha kifo cha mtoto huyo. Aidha Kivadashari ametaja jina la  dereva wa gari hiyo kuwa ni  Gabriel Endrew alimaarufu Dj BBG (43) mkazi wa Mwakibete jijini hapa.

   Amesema hilo  limetokea majira ya saa mbili asubuhi ambapo gari T161 CPP ilimgonga mtembea kwa miguu ambaye ni mtoto anayekadiriwa miaka 13 ambapo amefahamika kwa jina moja la Rechal na kumsababishia kifo wakati akikimbizwa hospitali.
  Pia, aliongeza kuwa gari hiyo imekamatwa na dereva anashikiliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano na kwamba polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

  0 0
 • 12/17/16--05:24: Appreciation
 • In memory of our beloved George Andrew Mkini.

  We, the family of the late George Andrew Mkini, wish to express our deep appreciation to those who have offered such kindness, support and messages of sympathy and comfort in our bereavement. Your many acts of kindness and sympathy continue to be a great comfort to us in our time of sorrow.
  We especially wish to thank all staffs of Luwona Hospital Iringa, Aga Khan Iringa, Kairuki Hospital and Muhimbili Dar es Salaam, without forgetting Ubungo Lutheran Church and Kitowo Iringa KKKT.

  There will be a thanksgiving mass on Monday, the 26th of December 2016,at 08hrs00, Ubungo Lutheran Church, let us all join together with love and thank God for George's life.

  May the Almighty God rest his soul in an eternal peace. Amen

  0 0

  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemteua Bi. Aziza Badru Mwanje kuwa Mkurugenzi mpya wa Fedha na Utawala kuanzia Januari Mosi, 2017.
  Uteuzi huo umefanywa leo (Desemba 17, 2017) na Kamati ya Utendaji ya TFF kufuatia mchakato wa usaili uliohusisha waombaji wengine wawili na kufanywa na Bodi ya Ajira ya TFF.
  Vilevile Kamati ya Utendaji imefanya mabadiliko ya wajumbe katika Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ambapo Wakili Patrick Sanga atakuwa Makamu Mwenyekiti wakati Mwenyekiti anaendelea kuwa Wakili Richard Sinamtwa.
  Wajumbe wengine walioongezwa kwenye Kamati hiyo ni Bw. Adam Mihayo na Bw. Hassan Hassanoo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA).
  Wakili Raymond Wawa ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF kuziba nafasi ya Bw. Joseph Mapunda ambaye ameomba kupumzika. Pia Bibi Mia Mjengwa ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake.

  IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

  0 0

  WAZIRI wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Stadi, Profesa Joyce Ndalichako ameitunuku nishani ya uzalendo kampuni ya Global Education Link (GEL) kutokana na mchango inaotoa katika maendeleo ya elimu nchini.

  Nishani hiyo aliitoa leo wakati akizindua mkutano mkuu wa 11 wa Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari nchini (TAHOSSA) mkoani Dodoma. 
  Mkurugenzi wa Global Education Link (kulia) akipokea tuzo kutoka kwa Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na ufundi Stadi Prof. Joyce Ndalichako.

  Rais wa Wakuu wa Sekondari Tanzania (TAHOSSA), Bonus Ndimbo alisema GEL imekuwa ni mdau mkubwa wa maendeleo katika elimu, sio tu kwa TAHOSSA hata kwa nchi kwa ujumla.

  “Tunaipongeza sana Global Education Link, kwani imekuwa karibu na jamii, imekuwa karibu na sekta ya Elimu na maendeleo ya nchi kwa ujumla,” alisema Katibu Mkuu wa TAHOSSA Diana Matemu.Global Education Link ni kampuni iliyoanzishwa Mwaka 2006 kwa lengo la kuwaunganisha wanafunzi wa Tanzania wanaotaka kusoma vyuo vikuu vya nje.

  Tangu imeanza shughuli zake kwa miaka 10 sasa, zaidi ya wanafunzi 5400 wamefaidika kwa kuunganishwa na vyuo mbalimbali vilivyoko Marekani, Canada, Uingereza, Afrika Kusini, Ukraine, India, Urusi, Malaysia, China na nyinginezo. 
  Mkurugenzi Mkuu wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel akizungumza na Wakuu wa Sekondari Tanzania baada ya kupewa nafasi ya kipekee ya kuwawakilisha wadau mbalimbali wa elimu waliokaribishwa katika mkutano huo mbele ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Ufundi stadi Prof Joyce Ndalichako.
  Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA) wakimsikiliza Mkurugenzi wa Global Education Link, Abdulmalik Mollel (hayuko pichani).

  Akizungumza baada ya kukabidhiwa nishani hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel alishukuru na kusema anafanya hivyo kwa lengo la kusaidia Serikali na Watanzania kwa ujumla katika kuharakisha maendeleo nchini.

  Kikubwa ambacho Mkurugenzi wa GEL alisema ni kuwa mpango wa mafunzo kwa wanafunzi utasaidia kuwafanya wanafunzi kuchagua kozi ambazo zitakuwa na tija kwao na taifa kwa ujumla.

  0 0

  BAADA ya maandalizi ya takribani wiki tatu, hatimaye Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, kesho inatarajia kufungua pazia la mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) kwa kukipiga dhidi ya African Lyon, mchezo utakaofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam saa 10.00 jioni.
   Mshambuliaji wa Azam FC, Yahaya Mohammed, akifumua shuti wakati wa mazoezi hayo
   Wachezaji wa Azam FC wakifanya mazoezi ya kusafa wakati wa mazoezi hayo.
   Wachezaji wa Azam FC wakifanya mazoezi ya kusafa wakati wa mazoezi hayo.
   Kipa wa Azam FC, Aishi Manula, akiokoa mchomo kwenye mazoezi ya timu hiyo.
  Beki wa kulia wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Shomari Kapombe, akimiliki mpira mbele ya Abdallah Kheri, wakati wa mazoezi ya mwisho ya timu hiyo leo asubuhi kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) utakaofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam dhidi African Lyon kesho Jumapili. Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akimtwisha ndoo ya maji bibi Agness Silima ikiwa ni ishara ya kuzindua mradi wa maji wa kijiji cha Onderet wilayani Arusha 
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipiga ngoma ya msanja iliyokuwa ikichezwa na wnanwake wa Arusha baada ya kuwasili kwenye kijiji cha Ondenderet wilayani Arusha Desemba 27, 2016.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama ngoma ya wanawake wa kimasai baada ya kuzindua mradi wa maji wa kijiji cha Ondenderet wilayani Arusha Desemba 27, 2016. kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.


   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikabidhiwa kirungu na wazee wa kimasai ikiwa ni ishara ya kumsimika kuwa mmoja wa wazee wa kabila hilo katika mkutano wa hadhara aliouhutubia katika kijjiji cha Namanga kilichopo kwenye mpaka wa Kenya na Tanzania  wilayani Longido
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wazee wa kimasai baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Namanga kilichopo kwenye mpaka wa Kenya na Tanzania wilayani Longido Desemba 16, 2016.  Wapili kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Desemba 16, 2016 alikabidhi pikipiki 10 kwa vijana wa bodaboda wa Namanga na  Longido  mkoani Arusha . Pichani, Waziri Mkuu akikabidhi pikipiki hizo baada ya kuhutubia mkuano wa hadhara katika kijiji hicho. Picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0
 • 12/17/16--06:05: IN LOVING MEMORY
 • It is exactly one year since your sudden depart. You have left an irreplaceable gap within our hearts for the love and kindness you carried with you was one of a kind,you are dearly missed by your family and friends. Physically you may not be here but forever you will stay in our hearts and prayers.

  May your soul rest in peace.

  0 0  0 0

  Masharti hayo, ni kwa klabu kutumia makocha wenye sifa kwa mujibu wa kanuni ya 72 ya Ligi Kuu ya Vodacom. Kwa mujibu wa Bodi ya Ligi Kuu ya Shirikisho la Mpira wa Tanzania (TFF) na kwa mujibu wa kanuni hiyo, makocha wanaopaswa kukaa kwenye benchi la Ligi kuu kwa msimu huu wasipungue sifa ya kuwa na leseni B ya CAF.
  Pia kwa timu za Ligi Daraja la Kwanza na Pili, masharti ni lazima makocha wawe na sifa za kuzinoa timu hizo ambazo zimeanishwa kwenye kanuni za ligi husika.

  "Kadhalika, tunaagiza klabu kutotumia wachezaji wa kigeni au makocha kama hawana vibali vya ukaazi na kufanya kazi kutoka Idara ya Uhamiaji nchini iliyoko chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani" imesema taarifa toka TFF. 
  Masharti hayo yametolewa wakati wa kuanza kwa duru la Pili la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara linaloanza leo Jumamosi Desemba 17 kwa michezo minne kabla ya michezo mingine minne kufanyika kesho  Jumapili Desemba 18, mwaka huu.
  Katika mechi zaleo Mabingwa watetezi wa taji hilo, Young Africans SC ya Dar es Salaam itakuwa mgeni wa JKT Ruvu ya Pwani kwenye mchezo utakaofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
  Licha ya kwamba mwenyeji wa mchezo huo ni JKT Ruvu ambayo uwanja wake wa nyumbani mara nyingi huwa ni Mabatini ulioko Mlandizi, lakini kwa mujibu wa Kanuni ya 6 (5) na (6) ya Ligi Kuu Bara, mechi zake za nyumbani dhidi ya Simba, Young Africans na Azam FC, hufanyika Uwanja wa Uhuru.
  Michezo mingine ya leo ni Kagera Sugar kuwa mgeni wa Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya wakati Ruvu Shooting ya Pwani itakuwa mwenyeji wa Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye Uwanja wa Mabatini, Pwani ilihali Mwadui ya Shinyanga itaikaribisha Toto Africans ya Mwanza kwenye Uwanja wa Mwadui Complex.
  Kesho Jumapili, Desemba 18, mwaka huu Mbao FC ya Mwanza itacheza na Stand United ya Shinyanga kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza wakati Ndanda itakuwa mwenyeji wa Vinara wa Msimamo katika Ligi Kuu ya Vodacom, Simba kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
  African Lyon ya Dar es Salaam itaikaribisha Azam FC pia ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Uhuru jijijini  hiyo kesho,wakati Majimaji ya Songea itakuwa Mbeya kucheza na Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine.


  0 0

  Ni Mjini New Delhi bendera ya Tanzania kwa mara nyingine inapeperushwa katika michezo inapeperushwa na  Bondia  Francis Cheka ambaye anaingia ulingoni dhidi ya mpiganaji wa India Vijender Singh katik pambano la ubingwa la Super Middleweight .

  Kwa mujibu wa msomaji wetu Khadija Deddah ambaye yuko nchini India, pambano hilo linatarajiwa kuanza wakati wowote kuanzia sasa.
  Francis Cheka ambaye ni bingwa wa zamani  anapambana na  Singh ambaye anatetea taji lake la WBO Asia Pacific super middleweight. Vijender ambaye alishinda taji hilo Julai mwaka huu kwa kumtandika bingwa wa zamani wa Ulaya Kerry Hope wa Australia mpaka sasa hajapoteza kitu ulingoni. 

  Katika gemu hiyo ya raundi 10 Francis Cheka anatarajiwa kutumia uzoefu wake mkubwa kumtandika bingwa huyo na kumpokonya mkanda wake. 
  Wakati wa  upimaji uzito jana Francis alisema kwamba atazungumza ulingoni wakati Vijender akisema kwamba mkanda hauendi kokote utabaki nchini India. 

  Cheka mwenye umri wa miaka 34 ni veterani akiwa amepigana mara 43 na kushinda mara 32 zikiwamo TK 17. Mpambano wa Cheka na  Singh utatanguliwa na mapambano mengine matano ya kirafiki ya kimataifa.
   Watanzania (wanafunzi) walifika uwanjani kumshangilia Cheka
   Bango la pambano
   Uwanja wa pambano
   Kutoka kushoto ni  Naibu Balozi wa Tanzania nchini IndiA, Katibu wa Shirika la Kimataifa (AALCO) ambae ni Mtanzania, na Afisa wa Ubalozi
  Wanafunzi wa Ki-Tanzania wapo uwanjani kumshangilia Cheka

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa muda wa miezi mitatu kwa Halmashauri zote nchini kurudisha serikalini haraka maeneo ya michezo yaliyovamiwa na watu kwa ajili ya kufanya shughuli zao binafsi.

  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa agizo hilo baada ya kushiriki matembezi na kuzindua wa kampeni ya Kitaifa ya kudhibiti Magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwenye viwanja wa Leaders Club jijini Dar es Salaam.

  Makamu wa Rais ameonya kuwa kama watendaji wa mikoa na halmashauri watashindwa kurudisha maeneo hayo basi watenge haraka maeneo mengine kwa ajili ya wananchi kufanya mazoezi kama hatua ya kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

  Katika kuunga mkono utaratibu wa kufanya mazoezi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewaagiza viongozi wa mikoa na wilaya zote kuweka utaratibu wa kufanya mazoezi angalau kwa mwezi mara Moja.

  “Nitamke kuwa kila Jumamosi ya pili ya mwezi itakuwa siku ya mazoezi kwa afya kwa sababu mazoezi ni afya na nawaasa wananchi kufanya mazoezi na kuanzisha na kujiunga na vikundi vya mazoezi na serikali itatimiza wajibu wake wa kuweka mazingira mazuri ya kufanyia mazoezi kote nchini”Makamu wa Rais pia ameagiza watendaji wa Wizara ya elimu, Sayansi na Teknolojia kurudisha mchakamchaka mashuleni kulingana na maeneo yalivyo.

  Amesema mchakamchaka utasaidia kuimarisha afya za wanafunzi na kukabiliana na magonjwa mbalimbali.
  “Natoa rai utaratibu wa mchakamchaka katika shule zetu urudishwe mara Moja katika Muda ambao utaonekana ni mwafaka kwa shule husika”.Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais ameiagiza Wizara ya Afya kukamilisha haraka mchakato wa kuunda kamati ya kushughulikia magonjwa yasiyo ya kuambukiza itakayojumuisha wadau kutoka wizara mbalimbali nchini.

  Amesisitiza kuwa mchakato huo ni lazima ukamilike tarehe 1 machi mwaka 2017.Kwa upande wake, Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema magonjwa yasiyo ya kuambukiza yamekuwa yanaongezeka sana duniani kote hasa kwenye nchi zilizo chini ya Jangwa la Sahara ikiwemo Tanzania ambapo magonjwa hayo mpaka sasa yanachangia asilimia 27 ya vifo Duniani.

  Amesema utafiti uliofanyika mwaka 2012 uliohusisha wilaya 53 hapa nchini umeonyesha viashiria hatarishi vya magonjwa hayo ambapo asilimia 26 ya wananchi ni wanene kupita kiasi,asilimia 26 wana lehemu nyingi mwilini na asilimia 25.9 wanashinikizo kubwa la damu.

  Utafiti huo pia ulionyesha kuwa asilimia 15.9 ya wananchi wanavuta sigara na asilimia 97.2 ya wananchi wanakula mboga mboga na matunda chini ya mara tano kwa siku.Waziri wa afya Ummy Mwalimu amesema watanzania wanaweza kukabiliana na magonjwa hayo kwa kufanya mazoezi ya viungo angalau mara tatu kwa wiki kwa muda wa nusu saa, kuzingatia ulaji wa vyakula unaofaa,kupunguza matumizi ya pombe kupita kiasi na kujiepusha na matumizi ya tumbaku.

  Kwa upande wake Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi katika nasaha zake amewahimiza Watanzania kufanya mazoezi kwa ajili ya kulinda afya zao.Amesema kama watanzania watafanya mazoezi wataepukana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwemo ugonjwa wa moyo,kisukari,uti wa mgongo na mifumo ya neva na figo.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Kudhibiti Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza kwenye viwanja vya Leaders Club.
  Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Alhaji Ali Hassan Mwinyi akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Kitaifa ya Kudhibiti Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza ambapo aliwaambia wananchi walishiriki kwenye tukio hilo kuwa siri kubwa ya mafanikio yake ya kuonekana yupo imara ni mazoezi hivyo aliwataka wananchi wajenge tabia ya kushiriki na kufanya mazoezi kwani kutawaepusha na maradhi mengi .
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalim akihutubia kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuzindua rasmi Kampeni ya Kitaifa ya Kudhibiti Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akiongoza matembezi ikiwa sehemu ya kuhamasisha jamii kufanya mazoezi akiongozana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Alhaji Ali Hassan Mwinyi (kushoto) na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalim kabla ya kufungua Kampeni ya Kitaifa ya Kudhibiti Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza kwenye viwanja vya Leaders Club viongozi wengine walioshiriki matembezi hayo ni pamoja na Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalah, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda .

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbali mbali mara baada ya kufungua wa Kampeni ya Kitaifa ya Kudhibiti Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza kwenye viwanja vya Leaders Club.

  0 0

   Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO - Dkt. Hassan Abbass akikitunukiwa Shahada yake ya Uzamivu ya Mawasiliano ya Umma (PhD) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania (SAUT) wakati wa Mahafali ya 16 ya chuo hicho leo Jijini Mwanza.
   Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO - Dkt. Hassan Abbass akipokea shada la maua mara baada ya kutunukiwa Shahada yake ya Udaktari wa Mawasiliano ya Umma kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania (SAUT) wakati wa Mahafali 16 ya chuo hicho leo Jijini Mwanza.
   Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO - Dkt. Hassan Abbass (kushoto) akifurahia jambo na mmoja wa Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT) Fr. Francis Ng’atigwa mara baada ya kutunukiwa Shahada yake ya Udaktari wa Mawasiliano ya Umma kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino Tanzania (SAUT) wakati wa Mahafali 16 ya chuo hicho leo Jijini Mwanza
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO - Dkt. Hassan Abbass (wanane kutoka kushoto mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu wenzake mara baada ya kutunukiwa Shahada yake ya Udaktari wa Mawasiliano ya Umma kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino Tanzania (SAUT) wakati wa Mahafali 16 ya chuo hicho leo Jijini Mwanza.

  0 0

  Kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya  Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Simon Msanjila, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia (MUST)  Profesa Mark Mwandosya na mwenyeketi wa baraza la chuo kikuu cha sayansi na teknolojia Profesa Penina Mlama kwa pamoja wakiwa katika maandamano kuelekea katika ukumbi wa Nyerere kabla ya hafla kuanza.Naibu Katibu Mkuu Waziri ya  Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Simon Msanjila akihutubia katika hafla hiyo ya mahafali ya nne ya Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia (Mbeya University of Science and Technology - MUST) kilichopo mkoani mbeya, Mh.Msanjila amekipongeza chuo hicho kwa kuongeza baadhi ya mafunzo ikiwemo mafunzo ya ufindi na mafunzo ya sayansi ya kiafya kwa kushirikiana na hospitali ya Rufaa mkoani mbeya.Pia mh.Simon Msanjila ametoa wito kwa kila mtu mwenye uwezo wa kujifunsa mafunzo ya sayansi na teknolojia yatolewayo katika chuo kikuu cha sayansi na teknolojia kilichopo mkoani mbeya na kuwataka wahitimu kuzikimbilia fursa mbalimbali  haswa katika harakati za kutafuta ajira. Sehemu  ya wahitimu wa stashahada ya kawaida na stashahada ya kwanza katika fani mbalimbali za sayansi na teknolojia wakitunukiwa. Jumla ya wahitiumu wote waliomaliza kozi mbalimbali ni 804 ambapo idadi kubwa ni jinsia ya kime.Wahitimu sambamba na wageni waalikwa na wafanyakazi wa chuo hicho cha sayansi na teknolojia walio hudhuria hafla hiyo ya mahafali ya nne ya MUST yaliyofanyika katika ukumbi wa Nyerere uliopo chuoni hapo mkoani Mbeya.PICHA NA MR.PENGO WA MMG MBEYA.

  0 0


older | 1 | .... | 1465 | 1466 | (Page 1467) | 1468 | 1469 | .... | 3283 | newer