Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109973 articles
Browse latest View live

Ridhiwani Kikwete aendelea na Ziara Jimboni kwake Chalinze

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mh Ridhiwani Kikwete ameendelea na ziara yake ya kushtukiza katika Jimbo lake kukaguwa miradi ya kimaendeo, December 9 amezunguka katika Zahanati na Shule za Secondary Chalize pamoja na mradi wa ufugaji kuku katika Kata ya Msoga ili kuona utendaji kazi pamoja na miradi ambayo inafanyika pia kuzichukua changamoto zilizopo na kuangalia jinsi ya kuzitatua.
Mh Mbunge Ridhiwani alitembelea katika Hospital ya Msoga ambayo ilijengwa na Rais Mstaafu Dr. Jakaya Mrisho Kikwete. Kupitia Ofisi ya Mbunge walitoa vifaa tiba katika Hospital hiyo ikiwamo X-RAY machine, Ado sound Mashine, Vitanda 70,Bed cover, Vitanda zaidi ya 70, mashine za dawa za usingizi zaidi ya tano, mafriji ya kuifadhia damu matatu, kiti kwa ajili ya tiba ya meno na vifaa vingine vingi.

Hospital ya Msoga inatarajiwa kuwa ya wilaya baada ya kukamilisha baadhi ya vitu ikiwemo samani, inaupungufu wa mabenchi ya kukalia wagonjwa 150, viti 150, Meza 40, na Mashelfu ya kuifadhia dawa pamoja na AC katika chumba hicho kwa ajili ya kuifadhia dawa, Ukosefu wa kichomea taka hatarishi pamoja na Mochwari Lakini pia kuna changamoto ya umaliziaji wa chumba cha kuifadhia digital x-ray machine ambayo ni kubwa iliyotolewa na Mh Mbunge
Chumba cha Darasa la Kompyuta katika Shule ya Sekondari Lugoba
Mh Mbunge akiwa katika eneo ambalo litajengwa tank kubwa la maji litakalo sambaza maji mji mzima wa chalize kutokea Ruvu.
Uchimbaji na Uwekaji maboba ya maji kutokea Ruvu kuja Chalinze ukiendelea.
Mh Mbunge akiwa anapewa maelekezo baada kutembelea eneo la ujenzi wa Kiwanda cha uchakataji matunda
Nyumba za walimu zikiwa zimemalizika katika Shule ya Secondari Merento


MASAUNI AZINDUA MASHINDANO NAGE MAPINDUZI CUP ZANZIBAR, ACHANGIA VICOBA JIMBONI KWAKE

$
0
0
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na mamia ya wananchi kabla ya kuzindua Mashindano maarufu ya Nage Mapinduzi Cup katika Viwanja vya Matumbaku, Wilaya ya Mjini, Unguja, Zanzibar. Mashindano hayo yanawahusisha wasichana kutoka majimbo mbalimbali ya mjini humo yameandaliwa kwa ajili ya Maadhimisho ya Sherehe ya Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao mwakani.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Chama cha Kuweka na Kukopa (Vicoba-Together) katika sherehe iliyofanyika Skuli ya Chekechea, Miembeni, Zanzibar. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Unguja. Masauni alikichangia chama hicho shilingi milioni tatu.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akimkabidhi Mkurugenzi wa Redio ya Coconut mjini Unguja, Zanzibar, Ally Dai, jezi kwa ajili ya Mashindano maarufu ya Nage Mapinduzi Cup ambayo yamezinduliwa na kiongozi huyo katika Viwanja vya Matumbaku mjini humo. Mashindano hayo yanawahusisha wasichana yameandaliwa kwa ajili ya Maadhimisho ya Sherehe ya Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao mwakani.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto aliyevaa kofia) akiyapokea Maandamano ya timu 38 za Mashindano ya Nage Mapinduzi Cup katika Viwanja vya Matumbaku, Wilaya ya Mjini, Unguja, Zanzibar. Mashindano hayo yanawahusisha wasichana kutoka majimbo mbalimbali ya mjini humo yameandaliwa kwa ajili ya Maadhimisho ya Sherehe ya Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao mwakani.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

JARIDA LA WIZARA YA HABARI TOLEO LA DESEMBA, 2016.

JARIDA LA NCHI YETU, MIAKA 55 YA UHURU WA TANZANIA BARA

VIONGOZI WA DUNIA WAPITISHA AZIMIO LA PARIS KATIKA MKUTANO WA OGP

$
0
0
Na Hassan Silayo-Paris Ufaransa.

Serikali themanini na mamia ya mashirika ya kiraia kutoka duniani kote yamesaini hatua ya pamoja katika Azimio la Paris, ikiwa ni pamoja na mambo kadhaa juu ya kupambana na rushwa.
Hii inakuja mwishoni mwa siku 3 katika mkutano wa nne wa mpango wa kuendesha shuguli za serikali kwa uwazi(OGP) uliofanyika Jijini Paris Nchini Ufaransa ambayo ulishuhudia  uzinduzi wa mageuzi mapya ya uendeshaji wa serikali kwa uwazi kwa wanachama 15 waliokatika mpango wa majaribio  wa OGP ikiwa ni pamoja na Manispaa ya Kigoma kutoka Tanzania.

Azimio la Paris ni pamoja na kumi na tisa vitendo pamoja, ambapo serikali na mashirika ya kiraia kukubaliana kufanya kazi pamoja kufikia matokeo yanayoonekana pato-oriented. Hatua ya pamoja ni pamoja na: Uwazi na mikataba ya wazi katika sekta ya maliasili, Uwazi juu ya ushawishi, kuondoa matumizi mabaya ya makampuni hewa, utekelezaji wa upatikanaji wa sheria ya habari, msisitizo wa Mapinduzi ya takwimu  kwa maendeleo endelevu na mabadiliko ya Hali ya Hewa, utekelezaji wa kanuni za mwongozo kwa ajili ya sera ya takwimu za wazi ;na kuongeza mwitikio wa huduma za umma.

Sanjay Pradhan, Mkurugenzi Mtendaji wa mpango wa kuendesha shuguli za serikali kwa uwazi, kuweka hatua kwa tukio la siku tatu kwa kuwakumbusha washiriki wa mazingira ya sasa kijiografia na kisiasa. "Harakati Open Government haijawahi kuwa chini ya tishio na bado kazi yetu haijawa muhimu sana kwa ajili ya dunia, hivyo tunahitaji wanaharakati wa mashirika ya kiraia, waandishi wa habari, wabunge, sekta binafsi kuongeza nguvu na kuungana il kupata ujasiri wa pamoja wa kupambana na maslahi. "

Akizungumza mwishoni mwa Mkutano huo Mratibu wa mpango wa kuendesha shuguli za serikali kwa uwazi Kigoma Ujiji Mhandisi Sultani Ndoliwa amesema wamejifunza mambo mengi ambayo yatasaidia manispaa kukuza maendeleo kwa raia na kusaidia kukabiliana na changamoto ya na kuzitatua  kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.

Hussein Ruhava Meya wa Kigoma Ujiji Manispaa ameshauri manispaa nyingine nchini Tanzania kuwa na tabia ya kusikilizag juu ya nini wananchi wanataka kwani itasaidia kujua ni nini wananchi wanataka na mwisho wa siku itasaidia kupunguza malamiko juu ya huduma duni za umma katika Sekta mbalimbali.

Anne Hidalgo, Meya wa Paris, akiwakaribisha viongozi kutoka maeneo yaliyo katika mpango wa majaribio wa OGP  alisema, "kukutana kwa serikali za mitaa,miji Jijini Paris ndiko ni tukio la kihistoria kwamba inaonyesha jinsi lazima ushiriki miji ni katika kukabiliana na changamoto za karne yetu." Serikali na asasi za kiraia viongozi kutoka Austin, Marekani; Bojonegoro, Indonesia; Buenos Aires, Argentina; Elgeyo Marakwet, Kenya; Jalisco, Mexico; Kigoma, Tanzania; La Libertad, Peru; Madrid, Hispania; Ontario, Canada; Paris, Ufaransa; Sao Paulo, Brazil,Scotland, Uingereza; Sekondi-Takoradi, Ghana; Seoul, Korea Kusini na Tbilisi, Georgia walihudhuria tukio.

Mameya kutoka mpango wa majaribio wa OGP  katika picha ya pamoja baada kumalizika kwa kikao hicho.

TASWIRA KATIKA MABANDA YA MAONESHO YA VIWANDA VYA NDANI KATIKA VIWANJA VYA SABASABA JIJINI DAR

$
0
0
Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Gaudensia Simwanza (kulia) akitoa maelezo kwa wateja wa waliofika katika banda la TFDA katika maonesho ya viwanda yanayoendelea katika viwanja Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Kaimu Meneja huduma kwa wateja na Elimu kwa Umma Ndugu Jemes Ndege( kulia)akitoa elimu kwa wananchi waliofika katika banda la TFDA katika maonesho ya viwanda yanayoendelea katika viwanja Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mwalimu wa Umeme VETA Kipawa, Athuman Ubaya akitoa maelezo kwa wananchi waliofika katika banda la TFDA katika maonesho ya viwanda yanayoendelea katika viwanja Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Uchumi na Biashara wa Nchini, Ukraine, Nataliya Mykolska akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Masoko na Mauzo wa Azam, Omary Kuwe walipotembelea banda la Azam katika Maonesho ya Viwanda yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Wananchi wakipata huduma katika banda MeTL katika maonesho ya viwanda yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI DESEMBA 10,2016

TAARIFA KUTOKA WIZARA YA AFYA


Waziri Nape azindua mashindano ya kuogelea ya vijana chini ya umri wa miaka 13 jijini Dar es Salaam

$
0
0
 Waziri wa Habari utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa mashindano ya kuogelea ya vijana chini ya umri wa miaka 13 yanayoandaliwa na Dar es Salaam Swimming Club yanayofanyika katika bwawa la shule ya Kimataifa Jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya washiriki wa mashindano ya kuogelea ya Vijana chini ya umri wa miaka 13 wakijaaandaa kuruka ndani ya bwawa la kuogelea kuanza kushindana katika mashindano hayo yaliyoandaliwa na Dar es Salaam Sewimming Club.
 Baadhi ya washiriki wa mashindano ya kuogelea ya Vijana chini ya umri wa miaka 13 wakijaaandaa kuruka ndani ya bwawa la kuogelea kuanza kushindana katika mashindano hayo yaliyoandaliwa na Dar es Salaam Sewimming Club.
 Baadhi ya washiriki wakifuatilia mashindano hayo ya Vijana ya kuogelea yaliyoandaliwa na Dar es Salaam Swimming Club. 
Waziri wa Habari utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiwavalisha medani baadhi ya washindi wa kuogelea mara baada ya kumalizika kwa mashindano hayo yanayoandaliwa na Dar es Salaam Swimming Club yanayofanyika Jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WHUSM.

KUSOGEZWA MBELE KWA TAREHE YA KUREJESHA FOMU ZA WAGOMBEA WA UONGOZI WA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA

$
0
0
Katibu wa Baraza la Vyama vya Siasa anatumia fursa hii kuwatangazia wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa kuwa, tarehe ya kurejesha fomu za wagombe imesogezwa mbele mpaka tarehe 14 Disemba, 2016 saa tisa na nusu (3:30) alasiri, kutokana na siku ya Ijumaa tarehe 09 Disemba, 2016 na Jumatatu tarehe 12 Disemba, 2016 kuwa ni sikukuu.
 Fomu zilizojazwa kikamilifu zinapaswa kurejeshwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Dar es salaam.
  
     Sisty L. Nyahoza
Kny: KATIBU WA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA
 10 Disemba, 2016

Ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano nas Mazingira Mhe Luhaga Mpina Zanzibar

$
0
0
Mratibu wa Kituo cha Tume Sayansi na Teknolojia Zanzibar Bi Afua Mohammed akitowa maelezo kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe, Luhaga Mpina alipofika katika Kituo hicho maruhubi Zanzibar akiwa katika ziara yake kutembelea miradi inayosimamiwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia Zanzibar.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akizunhgumza na waandishi wa habari Zanzibar baada ya kumalizia mazungumzo yake na kupoata taarifa ya Utendaji wa Kituo cha Tume ya Sayansi na Teknolojia Zanzibar katika ofisi zake ziliko maruhubi Zanzibar.
Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo Kizimbani Zanzibar Ndg Khatib Juma akitowa maelezo kwa Naibu Waziri Ofisi Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina wakiwa katika maabara ya kituo hicho kizimbani Zanzibar wakati wa ziara yake. 
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akiangalia mpunga unaofanyiwa utafiti katika Kituyo cha Utafiti wa Kilimo Kizimbani Zanzibar, akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kituo hicho Ndg Juma Khatib katikati. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


MASAUNI AFANYA ZIARA NIDA ZANZIBAR, ATEMBELEA WAGONJWA NA KUFANYA USAFI HOSPITALI YA MNAZI MMOJA

$
0
0
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimkabidhi Kitambulisho cha Taifa cha Wageni, Leonie Schollmeyer (kulia), wakati kiongozi huyo alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Zanzibar leo. Masauni licha ya kupewa elimu kuhusiana na utendaji wa kazi wa ofisi hiyo, pia alizungumza na watumishi wa Mamlaka hiyo na kuwataka kufanya kazi kwa weledi kwa kuwahudumia wananchi ili kuiletea mamlaka hiyo mafanikio zaidi.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akifanya usafi na wanachama wa Baraza la Vijana Shehia ya Miembeni katika Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar. Masauni alialikwa na Baraza hilo kushiriki kufanya usafi nao na baadaye aliwatembelea wagonjwa wa hospitali hiyo akiwa na Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mgeni Hassan Juma (hayupo pichani) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Marina Joel Thomas (hayupo pichani).  

 Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mgeni Hassan Juma (kushoto), Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa kofia) wakimsikiliza Nesi Msaidizi Mkuu wa Wodi ya Upasuaji wa Uti wa Mgongo na Kichwa katika Hopsitali ya Mnazi Mmoja, Hadia Mmadi, wakati alipokuwa anawafafanulia kuhusu wagonjwa wanavyopasuliwa. Viongozi hao walifanya ziara katika eneo hilo, mara baada ya kufanya usafi mazingira mbalimbali ya hospitalini hapo.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (watatu kushoto mstari wa mbele), Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Zanzibar, Hassan Haji Hassan (watatu kulia)  wakiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Mamlaka hiyo, mara baada ya Masauni kumaliza ziara yake ya kikazi kuitembelea Mamlaka hiyo.


SHIRIKISHO LA VYUO VYA ELIMU YA JUU-CCM WAMUUNGA MKONO RAIS DK. MAGUFULI KWA KUAHIDI KUENDELEA KUWATUMBUA HADHARANI MAFISADI

$
0
0
theNkoromo Blog, Dar.

SHIRIKISHO la Vyuo vya Elimu ya Juu-CCM, limemuunga mkono Rais Dk. John Magufuli, kwa kuamua maadhimisho yajayo ya Uhuru kufanyika Dodoma, likisema uamuzi huo umedhihirisha dahamira yake ya dhati ya kuhakikisha Dodoma inakuwa Makao Makuu ya nchi kwa vitendo.

Limemuunga, Rais Magufuli kwa kuweka wazi katika hotuba yake kwamba Serikali ya awamu ya tano itaendelea kuchukua hatua kali ikiwa ni pamoja na kuwatumbua hadharani wale waliozoea kutumbua hadharani mali za Watanzania na pia kuendelea kuchukua hatua kali katika masuala ya rushwa na ufisadi, kwa sababu rushwa ni saratani.


Shirikisho hilo, pia limemuunga Rais kwa tamko lake la hivi karibuni la kuamuru machinga, wachimbaji wadogo na wafugaji  kutofukuzwa hovyo hadi mamlaka zinazohusika zitakapotenga maeneo maalumu, likisema pongezi hizo ni kwa sababu Rais amedhihirisha kuwa anajali zaidi masikini na wanyonge.


Salam hizo zimesemwa leo, Desemba 10, 2016, na Katibu Msaidizi wa CCM, Daniel Zenda alipozungumza na Waandishi wa habari Ofisini kwake, Makao Makuu ya Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu-CCM, jijini Dar es Salaam, akitoa taarifa ya Shirikisho hilo kuingiza wanachama wapya 100 toka Chuo Kikuu cha Tiba na Afya Muhimbili.


"Kwa kweli tunayo mengi ya kumuunga mkono na kumpongeza Rais, hata hili la kununua ndege sita. Ndege hizi licha ya kusaidia kurahisisha usafiri wa anga pia zitasaidia sana kukuza utalii ambao  utachangia kuongeza mapato ya nchi, na ni matarajio yetu mapato yakiongezeka uchumi utakua na hata bei za bidhaa zitapungua na hivyo Watanzania walio wengi  kupata nafuu ya maisha".


"Pia sisi kama Watanzania lazima tumuunge mkono na kumpongeza Rais kwa kuendelea kuonyesha dhamira ya serikali ya awamu ya tano kutoa elimu bure kwa kitendo chake cha kutenga kila mwezi sh. bilioni 18.777 kwa ajili ya kutoa elimu bure kwa shule za msingi na sekondari na kwa Vyuo Vikuu sh. Bilioni 483 kutoka sh. bilioni 340 za mwaka jana, hali ambayo imewezesha ongezeko la wanafunzi kutoka 98,000 hadi kufikia 125,000 waliojiunga na vyuo vikuu mwaka huu", alisema Zenda.


Akizungumzia wanachama hao wapya ambao ni madaktari waatarajiwa, katika hafla iliyofanyika Upanga , Dar es Salaam, Zenda alisema, wakati akiwapokea, aliwaambia wamefanya vizuri kujiunga na CCM kwa kuwa wamejiunga na chama makini chenye serikali sikivu inayowajali wanyonge chini ya Rais Dk. John Magufuli.


Shirikisho linawa taka wanafunzi hao na Watanzania kwa kujumla kubeza propaganda zinazosemwa na baadhi ya wanasiasa, kwamba kwa nini  ndege zinanunuliwa wakati hakuna dawa katika hospitali.


 "Propaganda hii ni upotoshaji mkubwa wenye lengo la kutaka kuwafanya Watanzania hawana akili, maana kila mmoja anajua kwamba katika kipindi hiki kifupi alichoingia madarakani Rais Dk. Magufuli ameboresha sekta ya afya katika maeneo mengi ikiwemo upatikanaji wa dawa katika hospitali, zahanati na vutuo vya afya", Alisema Zenda.


Alisema, miongoni mwa maboresho aliyofanya Rais kwenye sekta ya afya ni pamoja na kuongeza bajeti ya sekta hiyo ya afya kwa ajili ya manunuzi ya dawa kutoka Sh. bilioni 31 hadi kufikia sh. bilioni 250 mwaka huu.

Katibu Msaidizi wa CCM, Daniel Zenda akizungumza wakati akiwapokea wanachama wapya 100 wa CCM kutoka Chuo Kikuu cha Muhimbili, katika hafla iliyofanyika jana, Upanga jinini Dar es Salaam.

RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN AONGOZA MAADHIMISHO SIKU YA MAADILI NA HAKI ZA BINADAMU DUNIANI

$
0
0

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na  Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi Zanzibar Nd,Asaa Ahmada Rashid (kulia) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe,Haroun Ali Suleiman mara alipowasili katika Viwanja vya Victoria Garden Mjini Ungujakatika sherehe za Maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu Duniani zilizofanyika leo
 Vijana waliobeba bango linalotoa ujumbe usemao Siku ya Maadili na Haki za Binadamu”Imarisha  Utawala Bora kwa Kukuza Uadilifu,Uwajibikaji,Haki za Binadamu na Mapambano Zidi ya Rushwa”wakati wa  matembezi ya maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu Duniani zilizofanyika leo katika Viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono vijana walioshiki matembezi katika  wa sherehe za maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu Duniani zilizofanyika leo katika Viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Haroun Ali Suleiman alipokuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) kuzungumza na Viongozi na Wananchi katika sherehe za Maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu Duniani zilizofanyika leo katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Viongozi na Wananchi katika sherehe za Maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu Duniani zilizofanyika leo katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja,(kulia) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Haroun Ali Suleiman na (kushoto) Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi Zanzibar Ndg. Asaa Ahmada Rashid.

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA VIONGOZI MBALIMBALI

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Christopher Olonyokie Ole -Sendeka kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhandisi Mathew Mtigumwe kuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Kilimo Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Maria Sasabo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Aloyce Kashindye Nzuki kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha  Balozi Grace Alfred Martin kuwa Mkuu wa Itifaki kutoka Wizara ya mambo ya Nje Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi pamoja na viongozi walioapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam. Wakwanza kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce Kashindye Nzuki, Katibu Mkuu Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe, Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olonyokie Ole Sendeka, Wakwanza kutoka kulia ni Mkuu wa Itifaki Balozi Grace Alfred Martin pamoja na Katibu Mkuu wa Mawasiliano Dkt. Maria Sasabo. Picha na IKULU
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Hoja ya haja - Uraia na Diaspora, TDC Global

BREAKING NEWZZZZZ: RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA ALHAJ ALIKO DANGOTE IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO, WAKATA MZIZI WA FITNA WA WAPIGA DILI

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika kikao cha pamoja na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote mara baada ya kumaliza kwa kikao chao Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kumaliza kikao chake na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote Ikulu jijini Dar es Salaam.

Mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na Video na IKULU. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Desemba 2016, amekutana na kufanya mazungumzo na Mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo  Mtwara, Alhaji Aliko Dangote.

Katika mazungumzo hayo, Rais Magufuli amemhakikishia mfanyabiashara huyo kuwa serikali ya Tanzania itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji wote nchini katika kutimiza lengo lake la kuwa na Tanzania ya Viwanda.

Rais Magufuli amesema kuhusu kiwanda cha kuzalisha Saruji cha Dangote kilichopo Mkoani Mtwara hapakuwa na tatizo lolote ila kulikuwa na watu  ambao  walitaka kujinufaisha binafsi kupitia mradi huo kwa kufanya biashara za ujanja kitu ambacho serikali yake haikiruhusu.

Amemtaka Dangote kununua gesi moja kwa moja kutoka TPDC ambacho ni chombo cha serikali badala ya kutumia watu ambao wamekuwa na nia ya kutengeneza faida tu.

''Iwapo unataka maelezo yoyote ama lolote linalokukwamisha uwasiliane na viongozi wa serikali badala ya kuwasiliana na watu ambao wako kwa ajili ya kufanya biashara ya ujanja ujanja kwa lengo la kupiga dili ''amesema Rais Magufuli.

Dokta Magufuli amesema Dangote ametaka eneo dogo ambalo angelitumia  kusafirishia saruji yake wakajitokeza watu ambao wametaka kumuuzia kwa shilingi bilioni 43  kitu ambacho hakina uhalisia wowote bali ni watu ambao wanataka kutengeneza faida kitu ambacho hakiwezekani.

Kwa upande wake mmiliki wa Kiwanda cha kuzalisha Saruji cha Dangote, Alhaji Aliko Dangote ameshangazwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa amefunga kiwanda kwa sababu amekatazwa kuagiza makaa ya mawe toka nje ya Tanzania kitu ambacho amesema hakiingii akilini kwa sababu makaa ya mawe ya Tanzania ni rahisi na yana ubora  kuliko kuagiza nje. 
Katika kuthibitisha hilo,  tayari Mfanyabiashara huyo ameingiza malori mapya 600 kwa ajili ya kusambazia saruji yake. Ameongeza kuwa lengo la kufanya biashara hapa nchini mbali na kutengeneza faida pia ana lengo la kuisaidia serikali ya Tanzania kutengeneza ajira hivyo hana sababu ya kuagiza mali ghafi toka nje ya nchi  ambazo zinapatikana nchini.

Alhaji Dangote amemuhakikishia Rais magufuli kuwa ataendelea kufanya kazi na Serikali ya  Tanzania  na kamwe hana  nia yoyote ya kufunga kiwanda chake kama inavyodaiwa na baadhi ya vyombo vya habari bali ana mpango wa kuangalia fursa nyingine zaidi za uwekezaji hapa nchini kutokana na uwepo wa sera nzuri za uwekezaji chini ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Katika hatua nyingineRais Dkt. John Pombe Magufuli amuapisha Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Olonyokie Ole-Sendeka anayechukua nafasi ya Dkt. Rehema Nchimbi ambaye amehamishwa kituo cha kazi na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida.

Wengine walioapishwa na Rais Magufuli ni Mhandisi Mathew Mtigumwe ambaye anakuwa  Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo (Kilimo), Dkt. Maria Sasabo Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Dkt. Aloyce K. Nzuki kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Bibi Grace Alfred Martin kuwa Balozi (Mkuu wa Itifaki).


Jaffar Haniu,

Naibu Mkurugenzi wa Mawasilino ya Rais, IKULU.

Dar es Salaam.


10 Desemba, 2016.

RC GAMBO AKABIDHI PIKIPIKI 200 KWA VIJANA JIJINI ARUSHA, WAMSHUKURU KWA HILO

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (kushoto) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Fabian Daqarro akimkabidhi pikipiki mmoja wa waendesha bodaboda wa jiji hilo katika kutekeleza mradi huo wa kutoa pikipiki 200 kwa viaja  uliozinduliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.
 Zoezi Hilo lililofanyika kwenye Viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha na kushuhudiwa Na Kamati ya Ulinzi Na Usalama ya Mkoa pamoja na viongozi wengine limeenda sambamba na ukamilishaji wa taratibu zingine Kama vile kila mmoja wao kupatiwa Bima Kubwa na Leseni ya muda (Lena).  Vijana wa Arusha wamempongeza Mkuu wa Mkoa Gambo Kwa kubuni Mradi huu Na kuahidi kuwa waaminifu katika marejesho ili vijana wengine waweze kunufaika. .
 Kijana akiondoka na pikipiki yake baada ya kukabidhiwa
Vijana wakiwa na pikipiki zao baada ya kukabidhiwa
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akiwa na waendesha bodaboda vijana 200 baada ya kuwakabidhi vitendea kazi hivyo
Shukurani toka kwa kiongozi wa waendesha bodaboda jiji la Arusha

Bunge Stars yashika nafasi bora katika michuano ya mabunge ya Afrika Mashariki mjini Mombasa, Kenya

$
0
0
Mabao mawili ya Kila kipindi yameiwzesha timu ya Bunge Stars  kumaliza nafasi bora baada ya kuifunga Bunge la Jumuiya ya Africa Mashariki mabao 4-2. Mabao hayo vyalifungwa na Cosato Chumi goli moja na Yusuf Gogo mabao matatu Kwa upande wa Netball Bunge Queen imemaliza nafasi ya pili baada ya kufungwa na Uganda katika  fainali magoli 38-29. Mpaka tunaenda mitamboni Burundi walikuwa uwanjani wakimenyana na Uganda ktk fainali
 Kocha mchezaji wa timu ya Bunge Stars   Venance Mwamoto na mshambuliaji hatari wa kikosi hicho Cosato Chumi wakiwa na waamuzi wa mchezo wao na timu ya Bunge la Jumuiya ya Africa Mashariki ambao wamewalamba mabao 4-2
 Wachezaji wa Bunge Stars wakijiandaa na mchezo waona timu ya Bunge la Jumuiya ya Africa Mashariki 
Wachezaji nyota wa Bunge Stars wakiwa wamekaa na mashabiki wao

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA MGENI RASMI SHEREHE ZA MAULID KITAIFA SINGIDA

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Siku ya Maulid ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) ambayo kitaifa itaadhimishwa mkoani Singida.

 Katibu wa Bakwata Mkoa wa Singida, Alhaji Buruhani Mlau alisema sherehe za Kitaifa za Maulid ya Mtume Mohammad (SAW) kwa mwaka huu zinatarajiwa kufanyika Mkoani Singida katika Kijiji cha Shelui, wilayani Iramba, Singida. 
 Wiki iliyopita, akitangaza utaratibu wa sherehe hizo, Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir alisema kwa mwaka huu, Maulid itasomwa usiku wa Desemba 11 na mapumziko yatakuwa siku inayofuata yaani Desemba 12. 
 Mufti wa Tanzania aliwataka Waislamu wote nchini waadhimishe Siku ya Maulid kwa kufanya usafi, kupanda miti na kuchangia damu. “Waislamu wanatakiwa kutumia siku hiyo kwa kufanya matendo mema na yenye kumpendeza Mwenyezi Mungu ikiwa ni pamoja na kufanya usafi kwenye mitaa yao na kuchangia damu ili kusaidia wenye uhitaji huo,” alisema.
Viewing all 109973 articles
Browse latest View live




Latest Images