Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1455 | 1456 | (Page 1457) | 1458 | 1459 | .... | 3283 | newer

  0 0

   Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani (katikati) akizungumza na wananchi wa Kata ya Ulaya wilayani Kilosa, Mkoa wa Morogoro, kuhusu utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini (REA II na REA III), wakati wa ziara yake wilayani humo hivi karibuni.
   Diwani wa Kata ya Ulaya wilayani Kilosa, Matokeo Kenedi (kushoto), akimweleza Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani (kulia) mahitaji ya umeme kwa wananchi wa Kata yake, wakati wa ziara ya Naibu Waziri kukagua miradi ya umeme wilayani humo hivi karibuni. Kulia kwa Naibu Waziri ni Meneja wa Tanesco Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Hassan Saidy.
   Nehemia Magendege kutoka Kijiji cha Ng’uruhe, Kata ya Pomerini wilayani Kilolo, akitoa maoni yake kuhusu utekelezwaji wa Miradi ya Umeme Vijijini (REA II na REA III) kwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani (hayupo pichani), wakati wa ziara yake wilayani humo hivi karibuni.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

   Picha hizi zimepigwa maeneo ya katikati ya jiji la Dar es salaam, Je waweza tambua mpigaji alikuwa wapi??

  0 0
 • 12/08/16--08:11: KIJIWE KIMENUNA LEO
 • Vijana wanojishughulisha na kazi ya ubebaji mizigo ya abiria wanaosafiri kwenda mikoani katika Stendi kuu ya Mabasi ya Mikoani na nchi za jirani, Ubungo jijini Dar es salaam wakisubiri abiria wa kuwabebea mizigo, ambapo kwa mujibu wa mmoja wao alisema leo mambo si shwari sana kama ilivyo kwa siku nyingine.

  0 0  0 0
 • 12/08/16--08:17: KRISMAS YAANZA KUNUKIA
 • Mfanyabiashara ndogondgo (mmachinga) akiwa amebeba mti wa Krismas kwa ajili ya kuuza ikiwa ni muda muafaka kabisa wa maandalizi ya msimu wa sikukuu za Krismas na Mwaka Mpya.

  0 0


  0 0

  Picha hii imepigwa leo maeneo ya Mabibo jijini Dar es salaam.
  Picha hii ilipigwa siku za nyuma kidogo huko katika Mji wa Boma, Mkoani Kilimanjaro.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mke wa Mwanzilishi wa Taifa la Sudani Kusini Rebecca Nyandeng De Mabior aliyefika Ikulu pamoja na ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mke wa Mwanzilishi wa Taifa la Sudani Kusini Rebecca Nyandeng Mabior Ikulu jijini Dar es Salaam. 
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mke wa Mwanzilishi wa Taifa la Sudani Kusini Rebecca Nyandeng De Mabior mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mabior Garang Mtoto wa Mwanzilishi wa Taifa la Sudani Kusini Hayati John Garang De Mabior Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU


  0 0

  Tunapokea hadithi fupi yenye maneno yasiyopungua #1000 wala kuzidi #3000. Dhamira ni #Utandawazi.
  Vigezo: Tumia lugha nyepesi, fasaha, yenye visa, wahusika na vionjo vya kisanii kuandika hadithi fupi. Zingatia jinsia na kuonesha badala ya kuhubiri. Si lazima utumie neno‘UTANDAWAZI’ katika hadithi yako.Mwisho wa kupokea hadithi ni tarehe 28 February 2017. Zawadi nono zitatolewa kwa washindi ikiwa ni pamoja na kuhudhuria warsha ya mafunzo ya uandishi.
   ANDIKA NA SOMA ni shindano la fasihi linalohusisha wanafunzi wa shule za sekondari nchini Tanzania.

  Shindano linadhamiria kuwapatia fursa vijana kushiriki mijadala ya kijamii kwa kutumia fasihi. Vivyohivyo, kupitia shindano hili tunawajengea ari na stadi zitakazowawezesha kuwa wasomaji mahiri na wachambuzi wa mambo anuwai katika jamii; pamoja na kuimarisha uwezo wao wa kuwasilisha fikra zao kwa ufasaha na wabunifu.


  0 0


  0 0

  The tourist Silver Cloud  cruise ship from the USA with more than 100 tourists has arrived and docked in Dar es salaam Port early morning today.Upon their arrival the tourists were met officials from Tanzania Tourist Board who among other things supplied them with tourism information materials including brochures, Dvds Cds, and tourist maps as well as briefed them about destination Tanzania.

  While in Dar es salaam , the tourists were expected to have a day tour of the  tour to explore Dar es Salaam's tourist attractions such as National Museum and House of Culture, Sandy Beaches, world famous Kivukoni fish market and Mwenge curio shops. For more CLICK HERE


  Marketing Officer of Tanzania Tourist Board, Mr. Hoza Mbura (right) shows a Dar-es-salaam city tourist map to the visiting tourists.

  Scanning for information on the Tanzania tourist’s travel map   Scanning for information on the Tanzania tourist’s travel map
   Scanning for information on the Tanzania tourist’s travel map
  Some of the visiting  tourists waiting for the shuttle bus to take them to town


  0 0


  0 0
 • 12/08/16--20:56: KUMBUKUMBU


 • 0 0

  Tanzania inakuwa nchi ya 50 barani  Afrika kufikiwa na Shirika la Ndege la Uturuki baada ya kuongezwa safari tatu kwa wiki kwenda Zanzibar

  Shirika la Ndege la Uturuki limeiongeza Zanzibar katika mtandao wa safari zake kuanzia Desemba 13, 2016. Hivi sasa shirika hilo linafanya safari 49 barani Afrika baada ya hivi karibuni kuongeza safari ya kwenda Visiwa vya Shelisheli.

  Shirika hilo maarufu barani Ulaya kwa sasa linafanya jumla ya safari 293 duniani kote, zikiwemo safari 50 kwenye nchi 31 za Afrika.

  Likiwa ni shirika la nne kwa kuwa na mtandao mkubwa wa safari duniani kote kuliko mashirika mengine, Shirika la Ndege la Uturuki sasa litahudumia miji ya kimataifa 244 ikijumlishwa na Visiwa vya Zanzibar ambavyo ni maarufu kwa biashara ya viungo. Watumiaji wa ndege za shirika hilo sasa watafurahia uzoefu watakaoupata kutokana na safari hizo mpya zinazojumuisha miji 20 maarufu duniani kama vile Frankfurt, Muscat, Munchen, Dubai, Paris, London, Milano, Amsterdam, Zurich, Bombay, Copenhagen, Stockholm, Rome, Brussels, Berlin, Vienna, Hamburg, Tel-Aviv, Düsseldorf, na Prague.

  Safari ya kwanza itazinduliwa Jumanne, Desemba 13, 2016 na wasafiri wataondoka Istanbul saa 6:30 usiku na ndege TK567 itakayowasili saa 3:30 asubuhi. Watarudi na ndege hiyo TK567 itakayoondoka Zanzibar saa 4:25 asubuhi na kuwasili Istanbul saa 11:45 jioni.
  Safari za Instanbul – Kilimanjaro – Zanzibar – Istanbul (IST-JRO-ZNZ-IST) zitakuwa tatu kwa wiki. Utaratibu wa kuweka mpango wa safari unapatikana kupitia tovuti www.turkishairlines.com kama ifuatavyo::

  0 0

  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

  Taasisi ya Global Education Link imeisaidia Serikali kuzalisha rasilimali watu wenye ujuzi na elimu ya kutosha ili watumike katika kuinua viwanda na uchumi wa nchi.
  Hayo yamesemwa  jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Abdulmaliki Mollel alipokuwa akiongea na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa maonesho ya kwanza ya viwanda Tanzania yaliyofanyika katika viwanja vya Sabasaba vilivyopo jijini humo.

  Mollel amesema kuwa Tanzania imeamua kuwa nchi ya viwanda lakini bila kuwa na rasilimali watu wenye ujuzi na elimu ya kutosha kuhusu uzalishaji na uendelezaji wa viwanda hakutakuwa na maendeleo kwani maendeleo yoyote mzizi wake ni elimu na ujuzi.
  “Kuna  baadhi ya masomo ambayo ni muhimu hayapatikani katika vyuo vya Tanzania na kama zinapatikana basi nafasi ni chache hivyo,taasisi hii ni kama daraja la kutengeneza rasilimali watu wenye ubora watakaoleta maendeleo ya nchi kupitia kusoma nchi za nje,”alisema Mollel.

  0 0  0 0

  Wananchi Wilayani Handeni wametakiwa kufuata maadili katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ili kujihahakikishia huduma bora za jamii.

   

   
  Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe alipokuwa akisikiliza kero za wananchi wa Kata ya Segera iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Handeni jana katika maadhimisho ya  siku ya Maadili na Haki za Binanadamu Kiwilaya yaliyoandaliwa na taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU).


  Gondwe alisema “ Maadli ni imani njema, sehemu yoyote yenye maadili haki za binadamu hufuatwa, hakuna ardhi itakayouzwa kiholela, wagonjwa watatibiwa vizuri kwenye vituo vya afya, wageni wataingia kwenye maeneo yetu kwa kufuata taratibu za nchi na shughuli zote zitafanyika kwa misingi ya Haki”.


  Aidha aliwataka watumishi wa umma na wananci kwa ujumla kufuata sheria, taratibu na kanuni pasipo kujali wala kubagua rangi au cheo cha mtu yeyote. Alisema kuwa Rushwa ni adui wa haki  na kuwataka kuikataa kwa kauli na vitendo.


  Wakati huohuo Mkuu wa Wilaya ya Handeni alivunja baraza la Ardhi la Kata kwa kulalamikiwa na wananchi kutotekeleza maajukumu yeke na kuwaagiza TAKUKURU Wilaya ya Handeni kulichunguza hadi ifikapo mwishoni mwa mwezi Januari 2017, na mapungufu yoyote yatakayobainika basi hatua za kisheria  zichukue mkondo wake maramoja.


  Vilevile aliwaaagiza  Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji kusimamisha shughuli zote za kilimo zinazofanywa kwenye msitu wa hifadhi ya kijiji


  Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe aliwataka Maafisa Watendaji na wenyeviti wa Vijiji kusimamia miradi yote ya maendeleo kwa  maadili na uadilifu kutokana na dhamana kubwa waliyonayo kwenye maeneo yao ya kiutawala. Vilevile aliwataka  kusoma tarifa za mapato na matumizi na kuwa tayari kujibu hoja za wananchi kuhusu taarifa za mapato na matumizi. “Mtendaji atakayeshindwa kusoma taarifa za mapato na matumizi atakua amejiondoa mwenyewe kwenye nafasi yake” Alisema Makufwe.


  Mkuu wa TAKUKURU Wilaya Bi. Esta Mulima, alisema TAKUKURU itaendelea kupambana na Rushwa kikamilifu na kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu madhara ya Rushwa. Aliwataka wananchi kufichua vitendo vya rushwa vinapotokea au dalili za vitendo hivyo ili hatua ziweze kuchukuliwa.


  Maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu hufanyika kila tarehe 10 Disemba Kitaifa, na Wilayani hapa yalifanyika tarehe 8 Disemba  kutokana na Muingiliano wa Majukumu yakiongozwa na kauli mbiu isemayo.


  kujenga na kukuza maadili, haki za binadamu, uwajibikaji, utawala bora na Mapambano dhidi ya Rushwa”.


  Alda  Sadango

  Afisa habari

  Halmashauri ya Wilaya ya Handeni


  9 Desemba 2016.
   Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Godwin Gondwe  na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe, wakisalimia wananchi wa Kata ya Segera
   Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni  BW. William Makufwe akizungumza na wananchi wa Kata ya Segera kwenye maadhimisho hayo.
  Mkuu wa TAKUKURU Wilaya Bi. Esta Mulima akizungumza na wananchi wa Kata ya Segera kwenye maadhimisho.
   Baadhi ya Maafisa wa TAKUKURU, Wilaya wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya. 

  Baadhi ya wananchi wa kata ya Segera . 


  0 0

  Rais Mstaafu na Kamishna wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Kugharamia Fursa ya  Elimu  Duniani  (UN Education Commission on Financing Global Education Opportunity) Desemba 8, 2016, alikutana na Rais wa Msumbiji,  Mheshimiwa Filipe Nyusi alipomtembelea jijini Maputo, Msumbiji.

  Katika nafasi yake ya Mjumbe Maalum wa Kamisheni hiyo, Rais Mstaafu amemkabidhi  Rais Filipe Nyusi Ripoti ya Kamisheni hiyo yenye mapendekezo ya namna Dunia inavyoweza kukabili janga la Elimu kwa kuwekeza katika Mpango wa Kizazi cha Elimu (A Learning Generation). Mpango huo unalenga kuleta mapinduzi makubwa ya Elimu katika nchi zinazoendelea ndani ya Kizazi Kimoja  (miaka 30). Azma kuu ya Mpongo huo ni kuwezesha ifikapo mwaka 2040, watoto wote kote duniani wawe wanapata elimu iliyo sawa, na kwa kiwango cha ubora unaolingana dunia nzima.
  Rais Mstaafu Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Mhe. Rais Filipe Nyusi ripoti ya Kamisheni ya UN ya Elimu jijini Maputo, Msumbiji.

  Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kwa sasa, hali ya elimu katika nchi zinazoendelea inalingana na ile ambayo nchi zinazoendelea zilikuwapo miaka 70 iliyopita. Aidha, ripoti inasisitiza kuwa, ikiwa nchi zinazoendelea zitaendelea kwa kasi ya sasa, itazichukua nchi hizo kati ya miaka 90 na 110 kufikia viwango vya sasa vya nchi zilizoendelea. 

  Aidha, ripoti inatahadharisha kuwa takribani ajira bilioni 2 zitakufa ifikapo mwaka 2050 kutokana na maendeleo ya teknolojia, ambapo asilimia 70 ya kazi hizo ziko katika nchi zinazoendelea. Hivyo, nchi zinazoendelea zinapaswa kuangalia upya aina ya elimu na stadi zinazotolewa ili kuendana na wakati ujao.
  Rais Mstaafu Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimpitisha Mhe. Rais Filipe Nyusi katika ripoti ya Kamisheni ya Elimu kuhusu Mapendekezo Mahsusi kwa nchi ya Msumbiji.

  Kwa ajili hiyo, Kamisheni inapendekeza njia mpya na bora za kufanya mageuzi katika elimu ikiwemo kuongeza usimamizi, kupanua fursa, kuingiza ubinifu na teknolojia na kuongeza uwekezaji katika elimu kwa kushawishi ushiriki wa Jumuiya ya Kimataifa na Sekta Binafsi. Iwapo mapendekezo hayo yatatekelezwa, nchi zinazoendelea zinaweza kufidia pengo hilo ndani ya miaka 30 ijayo. Rais Mstaafu ameiomba Msumbiji kujiunga na Mpango huo.

  Kwa upande wake, Rais Nyusi amepokea kwa furaha taarifa hiyo na kuelezea nia na dhamira ya nchi yake ya kujiunga na Mpango wa Kizazi cha Elimu. Kufuatia mazungumzo yao, mapema baadae  Rais Mstaafu alikutana na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Adriano Maleane, Naibu Waziri wa Elimu ya Juu, Sayansi na Elimu ya Fundi Mhe. Leda Hugo na Naibu Waziri wa Elimu Mhe. Armingo Ngunga kujadili mapendekezo mahsusi ya Kamisheni kwa nchi ya Msumbiji.
  Rais Mstaafu na Mjumbe wa Kamisheni ya Elimu Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Mhe. Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji, jijini Maputo.

  Ziara ya Rais Mstaafu itamfikisha katika nchi 14 barani Afrika ambapo zimechaguliwa katika awamu ya kwanza ya mpango huo. Tayari amekwishazitembelea nchi za Uganda, Malawi, Ethiopia na Msumbiji.na kufanya mazungumzo na viongozi wakuu wa nchi hizo.


  0 0

   Ofisa Mauzo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Fredrick Sawaki (kulia), akitoa maelezo kuhusu mafao yatolewayo na NSSF kwa wananchi waliotembelea banda la shirika hilo wakati wa  maonessho ya Viwanda vya Tanzania yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande).

   Ofisa Matekelezo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Sarah Mazengo (kushoto), akitoa maelezo kuhusu mafao yatolewayo na NSSF kwa wananchi waliotembelea banda la shirika hilo wakati wa  maonessho ya Viwanda vya Tanzania yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

  Wananchi wakiwa katika banda la NSSF.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

older | 1 | .... | 1455 | 1456 | (Page 1457) | 1458 | 1459 | .... | 3283 | newer