Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1456 | 1457 | (Page 1458) | 1459 | 1460 | .... | 3270 | newer

  0 0


   Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Bw. Ian Ferrao (kushoto) akimkabidhi ngao na cheti, Bi. Eunice Kahamba ambaye aliibuka mshindi katika tuzo ya Mauzo ya SYTYCS iliyoandaliwa na kitengo cha biashara (EBU ) cha kampuni hiyo, kwenye hafla ya kukabidhi zawadi jijini Dar es Salaam leo Desemba 9, 2016
  Baadhi ya wafanyakazi wa kitengo cha biashara (EBU) cha Vodacom Tanzania, wakishangilia huku wakimpongeza mshindi wa tuzo hiyo, Eunice Kahamba ambaye aliibuka mshindi katika tuzo ya Mauzo ya SYTYCS iliyoandaliwa na kitengo hicho, kwenye hafla ya kukabidhi zawadi jijini Dar es Salaam leo Desemba 9, 2016

  0 0

  Vodacom Tanzania Managing Director, Mr. Ian Ferrao (L) presents a trophy and Certificate to Ms. Eunice Kahamba who won an award on” So You Think You Can Sell”(SYTYCS), that was  coordinated by the Entrepreneur Business Unit (EBU) of the company, at the prize giving ceremony in Dar es Salaam today December 9, 2016.

  0 0

  Parliament of Tanzania’s Netball team commenced their search for the trophy with an emphatic 55-1 points over Parliament of Kenya in a one-sided encounter at the Makande Sports gymnasium.

  Parliament of Tanzania legislators ran over the Kenyan legislators in the entire game.  Kenya’s lone point was scored by West Pokot legislator, Hon Regina Ng’eris.  Parliament of Tanzania’s Hon Grace Khiwelo stood out tall, notching in 46 points for the team. Hon AminaMabrouk scored 7 points and Hon Esther Matiko 2 points.  Tomorrow, Parliament of Tanzania will face off with Parliament of Uganda in a match billed to be a tough one.

  In football, Parliament of Kenya beat Parliament of Tanzania Parliament 1-0 in an entertaining match. Stephen Njata scored towards the end of full-time to give his side the slim victory. But it was a case of several missed chances with the victors failing to net two penalties that came their way to extend their lead. With that, Parliament of Kenya’s football team also bid goodbye to the tournament in the group A, billed as the Group of death.  All teams finished with three points apiece with the rules on goals applying to break a tie.

  In Group B, EALA were awarded their match 2-0 versus Rwanda in Group B. The semi-finals clash today is thus expected to feature Tanzania and Burundi before EALA takes on Uganda in the next encounter.

  In the men’s volleyball match, Parliament of Kenya beat Parliament of Tanzania by 2 sets to 0. The sets were 25-16 and 25-23 in favour of the victors.

  In the second match of the day, defending champions, Parliament of Rwanda whipped EALA 2 sets to 0 of 25-23 and 25-10.    In women’s volleyball, Tanzania upset Uganda 2 sets to 1 scooping 25-19, 21-25 and 15-10.

  In golf, the golf tournament teed off by the Speaker of EALA, Rt Hon Daniel F. Kidega at the Nyali Golf Club. Parliament of Kenya scooped gold with 55 points while Parliament of Uganda was second netting the silver medal. EALA finished on bronze, but produced the overall best Man golfer in Hon Peter Mathuki.
  Kenya vs Tanzania in the volleyball match
  Action during the match between Parliament of Kenya and Parliament of Tanzania. Parliame​nt of Kenya were eliminated despite the 1-0 win over their opponents, Parliament of Tanzania

  0 0  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Mjaliwa amesema Serikali imetenga sh. bilioni 15 kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa vijana zaidi 2,500 ili kuwajengea uwezo waweze kushiriki kama nguvu kazi kwenye viwanda vinavyotarajiwa kujengwa nchini.

  Alitoa kauli hiyo jana usiku (Alhamis, Desemba 8, 2016) kwenye sherehe za utoaji wa tuzo ya muajiri bora wa mwaka 2016, zilizofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam. Tuzo hizo zimeandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE).

  Waziri Mkuu alisema Serikali imeanza kujielekeza katika kutoa mafunzo kwenye sekta za kipaumbele kwa kuzingatia Mpango wa Taifa wa Maendeleo kama kilimo biashara, mafuta, gesi, utalii, usafirishaji, ushonaji na bidhaa za ngozi.

  Alisema jitihada zinaendelea kwenye maeneo mengine ili waajiri wawe na wigo mpana wa kuwapata wafanyakazi wenye stadi stahiki kwa kuwa Serikali inatambua umuhimu wa wao kuwa nguvu kazi yenye ujuzi na umahiri mkubwa kwa lengo la kuongeza tija.

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alizungumzia changamoto inayolalamikiwa na waajiri ya uwepo wa tozo mbalimbali zinazotolewa na Mamlaka tofauti za Serikali kwa huduma ileile kuwa wanaitambua na tayari mchakato wa kuainisha sheria zote zinazoonekana kukwamisha uwekezaji pamoja na mazingira ya biashara nchini.

  SOMA ZAIDI HAPA

  0 0

  Baada ya kupitia mawasilisho ya pande zote kwa njia ya mahojiano, na vielelezo Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji imebaini mambo yafuatayo ambayo yanapaswa kuchukuliwa hatua za haraka:

  1. Mchezaji Hassan Hamis Ramadhan au Hassan Kessy alikuwa na Mkataba na Klabu ya Simba uliokuwa unaishia tarehe 15/06/2016.

  2. Young Africans SC walikiri mbele ya Kamati kupeleka jina la Mchezaji Hassan Ramadhani Kessy huko Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) tarehe 10/06/2016 huku mchezaji huyo akiwa ndani ya mkataba na klabu ya Simba.

  3. TFF kupitia Sekretarieti yake ilikuwa na nafasi ya kuweza kuielekeza Young Africans SC hatua stahiki za kuchukua ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na Klabu ya Simba kama taratibu zinavyoelekeza. Kama hatua hii ingechukuliwa kwa wakati mwafaka mgogoro huu usingekuwa na sura ya sasa na pengine usingekuwepo.

  4. Simba SC walileta machapisho yanayotokana na Mtandao/blog wa mtu waliomtaja kuwa ni Bin Zubeiry ukimwonyesha Mchezaji yuko na viongozi wa Young Africans.

  5. Young Africans SC ilionesha Mkataba iliosainiwa na Hassan Hamis Kessy tarehe 20/6/2016 na hivyo hakukuwa na sababu ya msingi ya kufanya mambo yaliyoainishwa kwenye kipengele cha 2 and cha 4 kabla ya kumalizika kwa mkataba kati mchezaji Haasan Kessy na Klabu ya Simba.

  6. Bila kuathiri hadhi ya Uanachama wengine wa TFF, Klabu ya Simba ni brand kubwa kama ilivyo Klabu ya Young Africans, umakini mkubwa upaswa kutumika katika kushughulikia brand hizi ili kuepuka madhara yasiyokuwa ya lazima.

  HATUA:
  Kitendo cha Klabu ya Young Africans kupeleka jina la mchezaji wa klabu nyingine CAF huku mchezaji huyo akiwa ndani ya mkataba na mwanachama mwingine wa TFF ni kosa kubwa kwa mujibu wa kanuni za ligi kifungu 69[5] ambalo linapaswa kupewa adhabu itakayopelekea wanachama wote kuheshimu nafasi ya TFF kwenye suala la usajili na sio kuanza kwenda CAF au kwingineko ili kulinda integrity ya soka la Tanzania. 

  Klabu ya Young Africans inatozwa faini ya Sh 3,000,000 (Sh milioni tatu) kwa mujibu wa kanuni na fidia kwa klabu ya Simba ya Sh 50,000,000 (Shilingi milioni hamsini).

  Ofisa wa TTF aliyehusika ama kwa kushirikiana na Uongozi wa Klabu ya Young Africans au kwa kutochukua hatua stahiki kwa wakati apelekwe kwenye mamlaka yake ya nidhamu, yaani, Katibu Mkuu wa TFF ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dcidi yake.

  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete Desemba 8, 2016 amafanya ziara katika vijiji vya jimbo lake kukagua Miradi ya kimaendeo na kuona namna utekelezaji wake, Katika kijiji cha Kwakonje Shule ya msingi kulikuwa na changamoto kubwa ya vyumba vya Madarasa lakini tayari ujenzi umeanza katika shule hiyo pamoja na Shule ya Msingi Kibindu, Mbali na Shule katika vijiji hivi changamoto nyingine kubwa ni Maji pamoja na Barabara lakini kupitia Mbunge wao, tayari wamerekebisha barabara ya kutoka Kwaruhombo kwenda kwa Mduma ambayo ni KM 8 iliyokuwa kero kubwa na wamechimba visima kwa msaada wa waturuki katika kijiji cha Kwamsanje lakini pia kutokana na mvua kutonyesha vizuri mwaka jana katika vijiji hivyo kuna changamoto ya uhaba wa chakula lakini kupitia ofisi ya mbunge ziliombwa tan 1200 katika ofisi ya Waziri Mkuu maafa na zikapatikana tan 200 kwa awamu ya kwanza lakini sasa zimepatikana tan 400 na chakula hicho kitagawiwa.
  Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akizungumza na wanakijiji wa Kibindu katika mkutano baada ya kufanya ziara ya kushitukiza kukaguwa miradi ya kimaendeleo katika Jimbo lake.
    
  Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akifungua mani katika kisima kilichojengwa kwa msaada wa watu wa Uturuki kupitia Ofisi ya Mbunge katika kijiji cha Kwamsanje baada ya kufanya ziara ya kushitukiza kukaguwa miradi ya kimaendeleo katika Jimbo lake.


  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyeshwa pembe za faru John na  Kaimu Mkurugenzi  Msaidizi wa Kitengo cha Kupambana na Ujangili wa Wanyamapori  (Acting Assistant Director of Antipoaching, Wildlife Division), Bw. Robert Mande, katika kikao klichofanyika kwenye Makazi yake jijini Dar es salaam Desemba 9, 2016. Kulia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanninayoelezea e maghembe.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akioneshwa pembe za faru John na Kaimu Mkurugenzi  Msaidizi wa Kitengo cha Kupambana na Ujangiri wa Wanyamapori (Acting  Assistant Director of Antipoaching, Wildlife Division), Robert Mande, katika kikao klichofanyika kwenye Makazi yake jijini Dar es salaam leo.(PICHA NA OWM)
   Kaimu Mkurugenzi  Msaidizi wa Kitengo cha Kupambana na Ujangiri wa Wanyamapori  (Acting Assistant Director of Antipoaching, Wildlife Division), Bw. Robert Mande (kulia) na Mkuu wa Hifadhi ya Ikorongo Gurunetya Serengeti, Nollosco Ngowe wakiwa wamebeba sanduku lenye pembe za faru John baada ya kumwonyesha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika kikao kilichofanyika kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Desemba 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  -------------------------------------
   WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea taarifa ya utaratibu uliotumika kumhamisha faru John kutoka Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Sasakwa Black Rhino Sanctuary iliyoko kwenye Hifadhi ya Grumeti.
  Akizungumza katika kikao kilichofanyika nyumbani kwake Oysterbay leo mchana (Ijumaa, Desemba 9, 2016) na kuhudhuriwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe na baadhi ya watendaji wa wizara yake, Waziri Mkuu amesema taarifa hiyo itafanyiwa kazi na wataalamu wa ofisi yake.
  “Nilipokea taarifa yenu jana saa 7 usiku lakini nikaahidi kuwa leo tukimaliza sherehe za maadhimisho ya Uhuru tukutane na kujadiliana kuhusu taarifa yenu,” amesema.
  Akisoma taarifa hiyo mbele ya Waziri Mkuu, Prof. Maghembe alisema hadi kufikia Desemba 2015 wakati faru John anahamishwa alikuwa na watoto 26 (sawa na asilimia 70.2) ya faru wote waliokuwepo ndani ya kreta.
  “Kati ya faru 37 waliokuwepo ndani ya kreta, watoto wake walikuwa 26 sawa na asilimia 70.2. Uamuzi wa kumuondoa John ulikuwa ni muhimu ili kuwezesha kuongezeka kwa faru weusi na kupunguza tatizo la ‘inbreeding’ ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro,” alisema Waziri Maghembe.

  Baada ya kuhamishiwa Sasakwa, Waziri Maghembe alisema Julai 10, 2016 afya ya faru John ilianza kudorora na alikufa tarehe 18 Agosti, mwaka huu. Taarifa hiyo iliandaliwa na Kamati ya Taifa ya Kuwalinda Tembo na Faru. Kamati hiyo inaundwa na Mkurugenzi Mkuu wa TAWIRI, Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Mkurugenzi Mkuu wa NCAA na Mhifadhi Mkuu wa Ngorongoro.

  Akikabidhi pembe za faru huyo mbele ya Waziri Mkuu, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Kupambana na Ujangili wa Wanyamapori, Bw. Robert Mande alimweleza kwamba pembe kubwa ya faru John ilikuwa na uzito wa kilo 3.6 na pembe ndogo ilikuwa na uzito wa kilo 2.3.
  Watendaji wa wizara waliohudhuria kikao hicho ni Kaimu Katibu Mkuu, Bw. Iddi Mfunda; Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Bw. Freddy Manongi; Mkurugenzi Mkuu wa TAWIRI, Bw. Simon Mduma; Kaimu Mkurugenzi Idara ya Wanyamapori, Bw. Alexander Songorwa na Mkuu wa Pori la Akiba la Ikorongo/Grumeti, Bw. Nollasco Ngowe.
  Desemba 6, mwaka huu, akiwa ziarani mkoani Arusha, Waziri Mkuu aliuagiza uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), umletee nyaraka zote zilizotumika kumhamisha faru maarufu kwa jina la ‘John’ kutoka kwenye hifadhi hiyo ifikapo Alhamisi, Desemba 8.

  Alitoa agizo hilo alipotembelea ofisi za makao makuu ya NCAA zilizoko wilayani Ngorongoro, mkoani Arusha na kuzungumza na watumishi wa mamlaka hiyo pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wafugaji ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani humo.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU
  IJUMAA, DESEMBA 9, 2016.

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Mhandisi Felchesmi Mramba, (kushoto),  akimwelezea jambo Makamu wa Rais wa Shirika la  Serikali ya Japan, linaloshughulikia uratibu wa misada ya maendeleo ya kimataifa, (JICA), Suzuki Noriko,  kuhusu hatua iliyofikiwa na TANESCO katika uboreshaji wa miundombinu ya kupoza na kusambaza umeme alipotembelea kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Ilala-Mchikichini jijini Dar es Salaam, ambapo JICA inashirikana na serikali katika kukiboresha kituo hicho.
  NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
  Makamu wa Rais wa Shirika la Serikali ya Japan linaloratibu Misada ya Maendeleo laKimataifa (JICA), Bw. Suzuki Noriko ametembelea kituo kipya cha kupoza na kusambaza umeme cha Ilala-Mchikichini kinachoendeshwa na Shirika la Umeme nchini Tanesco.

  Ziara hiyo aliifanya Desemba 9, 2016 ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Mhandisi Felchesmi Mramba, alimtembeza kujionea hatua mbalimbali zilizofikiwa katika uboreshaji miundombinu ya TANESCO ikiwemo jingo na mitambo.

  Jengo jipya la kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Ilala-Mchikichini jijini Dar es Salaam, ambacho JICA imechangia ujenzi wake.
  Ziara hiyo inakuja mwezi mmoja tu baada ya Waziri Mkuu wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa, kuzindua kituo cha udhibiti na usimamizi wa mifumo ya usambazaji umeme katika jiji la Dar  es salaam kilichoko Mikocheni jijini Dar es Salaam ambapo kituo hicho cha Ilala, ni sehemu ya mradi wa uboreshaji miundombinu ya umeme kwenye jiji hilo.

  JICA na mashirika mengine ya kimataifa yanafadhili mradi huo wa uboreshaji umeme jijini ambapo lengo ni kuwapatia wakazi wa jiji umeme ulio bora na wa uhakika zaidi, ambapo utekelezaji wa mradi huu umehusisha ujenzi wa kituo cha kupoza nguvu za umeme chenye ukubwa wa 100MVA (2X50MVA), 132/33KV cha City Centre, ujenzi wa mfumo wa njia ya usafirishaji umeme chini ya ardhi (Underground Transmission Line) na kwa kutumia minara (Overhead Line) ya msongo wa wa kilovolti 132 kutoka kituo cha Ilala hadi kituo cha City Centre umbali wa Kilomita 3.4, vile vile ujenzi wa mfumo wa njia ya usafirishaji umeme chini ya ardhi, (Underground Transmission Line) kutoka kituo cha Makumbusho hadi kituo cha City Centre umbali wa kilomita 6.67.

  Mhandisi Mramba, akiongoza ujumbe wa JAICA kutembelea kituo hicho.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim M. Majaliwa amewataka waajiri kuendelea kuwapa fursa wafanyakazi wao kwa kwenda kupata ujuzi wa aina mbalimbali kwani serikali imeadhimia kutoa mafunzo mahsusi kwa lengo la kuwajenga uwezo waajiriwa.

  Majaliwa amesema hayo wakati wa utoaji wa tuzo za mwajiri bora wa mwaka iliyoandaliwa na  Association of Tanzania Employer (ATE) zilizofanyika jana usiku na kuhudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na kazi, Ajira, Vijana na Wenye Uleamavu Jenista Mhagama na Naibu wake waziri Abdallah Possi.,

  Katika utoaji wa tuzo hizo, Majaliwa amesema kuwa waajiri wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ugumu wa upatikanaji wamitaji, tozo ya kuendeleza ujuzi na utiriri wa tozo mbalimbali ambapo huwa inawapa ugumu kuweza kuwapa stahiki waajiriwa na kwa wakati.

  Naye Mwenyekiti wa ATE, Almas Maige amesema kuwa bado wanakabiliwa na changamoto nyingi ila wanaimani kuwa kutokana na ushirikiano wanaoupata sasa hivi kutoka kwa serikali ya awamu ya tano wana uhakika wa kuweza kutimiza malengo ya waajiriwa ili kupata haki zao.

  Maige amesema kuwa bado wataendelea kuandaa tuzo hizi na zaidi Ubalozi wa Norway umeonesha nia nzuri ya kushirikiana nasi kuweza kuona tunafikia makengo mazuri.

  Mkampuni na mashirika mbalimbali waliweza kushiriki na kufanikisha hafla hiyo ikiwemoi NSSF, PPF, NHC, SSRA, Geita Gold Mine, Coca Cola, MeTL, ACACIA na mengine pia.

  Mshindi wa kwanza wa tuzo ya mwajiri bora ni Kampuni ya Bia ya Tanzania Breweries Limited (TBL) wakifuatiwa na Coca cCola Kwanza na mshindi wa tatu ni Geita Gold Mine.
   Waziri Mkuu  Kassim M. Majaliwa akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili kwenye Ukumbi wakati wa utoaji wa tuzo ya mwajiri bora wa mwaka 2016 jhafla iliyofanyika jana usiku Jijini Dar es salaam, Kushoto ni  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na kazi, Ajira, Vijana na Wenye Uleamavu Jenista Mhagama na Naibu wake waziri Abdallah Possi.

   Tuzo mbalimbali zikiwa zimeandaliwa kwa ajili ya kupatiw amakampuni yaliyoshiriki mwaka 2016.

  Waziri Mkuu  Kassim M. Majaliwa akizungumza wakati wa hafla ua utoaji wa tuzo ya mwajiri bora mwaka 2016 iliyoandaliwa na Association of Tanzania Employer (ATE).

  Mwenyekiti wa Association of Tanzania Employer (ATE), Almas Maige akizungumza wakati wa hafla ua utoaji wa tuzo ya mwajiri bora mwaka 2016 iliyofanyika jana usiku Jijini Dar es salaam.

  Waziri Mkuu  Kassim M. Majaliwa akimpatia tuzo ya mshindi wa kwanza ya tuo ya mwajiri bora mwaka 2016 Afisa Mwajiri Mkuu wa Tanzania Breweries Limited (LTD) David Magese jana Jijini Dar es salaam.

  Waziri Mkuu  Kassim M. Majaliwa akimpatia tuzo ya mshindi wa pili ya Tuzo ya mwajiri bora wa mwaka 2016 Meneja  Mwajiri Coca Cola Kwanza Sigifrid Faustine jana Jijini Dar es salaam.

  HABARI ZAIDI SOMA HAPA

  0 0

   Mabweni ya shule ya Secondary ya Ufundi ya Mtwara (Mtwara Technical Secondary School) yamewaka  moto asubuhi ya leo na kuteketea kabisa. Hakuna mtu aliyepata madhara kwani shule zimefungwa na hakukuwa na wanafunzi. Chanzo cha moto bado hakijajulikana. Polisi wanaendelea na uchunguzi
   Mabweni ya shule ya Secondary ya Ufundi ya Mtwara yakiwaka  moto leo asubuhi.
   Bweni la wasichana katika Shule ya Sekondari Mtwara likiteketea kwa moto leo. Chanzo cha ajali hiyo hakikuweza kujulikana  mara moja.
  Askari wa kikosi cha Zimamoto wakijitahidi kuzima moto huo
   Askari wa kikosi cha Zimamoto wakijitahidi kuzima moto huo
  PICHA ZOTE NA SIJAWA OMARI


  0 0

   Makomandoo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wakionyesha  uwezo wao wa kukabiliana na adui bila kutumia silaha za moto katika  maadhimisho ya miaka 55 ya uhuru kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam Desemba 9, 2016. 
  Makomandoo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wakionyesha  uwezo wa miili yao kuvumilia maumivu kwa mmoja wao kulalia misumari huku mwenzie akimkandamiza kwa miguu  katika  maadhimisho ya miaka 55 ya uhuru kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam Desemba 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wananchi waliohudhuria sherehe za miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama wakati wimbo wa Taifa ulipokuwa ukipigwa uwanjani hapo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride katika sherehe za miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
  Vikosi mbalimbali vya Majeshi vikipita mbele ya mgeni Rasmi kwa mwendo wa pole na Haraka katika sherehe za miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembea wasaidizi wake pamoja   na  Askari Polisi wa Usalama barabarani ambao huongoza misafara ya viongozi (VIP riders) baada ya kuwasili Ikulu  wakitokea katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
  ------------------------------------------------------------
  Katika kuadhimisha miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara tarehe  9 Disemba, 2016 Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya Ibara ya 45(1)(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa msamaha kwa wafungwa wafuatao:-


  (i)           Wafungwa wote wamepunguziwa moja ya sita (1/6) ya vifungo vyao zaidi ya punguzo la kawaida linalotolewa chini ya kifungu 49(1) cha Sheria ya Magereza Sura ya 58 isipokuwa wafungwa walioorodheshwa katika Ibara ya 2 (i-xx).


  (ii)         Wafungwa wagonjwa wenye magonjwa kama UKIMWI, KIFUA KIKUU (TB) na SARATANI (CANCER) ambao wako kwenye “terminal stage”. Wafungwa ambao wamethibitishwa na Jopo la Waganga chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya.


  (iii)       Wafungwa wazee wenye umri wa miaka sabini (70) au zaidi ambao umri huo umethibitishwa na Jopo la Waganga chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya.


  (iv)        Wafungwa wa kike walioingia na mimba gerezani, pamoja na wale walioingia na watoto wanaonyonya na wasionyonya.


  (v)          Wafungwa wenye ulemavu wa mwili na akili (Physical disability and mental disability) ambao ulemavu huo umethibitishwa na Jopo la Waganga chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya.


  2.      Aidha, Msamaha huu wa Mheshimiwa Rais hautawahusu wafungwa wafuatao:-


  (i)              Wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kunyongwa.

  (ii)            Wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kunyongwa na adhabu hiyo kubadilishwa kuwa kifungo cha maisha au kifungo gerezani.


  0 0


  0 0


  0 0


  0 0


  0 0


  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Tunduru JUMA HOMERA akiwa ameongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo wakitembea pembezoni mwa mto ruvuma ambao katika kijiji cha wenje  ambapo mto huo unatenganisha Tanzania na Nchi ya Msumbiji.

  "Watanzania  ambao wanashikiliwa nchini MSUMBIJI ni wakazi wa kijiji cha Mkapunda na wenje wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma ambapo vijiji hivyo vipo mpakani na kijiji cha Luimila cha wilaya ya Niassa nchini Msumbiji, Vijiji hivyo vya Tanzania na Msumbiji vinatenganishwa na Mto Ruvuma. Kwa undani wa habari hii angalia video yake hapo chini ".


older | 1 | .... | 1456 | 1457 | (Page 1458) | 1459 | 1460 | .... | 3270 | newer