Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

MIKOA NA HALMASHAURI ZATAKIWA KUWEKA TAHADHARI JUU YA KIPINDUPINDU

$
0
0

Na Ally Daud-Maelezo

MIKOA na halmashauri nchini zimetakiwa kuweka tahadhari juu ya ugonjwa wa kipindupindu kwa kuzingatia usafi binafsi na usafi wa mazingira hasa wakati wa mvua za vuli na msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka ili kuweza kuepuka ugonjwa huo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu mwenendo wa ugonjwa wa kipindupindu kwa mwezi Novemba 2016 uliofanyika jijini Dar es salaam.

“Mikoa na Halmashauri zote nchini ziwe katika hali ya tahadhari juu ya ugonjwa wa kipindupindu kwa kuzingatia usafi binafsi na usafi wa mazingira hasa wakati wa mvua za vuli na msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka ili kuweza kuepuka ugonjwa huo” alisema Waziri Ummy.

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa Mikakati ya kudhibiti ugonjwa wa Kipindupindu ishirikishe sekta mbalimbali za afya nchini bila kusahau jamii husika na kuhakikisha kila Halmashauri inaunda na kuimarisha Kamati ya Afya ya Kata. 

Aidha Waziri Ummy ameiagiza Mikoa na Halmashauri zote nchini kutoa taarifa ya wagonjwa wapya wa Kipindupindu ili jitihada za makusudi za kupambana na ugonjwa huo zifanyike mapema ili kujenga taifa lisilo na magonjwa ya mlipuko.

Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa takwimu zinaonesha katika mwezi Novemba 2016 jumla ya mikoa sita ikiwemo Morogoro yenye wagonjwa 282, Dodoma 96 na vifo 2, Mara 31, Kigoma 30 na vifo 4, Arusha 11 na Dar Es Salaam 8 kutoka wagonjwa 250 na vifo 4 kwa mwezi Oktoba mwaka huu.

Kwa wakati huohuo Waziri Ummy amepokea vifaa vya matibabu ya mabadiliko ya awali ya Saratani ya mlango wa kizazi vyenye thamani takribani milioni 100 za kitanzania kutoka Shirika la Kimataifa la Pink Ribbon Red Ribbon ili kupambana na ugonjwa huo nchini.

Akikabidhi msaada huo Mtendaji Mkuu wa Shirikahilo Bi. Celina Schocken amesema kuwa wametoa vifaa hivyo ili kuisaidia nchi kwa juhudi za kimakusudi katika kupambana na ugonjwa wa saratani ili kuokoa maisha ya wanawake wa Tanzania.

“Tumeamua kutoa vifaa hivi ili kuisaidia nchi kwa juhudi za kimakusudi katika kupambana na ugonjwa wa saratani ili kuokoa maisha ya wanawake wa Tanzania ”alisema Bi. Schocken.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kushoto akipokea vifaa mbalimbali vya matibabu ya mabadiliko ya awali ya Saratani ya mlango wa kizazi vyenye thamani takribani milioni 100 za kitanzania kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Pink Ribbon Red Ribbon  Bi. Celina Schocken jijini Dar es salaam.

salamu kutoka mwanza

$
0
0
Ankal!!
Pokea Salam kutoka Mwanza. Hii ni hali halisi ya barabara ya mwaloni, kata ya Kirumba Manispaaa ya Ilemela. Barabara hii inaelekea katika soko la kimataifa la samaki ILEMELA. Hali ya barabara hii iko hivi kwa zaidi ya miezi saba. 



MAGEREZA YAPATA MSAADA WA VIFAA VYA MICHEZO

$
0
0
 Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa(wa pili kulia) akipokea vifaa vya michezo kutoka kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya SAN LAM Life Insurance, Bw. Samuel Mika(wa pili kushoto) ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi hilo, Kamishna Gaston Sanga(wa kwanza kushoto) ni Afisa Uhusiano wa Kampuni ya SAN LAM, Bw. Rishia Kileo. Vifaa hivyo vitatumiwa na Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza katika Mashindano ya Kijeshi yanayotarajiwa kufanyika Zanzibar mwezi huu Desemba, 2016.
 Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa akitoa neno la shukrani kwenye hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa vya michezo vilivyotolewa na Kampuni ya SAN LAM Life Insurance. Hafla hiyo imefanyika leo Desemba 06, 2016 katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi hilo, Kamishna wa Magereza Gaston Sanga(kulia) ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Kampuni SAN LAM Life Insurance, Bw. Samuel Mika.
 Kaimu Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya SAN LAM Life Insurance, Bw. Samuel Mika akitoa maelezo mafupi kabla ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa Jeshi la Magereza leo Desemba 06, 2016 katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Michezo ya Jeshi la Magereza, SACP. Gideon Nkana akitoa utambulisho mfupi katika hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa Jeshi la Magereza leo Desemba 06, 2016 katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam.

Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, Dkt. Juma Malewa(katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza pamoja na Wawakilikilishi wa Kampuni ya SAN LAM Life Insurance(waliosimama). hafla hiyo ya makabidhiano ya vifaa vya michezo imefanyika leo Desemba 06, 2016 katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam.

TANZIA: MAREHEMU FELIX KAPINGA ATAZIKWA LEO TAREHE 06/12/2016 MKOANI NJOMBE

$
0
0
Wanajumuia ya wanafunzi waliosoma Tumaini University - Iringa, Songea Boys High School na Lugalo Secondary School wanasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa mwanafunzi mwenzao Marehemu Felix Kapinga (pichani) kilichotokea Usiku wa Tarehe 3/12/2016 katika Hospitali ya Ikonda Mission Mkoa wa Njombe baada ya kuugua kwa muda mfupi. 
Tunachukua fursa hii kutoa pole kwa Mke wa marehemu, Mtoto wa marehemu, Mama mzazi wa marehemu, wafanyakazi wenzake kutoka Njombe community Bank, Ndugu, jamaa, Marafiki na wana familia kiujumla kwa msiba huu walioupata, tunaungana nao katika kipindi hiki kigumu cha majonzi. 
Mazishi yanatarajiwa kufanyika leo tarehe 06/12/2016 huko huko Njombe katika eneo la kijiji kinachotambulika kwa jina la Ramadhani  ambako Mama mzazi wa marehemu ndiko anakoishi, shighuli za Mazishi zinategemewa kufanyika kuanzia saa 6.00 Mchana. Kwa taarifa zaidi unaweza ukawasiliana kwa namba 

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA 
JINA LAKE LIHIMIDIWE
AMIN.

MATUKIO YA UHAKIKI WA WASTAAFU WANAOLIPWA NA HAZINA MKOANI ARUSHA

$
0
0
Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Msaidizi Bw. Stanslaus Mpembe (kushoto)  akitoa ufafanuzi kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango namna zoezi zima la uhakiki wa wastaafu kanda ya kaskazini linavyokwenda kabla ya uzinduzi wa zoezi hilo. Zoezi hili ni kwa mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga. 
Zoezi la kuhakiki wastaafu likiendelea katika Ofisi za Makao Makuu, Halmashauri ya jiji la Arusha, Pichani ni baadhi ya wastaafu wakifanyiwa uhakiki.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Doroth Mwanyika akifurahia jambo na baadhi ya wastaafu wanaolipwa pensheni zao na Hazina, waliojitokeza kuhakikiwa wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo katika Ofisi za halmashauri ya Jiji la Arusha, zoezi litakalo dumu kwa siku tano hadi Ijumaa wiki hii katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Doroth Mwanyika akiongea na baadhi ya wastaafu waliofika katika Ofisi za Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa ajili ya uhakiki ambapo wastaafu hao wameiomba serikali iwaongezee kiwango cha pensheni wanacholipwa ili waweze kukabiliana na hali ngumu ya maisha. 

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

WAFANYAKAZI WA VODACOM TANZANIA WAENDELEA KUCHANGIA DAMU SALAMA

$
0
0
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakitoa damu kuchangia  Mpango wa Taifa wa Damu Salama Kanda ya Mashariki, katika ofisi za makao makuu Mlimani City jijini Dar es Salaam leo, ikiwa ni shughuli iliyopangwa na kampuni hiyo kuadhimisha Siku ya Ukimwi Duniani inayoadhiimishwa Desemba Mosi kila mwaka. Wafanyakazi hao walitoa damu lita 50 kuchangia mpango wa damu salama nchini.
Mtaalamu wa Maabara wa mpango wa Damu Salama Taifa Kanda ya Mashariki, Grace Isidori  (aliyesimama) akisaidia wafanyakazi wa Vodacom Tanzania kutoa damu kuchangia  mpango wa damu salama katika ofisi za makao makuu Mlimani City jijini Dar es Salaam leo,  ikiwa ni shughuli iliyopangwa na kampuni hiyo kuadhimisha Siku ya Ukimwi Duniani inayoadhiimishwa Desemba Mosi kila mwaka. Wafanyakazi hao walitoa damu lita 50 kuchangia mpango wa damu salama nchini.

Wachezaji wa Bunge Sports ya Tanzania katika michezo ya Mabunge ya Afrika Mashariki

$
0
0
Wachezaji wa Bunge Sports ya Tanzania katika michezo ya Mabunge ya Afrika Mashariki inayoendelea mjini Mombasa, Kenya. kutoka kushoto Mhe Bobali, Mhe Chumi, Mhe Zitto, Mhe Mchengerwa wakifuatilia kwa makini mchezo baina ya Uganda na Kenya kwenye Uwanja wa Mbaraki

SERIKALI YAHIDI KUTOA USHIRIKIANO WA KUTOSHA KWA UONGOZI MPYA WA TUCTA.

$
0
0
Na Daudi Manongi-MAELEZO

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu, Jenister Mhagama amesema Serikali itaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA) ili kuleta tija na ufanisi katika sekta ya kazi.

Waziri Mhagama aliyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wake na Viongozi hao wa TUCTA waliofika ofisini kwake kwa ajili ya kujitambulisha mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa shirikisho hilo.


“Tumefarijika sana kwa TUCTA kupata uongozi mpya ambao tuna uhakika wanachama wamezingatia masuala  muhimu katika uchaguzi wao ikiwemo weledi na kutazama dira ya sekta ya wafanyakazi nchini”.


Aidha aliongeza kuwa Viongozi hao wana jukumu kubwa la kuleta tija na maendeleo chanya katika sekta ya kazi nchini na kuhimiza kuwa wafanyakazi ni rasilimali muhimu katika kuleta maendeleo ya nchi.

Kwa mujibu wa Mhagama ameahidi Viongozi hao kufanya kikao kazi mapema iwezekanavyo kwani uchaguzi umekwisha na sasa kilichobaki ni kufanya kazi.


Pia amesisitiza ushirikiano wa kudumu kati ya Serikali, Waajiri na wafanyakazi ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa kutatua migogoro iliyopo.

Kwa upande wake Rais wa TUCTA, Tumaini Nyamghokya alimshukuru Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa kusimamia utu wa mtumishi kwa kuhaidi kuwalinda kutokana na baadhi ya viongozi kutoa lugha zisizosahihi.


Aidha, ameishukuru Serikali kwa kuwa karibu nao kwa muda wote na kuhaidi kuendeleza ushirikiano huo ili kuleta tija katika kazi.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu Mhe.Jenister Mhagama akimskiliza Rais wa TUCTA Bw.Tumaini Nyamghokya wakati viongozi wapya wa TUCTA walipomtembelea Ofisini kwake Magogoni Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu Mhe.Jenister Mhagama akizungumza na uongozi mpya wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini(TUCTA) ofisini kwake Magogoni Jijini Dar es Salaam.Waziri uyo amehaidi kuwapa ushirikiano wa kutosha viongozi hao ili kuleta tija na ufanisi katika sekta ya kazi.

Serikali yaagiza Mamlaka za Serikali za Mitaa kulinda mazingira

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi),George Simbachawene ameziagiza Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kuhakikisha zinatunga sheria ndogo ndogo kwa ajili ya uhifadhi vyanzo vya maji, barabara za mamlaka hizo na njia mbaya za kilimo zinazo athiri mazingira.

 Simbachawene ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Kibakwe aliyasema hayo  alipotembelea baadhi ya maeneo ya Mamlaka za Serikali za Mitaa wilayani Mpwapwa ambapo alitembelea kata ya Massa na Ruhundwa katika vijiji vya Mkoleko, Makose, Chogola, Winza, Njia Panda na Ikuyu na alijionea hali halisi ya maendeleo ya wananchi katika vijiji hivyo.

Aidha alibaini kuwapo kwa uharibifu mkubwa wa mazingira unaotokana na njia mbaya za kilimo katika kijiji cha Mkoleko na kumtaka Mkuu wa wilaya hiyo Bw. Jabir Shekimweri na timu ya wataalam wa wilaya kuchukua hatua za makusudi kunusuru hali ya mmomonyoko wa udongo unayotishia kutoweka kabisa kwa  kijiji hicho. 

“kamati ya huduma za Jamii ifanye kazi yake, mweke kontua na kuacha kulima na kukata miti katika kingo za makorongo ili kulinda mazingira” alisisitiza Simbachawene. Amewaasa wananchi kutumia fursa za ujio wa makao makuu ya nchi mkoani Dodoma kwa kulima mazao ya chakula na biashara kwani miundo mbinu ya lami kutoka Mbande kuja Kongwa, Mpwapwa, Gulwe hadi Kibakwe ujenzi wake unatarajiwa kuanza katika mwaka wa fedha 2017/2018.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George B.Simbachawene (MB) akifafanua juu ya kuanzisha ujenzi wa mradi wa maji ya uhakika wa kisima ambacho mkondo wake umepita chini sana, lakini pia alitoa agizo kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa kutunga sheria ndogo ndogo za matumizi bora ya ardhi na kutojenga au kulima karibu na barabara zinazopita katika maeneo yao.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George B.Simbachawene (MB) akikagua maendeleo ya Mradi wa kituo cha Afya katika kijiji cha Winza (Makao makuu ya kata ya Massa) ambapo asilimia kubwa ya mradi huo ipo katika hatua za mwisho, kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Mpwapwa Bw. Donald Ng’wenzi
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George B.Simbachawene (MB) ambaye pia Mbunge wa Kibakwe akikagua maendeleo ya Mradi wa kituo cha Afya katika kijiji cha Winza, mradi huo unatarajiwa kukamilika mapema mwakani.
 Mojawapo ya barabara inasimamiwa na Halmashauri ya wilaya ikiwa imetengenezwa vizuri na kuwezesha uchukuzi wa mazao, bidhaa na watu kuwa rahisi na kuchochea kasi ya maendeleo ya wananchi. Barabara hiyo inaungansha Kata za Massa, Ruhundwa, Rudi na Kibakwe na ipo wilayani Mpwapwa, pia ipo katika Mpango wa pili wa Taifa 2018/2019 kujengwa kwa kiwango cha lami. Awamu ya kwanza ni kutoka Mbande kuja Kongwa, Mpwapwa, Gulwe hadi Kibakwe unaotarajiwa kuanza mwaka wa fedha 2017/2018
  Sehemu ya ardhi katika kijiji cha Mkoleko, kata ya Massa iliyopo wilayani Mpwapwa ikiwa imeharibiwa vibaya kutokana na njia mbaya za kilimo, eneo lipo katika muinuko na limezungukwa na makorongo yanayopitisha maji kipindi cha masika hali inayosababisha uharibifu wa vyanzo vya maji na rasilimali misitu na mazingira.

Serikali ya Tanzania na Mauritius kuendeleza ushirikiano katika Sekta ya Sanaa na na Utamaduni.

$
0
0
 Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa,na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akipokea zawadi kutoka kwa Waziri wa Sanaa na Utamaduni wa Mauritius Mhe.Santaram Baboo baada ya mazungumzo baina yao kuhusu ushirikiano katika Sekta ya Sanaa na Utamaduni yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa,na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Wizara yake na viongozi wa Serikali ya Mauritius baada ya mazungumzo kuhusu ushirikiano katika Sekta ya Sanaa na Utamaduni yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel(aliyesimama) akiongea jambo wakati wa mazungumzo  kati ya Wizara yake na Serikali ya Mauritius katika  Sekta ya Sanaa na Utamaduni.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

WATUMISHI WOTE WA SERIKALI ZINGATIENI UHADILIFU KATIKA KAZI

$
0
0
Na Woinde Shizza,Arusha.

Watumishi wote wa Serikali wametakiwa kuzingatia uadilifu na uwajibikaji katika utendaji wao wa kazi.

Hayo yameelezwa na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Kassim Majaliwa Jana alipokuwa akiongea na watumishi wa wilaya na halmashauri ya Monduli Mara baada ya kuzindua wodi ya mama wajawazito ya hospital ya wilaya ya Monduli.

Aliwataka watumishi wote wa serikali kuzingatia uwadilifu,uwaminifu na uwajibikaji katika utendaji wao wa kazi ili dhana ya hapa kazi tu ichukue sehemu yake.

Majaliwa alisema Serikali ya awamu ya tano niyawawajibikaji,waadilifu katika sekta za umma .Amewataka watumishi wawasikilize,wawahudumie na kuwatumikia wananchi bila yakuweka ubaguzi wa aina yoyote ile.

Hii itasaidia kuonyesha matokea bora ya kila mtumishi kulingana na taaluma aliyonayo nakupelekea kuongeza ufanisi zaidi serikalini.Aidha amewataka viongozi wa halmashauri kusimamia fedha za miradi ya maendeleo zinazopelekwa na serikali na zikafanye shughuli ambazo zilipangiwa.


"Kila sekta katika halmashauri ihakikishe inapanga majukumu yake nakuyatekeleza kadri inavyopaswa"alisema Majaliwa.Aidha aliwataka wananchi kote nchini iwapo atataka Huduma n a kuhudumiwa vibaya asisite kutoa taarifa katika vyombo husika.

"Mwananchi yeyote ambae atapewa huduma vibaya na mtumishi wa serikali asisite kutoa taarifa sehemu husika ili mtumishi huyo aweze kuchukuliwa hatua Kali"alisema majaliwa.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitembelea Mradi wa umwagiliaji katika kijiji cha Jobag wilaya ya Karau ,mradi uliojengwa kwa ufadhili wa shirika la Worl Vision

NAIBU KAMANDA WA KAMANDI YA KIJESHI YA KUSINI MWA CHINA ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA JESHI JIJINI DAR LEO

$
0
0
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange (kulia), akimkabidhi nembo ya JWTZ, Naibu Kamanda wa Kamandi ya kijeshi ya Kusini mwa China luteni Jenerali Liu Xiaowu (kushoto),alipotembelea leo  Makao Makuu ya Jeshi, Upanga Dar es Salaam.

LIGI KUU VODACOM KUANZA KUTIMUA VUMBI DESEMBA 17, SIMBA NA YANGA FEBRUARI 18 MWAKANI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

LIGI kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea tena kwa duru la pili kuanzia Desemnba 17, huku timu zikishauriwa kukamilisha usajili kwa wakati huku Yanga na Simba kuumana Februari 18 2017..

Dirisha la usajili lililofunguliwa Novemba 15 linatarajiwa kufungwa Desemba 15 na timu zote zimeopewa mwongozo wa kutumia mfumo wa ule ule wa kutumia mtandao katika kuwasilisha majina hayo usiku wa Desemba 15.

Ofisa habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) Alfred Lucas amesema kuwa ligi inatarajiwa kuanza Desemba 17 kwa mechi nne kuchezwa kwenye viwanja tofauti nchini.

Lucas amesema kuwa kwa sasa ratiba hii imezingatia kalenda ya michezo ya kimataifa, kombe la mapinduzi na kombe la Shirikisho ilihali hawajaweza kuweka ratiba ya michezo ya kimataifa kwa timu zinazoshiriki michuano hiyo kwani ratiba ya Shirikisho la Mpira Afrika bado hawajaweka raiba wazi.

Katika ratiba hiyo, Kikosi cha Simba kitaanzia ugenini kuvaana Ndanda huku mabingwa watetezi Yanga wakiwa Uwanja wa Taifa kuumana na JKT Ruvu na Azam watakuwa ugeninio dhidi ya African Lyon.

Ofisa habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) Alfred Lucas

SERIKALI YATOA TAMKO KWA WACHIMBAJI WADOGO WA CHUMVI

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini prof,Jamse Mdoe (wa pili kushoto) akisomo mikakati mbalimbali ya serikali wakati akifungua akifungua mkutano wa chama cha wazalishaji chumvi wadogo,kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Wazalishaji Chumvi Habibu Nuru na viongozi wengine.

Na Anthony John Globu ya Jamii. 

SERIKALI imewataka wachimbaji wadogo wa chumvi kuhakikisha wanazalisha chumvi iliyo na ubora na yenye kiwango cha madini joto ilikuepuka madhara ya kiafya kwa watumiaji. 

Akizungumza leo hii Jijini Dar es salaam katika kufungua mkutano wa mwaka wa chama cha wazalashaji chumvi Naibu katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Prof, James Mdoe amesema Serikali inajitahidi kuboresha sheria za sekta ya wachimbaji wadogo na wazalishaji wa chumvi ilikuongeza uzalishaji wa mapato katika Taifa. 

Sambamba na hayo Mdoe alifafanua baadhi ya madhara ya kiafya kwa watumiaji chumvi isiyo na kiwango cha madini joto ni pamoja na kuharibu mimba na kuzaa watoto wenye ulemavu na madhara mengine ya kiafya. 

Katika uzinduzi huo wa wachimbaji wa chumvi, Prof. Mdoe alisema katika mwaka huu wa fedha 2016 hadi 2017 wizara yake itakamilisha kutengeneza kituo kimoja cha mfano wa mafunzo ya uzalishaji chumvi. Tumepanga kituo hicho kijwngwe katika wilaya ya Kilwa mkoani Lindi na kitakuwa ni kiwanda ambacho kina mchakato wote wa namna ya kuzalisha chumvi kwa ubora wa kimataifa.

Hivyo Hivyo Mwenyekiti wa chama hicho cha wachimbaji wadogo wadogo wa chumvi Habibu Nuru ameishukuru serikali kwa kuwasaidia tani 4 za madini joto pamoja na kilo miasaba zilizotolewa kwa wazalishaji hao ilikuweza kuboresha Chumvi.
Wadau mbalimbali walijitokeza kwenye mkutano huo.

WAZIRI MKUU ATEMBELEA MRADI WA UMWAGILIAJI KARATU

$
0
0
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitembelea Mradi wa umwagiliaji katika kijiji cha Jobag wilaya ya Karau, mradi uliojengwa kwa ufadhili wa shirika la World Vision.wakwanza kulia ni Mkurugenzi wa Miradi katika shirika hilo Revocatus Kamara.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitembelea Mradi wa umwagiliaji katika kijiji cha Jobag wilaya ya Karau ,mradi uliojengwa kwa ufadhili wa shirika la World Vision.

NDOTO YA MAMA MMOJA KITANDA KIMOJA INATIMIA –MAKONDA

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema ndoto ya mama mmoja kitanda kimoja itatimia endapo ujenzi wa Hospitali ya Mama na Mtoto inayojengwa Chanika kwa ushirikiano wa Shirika la Maendeleo la Korea Kusini na Mkoa wa Dar es Salaam utakamilika.

Makonda alisema ujenzi wa hospitali hiyo ni muda mwafaka kwa wanawake na watoto kuwa na uhakika wa kupata huduma ya afya.

Alisema hospitali hiyo inayojengwa itahudumia watu 1000 wa nje huku vitanda katika hospitali hiyo ni 160 kwa ajili ya akina mama na watoto.

Aidha alisema wananchi waendelelee kuunga mkono juhudi za Rais Dk. John Pombe Magufuli ya ulipaji kodi ili nchi iwe na uwezo hata kusaidia nchi nyingine kama wanavyofanya wa Korea.

Makonda alisema madaktari watakao kwenda katika hospitali hiyo watakuwa na makazi humo ili kuondoa usumbufu wa kusafiri kila siku.

Alisema serikali inawapenda wananchi wake kuhakikisha wanapata huduma ya afya bora hususani wanawake na watoto.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati mwenye miiwani) akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea Mradi wa Ujenzi wa Hospitali ya Mama na Mtoto ya Chanika leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipata maelezo kutoka kwa Meneja Mradi ujenzi huo, Bing Hunan leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akitembelea ujenzi wa hospitali hiyo leo jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

MSD YAZINDUA HUDUMA MAALUMU KWA WATEJA WAKUBWA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Na Dotto Mwaibale

BOHARI  ya dawa (MSD) imezindua mpango wa huduma maalumu kwa wateja wake wakubwa, kama moja ya hatua za kuboresha huduma kwa wateja. 


Mpango huo utawawezesha wateja hao kupata huduma ya haraka zaidi pindi wanapokuwa wanahitaji mahitaji yao.


Wateja hao ni pamoja na hosipitali ya Taifa ya Muhimbili, Taasisi ya Mifupa (MOI), Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, hosipitali ya Sekoutoure Mwanza, Hosipitali ya Kibong’oto, Mirembe, Hosipitaliza Amana, Temeke, Mwananyamala, KCMC, Hospitaliya Benjamin Mkapa na Taasisi ya Moyo ya JakayaKikwete.


Akizindua mpango huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee naWatoto Dk. Mpoki Ulisubisya amesema mpango huo ni moja ya maboresho yanayofanywa na MSD, ili kuhakikisha huduma zake zinatolewa kama inavyohitajika.


Dk. Mpoki pia amewasisitiza wateja hao wakubwa wa MSD kuhakikisha wanafanya maoteo sahihi ya mahitaji yao na kuyaleta MSD kwa wakati ilikuepusha ucheleweshwaji wa taratibu za manunuzi ambao pia tasababisha dosari kwenye upatikanaji wa dawa kwa wateja. 


Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu  amesema hatua ya kuwahudumia wateja hao kwa kiwango kizuri na cha uhakika itafanikiwa, hivyo Watarajie maboresho makubwa ya huduma. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee naWatoto Dk. Mpoki Ulisubisya (kulia), akizungumza na viongozi mbalimbali wa sekta ya afya wakati akizindua mpango wa huduma maalumu kwa wateja wakubwa Dar es Salaam leo asubuhi.
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)  Profesa Mohamed Janabi (kushoto), akizungumza katika hafla hiyo. 


Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu akizungumza kwenye mkutano huo.
Meneja Huduma kwa Wateja wa MSD, Salome Malamia akizungumza katika hafla hiyo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Waziri Nape afunga Mkutano Mkuu wa Waandishi wa habari za Mitandao 'Tanzania Bloggers Network' (TBN),ahidi kuanzisha tuzo.

$
0
0
 Na Beatrice Lyimo, Maelezo

Serikali inatarajia kuanzisha tuzo za umahiri kwa waandishi wa habari wa mitandao ya kijamii (blogs) nchini kuanzia mwaka 2017.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar  es salaam na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye wakati akifunga Mkutano Mkuu wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na semina ya wanachama wa umoja wa waendeshaji wa blog nchini.

Waziri Nape alisema kuwa lengo la tuzo hizo ni kuzisaidia blogs za Tanzania kubobea katika nyanja tofauti ikiwemo kilimo, mifugo, viwanda, hifadhi ya jamii kwa nia ya kuipa heshima tasnia ya habari nchini.

Aidha, Waziri Nape alisema kuwa tayari Serikali imeanza mazungumzo na   makampuni na taasisi mbalimbali kwa ajili ya kudhamini tuzo hizo ili kuhakikisha kuwa washindi wanapatikana kwa uwazi.

“Tuzo hizo zitakuwa za kwanza kwa namna zitakazovyoendeshwa kwa uwazi hivyo makampuni zaidi yanakaribishwa kuweza kuzidhamini mashindano hayo yatakayojielekeza kwenye nyanja tofauti” alisema Waziri Nape.

Waziri Nape pia alisema amewataka wamiliki na watendaji wa blogs nchini kushirikiana na Serikali ili kuweza kuijenga nchi.

“Tutumie fursa za kisiasa zilizopo, fursa za teknolojia ili kuhakikisha tiunajenga Tanzania tunayoitaka, ishaurini Serikali kwa kutumia taaluma mliyonayo ili kuweza kuipeleka nchi ya Tanzania tunayoitaka” alifafanua Waziri Nape.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akitoa Ufafanuzi wakati alipokuwa akieleza namna ya kuitambua mitandao ya Kijamii pamoja na uanzishaji wa Tuzo kwa Waendeshaji mitandao hiyo.
Waziri Nape alisema kuwa lengo la tuzo hizo ni kuzisaidia blogs za Tanzania kubobea katika nyanja tofauti ikiwemo kilimo, mifugo, viwanda, hifadhi ya jamii kwa nia ya kuipa heshima tasnia ya habari nchini.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye wakati akizungumza mapema leo jijini Dar wakati akifunga Mkutano Mkuu wa Tanzania Bloggers Network (TBN) iliokwenda sambamba na semina ya wanachama wa umoja wa waendeshaji wa blog nchini.Picha na Michuzi Jr.


Mwenyekiti wa Muda wa chama cha Waendesha mitandao ya Kijamii Tanzania Bloggers Network-TBN,Joachim Mushi akimkaribisha mgeni rasmi,Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kwa ajili ya kufunga mkutano huo na pia kuyotolea ufafanuzi baadhi ya mambo

.


Mmoja wa Wajumbe wa mkutano huo,Mzee John Kitime ambaye amebobea katika mambo ya Hakimiliki,akitoa elimu ya mambo ya Hakimiliki kwa washiriki wa mkutano huo.

Baadhi ya Waendeshaji wa mitandao hiyo wakiwa kwenye mkutano wao wa Mwaka wakifuatilia yaliyokuwa yanaendelea
Baadhi ya Wadau wakiendelea kusikiliza yaliyokuwa yakiendelea ukumbini humo.
Baadhi ya Waendeshaji wa mitandao hiyo wakiwa kwenye mkutano wao wa Mwaka wakifuatilia yaliyokuwa yanaendelea


RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN, KATIBU MKUU PAMOJA NA NAIBU WAZIRI WA TAMISEMI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemuagiza Waziri na Katibu Mkuu katika Ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kusitisha mara moja utekelezaji wa zoezi la kuwaondoa wafanyabiashara wadogo maarufu kwa jina la Machinga katika Jiji la Mwanza mpaka hapo mamlaka husika itakapokamilisha maandalizi ya maeneo watakapohamishiwa na kwa kuwashirikisha wamachinga wenyewe.


Rais Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa agizo hilo leo tarehe 06 Desemba, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam huku akionya kuwa kiongozi yeyote ambaye hayupo tayari kutekeleza agizo hilo aachie ngazi.


"Kumeibuka tabia ya Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kuwafukuza Wamachinga bila utaratibu wowote wa wapi wanawapeleka na wakati mwingine wanapelekwa maeneo ya mbali ambayo hayafai hata kwa kufanya biashara, hili jambo sio sawa hata kidogo.


"Sipendi Wamachinga wafanye biashara kwenye hifadhi ya barabara lakini hakuna sheria katika nchi hii inayosema mtu wa biashara ndogondogo au Mmachinga hatakiwi kukaa katikati ya mji, tukianza kwenda kwenye utaratibu wa namna hiyo maana yake tunaanza kutengeneza  madaraja ya Watanzania, kwamba kuna Watanzania fulani wa daraja fulani wanapaswa kukaa katikati ya mji na Watanzania wa daraja fulani hawatakiwi kukaa katikati ya mji, huo sio mwelekeo wetu na wala Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ambayo mimi na wewe (Makamu wa Rais) tulipita kuinadi, haisemi tutengeneze madaraja ya watu wanaostahili kukaa mjini na wengine hawastahili kukaa mjini, sasa nimeona hili nilizungumze na nataka kulirudia kwa mara ya mwisho"amesema Rais Magufuli.


Dkt. Magufuli ameelekeza kuwa Wamachinga waliondolewa katika maeneo yao Jijini Mwanza waachwe waendelee na shughuli zao mpaka hapo Halmashauri ya Jiji la Mwanza itakapokamilisha maandalizi ya mahali watakapohamishiwa na kwa kuwashirikisha Wamachinga wenyewe.


"Narudia na hii ni mara ya mwisho, kawaambieni hata Wamachinga wa Mwanza warudi kwenye maeneo yao mpaka watakapowatengenezea utaratibu mzuri, Kigamboni hapa palikuwa na wamachinga eneo fulani wamehama vizuri kweli, wakatengenezewa miundo mbinu yao katika soko lao na sasa hivi wanafanya kazi vizuri, na waliwashirikisha viongozi wa Wamachinga, lakini Mwanza imekuwa ni amri tu na wengine wanatumia hata msemo wa Hapa Kazi Tu, mimi sikusema msemo wa Hapa Kazi Tu wa namna hiyo, nadhani mmenielewa" amesisitiza Rais Magufuli alipokuwa akiwaekeleza Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Suleiman Jafo na Katibu Mkuu TAMISEMI Mhandisi Mussa Iyombe.


Wakati huo huo, Rais Magufuli ameagiza Wizara ya Nishati na Madini kusitisha mara moja zoezi la kuwaondoa wachimbaji wadogo katika Kijiji cha Nyaligongo kilichopo katika Kata ya Mwakitolyo Mkoani Shinyanga na badala yake wachimbaji hao waachwe waendelee na shughuli zao, na leseni ya mwekezaji anayedai eneo hilo ni lake aondolewe.


"Wale waliofukuzwa Shinyanga wabaki palepale, kama ni leseni ya huyo mwekezaji ifutwe, Mhe. Makamu wa Rais fuatilia hili, mweleze Waziri wa Nishati na Madini, waache kufukuza wananchi hovyohovyo, wale wanapata riziki yao, wanasomesha watoto wao lakini wanafukuzwa tu."Na hizi ndio ajira zenyewe, tulisema tunatengeneza ajira, wewe mwekezaji ni mmoja unakwenda kuwafukuza watu 5,000? haiwezekani na wala haingii akilini"amesisitiza Rais Magufuli.


Rais Magufuli amekemea vitendo vya wawekezaji wakubwa kupewa maeneo ambayo wachimbaji wadogo wanaendesha shughuli zao tena kwa mtindo kwa kutengeneza nyaraka zinaonesha mwekezaji husika alipewa eneo hilo kabla ya wachimbaji wadogo na kusisitiza kuwa mchezo huo hautavumiliwa.


Hata hivyo Rais Magufuli amesema maagizo yake hayana maana kuwa Wamachinga na Wachimbaji wadogo waendeshe shughuli zao kwa kuvunja sheria bali wazingatie sheria na Mamlaka zisiwanyanyase watu wanyonge





Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

06 Desemba, 2016.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwakaribisha Naibu Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo aliyeambatana na Katibu Mkuu wa TAMISEMI Mhandisi Mussa Iyombe  kabla ya kuanza kwa kikao chao cha pamoja na Makamu wa Rais  Samia Suluhu Hassan.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika kikao cha pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Naibu Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo pamoja na  Katibu Mkuu wa TAMISEMI Mussa Iyombe.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na  Makamu wa Rais Samia Suluhu mara baada ya kutoka kwenye kikao cha pamoja kilicho wahusisha Naibu Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo pamoja na  Katibu Mkuu wa TAMISEMI Mussa Iyombe Ikulu jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mara baada ya kumaliza kikao chao kilicho wahusisha Naibu Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo pamoja na  Katibu Mkuu wa TAMISEMI Mussa Iyombe Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

WATEJA WA DCB KUNUFAIKA NA KAMPENI ZA BORESHA MAISHA NA PATA FAIDA

$
0
0
Meneja mwandamizi wa Shughuli za Kibenki DCB Samwel Dyamo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kampeni ya boresha maisha na DCB pamoja na Pata faida na DCB itakayoanza kuchezwa kwa droo ya kwanza Desmba 17, Kushoto ni Meneja Masoko Boyd Mwaisame.


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

BENKI ya DCB imedhamiria kuendelea kuwa kuwajali wateja wake imeanzisha kampeni ya "boresha maisha na DCB" na " Pata faida na DCB" itakayoanza Desemba 17 kwa ajili ya kuwazawadia zawadi mbalimbali pamoja na fedha taslimu kwa wateja wapya na wa zamni.

Akizungumzia kampeni hiyo, Meneja mwandamizi wa Shughuli za Kibenki DCB Samwel Dyamo amesema kampeni boesha maisha na DCB na Pata faida na DCB itadumu kwa miezi mitatu na kila mwezi kutakuwa na droo moja itakayotoa washindi watatu wa fedha taslimu laki mbili,

Dyamo amesema kuwa mbali na fedha taslimu kutakuwa na washindi wengine wawili watakaopata simu za mkononi na washindi 20 watapata kila mmoja na watatangazwa mbele ya waandishi wa habari na kukabidhiwa zawadi zao.

Droo ya kwanza itachezeshwa Desemba 17 na itamalizika Februri 17 na wateja wanatakiwa kuweka fedha mara kwa mara kwenye akaunti mojawapo ya akiba binafsi, akaunti ya watoto na akaunti ya WAHI kiasi cha kuanzia sh 50,000/= na kuendelea na kuongeza amana mara mbili zaidi ya sh 500,000.

Dyamo amesema kuwa, mteja atakayeweka fedha hizo ataingia moja kwa moja kwenye droo hizo, mbali na kampeni hiyo pia kutakuwa na kutakuwa na Pata faida na DCB itakayokuwa inawapa faida wateja kwa kuwekeza nkupitia huduma yetu ya akaunti ya muda mrefu (fixed account) kwa kuweka kiais cha milioni 50 na kuendelea kwa kipindi cha mwaka mmoja na watapata faida ya asilimia 15 ya fedha zako.

Alisisitiza kuwa, hata kama utaziweka fedha zako kwa kipindi cha miezi sita bado utaendelea kufaidika zaidi na kuwataka kujitokeza kwa wingi hususani kwa wajasiramali, watu binafsi na taasisi mbalimbali.

Meneja wa matawi wa  DCB, Haika Machaku amewataka watanzania kujiunga na benki yao kwani asilimia kubwa ya faida inaenda kwa wananchi kwa ajili ya miradi mbalimbali.
Meneja wa matawi wa  DCB, Haika Machaku akizungumza na waandishi wa habari juu ya umuhimu wa wananchi kujiunga na benki yao ili kuweza kufaidika zaidi.
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images