Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Jumla ya Vikundi 16 kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini vinavyojihusisha na masuala ya kilimo vimekutanishwa na Tasisi za kifedha na mabenki ili kuwezeshwa kama mpango wa taasisi ya Land O Lakes.
Akizungumza na Globu ja Jamii,Mshauri wa biashara bunifu kutoka tasisi hiyo ,Renalda Lema amesema kuwa katika vikundi hivyo 16 wamewakilishwa na watu wawili wawili,ili kuwasilisha ubunifu wao kwa taasisi hizo na kupata fursa ya kupanua biashara yao.
“Kama ambavyo unaweza kuona wabunifu walivyotengeza mashine mbalimbali, ambazo zitaweza kumuondoa mkulima kutoka sehemu moja hadi nyingine, hasa katika serikali hii ambayo inahamasisha uchumi wa viwanda, hivyo sisi tumeona uchumi wa viwanda hauwezi kufanikiwa bila ya kuanza kuwawezesha wakulima katika hatua ya awali kabisa” amesema Renalda.
Ametoa wito kwa wadau na taasisi mbalimbali ambazo zinahitaji kuwawezesha wakulima hao kwa namna moja ama nyingine,kuwasiliana na taasisi ya Land O’ Lakes kuwakutanisha na wakulima hao.
Mkurugenzi wa tasisi ya fedha ya Brac, Mahufuzii Ashrafu , akizungumza na baadhi ya wabunifu waliokutanishwa na kampuni hiyo ili waweze kuwezeshwa kama mpango wa tasisi ya Land O Lakes ili waweze kufikia malengo waliyojiwekea.
Mbunifu wa mashine ya kukamua matunda kutoka mkoa wa Songwe, Yohana Mwanzyunga(wa kwanza kulia) akiwaonyesha washiriki wengine mtambo wa kukamua matunda.
Baadhi ya washiriki wakiangalia mashine ya kupukucha halizeti