Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109979 articles
Browse latest View live

WHITEDENT YATOA ZAWADI YA GARI

$
0
0
Mshindi wa Promotion ya Whitedent ya kubuni idadi ya dawa za meno ziliko
kwenye gari mkoani Arusha, Misana Butingo(kulia)akipokea funguo za gari
kutoka kwa Afisa Utamaduni na Michezo wa jiji la Arusha,Benson
Maneno(wapili kushoto) wengine ni Meneja wa Tawi la Whitedent Arusha Joyce Kisanga(kushoto) na Diwani wa Kata ya Themi, Melace Kinabo(picha na Woinde Shizza,Arusha).

KINANA KUFANYA ZIARA YA UKAGUZI WA MALI ZA CCM,AAGIZA WAHUSIKA WAJIPANGE NDANI YA MWEZI MMOJA.

TAFITI: MALARIA BADO NI GONJWA LINAOENDELA KUUA WATOTO WA CHINI YA MWAKA MMOJA KWA WINGI NCHINI.

$
0
0

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

Waziri wa Afya na Maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto, Ummy Mwalimu, amesema kuwa Utafiti unasema kuwa kiwango cha maambukizi ya Malaria kwa watoto chini ya mwaka mmoja kuwa malaria bado ni mojawapo ya magonjwa yanayoongoza kwa kusababisha vifo vya watoto Nchini.

Ummy amesema hayo jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa taarifa ya utafiti wa afya ya uzazi na mtoto na Malaria Tanzania ya mwaka 2015-16 (TDHS-MIS), katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam.

“ asilimia kubwa ya vifo vya watoto na akina mama wajawazito. Kiwango cha maambukizi ya malaria kwa watoto chini ya mwaka mmoja kimeongezeka kutoka asilimia 14 mwaka 2015/16 ukilinganisha na asilimia (9) ya mwaka 2010 kwa kutumia kipimo cha kutoa matokeo kwa haraka yaani Rapid Diagnostic Tests (RDT)” amesema Waziri Ummy.

Ameongeza kuwa anatambua kwamba, suala hili limeshaanza kufanyiwa kazi ndani ya Wizara na niwaombe wadau wote tushirikiane kwa pamoja katika kuendeleza juhudi zilizopo za kuhakikisha Malaria inamalizwa hapa Tanzania. Hivyo natambua Mpango wa Kudhibiti Malaria Tanzania (NMCP) upo katika utekelezaji wa awamu nyingine ya kusambaza vyandarua katika Kaya za Tanzania, tunategemea juhudi hizi na nyingine zinazofanywa na wadau wengine zitachangia kupunguza kiwango cha Malaria hapa nchini.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiongea na wadau mbalimbali katika uzinduzi wa Matokeo ya Utafiti wa Afya ya Mzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2015-16 Tanzania jijini Dar es Salaam leo.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akizindua Matokeo ya Utafiti wa Afya ya Mzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2015-16 Tanzania jijini Dar es Salaam leo.
 Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dr. Albina Chuwa akiongea na  wadau mbalimbali katika Uzinduzi wa Matokeo ya Utafiti wa Afya ya Mzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2015-16 Tanzania jijini Dar es Salaam leo.
 Meneja wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii Sylivia Meku akielezea kwa wadau wa afya Matokeo ya Utafiti wa Afya ya Mzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2015-16 Tanzania jijini Dar es Salaam leo.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dr. Albina Chuwa kabla ya uzinduzi wa Matokeo ya Utafiti wa Afya ya Mzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2015-16 Tanzania jijini Dar es Salaam leo, katikati ni Kaimu Katibu Mkuu  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dr. Mohamed Ally.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja wadau mbalimbali wa Takwimu na Afya katika uzinduzi wa Matokeo ya Utafiti wa Afya ya Mzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2015-16 Tanzania jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Benjamin Sawe- Maelezo)

HUU NDIO UVUKAJI WA BARABARA JIJINI MBEYA

KIKAO CHA KAMATI MAALUM YA HALMASHAURI KUU YA CCM ZANZIBAR.

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamko Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Auai wakiwa katika Kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja.
 Wajumbe wa Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar wakiwa katika kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja,chuini ya mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamko Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamko Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiendesha Kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MKURUGENZI AHAMISHIA OFISI CHINI YA MTI

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi , Marceline Ndimbwa amelazimika kufanyia kazi nje ya ofsi kutokana kukumbwa na majukumu ya kusimamia ujenzi wa madarasa ili kuenenda na kasi ya Rais John Pombe Magufuli aliyemuagiza kumaliza ujenzi huo ndani ya mwezi huu.

Katika hali isiyo ya kawaida Mkurugenzi huyo ambaye ameonekana katika eneo la ujenzi akiendelea na kazi zingine za kiofsi huku akiwa na lundo la mafaili ambayo alikuwa akiyasaini hili kuweza kuruhusu shughuli zingine za kiofisi zikiendelea.

Kwa upande wake Mkurugenzi huyo alipo ulizwa juu ya swala hilo amesema kuwa jambo ni la kawaida katika mazingira ya kazi,kwani jambo moja haliwezi kukwamisha shughuli nyingine zisiendelee wakati wananchi wana mahitaji ya haraka.

Amesema kuwa Rais alimuagiza kuhakikisha kuwa ujenzi huo unakamilika kwa wakati hivyo yeye kama mteule anahakikisha kuwa anatekeleza agizo hilo kwa wakati hili watu wa Malinyi waweze kunufaika na ahadi za Rais Magufuli.

Amemaliza kwa kutoa wito kwa wakazi wa malinyi kuwa na imani na serikali yao ambayo kipaumbele chake ni kutumikia wanyonge kwa kurekebishe miundombinu ya elimu kwa kipindi kifupi.

MAJALIWA AWASILI LOLIONDO KUENDELEA NA ZIARA YA MKOA WA ARUSHA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wanawake wa Kimasai wakati alipotembelea Kituo mafunzo ya kazi za mikono na utamaduni kilichojengwa na UNICEF katika kijiji cha Ololosokwan kilichopo Loliondo wilayani  Ngorongoro Desemba 15, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama kazi mbalimbali za mikono hasa mapambo yanayotengenezwa na wanawake wa kimasai katika kijiji cha Ololosokwan katika tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro wakati alipotembelea Kituo cha Mafunzo ya kazi za mikono na utamaduni  kijijini  hapo Desemba 15, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwa ndani ya nyumba ya asili ya wamasai maarufu kwa jina la Emanyatta katika kijiji cha Ololosokwan  kwenye tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro Desemba 15, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoka ndani ya nyumba ya asili ya wamasai maarufu kwa jina la emanyatta katika kijiji cha Ololosokwan kwenye tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro Desemba 15, 2016. 

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

KIGOGO WA CHADEMA NA ACT-WAZALENDO AHAMIA CCM NA WAFUASI WAKE

$
0
0

Aliyekuwa Mratibu wa Kanda ya Pwani wa Chadema, na Baadaye Mratibu wa Kampeni wa ACT Wazalendo wakati wa uchaguzi Mkuu ulipita, Nixon Tugara akikabidhiwa kadi ya CCM na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipoamua kuhamia CCM wakati wa uzinduzi wa jengo la Kitegauchumi la CCM, Upanga jijini Dar es Salaam, leo.
Nixon Tugara akifurahia kadi yake ya CCM baada ya kukabidhiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo la Kitegauchumi la CCM, Upanga jijini Dar es Salaam, leo
Tugara ambaye ni miongozi mwa watu waliosimamia ujenzi wa jengo hilo la Kitegauchumi akizungumza yaliyomsibu hadi kuhamia CCM, kutoka ACT Wazalendo na Chadema.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdultrahman Kinana akimshukuru Tugara kwa kuwa miongoni mwa viongozi waliosaidia katika kufanikisha ujenzi wa jengo la Kitegauchumi la CCM, lililopo Upanga jijini Dar es Salaam, ambalo amelizindua leo. Kulia ni Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha, Zakia Meghji.
Tugara akimshukuru Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MABALOZI WA NNE KWA WAKATI TOFAUTI NA KUFANYA NAO MAZUNGUMZO

$
0
0
Mabalozi wa Nchi Mbili za Brazil na Kenya wameipongeza serikali ya awamu ya Tano kwa mipango na mikakati yake ya madhubuti ya kulifufua Shirika la Ndege Tanzania -ATCL – kwa kununua ndege mpya kama hatua ya kuhakikisha shirika hilo linakuwa bora katika utoaji wa huduma za usafiri wa anga ndani na nje ya nchini.

Mabalozi hao wamesema hatua hiyo ya kuliimarisha Shirika la Ndege la Tanzania itasaidia kukuza shughuli za utalii na pato la taifa kwa ujumla.Balozi wa Brazil nchini Carlos Alfonso Puente na Balozi wa Kenya hapa nchini Chirau Ali Makwere wametoa pongezi hizo mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ikulu jijini Dar es salaama.

Kwa upande wake, Balozi wa Brazil nchini Carlos Alfonso Puente amesema kutokana na nchi hiyo kuwa ni miongoni mwa nchi kadhaa Dunia zenye viwanda wa kutengeneza ndege hivyo serikali ya Tanzania ina nafasi nzuri ya kununua ndege nchini Brazil hasa kulingana na mahusiano mazuri na ya muda mrefu yaliyopo kati ya nchi hizo mbili.

Kufutia wito huo wa Balozi wa Brazil Nchini, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji wa nchi ya Brazil kuja nchini kutangaza bidhaa wanazotengeneza hasa ndege kama hatua ya kuimarisha mahusiano ya biashara kati ya Brazil na Tanzania.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa kutokana na nchi ya Brazil kupiga hatua kubwa katika uzalishaji wa sukari na Tanzania ni moja ya nchi yenye maeneo mazuri kwa ajili ya uwekezaji huo hivyo ni muhimu kwa wafanyabiasha wa Brazil kuja nchini kwa ajili ya kuwekeza katika sekta hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Kenya Nchi Mhe. Ali Makwere, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Brazil Nchi Mhe. Carlos Alfonso Puente, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Denmark Nchi Mhe. E. Hebogand Jensen, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF), Mhe. Maniza Zaman, mara baada ya kumaliza mazungumzo,Ikulu jijini Dar es Salaam.

WAZIRI MWAKYEMBE AKAGUA UJENZI WA MAHAKAMA YA WILAYA KIGAMBONI

$
0
0
Serikali ya awamu ya tano yadhamiria kujenga mahakama za mwanzo katika kila kata nchini ili kurahisisha upatikanaji wa haki kwa wananchi.

Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe ameyasema hayo alipotembelea ujenzi wa Mahakama ya kisasa ya Wilaya Kigamboni ambayo inajengwa kwa kutumia teknolojia ya Moladi ambapo teknolojia hii inapunguza muda na gharama za ujenzi. Mahakama ya Wilaya ya Kigamboni inagharimu kiasi cha shilingi milioni 572 na  inatarajiwa kukamilika ifikapo Februari 2017. 

Waziri Mwakyembe amesema Wizara ya Mambo ya Katiba na sheria moja ya kipaumbele chake ni kurahisisha upatikanaji wa haki kwa wananchi hivyo huduma za kimahakama zitaendelea kuboreshwa ilim kusogeza huduma kwa wananchi. 

Waziri aliongeza kuwa Sheria ya Msaada wa Kisheria itakapoanza kutumika itasaidia wananchi hasa wasio na uwezo kupata haki zao kupitia wasaidizi wa kisheria.

“Sheria ya Msaada wa Kisheria itakapoanza kutumika itasaidia wananchi hasa wasio na uwezo kupata haki zao kupitia wasaidizi wa kisheria ambao watapatiwa mafunzo rasmi’. Waziri alisema.

Akiishukuru Serikali Mbunge wa Kigamboni Mhe. Faustine Ndugulile amesema anaishukuru Serikali kwa kujenga Mahakama ya kisasa Kigamboni na kusogeza huduma kwa wananchi na pia ameipongeza Serikali kwa kuanzisha sherian ya Msaada wa Kisheria ambayo itasaidia sana wananchi wa kipato cha chini.

Aidha, Mhe. Ndugulile ameomba changamoto za ucheleweshwaji wa kesi Mahakamani na rushwa ziweze kutafutiwa ufumbuzi maana ni kero kwa wananchi.
Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akisisitiza jambo wakati akiangalia mchoro wa jengo la Mahakama ya Wilaya Kigamboni alipotembelea leo (16/12/2016) ili kujionea ujenzi wa Mahakama hiyo ambao unatumia teknolojia ya Moladi.
Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akiangalia mchoro wa jengo la Mahakama ya Wilaya Kigamboni.
Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (mwenye miwani) akionyeshwa vyumba mbalimbali vitakavyotumika katika jengo la mahakama ya wilaya kigamboni ikiwemo mahabusu na vyumba vya mahakama.

KAILIMA RAMADHAN AFAFANUA SHERIA, KANUNI,TARATIBU NA MAADILI YA KUZINGATIWA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA DIMANI -ZANZIBAR

SERIKALI YATOA TAMKO KUHUSU UGONJWA WA ZIKA NCHINI

DKT. SHEIN AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA BRIGEDIA JENERALI MHAIKI, ZANZIBAR LEO

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (katikati) ​akifuatana na W​aziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt.​​Hussein Ali Mwinyi (kushoto) na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange (kulia) wakati Rais alipofika leo katika Hospitali ya Jeshi la Wananchi JWTZ Lugalo Dar es Salaam kwa ajili ya kuuaga mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali Cyril Ivor Mhaiki aliyekua Kamanda wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar,aliyefariki juzi hospitalini hapo baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali Cyril Ivor Mhaiki aliyekua Kamanda wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar, aliyefariki juzi katika hospitali ya Jeshi la Wananchi JWTZ Lugalo Dar es Salaam, ukibebwa na askari kupelekwa sehemu maalum kwa shughuli ya kuuagwa rasmi leo kabla kupelekwa kijijini kwao kwa mazishi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa ​akitoa heshima ya mwisho leo kwa mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali Cyril Ivor Mhaiki aliyekua Kamanda wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar,aliyefariki juzi katika hospitali ya Jeshi la Wananchi JWTZ Lugalo Dar es Salaam, baada ya kuugua kwa muda mfupi.

TIMBULO:NILIACHA UALIMU KUKIMBILIA MUZIKI

$
0
0
Na Humphrey Shao, 
Globu ya Jamii
Msanii wa muziki wa Bongofleva hapa nchini Ally Timbulo ameweka wazi kuwa aliacha ajira ya ualimu na kukimbia kwenye muziki.
Timbulo amesema hayo alipokuwa akizungumza na Ngazi kwa ngazi juu ya nini kilichomfanya ajiunge na muziki huo.
“Nilishaingia tayari katika ajira rasmi ya serikali kwa kufundisha shule ya sekondari ilala lakini siku chache baadae niliamua kuacha kazi ya ualimu na kujikita katika huu muziki ambao leo mimi unanilipa” amesema Timbulo.
Amesema kuwa licha ya swala hilo kuwa gumu kwa wazazi wake lakini ikafika baadae baba yake akaridhia kwa kumpa masharti ya kuakikisha kuwa licha ya kujiingiza katika muziki lakini nisiache dini kama ilivyo kwa watu wengine.
Pia amesema kuwa moja ya vitu vya msingi ambavyo alihusiwa na baba yake ni kuakikisha anapata mke mmoja ambaye tamfaa maishani badala ya kuwa kiluka njia kma wasani wengine hapa nchini.
Mbali na hayo alitumia fursa hiyo kuutambulisha wimbo wake mpya ambao amefanya Baraka Da Prince ambao ameuachia katika vituo mbalimbali vya televisheni hapa nchini na nchi jirani.
Timbulo amesema kuwa video ya wimbo wake huo mpya ambayo ameifanya nchini Kenya ni moja ya kazi zake nzuri zitakazoweza kumuongezea imani kwa mashabiki wake katika kipndi hiki cha kufunga na kufungua mwaka.

KINANA KUFANYA ZIARA YA UKAGUZI WA MALI ZA CCM


MAKONDA KUSAIDIA MATIBABU YA MTOTO ANAYESUMBULIWA NA UVIMBE KICHWANI

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ameahidi kutoa msaada wa shilingi milioni moja katika kila mshahara wake kwa moto mwenye umri wa miaaka mitano Alox Kombe  anayesumbuliwa na tatizo la uvimbe wa kichwa.

Kauli hiyo ameitoa leo ofisini kwake jijini Dar es salaam alipozungumza na waandishi wa habari   kwaajili yakusaidia matibu ya mtoto huyo mpaka pale atakapo pona.

"nitasimamia matibabu ya Alox mpaka pale atakapo pona kwa hiyo leo nitampatia shilingi laki mbili lakini  naomba kila mwezi waje kuchukua shilingi milioni moja katika mshaara wangu  kwaajili ya matibabu ya huyu mtoto anayesumbuliwa na tatitizo hili" Amesema  Makonda.

Sambamba na hayo baba wa mtoto huyo Andea Kombo mkazi wa gongolamboto jijini Dar es salaam   amemshukuru mkuu wa mkoa kwa msaada alioutoa kwaajili ya matibabu ya mtoto wake na kuomba watanzania watakaoguswa na tatizo hilo kumsaidia kwaajili ya matibabu ya mtoto huyo.

"namshukuru sana mkuu wa mkoa kwakuwa na moyo wa kujitolea na  pia kuweza kuahidi kunisaidia matibabu ya mtoto wangu mpaka pale atakapo pona pia nawaomba watanzania wezangu kunisaidi kwaajili ya matibabu ya mtoto wangu" amesemaa kombo.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akiwa amembemba mtoto huyo, alipofika ofisini kwake leo.
Baba wa mtoto, Alox Kombe akizungumza na waandishi wa habari na kumshukuru mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa kuwa na moyo wa kujitolea na pia kuweza kuahidi kusaidia matibabu ya mtoto wake mpaka pale atakapo pona.

TCRA YATOA UFAFANUZI SAKATA LA MWANZILISHI WA JAMIIFORUMS MAXENCE MELO

WAZIRI MKUU AMSIMAMISHA KAZI MWEKAHAZINA WA WILAYA YA BAH

$
0
0
*Aagiza arudishwe Longido kujibu tuhuma zinazomkabili


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi aliyekuwa Mwekahazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido, Bw. Issai Mbilu ambaye kwa sasa amehamishiwa Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma na kuagiza arudishwe haraka na kuja kujibu tuhuma za ubadhilifu sh. milioni 642.4 za miradi zinazomkabili.


“Tunaendelea kudhibiti na kuweka nidhamu ndani ya Serikali. Ukiharibu Longido usitegemee kuhamishiwa wilaya nyingine tunamalizana hapa hapa. Hatuwezi kuhamisha ugonjwa hapa na kuupeleka wilaya nyingine hivyo Mwekahazina huyu arudishwe haraka Longido,” amesisitiza.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Desemba 16, 2016) wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Arusha.

Pia amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Bw. Richard Kwitega kumuandikia barua Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) akimuomba amrudishe Mwekahazina huyo katika kituo chake cha kazi cha zamani ili aweze kujibu tuhuma zinazomkabili.

SOMA ZAIDI HAPA

RUBY ATOA CHOZI BAADA YA WIMBO WAKE MPYA KUVUJA

$
0
0

Na Mwandishi wetu.
Msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya Ruby, amelalamikia kitendo cha wimbo wake ujulikanao kwa jina la 'Kwikwi' kuvujishwa katika baadhi ya mitandao mbalimbali ya kijamii bila ya yeye kujua. Ruby amesema kuwa wimbo huo alitarajia kuutoa mwakani ikiwa kama ishara ya kufungua mwaka na kitu kipya. 
Msanii huyo ambaye amekua akitamba na wimbo wake wa 'Walewale' ambao aliutoa katikati ya mwaka huu huku ukionesha kuvutiwa sana na mashabiki wake. 
Mwaka huu Ruby alishiriki katika msimu wa nne wa Coke Studio Africa uliofanyika nchini Kenya na kushirikiana na wasanii wakubwa kama vile Yemi Alade wa nchini Nigeria pamoja na Nyashinski wa nchini Kenya.

VOA SWAHILI: Zulia Jekundu S1 Ep 104: Kanye West, Nick Cannon, Blac Chyna, Will Smith na Selena Gomez

Viewing all 109979 articles
Browse latest View live




Latest Images