Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109581 articles
Browse latest View live

SERIKALI YAJIPANGA KUREKEBISHA SERA NA SHERIA ZA KODI.

0
0


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejipanga kurekebisha Sera na Sheria za kodi ili kuwasaidia wafanyabiashara na wajasiliamali kupata thamani ya shughuli wanazozifanya.

Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizindua Mkutano wa Chama cha Wasindikaji wa Vyakula nchini (TAFOPA) uliofanyika katika ukumbi wa Mwl. Nyerere uliopo Jijini humo.Mama Samia amesema kuwa wafanyabiashara na wajasiliamali nchini wamekuwa wakilalamikia ongezeko la kodi katika bidhaa mbalimbali wanazozizalisha hadi kupelekea kushindwa kuona faida ya shughuli hizo hivyo ni muhimu kwa Serikali kusikiliza kilio chao kwa kutafuta namna bora itakayomaliza tatizo hilo.

“Serikali ya Awamu ya Tano imeliona tatizo hilo na imeahidi kulifanyia kazi kwa kuzipitia upya sheria hizo na kuzifanyia marekebisho ili kila mwananchi atoe kodi bila kinyongo na apate faida ya shughuli anayoifanya,”alisema Mama Samia.Amezitaja changamoto zingine ambazo Serikali itazifanyia kazi ni kujenga miundombinu katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya wajasiliamali, kupunguza muda wa upatikanaji wa leseni za biashara pamoja na kuhakikisha Mamlaka ya Serikali za Mitaa inatenga maeneo kwa ajili ya wajasiliamali hao.

Kwa upande wake Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema kuwa jambo analojivunia katika uongozi wake ni kuweza kuwahamasisha Watanzania kuelewa ujenzi wa uchumi wa viwanda ambapo kwa sasa nchi nzima wanazungumzia habari hiyo.“Asilimia kubwa ya wananchi wanazungumzia namna ya kuanzisha viwanda kama sehemu ya kujipatia kipato na ndio maana mikutano ya wajasiliamali imekua ikiongezeka siku hadi siku, hii inaonyesha dhahiri kuwa watanzania wameamua kushirikiana na Serikali katika kuinua uchumi wa nchi kupitia viwanda,”alisema Mwijage.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha TAFOPA, Susan Laizer amefafanua kuwa maeneo yatakapotengwa yatasaidia kupunguza uharibifu wa mazao ya chakula yanayovunwa wakati wa msimu husika pia yatatoa ajira nyingi kwa wananchi watakaokuwa wakifanya shughuli za uzalishaji katika maeneo hayo.“Tunaiomba Serikali yetu itusaidie kutenga maeneo kwa ajili ya shughuli zetu hadi kwenye sehemu za vijiji ili wakulima wapate soko la bidhaa zao kwa urahisi pamoja na kuepuka madalali wanaozorotesha vipato vyao,”alisema Bi. Susan.

Aidha, Bi Susan amempongeza Mama Samia kwa kuteuliwa na Umoja wa Mataifa kuwa mjumbe wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika kwenye jopo la kuwawezesha wanawake kiuchumi kwani ni sifa kwa Taifa na fursa kwa wasindikaji wote nchini.Chama hicho kimeanzishwa rasmi mwaka 1977 baada ya wanawake kupata mafunzo ya usindikaji wa vyakula yaliyotolewa na Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo Tanzania (SIDO) ikishirikiana na Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo Duniani (UNIDO). 

TRA YASHINDA TUZO YA UTUNZAJI BORA WA MAHESABU KWA TAASISI ZA UMMA

0
0
Na Ally Daud-MAELEZO

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imeshinda tuzo ya utunzaji bora wa mahesabu kwa taasisi za umma  zilizoandaliwa na   Bodi ya Ukaguzi na Wahasibu (NBAA) kwa mwaka 2015.



Akipokea tuzo hiyo Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Fedha (TRA) Bi. Anna Mndeme amesema kuwa wamepata tuzo hiyo kutokana na  kuwasilisha vizuri mahesabu ya mwaka wa fedha yaliyowasilishwa kufuatana na viwango vya uwasilishwaji  vinavyozingatiwa na Bodi ya Ukaguzi na Wahasibu (NBAA).



“Tumefanya vizuri na tumepata tuzo kwa kushika nafasi ya kwanza kutokana na  kuwasilisha vizuri mahesabu ya mwaka wa fedha yaliyowasilishwa kufuatana na viwango vya uwasilishwaji  vinavyozingatiwa na Bodi ya Ukaguzi na Wahasibu (NBAA)” alisema Bi. Mndeme.



Aidha Bi. Mndeme amesema kuwa tuzo hiyo ni chachu kwa TRA itayofanya waendelee kujituma zaidi katika ukusanyaji na utunzaji wa mapato ili kusaidia nchi kupata huduma bora za jamii kwa maendeleo ya taifa.



Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi TRA Bw. Richard Kayombo amesema kuwa huo ni uthibitisho kwamba TRA inafanya kazi  kwa ueledi na uwazi kupelekea kupata tuzo ya heshima.

Katika mashindano hayo Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) wameibuka washindi wa pili huku kampuni inayotengeneza Sementi  (Tanga Cement Plc) wakiibuka kuwa washindi wa jumla kwenye tuzo hizo .

 Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Fedha (TRA) Bi. Anna Mndeme kulia akipokea tuzo ya utunzaji bora wa mahesabu kwa taasisi za umma  kutoka kwa Mwakilishi wa Mhasibu Mkuu wa Serikali  Bw.Shogolo Msangi katikati  wakati wa sherehe za kukabidhi tuzo hizo kwa  wawasilishaji bora wa mapato kwa mwaka 2015 yaliyofanyika nje kidogo ya jiji la Dar es salaam wa kwana kushoto ni Mwenyekiti wa NBAA Prof. Isaya Jairo.

 Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt.Ayoub Rioba kulia akipokea tuzo ya utunzaji bora wa mahesabu kwa taasisi za umma baada kuwa mshindi wa pili  kutoka kwa kwa Mwakilishi wa Mhasibu Mkuu wa Serikali  Bw.Shogolo Msangi kushoto  wakati wa sherehe za kukabidhi tuzo hizo kwa  wawasilishaji bora wa mapato kwa mwaka 2015 yaliyofanyika nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.

 Afisa Mkuu wa Mapato kutoka kampuni ya kutengeneza sementi (Tanga Cement Plc) Bw. Pieter De Jager wa pili kulia akiwa ameshika tuzo ya washindi wa jumla kwenye masindano ya wawasilishaji bora wa mapato kwa mwaka 2015 yaliyofanyika nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.

 Mwakilishi wa Mhasibu Mkuu wa Serikali  Bw.Shogolo Msangi katikati waliokaa  akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa uwasilishaji bora wa mapato  wakati wa sherehe za kukabidhi tuzo hizo kwa mwaka 2015 iliyofanyika nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.


Picha Na Ally Daud-Maelezo

MAJALIWA AITEMBELEA FAMILIA YA MAREHEMU SKOINE MONDULI JUU

0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na  Napono Sokoine (wapili kulia) na  Nekiteto Sokoine (kulia) ambao ni  wajane wa aliyekuwa Waziri Mkuu, Marehemu Edward Sokoine wakati aipokwenda nyumbani kwa marehemu, Monduli Juu kuisalimia familia akiwa katika ziara ya wilaya  ya Monduli  leo Desemba 4, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliekuwa Waziri Mkuu, Edward Sokoine wakati alipokwenda nyumbani kwa marehemu, Monduli Juu akiwa katika ziara ya wilaya ya Monduli leo
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipokwenda nyumbani kwa  aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Sokoine, Monduli Juu kuisalimia familia akiwa aktika ziara ya wilaya  ya Monduli Desemba 4, 20, 16.  Kushoto kwake  wajane wa marehemu, Napono Sokoine (wpili kulia) na kulia ni  Nekiteto Sokoine . Kulia kwake  ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipokwenda nyumbani kwa  aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Sokoine, Monduli Juu kuisalimia familia akiwa aktika ziara ya wilaya  ya Monduli Desemba 4, 20, 16.  Kushoto kwake  wajane wa marehemu, Napono Sokoine (wpili kulia) na kulia ni  Nekiteto Sokoine . Kulia kwake  ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.(Picha na Ofisi ya Wziri Mkuu)

Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 14 kuanza kambi

0
0
Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Vijana wa Tanzania wenye umri wa chini ya miaka 14, leo Desemba 4, 2016 inaanza kambi rasmi katika Hosteli za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Vijana hao 22, wanaingia kambini kujiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Shelisheli unaotarajiwa kufanyika Desemba 17, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mchezo huo ambao una baraka za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), umepangwa kufuata taratibu zote za kimataifa ikiwa ni pamoja na kupigiwa Nyimbo za Taifa kwa timu zote sambamba na kupandisha Bendera za Mataifa husika.

Kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu wa timu ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 14, Oscar Mirambo anayepata ushauri kutoka kwa Mshauri Mkuu wa Maendeleo ya Soka la Vijana, Kim Poulsen kinatarajiwa kuwa na michezo minne ya kirafiki ya nyumbani kabla ya kucheza na Shelisheli.



DEATH ANNOUNCEMENT OF LEO MAPUNDA MWAKITALU IN FLORIDA, USA

0
0
It is with our deepest sorrow that we, Tanzanians living in Columbus, Ohio inform you of the death of our beloved brother Leo Mapunda Mwakitalu (pictured), who died on  Saturday December 03, 2016 of complications from chemo treatment at Halifax Hospital in Daytona Beach, Florida.

We are working closely with the deceased's family, friends and the Tanzania community at large on fundraising and plants to transport his body for funeral in Tanzania. We are counting on your moral and material support. More details to come. 







Please, feel free to reach out to the following for addional information;



(518) 961-2098 William Mwandambo
(614) 378-8655 Deo Mwalujua
(301) 806-3989 Lusajo Kibonde
(614) 806-9436 Abraham Aziz
(614) 843-6658 Andrew Mapunda
(614) 806-7636 Immanuel Lyatuu
(614) 364-6778 Kenan Haonga
(623) 225-9614 Liston Kayila
(214) 830-9906 Prosper Kiswaga
(301) 433-1048 Tumaini Katule
(413) 219-7055 Christian                                                                                                      Mwakapusya
                                                                          +255754281726 Isakwisa Kalinga

Please, keep Leo's family in your 
thoughts and prayers in this difficult time.

                                                                  Amen.

RAIS WA ZANZIBAR DKT SHEIN ATEMBELEA MAJENGO MAPYA YA ZIMAMOTO UWANJA WA NDEGE

0
0

Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameeleza kuridhika kwake na ujenzi wa ofisi za Zimamoto alizoagiza kujengwa ndani ya miezi miwili katika ziara yake aliyoifanya Oktoba 4 mwaka huu huko katika eneo la uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume. 
Dk. Shein alitoa agizo hilo mara baada ya kutembelea eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya Zimamoto huko katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, mnamo Oktoba 4 mwaka huu ambapo ujenzi huo ulionekana kusuasua kwa muda mrefu lakini leo ameeleza kuridhika na ujenzi huo. 
Katika maelezo yake mara baada ya kukagua jengo la ofisi hizo Dk. Shein alisema kuwa alipongeza hatua za ujenzi zilizofikiwa na kupongeza kwa kazi nzuri iliyofanywa licha ya kuwa imo katika hatua za ukingoni kumaliza.


“Niliahidi miezi miliwi iliyopita kuwa nitakuja kuangalia ujenzi wa jingo hili lakini leo nimekuja kwa furaha, kazi nzuri imefanyika na nimeridhika kwa kuona pamoja na maelezo mliyonipa ya asilimia ya hatua za ujenzi, hongereni sana”,alisema Dk. Shein. 
Aidha, Dk. Shein alisema kuwa ni matumaini yake makubwa kutokana na kasi ya ujenzi inavyokwenda si zaidi ya wiki mbili zijazo kazi hiyo itakuwa imemaliza kabisa. 
Dk. Shein alipongeza kwa mashirikiano makubwa yaliofanyika kati ya taasisi husika na kupelekea ujenzi huo kukamilika kwa wakati muwafaka kutokana na mipango mizuri waliyoifanya na kuitekeleza.


Alisema kuwa mradi wa ujenzi huo umejenga uzoefu mkubwa kwa taasisi husika katika masuala mazima ya kujenga kwa kujipangia taratibu zao wenyewe za ujenzi kama alivyoagiza ambazo zinaepusha matumizi makubwa ya fedha. 
Dk. Shein alieleza kuvutiwa kwake na ujenzi huo pamoja na sehemu muhimu zilizomo ndaji ya jingo hilo ambazo zinatoa fursa nzuri kwa wafanyakazi wa Zimamoto kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi kwani mambo yote yanayohitajika yamo ndani ya jengo hilo. 
Alisema kuwa ameridhishwa na ofisi zilizomo ndani ya jingo hilo, vyumba vya wafanyakazi wa kike na kiume, vyoo pamoja na stoo kwa ajili ya kuhifadhia vifaa vya shughuli za zimamoto. 
Pamoja na hayo, Dk. Shein alisisitiza haja ya kufanya kazi kwa mashirikiano ya pamoja na kuepuka mivutano ambayo haina tija katika utendaji wa kazi.


Pia, Dk. Shein alieleza matarajio ya ujio wa gari nne za zimamoto zinazotarajiwa kuwasili hivi karibuni ambazo mbili zimenunuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na mbili zimenunuliwa kutokana na mkopo wa fedha za Benki ya Dunia ambazo zinatoka nchini Afrika ya Kusini na Dubai. 
Sambamba na hayo, Dk. Shein alitumia fursa hiyo kueleza azma ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kuendelea kuwathamini watendaji wake katika sekta za umma ambapo tayari katika uongozi wake wafanyakazi wa sekta za umma wameshapandishiwa mishahara mara tatu mnamo mwaka 2011,2013 na 2015. 
Hata hivyo Dk. Shein alisema kuwa Serikali imo katika taratibu za kuangalia upandishaji wa madaraja kwa wafanyakazi hao wa sekta za umma kwa ngazi tofauti huku akisisitiza azma yake kwa vikosi vya SMZ kupata maslahi yanayolingana na yale ya vikosi vya SMT. 
Nae Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Haji Omar Kheri alimueleza Dk. Shein alitoa pongezi na shukurani kwa watendaji wa taasisi zote husika kwa kazi hiyo nzuri iliyofanywa na kutekeleza agizo lililotolewa na Rais kwa ufanisi mkubwa na hatua iliyobaki na ni kitaalamu. 
Kamishna wa Idara ya Zimamoto Zanzibar Ali Abdalla Malimosi nae alitumia fursa hiyo kumueleza Dk. Shein hatua zilizofikiwa katika ujenzi huo na kuwapongeza mafundi wa ujenzi huo huku akiwaahidi kuwapandisha daraja mafundi hao kutoka Idarani kwake waliojenga jengo hilo.


Mapema akiwa katika ukumbi wa wageni maalum wa uwanja wa ndege mkongwe wa Abeid Amani Karume, Dk. Shein alipata maelezo ya ukamilishaji wa ofisi hizo kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar, Abdulghani  Himid Msoma ambapo alieleza kuwa ujenzi huo umefikia  kiwango kisichopungua asilimia 92 ya kazi zote.


Musoma akiyataja maeneo matano yaliolengwa katika kutekeleza kazi hiyo ni pamoja na ukarabati mkubwa wa banda kongwe na kuligeuza kuwa jengo kubwa la kituo cha Zimamoto kilichotimia kwa mujibu wa mahitaji kamili ya kazi za Zimamoto. 
Aidha, ukarabati wa ofisi ndogo kwa ajili ya huduma za utawala, uimarishaji wa kituo kilichopo hivi sasa kwa kujenga kutumika kuwa ‘satellite post’, kusafisha bwawa na kukamilisha miundombinu ya maji na kuweka miundombinu ya kudumu ya umeme. 
Mwenyekiti huyo wa Bodi alisema kuwa kukamilika kwa mradi huo kumeleta mafanikio makubwa kwa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar, kwa vile uwanja umepata kituo cha Zimamoto cha kudumu kinacholingana na hadhi ya uwanja wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.


Kwa maelezo ya Mwenyekiti huyo, kazi hiyo ya ujenzi huo inatarajiwa kugharimu Tsh. Milioni 335 ambapo hadi sasa asilimia 92 zimetumika ambazo ni milioni 310 fedha zote hizo zimetolewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar.


Dk. Shein alimalizia ziara yake hiyo kwa kuangalia kituo kidogo cha Zimamoto ambacho kinatarajiwa kuwepo ndani ya eneo la uwanja wa ndege kama ilivyo kwa viwanja vyengine va kimataifa ambacho kinaendelea kufanyiwa ukarabati mkubwa.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Kamishana wa Kikoso cha Zima Moto Zanzibar Abdalla Malimosi wakati alipokuwa akiaangalia picha za magari mapya ya kikosi hicho yanayotarajiwa kuwasili hivi karibuni,wakati alipotembelea ujenzi wa majengo mapya ya kikkosi hicho leo huko katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Wilaya ya Magharibi "A"Unguja
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akizungumza na Viongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar na Uongozi wa Kikosi cha Zima Moto na Uokozi, wakati alipofika kutembelea ujenzi wa majengo mapya ya kikosi hicho leo
 Jengo hili kama linavyoonekana baada ya kumalizika  Ujenzi wake  ambapo Kikosi cha Zimamoto na Uokozi   itakuwa ni Ofisi ya Kikosi hicho.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akiangalia baadhi ya Vyumba vya Ofisi mpya ya Kikosi cha Zimamoto na Uokozi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume huko Kisauni Wilaya ya Magharibi "A"Unguja leo,(wa pili kulia)Kamishna wa Kikosi hicho Abdalla Malimosi na SACF Simai Haji Simai

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Kamishna wa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Abdalla Malimosi wakati  alipotembelea kituo kidogo kinachofayiwa matengenezo katika Uwanja wa  Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume   akiwa katika ziara maalum leo,(kushoto) Naibu Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji Mhe,Mohamed Ahmed Salum,(wa pili kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe,Haji Omar Kheri. Picha na Ikulu.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

FIBER BOAT 25 FEET WITH BRAND NEW YAMAHA 40HP ENGINE & TRAILER FOR IMMEDIATE SALE

0
0
  FIBER BOAT 25 FEET WITH BRAND NEW YAMAHA 40HP ENGINE & TRAILER FOR IMMEDIATE SALE  
-- CONTACT 0772342058 

Mahafali ya 10 ya Chuo Kikuu cha Ardhi yafana

0
0
 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi, Prof. Idrissa Mshoro akiwasili katika viwanja vya chuo hicho kwa ajili ya kuhudhuria katika mahafali ya 10 ya chuo hicho yaliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam.
 
 Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi, Mhe. Cleopa Msuya akimtunuku mmoja wa wanafunzi wa shahada ya Udaktari wa Falsafa (PhD) aliyoipata katika chuo hicho. Mahafali hayo yamefanyika jana Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya chuo hicho.
 Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi, Mhe. Cleopa Msuya (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine waliohudhuria kwenye mahafali ya 10 ya chuo hicho akiwemo Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la chuo hicho, Prof, Evelyne Ambede (wa pili kushoto), wa tatu kulia ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhandisi Stella Manyanya. Mahafali hayo yamefanyika jana Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya chuo hicho.
 
 Baadhi ya wahitimu shahada ya Udaktari wa Falsafa (PhD)   katika chuo hicho wakiwa katika viwanja vya chuo. Mahafali hayo yamefanyika jana jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wanafunzi wa shahada na stashahada waliohitimu katika chuo hicho wakiwa katika viwanja vya chuo. Mahafali hayo yamefanyika jana jijini Dar es Salaam. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA


Mamia wamuaga Mzee Mzimba, azikwa kijijini kwake Msoga

0
0


Mwili wa Marehemu Mzee Yusuph Mzimba ukisafirishwa kwenda Msoga Chalinze kwa maziko. Kwa mujibu wa mtoto wa Marehemu, Bw. Kampira, amesema kuwa Rais mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwaongoza waombolezaji katika maziko yatakayofanyika katika makaburri ya Familia uko kijiji kwake.
 Kisomo katika  msiba wa Mzee Yusuph Mzimba huko Magomeni Kwa Bi Nyau  jijini Dar es salaam kabla ya mwili wake kuswaliwa na kisha kupelekwa kijijini kwake Msoga, Chalinze, Mkoa wa Pwani kwa Mazishi leo Desemba 4, 2016.
 Mzee Ibrahim Akilimali akimzungumzia  marehemu Yusuf Mzimba huko Msoga kabla ya Mazishi.
 Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Bw. Imani Madega wakiwa msibani Msoga. Kushoto kwake ni Rais wa TFF Bw. Jamal Malinzi na kulia kwake ni Mzee Ibrahim Akilimali na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Majid Mwanga (kushoto)
 Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili  msibani kijini Msoga
Waombolezaji wakimalizia mazishi ya Mzee Yusufu Mzimba katika makaburi ya familia yake kijini Msoga jioni hii.
Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

RAIS DKT. MAGUFULI AWAONYA WANAOTAKA KUWACHAFUA VIONGOZI WASTAAFU

MFUKO WA LAPF KWA MARA NYINGINE WAIBUKA KIDEDEA KATIKA UTUNZAJI WA MAHESABU NCHINI

0
0


Na Dotto Mwaibale

MFUKO wa Pensheni wa LAPF, umetunukiwa tuzo ya kuwa kinara katika utunzaji  wa mahesabu dhidi ya mifuko mingine ya hifadhi ya jamii nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam juzi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo, Elyudi Sanga baada ya kupokea tuzo hiyo, Mkurugenzi wa Fedha wa mfuko huo, John Kida, alisema kwao ni mafanikio makubwa kwa kupata tuzo hiyo.

"Tunatumia njia za kisasa ya utunzaji wa mahesabu huku tukifunga mahesabu yetu kwa wakati jambo linalotupa fursa ya kuweka sawa mambo yetu ya mahesabu" alisema Kida.Alisema wamekuwa wakifunga mahesabu yao kwa kiwango cha kimataifa ndio maana wamekuwa wakiibuka washindi mara nyingi.

Kida alisema kuwa ushindi huo ni wa mara ya nane tangu kuanzishwa kwa utoaji wa tuzo hizo mwaka 2008.Meneja Masoko na Mawasiliano wa LAPF, James Mlowe, alisema kuwa wanachama wao wanatakiwa kuendelea kuwa na imani na mfuko wao na kuwa fedha zao zipo kwenye mikono salama.

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Pius Maneno, alisema makampuni na taasisi 56 zilishiriki katika mashindano hayo kwa  mwaka huu ambapo waligawanywa katika makundi 12 kulingana na huduma wanazozitoa.

Alisema tuzo hizo zina lengo la kuongeza uwazi na uwajibikaji katika suala zima la mahesabu na kuhakikisha viwanago vya kimataifa vinazingatiwa katika utunzaji wa mahesabu.Aliwataka wahasibu nchini kuandaa taarifa bora za fedha ili kuboresha hesabu za mashirika na makampuni na kuongeza uwazi katika shughuli zao.

Tuzo hizo ziliandaliwa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) na zilitolewa juzi katika Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (ACP) kilichopo Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa LAPF, John Kida (katikati mwenye tuzo), akiwa na wafanyakazi wenzake baada ya kutunukiwa tuzo ya Utunzaji Bora wa Mahesabu Dar es Salaam juzi. Kushoto ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa LAPF, James Mlowe.
 Mgeni rasmi katika hafla hiyo akisoma hutuba kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Profesa Isaya Jairo na katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa NBAA, Pius Maneno.
 Mkurugenzi Mkuu wa NBAA, Pius Maneno (kushoto), akimpongeza Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa LAPF, John Kida baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi NBAA. Profesa Isaya Jairo.
 Wafanyakazi wa Mfuko wa LAPF wakipita meza kuu baada ya kutunukiwa tuzo hiyo.
Washindi wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi na viongozi wa NBAA.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU DEC 5

BLOGGER SHAMIM MWASHA ASHINDA TUZO YA BLOG BORA YA MITINDO KATIKA SWAHILI FASHION WEEK 2016

0
0
Blogger nguli wa  Mitindo hapa nchini, Shamim Mwasha akipokea tuzo yake baada ya Blog yake ya 8020 Fashions kuwa Bora katika nyanja ya Mitindo, katika Usiku wa kumkia leo katika  Swahili Fashion Week 2016 ukumbi wa Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni  Jijini Dar es salaam.


LILLIAN NDANSHAU ASHINDA TUZO YA MBUNIFU CHIPUKIZI BORA KATIKA SWAHILI FASHION WEEK 2016

0
0
Mbunifu wa mavazi  anayekuja juu kwa kasi Lillian Ndanshau akifurahia baada ya kupokea  tuzo yake ya  Mbunifu Chipukizi Bora wa Mwaka  katika Swahili Fashion Week 2016, iliyotolewa na Kampuni Kongwe ya  Mavazi hapa nchini ya Khimji katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo.


SWAHILI FASHION WEEK YAFIKA TAMATI, MARTIN KADINDA AIBUKA MBUNIFU BORA WA MWAKA

0
0
Muandaaji wa Tamasha la Kimataifa la Maonyesho ya Mitindo ya mavazi la "Swahili Fashion Week" ambaye pia Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya 361, Mustafa Hassanali akizungumza kabla ya kukabidhi tunzo kwa Mbunifu Bora wa Mwaka 2016, iliyokwenda kwa Mbunifu Kijana, Martin Kadinda, ikiwa ni siu ya mwisho ya Tamasha hilo kwa Mwaka huu, lililoanza rasmi Desemba 2 - 4, 2016 katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar es salaam.
Muandaaji wa Tamasha la Kimataifa la Maonyesho ya Mitindo la "Swahili Fashion Week" ambaye pia Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya 361, Mustafa Hassanali akimkabidhi tuzo ya Mbunifu Bora wa Mwaka 2016, Mbunifu Martin Kadinda baada ya kuibuka kinara katika nyanja hiyo, katika Usiku wa mwisho wa Tamasha la Kimataifa la Maonyesho ya Mitindo ya mavazi la "Swahili Fashion Week" , lililomalizika usiku huu katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Mavazi yaliyobuniwa na Martin Kadinda.



















MAJALIWA AHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA MTO WA MBU

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye kijiji cha Mto wa Mbu wilayani Monduli akiwa katika ziara ya mkoa wa Arusha Desemba 4, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa ameshika ngao na Mkuki alivypewa na  Mzee wa Mila wa kabila la Wamasai, Laibon Meshuko Ole Mapii (kulia) kabla ya kuwahutubia wananchi kwenye shule ya msingi ya Laibon iliyojengwa na Laibon  Ole mapii na kukabidhiwa kwa serikali. Alikuwa katika ziara ya wilaya ya Monduli Desemba 4, 2016. Wengine pichani kutoka kushoto ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa, Jumanne  Maghembe, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Arusha, Lekule Laiza.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mzee wa mila wa Kabila la Wamasai, Laibon Meshuku Ole- Mapii  kabla ya kuzungumza na wananchi kwenye shule ya Misingi ya Laibon iliyojengwa na Ole- Mapii na kukabidhiwa kwa serikala. Alikuwa katika ziara ya wilaya ya Monduli Desemba 4, 2016.
 Baadhi ya wananchi wa  Mto wa Mbu wilayani Monduli wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara kijijini hapo akiwa katika ziara wilayani humo Desemba 4, 2016.
Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Maliasili na Utlii, Profes Jumanne Maghembe baada ya kuwahutubia wananchi kwenye shule ya msingi ya Laibon wilayani Monduli  Desemba 4, 2016. Katikati ni Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Zantel yamwaga ofa kibao mjini Tanga

0
0
Mkuu wa Mauzo wa Zantel Tanzania, Herbert Louis (kulia), akiwaonyesha baadhi ya wakazi wa mji wa Tanga kupitia simu ya mkononi jinsi mtandao wa kasi  wa 4G wa kampuni hiyo unavyofanya kazi pamoja na baadhi ya bidhaa, hudumana ofa maalumu  kwa ajili ya mji wa Tanga. Hafla hiyo ikiwa ni moja ya kampeni za masoko kufikisha huduma na bidhaa zao karibu na wateja ilifanyika katika Viwanja vya Tangamano mjini humo hivi karibuni.
Ofisa Masoko wa Zantel, Deus Mtena (kulia), akizungumza na baadhi ya wakazi wa mji wa Pongwe nje kidogo ya Jiji la Tanga jana kuhusu huduma, bidhaa na ofa maalumu kwa mji wa Tanga  ikiwa ni moja ya kampeni za masoko kufikisha huduma na bidhaa zao karibu na wateja.
Ofisa Masoko  Masoko wa Zantel, Emmiliana Vokolavene (wa pili kulia), akizungumza na baadhi ya wakazi wa mji wa Pongwe nje kidogo ya Jiji la Tanga jana kuhusu huduma, bidhaa wazitoazo na ofa maalumju kwa ajili ya Tanga  ikiwa ni moja ya kampeni za masoko kufikisha huduma na bidhaa zao karibu na wateja. 

BLOGGERS TANZANIA WAPEWA MAFUNZO YA NAMNA BORA YA UENDESHAJI WA MITANDAO YA KIJAMII

0
0


Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO, Dk. Hassan Abbas (wa pili kulia) akizungumza wakati wa kufungua mkutano mkuu wa siku mbili wa Tanzania Bloggers Network (TBN) uliofanyika katika ukumbi wa PSPF jijini Dar,pichani kulia ni Kaimu Meneja Mwandamizi kutoka benki ya NMB,Stephen Adili.
Mwenyekiti wa muda wa mitandao ya Kijamii Tanzania Bloggers Network (TBN), Joachim Mushi(aliyesimama)  akimkaribisha mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Idara ya Habari  MAELEZO, Dkt.Hassan Abbas  wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Tanzania Bloggers Network(TBN) uliofanyika katika ukumbi wa PSPF jijini Dar leo.

Baadhi ya Bloggers wakiwa kwenye mkutano wao unaoendelea hivi sasa.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


TANZANIA YAJIPANGA KUSHIRIKIANA NA MAURITIUS KATIKA SEKTA YA MIUNDOMBINU

0
0
Waziri wa Sanaa na Utamaduni wa Mauritius Bw. Santaram BABOO, akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Tanzania, Prof. Makame Mbarawa alipomtembelea ofisini kwake jijiin Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Tanzania, Prof. Makame Mbarawa, akifafanua jambo kwa Waziri wa Sanaa na Utamaduni wa Mauritius Bw. Santaram BABOO, walipokutana kwa majadiliano  kuhusu ushirikiano baina ya Wizara zao, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Tanzania, Prof. Makame Mbarawa (wa nne kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe kutoka nchini Mauritius, wa pili kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa na Utamaduni wa Mauritius, Dkt. Nalimi LUCKHEENARAIN, na wa tatu kushoto ni  Waziri wa Sanaa na Utamaduni wa Mauritius Bw. Santaram BABOO.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Twanga Pepeta kusindikiza utambulisho rasmi wa Yah TMK Taarab

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii


BENDI ya muziki wa dansi nchini African Star "Wana Twanga Pepeta" , watasindikiza utambulisho wa bendi mpya ya muziki wa taarabu Yah TMK Modern, utaofanyika  Desemba 17 mwaka huu, kwenye Ukumbi wa Dar Live, uliopo Mbagala Dar es Salaam. 

Mkurugenzi wa bendi hiyo Said Fella, alisema kuwa Twanga Pepeta watakuwepo kusindikiza utambulisho wa bendi hiyo ambayo ni mpya kabisa katika muziki wa taarabu hapa nchini. 

Alisema kuwa licha ya kuwepo Twanga Peoeta bado wanafanya mazunguko wa baadhi ya wanamuziki wa muziki wa kizazi kipya ambao nao watasindikiza usiku huo maalum wa Yah TMK Modern Taarab. 

Alisema onesho hilo la utambulisho limeandaliwa na kampuni ya Mkubwa na Wanawe ikishirikiana na Usher family entertainment, ikiwa na wasindikizaji mbalimbali. 

"Tunafanya utambulisho rasmi wa bendi yetu ambao tutaufanya Desemba 17 mwaka huu, maandalizi yanaendelea tumeshapata Twanga Pepeta ambao watasindikiza,Yah TMK Modern Taarab"alisema Fella. 

Ujio wa bendi hiyo unafuatia baada ya kambi ya nguvu ya takriban mwezi mmoja na nusu, hatua iliyozalisha nyimbo mbili kali “Sina Pupa” wa Mwanahawa Ali na “Kibaya Kina Mwenyewe” wa Aisha Vuvuzela. Yeah TMK inaundwa na wasanii wengi waliojiengua kutoka Jahazi kama vile Mohamed Mauji na Chidy Boy. 

Wengine ni  Babu Ali, Fatma Mcharuko na Aisha Vuvuzela, Omar Teggo na Mauwa Teggo. 
Viewing all 109581 articles
Browse latest View live




Latest Images