Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1444 | 1445 | (Page 1446) | 1447 | 1448 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Ndege iliyobeba watu 81, wakiwemo wachezaji wa klabu moja ya soka ya Brazil, imeanguka eneo la Medellin nchini Colombia.

  Maafisa wa usalama wanasema watu sita wamenusurika na ndege hiyo inayodaiwa kupata hitilafu za mfumo wake wa umeme.

  Ndege hiyo ilikuwa safarini  kutoka Bolivia na ilikuwa imewabeba wachezaji wa timu ya Chapecoense, ambao walikuwa wamepangiwa kucheza mechi ya fainali ya Copa Sudamericana, dhidi ya timu ya Medellin, Atletico Nacional.

  Taarifa zinasema ndege hiyo muundo wa British Aerospace 146 ambayo imekuwa ikitumiwa na shirika la ndege la Lamia la Bolivia ilikuwa na abiria 72 na wahudumu tisa na ilianguka eneo la milimani nje kidogo mwa mji wa Medellin majira ya saa sita usiku saa za huko (saa mbili asubuhi Afrika Mashariki).

  Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa maafisa wa uwanja wa ndege, marubani walisema ndege hiyo ilikuwa imepata matatizo katika mfumo wake wa umeme.

  Maafisa wa uwanja wa ndege wa Jose Maria Cordova de Rionegro uliopo Medellin, wamesema juhudi zote zinafanywa kuwaokoa manusura ingawa hali mbaya ya hewa inazuia maafisa kufikia eneo la mkasa kwa urahisi.

  Hakukutokea moto baada ya ndege hiyo kuanguka, jambo ambalo linaibua matumaini ya kupatikana kwa manusura na Maafisa wa uokoaji wanaweza tu kufika eneo la ajali kwa barabara

  Meya wa Medellin Mayor Federico Gutierrez amesema ajali hiyo ni "janga kubwa".                        

  0 0

  Halmashauri  ya wilaya  ya Namtumbo  mkoani  Ruvuma   hivi  karibuni  imeanza  mchakato  wa kuanzisha  Redio  ya  jamii (community  radio )itakayorusha  matangazo  yake  ndani  ya wilaya  hiyo   ya  Namtumbo.

  Ofisa  habari  wa  wilaya  ya  Namtumbo  Yeremias  Ngerangera  alisema  kuwa  mchakato  wa  kuanzisha  Redio  hiyo  ya  jamii unaendelea  vizuri  ambapo  kwa  hatua  ya awali  kamati  ya kuanzisha  Redio  iliundwa  na tayari  kamati  hiyo  imeanza kazi yake .

  Bwana  Ngerangera  alitaja  idara  zilizopo kwenye  kamati  hiyo  ni  idara  ya  mipango,idara  ya  utawala,idara  ya maendeleo  ya  jamii, idara  ya  afya ,idara  ya mazingira  pamoja na kukihusisha  kitengo cha  sheria  na usalama .
  Aidha  bwana  Ngerangera  alibainisha  sababu  za  halmashauri  hiyo  kuanzisha  Redio hiyo  ni  pamoja na  kurahisisha mawasiliano  kati  ya  uongozi  wa  halmashauri  hiyo  na wananchi  wake juu ya  maagizo  mbalimbali  ambayo  halmashauri inawataka  wananchi  wake kufanya.

  Pia  redio  hiyo   itatumika pia kuelimisha  jamii ya  Namtumbo kuhusiana  na  kilimo bora ,umuhimu  wa utunzaji  wa  mazingira ,umuhimu  wa kuwapatia  watoto  elimu,umuhimu  wa kuwa na afya bora pamoja na  kuwatangazia  wananchi mambo mbalimbali ya kimaendeleo.

  Kaimu  afisa  mipango  wa Halmashauri  ya  wilaya  ya  Namtumbo  Gwakisa  Mwaseba  ambaye  pia  ni  mwenyekiti  wa  kamati  ya kuanzisha  Redio  hiyo  alisema  kuwa  zaidi  ya milioni 103,400,000 zinahitajika  ili kukamilisha  zoezi  la kuanzisha redio hiyo.

  Bwana  Gwakisa  aliwataka  wadau  kutoka  sehemu mbalimbali  katika  nchi  hii ,wazaliwa  wa wilaya  ya  Namtumbo  na wenye  mapenzi  mema  na  Halmashauri  ya wilaya  ya Namtumbo  kushirikiana katika kuhakikisha  redio  hiyo  inaanzishwa .
  Pamoja  na mambo  mengine  aliwaomba  wadau  kuchangia uanzishaji  wa  redio  hiyo kwa kuwa redio  hiyo itakuwa  na umuhimu mkubwa kwa  Halmashauri  yetu ya Namtumbo  na wilaya nzima ya Namtumbo.

  Mkurugenzi  wa  Halmashauri  ya Wilaya ya Namtumbo  Christopher  Kilungu  aliitaka kamati  hiyo ya kuanzisha Redio  kufanya  mikutano yao na kuwasilisha mapendekezo ya kamati  yao  kwenye uongozi  wa Halmashauri kwa lengo  la kujiridhisha  na kuyajadili mapendekezo  hayo .

  Pamoja  na mambo  mengine  mkurugenzi  huyo  aliitaka  kamati  hiyo kufanya  kazi  yake  vizuri  na  kuhakikisha  Redio  hiyo  ya  Halmashauri  inaanzishwa  kwa madai kuwa Redio  hiyo  itakuwa  na tija kwa maendeleo  ya wananchi  wa Namtumbo  na Halmashauri  yao.

  Wananchi  wa wilaya  ya Namtumbo  walipoelezwa  kupitia  mikutano  ya Hadhara  kuhusiana  na Hatua  ya kuanzisha Redio  hiyo  walifurahishwa  na hatua hiyo kwa madai ya kuwasaidia katika kutoa  maoni  yao kupitia kadi za salamu zitakazosomwa  kwenye Radio  hiyo.

  Halmashauri  ya  wilaya  ya  Namtumbo  ina jumla  ya Tarafa  Tatu, kata  ishirini  na  moja  na vijiji  sabini  na moja  ambapo ina ukubwa wa kilomita  za mraba 20,375.

  0 0


  MKUU wa wilaya ya Tunduru JUMA HOMELA  aelezea mpango wa mahakama ya kutembea aliyoianzisha katika wilaya yake ya TUNDURU jinsi ulivyoleta mafanikio , katika kupunuza utoro mashuleni na mimba mashuleni.
  Attachments area Preview YouTube video RUVUMA TV@ SEHEMU YA PILI TUNDURU yafanikiwa kupunguza mimba kwa wanafunzi RUVUMA TV@ SEHEMU YA PILI TUNDURU yafanikiwa kupunguza mimba kwa wanafunzi

  0 0

  Waziri wa Maliasali na Utalii, Profesa Jumanne Magembe (kulia) katika Picha ya pamoja na Baadhi ya wana utamaduni wa sanaa ya maonyesho kutoka Mkoa wa Iringa siku ya Uzinduzi wa maonyesho hayo yafanyikayo katika Viwanja vya kichangani Mjini Iringa kwa nyanda za juu kusini na kuhitimishwa leo Viwanjani hapo Mjini Iringa.
  Waziri Magembe kulia akifurahia Jambo pindi alipo kuwa akitembelea katika baadhi ya mabanda ya Wadau wa Utalii walio jitokeza katika Viwanja hivyo Mjini Iringa.
  Waziri Magembe akipokea moja ya Zawadi kutoka kwenye kampuni ya Ivori Ya Mjini Iringa inayo fanya vyema katika kuzalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo Pipi za Ivori.
  Picha Zote na Mr.Pengo wa MMG Nyanda za juu Kusini.

  0 0


  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei akizungumza na vyombo vya habari, wakati akikanusha taarifa zinazoenezwa mitandaoni kuwa Benki hiyo iko mbioni kufunga baadhi ya matawi yake kwa madai kuwa imeyumba kiuchumi. Dkt. Kimei amekanusha taarifa hizo kwa kusema si ukweli na sasa wako kwenye mikakati ya kufungua matawi mengine 11 kabla ya Januari 2017.

  0 0

  Mfanyabaishara Ndama Hussein maarufu kama mtoto wa Ng’ombe amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, akikabiliwa na mashtaka sita ikiwamo kughushi na kutakatisha Dola za Kimarekani 540,390 (sawa na Sh, bilioni 1.181). Mshtakiwa huyo alisomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa.

  Upande wa Jamhuri uliongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Christopher Msigwa akisaidiana na Wakili wa Serikali Leonard Challo.

  Msigwa alidai kuwa Februari 20, mwaka 2014, jijini Dar es Salaam, mshtakiwa akiwa na lengo la kudanganya alighushi nyaraka za kusafirisha madini akionyesha kwamba Kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Limited imepewa kibali cha kusafirisha boksi nne za vipande wa dhahabu zenye uzito wa kilo 207 zenye thamani ya Dola za Kimarekani 8.2 kwa Kampuni yenye makazi yake nchini Austaria inajulikana kama Trade TJL DTYL Limited huku akijua nyaraka hizo za uongo.

  Katika shtaka la pili, Machi 6, mwaka 2014, jijini Dar es Salaam akiwa na nia ya kudanganya, aliandaa nyaraka za uongo kuonyesha kwamba hati ya kuondolea mizigo kutoka ofisi za Umoja wa Mataifa za tarehe hiyo, akiwa na lengo la kuonyesha kwamba vipande vya dhahabu vyenye uzito wa kilo 207 kutoka Jamhuri ya Congo, kuwa zinasafirishwa na Kampuni ya  Muru Platnum kwenda Austraria.

  Msigwa alidai katika shtaka la tatu, Februari 20, mwaka 2014 jijini Dar es Salaam, akiwa na nia ya kudanganya alighushi nyaraka zikionyesha kuwa ni fomu ya tamko la kodi akionyesha Kampuni ya Muru Platnum imelipa Dola za Kimarekani 331,200 kama kodi ya kuingiza mzigo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ya kilo 207 ya vipande vya dhahabu vyenye thamani ya Dola za Kimarekani 8,280,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo huku akijua ni uongo.

  Katika shtaka nne, Februari 20, mwaka 2014 jijini Dar es Salaam, mshtakiwa akiwa na nia ya kudanganya alitengeneza nyaraka zauongo za kuonyesha kuwa ni za bima kutoka Kampuni ya Phoenix  Ltd za terehe hiyo, akilenga kuonyesha kwamba Kampuni ya Muru Platnum imekatia bima boksi nne za vipande vya dhahabu zenye uzito wa kilo 207 vyenye thamani ya Dola za Kimarekani 8,280,000 huku akijua ni uongo.

  Katika shtaka la tano na sita, kati ya Februari 26 na Machi 3, mwaka 2014 jijini Dar es Salaam, alijipatia kwa njia ya uongo na kutakatisha Dola za Kimarekani, 540,390 (sawa na Sh. Bilioni 1.181) kutoka Kampuni ya Trade TJL DTYL Limited kwa madai kuwa angesambaza na kusafirisha nje ya nchi kilo 207 za vipande vya dhahabu vyenye thamani ya Dola za Kimarekani 8,280,000 lakini hakufanya hivyo.

  Ilidaiwa kuwa mshtakiwa alitakatisha fedha hizo zilizopatikana kwa njia ya jinai kwa kuelekeza kiasi hicho cha fedha kuingizwa katika akaunti iliyopo benki ya Stanbic yenye jina la Kampuni ya Muru Platnum na baadaye alizitoa zote na kuzitumia kwa matumizi yake binafsi huku akijua zimepatikana kwa njia ya udanganyifu.

  Upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na uliomba mahakama tarehe nyingine ya kutajwa.

  Hakimu Nongwa alisema kesi hiyo itatajwa Desemba 13, mwaka huu.

  Mshtakiwa alirudhishwa mahabusu kwa sababu mashtaka ya kutakatisha fedha hayana dhamana kwa mujibu wa sheria.

  0 0

  Rais John Magufuli akiagana na Rais wa Zambia, Edgar Chagwa Lungu kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere wakati mgeni huyo alipoondoka nchini kurejea nyumbani Novemba 29, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

    Rais John Magufuli akiwapungia wananchi waliojitokeza kumuaga Rais wa Zambia, Edgar Chagwa Lungu kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere wakati alipoondoka nchini kurejea nchini Novemba 29, 2016. Wengine pichani ni Makamu wa Rais, Samia Suluhu na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Inspekta Jenerali wa Polisi, Ernest Mangu kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Novemba 29, 2016. Wapili kulia ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange na watatu kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi John Kijazi.
   Rais John Magufuli akiongozana na  mgeni wake, Rais Edgar Chagwa Lungu wakati mgeni huyo alipoondoka nchini kurejea nyumbani kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Novemba 29, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
    Rais John Magufuli na Makamu wa Rais, Samia Suluhu wakishuudia wakati Rais wa Zambia Edgar Chagwa Lungu akiagana na Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere kabla ya kuondoka nchini kurejea nyumbani Novemba 29, 2016.

  0 0
  0 0

   Balozi wa Kuweit nchini Tanzania Jasem Alnajim akimkabidhi Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Juma Malik  Akili msaada wa moja ya  mashine  tatu za kupimia Presha alipotembelea Hospitali Kuu ya Mnazi mmoja mjini Zanzibar.
    Balozi wa Kuweit nchini Tanzania Jasem Alnajim akiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Juma Malik Akili wakiwapa zawadi akinamama waliojifungua katika wodi ya wazazi ya Hospitali kuu ya Mnazi mmoja.
   Balozi wa Kuweit nchini Tanzania Jasem Alnajim akimbeba mtoto mchanga alipotembelea wodi ya wazazi ya hospitali  kuu ya Mnazi mmoja Mjini Zanzibar.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali kuu ya Mnazi mmoja Dkt. Ali Salum Ali akimuongoza Balozi wa Kuweit nchini Tanzania Jasem Alnajim alipotembelea majengo mapya ya Hospitali hiyo yaliyofunguliwa hivi karibuni.Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

  0 0

  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage ameipongeza na kuishukuru Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa jitihada za kuendelea kuelimisha wafanyabiashara kutambua umuhimu wa kulipa kodi utakaoiwezesha Serikali kusonga mbele katika suala zima na ukuzaji wa viwanda vya ndani hapa nchini.

  Mhe. Mwijage aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa nne wa mwaka wa Taasisi isiyo ya kiserikali inayotoa Msimbomilia (Barcode) za bidhaa (GS1); uliofanyika tarehe 29 Novemba 2016 katika ukumbi wa mikutano wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

  Mkutano huo uliandaliwa kwa ushirikiano kati ya GS1 na TRA kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayowahusu wadau wao, kujadili mambo muhimu ya kodi yanayohusu umuhimu wa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) katika kuweza kupata msimbomilia (barcodes 620) na kuweza kuzitambulisha bidhaa za Tanzania kimataifa pamoja na kuadhimisha miaka mitano tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo.
  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage wa tatu kulia akikata keki kuadhimisha mwaka wa nne wa Taasisi isiyo ya kiserikali inayotoa Msimbomilia 620 (Barcode) za bidhaa (GS1) uliofanyika jijini Dar es salaam. Wa kwanza kushoto ni mwakilishi kutoka TRA ambaye ni Afisa Mkuu wa Elimu kwa Mlipakodi Bi. Rose Mahendeka na wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya GS1 Bw. Gideon Mazara wakishuhudia tukio hilo.

  Waziri Mwijage aliliagiza Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kuhakikisha kila mfanyabiashara anayemiliki viwanda vidogo na vya kati kuhakikisha anakuwa na TIN na namba ya msimbomilia 620 inayotolewa na GS1 Tanzania kabla ya kuhuisha vyeti vyao vya biashara.

  Aidha Waziri Mwijage amesema kuwa uchumi wa viwanda unatakiwa kukua nchini ili kuweza kuzalisha bidhaa bora zitakazouzwa ndani na nje ya nchi na kukusanya kodi stahiki itakayoiwezesha Serikali kutoa huduma bora za kijamii kwa maendeleo ya wananchi wa Tanzania .

  “Ifike wakati wafanyabiashara muwaelewe vizuri TRA na kulipa kodi stahiki ya Serikali, ili nchi iweze kusonga mbele” alisema Mhe. Mwijage.
  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage (katikati) akielezea na kumpongeza Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Shear Illusions Bi. Shekha Nasser (aliyeshika zawadi) kwa kulipa kodi stahiki ya Serikali ya kati ya Milioni 9 na 12 kila mwezi kupitia kampuni yake ambayo pia imeweza kutoa ajira kwa vijana zaidi ya12. Pongezi hizo alizitoa wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa nne wa Taasisi isiyo ya kiserikali inayotoa msimbomilia (Barcode) za bidhaa (GS1) uliofanyika jijini dar es salaam.

  Kwa upande wake Afisa Mkuu wa Elimu kwa Mlipakodi kutoka TRA Bi. Rose Mahendeka alisema kuwa wafanyabiashara wote ambao wanahitaji kutumia mfumo wa kuuza bidhaa kwa kuweka msimbomilia (Barcode 620) wanapaswa kupitia TRA kwa ajili ya usajili na uhakiki wa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) kabla ya kwenda kupata huduma ya msimbomilia 620.

  Bi. Mahendeka aliwasisitiza wadau hao kuhakikisha wanajisajili na TIN na wale waliojisajili kuhakikisha wanahakiki taarifa zao ili kurahisisha upatikanaji wa Msimbomilia 620 na kuiwezesha TRA kupata takwimu sahihi za wafanyabiashara wazalishaji na wanaouza bidhaa zao nje ya nchi.
  Baadhi ya wadau wa Taasisi isiyo ya kiserikali inayotoa Msimbomilia (Barcode 620) za bidhaa (GS1) wakimsikiliza kwa makini Afisa Mkuu wa Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bi. Rose Mahendeka akitoa elimu ya kodi wakati wa mkutano wa nne wa mwaka wa Taasisi hiyo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

  “Wafanyabiashara wote ambao wanahitaji kutumia mfumo wa kuuza bidhaa kwa kuweka Msimbomilia(Barcode 620) wanapaswa kupitia TRA kwa ajili ya usajili na uhakiki wa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi(TIN) kabla ya kwenda kupata huduma” alisisitiza Bi. Mahendeka.

  Aidha Bi. Mahendeka alisema kuwa wafanyabiashara ambao wanahitaji kuuza bidhaa zao kwa kutumia msimbomilia wanapaswa kulipa kodi bila ya kukwepa ili kuiwezesha Tanzania kupiga hatua kufikia uchumi wa viwanda na vilevile kuweza kutoa huduma bora kwa maendeleo ya jamii.

  Naye Mwenyekiti wa bodi ya GS1 Bw. Gideon Mazara alitoa rai kwa wafanyabiashara wanaozalisha bidhaa kutumia Msimbomilia 620 wa Tanzania na kuweza kutangaza bidhaa za hapa nchini ili kupata soko la kimataifa litakalowezesha nchi kufikia uchumi wa kati .
  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akiwa katika picha ya pamoja na baadi ya wadau wa Taasisi isiyo ya kiserikali inayotoa msimbomilia (Barcode 620) za bidhaa (GS1) mara baada ya kuhitimisha mkutano mkuu wanne wa Taasisi hiyo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

  0 0  0 0

  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba, ambaye yuko Nairobi kuhudhuria kikao cha Bunge la Afrika Mashariki, ametumia fursa hiyo kutembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Kenya na kuzungumza na watumishi.Katika kikao na Mhe. Waziri, watumishi wa Ubalozi walielezea changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika utendaji wa kazi, ikiwa ni pamoja na ufinyu wa bajeti. 

  Hata hivyo watumishi hao walisema wameweza kukusanya maduhuli ya kuridhisha na kuhudumia Watanzania wanaopatwa na matatizo kwa kuchangishana wakati mwingine.Mhe. Kolimba alieleza kuridhishwa kwake na utendaji wa watumishi wa Ubalozi wa Nairobi na kuwapongeza kwa moyo wa kujitolea. 

  Alisema Serikali itajitahidi kupatia balozi fedha na vifaa vya kazi kwa kadri ya uwezo wake, lakini akasisitiza watumishi wawe wabunifu na wajitolee kufidia pale upungufu unapojitokeza.Kikao cha Bunge la Afrika Mashariki kinachofanyika kwenye Bunge la Kenya kinatarajiwa kumalizika kesho.
  Baadhi ya watumishi wa Ubalozi wakijipanga kumpokea Mhe. Naibu Waziri
   Mhe. Kolimba akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Ubalozi.
   Naibu Waziri, Dkt. Kolimba (kushoto) akifurahia bidhaa za Tanzania kwenye ofisi za Ubalozi wa Nairobi akiwa na Kaimu Balozi, Bi. Talha Mohamed Waziri. 
  Naibu Waziri akiongea na watumishi wa Ubalozi. Kushoto ni Kaimu Balozi, Bi. Waziri na Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. James Lugaganya.

  0 0

  We have the honor of inviting all Tanzanians in Michigan as well as our friends to the annual Independence Day (Uhuru Day) celebration which will be held this year at the UAW Local 892 Banquet Hall in Saline, Michigan 48176 on Saturday December 10th, 2016 from 6:00PM - 2:00AM.

  Join us to celebrate our history, our culture and our future as we share East African cuisine which is highly influenced by Western, Indian and Middle Eastern cooking. On top of that DJ Mussa will be on the turntables with the best of African Beats and Hits while you Eat and thereafter on the dance floor! It can't get better than that!

  Get your tickets from me (MMM): 248 904 3509 or Mr. Mfinanga at 586 354 5479 or for those in Lansing (and surrounding areas) from Prof. Ngonyani @ 517 -512-8437, in Kalamazoo (and surround areas) through Mr. Emmanuel Turuka @ 269 267-2174, in Ann Arbor through Martin @ 734 239-3935 and in Detroit Area through Abdul Kufakunoga @248 515 5509.
  You can also purchase tickets online at www.evenbrite.com key word "Uhuru Day"
  Come one, Come all!

  0 0
  Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Jumanne  tarehe 29 Novemba , 2016  amefanya ziara ya kushtukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar Es Salaam  na kupiga marufuku uuzwaji wa sare za majeshi nchini na watu binafsi na kutaka wale wote wanaouza sare hizo wazikabidhi kwa majeshi husika mara moja.

  Rais Magufuli amepiga marufuku hiyo kufuatia maelezo kutoka kwa baadhi ya askari wa Jeshi la Magereza kuwa wamekuwa wakinunua sare za jeshi hilo kutoka kwa watu binafsi kinyume na taratibu za majeshi nchini na kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuwachukulia hatua mara moja wale wote watakaobainika kuuza sare za majeshi ya hapa nchini

  Hali kadhalika Rais magufuli amepiga marufuku kwa majeshi yote nchini kuingia ubia na watu binafsi kupangisha ama kuuza maeneo yao kwa ajili ya kufanya biashara na kutaka maeneo yote ya majeshi yabaki katika jeshi husika. 
  ''Haiwezekani sare za majeshi yetu hapa nchini kuuzwa na watu binafsi hilo haliwezekani kamwe labda baada ya kumaliza muda wangu , amesema Rais magufuli'' 
  Aidha Rais Magufuli ametoa shilingi Bilioni Kumi kwa Jeshi la Magereza kwa ajili ya kujenga nyumba mpya zitakazotumika kwa ajili ya makazi ya askari wa Jeshi la Magereza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam. 
  Hatua hiyo inafuatia kilio cha askari Magereza kuwa wengi wao wamekuwa wakiishi uaraiani kitu ambacho ni tofauti na taratibu za majeshi nchini na hata kuzorotesha utendaji kazi wa askari wa Jeshi hilo. 
  Amiri Jeshi Mkuu na Rais Dkt. John Pombe Magufuli pia ameagiza Jeshi la Magereza kuhakikisha wafungwa wanatumika katika uzalishaji mali badala ya mfumo wa sasa ambapo baadhi ya wafungwa wamekuwa  wakitutumia rasilimali za serikali bila kuzifanyia kazi.

   Rais Magufuli amewahakikishia Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza kuwa serikali itaendelea kuboresha maslahi yao na vitendea kazi kama inavyofanya kwa majeshi mengine nchini. 

  Jaffar Haniu

  Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

  Dar Es Salaam

  29 Novemba, 2016
    Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiweka saini kitabu cha wageni akiwa na  Kamishna Mkuu wa Magereza John Casmir Minja kabla ya kuongea na maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kushtukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam  Novemba 29, 2016
   Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipewa muhtasarai wa kazi  na Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja kabla ya kuongea na maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam Novemba 29, 2016
   Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akikaribishwa na Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja ili aongee  na maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam Novemba 29, 2016
   Mmoja wa askari wa Kikosi Maalumu cha Magereza akitoa kero zao mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli  alipofanya ziara ya kushtukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam leo Novemba 29, 2016
   Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akichukua maelezo kutoka kwa  maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam leo Novemba 29, 2016.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA 
  0 0
 • 11/30/16--01:15: GADO LEO


 • 0 0

  Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (kushoto) akimueleza jambo Mkuu wa wilaya Lindi, Shaibu Ndemanga (wapili kulia) juu huduma zitakazotolewa na mnara wa Airtel uliojengwa katika kijiji cha Cheleweni mara baada ya kuzindua mnara huo. katikati ni Meneja Mauzo wa Airtel Mkoa wa Lindi, Saleh Safy. Airtel imejenga mnara huo ambao utatoa mawasiliano katika vijiji vya Ng’apa ngapa, Cheleweni, Nchee, Nantumbya, Nanyuru pamoja na maeneo yanayowazunguka vijiji hivyo. Airtel imezindua huduma hiyo ili kuboresha , huduma za kifedha kwa njia ya mtandao Airtel Money na kuwaweza wananchi wa Lindi kupata mawasiliano ya uhakika katika kuendesha shughuli zao za kila siku kiuchumi na kijamii.
  Mkuu wa Wilaya Lindi, Shaibu Ndemanga akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa mnara wa Airtel utakaotoa huduma ya mawasiiano katika vijiji vya Ng’apa ngapa, Cheleweni, Nchee, Nantumbya, Nanyuru pamoja na maeneo yanayowazunguka vijiji hivyo. anaefuata ni diwani wa viti maalum Lindi Bi, Somoe Pamui na Meneja Mauzo wa Airtel Mkoa wa Lindi, Saleh Safy. 

  0 0
  0 0

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Willim Lukuvi anaendelea na ziara ya siku tatu katika mkoa wa Kigoma ambapo amefungua rasmi Baraza la Ardhi na Nyumba la Mkoa wa Kigoma pamoja na kutatua migogoro ya ardhi ya wananchi wa Kigoma. 

  Wananchi hao wamempongeza Mhe. Waziri kwa hatua anazozichukua katika kumaliza migogoro yao ya ardhi na kuwajengea Baraza la Ardhi na Nyumba ambalo jipya na lililo na viwango kushinda mengine yote hapa nchini.
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Willim Lukuvi akifungua Baraza la Ardhi na Nyumba la Mkoani Kigoma, Kushoto ni Mbunge wa Kigoma Mjini Mhe. Zitto Kabwe na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe.Brigedia Jenerali Emanuel Maganga.
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Willim Lukuvi akiongea na wananchi wa Kigoma Mjini na kutatua migogoro yao ya ardhi.


  0 0

  Mkandarasi anayejenga barabara ya Magole - Turiani (ChinaCivil Engineering Construction Corparation-CCECC) ameahidi kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo mapema, lakini ameiomba serekali imuunge mkono kwa kutoa fedha kwa wakati.

  Katibu Mkuu wa Asasi ya Urafiki wa Tanzania na China, Bwana Joseph Kahama,  amewambia waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam jana kuwa  siku za nyuma serekali imekuwa ikichelewa kutoa  fedha za ujenzi wa maradi na ujenzi umekuwa ukisimama mara kwa mara. Hata hivyo Kahama  amesema ana matumaini makubwa ya  ujenzi kukamilika  katika muda muafaka kwani kuna mawasilianao ya mara  kwa mara kati yao  na TanRoads.

  Serekali tayari imetoa  bilioni 41.8, kati ya bilioni 66.7 ambazo zinatarajiwa kujenga barabara hii.

  Kahama amesema kuwa hakuna tarehe mpya ya kukamilisha kazi ambayo pande mbili zimekubaliana. Lakini amesema wafanyakazi wana ari ya kazi na kuwa  mradi utakamilika mapema iwapo serekali itatoa fedha katika muda unaoruhusu ujenzi uendelee kwa kasi inayotakiwa.  Fedha ikichelewa, kasi ya ujenzi inavia na mradi unadorora, ameeleza.

  Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Steven Kabwe amekaririwa katika vyombo vya habari akimuhimiza mkandarasi kukamilisha kazi kabla au ifikapo Septemba 2017 na kwamba ujenzi usifike mwaka 2018.

  Kahama amesama kwamba Dr Kabwe amejionea mwenyewe hali halisi ya ujenzi wa barabara na kuhakikishiwa na Mhandisi  Khatibu Khamis kwamba kazi itakamilika katika muda muafaka  kwani hakuna tatizo la vifaa au wafanyakazi.  Tanzania na China, ameeleza,  zina mawazo sawa juu ya maendeleo ya wananchi na uhusiano wa kuwepo barabara katika kasi ya wananchi kujiletea maendelo.

  “Tunawasisitizia wenzetu jambo upatikanaji wa fedha mapema. Ujenzi wa barabara unaathiriwa na mambo mengi yasiyotarajiwa kama vile mvua kubwa au mafuriko.  Fedha isipotolewa kwa wakati, kuna hatari ya ujenzi kukwama,” amesisitiza Kahama.

  Barabara ya  Mikumi-Mzina inaunganisha Mkoa wa  Tanga  na Mikoa ya  Morogoro na Dodoma.

  0 0

  Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es salaam

  Wizara ya Fedha na Mipango imekamilisha ujenzi wa mfumo wa malipo moja kwa moja kupitia akaunti za walipwaji katika mtandao wa malipo wa Benki Kuu ya Tanzania (Tanzania Interbank Settlement System – TISS), katika mkoa wa Morogoro, hatua inayolenga kuongeza ufanisi wa miamala mbalimbali inayofanywa na serikali

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James amezitaja Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Halmashauri za Wilaya ya Kilombero, Morogoro, Mvomero, Kilosa na Ulanga, kwamba zitaanza kufanya malipo hayo kwa mfumo huo wa TISS kuanzia mwezi Desemba mwaka huu.

  “Nia ya Serikali ni kuhakikisha kwamba ifikapo mwezi Desemba, 2016 Halmashauri zote zilizopo katika Mkoa wa Morogoro ziweze kufanya malipo kwa kutumia mfumo wa malipo wa TISS” alisema Dotto James.   

  Amesema kuwa malipo hayo yatafanyika kwa kutumia mfumo wa malipo wa TISS uliojengwa katika mikoa yote Tanzania Bara ikiwemo Ofisi za Hazina Ndogo na Sekretariati za Mikoa, Wizara, Idara za Serikali zinazofanya malipo yake kupitia Ofisi Kuu ya Malipo (CPO) iliyopo Hazina, malipo ya Pensheni kwa wastaafu, Kitengo cha Kupambana na Fedha Haramu, Mfuko wa Bunge, Mfuko wa Mahakama na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

older | 1 | .... | 1444 | 1445 | (Page 1446) | 1447 | 1448 | .... | 3284 | newer