Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1464 | 1465 | (Page 1466) | 1467 | 1468 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga kwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Mhe. Balozi Dkt. Amina Mohammed wakisaini Makubaliano ya Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya. Makubaliano hayo yamesainiwa kufuatia Kikao cha Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JCC) kati ya Tanzania na Kenya kilichofanyika tarehe 1 hadi 3 Desemba, 2016 ambapo masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya nchi hizi mbili yalijadiliwa na kukubaliwa. Masuala ya ushirikiano ni pamoja na kilimo, uchukuzi, utalii, nishati na madini na uvuvi. Hafla hiyo fupi ya uwekaji saini makubaliano hayo imefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 16 Desemba, 2016. 
  Waziri Mahiga na Waziri Mohammed wakibadilishana makubaliano hayo mara baada ya kusaini. 
  Picha ya Pamoja 


  0 0


  Na Antony John Globu ya Jamii

  Kutokuielewa sheria kumeonekana kunaleta changamoto kubwa kwa jamii hali inayosababisha wananchi kukosa hakizao na kusababisha mlundikano wa kesi mahakamani.

  Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za mkuu wa mkoa leo, mkuu wa mkoa wa Dar es salaam,Paul Makonda amesema kutokana na changamoto hiyo serekali imeamua kupeleka wanasheria vijana watakao jitolea katika wilaya zote za dar es salaam ili kuwasaidia wananchi katika maswala ya kisheria.

  Makonda amesema kati ya changamoto zinazo wakabili wananchi wengi ni pamoja na malaamiko ya rushwa katika vyombo vinavyo toa haki, ucheleweshwaji wa kesi mahakamani, migogoro ya ardhi, migogoro ya ndoa, miradhi na waajiri kuwaachisha kazi waajiriwa bila kufuata taratibu.

  Aidha amewaambia wanasheria hao wametakiwa kutoa msaada wa kisheria kwa watu na makundi ya watu wasio na uwezo katika mashauri ya madai ya jinai, kushuhulikia malalamiko mbalimbali juu ya utoaji haki kutoka kwa wananchi na kuwaelekeza pamoja na kuwaelimisha wapi waende kupata suluhu ya haki zao.

  Hata hivyo mkuu huyo wa wilaya amesema swala la uandikaji wa miradhi ni changamoto kwa jamii hivyo nivyema wananchi wakapata msaada huo wa kisheria ili kupunguza changamoto mbalimbali za mashauri yanayohusiana na maswala ya miradhi.

  ‘’kati ya mambo munayotakiwa kufanya yaani wajibu wenu pia nipamoja na kuandika nyaraka tofauti za kisheria kama kuandika wosia, mikataba pamoja na kutoa msaada kwa njia ya simu’’ amesema makonda.
  Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wanasheria vijana watakao jitolea katika wilaya zote za Dar es salaam ili kuwasaidia wananchi katika maswala ya kisheria leo jijini Dar es Salaam. picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

  Mkuu wa Wilaya Temeke Mh.Felix Lyaniva akimshukuru Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kwa ubunifu wake wakupeleka wanasheria katika kila wilaya zote za Dar es salaam ili kuwasaidia wananchi katika maswala ya kisheria leo jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wilaya na wanasheria leo jijini Dar es Salaam.

  0 0  Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akizungumza kabla ya kumkaribisha Mpogolo kuzungumza

  Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, Rajab Luhwavi akimkaribisha kuzungumza, Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akizungumza na viongozi waandamizi wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma leo. katika mazungumzo hayo Mpogolo amewataka viongozi hao kumpa ushirikiano ili kuongoza vizuri, huku akisisitiza kuwa atakuwa akifanyakazi kwa kufuata mstari ulionyooka,na pale atakapokuwa akilazimika kusema hatakuwa akimung'unya maneno. Kulia ni Luhwavi.  Katibu wa Sekretarieti ya CCM, Anamringi Macha akikaribisha ugeni kabla ya mazungumzo ya Mpogolo na watumishi waandamizi wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma 
  Katibu Msaidizi Ndugu, Kazidi naye akitoa shukrani na maneno machache baada ya kupewa nafasi ya kuzungumza mwishoni mwa mazungumzo hayo
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo (watatu kushoto-walioketi) na Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi wakiwa katika picha ya kumbukumbu na viongozi hao waandamizi wa makao makuu ya CCM mwishoni mwa mazungumzo.


  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa  akizungumza na watumishi wa serikali na halmashauri ya wilaya ya Longido  kwenye ukumbi wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere  uliopo kwenye Ofisi za halmashauri hiyo Desemba 16, 2016.
    Baadhi ya watumishi wa serikali na halmashauri ya wilaya ya Longido  wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere uliopo kwenye Ofisi za halmashuri hiyo Desemba 16, 2016.
   Waziri  wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe  akiwasalimia  watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Longido kabla ya kumwalika Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa kuzungumza nao kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo wa Julius Kambarage Nyerere Desemba 15, 2016.
   Mkuu wa Wilaya ya  Longido , Daniel Chongolo,  akisoma taarifa ya maendeleo ya wilaya hiyo mbele ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye ukumbi wa halmashuri hiyo wa Julius Kambarage Nyerere Desemba 16, 2016.


  0 0

  Na Adili Mhina, Lindi.

  Tume ya Mipango imefanya ziara katika mradi wa ufugaji ngo’ombe na uzalishaji wa maziwa unaoendeshwa na watawa eneo la Narunyu wilayani Lindi na kushauri uongozi wa mradi huo kutumia fursa za mikopo ya kilimo ili kupanua wigo wa uzalishaji wa mazao ya mifugo pamoja na kuongeza uzalishaji wa nishati ya umeme kwa kutumia kinyesi cha wanyama.

  Mradi huo umekuwa ukizalisha maziwa na nyama kwa ajili ya biashara huku nishati ya umeme kwa ajili kuendesha shughuli za kiwanda hicho ikiwa inazalishwa kutokana na kinyesi cha wanayama hao.

  Kwa sasa uzalishaji umepungua baada ya kiwanda kushindwa kuzalisha nishati ya umeme ya kutosha na kuanza kutegemea umeme wa tanesco ambao kwa mujibu wa mmoja wa wasimamizi wa mradi huo, Bi Yasinta Mrose umesababisha gharama za uzalishaji kuongezeka. 

  Changamoto nyingine ni  kuharibika kwa baadhi mashine zinazotumika kuandaa malisho ya ngo’ombe, ukosefu wa soko la karibu kwa mazao ya nyama na maziwa, pamoja na uhaba wa maeneo kwa ajili ya malisho ambapo kwa sasa mradi una zaidi ya ng’ombe 400. 

  Kutokana na changamoto hizo, Kaimu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango Bibi Florence Mwanri aliueleza uongozi huo kuwa ni vyema wafanye taratibu za kuomba mkopo hususani katika benki ya kilimo ili waweze kuongeza mtaji, uzalishaji na kupanua soko. 
   Baadhi ya ng’ombe wa maziwa wa mradi wa ufugaji ngo’ombe na uzalishaji wa maziwa unaoendeshwa na watawa eneo la Narunyu wakiwa katika banda.
   Bi Yasinta Mrose (Mtawa) akimwonesha Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Florence Mwanri hatua za awali za kutengeneza gesi kwa kutumia kinyesi cha ng’ombe.
   Kaimu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango, Florence Mwanri akiwa ndani ya chumba ambapo gesi inazalishwa (gesi ipo ndani ya turubai lililojaa ndani ya chumba hicho linaloonekana chini).
   Mwonekano wa Kiwanda cha kuzalisha nishati inayotokana na kinyesi cha ng’ombe.


  0 0


  0 0


  0 0

  Na Humphrey Shao, 
  Globu ya Jamii

  MSANII na mtayarishaji wa filamu nchini ,Timoth Kachumia (TIKO) amewataja Idris Sultani na Irene Paul kuwa watasindikiza usiku wa wa kachumbari utakaofanyika katika ukumbi wa Aqua Coco Beach jijini Dar es Salaam.
  Akizungumza na Globu ya Jamii Tiko amesema kuwa wasanii hao pia watapata fursa ya kuonyesha filamu yao kwa mara ya kwanza inayokwenda kwa jina la ‘Kiumeni’.
  “Kachumbari show" itajumuisha vitu vingi sana ambapo wasanii tofauti watakapowekwa katika jukwaa moja na kufanya kazi tofauti za sanaa ikiwemo sanaa za maonyesho za majukwaani muziki wa bongofleva na filamu”amesema Tiko.
  Ameweka wazi kuwa katika shoo hiyo kutakuwa na mashindano ya kutafuta vipaji na Stand Up Comedy kutoka kwa wasanii wakali katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.  0 0


  0 0

   
  Mkuu wa chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Mbeya (MUST)  Profesa Mark Mwandosya, sambamba na uongozi wa chuo hicho na wanafunzi pamoja na wadau mbalimbali wamezungumzia haja mama ya  kuboresha huduma zitolewazo na  chuo hicho hasa kwa kutoa elimu kwa wanafunzi wa jinsi zote kwani idadi kubwa ya wanafunzi wa chuo hicho wengi ni jinsia ya kiume.

  Profesa mwandosya amesema wakati akihutubia katika Lecture yake ya kwanza chuoni hapo kuwa idadi kubwa ya  watu wanayakimbia masomo ya sayansi na teknolojia kwa dhana ya kuhisi masomo hayo ni magumu haswa kwa jinsia ya kike.
  "Masomo yasayansi na teknolojia yanamjenga mtu kiakili na kifikra pia kukupa uwezo mwanafunzi kujiajili pia kuwaajili watu.
  "Masomo ya sayansi na teknolojia sio magumu kama ambavyo wengi wanadhani...Uwezo wa kuwapata wanasayansi wazuri wenye kuweza kuwakilisha vizuri ndani na nje ya Tanzania tunao na wakati ni sasa kuwahimiza watoto wetu kuwaandaa vizuri kujifunza sayansi na teknolojia", amesema Profesa Mwandosya.
  Mkuu wa chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Mbeya (MUST)  Profesa Mark Mwandosya akihutubia wanafunzi wa chuo hicho pamoja na wadau mbalimbali kutoka ndani  na nje ya mkoa wa mbeya. 

  Profesa Mwandosya akihutubia hadhara katika hutuba aliyokuwa akiitoa kwa wanafunzi na wadau mbalimbali walio hudhuria chuoni hapo katika ukumbi wa Nyerere chuo cha Sayansi na Teknolojia  cha Mbeya (MUST) jijini Mbeya.
  Makamu mkuu wa chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) Profesa Joseph Msambichaka akizungumza na wadau pamoja na wanafunzi wa chuo hicho.
  Baadhi ya wadau na wanafunzi wa MUST wakimsiliza  profesa Mark Mwandosya. PICHA ZOTE NA MR.PENGO WA MMG MBEYA.

  0 0

  Mkulima wa Korosho kutoka Mtwara ambaye pia ni mdau  mkubwa wa Globu ya jamii, Bw. Bazil Lyakinana, leo amejinyakulia nondozz yake ya Shahada ya Umahiri wa Sayansi katika Menejiment ya Rasilimali watu (Masters of Science in Human Resource Management)  Chuo kikuu Mzumbe kampasi ya Dar es salaam. Hongera sana Bazil.


  0 0


  0 0
 • 12/16/16--12:30: A song from my son via smule
 • Shikamoo baba hope you are doing well ...check out this video when i decided to have some fun leo - Alihassan

  0 0

  Na  Mwene Said wa Blogu

  ya Jamii, Dar es Salaam.

  Mwanzilishi-mwenza na Mkurugenzi wa Kampuni  ya Jamii Media, Maxence Melo Mubyazi (40), leo amepelekwa mahabusu baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana katika kesi moja kati ya tatu zinazomkabili ikiwamo ya kuzuia Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi na kuendesha mtandao wa Jamii Forum bila usajili.

  Mapema jana asubuhi mshtakiwa huyo ambaye pia ni mfanyabiashara  na bosi wa mtandao huo, alifikishwa katika viunga vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  jijini Dar es Salaam mapema asubuhi.

  Alipandishwa kizimbani saa 3:29 kusomewa mashtaka katika kesi yake ya kwanza mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba. 
  Upande wa mashtaka  uliongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mohamed Salum akisaidiana na Wakili wa Serikali Mkuu, Yohanes Kalungula. 
  Wakili Salum alidai kuwa katika tarehe tofauti kati ya Aprili Mosi na Desemba 13, mwaka huu eneo la Mikocheni, jijini Dar es Salaam, mshtakiwa akiwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Jamii Media Ltd, inayoendesha mtandao wa kijamii wa Jamiiforums, akiwa anajua polisi wanafanya uchunguzi kutokana na taarifa zilizochapishwa katika mtandao huo, alishindwa kutoa taarifa. Ilidaiwa kuwa mshtakiwa alishindwa kutoa taarifa ambazo ziko chini yake huku akijua ni kosa. 
  Mshtakiwa alikana shtaka hilo, upande wa Jamhuri ulidaia kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika, na haukuwa na pingamizi la dhamana hivyo uliomba tarehe nyingine ya kutajwa. 
  Hakimu Simba alisema mshtakiwa atakuwa nje kwa dhamana kwa kuwa na wadhamini wawili wanaotoka taasisi zinazotambulika au serikalini, watakaotia saini hati ya dhamana ya Sh. Milioni 10 kila mmoja. 
  Mshtakiwa alitimiza masharti hayo dhidi ya kesi hiyo na imepangwa kutajwa Desemba 29, mwaka huu.

  Katika kesi ya pili, mshtakiwa alisomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Godfrey Mwambapa. Wakili Salum alidai kuwa katika tarehe tofauti kati ya Mei 10 na Desemba 13, mwaka huu eneo la Mikocheni, jijini Dar es Salaam, mshtakiwa kama Mkurugenzi wa Kampuni ya Jamii Media Ltd, inayoendesha mtandao wa kijamii wa Jamiiforums, huku akijua kwamba polisi wanafanya uchunguzi kuhusu taarifa zilizochapishwa katika mtandao wake, alishindwa kutoa taarifa hizo ambazo ziko chini yake. Mshakiwa alikana shtaka hilo. 
  Upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado unaendelea na haukuwa na pingamizi la dhamana na uliomba tarehe ya kutajwa. Hata hivyo, mshtakiwa katika kesi hii alishindwa kutimiza masharti ya dhamana kwa kutokuwa na wadhamini na alirudishwa mahabusu hadi Desemba 29, mwaka huu kesi yake itakapotajwa.

  Katika kesi ya tatu, mkurugenzi huyo alipandishwa kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa. 
  Wakili Salum alidai kuwa katika tarehe tofauti, kati ya Desemba, mwaka 2011 na Desemba 13, mwaka huu eneo la Mikocheni, jijini Dar es Salaam, mshtakiwa akiwa kama mkurugenzi wa kampuni hiyo, aliendesha mtandao wa kijamii ujulikanao kama Jamiiforums.com bila kuwa na usajili wa kuendesha mtandao huo. 
  Katika shtaka la pili, katika tarehe tofauti, kati ya Januari 26 na Desemba 13, mwaka huu eneo la Mikocheni, jijini Dar es Salaam, mshtakiwa akiwa mkurugenzi wa kampuni hiyo inayoendesha mtandao wa kijamii wa Jamiiforums huku akijua kwamba polisi wanafanya uchunguzi kuhusu taarifa zilizochapishwa katika mtandao wake alishindwa kutoa taarifa hizo ambazo ziko chini yake. 
  Mshtakiwa alikana mashtaka hayo. Upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. 
  Hakimu alisema mshtakiwa atakuwa nje kwa dhamana kwa kuwa na mashahidi wawili wanaotoka taasisi zinazotambulika watakaosaini hati ya dhamana ya Sh. Milioni Moja kila mmja pamoja na mshtakiwa. Mshtakiwa alitimiza masharti hayo na kesi yake itatajwa Januari 16, mwaka 2017.

   
   Mwanzilishi na Mtendaji Mkuu wa Mtandao wa JamiiForums, Maxence Melo akiongozwa na Askari Polisi wakati alipofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es salaam leo, kusomewa mashtaka yanayomkabili.
  0 0


  Na Stella Kalinga, Simiyu.
  Serikali Mkoani Simiyu imeagiza Shule zote za Serikali Mkoani humo kuhakikisha kuwa ifikapo Januari 09 mwaka 2017 zinatumia Chaki zinazotengenezwa Wilayani Maswa.

  Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka wakati wa ziara yake aliyoifanya  wilayani Maswa kwa lengo la kukagua ujenzi wa Miundombinu ya shule  ikiwa ni pamoja na vyumba vya madarasa.
  “Kuanzia Januari 09 mwakani shule zitakapofunguliwa Wakuu wa Shule, Walimu wakuu na Wazabuni wanaofanya kazi na shule za  Serikali  wahakikishe wananunua chaki zinazotengenezwa na Vijana wa Wilaya ya Maswa. Haya ni maelekezo na hayajadiliki”, alisema Mtaka.

  Mtaka amewataka Wananchi Mkoani Simiyu kujenga utamaduni wa kupenda na kuthamini vitu au bidhaa zinazozalishwa hapa nchini.
  Mkuu huyo wa mkoa ameongeza kuwa Maono ya Serikali ya Mkoa ni kuzalisha bidhaa zote ambazo malighafi yake yanapatikana hapa nchini na kubadili mtazamo na fikra za Watanzania walio wengi wanaoamini kuwa  bidhaa bora ni zile zinazotengenezwa nje ya nchi.

  Mtaka amewataka Viongozi wa Kisiasa kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Watendaji wa Serikali katika ngazi zote, ili waweze kufikia azma ya Mkoa wa Simiyu  kuwa Mkoa kiongozi kwa kutekeleza kwa Vitendo Ilani ya Chama cha Mapinduzi , ikiwa ni pamoja na kuifikia Tanzania ya Viwanda kwa kuanzisha viwanda vidogo hususani vya kuyaongezea thamani mazao yanayozaliswa mkoani humo.
    Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa (kulia) akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka (wa pili kulia) alipotembelea Shule ya Msingi Maswa kukagua ujenzi wa Vyumba vya madarasa  wakati wa ziara yake wilayani humo.
   Kiongozi wa kikundi cha Simiyu Umoja Arts Group cha Wilayani Maswa, Ally Kazembe  (kulia) akitoa maelezo juu ya utengenezaji wa sabuni kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (wa tatu kulia) alipotembelea kikundi hicho wakati wa  ziara yake wilayani humo.
  Mkuu wa Wilaya ya Maswa,Mhe.Dkt. Seif Shekalaghe akizungumza na wananchi wa wilaya hiyo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa MODECO wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


  0 0
 • 12/16/16--23:59: MDAU IMELDA ALAMBA NONDOZZ!!
 • Mdau wa siku nyingi wa globu ya jamii – IMELDA KILLIAN MITTI, amelamba nondozzz yake ya Utawala wa Biashara katika mahafali ya Taasisi ya Uhasibu kampasi ya Dar Es Salaam jana.
  Hongera sana Mdau Imelda, na endelea kuhabarika, kuburudika na kuelimika na Globu ya Jamii...
                                                 

  0 0

   Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP Ernest Mangu (wapili kulia) akiwaongoza askari na Maofisa wa Jeshi la Polisi katika matembezi ya pamoja ya kuimarisha afya ya mwili katika mkoa wa kipolisi wa Kinondoni Jijiji Dar es salaam leo, kulia ni Kamanda wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia nchini (DCP) Frasser Kashai, anayefuata ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni (SACP) Susan Kaganda.
   Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia wakiwa katika matembezi ya pamoja ya kuimarisha afya ya mwili yaliyoongozwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Ernest Mangu (hayupo pichani) yaliyofanyika katika mkoa wa kipolisi wa Kinondoni jijini Dar es salaam leo.
      Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia wakifanya mazoezi ya viungo mara baada ya kumaliza matembezi ya pamoja ya kuimarisha afya ya mwili yaliyoongozwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu (hayupo pichani) katika mkoa wa kipolisi wa Kinondoni leo. 
     Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia wakifanya mazoezi ya viungo mara baada ya kumaliza matembezi ya pamoja ya kuimarisha afya ya mwili yaliyoongozwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu 

  Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni (SACP) Susan Kaganda, akipita katikati ya dimbwi la maji maeneo ya Kinondoni Makaburini, yaliyotokana na mvua iliyonyesha mapema asubuhi, wakati akiwa katika matembezi ya pamoja ya kuimarisha afya ya mwili yaliyoongozwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Ernest Mangupamoja na askari na mofisa wa Jeshi la Polisi.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP Ernest Mangu (wapili kushoto) pamoja na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni (SACP) Susan Kaganda, wakifanya mazoezi ya viungo mara baada ya kumaliza matembezi ya pamoja ya kuimarisha afya ya mwili katika mkoa wa kipolisi wa Kinondoni.
  (Picha zote na Demetrius Njimbwi – Jeshi la Polisi)


  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa  akipokea taarifa ya maendeleo ya wilaya ya Arumeru baada ya kusomewa  taarifa hiyo na Mkuu  wa wilaya hiyo,   Alexander  Mnyeti kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Arusha leo  Desemba 17, 2016.
   Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa  akipokea taarifa ya maendeleo ya wilaya ya Arumeru baada ya kusomewa  taarifa hiyo na Mkuu  wa wilaya hiyo,   Alexander  Mnyeti kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Arusha leo  Desemba 17, 2016
   Sehemu ya watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Arumeru wakimsikiliza waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Arusha leo  Desemba 16, 2016.
  Watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Arumeru wakimsikiliza waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Arusha, leo Desemba 16, 2016.
  Watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Arumeru wakimsikiliza waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Arusha, leo Desemba 16, 2016.
   (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


  0 0
  0 0

   Mkurugenzi Mkuu mpya wa NIMR,Prof. Yunus D. Mgaya


older | 1 | .... | 1464 | 1465 | (Page 1466) | 1467 | 1468 | .... | 3270 | newer