Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1458 | 1459 | (Page 1460) | 1461 | 1462 | .... | 3286 | newer

  0 0


  0 0


  0 0


   Waziri wa Habari, Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akiwapongeza Wasanii mbalimbali waliojinyakulia tuzo zao usiku wa leo,zilizofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar,ambapo Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ali Kiba ameibuka kinara kwa kujinyakulia tuzo tatu.
   Waziri wa Habari, Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na Wasanii mbalimbali waliojinyakulia tuzo zao usiku wa leo.
  1
  Waziri wa Habari, Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akikabidhi Tuzo ya Heshima kwa DJ Boniventura Kilosa aka Bony Love baada ya kutangazwa mshindi wa heshima katika tuzo za EATV AWARDS 2016 zilizofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Malimani City jijini Dar es salaam.Tuzo hizo zimeandaliwa na kituo cha Televisheni cha EATV cha jijini Dar es salaam kinachorusha matangazo yake katika nchi za Afrika Mashariki.
  2
  DJ Boniventura Kilosa aka Bony Love akipongezwa na DJ John Dilinga mara baada ya kupokea tuzo yake ya Heshima katika tuzo zilizoandaliwa na Kituo cha Televisheni cha EATV.
  5
  Mwanamuziki Lady Jay Dee akipongezwa na mwenza wake baada ya kupokea tuzo yake katika hafla ya utoaji wa tuzo za EATV AWARDS zilizofanyika kwenye ukumbi wa Malimani City jijini Dar es salaam.
  1
  Mwanamuziki Ali Kiba akipokea tuzo yake ya ushindi wa Wimbo Bora wa Mwaka kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania ,Nandi Mwiyombela  katika Tuzo za Muziki za EATV AWARDS zilizofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.

  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Hassan Suluhu akikata utepe kama ishara ya kuzindua  Makati wa Taifa Dhidi ya Rushwa na Mpango wa Utekelezaji Awamu ya Tatu, kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais utumishi na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki akishuhudia zoezi hilo pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Bw. Valentino Mlowola.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Hassan Suluhu akihutubia watumishi na wananchi wakati wa kilele cha  Maadhimisho ya siku ya maadaili na haki za binadamu zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam
   Makatibu Wakuu wa Wizara mbali mbali pamoja na viongozi wa Dini wakifuatilia kwa makini hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati akihutubia kwenye Kilele Cha Maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu.


  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  MSTAHIKI meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Jacob Masawe amesema kuwa eneo litalakolokuwa limepimwa na kugundulika ni eneo la wazi au kwa ajili ya huduma za kijamii kama Manispaa wapo tayari kulipa fidia kwa wananchi ili kupisha.

  Hayo ameyasema leo kwenye mkutano na wananchi wa mtaa wa Kunguru, kata ya Goba wakiwa pamoja na taasisi binafsi inayijishughulisha na masuala ya upangaji na upimaji wa maeneo nchini HUSEA. 

  Jacob amesema, anatoa sifa kubwa sana kwa hatua iliyofikiwa na wananchi wa Kunguru kwa kuamua kupima maeneo yao wenyewe na zaidi kwani Halmashauri ndiyo wenye majukumu ya kufanya hivyo ila kwa hatua hiyo waliyofikia kwa kushirikiana na HUSEA wamefanya jambo kubwa sana na wanawaunga mkono kwa jitihada hizo. 

  "Kutakapotokea kama kuna eneo ambalo ni eneo la wazi au kwa ajili ya huduma za kijamii na limejengwa na mkakubaliana kupata eneo lingine kwa ajili ya shughuli hizo basi msisite kutuambia kwani ili sisi kama Halmashauri tuweze kulipa fidia, "amesema Jacob. 

  Mwenyekiti wa HUSEA, Renny Chiwa amesema kuwa kwa hatua hii imeweza kusaidia katika kupanga maeneo ya mtaa wa Kunguru na zaidi wananchi wameweza kushirikiana nao kwa hatua nzuri mpaka kufikia kuweka makubaliano ya upangaji wa maeneo na kuna baadhi ya wananchi wamejitolea kuacha maeneo yao kwa ajili ya kuendeleza mipango endelevu. 

  Katika eneo la Kunguru, kumeweza kupatikana kwa maeneo 1432 na wameweza kuyapima na waliweza kupata ushirukiano mzuri kutoka kwa Wizara ya Ardhi na waliweza kuwapa ramani halisi ya eneo hilo ila kutokana na wanachi tayari wameshajenga wamepata sura ya ramani ambayo ni mpya na itakapokamilikwa kupimwa kuanzia mwezi Januari mwakani watafanya mabadiliko ya ramani hiyo. 

  Mkurugenzi wa Mipango Miji na Vijiji, Prof John Lupala amesema kuwa wao kama Wizara wamedhamiria kuhakikisha wanashirikiana na makampuni binafsi kuweza kupima na kupanga maeneo ya makazi ya watu mjini na vijijini na zaidi mpaka kufikia mwaka 2016 ni asilimia 15 tu ya maeneo yamepimwa. 

  Mradi huo ulianza mnamo mwezi Mei mwaka huu na uliweza kupata changamoto mbalimbali kutoka kwa wananchi ikiwemo watu kusema kuwa ni makampuni ya kitapeli ila baada ya kuwapa elimu waliwez kuelewa na siku ya kwanza ya mkutano huo wananchi zaidi ya 800 walijiandikisha kwa ajili ya kupimiwa maeneo yao. 
  Mstahiki meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Jacob Masawe akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Kunguer kata ya Goba wakati wa Mkutano wa Upangaji na Upimaji wa eneo hilo unaoendeshwa na Kampuni ya HUSEA, kulia ni Mwenyekiti wa HUSEA, Renny Chiwa na kushoto ni Mkurugenzi wa Mipango Miji na Vijiji, Prof John Lupala 
  Mwenyekiti wa HUSEA, Renny Chiwa .

  akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Kunguer kata ya Goba wakati wa Mkutano wa Upangaji na Upimaji wa eneo hilo na kuelezea namna kampuni yake ilivyojikita katika kuhakikisha wanasaidiana na serikali kwenye utatuzi wa migogoro na upangaji wa maeneo. Akiwa amekaa meza moja na Diwani wa kata ya Goba Ibrahim Kenya (wa kwamza kushoto), Mkurugenzi wa Mipango Miji na Vijiji, Prof John Lupala. 
  Wananchi wakiwa wanaelezewa namna Mtaa wa Kunguru ulivyopimwa na kutakiwa kupangwa.

  0 0


  Na Anthon John Globu ya jamii.
  IKIWA  imesalia siku moja kufikia maadhimisho ya kuzaliwa Mtume Muhammad Kiongozi wa waislam wa madhebu ya shia Ithnashariya  Tanzania  Shekhe Hemed  Jalala amewataka  watanzania kuwa na tabia ya kuhurumiana hasa wenye uwezo kuwahurumia wasio na uwezo.

  Akizungumza na waandishi wahabari Leo katika ukumbi wa habari maelezo Jijini Dar es salaam amesema Mtume Mohammad alifundisha kuwa dini imekuja kutunza Upendo na amani hivyo ni vyema waTanzania  kuishi kwa Upendo bila kujali utofauti wa dini zao.
    
  "Mtu kupenda nchi ni katika amani na pia dini imekuja kutunza upando na amani watanzania tusibaguane kutokana na dini zetu" amesema Jalala.

  Hata Hivyo Sheikh Hemed amebainisha kuwa ni vyema jamii kuyaishi maisha aliyoishi Mtume Mohammad ikiwa ni pamoja na sifa kuumbili alizokuwa nazo Mtume ambazo  nikuwa mkweli na mwaminifu.
    
  Sambamba na hayo ameongeza kuwa Kazi kubwa inayotakiwa kufanywa na watanzania hasa kwa kipindi hiki chakukumbukwa kwa kuzaliwa kwa Mtume ni kuishi kwa amani na ushirikiano kwa kuwa vitabu vyote vya dini vimekuja kuunganisha watu.            
  Shekhe Hemed Jalala  akizungumza na waandishi wa habari kueleka maadhimisho ya Siku ya kuzaliwa Mtume ( S.A.W), kulia ni mlezi wa Hauzat  Imamu Swadiq Mzee Rashidi  Mashtog na  upande wa kushoto ni  Naibu kiongozi Mkuu Mohammad Abdi .            

  0 0
  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 

  Vijana wametakiwa kubeba uchumi wa viwanda wa Tanzania inayojengwa katika serikali ya awamu ya Tano ya Dk. John Pombe Magufuli.

  Hayo ameyasema Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Edwin Rutageruka wakati wa semina ya vijana iliyofanyika katika maonesho ya viwanda yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba leo jijini Dar es Salaam.Amesema semina imefika muda mwafaka kutokana na nchi kwenda katika sekta ya viwanda ambapo vijana ndio sehemu yao.

  Amesema sekta ya viwanda inategemea vijana ambao ndio waendeshaji wa viwanda katokana na ujuzi wao wa kuendea viwanda hivyo.Nae Mwakilishi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation, amesema vijana wanatakiwa kutumia fursa ya viwanda pamoja na ujasirimali na kuachana na kufikiria suala la kuajiriwa.

  Amesema Taasisi Doris Mollel Foundation,imeona inawajibu wa kutoa elimu kwa vijana katika kuendea sekta ya viwanda.Amesema kuwa kila mmoja akatumia nafasi yake vizuri Tanzania inaweza kuondoka ilipo sasa na kusogea sehemu nyingine katika uchumi wa viwanda .

  Akifunga simina hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link (GEL),Abdulmalik Mollel amesema hakuna tatizo la ajira kwa vijana kuajiriwa kinachofanya vijana na kukosa mafunzo ya kazi ambayo wanakwenda kufanya.Amesema kutokana na mafunzo hayo kupitia maonesho ya viwanda atafanya mafunzo vijana ambao wanakwenda kutumika katika viwanda wakiwa wanakitu kichwani.

  Mollel amesema hakuna mtu anaweza akamuachia kijana kiwanda kwa elimu alioipata anatachotaka mwajiri ni kijana mwenye ujuzi wa kutumikia kiwanda chake.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Edwin Rutageruka akizungumza katika ufunguzi wa semina ya vijana kuelekea uchumi wa viwanda iliyofanyika katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
  Mwakilishi wa Taasisi Doris Mollel Foundation, Erick Kajwahura akizungumza katika semina vijana kuelekea uchumi wa viwanda iliyofanyika katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link (GEL),Abdulmalik Mollel akifunga semina ya kuelekea uchumi wa viwanda iiyofanyika katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam leo.


  0 0

  Na Raymond Mushumbusi WHUSM.

  Wadau wa Sanaa nchini wameshauriwa kujitokeza kudhamini tuzo kwa ajili ya wasanii wa muziki na filamu nchini ili kuendelea kuzipa nguvu tasnia hizo kwa maendeleo yake.

  Ushauri huo umetolea jana na wazori wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokuwa akizungumza katika hafla ya utoaji tuzo kwa wasanii wa muziki na Filamu nchini zilizoandaliwa na kituo cha Televisheni cha East Africa (Channel 5).

  Ameongeza kuwa wadhamini wengi wajitokeze kwa ili kuongeza idadi ya tuzo zenye kiwango kinachostahili zenye kuzingatia weledi na usawa katika utoaji wake.“Niwaombe wadau wa sanaa nchini jitokezeeni kudhamini tuzo hizi za filamu na Muziki ili tuwe na tuzo nyingi zaidi na zenye viwango vya kimataifa”Alisistiza Mhe. Nnauye.

  Kwa upande wake katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Muingereza amesema kuwa BASATA itaendelea kushirikiana na wasanii na wadau wa Sanaa katika kuandaa na kusimamia tuzo mbalimbali ikiwa ni nia ya Serikali kuikuza tasnia ya muziki na filamu ambayo ni moja ya tasnia inayoajiri vijana wengi kwa sasa.

  “Nawaalika wadau wa Sanaa na wasanii wote sisi tuko tayari kushirikiana nao katika kulisukuma hili guruduma la maendeleo ya Sanaa nchini na nawasahuri tufate tu utaratibu katiaka kuandaa kazi zenu za sanaa” alisema Bw. Muingereza.

  Aidha mwakilishi wa Bodi ya Filamu Tanzania Bw.Romanus Tairo amesisitiza wasanii wa filamu nchini kufata sheria na gtaratibu zote kabla ya kuandaa na kusambaza filamu zao.

  “Nawaomba wasanii wote wa filamu nchini kufuata Sheria na taratibu zilizopo za kusajili filamu zote zikakaguliwa na kuoewa kibali cha kuoneshwa sehemu mbalimbali”Alisema Bw.Tairo.
  Tuzo za Muziki na Filamu za EATV zimeanzishwa kwa dhumuni la kuongeza chachu ya maendeleo ya tasnia ya muziki na filamu nchini na jumla ya tuzo nane zilitolewa kwa wasanii wa muziki na filamu na tuzo moja ya heshima ilitolewa kwa msanii aliyetoa mchango mkubwa katika tasnia ya muziki nchini Bw. Bonny Kilosa (Dj Bonny Love).

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 

  WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk.Philip Mpango amesema vijana ndiyo wanaweza kuleta mapinduzi ya sekta ya viwanda vinavyojengwa. 

  Dk.Mpango ameyasema hayo  jana wakati alipotembelea Maonesho ya Viwanda yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam, ameseama vijana lazima wachangamkie fursa ya viwanda pamoja na ujasiriamali. 

  Amesema nafasi za ajira ni chache ikilinganishwa na idadi ya vijana wanaohitaji hivyo sekta binafsi ndiyo inaajiri sehemu kubwa ikiwemo kujiajiri. Dk. Mpango amesema sekta ya viwanda inahitaji rasimali watu ambao ni vijana wa kufanya hivyo kwa ujuzi wao. 

  Aidha amesema kila mtu anatakiwakulipa kodi ili serikali iweze kutoa huduma kwa wananchi na kodi isipotumika kwa malengo wananchi wanaweza kuhoji kodi i yao.

  Dk. Mpango amesema serikali haitaki kuibana sekta binafsi ishindwe kupumua kutokana na kodi kinachofanyika kuangalia uwezo wa ulipaji kodi kwa kilakinachozalishwa. Waziri huyo ametoa maagizo kwa Mamlaka ya Chakula Dawa (TFDA), kuwatembelea wajasiriamali ili kuweza kupata changamoto zao.  
  Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link (GEL),Abdulmalik Mollel wakati alipotembelea banda hilo katika viwanja vya sabasaba jana jijini Dar es Salaam. 
  Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango akitoa maagizo kwa Meneja Uhusiano kwa Umma wa TFDA, Gaudensia Simwanza wakati alipotembelea banda la TFDA katika viwanja vya sabasaba jana jijini Dar es Salaam. 
  Wananchi wakipata huduma katika banda la majani ya chai katika maonesho ya viwanda yanayoenelea katika viwanja sabasaba jijini Dar es Salaam. 
  Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.  0 0

  Na Adili Mhina, Lindi.

  Kaimu Katibu Mtendaji, Wizara ya Fedha na Mipango upande wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri amefanya ziara katika eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata Gesi Asilia lililopo katika mtaa wa Likong’o Manispaa ya Lindi na kushauri uongozi wa Manispaa hiyo kuongeza  juhudi za kuhakikisha wananchi waliopisha mradi huo wanalipwa fidia kwa wakati.
  Mwanri alieleza kuwa ni vyema uongozi ukatilia mkazo umuhimu wa kuwalipa fidia wananchi ili waweze  kujiletea maendeleo yao kwa kuwa hawawezi tena kuendelea kutumia eneo hilo.
  Alieleza kuwa dhamira ya Serikali ya kujenga uchumi wa viwanda inaenda sambamba na kuwajali wananchi wake kwa kutoa fidia kwa mujibu  kanuni na sheria pale wanapolazimika kuachia  maeneo yao ili kupisha miradi ya maendeleo.
  Mwanri aliongeza kuwa pamoja na kuwa mradi huo utakapojengwa na kukamilika utakuwa na faida kwa maendeleo ya Taifa kwa ujumla utasaidia pia kuinua kipato kwa wanachi wa Lindi kutokana na fursa mbalimbali za ajira zitakazojitokeza kwa wakazi hao.
   Nae Mtendaji wa Mtaa wa Ling’oko ambapo ndipo mradi huo unapotekelezwa, Bw. Jacob Anton alieleza kuwa wananchi wa eneo hilo wana matarajio makubwa na wanatoa ushirikiano wa kutosha kwa Serikali kwa kuwa wanaamini ujio wa kiwanda hicho utasaidia kuboresha maisha yao.
  Timu ya Ukaguzi wa Miradi kutoka Tume ya Mipango ikiongozwa na Naibu Katibu Mtendaji huyo, kwa sasa inaendelea na zoezi la ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo katika Mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara ambapo itatembelea miradi ya Serikali na ile ya sekta binafsi kwa lengo la kuhakikisha malengo ya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016/17-2020/21) yanatekelezwa kwa ufasaha.
   Kaimu Katibu Mtendaji, Wizara ya Fedha na Mipango upande wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri akikagua nyaraka mbalimbali ikiwemo ramani ya eneo litakalojengwa kujengwa kiwanda cha kuchakata gesi asilia katika eneo la Likong’o Mkoani Lindi. 
   Afisa Ardhi wa Manispaa ya Lindi, Bw. Munisi Andrew (aliyeshika nyaraka) akisikiliza maelekeza kutoka kwa Kaimu Katibu Mtendaji, Wizara ya Fedha na Mipango - Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri. Wengine ni maafisa wa manispaa hiyo pamoja na wataalamu kutoka Tume ya Mipango.
   Afisa Mipango Miji Manispaa ya Lindi, Bw. Ismaelo Chepa (mwenye t-shirt) akitoa maelezo juu ya ramani ya eneo la ujenzi wa kiwanda cha kuchakata gesi. Pembeni ya Kaimu Katibu Mtendaji ni Mchumi Kuu kutoka Tume ya Mipango, Bibi Salome Kingdom.


  0 0

   Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM, kilichofanyika leo mjini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, na Kushoto ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein.
   Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk John Magufuli akiwa na baadhi ya viongozi kabla ya kikaokuanza. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Kushoto, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha Dk Magufuli kufungua kikao
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha Dk Magufuli kufungua kikao
   Mwenyekiti wa CCM, Dk John Magufuli akimsalimia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar, Dk Shein, alipowasili ukumbini.


   Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akimsalimia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Jerry Silaa, alipowasili ukumbini kwenye kikao cha kamati kuu ya CCM, kilichofanyika mjini Dar es Salaam, leo.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Mbwa ni mnyama kama wanyama wengine ambao huweza kupata magonjwa mbalimbali ambayo hupelekea kufa au kuwapa vilema vya maisha. Mbwa ni kama binadamu yoyote tu ambaye akishambuliwa na magonjwa basi anaweza kuwa dhaifu na kupelekea kupoteza maisha au kupona lakini pia ni wanyama kama binadamu tu wengine ambao hata wakipatwa na baadhi ya magonjwa basi wanaweza kustahimili na kupona kabisa.

  Basi leo tutaangalia baadhi ya magonjwa yanayowapata viumbe hivi vinavyopendwa sana na rafiki mkubwa wa binadamu. Kama ilivyo kwa wanyama wengine na binadamu ugonjwa uanza kuonekana kutokana na dalili flani ambapo ndio zinakupa taarifa za kuhisi kuwa mnyama huyu ni mgonjwa. Lakini kuna baadhi ya magonjwa ukiona dalili zake basi unajua kabisa kuwa ishatafuna sehemu kubwa na kupona ni majaaliwa na hali ipo hivyo hivyo kwa wanyama kama Mbwa.

  Tuanze na Huu leo

  1:Parvovirus Infection (Kwa kifupi uitwa Parvo)
  Ugonjwa huu ni ugonjwa unaosababishwa na Virusi ambapo mara nyingi hushambulia mbwa wadogo wenye umri wa kuanzia wiki sita mpaka miezi sita. Ugonjwa huu ni moja ya ugonjwa mbaya sana kwa mbwa kwasababu unapomuingia tu basi matumaini ya kupona kwa mbwa huyo ni madogo sana kwasababu ni ugonjwa ambao ukimpata mbwa ndani ya masaa 24 unaweza kupelekea kifo kwa mbwa huyo.

  Ugonjwa huu husambulia sana mapigo ya moyo na kupelekea mapigo ya moyo ya mbwa huyo kwenda mbio sana, na kumfanya hapoteze hamu ya kula, joto kushuka sana.


  0 0


  0 0


  0 0
  0 0

  Na Dotto Mwaibale

  WAFANYABIASHARA katika Soko la Madenge katika Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam wamejenga kisima cha maji salama chenye thamani ya sh.milioni 5.6 kwa kutumia nguvu zao na fedha za  ushuru wanaolipa.

  Akizungumza na mtandao wa  www. habari za jamii.com Katibu Mkuu wa Soko hilo Shaban Malonji 'maarufu kama Wailala' alisema umoja walionao wafanyabiashara katika soko hilo ndio uliofikia maazimio ya kujenga kisima hicho chini ya viongozi wao.

  " Binafsi napenda kuwapongeza wafanyabiashara wa soko letu kwa kuwa na umoja ambao umefanikisha kukamilisha ujenzi wa kisima hiki ambao utakamilika rasmi mapema wiki hii" alisema Malonji.

  Malonji alisema kwa muda mrefu changamoto yao ilikuwa ni kukosa maji sokoni hapo ndipo walipokaa na wafanyabiashara wa soko hilo na kufikia maazimio ya kujenga kisima hicho ambacho kitakuwa kikitoa huduma ya maji sokoni hapo.

  Alisema fedha za ujenzi wa kisima hicho zimetokana na ushuru wanaotoa wafanyabiashara hao na fedha zinazopatikana baada ya kulipa huduma ya choo cha kulipia pamoja na fedha za ushuru asilimia 10 wanazopewa na Manispaa.
   Fundi Martin Justine akitengeneza paa la kisima cha maji safi kinacho jengwa Soko la Madenge Temeke jijini Dar es Salaam kwa nguvu za wafanyabiashara. Ujenzi wa kisima hicho umegharimu sh.milioni 5.6.
   Katibu Mkuu wa Soko hilo, Shaban Jabir Malonji 'maarufu kama Wailala' akimuonesha mwandishi wa mtandao huu (hayupo pichani), kisima hicho.
   Katibu Mkuu wa Soko hilo, Shaban Jabir Malonji 'maarufu kama Wailala' akimuonesha mwandishi wa mtandao huu (hayupo pichani), kisima hicho.


   Katibu Mkuu wa Soko hilo, Shaban Jabir Malonji 'maarufu kama Wailala'  akinawa maji yanayotoka katika kisima hicho ambacho ujenzi wake umekamilika kwa asilimia kubwa.


  0 0

  NA VICTOR MASANGU, MSOGA 
  .
  KATIKA kukuza sekta ya michezo hapa nchini hususan soka la vijana wadogo wa shule Rais Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete kwa kushirikiana na serikali ya chini watarajia kujenga kiwanja cha michezo cha kisasa katika Kijiji Cha msoga kilichopo halmashauri ya mji mdogo Chalinze Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
  Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete (kushoto) na Mwakilishi wa Balozi wa China nchini Tanzania, Yang Tong (koto jeusi) wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete alipokuwa akifafanua jambo.Picha zote na John Sambila, Chalinze.

  Akizungumza katika halfa maalumu iliyoandaliwa kwa ajili ya kwenda kutembelea eneo ambalo litajengwa uwanja huo Kikwete amesema kwamba uwanja huo wa wa mpira wa miguu utajengwa kwa ufadhili wa serikali ya watu wa chini na kuongeza utakuwa ni mkombozi mkubwa katika kukuza na kuinua vipaji kwa vijana wadogo.

  Kikwete alisema kwamba lengo lake kubwa ni kuhakikisha kwamba Tanzania katika siku za usoni inakuwa ni wachezaji wengi wenye vipaji ambao wataweza kuunda timu nzuri ya Taifa ambayo itaweza kufanya vizuri katika mashindano mbali mbali ya Kimataifa. 
  Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akizungumza katika hafla hiyo. 

  “uwanja huu wa mpira wa miguu pindi utakapokamilika utaweza kuwa ni mkombozi mkubwa wa vijana wadogo hususan wale wa shule, hivyo nimeshazungumza na rafiki zetu wa serikali ya china na wamekubali kutujengea kwa hivyo ni jambo la msingi sana katika kuendeleza sekta ya michezo kwa watoto wetu hawa mbao wataweza kuleta mafanikio makubwa katika siku zijazoa,”allisema Kikwete.
  Katika hatua nyingine Kikweke ametoa pongeza kwa serikali ya china kwa kuona umuhimu wa kuweza kusaidia kujenga kiwanja hicho, na kuongeza kuwa pindi kitakapokamilika kitakuwa ni michezo mingine ambayo itakuwa ikifanyika mbali na mchezo huo wa soka lengo ikiwa ni kuwapa fursa vijana kuweza kuonyesha vipaji walivyonavyo.

  Naye Mwakilishi wa balozi wa china nchini Tanzania Yang Tong ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano wa dhati katika kukuza sekta ya mchezo hususan kwa vijana wadogo ikiwa samba na kujenga viwanja ili watoto wasiweze kucheza katika viwanja vya vumbi.
  Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhione Kikwete alisema kwamba lengo lake kubwa ni kuhakikisha anakuza michezo wa vijana wadogo katika jimbo lake hivyo kukamilika kwa ujenzi wa uwanja huo kutaweza kuwasaidia vijana kukuza vipaji vyoa.

  Nao baadhi ya wadau wa mcheo wa soka katika kiji hicho cha msogo akiwemo i Michael James pamoja na Mohamed Halfan wamempongeza Rais mstaafu Jkaya Kikwete kwa ubunifu wa ujenzi huo wa uwanja kwa ajili ya vijana wadogo kwani kutaweza kusaidia kwa kisi kikubwa katima kuleta mabadiliko chanya katika mchezo huo.
  KUKAMILIKA kwa ujenzi huo wa kiwanja cha kisasa cha mpira wa miguu katika kijiji cha soga ambacho alizaliwa rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete kutaweza kutoa fursa kwa vijana wadogo kuweza kukuza na kuonyesha vipaji walivyonavyo katika medani ya mchezo wa mpira wa miguu.

  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  MAMLAKA ya maji safi na taka Dar es Salaam (DAWASCO) Mkoa wa Ilala imeanzisha mpango kabambe wa kupambana na tatizo la ukosefu wa maji safi na huduma ya maji taka kwa kufungua dawati la DAWASCO katika kila ofisi ya serikali ya mtaa.

  Akizungumza na Globu ya Jamii, Meneja wa Dawasco mkoa wa Ilala, Christian Kaoneka  amesema kuwa dawati hilo litasaidia kulinda mfumo na kupunguza kero kwa wananchi kwa kudhibiti  mivujo ya maji katikati ya jiji kwa kushirikiana na viongozi wa mitaa na Madiwani ambao wao ndio wapo karibu na wananchi.

  “Uwepo wa Dawati hili la DAWASCO katika kata ya Gerezani kumesaidia kutatua kero ya muda mrefu ya uvujajai wa maji katika barabara ya Nyerere jirani na hoteli ya Collesium na hii imefanikiwa kwa kushirikiana na watu wa serikali ya mtaa” amesema Kaoneka.

  Amesema ufunguzi wa dawati hili unafungua fursa ya kila mwananchi kuwa huru kueleza utendaji wa Dawasco Ilala aidha kutakuwa na mtu maalum wa kupokea maunganisho mapya kwa wateja wapya na changamoto zote.

  Amesema kuwa  changamoto bado zipo nyingi hivyo anawaomba wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha hasa katika swala zima la usafi wa mazingira katika mifumo ya Maji Taka kwa kuwaomba wasitupe mifuko ya Plastiki hovyo pia waweze kusaidia kufichua watu wote wanaojiusisha na wizi wa maji.

  Amemaliza kwa kusema kuwa kuna operesheni maalum kwa wezi wa maji ambayo inafanyika mtaa kwa mtaa kwa takayekutwa hatua kali za kisheria zitachukulia dhidi yake .

  Ametaja kuwa tayari ameshakutana na viongozi wa kata ya Kariakoo, Gerezani, Buguruni, Mchikichini, Kisutu, Upanga , Jangwani na Kivukoni kwa ajili ya kuimarisha operesheni hiyo.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela (watatu kulia) akikabidhi hundi kwa mawanachama wa Mfuko wa LAPF, Nchama Renatus (wapili kushoto) ambaye ni mnufaika wa fao la zazi kwa wanawake wanachama wa mfuko huo na kuhuhudiwa na wanufaika wengine wa Mkoani Mwanza jana. Kushoto ni Meneja wa LAPF Kanda ya Ziwa, Yesaya Mwakifulefule ambapo alisema Sh bilioni 8.3 zimetumika kuwalipa fao la uzazi wanawake wanachama wa mfuko huo.

  Mfuko wa LAPF umeweza kulipa fao la uzazi kwa jumla ya wanchama elfu kumi Tangu mfuko  huo uanze kulipa fao hilo kwa wanchama wake mwaka 2012.

  Akiongea katika hafla hiyo Meneja wa LAPF, Kanda ya ziwa,  Yessaya Mwakifulefule amesema LAPF imetumia zaidi ya shilingi  bilioni 8.3 kulipa fao la uzazi kwa kina mama wanachama wa Mfuko huo.

  Akikabidhi hundi ya malipo hayo kwa mwanachama Nchama Renatus ambae ni mwalimu wa shule ya msingi Uhuru iliyopo Nansio Ukerewe,Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela ameupongeza mfuko wa LAPF kwa kuwajali wanachama wake na kulipa mafao kwa wakati.
   Meneja wa LAPF Kanda ya Ziwa, Yesaya Mwakifulefule akiwa amemapaka mtoto wa Mwanachama wa mfuko Nchama Renatus (katikati) baada ya mama huyo na wenzake kukabidhiwa hundi zao za fao la uzazi. Jumla ya sh bilioni 8.3 zimetumika kuwalipa fao la uzazi wanawake wanachama wa mfuko huo mkoani Mwanza. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela akiwa amepakata mtoto wa mnufaika.
  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela (watatu kulia) akikabidhi hundi kwa mawanachama wa Mfuko wa LAPF, Nchama Renatus (wapili kushoto) ambaye ni mnufaika wa fao la zazi kwa wanawake wanachama wa mfuko huo na kuhuhudiwa na wanufaika wengine wa Mkoani Mwanza jana. Kushoto ni Meneja wa LAPF Kanda ya Ziwa, Yesaya Mwakifulefule ambapo alisema Sh bilioni 8.3 zimetumika kuwalipa fao la uzazi wanawake wanachama wa mfuko huo.
   Picha ya pamoja ya wanufaika na mgeni rasmi.
  Meneja wa LAPF Kanda ya Ziwa, Yesaya Mwakifulefule akisalimia.

older | 1 | .... | 1458 | 1459 | (Page 1460) | 1461 | 1462 | .... | 3286 | newer