Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

TAARIFA KUTOKA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) KWA UMMA.


MBUNGE RUFIJI ACHUKIZWA NA BAADHI YA WATENDAJI WA VIJIJI AMBAO NI MAFISADI NA WALA RUSHWA

$
0
0
NA VICTOR MASANGU, RUFIJI

IMEELEZWA kuwepo kwa sakata la kutokea kwa migogoro ya ardhi kila kukicha katika Wilaya ya Rufiji  Mkoa wa Pwani  kunachangiwa kwa kiasi kikubwa na baadhi ya watendaji wa vijiji kuendekeza masuala ya rushwa ,ufisadi na kuuza maneo kiholela  hali ambayo inasababisha kuchochea  vurugu na mapigano ya mara kwa mara kati ya jamii ya wakulima na wafugaji .

Hayo yamebainishwa na Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa wakati wa ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kuweza kukagua shughuli mbali mbali  za kimaendeleo pamoja na kuona  changamoto zinazowakabili wananachi wake ili kuweza kuona namna ya kuzitafutia ufumbuzi.

Mchengerwa alisema kwamba katika Jimbo lake la Rufiji kumekuwepo na baadhi ya wenyeviti wa vijiji na watendaji kuwa na tamaa kwa kuamua kuuza hekari moja ya ardhi kwa kiasi cha shilingi elfu tisa hali ambayo amedai hawezi kuwavumilia na atakikisha anashirikiana na viongozi wa serikali kuvunja mikataba yote kwa wawekezaji waliojipatia maeneo  kinyume cha sheria.

“Jamani wananchi wangu kwa hili suala mimi siwezi kukubaliana nalo hata kidogo yani baadhi ya watendaji wa vijiji wanafanya mambo kinyume cha sheria na taratibu kabisa, wanauza ardhi kwa bei ya shilingi elfu tisa, hapa hili nitalivalia njuga na wawezezaji wote walionunua maeneo inabidi tukae nao tena chini kuwekeana mikataba hii sio sahihi hata kidogo,”alisema Mchengerwa.

Aidha Mchengerwa katika hatua nyingine alisema kutokana  na kuwepo na hali ya sintofahamu kwa wananchi wa  kata nzima ya Chumbi  kuhusiana na suala zima la baadhi ya  watendaji wa kijiji hicho kutuhumiwa  kuhusika kujihusisha na uuzaji wa maeneo na kufanya  ubadhilifu wa fedha amewataka kutomkaribisha mwekezaji wa  yoyote mpaka Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injia Evarist Ndikilo atapokwenda kusikiliza kilo chao na  kulitatua sakata hilo la ardhi.

Pia Mchengerwa alisema kuwa maeneo mengi  yameuzwa bila ya kuzingatia sheria na taratibu, hivyo katika eneo la kijiji cha Chumbi anatambua kuna migogoro mingi ya ardhi hiyo katika kulitataua suala hilo atahakikisha anashirikiana na viongozi wa ngazi ya Mkoa kwa lengo la kuweza kurudisha ardhi ambayo imechukuliwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha Chumbi Salumu Mtimbuko  ambaye pia ni Diwani wa kata ya Chumbi baada ya kutuhumiwa kuhusika katika uuzaji wa ardhi kiholela na ubadhilifu wa fedha na wananchi alisema kwamba kuna baadhi ya wawekezaji wamenunua zaidi ya hekari 2900 wakati yeye bado ajaingia maadarakani.

WANANCHI  wa kijiji cha Chumbi A,B,na C kata ya Chumbi  Wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani kwa sasa wanakabiiwa na sakata la kuwepo kwa  migogoro mikubwa ya ardhi inayosababishwa na baadhi ya viongozi wa kijiji kujiuzia maeneo kiholela bila ya kuzingatai sheria na taratibu zilizowekwa hali inayopelekea kuwepo kwa uvunjifu wa amani.
 Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa akiwawahutubia wananchi wa kijiji cha Chumbi Wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani katika mkutano wa adhara wa kujadili changamoto zinazowakabili hususan migogoro ya ardhi.(PICHA ZOTE NA VICTOR  MASANGU)

KAMPUNI ZA WATUMISHI ZISIPEWE ZABUNI NDANI YA HALMASHAURI WANAZOZITUMIKIA-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Bi. Theresia Mahongo kuhakikisha kampuni zinazomilikiwa na madiwani na watumishi wa halmashauri hiyo hazipewi  zabuni zinazotolewa katika maeneo yao kwa ajiliya  kuepusha migongano ya kimaslahi.

Ametoa agizo hilo leo (Jumatatu, Desemba 5, 2016) wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Karatu mkoani Arusha katika ukumbi bwalo la  Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Karatu akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani hapa.

"Hauzuiliwi kufanya biashara ili mradi kampuni yako isifanye kazi katika halmashauri ambayo wewe unaitumikia na una nguvu nayo ili kuepusha migongano ya kimaslahi kwani miradi yote utajilundikia," amesema.
Pia amewataka Wakuu wa Idara katika halmashauri hiyo walisaidie Baraza la Madiwani katika kubaini vyanzo vipya vya mapato kwa lengo la kuongeza mapato ya halmashauri yao.

Wakati huo huo Waziri Mkuu amewataka watumishi wa halmashauri wa umma  kujitathmini na kujiridhisha kama wanafuata misingi ya utumishi katika utendaji kazi wao wa kila siku. Amewasisitiza  wawatumikie wananchi kwa uadilifu na uaminifu mkubwa.

"Hatuhitaji kuwa na mtumishi mvivu, asiyewajibika, mwizi, mla rushwa na asiyekuwa muadilifu mahali pa kazi.Na  atakayeona ameshindwa kutunza na kusimamia fedha za miradi ya maendeleo ya wananchi atoe taarifa hatutaki watu kufanya kazi kwa mazoea," amesema.

Waziri Mkuu ameongeza kuwa " watumishi wa umma lazima mbadilike na muwe na nidhamu ya kazi. Muache malalamiko fanyeni kazi na msitafute  sympathy (huruma) kutoka kwa watu kwani Serikali haitamuonea mtumishi yeyote ," amesema.

Amesema katika baadhi ya ofisi za Serikali kuna ugonjwa wa watumishi wanapoona wageni wamelifika kwa ajili ya kupatiwa huduma wanawapita bila ya kuwasikiliza. " sasa hatutaki watumishi wa namna hiyo, Jukumu lako ni kumtumikia Mtanzania na tunataka kuona mabadiliko. Hatutaki kuona watu wakizubaa maofisini,".

Waziri Mkuu amesema Serikali ikikuta wananchi wanalalamika kutokana na kutoridhishwa na  huduma zitolewazo na watumishi wa umma itahakikisha watumishi hao wanachukuliwa hatua. Serikali ni ya Watanzania wote hivyo lazima wahudumiwe vizuri bila ya kujali uwezo wao kifedha wala itikadi zao za kidini na kisiasa.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMATATU, DESEMBA 5, 2016.

Viwanda 400 kushiriki maonyesho ya viwanda Dar

$
0
0
Zaidi ya viwanda 400 vinatarajia kushiriki maonesho ya aina yake ya viwanda vya Tanzania, maonesho yenye lengo la kuitangaza na kuikuza sekta ya viwanda ili iweze kuchangia pakubwa katika uchumi wa taifa.

Maonesho hayo yanatarajia kuanza (kesho) Jumatano Desemba 07 na kufikia kilele chake Desemba 11 katika Uwanja wa maonesho ya Biashara ya kimataifa wa Mwl.J.K Nyerere maarufu kama Sabasaba jijini Dar es salaam.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni(BRELA),,Bwana Frank Kanyusi alisema jana jijini Dar es salaam kuwa, lengo la maonesho hayo ni kutekeleza azma ya serikali ya ya awamu ya tano, ya kuifanya Tanzania kufikia hatua ya kuwa nchi ya viwanda.

Bwana Kanyusi alisema maonesho hayo yatatoa fursa kwa viwanda vidogo, vya kati pamoja na viwanda vikubwa, kuonyesha bidhaa wanazozalisha nchini, na kutoa hamasa kwa watanzania kutumia bidhaa hizo.

“Tunataka wazalishaji kwenye viwanda vya chini hadi viwanda vikubwa, waje wawaonyeshe watanzania kile ambacho kinazalishwa, huku tukitarajia wananchi watahamasika katika kununua bidhaa hizi zinazozalishwa Tanzania,” alizema Bwana Kanyusi .

Alisema kusanyiko hilo la wazalishaji, wafanyabiashara na wananchi, itakuwa fursa nzuri ya kutoa huduma mbalimbali zinazohusiana na uwekezaji katika sekta ya viwanda na biashara, huduma ambazo zitapatikana kwenye viwanja vya maonyesho na kutolewa na watendaji wa BRELA.

“Maonesho hayo ni fursa pia kwa washiriki na wananchi kupata huduma za haraka na za papo kwa papo zinazoihusu sekta za viwanda na biashara, kama vile usajili wa makampuni, alama na majina ya biashara, utoaji wa leseni za viwanda, pamoja na urasimishaji wa biashara, ” aliongeza.

Alisema BRELA itakuwa na banda maalum ambalo litatoa huduma hizo kwenye viwanja hivyo vya maonesho, na kuwataka washiriki na wananchi wengine wenye kuhitaji huduma za usajili ama leseni za viwanda vidogo na vikubwa, kutumia fursa ya maonesho hayo kupata huduma nyingi na za haraka zitakazotolewa muda wote wa maonesho hayo.

Akizungumzia urasimishaji wa biashara, Bwana Kanyasi alisema ni wakati muafaka kwa watanzania kufanya urasimishaji wa biashara zao, kwa lengo la kuwafanya waendeshe ama kumiliki biashara halali na inayotambulika kisheria, na hivyo kuwaondolea usumbufu usiokuwa wa lazima kutoka kwenye taasisi na vyombo mbalimbali vya serikali.

“Ni jambo la msingi kwa wafanyabiashara ama wamiliki wa viwanda na wazalishaji, kuzifanya biashara zao ziwe rasmi na kuhakikisha wanazisajili majina ama alama wanazotumia,” alisema na kuongeza kuwa hatua hiyo itarahisisha bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya Tanzania kupenya kirahisi sokoni ndani na hata nje ya nchi.

Maonyesho hayo yameandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali likiwamo Shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNIDO), Shirika la viwanda vidogovodogo (SIDO), Shirika la viwango Tanzania (TBS), pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Washirika wengine katika kuyaandaa maonesho hayo ni pamoja na Shirika la Maendeleo Tanzania (NDC), Ukanda huru wa uwekezaji (EPZA), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC), Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Kampuni inayojihusisha na alama za biashara ya GSI, pamoja na wadau wengine toka Kisiwani Zanzibar, huku lengo likiwa ni kuharakisha ukuaji wa sekta ya viwanda na biashara nchini Tanzania.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA),Bw.Frank Kanyusi akizungumza jambo juu ya maonesho ya viwanda vya Tanzania yatakayoanza Desemba (kesho) 07 hadi Desemba 11 katika uwanja wa maonesho ya Biashara ya kimataifa wa Mwl.J.K Nyerere maarufu kama Sabasaba jijini Dar es salaam yenye lengo la kuitangaza na kuikuza sekta ya viwanda ili iweze kuchangia pakubwa katika uchumi wa nchi. BRELA itatoa huduma zake za urasimishaji wa biashara katika maonesho hayo.                

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YAPOKEA TUZO YA NBAA

$
0
0
Wahasibu nchini wametakiwa kuzingatia viwango vya uhasibu vinavyotakiwa na kukubalika kitaifa na kimataifa wakati wa kuandaa taarifa za fedha kwa kuzingatia maslahi ya Taifa.

Wito huo umetolewa na Kamishna Msaidizi Sera, kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Shogholo Msangi, wakati akikabidhi tuzo za Taarifa Bora za Fedha kwa mwaka 2015/2016, kwaniaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dotto James tukio lililofanyika katika Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC), kilichoko Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam


Katika tukio hilo ambalo liliambatana na kufungwa  kwa Mkutano wa mwaka wa Wahasibu unaojumuisha nchi za Afrika Mashariki, Wizara ya Fedha na Mipango, kupitia Fungu 50, imepata tuzo ya kuandaa vitabu bora vya mahesabu vinavyokidhi viwango vilivyowekwa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi (NBAA).


Bw. Msangi amesema kuwa taarifa za fedha hutumika katika matumizi mbalimbali katika Sekta ya umma na binafsi, hivyo iwapo taarifa hizo zitakuwa katika viwango vyenye ubora zitaongeza imani ya wananchi kwa Serikali yao.


Amesema kuwa taarifa hizo pia hutegemewa na wawekezaji katika kupanga maamuzi yao ya uwekezaji hapa nchini hatua itakayosaidia nchi kufikia malengo yake ya kuwa nchi ya viwanda na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Bw. Pius Maneno, amesema kuwa, kumekuwa na mafanikio makubwa katika utoaji wa taarifa za fedha kwa upande wa Taasisi za Umma na Binafsi mwaka huo ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

“Mwaka uliopita Taasisi nyingi za umma zilishindwa kufikia asilimia 75 ambacho ndicho kiwango cha chini kabisa cha Taasisi kuingia katika ushindani wa Tuzo ya taarifa bora ya Fedha ya mwaka, lakini kwa mwaka huo, Taasisi za Serikali zilizokidhi kiwango hicho ni zaidi ya Asilimia 50.” AliongezaBw. Maneno.


Aidha, amesema kuwa katika kutafuta mshindi wa Tuzo hiyo taasisi mbalimbali zimehusishwa ikiwemo Mamlaka ya Bima Tanzania, Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Taasisi ya Utawala wa Fedha na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kabla ya matokeo kuthibitishwa na Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA).


Naye Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA Prof. Isaya Jairo amebainisha faida za tuzo ya taarifa bora ya fedha kuwa ni pamoja na kujenga uwazi, uwajibikaji, uadilifu na kuwa na taarifa ya fedha yenye viwango.Amezitaka Taasisi nyingi kushiriki katika ushindani ili kuboresha taarifa za fedha za Mashirika yakiwemo ya umma na binafsi, huku akitoa wito kwa Serikali kuziagiza Taasisi zake kushiriki kikamilifu.

Miongoni mwa wizara zilizoibuka na ushindi wa Tuzo hiyo ni Wizara ya Fedha na Mipango Fungu 50 ambapo iliwakilishwa na Mhasibu wake Mkuu Bw. Christopher Lupama kupokea Tuzo hiyo, ambaye amebainisha kuwa Tuzo hiyo imewapa nguvu ya kuendelea kufanya vizuri katika utoaji wa Taarifa ya Fedha yenye viwango.


Taasisi 56 zimeshiriki kuwania tuzo hiyo inayoandaliwa kila mwaka na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA).
 Mhasibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Fungu 50 Bw. Christopher Lupama, (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa alioambatana nao wakati wa kupokea tuzo ya Taarifa Bora ya Fedha kwa mwaka 2015, katika Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (NBAA) kilichopo Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
Kamishna Msaidizi wa Sera wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Shogholo Msangi (kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Prof. Isaya Jairo wakibadilishana mawazo wakati wa zoezi la kuwakabidhi washindi wa Tuzo ya Taarifa bora ya Fedha kwa mwaka 2015, tukio lililofanyika katika Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC) kilichopo Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
  Kamishna Msaidizi wa Sera wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Shogholo Msangi akiwa katika picha ya pamoja na na washindi wa tuzo ya Taarifa Bora za Fedha kwa mwaka 2015, katika Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (NBAA) kilichopo Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.

ReadytoWork YA Benki ya Barclays yazidi kutoa fursa kwa wanafunzi wa UDSM

$
0
0
Meneja Masoko wa Benki ya Barclays Tanzania, Joe Bendera (kwa pili kulia), akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), wakati akiitambulisha program ya ‘ReadtoWork’ ya benki hiyo yenye lengo la kuwaandaa wahitimu wa vyuo vikuu na elimu ya juu kujiandaa na ajira au kujiajiri. Wengine ni baadhi ya washikiri na wawezeshaji katika mkutano huo ambao pia kituo cha televisheni cha EATV kilikuwa kikitambulisha tuzo na wasanii wanaowania tuzo hizo zinazotambuliwa na Baraza la Sanaa la Taifa.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakihudhuria mkutano huo. 
Meneja Masoko wa Benki ya Barclays Tanzania, Joe Bendera (katikati), akihojiwa na wandishi wa habari katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati wa mkutano ambapo benki hiyo iliitambulisha program yake ya ‘ReadtoWork’ yenye lengo la kuwaandaa wahitimu wa vyuo vikuu na elimu ya juu kujiandaa na ajira au kujiajiri.
Meneja Masoko wa Benki ya Barclays Tanzania, Joe Bendera (kushoto), akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika mkutano ambapo benki hiyo iliitambulisha program yake ya ‘ReadtoWork’ yenye lengo la kuwaandaa wahitimu wa vyuo vikuu na elimu ya juu kujiandaa na ajira au kujiajiri.

BALOZI LIUNDI – “NIDHAMU KATIKA UTUMISHI YAIPAISHA TANZANIA KIMATAIFA”

$
0
0
Judith Mhina - MAELEZO.

Nidhamu katika Utumishi wa Umma inayosisistizwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Imeiweka Tanzania katika ramani ya dunia.
Hayo yamesemwa na Balozi Christopher Liundi katika mahojiano kwa njia ya simu yaliyofanyika jana jumapili. Mheshimiwa Balozi Liundi alisema;
Tanzania sasa dunia nzima, na ndivyo ilivyokuwa kwa Tanzania utakumbuka enzi za Baba wa Taifa. Rais wetu anaifufua ile ari na  kurejesha heshima iliyokuwepo hapo awali ;Ameeleza kwamba nidhamu katika kila kitu ni jambo la msingi sana, iwe katika utumishi wa Umma au wa Sekta binafsi, barabarani, Nidhamu inatakiwa itoke moyoni mwako na ufurahie hali ya kuwa na nidhamu. Nidhamu katika Utumishi wa Umma ni lazima ni msingi kwa vijana wetu katika kupata ajira bila ya malamiko kutokana na Waajiri na wadau wengine kuwa vijana hawafanyi kazi au wavivu, hawana nidhamu, na viwango.
Balozi Liundi amefafanua kuwa, enzi za Baba wa Taifa unapokwenda popote duniani, ukisema niketoka Tanzania kila mtu anajua Mtanzania ni mkweli, muwazi  na ana nidhamu ya hali ya juu. Mtanzania hawezi kupokea wala kutoa rushwa, hashiriki kwenye masuala yoyote ya kuiharibia heshima nchi yake, mwenye kutumia madaraka yake vizuri, na asiyefuja mali ya umma.Amesema wakati umefika kwa Watanzania kumuunga mkono Rais wetu katika kuhakikisha kwamba nidhamu katika utumishi wa Umma inakuwepo.
Akiongea kuhusu miaka 55 ya Uhuru wa Tanganyika Balozi Liundi amesema kauli ya Rais Magufuli la kutaka Taifa liondokane na umasikinini kwa kufufua au kujenga viwanda vidogo vya kati na vikubwani lazima utekelezwe.
Balozi Liundi amempongeza Rais kwa jitihada zake za kuwaweka katika utayari wafanyabiashara binafsi wa Tanzania katika kujenga viwanda. Akiongea na wananchi alipokwenda kufungua kiwanda cha matunda cha Azam cha Salim Said Bahkresa atahakikisha changamoto zilizopo kama umeme kwa kuagiza TANESCO wamfungie umeme na kumpa shamba la hekari 1000 bure ili kupanda miwa kwa ajili ya kuzalisha sukari. “Kazi ya Serikali ni kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji ambao kwa vitendo Rais amelithibitisha hili”.
Pia nampongeza kwa kuanzisha mfumo unaomtaka kila mfanyabiashara kuwa na mashine za kulipa kodi: “Mpaka sasa imefikia mahali nchi nyingine za nje wameanza kuiga utendaji wa kazi wa Rais wetu hili ni jambo la kujivunia”. Hivyo tumuunge mkono katika hii vita ya ukusanyaji kodi. 
Tunapoadhimisha miaka 55 ya Uhuru wetu tukumbuke kauli ya Mwalimu Nyerere alisema: “ UHURU  NA KAZI”, ni kweli kabisa lazima tufanye kazi kama anavyosisitiza Rais wetu  Magufuli “HAPA KAZI TU”. Maendeleo hayaji kwa kupiga hadithi ni lazima watu wafanye kazi na asiyefanya kazi na asile.

UONGOZI WA PANGANI KUADHIMISHA UHURU KWA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI.

$
0
0
Na: Frank Shija –MAELEZO

WAKAZI wa Pangani waaswa kujitokeza kwa wingi katika wiki moja ya maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara inatarajia kuanza siku ya Desemba 7 mwaka huu.

Wiki hiyo inalenga kutoa fursa kwa wananchi kuelezea ,kusikilizwa na kutatuliwa kero zao zinazohusu masuala mbalimbali ikiwemo rushwa na ufisadi.Kauli hiyo imetolewa jana (leo) na Mkuu wa Wilaya ya Pangani Bi.Zainab Abdallah alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi katika mahojiano maalum kuhusu maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara. 

Bi. Zainabu amesema kuwa katika kuadhimisha miaka 55 ya Uhuru Wilaya yake imeandaa Wiki ya Uhuru ambayo itatumika kwa Taasisi za Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mahakama na Serikali kwa ujumla kusikiliza kero za wananchi hasa zinazohusu masuala ya Rushwa na Ufisadi.

“Mimi kama mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Mahakama nimemzungumza na Mahakimu kujitahidi kuharakisha usikilizwaji wa kesi zote zinazohusiana na rushwa kwani mueleke wa Serikali yetu ni kutokomeza rushwa kabisa,” alisema Bi. Zainab.Aliongeza kuwa Wilaya yake imeamua kuandaa wiki hii ili kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali ya Awamo ya Tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kukabiliana na adui rushwa na ufisadi kwa vitendo.

Amesema kuwa kutokana na dhamira ya dhati aliyonayo Mhe. Rais Magufuli katika kukabiliana na rushwa na ufisadi ametoa wito kwa Watanzania wote kuunga mkoni jitihada hizo.

“Ni wahakikishie Watanzania kwamba Serikali yao imedhamiria kwa dhati kubwa kuhakikisha inatokomeza tatizo la rushwa na ufisadi kwani watu wamekuwa wakihujumu uchumi wa taifa katua Awamu hii haitafumbia macho watu wa namna hiyo,” alisisitiza Bi. Zainabu.

Aidha ameongeza kuwa mbali na kusikiliza kero za wananchi wiki hiyo pia itatumika kuhamasisha wajasiriamari wadogo wadogo kuanzisha viwanda ili kutekeleza azma ya kuwa na Tanzania ya Viwanda.Desemba 9 kila mwaka Tanzania imekuwa ikiadhimisha siku ya Uhuru wa Tanzania Bara ambapo kwa mwaka huu kitaifa yatafanyika Dar es salaam na kauli ya mwaka huu ni “Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na Kuhimarisha Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo ya Nchi Yetu.”

Azam FC yaanza mazoezi rasmi leo

$
0
0
KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, leo asubuhi kabla ya kuanza rasmi mazoezi ya maandalizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) utakaoanza rasmi Desemba 17 mwaka huu, wachezaji na benchi la ufundi walisimama kwa dakika moja kuomboleza kifo cha mchezaji wa timu ya vijana ya Mbao, Ismail Khalfan.

Khalfan alifariki dunia jana wakati akikimbizwa hospitali baada ya kudondoka uwanjani kufuatia kugongana na beki wa Mwadui kwenye mchezo wao wa michuano ya Ligi ya Taifa ya Vijana kituo cha Bukoba mkoani Kagera kinachohusisha timu za Kundi B.

Kikosi hicho kimerejea tena kwenye mazoezi kufuatia kuwa mapumzikoni kwa muda wa takribani wiki mbili mara baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza.

Ni wachezaji watatu tu wa Azam FC waliokosekana kwenye mazoezi hayo wakiwa na ruhusa maalumu, ambao ni beki Erasto Nyoni, washambuliaji wapya kutoka Ghana, Samuel Afful na Yahaya Mohammed, wanaotarajiwa kuanza rasmi kujifua na wenzao kuanzia kesho Jumanne.

Wachezaji wengine walioshindwa kufanya mazoezi ni winga Khamis Mcha, anayesumbuliwa na maumivu ya nyonga ambaye alipewa programu maalumu ya mazoezi na Mtaalamu wa Viungo wa Azam FC, Sergio Perez Soto, huku beki wa kushoto, Gadiel Michael, akiwa ameteguka mkono alioumia wakati akifanya mazoezi binafsi wakati wa likizo iliyopelekea kufungwa plasta gumu ‘p.o.p’.

Akizungumza na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz kuhusu programu yake ya wiki hii, Kocha Mkuu wa Azam FC, Zeben Hernandez, ameelezea kufurahishwa na namna wachezaji wake walivyorejea mazoezini wakiwa na hali nzuri licha ya kutoka mapumzikoni hali ambayo inampa wakati mzuri kukiandaa kikosi chake kuelekea mechi za mzunguko wa pili.

“Tumeanza mazoezi leo kwa spidi kubwa kwa ajili ya kuingia kwenye mzunguko wa pili wa ligi, tumeanza kwa mazoezi mara moja leo, kesho (Jumanne) tutafanya mara mbili asubuhi na jioni kwa ajili ya kuwa fiti zaidi tayari kuingia kwenye ushindani, kwa sasa tunawasubiria wachezaji wambao hawajafika (Erasto, Yahaya, Afful), ambao watajiunga nasi kesho,” alisema.

Katika kuimarisha safu yake ya ulinzi, Azam FC imemrejesha kikosini beki wake wa kati, Abdallah Kheri, aliyekuwa akicheza kwa mkopo kwenye timu Ndanda ya Mtwara katika mzunguko wa kwanza wa ligi.

Azam FC inayoshika nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na pointi 25, inatarajia kufungua dimba la raundi ya pili ya ligi, kwa kukipiga na African Lyon Desemba 18 mwaka huu, mchezo unaotarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.


MAKAMU MKUU WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM AONGEZEWA MUDA

SERIKALI KUENDELEA KUWEKA MKAZO WA USAMBAZAJI UMEME KUFIKIA MALENGO YA DUNIA 2030

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

SERIKALI kwa kupitia Waziri wa Nishati na Madini, Mh Sospeter Muhongo, imesema itaendelea kufanya kazi kwa bidii ya kusambaza umeme ili kufikia malengo ya Duniaya kuhakikisha kwamba ifikapo mwaka 2030 Watanzania wote waweze kupata nishati hiyo muhimu.Waziri Muhongo aliyasema hayo wakati akifungua Mkutano wa Kikanda wa Nishati Endelevu kwa Wote uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Alisema usambazaji wa umeme umefanyika kwa kiasi kikubwa lakini bado wanaendelea na miradi ikiwa na lengo la kuwapatia wananchi nishati kwa uhakika kutokana na vyanzo vya nishati vilivyopo hapa nchini.

Profesa Muhongo amesema mradi wa usambazaji wa umeme vijijini umerahisisha upatikanaji wa maendeleo ya haraka kwa Watanzania wengi, hususan wale wanaoishi maeneo ya vijijini ambayo serikali imeendelea kuweka mkazo wa kufikisha huduma hiyo.

Naye Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez, alisema kukosekana kwa nishati ya umeme wa uhakika duniani kwa nchi masikini kunawafanya wananchi wakose huduma muhimu kama vile elimu afya pamoja na kufifisha maendeleo ya ukuaji wa sekta binafsi, 

Aidha Rodriguez alisema Umoja wa Mataifa utaendelea kuwezesha nchi zinazoendela ikiwemo Afrika kuwezesha kifedha katika upatikanaji wa nishati ya umeme ili kuweza kufikia lengo la Dunia 2030.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa Kikanda wa Nishati Endelevu kwa Wote uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya washiriki wa mkutano wa Kikanda wa Nishati Endelevu kwa Wote uliofanyika jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo.

MAONESHO YA VIWANDA TANZANIA VIWANJA VYA SABASABA JIJINI DAR ES SALAAM KUANZIA TAREHE 7 HADI 11 DESEMBA

$
0
0
Waheshimiwa Viongozi, 
Karibuni sana kwenye Maonesho ya Kwanza ya Viwanda vya Tanzania yatakayofanyika katika Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl. J.K. Nyerere, Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam kuanzia tarehe 7 - 11 Desemba 2016. 
Mpaka sasa kuna viwanda vidogo, vya kati na vikubwa vya Tanzania vipatavyo 400 ambavyo vimethibitisha kushiriki. 
Tunawaomba Viongozi wote ambao wangependa kutembelea Maonesho haya, watufahamishe kupitia: Simu +255 22 2850238+255 714 077 649, barua pepe: info@tantrade.or.tz ili tuwaandalie Protokali waweze kutembelea washiriki ambao wangependa kuwatembelea. Karibuni sana.

SERIKALI YAWATAKA WATENDAJI NA WAMILIKI WA BLOGS KUZINGATIA SHERIA ZA NCHI

$
0
0
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO,Dar es Salaam

SERIKALI imetoa wito kwa wamiliki na watendaji wa mitandao ya kijamii (Blogs) nchini kufuata Misingi, Sheria na Maadili ya taaluma ya habari.
Wito huo umetolewa leo Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Idara ya Habari(MAELEZO) Dkt. Hassan Abbas wakati wa uzunduzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Tanzania Bloggers Nertwork(TBN) na mafunzo kwa wanachama hao kuhusu uendeshaji wa mitandao ya jamii kwa manufaa.
Mkurugenzi Abbas alisema kuwa Blogger ni mwandishi wa habari, mwanahabari, na mwanataaluma ya habari hivyo anawajibu wa kuhakikisha anaandika na kusambaza taarifa zenye ukweli kwa manufaa ya nchi.
“Mitandao ya kijamii inalisha sehemu kubwa ya taarifa duniani hivyo wamiliki na watendaji wanapaswa kufuata misingi mikuu mitatu ya uandishi wa habari, ambayo ni ukweli, ukweli, ukweli ili kuweza kuheshimika na kusonga mbele” alifafanua Abbas.
Aidha Dkt. Abbas amewataka watendaji wa Blogs kushirikiana na Serikali katika kutoa Elimu kwa umma kuhusu Sheria ya Huduma ya Habari iliyopitishwa hivi karibuni.
Akijibu baadhi ya changamoto zinazowakabili wamiliki wa mitandao ya kijamii,  Dkt. Abbas  ametoa rai kwa vyombo vya habari pale watumiapo kazi zao wanapaswa kuwatambua au kuomba idhini kwa mmiliki wa picha au makala husika.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa muda wa TBN  Bw. Joachim Mushi alisema mkutano huo, ambao mdamini mkuu ni Benki ya NMB,  unalenga kuwafundisha wanachama juu ya uendeshaji mitandao ya kijamii kwa manufaa, upashaji habari kwa kutumia mitandao yao kwa kuzingatia maadili na namna ya kunufaika na mitandao hiyo.Naye Mkurugenzi Mtendaji na mwanzilishi wa Jamii Media Maxence Melo akiwakilisha mada kuhusu masuala mbalimbali ya umoja na mikakati ya kujenga chama alisema kuwa ili blogger kuweza kufika walipokusudia wanatakiwa kwenda na wakati.
Alisema kuwa kumekuwa na changamoto mbalimbali za ndani na nje ya ya bidhaa ama kampuni kuweza kufa, hivyo wamiliki wa mitandao ya kijamii wanapaswa kuwa wabunifu na wafuatiliaji ili kuweza kujua mteja anahitaji nini na kwa wakati gani.
Kauli mbiu ya mkutano huo ni “Mitandao ya kijamii ni ajira, itumike kwa manufaa” ni matokeo mazuri ya ushirikiano kati ya TBN na wataalamu wa masuala ya habari na mitandao ya kijami.
Mkurugenzi Idara ya Habari(MAELEZO) Dkt.Hassan Abbas (wa pili kulia).

HUSSEIN PAMBAKALI APANDISHWA MAHAKAMANI KWA DENI LA MILIONI 75

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

MMILIKI wa maduka ya nguo Jijini Dar es Salaam,Hussein Mkangala (38) maarufu 'Hussein Pamba Kali' amefunguliwa mashtaka ya kesi ya madai baada ya  kushindwa kulipa Sh.Milioni 75 alizokopa kutoka kwa Anna Kiabi.

Shauri hilo lilitajwa leo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni ambapo upande wa mdai ulikuwa unasimamiwa na Wakili Jonas Nkya, wakati ule wa mdaiwa ukiongozwa na Ernest Swai.

Mbele ya Hakimu Is -Haq Kuppa, Upande wa mdai ulisema kwamba Novemba 20 mwaka jana mfanyabiashara huyo alikopeshwa kiasi cha sh. Miloni 80 kwa makubaliano atamlipa kwa kipindi walichokubaliana kitu ambacho amevunja makubaliano.

Wakili Nkya alidai Mei 22 mwaka huu mdaiwa Husseni alimtuma mdogo wake aitwaye Hassan Mkangala, apeleke fedha kiasi cha sh. Milioni 5 kwa Anna na kiasi kilichobakia hakulipa tena.

Kwa upande wa utetezi wao waliomba mahakama hiyo iwape muda wa siku 6 ili waweze kujibu madai hayo.

Hivyo Hakimu Kuppa aliahirisha kesi hiyo hadi Desemba 15 mwaka huu itakapotajwa tena lakini Mdaiwa hakufika mahakamani.

Rais Magufuli akutana na wawakilishi wa Boeing, asema Tanzania itanunua ndege 4 pia aagana na Balozi wa Cuba na Dkt Tonia Kandiero wa AfDB

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 05 Desemba, 2016 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Masoko ya Afrika wa Kampuni ya utengenezaji wa ndege ya Boeing yenye makao yake nchini Marekani Bw. Jim Deboo ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali za kununua ndege kubwa kutoka kampuni hiyo.


Mazungumzo hayo yamefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu Uchukuzi Dkt. Leonard Chamriho na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James.


Baada ya Mazungumzo hayo Rais Magufuli amesema Serikali yake ya Awamu ya Tano imedhamiria kununua ndege nyingine nne zikiwemo ndege kubwa 3 ambazo zitasaidia kuinua uchumi wa nchi kwa kuwezesha watalii kuja hapa nchini moja kwa moja kutoka nchi zao.


"Sisi hapa tunazungumza kuwa watalii hawajafika hata milioni 2 kwa mwaka, lakini nchi kama Morocco inapata watalii zaidi ya milioni 12 kwa mwaka, hii yote ni kwa sababu hatuna mashirika ya ndege ya kwetu, watalii wakitaka kuja hapa ni lazima waje kwa kuungaunga, wafikie nchi nyingine halafu ndipo wapate moyo wa kuja huku, licha ya kwamba sisi Tanzania ni miongoni mwa nchi 5 duniani zenye maeneo mazuri yenye utalii.


"Kwa hiyo niwaombe tu Watanzania wapende mali zao, kwa sababu wakati mwingine nikiangalia mitandao na magazeti ni ajabu huwezi kuamini kama hao ni Watanzania, unakuta wanasifia tu ndege za watu wenginena wanazibeza za kwao"amesisitiza Rais Magufuli.


Mhe. Rais Magufuli ametaja aina ya ndege mpya ambazo Serikali itazinunua kuwa ni ndege 1 aina Bombardier Q400 Dash 8 NextGen inayotarajiwa kufika nchini Mwezi Juni 2017, ndege 2 aina ya Bombardier CS300 zenye uwezo wa kuchukua kati ya abiria 137 na 150 na zinazotarajiwa kuwasili nchini kati ya Mei na Juni, 2018 na ndege moja aina ya Boeing 787 Dash 8 Dream Liner yenye uwezo wa kuchukua abiria 262 na inayotarajiwa kuwasili nchini Juni, 2018. Malipo ya awali kwa ndege hizi yameshafanyika.


Dkt. Magufuli amewataka Watanzania kuunga mkono juhudi hizi za Serikali zenye lengo la kuinua utalii na kuimarisha uchumi wa nchi.


"Tumeleta ndege aina ya Bombardier hapa, zimepunguza gharama za safari mfano kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza, sasa wanalipa kati ya 160,000/ hadi 200,000/- wakati nauli ilishafika Shilingi laki 8 na kitu, lakini watu wengine utakuta wanazungumzazungumza wee maneno ya hovyo kwa kutumiwa, tumeshaamua na tutafanya hivyo"amesisitiza Rais Magufuli.


Wakati huo huo, Rais Magufuli ameagana na aliyekuwa Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika hapa nchini (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero ambaye amepandishwa cheo na kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Ukanda wa Kusini mwa Afrika katika ofisi zake zilizopo Afrika Kusini.


Rais Magufuli amemshukuru Dkt. Tonia Kandiero kwa juhudi kubwa alizozifanya akiwa Mwakilishi Mkazi wa AfDB hapa nchini ambapo miradi mikubwa na muhimu katika maendeleo imetekelezwa na inaendelea kutekelezwa.


Akizungumza baada ya kuagana na Rais Magufuli Dkt. Tonia Kandiero amemshukuru Rais Magufuli na Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano alioupata katika kipindi cha miaka 6 aliyokuwa hapa nchini na amesema anaondoka akiwa ameiwezesha Tanzania kupiga hatua kubwa ya kimahusiano na AfDB ambapo miradi yenye thamani ya Dola za Kimarekani Bilioni imetekelezwa hususani katika ujenzi wa miundombinu ya barabara.


Katika hatua nyingine, Rais Magufuli ameagana na Balozi wa Cuba hapa nchini Mhe. Jorge Luis Lopez Tormo anayemaliza muda wake baada ya kuiwakilisha nchi ya Cuba kwa miaka minne.


Rais Magufuli amemshukuru Mhe. Jorge Luis Lopez Tormo kwa uhusiano na ushirikiano mzuri aliouendeleza kati ya Tanzania na Cuba uliojengwa na waasisi Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wa Tanzania na Mhe. Fidel Castro wa Cuba.


Mhe. Jorge Luis Lopez Tormo amemshukuru Rais Magufuli na Serikali kwa kuendeleza uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Cuba na amesema anaondoka akiwa anaamini kuwa uhusiano kati ya nchi hizi utaendelea kuwanufaisha wananchi ikiwemo miradi mikubwa ya maendeleo na huduma za kijamii.

  
Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam


05 Desemba, 2016.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi wa mauzo wa kampuni ya Ndege ya Boeing Jim Deboo aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo pamoja na ujumbe wake.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitazama kitabu cha  picha ya ndege aina ya Boeing 787-8 Dream liner wakati alipokuwa akisikiliza maelezo yake kutoka kwa Mkurugenzi wa mauzo wa kampuni ya Ndege ya Boeing Jim Deboo. Ndege hiyo itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 262 na itakuwa na uwezo wa kuruka kutoka nchini Marekani hadi Tanzania bila kutua mahali popote.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kuhusiana na ununuzi wa ndege hiyo mpya aina ya Boeing 787-8 Dream liner mara baada ya kumaliza mazungumzo na Mkurugenzi wa mauzo wa Kampuni ya Ndege ya Boeing Jim Deboo Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Cuba anayemaliza muda wake nchini George Luis Lopez Tormo aliyefika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo. Dkt. Tonia ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) katika Ukanda wa Kusini Mwa Afrika katika Ofisi zake zilizopo Afrika ya Kusini.PICHA NA IKULU .


Rambirambi za serikali kwa mchezaji wa mbao FC aliyefia uwanjani Bukoba

MKUTANO MKUU WA MWAKA WA TBN WAFUNGULIWA DAR, SERIKALI YAITAMBUA RASMI MITANDAO YA KIJAMII

$
0
0






Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar

SERIKALI imetangaza rasmi kuitambua mitandao ya Kijamii (Blogs) kuwa chombo rasmi cha habari nchini. Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk.Hassan Abbas,  wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka na Mafunzo ya Tanzania Bloggers Network (TBN), uliofanyika jijini Dar es Salaam jana Jumatatu.

"Serikali sasa inaitambua rasmi mitandao ya kijamii kuwa ni chombo cha habari kama ilivyo vyombo vingine nchini hivyo nawaomba wakuu wa vitengo vya habari serikalini kushirikiana na wanamitandao hiyo katika kutoa taarifa mbalimbali" alisema  Dkt. Abbas.

Dkt. Abbas alivitaka vyombo vya habari hasa magazeti pale wanapotumia picha kutoka mitandao ya kijamii kueleza chanzo cha picha hiyo tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo picha zao zinatumika bila ya kutaja chanzo.
Katika hatua nyingine Dkt. Abbas alisema Blogs hazina tofauti na vyombo vingine hivyo ni vema wanapotoa habari zao kuzingatia sheria na weledi wa kazi vinginevyo sheria itawakumba kama ilivyo kwa magazeti na vyombo vingine.
Dkt. Abass aliwataka wanamitandao hao kujiunga na TBN ili iwe rahisi kutatuliwa changamoto walizonazo kuliko kila mmoja kuwa kivyake.

Wanamitandao hao wakizungumzia changamoto waliyonayo walimwambia mkurugenzi huyo kuwa wamekuwa wakibaguliwa na maofisa habari wa serikalini ikiwa pamoja na kunyimwa 'Press Card' jambo linalokwamisha utendaji wao wa kazi.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas akihutubia wakati wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tanzania Bloggers Network (TBN), Dar es Salaam jana  asubuhi. 

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas (kulia), akihutubia wakati wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tanzania Bloggers Network (TBN), Dar es Salaam jana asubuhi. Kushoto ni Mwenyekiti wa muda wa TBN, Joachim Mushi.

 Mkurugenzi Mkuu wa mtandao wa Jamii Forums Bw. Maxence Melo akitoa moja ya somo katika mafunzo hayo.


 Baadhi ya washiriki wakiwa katika mkutano,mafunzo hayo.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

BancABC YAZINDUA OFA YA RIBA ASILIMIA 16 KWA WATEJA WANAOFUNGUA AKAUNTI YA MUDA MAALUM MSIMU HUU WA SIKUKUU

$
0
0
Mkuu wa Masoko na Hazina wa BancABC, Barton Mwasamengo, (kushoto), na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi na wafanyabiashara wadogo wadogo, Joyce Malai, wakionyesha kadi inayoonyesha uzinduzi wa ofa ya riba asilimia 16% kwa wateja wanaofungua akaunti ya amana ya muda maalum msimu huu wa sikukuu. Uzinduzi huo ulifanyika Desemba 5, 2016 makao makuu ya BancABC jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Masoko na Hazina wa BancABC, Barton Mwasamengo, (kushoto), na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi na wafanyabiashara wadogowadogo, Joyce Malai, wakati wa mkutano na waandishi wa habari, kuzindua ofa ya riba asilimia 16% kwa wateja wanaofungua akaunti ya amana ya muda maalum msimu huu wa sikukuu. Uzinduzi huo ulifanyika Desemba 5, 2016 makao makuu ya BancABC jijini Dar es Salaam.
 Bi.Upendo Nkini(kulia), akiwakaribisha maafisa hao tayari kuzungumza na waandishi wa habari.

DKT KALEMANI AWAAHIDI WAKAZI LYAMKENA KUSHEREHEKEA KRISMAS WAKIWA NA UMEME

$
0
0
Na Veronica Simba - Makambako

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani ametoa ahadi kwa wakazi wa Kijiji cha Lyamkena kilichopo Makambako mkoani Njombe, kuwa watasherehekea sikukuu ya Krismas hapo Desemba 25 mwaka huu wakiwa na umeme. 

Dk Kalemani aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi husika jana kijijini hapo, mbele ya Mbunge wa Makambako Deo Sanga, akiwa katika ziara kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme.Naibu Waziri alimwagiza Meneja anayesimamia Mradi wa Umeme wa Makambako – Songea, Didas Lyamuya, kuhakikisha kazi ya kutandaza nyaya inafanyika usiku na mchana ili umeme uwake katika eneo hilo kufikia Desemba 25.

“Tumekubaliana na Meneja, amejipanga kuanzia wiki ijayo wataanza kutandaza nyaya na watakamilisha ndani ya siku 10,” alifafanua.Aidha, Dk Kalemani alimwagiza Meneja huyo kuviingiza katika Mradi huo mkubwa wa umeme, vijiji vya Kihumba na Katani ambavyo vilisahaulika, ili vipatiwe umeme sambamba na maeneo mengine yote kama yalivyoainishwa katika Mradi.
Meneja wa Mradi wa Umeme wa Makambako – Songea, Didas Lyamuya (katikati), akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani (kulia) na Mbunge wa Makambako, Deo Sanga (kushoto), kuhusu maendeleo ya Mradi huo wakati wa ziara ya Naibu Waziri mkoani Njombe hivi karibuni
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Lyamkena kilichopo Makambako mkoani Njombe hivi karibuni, wakati akiwa katika ziara kukagua miradi ya umeme.
Wananchi wa Kijiji cha Lyamkena, Wilaya ya Makambako mkoani Njombe, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani (hayupo pichani), wakati wa ziara yake mkoani humo hivi karibuni, kukagua miradi ya umeme.
Wananchi wa Kijiji cha Lyamkena, Wilaya ya Makambako mkoani Njombe, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani (hayupo pichani), wakati wa ziara yake mkoani humo hivi karibuni, kukagua miradi ya umeme.


SALAMU ZA RAMBI RAMBI - KIFO CHA PROF. MTULIA

Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>