Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

ARUSHA EMERGING AND LARGE CORPORATES TO BENEFIT FROM NMB EXECUTIVE NETWORK

$
0
0
National Microfinance Bank Plc (NMB) has today organized a meeting event of NMB Executive Network members from Northern zone, a meeting that brought together over 120 corporates which includes our existing and prospect customers.

NMB Executive Network is a forum that started in 2014 by targeting major cities DSM, Mwanza, Mbeya, Morogoro, Arusha and Kilimanjaro which has as well been extended to other big Regions.

The main aim of the network is to foster rewarding relationship with NMB business customers. This is achieved by providing forums for customers to explore business opportunities through training, capacity building and networking opportunities.
The NMB Chief of Wholesale Banking Officer Mr. Richard Makungwa, said that the aim of holding such meetings is to strengthen business relations with its top end business and corporate customers.

“NMB is committed in ensuring that we do continuous improvement of products and services to match the changing needs of customers. This is achieved through feedback from customers and their segmentation,” Said Mr. Makungwa.

Mr. Makungwa further said that improvements done by the bank so far will help to bring services more close to this segment of customers where they will not only get the best services but also acquire various trainings including the ones received at the meeting on Wellness and Governance.

Members of the Executive Network normally get trained on capacity building in areas affecting business (Business planning, Taxation, Business Regulations), sponsorship to major trade countries (China, Hong Kong, Dubai), Fast track counters at all NMB Branches, Preferential forex rates, Special customer ID as a recognition to all NMB Branches – all these are done in order to support businesses become and remain competitive.

Mr. Makungwa said that corporate customers use NMB services for current account and payments while others use NMB for internet banking or trade finance and foreign exchange. And a large proportion is using the lending products.
NMB Managing Director – Ineke Bussemaker delivering a key note address to the NMB Executive Network meeting in Arusha over the weekend. NMB organized the NMB Executive Network that brought together over 100 top ends Business Customers and corporates from Northern zone who commands the annual turnover of over TZS 10 Billion each. Limited top end SME’s customers with turnover of over TZS 2.5Billion were also invited in the gathering which among others they discussed on ways to improve their business relationship and foster rewarding relationship between the bank and its top end customers.

VETA yatoa mafunzo kwa wajasiriamali zaidi ya 200 kata ya Bunju

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

WAJASIRIAMALI zaidi ya 200 katika Kata ya Bunju jijini Dar es Salaam wamepata mafunzo ya siku 10 katika ujuzi mbalimbali ili kuwasaidia kukuza ujasiriamali na kuongeza kipato katika familia na jamii kwa ujumla. 

Mafunzo hayo yaliendeshwa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Kanda ya Dar es Salaam kuanzia tarehe 14 hadi 25,November 2016 chini ya Mpango wa Kukuza Ujasiriamali katika Sekta isiyo Rasmi (INTEP) na yalihusisha stadi za utegenezaji wa Batiki, Mapishi, Mapambo na Ufundi wa Upakaji rangi.

Akizungumza katika hafla ya kufunga Mafunzo hayo siku ya Ijumaa November 25, 2016 Afisa Mtendaji wa Kata ya Bunju Shumasike Shumasike alisema, mafunzo hayo yameongeza fursa ya ajira kwa wananchi wake na kuiomba VETA kuendelea kutoa mafunzo ya namna hiyo zaidi kwani yatawasaidia wananchi wa kawaida kwa kiasi kikubwa.

Alisema, waliopata mafunzo ni watu ambao walikuwa hawana shughuli yeyote ya kuwaingizia kipato hivyo kupata mafunzo yameonyesha njia ya kuweza kuingia katika soko la ajira kwa kuanzisha biashara mbalimbali.

Shumasike aliwaasa wanufaika wa mafunzo kutumia vyema vyeti walivyovipata na kuidhihirishia jamii kuwa ujuzi walioupata ni wa manufaa makubwa kwao na kwa jamii inayowazunguka na sio kurudi katika hali waliyokuwa nayo mwanzo.

Alisema fedha ya ahadi ya Rais iliyotolewa kwa kila mtaa kunufaika na sh. Milioni 50 kwa ajili ya wajasirimali zitatolewa kwa vikundi na sio kwa mtu mmoja mmoja hivyo wajiandae kwa kutengeneza vikundi na kuvisajili ili fedha hizo zitakapowasili waweze kunufaika.

Naye Mkurugenzi wa Kanda ya VETA Dar es Salaam, Habib Bukko alisema anaamini waliopata mafunzo hayo watayatumia ipasavyo katika kubadilisha maisha yao na kwamba VETA inaendelea na juhudi za kuhakikisha mafunzo hayo yanafikia makundi mengi zaidi.

Mmoja ya walionufaika na Mafunzo hayo, Joyce Lweganwa amesema watatumia mafunzo hayo katika kutengeneza kipato na kuitaka VETA kufikia watu wengine kutokana na ukweli kwamba wahitaji wa mafunzo ya aina hiyo ni wengi sana katika jamii.

Afisa Mtendaji wa Kata ya Bunju Shumasike Shumasike akijionea bidhaa mbalimbali za batiki zilizotengenezwa na wajasiriamali waliopatiwa mafunzo na VETA jijini Dar es Salaam.
.Sehemu ya wajasiriamali waliopata mafunzo ya mapishi wakionesha vyakula mbalimbali walivyoandaa baada ya mafunzo
Wahitimu wa mafunzo ya Upakaji rangi katika picha ya pamoja na Mtendaji wa Kata ya Bunju Shumasike Shumasike wakati wa kufunga mafunzo hayo jijini Dar es Salaam.

Moja ya kazi waliyoifanya wahitimu wa mafunzo ya upambaji waliopata mafunzo kutoka VETA kama bwana harusi na Bibi harusi .

Afisa Mtendaji wa Kata ya Bunju katika picha ya pamoja na wajasiriamali waliopata mafunzo ya utengenezaji batiki yaliyotolewa na VETA.

WAKAZI 800 WA KEREGE WAPATA HUDUMA ZA BURE ZA MATIBABU YALIYOANDALIWA NA KLABU YA ROTARY YA OYSTER BAY

$
0
0
Klabu ya Rotary ya Oyster Bay pamoja na madaktari na wafanyakazi wa kujitolea wametoa huduma za matibabu kwa wakazi wa Kerege wilayani Bagamoyo. Kambi hiyo ya matibabu imeeefanyika Jumapili tarehe 27 Novemba katika shule ya Msingi ya Kerege.

Vipimo na matibabu vilitolewa bure kwa magonjwa kama vile malaria, upungufu wa damu, kisukari na shinikizo la damu, masikio, pua na koo (ENT), magonjwa ya ngozi, macho pamoja na meno. Huduma nyingine zilizotolewa zilikuwa pamoja na ugawaji wa miwani zilizotolewa kwa watu waliokutwa na matatizo ya macho.
Zoezi la Kambi hiyo ya matibabu bure likiendelea katika mji huo wa Kerege.
Huduma za ushauri kwa wajawazito na vifaa vya kujifungulia vilitolewa bure kwa wajawazito; huduma za ushauri nasaha na upimaji wa UKIMWI pia zilitolewa. Kwa mara ya kwanza, elimu ya usafi na taulo za wanawake zilitolewa kwa wasichana.

Akizungumza katika kambi hiyo, Alfred Woiso, Rais wa Klabu ya Rotary ya Oyster Bay alisema, “Ni furaha yetu kuwa hapa kwa mara nyingine tena na tunafurahi kuona wakazi wa Kerege wamejitokeza kuja kupata huduma hizi. Tumetoa huduma kwa watu waliokuwa na matatizo mbalimbali. Tumeona wagonjwa wengi wenye magonjwa sugu kama kisukari na shinikizo la damu. Inaonekana kuna haja ya kupanua wigo wa huduma zetu kwa vile kuna mahitaji ya huduma za matibabu ya magonjwa mengine.”

Kambi hiyo ya matibabu ilihudhuriwa na wagonjwa wapatao 800 kutoka Kerege na maeneo ya jirani. Kambi hii inayoandaliwa na Klabu ya Rotary ya Oyster Bay imefanyika Kerege kwa mara ya sita sasa kwa lengo la kuwasaidia wakazi wa Kerege kupata huduma za matibabu, wakazi ambao kwa kawaida hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu.

Kambi hiyo ya matibabu imedhaminiwa na Diamond Trust Bank na kuandaliwa kwa ushirikiano na Shree Hindu Mandal Hospital, Vital Supplies, Whitedent, vClick Concepts Inc, MAK Books and Brains, ABACUS Pharmaceuticals, Fazel Foundation na wanachama wa Klabu ya Rotary na Rotaractor.
Zoezi la Kambi hiyo ya matibabu na upimaji bure likiendelea katika mji huo wa Kerege.
Mmoja wa wananchi wa Kerege (kulia) akipima macho katika kambi hiyo.

NSSF YAWAONDOA WAPANGAJI WALIOSHINDWA KULIPA KATIKA NYUMBA ZA KIJICHI

$
0
0
SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), limeendelea na kazi ya kuwaondoa wadaiwa sugu. 

Wadaiwa hao ni wale walionunua nyumba na kushindwa kulipa deni lililobaki kwa muda uliopangwa.Akizungumza jjijini Dar es Salaam, Kaimu Meneja Mipango na Uwekezaji wa NSSF, Radhia Tambwe, alisema kwamba nyumba hizo ni za Mtoni Kijichi.Radhia alisema kwamba kazi hiyo itafanyika kwa wadaiwa  saba.

“Wakazi wa nyumba zote hizo walitolewa na kampuni ya udalali ya Majembe Action Mart kwa kushirikiana na NSSF,”alisema.Aidha alisema kwamba wadaiwa hao waliondolewa katika nyumba hizo baada ya taratibu za kisheria kufuatwa hivyo nyumba hizo zitauzwa kwa watu wengine.


Aidha alisema kwamba kazi hiyo ni endelevu kwa wale watakaoshindwa kulipa madeni yao kama mikataba inavyosema.Shirika la NSSF limewataka walionunua ama kupanga nyumba kulipa kwa mujibu wa mikataba yao ili kuepuka adha ya kutolewa vyombo vyao nje na kupata hasara.
 Vyombo vya baadhi ya wakazi wa nyumba za Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam vikitolewa nje baada ya wamiliki wa nyumba kushindwa kulipia nyumba hizo kwa mujibu mikataba waliyokubaliana na Shirika hilo. (Picha na Francis Dande).

UN NA EU WAENDELEZA KAMPENI YA UELEWA WA MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU

$
0
0
UMOJA wa Ulaya (EU) na Umoja wa Mataifa (UN) wamejiunga pamoja kuendesha kampeni ya uelewa wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) nchini Tanzania . Aidha kwa pamoja wamezuru miradi iliyofadhiliwa na EU. Wakiwa Mkoani Iringa wamepata nafasi ya kuzungumza na wanachuo 1,000 kutoka vyuo vikuu vya Iringa na Mkwawa kwenye semina iliyoelezea malengo hayo ya dunia ambayo ni sehemu ya ajenda 2030 ya maendeleo endelevu duniani.

 Kampeni hiyo imelenga kuwafanya vijana waelewe malengo 17 ya dunia ambayo kwa sasa yana mwaka mmoja tangu yapitishwe na kuwatanabaisha wajibu wao katika kufanikisha utekelezaji wake ndani ya mazingira ya Tanzania.

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela ripoti na makabrasha mbalimbali ya Umoja wa Mataifa mara baada ya kuhitimisha semina kuhusu SGDs kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa.
Mwongoza wageni katika Makumbusho ya mkoa wa Iringa, Deonis Mgumba akitoa maelezo ya vifaa mbalimbali vilivyokuwa vikitumika enzi za utawala wa kichifu kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto) na Katibu Tawala Msaidizi -Miundombinu wa Mkoa wa Iringa, Henry Mditi (katikati) walipotembelea makumbusho hayo mjini Iringa.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro wakitwanga mahindi kienyeji katika moja ya kinu kilichokuwa kinatumika enzi hizo za utawala wa kichifu kilichopo katika makumbusho hayo.
Mwongoza wageni katika Makumbusho ya mkoa wa Iringa, Matatizo Kastamu akitoa maelezo ya picha mbalimbali zenye kumbukumbu za utawala wa kichifu na historia ya mji wa Iringa kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro.
Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro (kushoto), Mtalaam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu na Meneja wa Mradi wa Fahari Yetu, Jan Kuever wakipitia vipeperushi vyenye maelezo ya kina ya Mradi wa Fahari Yetu unaoendesha Makumbusho na Kituo cha Utamaduni mkoa wa Iringa.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro katika picha ya pamoja kwenye sanamu maalum za mavazi ya kipindi cha utawala wa Chifu Mkwawa walipotembelea Makumbusho ya mkoa wa Iringa.

HABARI ZAIDI SOMA HAPA

WAZIRI LWENGE ATEMBELEA KIWANDA CHA KUTENGENEZA MABOMBA NCHINI

$
0
0
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge akiangalia aina ya bomba lililotumika kwenye mradi wa Ruvu Chini na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Tanzania Steel Pipes Limited, Nicolas Loh (kulia) pamoja na Meneja Biashara, Ryan Koh.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge akiwa kwenye karakana ya kiwanda hicho.
Mafundi wakiwa kazini katika karakana ya Kiwanda cha Tanzania Steel Pipes Limited.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge akimsikiliza Mkurugenzi wa Kiwanda cha Tanzania Steel Pipes Limited, Nicolas Loh na kujionea moja ya mabomba yanayotengenezwa na kiwanda hicho.

……………………………………………………..

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge mwishoni mwa wiki alitembelea Kiwanda cha Tanzania Steel Pipes Limited (TSP) kilichopo Shekilango, Dar es Salaam.

Kiwanda hicho kinachotengeneza mabomba ya maji, ambayo pia yanatumika katika utekelezaji wa miradi ya maji nchini, ukiwemo mradi ya maji ya Ruvu Chini, KASHWASA na Ruvuma.

“Nimeridhishwa na uwekezaji wa kiwanda hiki cha mabomba, ambacho kina uwezo wa kuzalisha mabomba yenye ubora wa kutekeleza miradi yetu ya maji nchini”.

“Hii ni hatua kubwa kwa nchi yetu ikizingatiwa kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuinua uchumi wa viwanda nchini, hivyo maendeleo ya kiwanda hiki ni hatua nzuri ya kufikia lengo hilo”, alisema Waziri Lwenge.

Inj. Lwenge alisema uwezo ilionao kiwanda hiki ni chachu ya maendeleo kwa Sekta ya Maji na Umwagiliaji kwani kwa muda mrefu Serikali imekuwa ikununua mabomba kutoka nje ya nchi, na hata yanayotengenezwa hapa mengi ni ya plastiki ambayo hayadumu muda mrefu ukilinganisha na ya chuma.

Naye Mkurugenzi wa kiwanda cha Kiwanda cha Tanzania Steel Pipes Limited (TSP) alisema nia yao kubwa ni kutengeneza bidhaa nzuri zenye ubora wa kimataifa na kushindana katika soko la kimataifa, na kuiomba Serikali itumie bidhaa za wawekezaji wa ndani zenye ubora wa hali ya juu.

Alisisitiza bidhaa zao zinatengenezwa hapa nchini tangu hatua ya awali na wala si kuagizwa kutoka nje, zina uwezo wa kudumu mpaka miaka 50, zinatumika nje ya nchi ikiwemo Rwanda, ambapo zinatumika kwenye miradi mikubwa ya maji.

Dhumuni la ziara hiyo lilikuwa ni kujionea uwezo wa kiwanda hicho kwa upande wa uzalishaji na ubora wa bidhaa zao.

WAZIRI NAPE NNAUYE APOKEA PICHA YA RAIS DK JOHN POMBE MAGUFULI ILIYOCHORWA NA KIKUNDI CHA ANGAVU

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye (kulia) akipokea picha ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kutoka kwa Mwenyekiti wa Angavu Youth Group Athumani Salum (kulia) leo jijjini Dar es Salaam. Picha hiyo imechorwa kwa ustadi na kikundi cha Angavu Youth Group.
Muonekano wa picha ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli iliyoichora kwa ustadi na kikundi cha Angavu Youth Group ambapo imekabidhiwa leo jijini Dar es Salaam kwa Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye kwa niaba ya Mheshimiwa Rais.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kabla ya makabidhiano ya picha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli iliyochorwa na kikundi cha Angavu Youth Group leo jijini Dar es Salaam. Picha hiyo imekabidhiwa kwa Waziri huyo kwa niaba ya Mhe. Rais. kushoto ni Mwenyekiti wa Angavu Youth Group Bw. Athumani Salum na kulia ni Katibu wake Bi. Oliver Charles.Picha na Anitha Jonas – MAELEZO
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye (kulia) akisikiliza kwa makini hotuba iliyokuwa ikisomwa na Katibu wa Angavu Youth Group Bi.Oliver Charles (katikati) wakati wa makabidhiano ya picha ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo jijini Dar es Salaam.

RAIS DKT. MAGUFULI AMWANDALIA RAIS EDGAR LUNGU DHIFA YA KITAIFA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na  mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Lungu wakiwasili katika ukumbi wa Ikulu kwa dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Ikulu jijini Dar es salaam usiku huu.
 Meza kuu ikiwa imesimama kwa Wimbo wa Taifa
 Rais Dkt Magufuli akimsindikiza mgeni wake Rais Edgar Lungu wa Zambia kusalimiana na viongozi mbalimbali
 Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi. Kulia ni Naibu Spika Dkt Tulia Ackson
 Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa dhifa hiyo
 Rais Dkt Magufuli akigonganisha glasi na mgeni wake Rais Edgar Lungu wa Zambia katika dhifa hiyo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

WAZIRI NAPE ATUMA SALAMU ZA PONGEZI KWA RAIS WA CHAMA CHA RIADHA TANZANIA

JAFFO AFUNGUA MAFUNZO YA SHERIA YA MANUNUZI YA UMMA MKOANI DODOMA

$
0
0
Naibu Waziri Jaffo ametoa kauli hiyo alipokuwa akifungua mafunzo ya Sheria ya Manunuzi ya Umma inayoendeshwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) kwa Maafisa Masuhuli, Wenyeviti wa Bodi za Zabuni, Wakuu wa Vitengo vya Usimamizi wa Manunuzi na Idara Nunuzi inayofanyika mjini Dodoma.

Amesema uzoefu unaonesha kuwa baadhi ya watumishi wa Umma ambao wamepewa dhamana ya kusimamia michakato ya manunuzi kwenye taasisi zao wamekuwa hatekelezi wajibu wao ipasavyo na hivyo kusababisha kupatikana kwa wazabuni ambao hawana uwezo wa kutekeleza kazi husika aau kazi kutekelezwa chini ya kiwango.



Akitolea mfano baadhi yao, Naibu Waziri Jaffo amesema “baadhi ya wajumbe wa bodi za zabuni wamekuwa wakishiriki katika vitendo visivyo vya kiuadilifu na mwisho tunapata wazabuni wasio na vigezo na hivyo kusababisha hasara kwa Serikali”.



Alitoa pia wito kwa wakuu wa taasisi za umma kuepuka vitendo vya mgongano wa kimaslahi kwenye michakato ya manunuzi ya umma na kutokubali kuyumbishwa na wasiasa. “Naomba kuwasihi wakuu wa taasisi msikubali kuyumbishwa na wanasiasa ambao wameingiza kampuni zao kwenye michakato ya manunuzi kwani hali hiyo husababisha kazi nyingi kutekelezwa chini ya kiwango na hivyo kukosa thamani ya fedha kwenye miradi inayotekelezwa kwa fedha za Umma,” alisema Naibu Waziri.



Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Dkt. Laurent Shirima, alielezea baadhi ya maeneo yenye changamoto kubwa kwenye manunuzi ya umma kuwa ni pamoja na usimamizi wa mikataba ya manunuzi. “Eneo la utekelezaji wa mikataba ndilo linalotumia fedha nyingi kwenye mchakato mzima wa manunuzi ya umma. Hivyo usimamizi mzuri katika eneo hili ni muhimu sana, lakini tumeshuhudia mapungufu mengi kwenye eneo hili kupitia ukaguzi ambao ambao tumeufanya katika mwaka wa fedha 2015/16,” alisema Dkt. Shirima.


Mafunzo hayo yanayoendeshwa na PPRA ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, ya kuitaka Mamlaka hiyo kuwapatia mafunzo kuhusu sheria ya manunuzi wakuu wa taasisi za umma ili wawe na uelewa wa kutosha katika kusimamia shughuli za manunuzi ya umma kwenye taasisi zao.



Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mheshimiwa Selemani Said Jaffo amewataka watumishi wa Umma wanaoshiriki kwenye michakato ya manunuzi kuzingatia udilifu wakati wanapotekeleza majukumu yao ili kuzuia upotevu wa fedha za serikali zinazoelekezwa kwenye manunuzi mbalimbali.

MANUNUZI YA PAMOJA KUPITIA GPSA: SERIKALI YAOKOA BILIONI MOJA KWENYE MAGARI

$
0
0
Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) Jacob Kibona akiwaonyesha Waandishi wa Habari (hawapo pichani) Kitabu cha wageni chenye nembo ya serikali, alisema wakala wake pekee ndiyo wenye mamlaka ya kusambaza vitabu hivyo na nyaraka mbalimbali za serikali zenye nembo hiyo kwa taasisi za umma kwa lengo la kulinda uhalisia wa nembo ya serikali yenye alama ya Bibi na Bwana.

Na Barnabas Lugwisha

Serikali kupitia Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) hivi karibuni imeokoa shilling bilioni 1.3 baada ya wakala hiyo kununua kwa pamoja magari 392 katika mpango wa serikali wa manunuzi ya pamoja.

Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala hiyo, Bw Jacob Kibona, amewaambia Waandishi wa Habari jana kuwa fedha hizo zimeokolewa na serikali baada ya kununua magari 392 kwa pamoja kwa Sh. bilioni 56.1 badala ya shilingibilioni 58.1 iwapo kila taasisi ingenunua magari yake.

“Kwa kweli huu mpango wa manunuzi yapamoja ni mpango mzuri sana ambao unaiwezesha serikali kuokoa fedha nyingi,” Alisema

Alisema fedha zilizookolewa zitaiwezesha serikali kufanya shughuli nyingine za maendeleo ya ummana kama vile kuboresha miundombinu ya barabara, huduma za afya na elimu.
 
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) Jacob Kibona akiwaonyesha waandishi wa Habari (hawapo pichani) faili lenye nembo ya serikali, alisema wakala wake pekee ndiyo wenye mamlaka ya kusambaza mafaili hayo kwa lengo la kulinda uhalisia wa nembo ya serikali yenye alama ya Bibi na Bwana.


Amesema taasisi yake pia katika kipindi cha Julai hadi Oktobamwaka huu, imezikabidhi taasisi za serikali magari ya aina mbalimbali yapatayo 136.

SERIKALI YA TANZANIA NA CHINA KUENDELEA KUSHIRIKIANA KATIKA KUENDELEZA SEKTA YA HABARI

$
0
0
Na Shamimu Nyaki-WHUSM.

Serikali  imeahidi kuendeleza ushirikiano na Serikali ya China katika kuimarisha sekta ya habari  ili kuendana  na kasi ya mabadiliko ya teknolojia ya utoaji wa habari.

Hayo  yamesemwa na Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye  jana Jijini Dar es Salaam katika mazungumzo  na Naibu  Waziri wa Uenezi  wa China Ndg. Sun Zhijun yaliyolenga kuimarisha sekta ya habari nchini.

“Tunashukuru kwa uhusiano mzuri uliopo baina ya serikali zetu  ikiwemo hii ya  kuendeleza sekta ya habari ambayo ni muhimu  na inamchango mkubwa katika kuleta maendeleo na kutoa ajira kwa watanzania”.Alisema Mhe Nape.
Mhe. Nape anaongeza kuwa ushirikiano huo  utasaidia nchi zote mbili kuwa na uwezo wa kuwafikia wananchi kwa ukaribu zaidi kupitia vipindi mbalimbali vinatakavyokuwa vikirushwa na vyombo vya habari vya nchi hizo kwa lugha zote mbili.

Kwa upande wake Mhe. Naibu Waziri wa Uenezi wa China Mhe.Sun Zhijun ameahidi kufanya mageuzi katika soko la habari kupitia radio na Luninga ambazo  zitatoa fursa ya kuonyesha vipindi mbalimbali vya Kiswahili na hivyo kusaidia katika kukuza na kueneza lugha hiyo.

“Ushirikiano wetu ni wa tangu enzi na enzi hivyo ni budi kuutunza na kuulinda umoja wetu ndo maana tukaona kuna umuhimu  wa kuimarisha  sekta ya habari ambapo Serikali yetu ya China itakuwa ikirusha  vipindi vya radio na luninga kama vile muziki na filamu za kiswahili katika vyombo vyetu vya habari ”.Alisema Mhe.Zhijun.

Vyombo vya Habari vya Tanzania na China vimekuwa vikishirikiana katika kubadilishana Habari na vipindi mbalimbali kupitia Chaneli zao na hivyo kusaidia ushirikiano kati ya nchi hizi mbili kuendelea  kuimarika na kustawi zaidi.
 Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na wajumbe wa Serikali ya China (Hawapo pichani) wakati wa mazungumzo ya kuimarisha sekta ya habari  nchini yaliyofanyika  jana  Jijini Dar es Salaam.


 Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (wa tatu kushoto) akiwa na ujumbe wa Serikali ya China wakati wa mazungumzo ya kuimarisha sekta ya habari  nchini yaliyofanyika  jana Jijini Dar es Salaam.Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC).

Mtanzania wa Kwanza Kupanda Mlima Evarest Katika Mwaka 2012 na wa Tatu Kupanda Mlima Huo Mkubwa Duniani

$
0
0
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said, akimtambulisha Mgeni wake Ndg Wilfred Moshi kwa Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zuberi Ali Maulid, alipofika kutembelea na kujionea shughuli za Baraza la Wawakilishi wakati wa Mkutano wake leo asubuhi.  
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Mtanzania wa Kwanza na Muafrika wa Tatu Duniani kupanda Mlima wa Evarest Ndg Wilfred Moshi alipofika katika jengo la Baraza la wawakilishi Zanzibar akiwa mgeni wa Mhe Simai Mohammed Said Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akimsikiliza Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akitowa maelezo ya mgeni wake Ndg Wilfred Moshi ambae ni Mtanzania wa Kwanza kupanda Mlima Evarest.
Ndg Wilfred Moshi akitowa historia yake kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipofika katika majengo ya Baraza la Wawakilishi kwa mualiko wa Mhe. Simai Mohammed Said Mwakilishi wa Tunguu Zanzibar. akitowa historia yake ya kufanikiwa kupanda mlima huo mkubwa duniani na kuelezea tayari ameshapanda Mlima Kilimanjaro zaidi ya mara 100.  

Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot.

KONGAMANO LA PANDA LAWAKUTANISHA WANAFUNZI WA KIKE TOKA VYUO MBALIMBALI NCHINI

$
0
0
Mwanzilishi wa Taasisi ya Her Initiative, Lydia Charles (kushoto) akimtambulisha Mwenyekiti mpya wa Taasisi hiyo, Irene Enock wakati wa Kongamano la siku moja lililowajumuisha wanafunzi wakike kutoka vyuo mbalimbali nchini pamoja na wadau mbalimbali wanaojishughulisha na biashara, ujasiriamali na vyombo vya habari, likiwa na lengo la kukuza upeo na uelewa wa wasichana katika maswala mbalimbali ya maendeleo. Kondamano hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Yombo 4 ndani ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

Her Initiative iliyojulikana mwanzo kama Teen Girls Supportive Initiative (TGSI) kwa kushirikiana na DUMA waliandaa Kongamano lililojulikana kama Panda. Kongamano hilo liliwajumuisha wanafunzi wakike kutoka vyuo mbalimbali nchini pamoja na wadau mbalimbali wanaojishughulisha na biashara, ujasiriamali na vyombo vya habari yote katika lengo la kukuza upeo na uelewa wa wasichana katika maswala mbalimbali ya maendeleo.

Her Initiative ni asasi ya wasichana ambayo ndio mhimili wa maongezi. Her Initiative inawapa wasichana nafasi ya kuwakilisha na kusimamia maswala yao wenyewe ya kiuchumi, elimu, kiutamaduni na kiafya, na inamjengea uwezo msichana wa kutafuta suluhu ya changamoto zake mwenyewe bila kutegemea watu wengine. Vyote hivi hufanyika kupitia kampeni, matamasha, semina na kuwapa msaada wa mahitaji ya kielimu, kiuchumi na kiafya kwa kushirikiana na wadhamini mbalimbali.

Panda ni event inayohusu ujasiriamali, uvumbuzi, ubunifu na matumizi mazuri ya pesa. Kama tunavyofahamu, wasichana tuna matumizi mengi ya pesa na mara nyingi matumizi haya huzidi kipato cha pesa tunachokipata. Kwa kuona hilo wasichana hao waliamua kuandaa tamasha ili kusaidiana kuepuka hatari zinazoweza kutokana na kutokuwa na uchumi imara. Madhumuni ni kumjengea msichana hali ya kujitegemea kwa kumfundisha namna ya kuhifadhi pesa kupitia benki tofauti na mifuko mbalimbali ya jamii.

Mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Yombo 4 ndani ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam, ulifunguliwa na Mbunge wa Jimbo la Handeni Vijijini, Mboni Mhita ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika shughuli hii. Wageni wengine waliohudhuria na kutoa maneno ya ushauri kwa wasichana ni pamoja na Dr. Sebastian Ndege "CEO wa Jembe Group ", Shekha Nasser wa Shear Illusions, Irene Kiwia mwanzilishi wa Frontline Portel Novelli, Vanessa Mdee Mwanamuziki,Mc Pilipili Mchekeshaji, Idriss Sultan Mchekeshaji na Millard Ayo mmiliki wa online Television.
Mbunge wa Jimbo la Handeni Vijijini, Mboni Mhita ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika Kongamano hilo, akitoa nasaha zake kwa wanafunzi wakike kutoka vyuo mbalimbali nchini katika kukuza upeo na uelewa wa wasichana katika maswala mbalimbali ya maendeleo.
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jembe Group, Dkt. Sebastian Ndege akitoa mada katika Kongamano la siku moja lililowajumuisha wanafunzi wakike kutoka vyuo mbalimbali nchini pamoja na wadau mbalimbali wanaojishughulisha na biashara, ujasiriamali na vyombo vya habari, likiwa na lengo la kukuza upeo na uelewa wa wasichana katika maswala mbalimbali ya maendeleo. Kondamano hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Yombo 4 ndani ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Shear Illusions, Shekha Nasser akitoa mada katika Kongamano la siku moja lililowajumuisha wanafunzi wakike kutoka vyuo mbalimbali nchini pamoja na wadau mbalimbali wanaojishughulisha na biashara, ujasiriamali na vyombo vya habari, likiwa na lengo la kukuza upeo na uelewa wa wasichana katika maswala mbalimbali ya maendeleo. Kondamano hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Yombo 4 ndani ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

PROFESA MUHONGO, WAZIRI WA NISHATI ZAMBIA WAKUTANA KUZUNGUMZIA BOMBA LA TAZAMA

$
0
0

Na Veronica Simba.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Waziri wa Nishati wa Zambia, David Mabumba, wamekutana na kufanya mazungumzo kuhusu kuboresha Bomba la Mafuta la TAZAMA ili liweze kuwanufaisha wananchi wa Tanzania na Zambia kama ilivyokusudiwa.



Mazungumzo yao yaliyofanyika mapema leo, ofisini kwa Waziri Muhongo jijini Dar es Salaam, ni kufuatia makubaliano ya marais wa nchi husika, Dk John Magufuli na Edgar Lungu; kuhusu kuboresha zaidi Bomba la TAZAMA na Reli ya TAZARA.



Marais Magufuli na Lungu, walifikia makubaliano hayo jana katika mazungumzo rasmi yaliyofanyika Ikulu ya Dar es Salaam ambayo ni mojawapo ya shughuli mbalimbali zilizopangwa katika ratiba ya ziara ya siku Tatu (3) ya Rais Lungu iliyoanza nchini Jumapili, Novemba 21 mwaka huu.



Waziri Mabumba ambaye alifuatana na Ujumbe wa Viongozi na Maafisa waandamizi kutoka TAZAMA na wizarani kwake; aliafiki mapendekezo yaliyotolewa na Waziri Muhongo kuhusu namna pande hizo mbili zitakavyoshirikiana katika utekelezaji wa agizo la Marais wao ambayo ni pamoja na wataalam wa pande zote kukutana na kufanya majadiliano pamoja na kufanya ziara kukagua utendaji kazi wa Bomba hilo.



Aidha, Mawaziri hao walijadiliana kuhusu namna ambavyo Zambia itanufaika na gesi asilia iliyogunduliwa Kusini mwa Tanzania.

Kikao hicho pia, kilihudhuriwa na viongozi waandamizi wa Wizara ya Nishati na Madini – Tanzania, akiwamo Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara, Profesa James Mdoe.


 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati), akijadiliana jambo na Waziri wa Nishati wa Zambia, David Mabumba (kushoto) na Mkurugenzi kutoka Bomba la Mafuta la TAZAMA, D. Legge (kulia).
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (Kulia), na Waziri wa Nishati wa Zambia, David Mabumba wakifurahia jambo mara baada ya mazungumzo baina yao yaliyofanyika Ofisini kwa Waziri Muhongo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) na Waziri wa Nishati wa Zambia, David Mabumba (wa tatu kutoka kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe ulioambatana na Waziri Mabumba. Wa Tatu kutoka Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu, Profesa James Mdoe.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA AFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA MTANDAO WA KUPAMBANA NA UNYOJI WA KINGONO KWA WATOTO

$
0
0
NA ANTHONY ISHENGOMA.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Sihaba Nkinga leo amefungua  mkutano wa mashauriano wa kanda ya Afrika kuhusu Mtandao wa Kuzia Unyonyaji  na Usafirishaji  wa Watoto kwa lengo la kuwafanyisha ngono.



 Akiongea katika Mkutano huo Bi Sihaba Nkinga amesema Tanzania kama mwanachama wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika imeridhia na kutekeleza mikataba mbalimbali ikiwemo kutunga sera na sheria pamoja na  mikakati ya kupambana na ukatili dhidi ya watoto.



Aliendelea kusema mwaka huu Tanzania ni Nchi pekee barani Afrika ambayo imechaguliwa kama nchi ya kuigwa kwenye juhudi za dunia kupambana ukatili wa wanawake na watoto akizataja Nchi nyingine kuwa za Mexico, Indonesia na Sweden.



Katibu Mkuu Sihaba Nkinga amesema kuwa Tanzania imechaguliwa kuwa moja ya Nchi zinazounda ushirikiano wa kimataifa wa kupambana na ukatili wa Wanawake na Watoto kwasababu ilikuwa Nchi ya pili duniani kuitikia wito wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa kutaka Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wa kufanya tafiti za ukatili dhidi ya  Wanawake na Watoto barani Afrika. 



Akiongea katika Mkutano huo wa mtandao wa kuzuia unyonyaji kingono kwa watoto Afrika Bi. Sihaba Nkinga amesema  taarifa ya utafiti huo ilyofanyika mwaka 2009 na kusambazwa mwaka 2011 ilitoa majibu ya yaliyonesha kuwepo kwa ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika ngazi zote ikiwemo ngazi ya familia, shule na njiani kuelekea shuleni.



Aidha ameviambia vyombo vya Habari vilivyokuwepo katika Mkutano huo kuwa hii ndio sababu kwasasa Tanzania inajipanga kuzindua Mpango Mkakati wa kupambana na kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto mapema tarehe 13 mwezi desemba.



Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali la KIWOEDE Bi. Justa Mwaitaka amesema mtandao huu unakutana kujadili namna bora ya kupeana taarifa za Watoto wanaosafirishwa kwa lengo la kunyonywa kingono ndio maana kuna Nchi 21 kutoka barani Afrika.



Aliongeza kuwa Mkutano huu utaangalia sheria zilizopo kama zinakidhi haja ya kupambana na ukatili dhidi ya watoto akizitaja sheria za Tanzania kuwa na utaratibu unaochelewesha upatikanaji wa haki za watoto pindi inagundulika kuwepo kwa ukatili dhidi ya watoto taratibu za kisheria na kimahakama zinakuwa ngumu katika utekelezajia wake.
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akifafanua jambo kwa vyombo vya habari kuhusu Mkutano wa Mtandao wa Kimataifa wa kuzuia unyonyaji na usafirishaji wa watoto kwa lengo la kuwafanyisha ngono unaoendelea leo jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga pamoja na baadhi ya Wajumbe wa bodi ya Mtandao wa Kupambana na Usafirishaji na unyonyaji watoto Kingono Duniani wakifuatilia maendeleo ya Mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa Mtandao wa Kupambana na Usafirishaji na unyonyaji watoto Kingono leo jijini Dar es Salaam.

MWAKILISHI WA UNICEF AKUTANA DK.SHEIN

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mwakilishi wa UNICEF katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ms. Maniza S. Zaman alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na ujumbe aliofuatana nao leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Mwakilishi wa UNICEF katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ms. Maniza S.Zaman alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na ujumbe aliofuatana nao leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Mwakilishi wa UNICEF katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ms. Maniza S.Zaman (wa pili kulia) alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na ujumbe aliofuatana nao leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Mwakilishi wa UNICEF katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ms. Maniza S.Zaman baada ya mazungumzo yao alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na ujumbe aliofuatana nao leo, [Picha na Ikulu.] 29/11/2016.

Mtanzania afungua mgahawa Sweden

$
0
0
 Mgahawa mkubwa unaotoa huduma za chakula cha Kitanzania unaomilikiwa na mpishi maarufu duniani, Issa Kapande `Chef Issa', umefunguliwa nchini Sweden na kuvunja rekodi ya dunia.Mgahawa huo ulizinduliwa na balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu.

Balozi Msechu alimpongeza Issa Kapande na mkewe kwa kufanikisha kuwapo kwa mgahawa huo ambao umeweka rekodi kuwa mgahawa mkubwa kuliko yote ya Kiafrika katika nchi za Ulaya.

Aidha, alimshukuru Torvald Brahm mwenyeji wa mji huo kwa kumuunga mkono Issa hadi kufanikisha ndoto yake ya kuwa na mgahawa wa kwanza wa Kiafrika katika mji wa Trollhattan utakatoa huduma ya chakula cha kitanzania.

Katika uzinduzi huo ambapo wenyeji wa manispaa hiyo akiwemo Meya na mwenyekiti wa Trollhattan, Paul Akerlund na msaidizi wake Peter Eriksson walikuwepo, balozi ambaye ndio kwanza ameanza kazi alielezea kufurahishwa na juhudi za Kapande.

Alisema Issa ameonesha njia kwamba inawezekana kwa watu waliopo Ughaibuni sio tu kuajiriwa, bali kujiajiri katika nyanja mbalimbali.Alisema hilo linawezekana kutokana na kufuatilia kwa karibu taratibu za wenyeji na kisha kutumia mafunzo yaliyopo kukamilisha ndoto."Ni dhahiri kuwa, Chef Issa kwa kupitia taaluma yake ya upishi amewezeshwa kumiliki mgahawa huu hapa Trollhattan,S weden kwa hilo, napenda tuishangilie na kuipigia makofi Sweden na Trollhattan."Alisema akimpongeza kijana huyo ambaye pia amewekeza mkoani Mtwara.

KUSOMA ZAIDI KWA CHANZO;BBC 

MHE. POSSI: JAMII IWASHIRIKISHE WATU WENYE ULEMAVU KATIKA FURSA ZOTE ZA MAENDELEO

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu, Mhe. Dkt. Abdallah Possi ameiasa jamii kuwashirikisha watu wenye ulemavu katika shughuli zote za maendeleo ili kusaidia kuwainua na kuondokana na dhana ya utegemezi na kuwakwamua kiuchumi.
Dkt.Possi ameyasema hayo wakati wa ziara yake katika Wilaya za Mbinga, Songea Vijijini na Nyasa mkoani Ruvuma ambapo alitembelea Shule zenye kuhudumia watu wenye mahitaji maalum za Songea Boys, Luhira, Huruma na Kituo cha Kulelea wenye ulewavu cha Peramiho Disabled Persons Action (PEDIPA) na Kituo cha kulele wazee na wenye ukoma cha Nge Wilayani Nyasa.
Katika ziara hiyo Mhe.Possi alibaini changamoto nyingi za watu wenye ulemavu na kuishauri jamii namna pekee ya kutatua changamoto wanazokabiliana nazo ni jamii kuona umuhimu wa kuwashirikisha watu hao katika mipango yote ya maendeleo.

“Halmashauri ziandae mipango ya kuwawezesha watu wenye ulemavu kuweza kushiriki kikamilifu katika kujitafutia kipato na hii itasaidia kuondokana na hali ya utegemezi na kuondoa mitazamo hasi juu ya watu wenye ulemavu kuwa hawawezi” .Alisema Mhe.Possi.
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi  akizungumza na baadhi ya watu wenye ulemavu (hawapo pichani) na watendaji wa Serikali juu ya umuhimu wa kuwashirikisha watu wenye ulemavu katika shughuli za maendelea wakati wa ziara yake Wilayani Peramiho mkoa wa Ruvuma Novemba, 2016.
 Baadhi ya watu wenye ulemavu wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao alipotembelea kituo cha kulelea watu wenye mahitaji maalum cha Peramiho Disabled Persons Action(PEDIPA) wakati wa ziara yake Peramiho. 
 Mhazini wa kikundi cha kulelea watu wenye mahitaji maalum cha Peramiho Disabled Persons Action (PEDIPA) Mwl.Elswida Charles akimkabidhi risala ya kikundi hicho kwa  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi Peramiho Ruvuma.
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi   akimkabidhi Mwenyekiti wa PEDIPA Bw.Pius S.Kayombo Kiti Mwendo ili kumsaidia katika shughuli zake za kila siku.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MINISTRY OF WATER AND IRRIGATION, GIZ SIGNED THE IMPLEMENTATION AGREEMENT

$
0
0

Ministry of Water and Irrigation and the German Agency for International Cooperation (GIZ) have signed the Implementation Agreement at the Ministry’s HQ at Ubungo, yesterday.


The agreement outlines the interventions that will be carried out within the framework of Technical Cooperation between the Governments of the United Republic of Tanzania and of the Federal Republic of Germany.


Speaking at the signing ceremony the Ministry of Water and Irrigation’s Permanent Secretary, Eng. Mbogo Futakamba said that, with GIZ’s support, several instruments for policy coordination and implementation have been put in place, including the Water Supply and Sanitation Regulations and the Water Sector Programme Implementation Manual.


Eng. Futakamba continued by saying, the current 3-year cycle of GIZ’s support to the Water Sector Programme, which runs from March 2016 to February 2019with a funding envelop of Euro 9.5 million, will concentrate on a number of distinct working areas of Sectoral Framework and Sector Finance, Urban Water Supply and Sanitation, Regulatory Framework and Climate-Sensitive Water Resources Management.


Meanwhile, the GIZ Country Director, Dr. Regine Qualmann said that, it is in the interest of the Government of Germany that, through effective cooperation with Tanzanian Government the implementation of the GIZ supported water sector development programme will achieve its intended objectives and targets, and to do so in a sustainable manner. As we will always support Tanzania and its development as far as our cooperation is concerned.


The cooperation between Tanzania and Germany existed since 1975, and it has been guided by a shared vision of promoting Tanzania’s development in a sustainable manner. Over the years, the focus and priorities have somewhat changed, in order to adapt to changing conditions and priorities on site, but also to take on board changing global initiatives and development agendas.


Yesterdays’ signing ceremony signalled the continuation of the joint commitment of the two Governments, towards accomplishing some of the unfinished global commitments of the (8) Millennium Development Goals (MDGs), which have now been reformulated into (17) measurable Sustainable Development Goals (SDGs), under the Global Agenda for 2030.


 The Ministry of Water and Irrigation’s Permanent Secretary, Eng. Mbogo Futakamba together with the Counsellor- Head of Cooperation at the Embassy of  Federal Republic of Germany in Tanzania, Julia Hannig (at the left) and the GIZ Country Director, Dr. Regine Qualmann.
 The invitees listening to the presentantion.
 The Ministry of Water and Irrigation’s Permanent Secretary, Eng. Mbogo Futakamba together with the GIZ Country Director, Dr. Regine Qualmann signing the agreement.
 The Ministry of Water and Irrigation’s Permanent Secretary, Eng. Mbogo Futakamba together with the GIZ Country Director, Dr. Regine Qualmann exchanging the agreement documents.

The Ministry of Water and Irrigation’s Permanent Secretary, Eng. Mbogo Futakamba together with the GIZ Country Director, Dr. Regine Qualmann in a group photo with ministry’s, GIZ’s and EWURA’s representatives.

Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images