Na Ripota wa Globu ya Jamii.
Kati ya mambo ambayo tumekuwa tukipewa sifa waafrika bila kujali sifa nzuri au mbaya ni pale tunavyokua tunaenzi tamaduni zetu ambazo tangu wazungu wanaingia karne ya kumi na tisa bara la Afrika wakaona kama tusiostarabika na akuna taifa au bara lisilo na utamaduni na likafuata.
Afrika tuna mambo mengi ndani ya utamaduni ambayo yanajumuisha michezo,lugha,vyakula,mavazi. Katika mashindano ya mpira wa miguu kwa Mataifa ya Afrika maarufu kama AFCON yamebakiza siku zipatazo 26 ili yaanze katika ardhi ya nchi ya Gaboni. Ni tarehe 14/1/2017 yanaanza na ni kipindi ambacho waafrika tunakipenda na kufurahia sana tena sana kwasababu ya kutangaza utamaduni na vivutio mbalimbali kutoka nchi shiriki wawapo mashindanoni.
Msimu wa kuangalia singeli za mataifa ya afrika umewadia kwani kila shabiki atakuwa na mtindo wake, sisi ni ngoma mwanzo mwisho huku wachezaji wakitusapot kucheza nao wafungapo magoli hapo ndo utakapo ona umahili wa Asamoah, Adebayor na wengine katika ngoma wachezazo.
Afrika yetu ngoma yetu kombe letu sisi ni kusasambua tu wakati Ulaya wakilalamikia wachezaji kwenye vilabu vyao. Asili haachi asili ndiyo maana hata magoli yatakayo fungwa na wachezaji wenye asili ya Afrika yana ushangiliaji mzuri na wakunogesha kuliko wazungu .
Unamkumbuka Bafetimbi Gomis unamkumbuka Junior Agogo unamkumbuka Muntari ile 2006 kule Ujerumani ,unazikumbuka mbwembwe za kucheza Kiplanonga kwa style ya Azonto hii ndo Afrika . Kwangu kombe la dunia naweza nikaikosa mechi halafu ikawa poa lakini sio Afcon hapa ndo unaposema Hadithi njoo mangoma njoo utamu kolea sijui Uganda watatusapraizi na ngoma zipi isije ikawa kama wenzao Rwanda 2004 kule Tunisia ila kama Tanzania ingekuwepo najua jukwaa lingeshikwa na sholomwamba na manifongo asingekaa shabiki.
Klabu nyingi barani ulaya zimekuwa zikilalamikia ratiba yetu na kuwaomba FIFA waishinikize CAF kubadili kalenda yake kwasababu muda huo zile timu zenye wachezaji wenye asili ya Afrika na timu zao zikiwa zimefudhu mashindano hayo hutakiwa katika nchi zao na kutumikia vikosi vya nchi zao kitu ambacho huacha pengo kwenye vilabu vyao ulaya.
Hakuna asiyefahamu nyakati walizokua wakipitia Klabu kama Manchester City, Chelsea, Arsenal kwa nyakati tofauti pale wachezaji wao muhimu wakitumikia mataifa yao.
Katika uhalisia wa uafrika ulivyo hakuna mchezaji ambaye hapendi kujumuishwa kwenye nchi yake ila wako wanaingia katika mitego ya vilabu vyao kutoa taarifa za ugonjwa huku ikiwa tofauti kwa mchezaji husika ,lilitokea kwa Michael Essieni mwaka 2008 katika mashindano yaliyoandaliwa Ghana Chelsea .
Wakitoa taarifa za ugonjwa yaani majeruhi kumbe ilikua udanganyifu kitu ambacho kilimharibia Essien kwao Ghana akaja kurejea 2010 pale Angola na hakuwa fiti kwani alikuja kuumizwa na Didier Drogba kwenye mechi ya robo fainali, mtego huo umewahi pia kuteguka kwa Sadio Mane na Kouyatte mwaka 2015 lakini ukweli toka kwa baadhi ya wakongwe waafrika kama Bernard McCarthy anasema hakuna mwafrika asiyetaka kuja kutumikia taifa lake ila ni ujanja unaofanywa na maboss.
Tuleteeni Afcon yetu.