Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1448 | 1449 | (Page 1450) | 1451 | 1452 | .... | 3286 | newer

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imepiga marufuku uchapaji holela wa vitabu vya kufundishia na kujifunzia kwa wachapaji binafsi na badala yake uchapaji huo utasimamiwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TEA) ili kuthibiti ubora.

  Amesema mbali na kudhibiti wa ubora pia uamuzi huo unalenga kuwa na kitabu kimoja kwa kila somo kwa kila mwanzfunzi kwa nchi nzima ili kuweka uwiano mzuri katika ufundishaji na upimaji wa wanafunzi .

  Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Ijumaa, Desemba 2, 2016) wakati akizungumza na walimu wa halmashauri ya Jiji la Arusha na wilaya ya Arusha kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) akiwa katika siku ya kwanza ya ziara ya kikazi mkoani Arusha.

  Ziara hiyo inalenga kukagua utelelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM,Utendaji wa Serikali, kusikiliza na kujionea kero zinazowakabili wananchi  wa Mkoa huo kwa kushirikiana na viongozi wa Mkoa ili kuweza kuzitafutia suluhisho.

  Amesema kipindi cha nyuma vitabu vilikuwa vinachapwa na watu mbalimbali hivyo kusababisha malalamiko makubwa kutokana na vitabu hivyo kuwa na makosa mengi. “Sasa vitabu vikibainika kuwa na makosa tutaibana Taasisi ya Elimu Tanzania,”.

  Aidha, amesema Serkali itahakikisha kila mtoto anakuwa na kitabu chake ili kuwawezesha kusoma vizuri na kuwa na uelewa wa kutosha ikiwa ni pamoja na kuwarahisishia walimu katika ufundishaji.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0

  Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imemnyima dhamana Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA) Mhe. Godbless Lema. Mahakama hiyo imeeleza kuwa mawakili wa mtuhumiwa huyo walipaswa kuonesha kusudio la kukata rufaa ndani ya siku 10 kabla ya kukata rufaa.

  Hii ni mara ya tano mbunge huyo anakosa dhamana mahakamani tangu alipokamatwa Novemba 3 mwaka huu akiwa mjini Dodoma na kusafirishwa hadi Arusha katika kesi ya uchochezi inayomkabili.

  0 0


  Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma A. Malewa 
  (kulia) na Kamishna Jenerali mstaafu John Casmir Minja

  0 0

                                                             

  VIP LOUNGE by AMSTERDAM TREAT

  VIP FRONT ROW guests will have a dedicated ENTRY and a LOUNGE hosted by Amsterdam Treat at the National Museum during the #sfw2016. Have you gotten your VIP FRONT ROW tickets?

  SHOPPING FESTIVAL - EXHIBITORS

  AWARDS
  DESIGNERS
  CONTACT US

  Have you Gotten your Tickets to #fashionweek?

  TICKETS(Normal & VIP FRONT ROW) are NOWAVAILABLE AT EPIDOR and Colosseum Hotel & Spa in MASAKI  and ONLINE on JUMIA MARKET
  Tickets at Gate will be @40,000/=TZS

  9th Swahili Fashion Week & Awards Sponsored By:


  0 0  0 0

   Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Singida Bw. Buhacha Baltazar Kichinda ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya utawala na rasilimali watu akiwaaga Vijana 43 wanaojiunga na kambi ya JKT Makutopora kikosi cha KJ 834 kwa hiyari kwa mkataba wa miaka ya miwili. Bw. Kichinda amesema wakiwa jeshini watafundishwa uzalendo, ukakamavu, stadi za jamii na nidhamu. Pia amewaasa wazazi kuwapeleka shule watoto wao  na kupokea fursa kama za jeshi.
  Kulia ni Afisa Tawala ofisi ya Mshauri wa Mgambo Meja Rhinocerus Magembesoni 

   Vijana 43 wa Kihadzabe wakipanda mabasi kuelekea katika kambi ya JKT Makutopora kikosi cha KJ 834 kujiunga na kikosi hicho kwa hiyari kwa mkataba wa miaka ya miwili mara baada ya kuagwa na mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Singida. Jamii ya kihadzabe huendesha maisha yao kwa kuwinda na kula nyama pori, matunda ya porini, asali na mizizi.
   Mmoja wa kijana wa kihadzabe Zuhura Ramadhani Longa ambaye alikuwa akiwasindikiza vijana wenzake kuwinda na kurina asali, amesema ameamua kujiunga na jeshi ili aweze kuisaidia familia yake lakini pia aweze kulitumikia Taifa.
   Vijana 43 wa Kihadzabe wakipunga mikono kuonyesha utayari wa kujiunga na kambi ya JKT Makutopora kikosi cha KJ 834 kwa hiyari kwa mkataba wa miaka ya miwili mara baada ya kuagwa na mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Singida. Jamii ya kihadzabe huendesha maisha yao kwa kuwinda na kula nyama pori, matunda ya porini, asali na mizizi.
  Vijana wa Kihadzabe ambao walikuwa wanawinda na kurina asali, wamesema wameamua kujiunga na jeshi ili waweze kusaidia familia zao na pia kulitumikia Taifa. Picha na Ofisi ya RC Singida

  0 0  0 0


  0 0

  WANAWAKE NA MAENDELEO FOUNDATION

  D A R ES SALAAM | IJUMAA |DESEMBA 2, 2016

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


  Katika gazeti la Raia Mwema toleo No 486 la Tarehe 30 Novemba, 2016 kumeandikwa habari yenye kichwa kilichosomeka “Mali za Salma Kikwete kuuzwa kwa mnada?”.  Katika habari hiyo kumetolewa madai ati kwamba taasisi ya WAMA inayoongozwa na Mheshimiwa Mama Salma Kikwete inao mzigo mkubwa bandarini ambao haujalipiwa ushuru na kodi. Na kwa sababu hiyo, Mamlaka ya Mapato Tanzania imepanga kuuza mali hizo.

  Kwa niaba ya Taasisi ya WAMA napenda kutoa masikitiko yetu kwamba habari hizo ni za uongo na hazina ukweli wowote. Kwa maoni yetu gazeti hilo lina dhamira mbaya dhidi ya Taasisi ya WAMA na Mwenyekiti wake, Mheshimiwa Mama Salma Kikwete. Nia yao ni kupaka matope na kuchafua majina na sifa ya taasisi yetu na kiongozi wake.

  Ukweli kuhusu jambo hili ni kwamba, WAMA ilitumiwa maboksi Kumi na Moja (11) ya vitabu vikiwa ni zawadi (grant) kutoka Nakayama Foundation ya Japani ambayo ndiyo iliyofadhili ujenzi wa Shule ya Sekondari ya WAMA-Nakayama iliyopo Nyamisati, Kibiti. Maboksi hayo yaliyotumwa kupitia BL 243016002211 yaliwasili bandarini tarehe 27/06/2016. Yalitolewa tarehe 10/8/2016 baada ya WAMA kulipia kodi zote na ushuru wote unaotahili tarehe 26/07/2016.

  Vitabu hivyo vimekwishapelekwa shuleni na wanafunzi wanavitumia. Hakuna mzigo wowote wa Taasisi ya WAMA uliopo bandarini unaosubiri kutolewa wala kuuzwa na TRA. Hivyo basi, gazeti hilo kuandika kuwepo kwa mzigo mkubwa wa WAMA bandarini ni jambo la kughushi ambalo limefanywa kwa dhamira mbaya na kwa sababu wanazozijua wao.

  Tumelitaka gazeti la Raia Mwema limuombe radhi Mwenyekiti wa WAMA Mheshimiwa Mama Salma Kikwete na kuiomba radhi WAMA Foundation kwa kuandika taarifa za uongo. Gazeti hilo limechafua sifa ya Mwenyekiti wa WAMA na WAMA Foundation kiasi ambacho wanao wajibu wa kuomba radhi na kusafisha majina na heshima zetu mbele ya jamii.

  Ikiwa hawatatekeleza haya ndani ya kipindi cha siku Saba, yaani kabla ya tarehe 07 Desemba, 2016, tutalazimika kuchukua hatua zipasazo za kisheria.


  Daudi Nasib,

  Katibu Mtendaji,

  Dar es Salaam,

  Tel: +255 22 2781287


  info@wamafoundation.or.tz


  0 0


  0 0

  Mshehereshaji katika Tamasha la Kimataifa la Maonyesho ya Mitindo la "Swahili Fashion Week" lililoanza rasmi usiku wa Desemba 2, 2016 katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar es salaam, Lilian Kamazima akizungumza wakati wa kuwashukuru wadhamini mbalimbali waliolifanikisha Tamasha hilo, ikiwemo Globu ya Jamii. Tamasha hilo lileanza rasmi Desemba 2 na linatarajiwa kumalizika Desemba 4, 2016.

  Mbunifu wa Mitindo ya Mavazi nchini, Jamilla VeraSwai akipita jukwaani baada ya Wanamitindo kuonyesha mavazi yake.
  Mbunifu wa Mitindo ya Mavazi nchini, Lilian Patropa akipita jukwaani kuwashukuru watazamaji baada ya Wanamitindo kupita kuonyesha mavazi yake.

  0 0

  Every year, International Day of Persons with Disabilities is an opportunity for the world to stand together against the discrimination of women and men with disabilities and to raise the flag for inclusion and empowerment through education, the sciences, culture and communication and information. 

    The 2030 Agenda for Sustainable Development connects inclusion and development – this is vital, because persons with disabilities continue to face discrimination, violence, stigma, and exclusion. This is particularly true for the most vulnerable groups in society, such as migrants, refugees and indigenous people with disabilities.

   Women and girls also shoulder heavy burdens, lacking opportunities, at greater risk from abuse, violence and exclusion. These challenges throw a shadow over societies as a whole.In this year of action to take forward the 2030 Agenda, our message is clear -- sustainable development will not be possible without the full inclusion of persons with disabilities at every level, without their roles and voices built into all decision-making and policies. 

    UNESCO is pulling out all the stops to support implementation of the 2006 United Nations Convention on the Rights of Persons with Disabilities and to take forward the new Sustainable Development Goals. We need redoubled efforts to ensure that all women and men with disabilities around the world are integrated fully into all aspects of social, political, cultural and economic life, to build a world that is pluralistic, open, participatory and knowledge-based. 

  This is how our societies will become truly inclusive.This must begin with education. UNESCO is leading support to its Member States to implement SDG4-Education 2030, which commits all countries to ensure equal access to all levels of education and vocational training, regardless of disability status.We must raise visibility for stronger advocacy. 

  This is the importance of the UNESCO/Emir Jaber al-Ahmad al-Jaber al-Sabah Prize for Digital Empowerment of Persons with Disabilities, which will recognize this year the outstanding contribution of individuals and organizations in promoting the inclusion and accessibility, and enhancing the lives of persons with disabilities through application of digital solutions, resources and technologies. 

  UNESCO has also revised the International Charter of Physical Education, Physical Activity and Sport, to reinforce physical education, physical activity and sport around the world, and the Organisation is accompanying Member States in reviewing national physical education policies to become child-centered, flexible, sensitive, and inclusive, independently of abilities. 

    In this spirit, we dedicate the 2016 International Day of Persons with Disabilities to promoting the 17 Sustainable Development Goals, to build together a more inclusive and equitable world for all.

  0 0  SIMU.TV: Waziri mkuu Kassim Majaliwa ameitaka idara ya uhamiaji nchini kudhibiti kwa uhakika wahamiaji haramu nchini; https://youtu.be/PGP6JbSVzSk

  SIMU.TV: Siku chache baada ya agizo la Rais Magufuli kupiga marufuku uagizaji wa sare za jeshi kutoka kwa watu binafsi, wizara husika zimeanza kuchukua hatua kudhibiti biashara hiyo; https://youtu.be/P_3z1pxdzMU

  SIMU.TV: Serikali imetaifisha tani tano za samaki aina ya Sangara waliokamatwa baada ya kuvuliwa kinyume cha sheria huko mkoani Mwanza; https://youtu.be/hGSOK_QDTOY

  SIMU.TV: Uongozi wa wilaya ya Morogoro umewataka wafugaji wanaolisha mifugo yao katika shamba la Mkulazi kuondoka katika eneo hilo kupisha uwekezaji; https://youtu.be/2P8VQMfpliE

  SIMU.TV: Wizara ya Afya kupitia bodi ya maabara binafsi imezitaka kufungiwa kwa maabara bubu zilizozagaa mkoani Geita ambazo zinaendeshwa kinyume na sheria; https://youtu.be/uVs47Jve0_w


  0 0

  Na Henry Mdimu
  Mtangazaji machachari wa vipindi vya TV aliyevunja rekodi katika ukosoaji uliotukuka, Salama Jabir (pichani) ametajwa kuwa ndiye atakayeendesha tuzo za EATV Jumamosi ijayo  katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
  Roy Mbowe, Mratibu Mkuu wa tunzo hizo amable pia ni mkuu wa Masoko wa EATV amemtaja mwanadada huyo jana usiku saa nne kwamba ndiye atakayekuwa Mc kwa masaa matatu mfululizo akiongoza shughuli hiyo ambayo itarushwa live na kituo cha EATV pekee.
  Jumla ya tuzo tisa zitatolewa kwa wasanii wa muziki na filamu waliofanya vyema kwenye tasnia hiyo huku tuzo moja ya heshima ikitolewa kwa mdau mwenye mchango uliotukuka katika tasnia ya sanaa kwa mwaka 2015/16.  0 0

  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

  Chuo Kikuu cha Ardhi kimetoa zawadi na tuzo kwa wanafunzi 104 waliofanya vizuri kitaaluma ili kutoa hamasa kwa wanafunzi wengine kuweka juhudi katika masomo.

  Zawadi hizo zimetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Idrissa Mshoro ambaye ametangaza kuwa jumla ya wanafunzi wanne kati ya waliofanya vizuri wamepata alama sawa hivyo kuibuka washindi wa jumla kwa mwaka 2016. 

  Akisoma hotuba wakati wa sherehe hizo, Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho (Taaluma), Prof. Gabriel Kassenga amesema kuwa sherehe hizo zimekuwa zikiwezeshwa na wadau mbalimbali waliojitoa kwa hali na mali kutoa zawadi na tuzo kwa wanafunzi waliofaulu vizuri kwenye vipengele mbalimbali vya taaluma hivyo amewasihi wadau hao kuendelee kuunga mkono jitihada zinazofanywa na wanafunzi hao ili kuwashawishi wanafunzi wengine kufanya vizuri.

  “Zawadi mbalimbali zinazotolewa na wafadhili zimekua zikiwasaidia wanafunzi hawa kuongeza tija kwenye maisha yao ya kielimu na kiuchumi kwani wengi wao wamekuwa wakizitumia fedha hizo kama mitaji ya kufanyia biashara pindi wamalizapo masomo yao,”alisema Prof. Kassenga.
  Amefafanua kuwa mwaka huu umekuwa wa tofauti kwani idadi ya wanafunzi wanawake na wanaume waliopata tuzo hizo iko sawa tofauti na miaka mitatu iliyopita ambapo wanawake walikua wakiongoza kwa asilimia 3.7 kwa kupata tuzo nyingi wakati wanaume wakiwa ni asilimia 2.2. 

  Prof. Kassenga ametaja baadhi ya zawadi zilizotolewa na wafadhili walioshiriki katika shughuli hiyo kuwa ni vyeti, Kompyuta mpakato (laptop),vifaa vinavyotumika katika kupimaji wa ardhi pamoja na fedha taslimu.Aidha, Prof. Kassenga ametoa rai kwa kwa wanafunzi wote waliomaliza chuoni hapo kuwa juhudi walizokuwa wakizionyesha wakati wa masomo waende wakaziendeleze katika jamii zinazowazunguka pamoja na kwenye shughuli mbalimbali za ujenzi wa Taifa ili wakawe mfano bora kwa vizazi vijavyo.

  Kwa upande wake Emily Elandogo ambaye ni mmoja kati ya wanafunzi waliopewa zawadi hizo amewashukuru walimu wa chuo hicho kwa elimu wanayoitoa ambayo itakua ni chanzo cha kuwaletea maendeleo sehemu yoyote watakapokuwa pia ametoa ushauri kwa wanafunzi wenzake kuitumia vizuri elimu waliyoipata ili iweze kuwasaidia katika maisha yao. 

  Mahafali ya Kumi ya chuo hicho yanategemewa kufanyika Disemba 3 mwaka huu katika viwanja va chuo hicho ambapo wahitimu wa shahada mbalimbali watatunukiwa stahili pamoja na vyeti vyao.  
  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi, Prof. Idrissa Mshoro (katikati kulia) akiteta jambo na Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho (Taaluma), Prof. Gabriel Kassenga(katikati kushoto), pembeni kulia ni Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa chuo hicho (Mipango, Fedha na Utawala),Prof. Robert Kiunsi, pembeni kushoto ni Maafisa Waandamizi wa chuo hicho. Shughuli hizo zimefanyika leo Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya chuo hicho.
  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi, Prof. Idrissa Mshoro akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa chuo na wanafunzi waliofanya vizuri kitaaluma wakati wa shughuli za ugawaji wa vyeti na zawadi kwa wanafunzi waliofaulu masomo mbalimbali uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya chuo hicho.
  Mmoja kati ya washindi wa jumla wenye alama za juu, Anyighwile Lwijiso akipokea zawadi kutoka kwa mmoja wa wafadhili ambao ni Kampuni ya Hightech System mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi. Shughuli hizo zimefanyika leo Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya chuo hicho.

  0 0


  0 0

   Kamanda wa kikosi cha askari wa usalama barabarani wa Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Awadhi Haji akiongea na madereva wa daladala mapema asubuhi leo jijini humo baada ya kukamata baadhi yao wakiendesha magari wakiwa wamelewa. ACP Haji amewataka madereva hao na waendesha vyombo vya moto wengine kujiepusha na jinai hiyo ya kuendesha gari wakiwa wamelewa kwani ni hatari kwao binafsi na kwa watumiaji wa barabara. Amesema zoezi hilo la ukaguzi wa madereva wanaofanya kazi wakiwa wamelewa ni endelevu na kwamba atakayepatikana atachukuliwa sheria mara moja bila simile.
  Mmoja wa madereva wa daladala akipimwa pumzi kuona kama amelewa ama la. Madereva kadhaa walikutwa wamelewa na kuchukulia hatua.

  0 0
 • 12/02/16--23:41: JE UNAHITAJI PILIPILI KALI?
 • KARIBU KALI NI PILIPILI INAYOTENGENEZWA NCHINI UINGEREZA NA WATANZANIA. KWA MUHITAJI WASILIANA NASI...
  MK GLOBAL TRADE LTD
  TEL :44 01908 237175
  THANKS

  0 0
 • 12/02/16--23:42: Article 6


 • 0 0


  SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) linawatangazia wateja wake wa Mikoa ya Dodoma, Singida, Shinyanga, Tabora, Mwanza,  Geita, Mara, Simiyu na na baadhi ya maeneo ya Mikoa ya  Arusha, Manyara, Kilimanjaro  na Tanga na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Dar es Salaam (Tazara, Mlimani City, Mandela Road, Ubungo na Kimara, Sinza, Mabibo) kuwa yatakosa Umeme siku ya Jumapili DESEMBA 04, 2016 kuanzia saa 02:00 Asubuhi hadi saa 11.00 Jioni.

  SABABU: Kuruhusu Mkandarasi anayejenga Njia Kuu ya Kusafirisha Umeme ya Msongo Mkubwa ya Kilovolti 400 maarufu kama (Backbone Transmission Line 400 kV) kutoka Iringa hadi Shinyanga.

  SABABU: Kuzimwa kwa njia ya Umeme ya Msongo wa Kilovolti 33 Kituo cha Ubungo Dar es Salaam ili kumruhusu Mkandarasi kufanya matengenezo yenye lengo la kuboresha na kuimarisha hali ya upatikanaji wa Umeme Nchini.  

  Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

  Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano

  TANESCO Makao Makuu

   
   Mhandisi wa umeme wa TANESCO akiwa kazini jijini Dar es Salaam
older | 1 | .... | 1448 | 1449 | (Page 1450) | 1451 | 1452 | .... | 3286 | newer