Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1459 | 1460 | (Page 1461) | 1462 | 1463 | .... | 3285 | newer

  0 0

   Serikali ya wilaya ya Hanang mkoani Manyara, imeagiza kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria zaidi ya viongozi 8 wa serikali ya kijiji cha Gidika pamoja na mtendaji wa kata ya Getanusi kwa kusababisha mgogoro wa zaidi ya miaka mitano kutokana na kukiuka maazimio ya mkutano mkuu wa kijiji hicho juu ya ugawaji wa ardhi kwa wananchi wa eneo hilo.

  Maagizo hayo yalitolewa na mkuu wa wilaya ya Hanang Mhe. Sara Msafiri, huku kaimu afisa ardhi wilayani humo akifafanua juu ya utaratibu wa eneo hilo ambalo limetolewa na serikali kwa wananchi kugawiwa katika kata hii ya Getanus baada ya shamba hilo kurejeshwa kwa wananchi ikiwa ni sehemu ya shamba lililokuwa chini ya NAFCO.

  Baada ya maagizo hayo ikiwemo kurejeshwa maeneo yaliyouzwa kinyume cha taratibu pamoja na yale ambayo viongozi walijigawia kinyume na mkutano mkuu wa kijiji.
  Aidha inadaiwa wananchi wa kata hio hutoa vitisho vya kuwapiga mishale viongozi wa kijiji pamoja na wataalam wa upimaji wa ardhi pindi wanapojaribu kuendesha zoezi la upimaji katika eneo hilo.

  0 0  0 0

   Mazoezi ya kwanza ya wiki ya kikosi cha Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC katika uwanja wao wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es salaam, kujiandaa na mchezo wa kwanza wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya African Lyon, utakaofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Jumapili hii saa 10.00 jioni.
   Mazoezi ya kwanza ya wiki ya kikosi cha Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC katika uwanja wao wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es salaam, kujiandaa na mchezo wa kwanza wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya African Lyon, utakaofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Jumapili hii saa 10.00 jioni.
   Mazoezi ya kwanza ya wiki ya kikosi cha Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC katika uwanja wao wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es salaam, kujiandaa na mchezo wa kwanza wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya African Lyon, utakaofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Jumapili hii saa 10.00 jioni.
   Mazoezi ya kwanza ya wiki ya kikosi cha Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC katika uwanja wao wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es salaam, kujiandaa na mchezo wa kwanza wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya African Lyon, utakaofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Jumapili hii saa 10.00 jioni.
  Mazoezi ya kwanza ya wiki ya kikosi cha Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC katika uwanja wao wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es salaam, kujiandaa na mchezo wa kwanza wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya African Lyon, utakaofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Jumapili hii saa 10.00 jioni.

  0 0

  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustin SAUT, Padri Dkt.Thadeus Mkamwa (kushoto), akitoa taarifa kuhusiana na Mahafali ya 18 ya chuo hicho yatakayofanyika kwa siku mbili, Ijumaa Desemba 16 na Jumamosi Desemba 17 mwaka huu chuoni hapo Malimbe Jijini Mwanza. 
  Kulia ni Bw. Bernald James ambaye ni Mkuu wa Mawasiliano, Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania.Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Mwanza Mhashamu Yuda Thadeus Rwaichi. 
  Jumla ya wahitimu 2421 wa fani mbalimbali wanatarajiwa kutunukiwa vyeti, shahada, shahada za uzamili na uzamivu katika mahafali hayo huku wanafunzi wanafunzi 746 wakishindwa kutunukiwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutolipia ada.
  Mahafali hayo yatatanguliwa na Siku ya Jamii itakayofanyika Jumatano Disemba 14 ambapo kutakuwa na Maonesho ya Kitaaluma.

  0 0

  We are thrilled for your support!!!
  Our fundraising event on Saturday, December 10, 2016 was a huge success. Because of your participation in our auction and generous donations, we were able to raise $7,041 whereas our goal was $5,000. This is $2,041 or about 41% above our goal.
  Please, accept our most sincere thanks for your support. It may not be possible to mention each one by name, but we are indeed grateful to each one of you for your involvement, role played during the event, and even attending our fundraising event. The recap of the money collected is given below:
  Contributions:
  $3,511 Total Cash
  $800 Total Checks
  $4,311 Total Contribution
  Auction:
  $1,295Total Cash
  $280 Total Checks
  $815 Total Quick Pay
  $2,390 Total from the auction
  Pledges:
  $340 Total Pledges

  $7,041 Total Collection
  ($100) Cash - Hall Rental
  $6,941 Total - Bank Deposit

  Summary:
  $4,706 Total Cash on hand
  $1,080 Total checks
  $815 Total Quick Pay
  $340 Total pledges
  $6,941 Bank Deposit
  With your donations, the family will be able to meet immediate financial needs to transport the body of our beloved Brother Leo Mapunda Mwakitalu to Tanzania, and other family arrangement associated with the funeral plans.
  Again, your generous donations and support are very much appreciated.
  May GOD bless you!
  Organizing Committee
  WaTanzania Columbus, Ohio na vitongoji wakijumuika pamoja siku ya Jumamosi Desemba 10, 2016 kwenye harambee ya mpendwa wao Leo iliyofanyka Columbus Ohio kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusafirisha mwili wa marehemu nyumbani Tanzania kwa mazishi. Leo alifariki Desemba 3, 2016 Florida nchini Marekani. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


  0 0

   Wananchi wakiangalia daladala lenye namba za usajili T 161 CRP lililoacha njia na kupinduka Mbagala Misheni kwa Bluda Dar es Salaam leo asubuhi na kujeruhi watu watatu.
  Daladala likiwa mtaroni.

  Na Dotto Mwaibale
  WATU watatu wamejeruhiwa vibaya baada ya daladala walikuwa wamepanda kutoka Temeke kwenda Mbagala Kuu kuacha njia na kupinduka jijini Dar es Salaam.
  Askari wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa kipolisi wa Temeke ambaye hakupenda kutaja jina lake kwa kuwa si msemaji wa polisi alisema ajali hiyo imetokea majira ya saa 12 na nusu asubuhi. Alisema daladala hilo liliacha njia na kutumbukia kwenye mtaro eneo la Mbagala Misheni kwa Bluda baada ya kuteleza kutokana na mvua zilizokuwa zikinyesha.
  Alisema baada ya ajali hiyo wananchi walifika kutoa msaada kwa majeruhi ambao walikimbizwa Hospitali ya Temeke kwa matibabu.
  Alitaja daladala hilo kuwa ni lenye namba za usajili T 161 CRP ambapo alitoa mwito kwa madereva kuwa waangalifu wanapoendesha magari yao hasa katika kipindi ambacho mvua zinanyesha.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewashukuru na kuwapongeza madaktari wa Taasisi ya Bilal Muslim Tanzania ambayo imetoa huduma ya matibabu ya macho kwa zaidi ya wananchi 4,000 wa mkoa wa Dodoma

  Ametoa pongezi hizo jana usiku (Jumapili , Desemba 11, 2016) wakati akizungumza na madaktari waliotoa huduma hiyo walipomtembelea katika makazi ya Waziri Mkuu mkoani Dodoma

  Waziri Mkuu alisema huduma wanayoitoa ni muhimu kwa kuwa imewezesha watu ambao walikata tamaa ya kuona wameona, hivyo aliwaomba waendelee kwenda katika maeneo mengine nchini ili Watanzania wengi zaidi waweze kunufaika.

  "Nawashukuru kwa mchango mkubwa mnaoutoa katika kuunga mkono jitihada za Serikali kwenye utoaji wa huduma za matibabu ya macho bure na kuwawezesha hata wale wasiokuwa na uwezo kupata huduma ," alisema .

  Serikali ya awamu ya Tano ina dhamira ya dhati kuwatumikia wananchi na kutoa huduma kwa wote , hivyo tuko tayari kushirikiana  na taasisi yeyote ambayo inakusudia kuwafikia wananchi.   

  Waziri Mkuu alisema “katika utoaji huduma za jamii , Serikali inathamini sana mchango wa taasisi binafsi na za dini ambazo ziko mstari wa mbele kushirikiana na jamii kwa ujumla,”.

  Katika hatua nyingine Waziri Mkuu aliwakaribisha madaktari hao kuja kuwekeza katika sekta mbalimbali mkoani Dodoma. “Hapa ndio makao makuu ya Tanzania , hivyo nawakaribisha mje kuwekeza, ardhi ya kutosha ipo . Mnaweza kuja kujenga hospitali kubwa ya macho," alisema .

  Naye Naibu wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na  Ajira, Mheshimiwa, Anthony Mavunde alisema jumla ya watoto 250 wamefanyiwa upasuaji wa macho  na madaktari hao ambao walianza kutoa huduma hiyo Desemba 8, 2016 na wanatarajiwa kumaliza Desemba 12, 2016

  "Nawashukuru kwa moyo wenu wa kujitolea  kuja kusaidia watu wenye mahitaji ya matibabu ya macho . Mkoa wa Dodoma una changamoto kubwa ya matatizo ya macho .Nimefarijika sana kuona  baadhi ya akinamama waliokuwa wamekata tamaa ya kuona wameweza kuona tena,” alisema.

  Naye Mtaribu wa taasisi hiyo, Noorelain Sharrif alimuahidi Waziri Mkuu kwamba wataendelea kushirikiana na Serikali katika utoaji wa huduma za matibabu ya macho bure kwa wananchi wenye mahitaji na wako tayari kwenda popote nchini kutoa huduma hiyo

  “Tuko tayari kushirikiana na Serikali katika kutimiza wajibu wetu kwa jamii , tutafanya hivyo wakati wowote na kwa wananchi wote,” alisema.

  0 0  0 0

  A High Level Dialogue between the officials of the East African Community and the Development Partners concluded on 6th December 2016, in Dar es salaam, Tanzania, with the Development Partners commending the Secretary General of the East African Community, Amb. Liberat Mfumukeko for his outstanding work and commitment in enhancing efficiency of EAC processes and procedures through introduction of reforms.

  At the dialogue, held at the official residence of the Norwegian Ambassador to United Republic of Tanzania, H.E. Hanne-Marie Kaarstad, the Development Partners expressed renewed confidence in EAC with UK, Canada, France and Turkey committing to resume contributions to the EAC through the Partnership Fund in the next financial year.

  The Secretary General was accompanied by Hon. Christophe Bavizamo, Deputy Secretary General in charge of Productive and Social Sectors; Hon. Jesca Eriyo, the Deputy Secretary General in charge of Finance and Administration; and other Senior Officers from the EAC Secretariat.

  Prior to the dialogue, the Secretary General met and held discussions with H.E. Hanne-Marie Kaarstad, the Norwegian Ambassador, who is also the Chair of the Partnership Fund High Level Committee. Their discussions revolved around the future of the Partnership Fund including the succession of the Partnership Fund Chairmanship and recruitment of a dedicated Manager for the Fund. She expressed her appreciation for the outstanding work the Secretary General had exhibited since he took over the leadership of the Community. H.E. Hanne-Marie has been the Chair of the Committee for the last 3 years and will be completing her term on 31st December 2016.

  READ MORE HERE

  0 0

  Kamera ya Globu ya Jamii imewanaja vijana hawa wakiwa wamedandia gari kwa nyuma ambapo chini yake kuna ujumbe usomekao "Mashujaa wa Unyanyembe", katika barabara ya Kawawa, Jijini Dar es salaam.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania, Alhaj Abukary Zubeiry Bin Ally baada ya kuwasili Shelui mkoani Singida kuwa mgeni rasmi katika Baraza la Maulid Desemba 12, 2016. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba baada ya kuwasili Shelui mkoani Singida kuwa mgeni rasmi katika Baraza la Maulid Desemba 12, 2016. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, January Makamba. Muungano na Mazingira.
  Baadhi ya washiriki wa Baraza la Maulid wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia Baraza hilo , Shelui mkoani Singida, Desemba 12, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0


   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akimuangalia Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji akitia ubani kama ishara ya Kuyafungua Maluid matukufu ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) Sherehe zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja
   Waislamu na Wananchi waliohudhuria katika sherehe tukufu ya Maulid ya kuzalia kwa Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Unguja
   Ustadh Ali Muombwa Hassan wa Chuo cha Kiislamu akitoa Tafsiri ya Qur'aan Tukufu  ya Suratul Touba (Aya 128 hadi 129) iliyosomwa  katika  sherehe tukufu ya Maulid ya kuzalia kwa Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Unguja
   Wanafunzi wa Madrassa Hidayatul Munineema na Nurul Islamia ya Mpendae Mjini Unguja wakisoma Qaswida YaRabii Swali katika sherehe tukufu ya Maulid ya kuzalia kwa Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Unguja
  Ustadh Mohamed Khamis Rashid wa Kiweani Pemba akisoma maulid Barzanji mlango wa kwanza katika sherehe tukufu ya kuzalia kwa Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Unguja. Picha na IKULU, Zanzibar.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0
 • 12/12/16--06:08: HAYA SASA NI MAKUSUDI
 • Pichani ni Gari ndogo aina ya Subaru ililazimisha kuvuka upande wa pili kwa barabara eneo la Tabata jijini Dar, huku taa nyekundu ikiwa imewaka.
  Askari wa Usalama barabarani ambaye alilazimika kuingia barabarani na kumtaka dereva wa gari hilo kusimama na kumuelekeza sehemu ya kuegesha kutokana na tukio hilo, ili taratibu zingine za kisheria ziweze kufuatwa.

  0 0

   BAADA ya kupona majeraha ya nyonga, beki wa kulia wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Shomari Kapombe, amesema kuwa hivi sasa anapambana vilivyo kurejesha makali yake yaliyomfanya akubalike na mashabiki wa timu hiyo.

  Beki huyo kipenzi wa mashabiki wengi wa soka nchini, amerejea mazoezini hivi sasa kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), alishindwa kuitumikia vema timu hiyo baada ya kukosa mechi 10 za mwisho za mzunguko wa kwanza wa ligi kufuatia majeraha hayo.

  Akizungumza na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz Kapombe alisema kuwa kwa sasa anazidi kujiandaa vema kupitia mazoezi wanayopewa na benchi la ufundi la timu hiyo pamoja na mengine binafsi anayoyafanya peke yake.

  “Mimi binafsi nimejiandaa vizuri na naendelea kujiandaa vizuri kwa mazoezi ambayo tunapewa na mengine ya kwangu binafsi, yote hayo nafanya ili kupambana na kurejesha makali yangu ili kuisaidia Azam FC,” alisema.

  Kapombe alisema kwa sasa anaendelea vizuri na afya yake ipo vizuri kabisa kuweza kupambana kwa ajili ya kufanya vizuri kwenye mzunguko wa pili wa ligi unaoanza Jumamosi ya wikiendi hii.

  Sura mpya dirisha dogo

  Kapombe pia alifurahishwa na namna wachezaji wapya waliosajiliwa kwenye dirisha dogo la usajili, ambapo amedai kuwa ni wachezaji wazuri na anaamini ya kuwa wataisadia sana Azam FC kuelekea mechi za mzunguko wa pili.

  “Mpaka sasa kuna sura mpya ambazo zimeongezwa, ni wachezaji wazuri wanaokuja kuziba mapungufu ambayo tumayaona mzunguko wa kwanza, kila mchezaji aliyekuja hapa anasifa yake na uzuri wake kuweza kuisaidia timu yetu katika kufikia malengo tuliyojiwekea,” alisema.

  Hajawaacha mashabiki

  Beki huyo mwenye sifa ya kupandisha mashambulizi kwa kasi na uwezo kufunga mabao, aliyeweka nyavuni mabao 11 msimu uliopita, kuelekea raundi ya pili ya ligi amewaachia ujumbe mashabiki wa timu hiyo akiwaambia kuwa waunganishe nguvu kuwasapoti uwanjani katika mechi zao.

  “Mimi ninachowaomba mashabiki wa Azam FC ni waendelee kuwa nasi katika vipindi vyote vya shida na raha, waunganishe nguvu na waendelee kutusapoti katika mechi za raundi ya pili ili na sisi tuweze kufika pale Azam FC inapohitajika kufika,” alimalizia.

  Azam FC inayodhaminiwa na kinywaji safi cha Azam Cola, kinachoburudisha koo na kuchangamsha mwili pamoja na Benki bora kwa usalama wa fedha zako ya NMB, inatarajia kufungua ng’we ya mzunguko wa pili kwa kukipiga na African Lyon Jumapili hii Desemba 18 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam saa 10.00 jioni.

  0 0

  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge la Israel (Knesset) Mhe. Yuli Yole Edelsten wakati Mhe. Spika alipomtembelea Bungeni hapo. Mhe Ndugai yupo nchini Israel kwa ibada ya Hija.(Picha na Ofisi ya Bunge).

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Waioba akimkabidhi Cheti cha kupanda Mlima Kilimanjaro,Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi,Jenerali Mstaafu George Waitara.
  Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akimkabidhi Cheti cha kupanda Mlima Kilimanjaro,Naibu Kamnada wa kikosi cha ardhini,Brigedia Jenerali Jairo Mwaseba aliyefanikiwa kufika kilele cha Gilman's umbali wa mita 5685 kutoka usawa wa Bahari.
  Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akimkabidhi Cheti cha kupanda Mlima Kilimanjaro,Mwenyekiti Mstaafu wa Bodi ya Utalii (TTB) Balozi Charles Sanga aliyefanikiwaa kufika kilele cha Stella umbali wa mita 5756.
  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu ,Jenerali George Waitara na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na waongoza watalii walioshiriki kufanikisha safari ya Waandishi wa Habari na Askari wa jeshi la Ulinzi kupanda mlima Kilimanjaro. Na Dixon Busagaga wa Blogu ya Jamii Kanda ya Kaskazini. 
  0 0

  Wateja wa Vodacom Tanzania wameletewa promosheni mpya inayojulikana kama”Nogesha Upendo”ambayo itawawezesha wateja wake kujishindia zawadi ya fedha taslimu ,muda wa bure wa maongezi na MB za Interneti kila siku katika msimu huu wa sikukuu. Zawadi zenye thamani ya shilingi Bilioni 5 zitatolewa kwa wateja ambapo wateja wapatao 500 wataweza kujishindia shilingi milioni 1kila mmoja katika kipindi chote cha msimu wa promosheni.

  Akiongea wakati wa uzinduzi ,Afisa Mtendaji Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia alisema “Vodacom Tanzania tunayo furaja kuzindua promosheni ya msimu wa sikukuu ya Nogesha Upendo inayolenga kuleta shamrashamra za furaha ya sikukuu kwa wateja wetu.

  Tunajua sikukuu hizi zinaleta familia za kitanzania na marafiki pamoja kufurahi na kutumiana salamu za upendo, tumeleta promosheni hii kwa ajili ya kuwazadia wateja wetu wote kila wanaponunua vifurushi vya muda wa maongezi na Data kila siku. ”Promosheni hii itawezesha wateja wetu 500 kujishindia kila mmoja shilingi milioni 1/- katika droo za wiki na wengine watajishindia shilingi 100,000/- katika droo za kila siku katika msimu huu wa sikukuu kupitia promosheni hii”.

  Aliongeza kusema “Mbali na wateja kujishindia dakika tano za muda wa bure wa maongezi na kuperuzi internet,wateja wa Vodacom pia kila watakaponunua vifurushi wataingizwa kwenye droo za kila siku na kila wiki za kujishindia vitita vya fedha.Kiasi cha shilingi milioni 700 zimetengwa kwa ajili ya kuwazawadia wateja wetu katika msimu huu wote wa sikuu”.

  Kwa ujumla, Vodacom imetenga zawadi zenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 5/- kwa ajili ya kuzawadia wateja wake kwa njia ya fedha taslimu, muda wa maongezi na bando za intaneti(MB). Promosheni hii itakayodumu kipindi cha miezi 2 kuanzia leo ni kwa ajili ya wateja wote wa Vodacom ambao laini zao ziko hewani na watakanunua vifurushi vya kupata huduma mbalimbali za kampuni.

  “Promosheni ya Nogesha Upendo imebuniwa kwa ajili ya kuwashukuru wateja wetu kwa kutuunga mkono muda wote, Tunawatakia heri katika msimu wa sikukuu na tunawakumbusha wakati wote kufuatilia zawadi watakazokuwa wanazishindia kutoka mtandao wa Vodacom kuanzia muda wa maongezi na fedha taslimu zitakazowawezesha kufurahia sikukuu pamoja na familia zao na marafiki. Hivi ndivyo Vodacom tumejizatiti kufanya Maisha ya wateja wetu kuwa murua na kusambaza upendo”alisisitiza Mworia.
    Afisa Mkuu wa Masoko wa Vodacom Tanzania,Ashutosh Tiwary (kushoto)na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano, Nandi Mwiyombella (kulia) wakimsikiliza Afisa Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Uhusiano wa Kampuni hiyo, Rosalynn Mworia (katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Promosheni ya”Nogesha Upendo” leo jijini Dar es Salaam itakayowawesha wateja wa kampuni hiyo kujishindia muda wa maongezi,Vifurushi vya intaneti pamoja na  fedha taslimu, shilingi Bilioni 5/- zimetengwa kwa ajili ya promosheni hii ambapo wateja 500 watajishindia shilingi Milioni 1/- kila mmoja  kupitia droo za kila wiki kwa msimu huu wa sikukuu.

  Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kuzinduliwa rasmi Promosheni ya Nogesha Upendo leo jijini Dar es Salaam itakayowawesha wateja wa kampuni hiyo kujishindia muda wa maongezi,Vifurushi vya intaneti pamoja na  fedha taslimu, shilingi Bilioni 5/- zimetengwa kwa ajili ya promosheni hii ambapo wateja 500 watajishindia shilingi Milioni 1/- kila mmoja kupitia droo za kila wiki kwa msimu huu wa sikukuu.

  0 0

  Mtu mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja, akiwa amebebwa na wasamalia wema na kupandishwa kwenye Bajaj, mara baada ya kupata ajali iliyohusisha pia magari manne asubuhi ya leo katika Barabara ya Mandela, eneo la Tabata jijini Dar es salaam. Chanzo cha ajali hiyo inadaiwa kuwa ni moja ya gari lililokuwa mbele kusimama ghafla kufuatia mtu huyo aliyekuwa akivuka barabara. 
  Mashuhuda pamoja na Askari Polisi wakimsikiliza majeruhi huyo (aliekuwa amelala chini kando ya barabara) baada ya kupata ajali hiyo.


  0 0

  Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imekutana leo tarehe 13/12/2016 jijini Dar es salaam kwa kikao cha siku moja cha kawaida. Kikao hicho kimeongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli.

  Pamoja na mambo mengine, Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imepokea taarifa ya Tathimini ya Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, baada ya kuitafakari taarifa hiyo, Halmashauri Kuu imeamua yafuatayo;-

  1. Kupunguza idadi ya wajumbe wa vikao na idadi ya vikao vya Chama katika ngazi mbalimbali ili kuongeza ufanisi wa utendaji wa Chama na kuongeza muda wa viongozi wa Chama kufanya kazi za Chama kwa Umma badala ya kutumia muda mwingi vikaoni.

  Ili kuwa  na vikao vya Chama vyenye tija imeamuliwa kama ifuatavyo:-

  a). Halmashauri Kuu ya Taifa kwa sasa ina jumla ya wajumbe 388 idadi ambayo ni kubwa sana, hivyo imeamuliwa idadi hii ipunguzwe na kuwa wajumbe 158 kama  ifuatavyo:-


  0 0

  Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Charlse Mwijage akizungumza wakati wa uzinduzi kitabu maalum cha kuanisha fursa mbalimbali zilizopo nchini, iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mitutano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Jijini Dar es salaam.

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  WIZARA  ya Viwanda na biashra kupitia kituo cha uwekezaji(TIC)  wameingia makubaliano na wataalamu nguli wa utafiti kuanisha fursa zote zilizopo nchini.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Waziri wa Viwanda Biashara na uwekezaji ,Charlse Mwijage amesema kuwa wataalamu hao wataweza kutusaidia kuto ahabari za kutosha juu ya fursa zilizopo hapa nchini.
  Mkurugenzi Mkazi wa Oxford Business Group, Ivana Carapic akizungumza katika hafla hiyo.

  “Sijaridhika na namna tunavyojitangaza hivyo  tunapashwa kuandika habari  nyingi  juu vitu tulivyonavyo hasa hzi fursa kupita majarida makubwa duniani na vyombo mbalimbali vya habari” Amesema Mwijage.


  Ameitaka tasisi hiyo kutengeneza kitu ambacho watanzania awawezi kutengeneza na kufikisha mahali ambapo wataalamu wetu awawezi kufikisha kwa uraisi lakini wao watafika na kusikilizwa.

  Waziri Mwijage ametaja kuwa mara baada ya Asia kukua katika uwekezaji sehemu iliyobaki ni Afrika  na nchi yenyewe ni Tanzania ambapo kuna kila namna na mazingira ya uwekezaji kwa tasisi za nje.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Clifford Tandari (kulia) akishikama mkono na Mkurugenzi Mkazi wa Oxford Business Group, Ivana Carapic mara baada ya kuaisiana makubaliano ya kiutafiti katika kuanisha fursa mbalimbali zilizopo nchini, iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mitutano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Jijini Dar es salaam.

  Kwa upande wake mkurugenzi wa TIC, Clifford Tandari amemuakikishia waziri kuwa watalaam hao wana uwezo wa hali ya juu na watawaeza kutengeza kitu ambacho watalaamu wetu awawezi pia kupitia mtandao wa unaofahamika ulimwenguni wataweza kuinganisha mtandao wa TIC hili kila mtu apate kujionea vitu vilivyopo hapa nchini.
  Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Charlse Mwijage (katikati) akizungumza jambo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Clifford Tandari. Kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Oxford Business Group, Ivana Carapic. 
  Baadhi ya Watendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini wakifatilia mkutano huo.

older | 1 | .... | 1459 | 1460 | (Page 1461) | 1462 | 1463 | .... | 3285 | newer