Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1447 | 1448 | (Page 1449) | 1450 | 1451 | .... | 3270 | newer

  0 0

   Mwenyekiti Mteule wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA), Shaibu Mashombo (wa nne kushoto), akiwa na viongozi wenzake wateule waliochaguliwa katika mkutano mkuu wa chama hicho 2016 jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Dismas Vyagusa, Violeth Shirima, Dk. Godfrey Swai, Dk.Nderineia Swai, Dk. Feliciana Mmasi,  Dk. Mwanahamisi Hassan na Dk.Elihuruma Nangawe ambaye alikuwa Mwenyekiti wa chama hicho aliyemaliza muda wake. Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Na  Immaculate Makilika –MAELEZO

  Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam  Mzee Yusufu  Makamba asema Rais Magufuli anafanana na Yohana Mbatizaji kwa vile ni kiongozi  anayefanyakazi bila kuogopa.
  Makamba ametoa kauli hiyo leo kwa njia ya simu katika mahojiano maalum na  Mwandishi  wa habari hizi. Alisema kuwa  Rais ni kiongozi mchapakazi ambaye hayumbushwi na maneno wala vitisho  kwa vile anasema ukweli katika kutekeleza majukumu yake.
  “Yohana Mbatizaji alisema ukweli na hakutikiswa na upepo, hakuogopa macho ya watu wala hakuwa mtu wa majigambo, kama ilivyoandikwa katika Biblia Takatifu Marko 6:12, na hivyo ndiyo navyomfananisha Rais wetu Magufuli na viongozi wote tumuunge mkono” alisema Makamba.
  Aidha, kuhusu miaka 55 ya Uhuru , alisema kuwa ni vyema Watanzania  wakazingatia wito wa uhuru ni kazi, na kwa kuwa Serikali hii imeweka mkazo katika ufanyaji kazi.
  Makamba  alisema kuwa katika Awamu hii ya HAPAKAZI TU, inaakisi wito wa Uhuru katika vipindi mbalimbali kuanzia kipindi cha Uhuru ni kazi na Uhuru na kazi mara baada ya kupatikana kwa Uhuru  na kuwakumbusha  watanzania kuulinda Uhuru.
  “Ni lazima kuulinda Uhuru kwa gharama yeyote ili amani na mshikamano uendelee kuwepo basi hatuna budii kuepuka lugha zenye  maneno ya uchochezi, ukabila na udini” alisema Makamba

  0 0

  @instincts_records presents SIJUTII REMIX Official Music Video in HD Starring @wakazimusic & @iamrubyafrica (Link On Wakazi Bio) Shot/Directed by @Einxer Edited by @meckykaloka Color Graded by @Dave4official

  0 0

  Na Rhoda Ezekiel Globu ya Jamii-Kigoma.

  WILAYA ya Kakonko Mkoa wa Kigoma imeelezwa kuendelea kuporomoka kiuchumi kutokana na mzunguko mdogo wa fursa za kibiashara kupelekwa wilaya ya jiran na watumishi wa idara  inayohudumia  wakimbizi katika kambi ya mtendeli kuishi Wilayani Kibondo, hali inayo pelekea shughuli zao zote kufanyika Wilayani humo.

  Kufuatia hali hiyo mkuu wa Wilaya Kanali Hosea Ndagala  alitoa  wito kwa watumishi  hao kutoa fursa za kiuchumi kwa wafanya biashara wa Wilaya ya Kakonko wakati wa ujenzi wa nyumba za kudumu za wakimbizi, lengo likiwa ni kuongeza mzunguko  wa kibiashara kwa Wananchi wanao izunguka kambi hiyo na kuacha tabia ya kutoa tenda zote za ujenzi kwa wafanya biashara wa Wilaya ya Kibondo.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana Wilayani humo, Ndagala alisema watumishi wengi wa Kambi ya mtendeli wamekuwa wakifanya biashara na wafanya biashara wa Kibondo,wakati kambi hiyo inahudumia wakimbizi katika Wilaya ya Kakonko hali inayo pelekea uchumi wa wananchi wa Kakonko waliotegemea kuupata kupitia kambi hiyo kuanzishwa kukosekana na kuhamia wilya nyingine ya Kibondo.

  Ndagala alisema halmashauri ya Wilaya ya Kakonko ni halmashauri ambayo uchumi wake bado upo chini,unahitaji kuinuliwa hivyo akawaomba wafanyakazi wa kambi ya Mtendeli pamoja na shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR kutoa vipaumbele kwa  Wananchi wa Wilaya ya Kakonko ili kuinua uchumi wa Wilaya hiyo kwa kuwapatia ajira za ujenzi na ununuzi wa vifaa vya ujenzi kwa wafanya biashara wa Kakonko.

  Hata hivyo Mkuu huyo aliwaomba watumishi wote  wa Kambi hiyo na mashirika yanayo hudumka wakimbizi kurudi kuishi Kakonko kwakuwa sababu iliyo kuwa ikiwapelekea waishi Kibondo ya kukosekana kwa Nyumba za kupanga Wilayani humo limekwisha Wananchi wamejitahidi kujenga nyumba zenue ubora ambazo wanaweza kupanga na kufanya kazi zao za kuhudumia wakimbizi wakiwa wilayani humo.

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.


  BARAZA la wadhamini Simba limeweka msimamo wake wa kutokuutambua mkutano mkuu wa dharula uliotarajiwa kufanyika Desemba 11 na kuutaka uongozi wa klabu hiyo kuusimamisha mara moja mpaka pale madai ya wanachama yatakapovumbuliwa ikiwemo elimu kwa wanachama hao.

  Taarifa hiyo iliyotolewa leo na Mwengekiti wa Baraza Mzee Hamis Kilomoni imesema kuwa baada ya kusoma nakala za barua za malalamiko zilizowafikia kutoka kwa baadhi ya wanachama wamekuta mambo mengi ya msingi huku wao kama ba

  Ametaja baadhi ya mambo hayo, ni kuwa uongozi wa klabu ya Simba haujatoa elimu ya hisa kwa wanachama wake kama ilivyotakiwa, wanachama kuwekeana chuki miongoni mwao mpaka kufikia hatua ya kutukanana na kupigana ambapo mbali na hilo pia Uongozi wa Simba haukutoa taarifa za maboresho ya uendeshaji wa klabu kama mkutano mkuu wa Julai 31 ulivyotaka.

  Kilomoni ameendelea na kusema, wao kama baraza la wadhamini na hawakuwa wameshirikishwa katika mchakato wowote wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu wamechukua hatua ya kuusimamisha mkutano huo mpaka pale uhakiki wa wanachama utakapofanyika kupitia kwa msajili wa vyama chini Baraza la Michezo Tanzania (BMT) kwani kwenye mkutano mkuu wa awali wengi waliingia na risiti na sio kadi, na kumtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kuusimamisha mkutano mkuu huo wenye kila dalili za uvunjifu wa amani huku kumbukumbu ikionesha kuwa Rais Evance Aveva alitolewa chini ya ulinzi mkali kwenge mkutano uliopita.

  Baraza la wadhamini limewataka uongozi wa klabu ya Simba kutoa elimu kwa wanachama kama ilivyokuwa imekubaliwa kupitia matawi na mikutano ya wanachama.

  0 0

  NEW MUSIC FROM SPICY (GROUP MEMBER OF 2NITE ENTERTAINMENT)  
  Spicy is Mr. Flavour's pianist 
  Enjoy the good music

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii


  UONGOZI wa timu ya Ruvu Shooting umeingia kndarasi na Kocha Malale Hamsini kuifundisha timu hiyo kipindi cha mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom, Tanzania Bara baada ya kubwagiwa manyanga na ndugu zao JKT Ruvu.

  Kocha Malale tayari amewasiri kambini Mabatini ambapo Jumatatu, Desemba 5, 2016 ataanza rasmi majukumu aliyokabidhiwa ya kukinoa kikosi hicho kama Kocha mkuu.

  Uongozi wa Ruvu Shooting umesema, umefikia maamzi ya kumchukua kocha Malale kutokana na uwezo wake mzuri wa kufundisha mpira kama unavyopambanuliwa na mafanikio makubwa katika timu alizowahi kuzifundisha.

  "Malale ni kocha mzuri sana, ameifundisha timu ya JKU kwa mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuipandisha hadi ligi kuu ya Zanzibar mwaka 2013, msimu wa 2014 ikiwa mikononi mwake ilishika nafasi ya pili katika ligi hiyo ya Zanzibar, aliifikisha timu hiyo nusu fainali ya mashindano ya kombe la Mapinduzi, pia aliiwezesha kutwaa ubingwa wa mashindano ya majeshi mwaka 2013 Jijini Dar es salaam" wamesema.

  Waliongeza kwamba, mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, msimu wa 2015/16 alikwenda kuifundisha Ndanda FC ambayo ilimaliza mzunguko wa kwanza wa ligi ya msimu huo ikiwa ya pili kutoka mwisho lakini akaiwezesha timu hiyo kumaliza ligi ikiwa nafasi ya saba!

  Aidha uongozi wa Ruvu Shooting ulisema kwamba, Malale akiwa na timu ya JKT Ruvu msimu huu wa ligi, mbali na timu hiyo kutokuwa katika nafasi nzuri ya msimamo ameiwezesha timu hiyo kuonesha ubora wa kucheza mpira wa kufundishwa.

  "Tunaimani Malale ni kocha mzuri, kwa ushirikiano wake na msaidizi wake Seleman Mtungwe ambaye naye ni kocha bora mwenye viwango, timu yetu itakuwa imara na bora zaidi, itakuwa tishio na tutafanya vizuri mno katika msimu huu wa ligi" walisema Ruvu Shooting.

  Malale pia ni kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes, alianza rasmi kazi ya ukocha mwaka 2004 akiifundisha kwa mafanikio makubwa timu ya Ngome ya Fuoni na baadaye timu ya Faru ya Jumbi.  0 0

  Gari ndogo ikivuka katika Barabara ya Mabasi ya Mwendo kasi, eneo la Magomeni Makuti (Moroco hotel zamani), Jijini Dar es salaam. Pamojana kwamba Matumizi ya barabara yamebadirika kwa maeneo mengi hapa mjini, lakini gari hii imeendelea kuutumia utaratibu ule ule wa zamani. sasa sijui ni makusudi au ndio kutokujua kama kuna mabadiriko hayo.

  0 0

  Mmoja wa wakazi wa jiji la Dar akivushwa barabara mtaa wa Samora mapema leo jijini Dar,huku moja ya gari ikivunja sheria za Barabarani bila kujali usalama wa wapita njia ama vyombo vingine vya moto,hali inayoweza kusababisha ajali.Madereva wanapaswa kuwa makini wakati wote waendeshapo vyombo vya moto ikiwemo na kuzijua njia wazipitazo kuepuka kuwa chanzo cha ajali. 

  0 0  0 0  0 0

  Shirikisho la Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu-CCM, limefanya semina ya utendaji kwa makatibu wake wote wa matawi katika mkoa wa Dar es Salaam, kwa lengo la kuwajengea uwezo katika kazi zao ili kuliimarisha Shirikisho na Chama Cha Mapinduzi.

  Katibu Msaidizi wa CCM, Daniel Zenda alisema, katika semina hiyo iliyofanyia Novemba 30, mwaka huu, jumla ya Makatibu 32 walihudhuria na kuondoka wakiwa wameongeza upeo wao katika kazi zao za chama.

  Alisema, moja ya mambo ambayo walifundwa Makatibu hao ni namna nzuri ya kuwezesha Chama Cha Mapinduzi kupata wanachama wapya miongoni mwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza katika vyuo vikuu, kwa kuwa tegemeo na uhai wa Shirikisho hilo ni wanafunzi wa aina hiyo.

  "Unajua Shirikisho linatilia mkazo sana katika kuhakikisha Makatibu wa Matawi wanashughulika kwa juhudi kubwa kuhakikisha kila wakati tunapata wanachama wapya hasa hawa wanaokuwa wanajiunga katika vyuo katika mwaka wa kwanza kwa kuwa hawa wanakuwa bado wabichi na wenye nguvu kutumikia Shirikisho na Chama kwa jumla", alisema Zenda na kuongeza.

  "Shirikisho linalipa kipaumbele suala la kuingiza wanachama kutoka wale wa mwaka wa kwanza kwa sababu kuingia kwa wanavyuo wapya vyuoni kuna kuwa na maana pia kuwa wapo wanaondoka kutokana na kuhitimu masomo yao, ambao baada ya kuhitimu wanaweze kushindwa kuendelea kuwa wanachama wazuri wa shirikisho kutokana na kubanwa na shughuli nyingine".
   Katibu Msaidizi wa CCM, Daniel Zenda akiongoza semina hiyo
  🔺Washiriki wakiwa kwenye semina hiyo katika Ukumbi wa Sekretarieti, Makao Makuu ya Umoja wa Vijana wa CCM, jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mh Anthony Mtaka (wa pili kulia) akiwa pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Profesa Elifas Bisanda (katikati mwenye tai),  Katibu Tawala wilaya ya Ilala (DAS) Edward Mpogolo (wa pili kulia) Bw Hume wa OUT na Derek Murusuri (kushoto) baada ya majadiliano ya muda mfupi kuhusu mchango wa OUT kwenye maendeleo ya elimu nchini Tanzania jijini Dar leo.

  0 0

  Na.Anthony John blog jamii.

  Naibu Waziri wa nchi ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali  za mitaa  (TAMISEMI) Mh Suleiman Jaffo amewataka watumishi wa umma kufanya kazi kwa kujiamini  katika kutekeleza majukumu yao ili kuleta mabadiliko  ya  kimaendeleo katika Taifa.

  Mh Jaffo ameyasema hayo  leo wakati akizungumza na watumishi wa umma  wa manispaa ya Ilala na jiji la Dar es slaam,  watendaji ,wabunge pamoja na madiwani  na kuwaelekeza wakuu wa idara kufanya kazi na kuwapa ushirikiano watumishi wa ngazi  za chini  katika idara zao na kuacha kuwanyanyasa .

  ‘’Nawaagiza wakuu wa idara  muache kuwa nyanyasa watumishi walio  chini yenu kwakuwa  wengi wanafanya kazi kwa hofu ya kuogopa kutumbuliwa  nakupelekea kutokuwa na amani katika maeneo yao ya kazi.’’ Alisema  Jaffo.

  Aidha amesema  wizara yake itatoa ushirikiano kwa  watumishi wote wanaotekeleza majukumu yao kwa moyo na bidii na amewaagiza wakuu wa idara kuwa na utaratibu wa kutambua kazi za watumishi wanao jituma na kuvuka malengo ya kazi walio wekewa  hatakama hakuna pesa za kuwapa  angalau waandikiwe barua ama kupewa vyeti vya kutambua michango yao mahala pakazi.

  Hata hivyo amempongeza  mkuu wa mkoa wa Dar es salaam , mkurugenzi wa jiji pamoja na madiwani  kwa kusimamia  suala  la usafi wa jiji kuwa nzuri  kwakuwa kipindi cha nyuma jiji lilikuwa halitamaniki.‘’Zamani jiji la Dar es salaam  lilikuwa chafu  lakini kwa sasa  hali imekuwa nzuri ukilinganisha na kabla ya kampeni ya usafi haijaanza.hayo amesema Jaffo.


  Pamoja na hayo mh Jaffo ameuagiza uongozi  wa manispaa ya ilala kwa kushirikiana na katibu tawala  mkoa wa  Dar es salaam  kupitia upya mkataba alio pewa mpangaji katika eneo lilotolewa na Dawasco kwa ajili ya kujenga shule ya kata ya secondary  Buguruni   kutembelea eneo hilo na kisha kufanya maamuzi ili eneo hilo liweze kujengwa shule.

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza  na watumishi wa serikali na halmashauri wa mkoa wa Arusha kwenye ukumbi wa Simba wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha, Desemba 2, 2016.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea  taarifa ya mkoa wa Arusha kutoka kwa Mkuu wa Mkoa huo, Mrisho Gambo baada ya kusomewa taarifa hiyo katika mkutano wake na watumishi wa serikali na halmashari kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) Desemba 2, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea bahasha yenye nyaraka mbalimbali zinazoonyesha ubadhirifu  unaofanyika katika halmashauri ya Wilaya ya Arusha kutoka kwa  Benard Mtei wa Idara ya Afya katika halmashauri hiyo wakati alipozungumza  na watumishi wa serikali na halmashauri mjini Arusha Desemba 2, 2016. 
  Baadhi ya watumishi wa serikali na halmashauri wakimsikiliza  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza  nao kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Desemba 2, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Na Eleuteri Mangi – WHUSM.

  Serikali imesaini Mkataba na Klabu ya Yanga kutumia Uwanja Mkuu wa Taifa pamoja na Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya michezo yote ya Kimataifa pamoja na michezo ya Ligi Kuu ya ndani.  Mkataba huo umesainiwa leo jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel kwa niaba ya Serikali na Kaimu Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga Baraka Deusdedit kwa niaba ya Klabu ya Yanga.  Katika Mkataba huo, Klabu ya Yanga imeruhusiwa kutumia viwanja hivyo kama viwanja vyake vya nyumbani kwa sharti la kuvitunza viwanja hivyo wakati wote wanapovitumia.  Miongoni mwa masharti hayo ni kutunza viwanja, mali na vifaa vyote vilivyopo katika viwanja hivyo, na endapo kutatokea uharibifu wowote utakaofanywa na wachezaji ama mashabiki, Klabu hiyo itawajibika kubeba gharama za matengenezo yote yatakayotokana na uharibifu huo.  Aidha, Klabu ya Yanga inaweza kutumia viwanja hivyo kwa mazoezi ya kujianadaa na mechi zinazowakabili.


   Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati) akisaini Mkataba kwa niaba ya Serikali na Klabu ya Yanga ya jijini Dar es salaam ambayo iliwakilishwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Klabu hiyo Baraka Deusdedit (kulia) leo jijini Dar es salaam. Mkataba huo unahusu Klabu ya Yanga kutumia Uwanja Mkuu wa Taifa na Uwanja wa Uhuru katika mechi za Kimataifa na Ligi Kuu. Wa kwanza kushoto ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Sheria Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Evordy Kyando. 
   Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akibadilishana Mkataba waliosaini na Kaimu Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga Baraka Deusdedit leo jijini Dar es salaam.  Mkataba huo unahusu Kalabu ya Yanga kutumia Uwanja Mkuu wa Taifa na Uwanja wa Uhuru, Wa kwanza kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Alex Nkenyenge.

  Picha ya pamoja ya Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (wa pili kushoto) mara baada ya kusaini Mkataba na Klabu ya Yanga leo jijini Dar es salaam. Wa pili kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga Baraka Deusdedit.

  0 0

  Mwenyekiti wa muda wa mitandao ya Kijamii Tanzania Bloggers Network (TBN), Joachim Mushi (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano mkuu wa chama cha Bloggers Tanzania (TBN) utakaofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa PSPF jijini Dar es Salaam.Kulia ni Katibu wa TBN,Khadija Khalili na Mwisho kushoto ni Meneja wa Mitandao wa NMB,Joyce Nsekela.

  Akizungumza  mbele ya Wanahabari  mapema leo (hawapo pichani) ndani ya Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO,Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN),Joachim Mushi amesema kuwa mkutano huo unatarajiwa kufanyika kuanzia Desemba 5 na 6 ,2016 hapa hapa jijini Dar,ambao utawashirikisha wanachama wapatao 150 kutoka Tanzania Bara na Visiwani.Mushi alisema kuwa katika mkutano huo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari,Michezo,Utamaduni na Sanaa Mh Nape Mosses Nnauye,

  "Mgeni rasmi anaetarajiwa kufungua mkutano huo ni  Waziri Nape Nnauye,lengo kuu la mkutano huo likiwa ni kupeana elimu na kubadilishana mawazo  juu ya uendeshaji wa Mitandao ya Kijamii kwa manufaa,upashaji habari kwa kutumia mitandao yao kwa kuzingatia maadili  na namna ya kunufaika na mitandao hiyo kwa waendeshaji",alisema Mushi.

  Alisema kuwa uendeshaji wa Mitandao baadhi yao wanaifanya ni kama ajira nyingine,hivyo kimsingi lazima wakubali kuwa mitandao hii imekuwa tegemeo kubwa la kusambaza habari mbalimbali tena kwa muda mfupi tangu kutokea kwa tukio fulani,hivyo kuna kila sababu ya kuendelea kuwapiga msasa wanaoiendesha ili kupunguza matumizi mabaya  ya mitandao hii,

   Mkutano huo utakaokuwa wa aina yake na kuiandika historia tangu kuanza kwa mitandano ya Kijamii hapa nchini,umedhaminiwa na Benki ya NMB ambaye ni mdhamini mkuu ,NHIF, SBL, PSPF na Coca Cola
  Ofisa Uhusiano wa NMB, Doris Kilale akizungumzia udhamini wa benki ya NMB katika mkutano mkuu wa Chama cha Bloggers Tanzania (TBN) utakaofanyika kwa siku mbili na kuwakutanisha blogger kutoka Tanzania Bara na Visiwani.   
  Mwenyekiti wa muda wa Chama cha Bloggers Tanzania (TBN), Joachim Mushi(wa pili kutoka kulia) akipokea hundi ya shilingi milioni 10 kutoka kwa Ofisa Uhusiano wa NMB, Doris Kilale kwa ajili y kudhamini mkutano huo.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha kumbukumbu cha maombelezo ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo na mpigania ukombozi Fidel Castro aliyefariki dunia novemba 25,2016 mjini Havana, aliyesimama kushoto ni Balozi wa Cuba nchini Balozi Jorge Luis Lopez Tormo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha kumbukumbu cha maombelezo ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo na mpigania ukombozi Fidel Castro aliyefariki dunia novemba 25,2016 mjini Havana.


  0 0

   Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (wapili kulia) akipokea vitabu vinavyotumika kuhamasisha jamii hasa wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari kujiepusha na matumizi ya Dawa ya Kulevya pamoja na kuhifadhi mazingira kutoka kwa ujumbe kutoka Kampuni ya Shree All World Gayarti Pariwar inayohamasisha jamii huru isiyotumia Dawa ya Kulevya, kutunza na kuhifadhi mazingira pamoja na kuwa na mazoezi ya afya kwa jamii walipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
   Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (wa pili kulia) akisalimiana na Bw. Kishor Thakrar kutoka  Kampuni ya Shree All World Gayarti Pariwar inayohamasisha jamii huru  isiyotumia Dawa za Kulevya, kutunza na kuhifadhi mazingira pamoja na kuwa na mazoezi ya afya kwa jamii walipomtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kumpatia vitabu vinavyohamasisha jamii iliyo huru, leo jijini Dar es Salaam. 

   Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (wapili kulia) akizungumza na ujumbe kutoka Kampuni ya Shree All World Gayarti Pariwar inayohamasisha jamii huru isiyotumia Dawa za Kulevya, kutunza na kuhifadhi mazingira pamoja na kuwa na mazoezi ya afya kwa jamii walipomtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kuwasilisha vitabu wanavyovitumia kutoa elimu hiyo kwa jamii hasa katika shule za msingi na sekondari leo jijini Dar es Salaam. 

  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu nchini Mhe.Abdulla Ibrahim Ghanim Alsuwaidi alipowasili katika ofisi za ubalozi huo kushiriki sherehe ya madhimisho ya miaka 45 ya muungano.Tanzania na UAE zimepiga hatua kubwa za ushirikiano hususan ya kiuchumi ambapo kwa takwimu za Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) hadi Juni, 2015 makampuni 67 ya uwekezaji kutoka UAE yamewekeza hapa nchini katika sekta mbalimbali wenye thamani ya USD 497.12 Millioni na kuajiri Watanzania 9,044. Taifa la Umoja wa Falme za Kiarabu unaundwa na falme saba ambazo ni Abu Dhabi, Dubai, Sharjah, Ras Al Khaimah, Fujairah, Ajman na Umm al-Quwain.
                                             
  Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Taifa la Umoja wa Falme za Kiarabu Mhe. Abdulla Ibrahim Ghanim Alsuwaidi wakati wa sherehe ya maadhimisho ya miaka 45 ya muungano wa falme hizo
  Mhe.Waziri Balozi Dkt.Mahiga akivalishwa skafu maalum.
  Kwa habari kamili BOFYA HAPA

older | 1 | .... | 1447 | 1448 | (Page 1449) | 1450 | 1451 | .... | 3270 | newer