Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1446 | 1447 | (Page 1448) | 1449 | 1450 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi , Abdulrahmani Kaniki akimkabidhi cheti cha Upelelezi Polisi Konstebo Jonathani Tossi wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya upelelezi kwa askari polisi wa Kinondoni katika chuo cha maafisa wa polisi Kidatu mkoani Morogoro
  Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi , Abdulrahmani Kaniki akifafanua (katikati) jambo wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya upelelezi kwa askari polisi wa Kinondoni katika chuo cha maafisa wa polisi Kidatu mkoani Morogoro. Kulia ni Kamishina wa Polisi operesheni na mafunzo, Nsato Marijani 
  Kamishina wa Operesheni na Mafunzo ( CP) Nsato Marijani akimsikiliza mwakilishi wa Taasisi ya Hans Sidel Bi Juliana wakati wakimsubili Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi kuwasili katika chuo cha maafisa wa Polisi Kidatu kwa ajili ya kufunga mafunzo ya upelelezi kwa askari Polisi wa mkoa wa kipolisi Kinondoni. ( picha na Tamimu Adam- Jeshi la Polisi).


  0 0

   Mkuu wa Chuo cha Bandari, Dk. Joseph Kakeneno akimkaribisha Balozi wa Korea Kusini hapa nchini, Mhe. Song Geum-young kutoa mhadhara wake kwa Wanachuo.
   Balozi wa Korea Kusini hapa nchini, Mhe. Song Geum-young akitoa mhadhara kwa wanachuo. Kulia ni Mkuu wa Chuo cha Bandari, Dk. Joseph Kakeneno.

  Baadhi ya Wanachuo cha Bandari wakifuatilia mhadhara uliokuwa ukitolewa na  Balozi wa Korea Kusini.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Zainab Nyamka, Globu ya Jamii .

  MKURUGENZI wa Elimu ya Juu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia  Prof Silvia Temu amesema kuwawanafunzi wanaohitimu wanatakiwa kwenda kufanya kazi kwa juhudi kubwa na kutokuacha kujiendeleza na kujifunza kwani dunia inabadilika na magonjwa yanazidi kujitokeza kila siku.

  Aliyasema hayo, wakati wa kongamano la Mjasiri lililowakutanisha wanafunzi waliosoma zamani katika Chuo Kikuu cha Afya, Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) na wanafunzi wanaohitimu na kuwataka kuendelea na utafiti wa magonjwa mbalimbali yanayowazunguka jamii.

  Prof Temu amesema kuwa MUHAS wameweza kufanya kitu kizuri sana kwa kuwakutanisha wanafunzi waliomaliza hapa na mkusanyiko huu utasaidia kuweza kuleta mawazo mapya na zaidi yatasaidia kwenye kukuza na kuendeleza sekta ya afya.

  "kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Joyce Ndalichako, tunaoenda kuwapongeza sana MUHAS kwa jitihada nzuri waliyofanya ya kuwakutanisha pamoja wanafunzi waliosoma miaka ya nyuma pamoja na hawa wanaohitimu katika ngazi mbalimbali kwani tunachokijua ni kuwa watabadilishana uwezo hasa kwa wale waliokuwa washapata uzoefu wa muda mrefu,"amesema Prof Temu.

  Makamu Mkuu wa Chuo cha MUHAS, Prof. Ephata Kaaya amesema kuwa  kongamano hili la Majasiri litaleta manufaa makubwa sana kwani kutawawezesha wanafunzi wanaohitimu na waliomaliza miaka ya nyuma kufanya kazi kwa pamoja, kwani Majasiri wanachangia kwa kiwango kikubwa katika Chuo kwa kutoa mawazo na hata fedha kwa ajili ya kuendeleza maendeleo ya chuo.

  Kaaya amesema kuna changamoto nyingi sana  katika kuendeleza maendeleo ya chuo hususani kwa upande wa fedha ila kwa kuwakutanisha hawa Majasiri kutasaidia kwa namna moja au nyingine kwenye kutatua matatizo ya chuo cha MUHAS.
  Mkurugenzi wa Elimu ya Juu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia  Prof Silvia Temu akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia  Prof Joyce Ndalichako wakati wa Kongamano la Majasiri wa Chuo Kikuu cha Afya, Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) leo Jijini Dar es salaam.
   Mkurugenzi wa Elimu ya Juu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia  Prof Silvia Temu (katikati)akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kutoka kushoto ni
  Makamu Mkuu wa Chuo cha MUHAS, Prof. Ephata Kaaya, Mwenyekiti wa kamati ya Chuo Mariam Joy Mwaffisi, kutoka kulia ni makamu mwenyekiti wa kongamano Dr Ellen Senkoro na Mwenyekiti wa wa kongamano hilo  Prof Charles Mgone.
  Mkurugenzi wa Elimu ya Juu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia  Prof Silvia Temu akiangalia baadhi ya maonesho yaliyoandaliwa na Wahitimu wanaomaliza kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) leo Jijini Dar es salaam.
   Mkurugenzi wa Elimu ya Juu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia  Prof Silvia Temu akiwa na Makamu Mkuu wa Chuo cha MUHAS, Prof. Ephata Kaaya (kushoto),  Mwenyekiti wa wa kongamano la Majasiri wa Chuo hicho Charles Mgone.
   Baadhi ya wahitimu na wahitimu wakiwa makini kufuatilia kongamano hilo. Picha zote na Zainab Nyamka.


  0 0

  Timu ya Taifa ya mchezo wa kuogelea, imetamba kufanya vyema katika mashindano ya Dunia yaliyopangwa kuanza Desemba 6 mjini Windsor, Canada.

  Tanzania itawakilishwa na jumla ya wogeleaji sita ambao wamepatikana kutokana na michujo mbalimbali ikiwa pamoja na mashindano ya Taifa yaliyofanyika mwezi Machi mwaka huu kwenye bwawa la kuogelea la Hopac.

  Waogeleaji hao ni Hilal Hilal ambaye ni nahodha, Adil Bharma, Denis Mhini na Joseph Sumari ambao ni wanaume ambapo kwa wanawake ni pamoja na muogeleaji namba moja nchini, Sonia Tumiotto na Catherine Mason.

  Akizungumza leo, Hilal alisema kuwa wamejiandaa vizuri chini ya kocha wao, John Belela na morali ipo juu kutokana na mafanikio waliyopata hivi karibuni katika mashindano ya kanda ya tatu yaliyofanyika Kigali, Rwanda na Tanzania kushika nafasi ya kwanza.

  Hilal alisema kuwa lengo lao ni kupigia taifa lao na wanaamini watafanya vyema na hasa baada ya kuwaongeza wigo wa waogeleaji.

  "Tumejiandaa kufanya vizuri, kama mjuavyo kwenye mashindano ya Afrika ya kanda ya tatu Tanzania ndiyo ilikuwa bingwa, tulipata medali 99, ushindani huu tutakwenda kuuendeleza Canada," alisema Hilal.
  Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Anastazia Wambura akikabidhi bendera kwa nahodha wa timu ya Taifa ya Kuogelea, Hilal Hemed Hilal.

  0 0


  KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, itakuwa mkoani Kigoma wikiendi hii  siku ya Jumamosi Desemba 3, 2016 kusaka vipaji vya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (U-17).

  Huo ni mwendelezo wa mpango wa Kitaifa wa timu hiyo wa kutengeneza kikosi imara cha timu ya vijana wa umri huo, ambapo inakwenda Kigoma kutokana na mkoa huo kuwa historia ya kisoka nchini ya kutoa wanasoka wengi waliotamba.

  Majaribio hayo ya pili kuelekea mwisho wa kufungwa zoezi hilo, yatafanyika ndani ya Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma Jumamosi hii kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 8.00 mchana na vijana wanaotakiwa ni wale waliozaliwa kuanzia mwaka 2000 hadi 2004.

  Mpaka sasa zoezi hilo limeshahusisha mikoa sita, ambayo ni Dar es Salaam, Tanga, Morogoro & Dodoma, Visiwani Zanzibar, Mbeya na Mwanza, ambapo kiujumla Azam FC imewafanyia usaili jumla ya vijana 3, 265 na kuvuna 70 pekee kati ya hao waliochaguliwa, huku 151 wakiwekwa akiba kwenye kumbukumbu za mradi huo.

  Vijana hao wote waliochaguliwa kwenye mikoa mbalimbali, wanasubiria kuitwa kwenye mchujo wa mwisho utakaofanyika ndani ya Uwanja wa Azam Complex baadaye mwezi huu Desemba, ambao ndio utatoa vijana bora watakaounda timu hiyo.

  0 0


  Kufuatia Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumteua Jenerali (Mst) George Marwa Waitarakuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TANAPA tarehe 29 Oktoba, 2016, Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Profesa Jumanne A. Maghembe (Mb) amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi hiyo kwa mujibu wa Sheria ya Uanzishwaji wa TANAPA Sura ya 282 Jedwali la Pili ikisomwa pamoja na kifungu cha 8(1)(b) cha Sheria hiyo.


  1)        Bi. Devotha Mdachi, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania.

  2)     Dkt. Lucy Lugwisha, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi  

  waMazingira.

  3)        Kamishina Marijan M. Sato, Mkuu wa Operesheni  na Mafunzo,    Makao Makuu  Jeshi la Polisi.

  4)          Profesa Alexander Songorwa, Mkurugenzi wa Wanyamapori     kutoka   Wizara ya Maliasili na Utalii.

  5)          Profesa Wineaster Anderson, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar  es  Salaam, na Mwenyekiti wa Taasisi ya Maliasili na Utalii Endelevu Afrika (NARESTi Africa).

  6)          Bw. George Fumbuka, Mhasibu aliyethibitishwa ambaye pia ni Mtendaji Mkuu na Mwenyekiti wa Kampuni ya CORE Securities.

  7)        Dkt. Chanasa Mpelumbe Ngeleja, Daktari Mkuu wa Mifugo,Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

  8)     Bw. Allan J. H. Kijazi, Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA      


                    
  Uteuzi wa Mwenyekiti na Wajumbe hao ni wa muda wa miaka mitatu kuanzia tarehe 29/10/2016 hadi tarehe 28/10/2019.


            IMETOLEWA NA:

                                               

  Maj. Gen. Gaudence S. Milanzi

  KATIBU MKUU

  WIZARA YA MALI ASILI NA UTALII

  30 Novemba, 2016.
  0 0

  Na Anna Nkinda – JKCI.

  1/12/2016 Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe. Azzan Musa Zungu amewashukuru wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa huduma nzuri ya matibabu wanayompatia na kuiomba taasisi hiyo kutoa huduma kama hiyo kwa watanzania wote.

  Mhe. Zungu ambaye amelazwa katika Taasisi hiyo amezitoa  shukrani hizo leo wakati akiongea na waandishi wa habari waliotaka kufahamu kuhusu maendeleo ya afya yake.

  “Namshukuru Mwenyezi Mungu naendelea vizuri hali yangu siyo kama jana. Nilianza kuumwa majira ya saa nane  8:30 mchana nikiwa nyumbani katika mazingira magumu ambapo mapigo ya moyo yalipanda ghafla nikapelekwa Hospitali ya Amana na baadaye  Muhimbili  kitengo cha Huduma ya dharula majira ya saa 12jioni  kisha  nikaletwa  hapa”. 

  “Kwa namna ya pekee nawashukuru sana wafanyakazi wa Amana, Muhimbili na Taasisi ya Moyo ambao wamenipokea na kunipa  huduma nzuri na kama mnavyoniona afya yangu inaendelea vizuri tofauti na nilivyokuja jana”. alisema Mhe. Zungu.

  Aidha Mhe. Zungu aliwataka watanzania kujiunga na mfuko wa Taifa wa Bima ya afya ambao hata yeye ni mwanachama  kwa kuwa mwanachama wa mfuko huu kutawasaidia kupata matibabu pindi watakapoumwa bila ya kutoa fedha  mfukoni.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji  wa JKCI Prof. Mohamed Janabi alisema hali ya Mhe. Zungu  inaendelea vizuri tofauti na walivyompokea jana.  Hivi sasa madaktari wako katika uchunguzi wa matatizo ya Moyo baada ya hapo watajuwa tatizo na kumpatia tiba  na anaamini baada ya siku tatu zijazo anaweza kuruhusiwa.

  “Kipindi cha nyuma viongozi wenye matatizo kama haya walikuwa wanapelekwa  nje ya nchi kwa ajili ya matibabu  hivi  sasa Serikali imeboresha  huduma za matibabu ya Moyo  hivyo basi wagonjwa  wengi wanatibiwa hapa nchini”, alisema Prof. Janabi.

  Aliwashauri wananchi kupima afya zao japo mara moja kwa mwaka, wakiona dalili za viashiria vya ugonjwa wa Moyo waende haraka  Kituo cha Afya kilichopo jirani kwa ajili ya matibabu. 

  Prof. Janabi alimalizia kwa kuwasisitiza wananchi kufanya  mazoezi na kula vyakula sahihi na kwa upande wa wagonjwa wa Moyo wanatakiwa kumeza  dawa kipindi chote cha maisha yao wasiache kunywa dawa kwani wagonjwa wengi wanaorudi kupata matibabu ni wale walioacha  kumeza dawa.
  Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe. Azzan Musa Zungu akiwa amelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya moyo ambapo kwa sasa hali yake inaendelea vizuri. Kutoka kulia ni Muuguzi Mwandamizi Sr. Chagui Mgaza na kushoto ni Mwinyi Maulidi ambaye ni dereva wa Mhe. Zungu.Picha na Anna Nkinda - JKCI

  0 0  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushrikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb) anatarajiwa kuongoza ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Mawaziri wa Afrika na Korea unaotarajiwa kufanyika nchini Ethiopia tarehe 06 na 07 Desemba, 2016 mjini Addis Ababa, Ethiopia.


  Mkutano huu ambao umeandaliwa na Serikali ya Korea kwa kushirikiana na Umoja wa Afrika una lenga kukuza ushirikiano pamoja na kuandaa maeneo mapya ya ushirikiano baina ya Korea na mataifa ya Afrika katika miaka mitatu ijayo.


  Tanzania ni moja ya nchi nne (4) za Afrika ambazo Korea imezichagua kuanzisha mahusiano ya kimkakati “strategic partnership” yatakayozifanya nchi hizo kupewa kipaumbele katika kupokea misaada na mikopo nafuu kutoka Korea katika kipindi cha miaka mitano ijayo kati ya 2016 hadi 2020.


  Katika kipindi hicho Tanzania itapokea kiasi cha dola za Kimarekani milioni 300 ikiwa ni asilimia 17.1 ya msaada utakaotolewa Barani Afrika, hivyo kuifanya Tanzania kuwa nchi inayoongoza Barani humo kupata msaada wa Jamhuri ya Korea.


  Pamoja na ushiriki kwenye Mkutano huo, imependekezwa ufanyike mkutano baina ya Tanzania na Serikali ya Korea kuzungumzia masuala ya ushirikiano baina ya nchi zetu mbili. Aidha, ushiriki wa Tanzania kwenye mkutano wa Afrika na Korea ni fursa muhimu ya kukuza mahusiano baina ya nchi zetu mbili hususan katika Nyanja ya uchumi. Serikali ya Korea ilitoa ahadi ya kuongeza uwekezaji Barani Afrika hususan katikasekta za nishati, miundombinu na viwanda.


  Itakumbukwa kuwa, tayari Jamhuri ya Korea inashirikiana na Tanzania katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Mradi wa kuendeleza kilimo cha Mwani Zanzibar wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 3.6 na Awamu ya Pili ya Mradi wa kuboresha Uchunguzi wa Afya ya Uzazi Jijini Dar es Salaam wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni nne (4).


  Miradi mingine ambayo Jamhuri ya Korea inashirikiana na Tanzania ni ujenzi wa Daraja la Selander Jijini Dar es Salaam, Mradi wa Daraja la Kikwete kwenye Mto Malagarasi Mkoani Kigoma na Ujenzi wa Hospitali ya Kimataifa iliyopo eneo la Mloganzila Jijini Dar es Salaam.


   Imetolewa na:

  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

  Dar es Salaam, 01Desemba, 2016.
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga akizungumza kwenye mkutano na Waandishi wa Habari. Katika mkutano huo Bi. Kasiga aliwaeleza Waandishi wa Habari kuhusu Mkutano wa Nne wa Mawaziri wa nchi za Afrika na Korea utakaofanyika Mjini Addis Ababa, Ethiopia tarehe 06 na 07 Desemba, 2016. Mkutano huo utajadili masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya Afrika na Korea pamoja na maeneo mapya ya mashirikiano. 
  Afisa Mambo ya Nje, Bi. Bertha Makilagi akifuatilia mkutano kati ya Bi. Kasiga na Waandishi wa Habari. Wengine ni Waandishi wa Habari waliohudhuria mkutano huo. 
  Sehemu ya Waandishi wa Habari wakisikiliza na kunukuu kwa makini mkutano uliokua ukiendelea 

  Mkutano ukiendelea.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Aziz Mlima akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Kenya uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo pamoja na mambo mengine utajadili maeneo mbalimbali ya ushirikiano ikiwemo sekta ya Elimu, Afya na Kilimo. 
  Balozi wa Kenya hapa nchini, Mhe. Chirau Ali Mwakwere akifuatilia ufunguzi wa Mkutano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya 
  Sehemu nyingine ya wajumbe kutoka Tanzania wakifuatilia mkutano .  0 0

  Moja ya eneo la lililotumiwa na kampuni ya Polyphon Film ya nchini Ujerumani ikirekodi Filamu inayozungumzia maisha kwa ujumla eneo la Kogatende ndani ya Hifadhi ya taifa ya Serengeti mkoa wa Mara na inatarajiwa kukuza utalii . 
  Mkurugenzi wa kampuni ya Hatari Lodge ya jijini Arusha(kushoto)Gabriel na Meneja Uzalishaji wa kampuni ya Polyphon Film,Manuel Shrouder wakiwa eneo la kutengeneza filamu hiyo itakayooneshwa kwenye kituo maarufu cha Runinga cha ZDF nchini Ujerumani na kutazamwa na zaidi ya watu 10 milioni katika nchi tatu zikiwemo Austria na Uswizi. 
  Meneja Uzalishaji wa kampuni ya Polyphon Film,Manuel Shrouderk(kulia)akisalimiana na Mkurugenzi wa Utalii na Masoko wa shirika la Hifadhi za Taifa(Tanapa)Ndg Ibrahim Mussa(katikati) anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Hatari Lodge ya jijini Arusha,Gabriel.  
  Sehemu ya magari yaliyobeba vifaa vya kutengeneza filamu hiyo ambayo imegharimu kiasi cha Euro 1.7 milioni.


  0 0  Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Kanali mstaafu Abdulrahman Kinana amemtumia salamu za rambi rambi Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam Ndg. Ramadhan Madabida kufuatia kifo cha Muasisi wa TANU Bibi Hadija Bint Kamba, kilichotokea jana tarehe 30 Novemba, 2016 jijini Dar es salaam.

  Bibi Hadija Bint Kamba ni miongoni mwa wanaharakati waliopigania uhuru na ukombozi wa Taifa letu. Ameshiriki kuanzisha Baraza la Wanawake Tanganyika mwaka 1955 na baadae Umoja wa Wanawake wa Tanganyika (UWT) tarehe 02 Novemba 1962 akishirikiana na Bibi Titi Mohamed.

  Bibi Hadija hakuwahi kushika nafasi za uongozi ndani ya Chama na Serikali baada ya uhuru mpaka mwaka 1985 ambapo Mwalimu Nyerere alimtangaza mbele ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Baraza la Wazee wa Dar es salaam Diamond Jubilee, kuwa ni mtu aliyetoa mchango mkubwa katika ujenzi wa Chama na Nchi, tangu wakati huo Bibi Hadija Bint Kamba alihudhuria Mikutano mikuu ya Chama kama mjumbe mwalikwa mpaka umri ulipomzuia kuweza kushiriki.

  Bibi Hadija Binti Kamba, atakumbukwa na wanachama wa CCM kwa uadilifu, uvumilivu, ujasiri na mchango wake mkubwa katika ujenzi na uimarishaji wa Chama chetu, na kwamba mchango wake katika kupigania uhuru na kuleta ukombozi na maendeleo kwa Wanawake wa taifa hili utaendelea kuenziwa na kuthaminiwa na Watanzania.

  Hakika sisi ni wa MwenyeziMungu na kwake yeye ndio marejeo yetu. 

  Imetolewa na:- 


  Christopher Ole Sendeka (MNEC)
  MSEMAJI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
  01.12.2016

  0 0

  Frank Mvungi-Maelezo

  Kuelekea Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara Serikali imepongezwa kwa Mafanikio yaliyofikiwa katika kipindi chote tangu awamu ya kwanza hadi awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

  Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe. Daniel Chongolo wakati wa mahojiano maalum kuhusu maadhimisho ya miaka hamsini na tano ya Uhuru yanayotarajiwa kufanyika kitaifa tarehe 9 Desemba mwaka huu.

  “Tumepiga hatua kubwa katika upatikanaji wa huduma za jamii kama vile elimu,Afya,Maji,usafirishaji na miundo mbinu ukilinganisha na wakati tunapata Uhuru” Alisisitiza Chongolo

  Katika Sekta ya elimu Chongolo anabainisha kuwa Serikali katika awamu zote tangu awamu ya kwanza hadi sasa zimekuwa zikiweka kipamaumbele katika Sekta hiyo hali iliyochangia kuongezeka kwa shule za msingi ,Sekondari na Vyuo Vikuu .

  Akifafanua zaidi Chongolo ameongeza kuwa elimu bure ni miongoni mwa dhamira ya Serikali ya Awamu ya tano ya kuwaletea wananchi wake maendeleo na kuzidi kuendeleza azma ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ya kupamabana na maudui watatu ambao ni ujinga,maradhi na umasikini. 

  Akizungumzia kuhusu miundo mbinu ya barabara anabainisha Tanzania ya sasa ina tofauti kubwa na wakati Taifa lilipokuwa likipata Uhuru ambapo barabara za lami na madaraja yalikuwa machache lakini hivi sasa Mikoa yote inafikika kwa urahisi.
  0 0

  Na Amina Kibwana,Globu ya Jamii

  Kampuni ya Uwekezaji ya Taifa (NICOL) inatarajia kurudi upya mara baada ya kuingia hasara ya sh. Billion 10 pamoja na kukabiliana na kesi Mbalimbali ikiwemo  kupinga maamuzi ya wanahisa kuchagua uongozi pamoja na maamuzi ya kusitishwa kwa mkutano mkuu uliolenga kuzungumzia maswala ya mahesabu na muelekeo wa Kampuni.

  Akizungumza na waandishi wa Habari  Mwenyekiti wa NICOL Dk. Gideon Kaunda amesema kuwa kesi ya mwisho ya 41 iliamuliwa  mahakamani mara baada ya Mlalamika  makamu mwenyekiti wa TPSF Salum Shamte kutokuhudhuria mahakamani na hoja hizo zilikataliwa na Mahakama kuamua kuwa mkutano huo ulikuwa wa halali na ambapo mnamo Novemba 26 mkutano huo uliendelea.

  “Mkutano ulikwenda vizuri ambapo zaidi ya watu 300 kutoka mikoa mbalimbali walihudhuria pamoja na mashirika mbalimbali ya umma ambayo yalikuwa yamewekeza  wakiwemo PSPF, walifanikiwa kuhudhuria”. Alisema Kaunda 

  Aidha alisema kuwa Kampuni hiyo iliingia hasara kutokana na  uongozi uliopita kuwa na malimbikizo ya sh. Billion 10 kutokana na mahesabu yaliyofanywa, ambayo taarifa ilionesha kuwa kampuni ilikuwa inapata faida kwa wakati huo  sio sahihi,pamoja na kutokufuatwa kwa sheria na utovu wa nidhamu.

  Kwa upande wake Mtendaji  Mkuu wa NICOL  Adam Wanuza amesema kuwa kuwa pamoja na hasara hiyo,ukiwemo uwekezaji mbovu umechangia kutokana na makampuni mbalimbali kuchukua mkopo katika Kampuni ya Nicol.

  Naye Naibu Waziri Mstaafu katika sekta ya Uchukuzi ambaye pia ni Mtaalamu katika Masuala ya Biashara Dk. Athumani Mfutakamba amesema kuwa kufanikiwa kwa Mkutano huu ni ishara tosha ya kuzaliwa upya kwa NICOL katika jitihada za Kampuni ya uwekezaji ya kizalendo na jitihada hizi lazima ziungwe mkono na wazalendo wote wanaotaka maendeleo ya uchumi wa Taifa la Tanzania katika fursa mbalimbali.

  Kampuni ya Nicol itarudi Rasmi kupitia uongozi mpya sambamba na kuanza kutoa elimu Maalumu kwa wawekezaji katika soko la Hisa mnamo mwanzoni mwa mwaka 2017.
  Mwenyekiti wa kampuni ya Uwekezaji wa Taifa (NICOl) Bw. Gideon Kaunda kulia akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es salaam mara baada ya kupata uongozi mpya wa kampuni hiyo ulioteuliwa rasmi hivi karibuni na bodi ya NICOL kushoto ni Mtendaji Mkuu Bw. Adam Wamunza.

  0 0

   Na Bashir Nkoromo.
   
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ameongoza mamia ya wananchi katika maziko ya muasisi wa chama cha Tanganyika African Union (TANU) na baadaye Chama Cha Mapinduzi (CCM), Khadija Kamba, aliyefariki juzi na kuzikwa jana katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

  Kinana ambaye alifuatana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi, akitoa salam za zambirambi za Chama, alisema, CCM itamkumbuka na kuuenzi daima mchango mkubwa alioutoa hasa wakati wa harakati za ujenzi wa TANU na harakati za ukombozi wa Tanzania wakati wa uhai wake.

  "Binti Kamba alikuwa ni nguzo na chachu muhimu katika kuasisiwa kwa TANU na mpambanaji aliyekuwa mstari wa mbele katika harakati za kutafuta Uhuru wa nchi hii, hivyo Chama kitambukumbuka na kumuenzi daima Mama huyu", alisema Kinana, wakati akitoa salam za rambirambi wakati wa maziko.

  Kinana alisema, licha ya kuwa muasisi, lakini Binti Kamba kamtika maisha yake, aliendelea kuwa nwanachama na kada mwaminifu wa Chama Cha Mapinduzi na kuendelea kuwa kisima cha kuchota hekima na maarifa hadi anafariki dunia.

  Alisema, kutokana na kuguswa na msiba huo, kwa nafasi yake ya Katibu Mkuu wa Chama, ameandaa hitima itakayosomwa keshokutwa katika Msikiti wa Masjid Quba, kumuombea maghfira.

  Binti Kamba, ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 94, alifariki juzi asubuhi, nyumbani kwa mwanae wa kulea, Kamba Abdallah, jijini Dar es Salaam.

  Msafara kwenda kwenye maziko Kisutu ulianzia nyumbani kwa marehemu, Ilala Bungoni, Dar es Salaam, baada ya kuswaliwa, ambako miongoni mwa waombolezaji waliokuwepo ni pamoja na Muasisi mwingine wa TANU Kingunge Ngombale-Mwiru, ambaye mwaka jana alihamia Chadema kumfuata aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chama hicho Edward Lowassa.

   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rajab Luhwavi, akishiriki kubeba jeneza lenye mwili wa Muasisi wa TANU, Khadija Kamba, katika makaburi ya Kisutu, wakati wa mazishi yaliyofanyika leo, Desemba 01, 2016, katika makaburi hayo mjini Dar es Salaam. (Picha na Bashir Nkoromo).

  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimwaga udogo kaburini wakati wa mazishi ya Muasisi wa TANU, Khadija Kamba, katika Makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam, leo Desemba 01, 2016. Nyuma yake ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi. (Picha na Bashir Nkoromo).

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera  na Katibu Tawala wa Mkoa  huo , Eliakim Maswi  (kulia) wakati  aliposimama kwa muda mjini Babati akitoka Dodoma kwenda Arusha Desemba 2, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa mkoa wa Manyara wakati aliposimama kwa muda mjini Babati akitoka Dodoma kwenda Arusha, Desemba2, 2016. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Babati, Raymound Mushi wakati aliposimama kwa muda mjini Babati akitoka Dodoma kwenda Arusha, Desemba 2, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa mkoa wa Manyara wakati aliposimama kwa muda mjini Babati akitoka Dodoma kwenda Arusha Desemba2, 2016.

  0 0


  Na Dotto Mwaibale

  SERIKALI imeitaka Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kutoa hadharani majina ya wahasibu wabadhilifu ili jamii iweze kuwatambua.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha Dk.Philip Mpango kwa niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akizindua Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC), kilichopo Bunju na  Kongamano la Uhasibu la 2016 la siku tatu Dar es Salaam leo.

  "Ni vizuri mkaanza kutoa hadharani majina ya wahasibu wasio waadilifu ili jamii iweze kuwajua" alisema Mpango.Mpango alisema kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho kutaisaidia serikali kuelekeza fedha zilizokuwa zikitumika na bodi hiyo kukodi kumbi kwa kazi zake mbalimbali kupelekwa kufanya kazi zingine za maendeleo.

  "Nawaombeni mkitunze kituo hiki ili kitimize malengo yake ya kuleta manufaa kwa wananchi na taifa kwa ujumla" alisema Mpango.Aliwataka wahasibu nchini kutumia taaluma yao kuisaidia serikali hasa katika kipindi hiki cha nchi kuelekea kwenye uchumi wa viwanda badala ya wao kushirikiana na wafanyabishara wasio waaminifu kuiibia serikali.
   Waziri wa Fedha, Dk. Philip Mpango (kulia), akikata utepe kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuashiria kuzindua rasmi Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC), kilichopo Bunju jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa  Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Profesa Isaya Jairo na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa GEPF, Joyce Shaidi.

   Mwonekano wa baadhi ya majengo ya kituo hicho.
   Mwonekano wa ukumbi wa mikutano wa kituo hicho.
   Mkutano ukiendelea.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

   
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Longido, Daniel Chongolo baada ya kuwasili jijini Arusha kuanza ziara ya kazi mkoani humo Desemba 1, 2016.Pichani kati ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mh.Mrisho Gambo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Monduli, Iddi Kimanta baada ya kuwasili jijiniArusha kuanza ziara ya kazi Desemba 1, 2016.
   Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige  baada ya kuwasili jijiniArusha kuanza ziara ya kazi Desemba 1, 2016.

  0 0

    Na Mathias Canal

  Mwili wa Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) EX Peter Kakamba umeagwa na wamia ya wakazi wa Mkoa wa Singida wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Injinia Methew Mtigumwe.

  Kakamba alifariki dunia alfajiri ya tarehe 30/11/2016 katika hospital ya taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.

  Kakamba alizaliwa mwaka 1963 katika kijiji cha Kawajense Wilayani Mpanda, mkoa wa Katavi. Alisoma shule ya msingi Shanwe Kawajense  mwaka 1973 hadi 1980, Kidato cha kwanza hadi cha nne katika shule ya Sekondari Kantalamba mwaka 1981 hadi 1984 ambapo kidato cha tano na sita alisoma katika shule ya Sekondari Umbwe mkoani Kilimanjaro mwaka 1985 hadi 1987. Mwaka 1992 hadi 1994 alisoma Astashahada ya Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

  Marehemu alijiunga na Jeshi la Polisi mwaka 1988 ambapo katika utumishi wake alipandishwa vyeo mbalimbali ikiwemo Konstable wa Polisi (1989), Sagenti wa Polisi (1991), Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (1997), Mkaguzi wa Polisi (2003), Mrakibu Msaidizi wa Polisi (2006), Mrakibu wa Polisi (2008), Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (2011), Kamishna Msaidizi wa Polisi (2015) na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (2016).
  Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa kamanda jeshi la polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Kakamba ukitolewa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi maeneo ya VETA mjini hapa kwa ajili ya kuagwa na viongozi mbalimbali na wananchi wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew John Mtigumwe. Baada ya kuagwa kwa mwili huo umesafirishwa hadi kijiji cha Kawajese Mkoani Katavi kwa ajili ya mazishi. 
  Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Kamanda jeshi la polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Kakamba ukitolewa kwenye basi dogo lililobeba mwili huo kutoka hospitali ya taifa Muhimbili jijini Dar-es-salaam. Mwili huo umefikishwa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi mjini Singida kwa ajili ya kuagwa leo (01/12/2016).  
  Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Mageni Lutambi akiwashukuru wananchi waliojitokeza kwa wigni kuungana na familia kwa ajili ya kuaga mwili wa aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Charles Kakamba, Dkt Lutambi amesema Ofisi ya Mkuu wa Mkoa iko pamoja na wafiwa na watashiriki mazishi kijiji cha Kowajese Mkoani wa Katavi.
   Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida SSP Mayalla Towo akiwashukuru wananchi, taasisi na mashirika mbalimbali walioshiriki msiba huo, Towo amesema marehemu alikuwa kiongozi bora aliyependa kuwafundisha na kuwaelekeza ujuzi na maarifa aliyonayo watumishi walio chini yake.


  0 0

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe amesema Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa hakuna magogo na malighafi ya misitu  yatakayosafirishwa kwenda nje ya nchi kabla ya kuchakatwa.
  Amesema , hiyo itasaidia  kuongeza thamani  pamoja na  kupunguza tatizo la  ajira  kwa vijana wengi kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo kwa ajili ya kutengezea vifaa mbalilmbali vitakanavyo na mazao ya misitu kutokana na Magogo na Malighafi ya misitu kuchakatwa ndani ya nchi.  Amesema hayo leo kwenye mkutano wa kutathmini mafanikio na changamoto  zinazoikabili sekta ya maliasili nchini  tangu novemba 2015 hadi novemba 2016, uliowakutanisha wadau wa Maliasili kutoka sekta binafsi na Serikalini kujadili  sekta za misitu , wanyampori pamoja na  mambo kale.  Amesema kuwa  Misitu ni sekta inayokabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ukataji miti hovyo uvunaji haramu wa magogo pamoja na usafirishaji haramu wa magogo kwenda nje ya nchi.Amesema katika kukabiliana na changamoto hizo Serikali imeanza kuona namna ya  kuwalipa  sekta binafsi na watu  wenye kipato cha chini cha kati watakaokuwa wanapanda miti kama motisha  kutokana na  mchango mkubwa  wa  misitu wa kuzalisha hewa safi duniani kwa  kuondoa hewa ya  ukaa.
  Amesema mpango huo kamambe wa kuwalipa watakaopanda miti kwa wingi  itakuwa ni  njia muafaka ya kuondokana na tatizo la ukame linaaloendelea kutokea kutokana miti mingi kuendelea kukatwa kwa ajili ya mkaa na matumizi mengine kuongezeka kwa kasi.
   Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe wa pili kulia akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (wa kwanza kulia)  wakiwa kwenye mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam wa kutathmini mafanikio na changamoto  zinazoikabili sekta ya maliasili nchini  tangu novemba 2015 hadi novemba 2016, uliowakutanisha wadau wa Maliasili kutoka sekta binafsi na Serikalini kujadili  sekta za misitu , wanyampori pamoja na  mambo kale ( Picha na Lusungu Helela- Maliasili)
   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Eng. Angelina Madete  akichangia hoja kwenye mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam wa kutathmini mafanikio na changamoto  zinazoikabili sekta ya maliasili nchini  tangu novemba 2015 hadi novemba 2016.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe wa akiwa na wadau wa Maliasili wakisiliza kwa makini  uwasilishaji wa mada kuhusu  sekta za misitu , wanyampori pamoja na  mambo kale  kwenye mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam wa kutathmini mafanikio na changamoto  zinazoikabili sekta ya maliasili nchini  tangu novemba 2015 hadi novemba 2016.

  Baadhi ya wadau wa Maliasili kutoka serikalini na Sekta binafsi wakifuatilia kwa makini uwasilishaji wa mada za Maliasili  kwenye mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam wa kutathmini mafanikio na changamoto  zinazoikabili sekta ya maliasili nchini  tangu novemba 2015 hadi novemba 2016.


  0 0


older | 1 | .... | 1446 | 1447 | (Page 1448) | 1449 | 1450 | .... | 3285 | newer