Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1442 | 1443 | (Page 1444) | 1445 | 1446 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii

  Benki ya United Bank of Africa (UBA), jana imetoa msaada wa viti, Magodoro, Magongo ya kutembelea na vitabu vya kujisomea kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu ya shule ya sekondari ya wavulana Pugu jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza wakati wa kutoa vifaa hivyo, Meneja wa benki hiyo nchini ,Peter Makao, amesema kuwa wamechagua kutoa vifaa hivyo katika shule hiyo kutokana na mahitaji ya watoto hao ambao wamekuwa wakisoma katika mazingira magumu.

  “Vitu hivi ambavyo tumevitoa leo vitasaidia kwa kiasi kikubwa kuwapunguzia watoto hawa wenye mahitaji maalum kusoma kwa mawazo kwa kujiona kwamba wao ni sehemu hii ya shule kwa kupata mahitaji yao wote kama ilivyo kwa wengine”Amesema Makao 

  Ametoa wito kwa wanafunzi hao kusoma kwa bidii ili waweze kufanikiwa katika jamii na baadae wajivunie kuwa walisoma pugu .
  Wanafunzi wa Pugu sekondari wakishusha kwenye gari vifaa vilivyokabidhiwa na benki ya UBA kwa ajili ya wanafuzni wenye mahitaji maalum
  Mkurugenzi mkuu wa Benki ya UBA,Peter Makao akiwa na Meneja Operesheni Omary wakikabidhi mafuta ya ngozi kwa kijana mwenye ulemavu wa ngozi ,Daudi Nyangusi na Meneja ufadhili wa eleimu kutoka TEA , Tito Mganwa.
  Mkurugenzi mkuu wa Benki ya UBA,Peter Makao akiwa meneja operesheni Omary wakikabidhi vitabu kwa wanafunzi Salum Mohamed na Ramadhani Juma pamoja na Meneja ufadhili wa eleimu kutoka TEA , Tito Mganwa.
  Wafanyakazi waUnited Bank of Afrika wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wenye ulemavu wa shule ya Sekondari ya wavulana pugu jijini Dar es Salaam.


  0 0

  MBUNGE wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega amewataka vijana wa Chama cha Mapinduzi kujitokeza Kwa wingi katika uchaguzi Mkuu ujao wa Chama unaotarajia kufanyika mapema mwakani 2017.

  Amesema kuwa wanatakiwa kujitokeza Kwa wingi ili kushika nafasi mbalimbali za uongozi ndani Chama na lengo hasa kutaka kumsaidia Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa Ambaye ni rais wa Tanzania Dkt John Magufuli katika kutekeleza majukumu Yake.

  Akizungumza na Halmashauri kuu ya CCM kata ya Viazi Jana wilayani humo .alisema kuwa Kwa Dkt.Magufuli hakuna jambo la uzoefu kwake yeye ni Kazi tu.nakudai watu walidhani wimbo wa mabadiliko Kwa Dkt. Magufuli ilikuwa ni mzaha na sasa namba inasomeka kweli.

  "Mkitaka kujuwa Kuwa rais Dkt.Magufuli hakuna uzoezi angalieni Leo anachofanya Paul Makonda Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Kazi anayoifanya nikijana ambaye ametoka chuo juzi na akaaminiwa na wakubwa Leo anapiga Kazi hivyo lazima vijana tujiamini "alisema Mbunge Ulega.

  Akizungumza na Halmashauri kuu ya Kata ndani ya CCM alitumia mkutano huo kuwapongeza Kwa Kazi kubwa ya kukipambania Chama ambayo waliifanya katika Uchaguzi ulimalizika mwaka 2015.

  Alisema kutokana na Kazi hiyo kubwa ambayo wameifanya yeye kama Mbunge ameamua kutoa Zawadi Kwa Kata Kumi ambazo kiukweli waliongoza Kwa kukipa kura nyingi Chama cha Mapinduzi CCM hivyo ameamua kutoa zawaidi ya Pikipiki.Mbunge Ulega aliwasisitiza wanaCCM kuhakikisha wanamuunga mkono Kwa asilimia mia moja Rais Dkt.Magufuli ambaye amedhamiria kuwatumikia watanzania kivitendo.

  "Lazima tufanye Kazi ya kuwatimikia watanzania na hasa kutimiza ahadi zetu ambazo tulizitoa Kwa wananchi ili hata tutakaporudi mwaka 2020 ili iwe kazi nyepesi kuwaambia wananchi kwamba tumetekeleza moja mbili Tatu."alisema Ulega.Aidha aliwataka wanaCCM kuondoa fitina na majungu katika kipindi hiki bali kazi iliyokuwa mbele ni kuchapa Kazi Kwa ajili ya wananchi na si vinginevyo.

  Ulega pia aliwaeleza makada hao wa Chama cha Mapinduzi aliwahakikishia kuwa hadi kufikia mwaka 2020 kushirikiana na wanaCCM kujenga Ofisi za Kata ndani Chama.
   Mbunge wa mkuranga Mh Abdala Ulega akimkabidhi Pikipiki Mwenyekiti wa vianz Bw Rashid Gadaf . Picha zote na Yasir Adam Blogu ya Jamii. 
   Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Mh Abdala Ulega akizungumza na wajumbe wa Halmashaur kuu kupitia chama cha CCM kata ya vianzi wilayani Mkuranga ,Wakati huohuo Mh.Ulega  alikabidhi Pikipiki Kwa Viongozi wa  Chama cha Mapinduzi CCM Kata  Viazi Mara baada ya kualikwa Kwenye mkutano wa ndani wa  Halmashauri kuu  ya CCM  Kata hiyo.
  Diwani wa Kata ya Vianzi akizungumza na wajumbe ya Halmashaur kuu wa kata ya vianzi kupitia chama cha Ccm wilayani mkuranga
  Mwenyekuti wa Kata ya Vianzi Bw Rashid Gadafi akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu kutoka chama cha Ccm wilayani mkuranga.

  0 0


  https://si.se/swedish-lucia-for-dummies/
  #LuciaInTz and #SwedenInTz.


  0 0
  0 0

  The prime minister of Tanzania Hon. Kassim Majaliwa led a number of Dsm citizens in the fundraising gala dinner held over the weekend. The event, themed ‘“A Desk for every child”  was organized by the Hassan Maajar Trust in association with Bank M, and was aimed at raising funds for  providing desks to students for Primary schools in the country. During the event TZS 203mio was raised.

  Speaking during the event, Hon. Majaliwa – who was the chief guest, said that the efforts shown by the Hassan Maajar Trust and its partners in serving the community deserves recognition. He congratulated Bank M which has been the main sponsor of HMT since inception in the year 2011 and encouraged them to continue with their corporate social responsibility strategy in supporting the key sectors of national development.

  Speaking at the end of walk, the HMT Chairperson, Ambassador Mwanaidi Maajar said the support extended by its corporate partners has continuously contributed to the success of the project. “Since its launch, HMT in partnership with the public and corporate Tanzania has succeeded to provide over 9,100 desks lifting over 30,000 boys and girls off the floor onto desks in thirteen regions of Tanzania, thanks to all our sponsors” said Ambassador Maajar.

  Bank M’s CEO Designate Ms. Jacqueline Woiso said that the bank is proud to be partnering with the Hassan Maajar Trust in such a noble cause and commended the Trust for an ongoing job well done in the previous years. “Having over 30,000 children lifted off the floor and seated on desks is an achievement we can all be proud of. We have jointly made sitting on the floor a history for thousands of Tanzanian school children. It is our policy to work together with other reputable organization in making a difference to the needy communities of this land” said Ms. Woiso 

  HMT is dedicated towards improving the learning environment in schools by addressing and tackling the national school desk deficit across Tanzania.
  The Prime Minister of Tanzania Hon. Kassim Majaliwa receiving a dummy cheque from the Deputy Secretary, Ministry of Education, Science and technology Dr. Leonard Akwilapo during the fundraising event took place last night at diamond Jubilee which was organized by the Hassan Maajar Trust in partnership with Bank M with the aim of raising funds to improve learning environment in schools. Looking on is the Bank M CEO designate Ms. Jacqueline Woiso (centre) and the Hassan Maajar Trust Board chair Amb. Mwanaidi Maajar.

  0 0

  KAIMU Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Thobias Mwilapwa amewakata wawekezaji kutoka nchini India kuwekeza mkoani humo kutokana na kuwepo kwa fursa nyingi za kiuchumi zikiwemo kilimo, utalii, elimu na Afya ili kuweza kunufaika nazo.

  Mwilapwa alitoa kauli hiyo juzi wakati akifungua kongamano la kibiashara kati ya Tanzania na India uliofanyika katika hotel ya Tanga beach jijini Tanga uliowahusisha wafanyabiashara kutoka India na Mkoa wa Tanga.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Mnauye (katikati) akizungumza jambo na Balozi wa India nchini, Sandeep Arya (kushoto) wakati wa kongamano la wafanyabiashara kati ya Tanzania na India uliofanyika katika ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Resort, Mkoani Tanga.  kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Mhandisi Zena Saidi.

  Kongamano hilo lilikuwa na lengo lilikuwa ni kushirikisha mawazo na kuona ni kwa namna gani wanaweza kuzitumia fursa mbalimbali zilizopo mkoani hapa ili kufanya uwekezaji ambao utaweza kuleta tija ya kimaendeleo.

  Alisema kuwa India ni miongoni mwa nchi ambazo zimesaidia kukuza uchumi kwa baadhi ya nchi ikiwemo Tanzania hivyo uwepo wao katika suala la uwekezaji linaweza kuwa chachu ya kuweza kuinua kasi ya ukuaji wa maendeleo.

     “India ni miongoni mwa nchi ambazo zimesaidia kukua kwa uchumi kwa baadhi ya nchi dunia ikiwemo Tanzania kutokana na hilo niwatake muona namna ya kuwekeza mkoani hapa kwani yapo maeneo mengine mnayoweza kufanya hivyo “Alisema.

  Balozi wa India nchini Tanzania, Sandeep Arya akizungumza wakati wa kongamano hilo kushoto kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Mhandisi Zena Saidi na Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Mnauye.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi awasili Mkoani Kigoma kwa Ziara ya siku tatu za utatuzi wa migogoro ya ardhi.
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akipokelewa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe.Brigedia Jenerali Emanuel Maganga.
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akisalimiwa Mbunge wa Kigtoma Mjini Mhe. Zitto Kabwe.

  0 0


  0 0

  East African Community Headquarters, Arusha, Tanzania, November 28th, 2016: The 6th Africa Regional Platform (AfRP) on Disaster Risk Reduction (DRR) concluded over the weekend in Mauritius.

  It was organized by the African Union and United Nations International Strategy for Disaster Risk Reduction and co-hosted by the SADC and the Government of Mauritius. The East African Community was represented both at the Experts segment and in the High Level Ministerial Session by Mr. Jean Baptiste Havugimana, the Director for Productive Sectors.

  The AfRP is a biennial forum that brings together African Member States, intergovernmental organizations and development partners to review progress in the implementation of the continental and global disaster risk reduction frameworks.
  The 6th AfRP on DRR is the first continental meeting on DRR organized after the adoption of the Sendai framework on DRR by UN member states in Sendai, Japan in March 2015. The Framework provides a critical strategy for building resilience and addressing the impact of disasters representing a serious threat to millions of people in Africa and across the world. The 6th AfRP was a concrete opportunity for Africa to set up a functional path to alleviate the suffering of the most vulnerable communities in Africa.

  The Platform also enabled delegates sharing of good practices, success stories and lessons learnt with a view to enhancing coordination, increasing awareness, and mobilizing commitments to disaster risk reduction across Africa.
   The outcome of the 6th Africa Platform on DRR is an Africa Statement of DRR, the Mauritius Declaration on continental commitment and a revised Programme of Action on DRR for Africa.

  During the Experts segment, Mr. Jean Baptiste Havugimana was a panelist under the theme: “Risk governance to showcase the status of EAC in implementing the Sendai Framework and the role of the DRR Act in achieving priority two of the Sendai Framework - Enhancing Risk governance”. 

  Mr. Havugimana further presented during the Ministerial Session the EAC Position Paper and Commitment in the implementation of the Sendai Framework. The Statement was a summary of discussions held by all EAC delegations during their session as a REC.

  0 0

  Na Felix Mwagara, MOHA.

  WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amefanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini, Sara Cooke na kumuakikishia ushirikiano zaidi kati ya Wizara yake na Ubalozi huo nchini.

  Mazungumzo hayo ya zaidi ya saa moja yalifanyika ofisini kwa Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo ambayo yalijadili masuala mbalimbali ikiwemo uimarishaji wa ushirikiano kati ya Wizara na ofisi ya Balozi huyo nchini.

  Waziri Mwigulu alimuakikishia Balozi huyo kuwa Tanzania itaendelea kuwa salama kwa kuwa Wizara yake imejipanga vizuri kuendelea kuwalinda raia na mali zao pamoja na wageni wote waishio nchini.

  “Mheshimiwa Balozi nashukuru sana kwa kunitembelea, najisikia furaha kwa ujio wako na karibu sana wakati wowote, Wizara yangu pamoja na nchi yangu kwa ujumla tutaendelea kushirikiana nanyi katika masuala mbalimbali,” alisema Mwigulu.

  Hata hivyo, Balozi Sara alimshukuru Waziri Mwigulu kwa mazungumzo waliyoyafanya na kumuhakikishia ushirikiano zaidi kati ya Uingereza na Tanzania.

  Pia kikao hicho kiliudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira pamoja na Naibu Balozi wa nchi hiyo, Matt Sutherland.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini, Sara Cooke (kulia) masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Uingereza na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo.
  Balozi wa Uingereza nchini, Sara Cooke (wapili kulia) akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati), kuhusiana na masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi yake na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira, na kulia ni Naibu Balozi wa nchi hiyo, Matt Sutherland.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto) akimshukuru Balozi wa Uingereza nchini, Sara Cooke, mara baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika ofisini kwa Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo. Balozi huyo alimtembelea Waziri huyo kwa lengo ya kujadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Uingereza.

  0 0

  Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania imetangaza dhamira yake ya kuuza hisa kwa umma itakayofuatiwa na   kujiunga kwenye   Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) ikiwa ni utekelezaji wa sheria ya  Elektroniki na Mawasiliano ya Posta (EPOCA) na sheria ya Fedha ya mwaka 2016 ambayo inaelekeza makampuni ya simu  kumilikisha  asilimia 25 ya hisa zake kwa wananchi kwa kujiunga na Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).
  Akizungumzia  hatua hiyo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom, Bwana Ian Ferrao (pichani) alisema “Tunayo furaha kutangaza kuwa tumeanza rasmi mchakato wa kuuza hisa kwa umma kwa mujibu wa matakwa ya sheria na  tumewasilisha maombi na utaratibu mzima utakaotumika kuuza hisa zetu na ratiba yetu nzima kuhusiana mchakato huu kwenye Mamlaka ya Usimamiaji wa  Masoko ya Mitaji  na Dhamana (CMSA) na Soko la Hisa  (DSE).   Hatua hii ni kubwa na inadhihirisha kuwa Vodacom ipo mstari wa mbele katika kutekeleza agizo la kuuza hisa zake kwa umma  na inadhihirisha jinsi ilivyojipanga  kuendelea kuboresha na kukuza sekta ya mawasiliano nchini Tanzania katika siku za usoni”.
  Uuzaji wa hisa kwa umma  na kujiunga na Soko la Hisa kunapitia  hatua mbalimbali za  kupata vibali kutoka taasisi za serikali zenye mamlaka ya kupitia maombi na kutoa  vibali vya utekelezaji wake.Ferrao aliendelea kueleza “Tunaamini uuzaji wa hisa zetu kwa umma utazidi kukuza shughuli za Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE),kunufaisha watanzania kiuchumi na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla.Kampuni yetu haitajulikana kwa jina la mwanzo la Vodacom Tanzania Limited bali imekuwa na jina la
  Vodacom Tanzania Public Limited Company (Plc) ikiwa ni hatua ya awali ya kujiandaa kuingia sokoni. Tunawahakikishia kuwa mchakato wa kuingia kwenye hatua hii umeanza vizuri kwa mafanikio na tunaendelea kuwashirikisha wadau mbalimbali kutoka serikalini kuhakikisha tunatimiza dhamira ya kuanza  kuuza hisa kwa wananchi yenye dira ya kuleta manufaa kwa wote.”
  Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao,(kulia) akimkabidhi hati ya maombi ya kujiunga na soko la hisa la Dar es Salaam,(DSE)  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji na Dhamana (CMSA) Nicodemus Mkama(wapili kushoto) wakati wa hafla fupi iliyofanyike mwishoni mwa wiki katika ofisi za CMSA jijini Dar es Saalaam,Kushoto ni Meneja Uhusiano wa CMSA, Charles Shirima.
  Mkurugenzi wa  Ushauri wa kutoka huduma za Orbit Securities Company Ltd. Gerase Kamugisha(kushoto)Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao, Mkurugenzi Mtendaji wa DSE,Moremi Marwa, Mkuu wa masuala ya kifedha  wa Orbit Securities Company Ltd, Godfrey Gabriel, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia,wakionyesha hati za maombi ya kuijiunga na soko la hisa la Dar es Salaam,(DSE) mwishoni mwa wiki.
  Ferrao alitoa msisitizo kuwa Vodacom inalo jukumu kubwa kuhakikisha hatua hii inaleta manufaa kwa pande zote zinatazohusika kuanzia  wanunuaji wa hisa, kuendelea kuwekeza , kuendelea kuleta mapinduzi ya ubunifu wa kiteknolojia na kuimarisha ubora wa huduma za kampuni kwa wateja wake “Tutaendelea kutoa mchango mkubwa wa ufanikishaji wa sera ya nchi ya miaka 5 ya kukuza sekta ya mawasiliano.Tutaendelea pia kuwaletea taarifa mbalimbali kuhusiana na mchakato wa kuuza hisa kwa umma unavyoendelea”Alisema Ferrao.

  0 0

  Wanafunzi wawili wa shule ya Academic International ya Tanzania wameweka historia katika mitihani ya mtahala wa Cambridge baada ya kushinda nafasi ya kwanza duniani katika masomo ya hisabati na kompyuta.

  Wanafunzi hao ni Harshvardhan Babla aliyekuwa wa kwanza katika mtihani wa somo la kompyuta kwa wanafunzi wa kidato cha tano Abishek Sankaranarayanan aliyeshinda nafasi ya kwanza katika mtihani wa hisabati kwa wanafunzi wa kidato cha nne.

  Wanafunzi hao walikabidhiwa vikombe na vyeti na mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni wa India, Inder Jit Sagar. Pia walimu wa masomo hayo, Thadei Mwinuka ambaye anafundisha somo la kompyuta na Walter Mlowe wa somo la hisabati nao walikabidhiwa vyeti vya pongezi kwa kufanya vizuri.

  Akizungumza katika halfa maalum ya kuwapongeza wanafunzi hao na walimu wa masomo hayo, Mkuu wa shule hiyo, Shyama Santhosh alisema kuwa wamefarijika na ushindi huo ambao umeiletea sifa shule, walimu nan chi kwa ujumla.

  “Huu ni ushindi mkubwa kwa shule, walimu nan chi kwa ujumla, mtihani wa Cambridge unafanywa na maelfu ya shule duniani na shule yetu imeibuka katika nafasi ya kwanza kwa masomo hayo mawili, ni jambo la kujivunia sana, hii inaonyesha kuwa walimu wetu wapo makini katika kufundisha,” alisema Santhosh.

  Mkurugenzi wa shule hiyo, Yusuf Kalindaga amesema kuwa wanajivunia kwa matokeo hao mazuri ambayo yamewafanya kuwa shule pekee Tanzania kushika nafasi hizo za kwanza.
  Wanafunzi wa shule ya Academic International school, Harshvardhan Kabla (kushoto) ambaye ameshika nafasi ya kwanza duniani katika somo la Kompyuta kwa wanafunzi wa “A Level” kwa mitihani ya Cambridge na Abishek Sankaranarayanan(kulia) ambaye ameshinda nafasi ya kwanza kwa somo la hisabati kwa mitihani ya Cambridge kwa wanafunzi wa kidato cha nne wakiwa katika picha ya pamoja katika sherehe maalum ya kuwapongeza.
  Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni wa India, Inder Jit Sagar akimkabidhi cheti na kombe mwanafunzi wa Shule ya Academic International, Harshvardhan Kabla (kulia) kwa kushinda nafasi ya kwanza duniani katika somo la Kompyuta kwa wanafunzi wa “A Level” kwa shule zinazofuata mtahala wa Cambridge.
  Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni wa India, Inder Jit Sagar akimkabidhi cheti na kombe mwanafunzi wa Shule ya Academic International, Abishek Sankaranarayanan(kulia) kwa kushinda nafasi ya kwanza duniani katika somo la Hisabati kwa wanafunzi wa “O Level” kwa shule zinazofuata mtahala wa Cambridge.
  Baadhi ya wazazi na wanafunzi wa shule ya Academic International wakiwa katika hafla hiyo .
  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu kwenye chumba cha watu mashuhuri cha uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dr es salaam Novemba 28, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Mchechu kwenye uwanja wa ndge wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Novemba 28, 2016.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo (aliyesimama) akiongea na madereva wa boda boda kuwaelezea mpango wa Serikali wa kuwapatia Pikipiki 200.

  Nteghenjwa Hosseah

  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo amekutana na waendesha bodaboda wa Jiji la Arusha na kuwajulisha kuhusu mpango wa Serikali wa kuwakwamua kiuchumi kwa kuwawezesha kupata Pikipiki bila Riba wala dhamana.

  Rc Gambo amekuja na Mpango huu wa Kuinua uchumi wa Vijana kwa kuwapatia Pikipiki baada ya kukutana na kundi hili la waendesha boda boda kwa mara na kusikiliza malalamiko yao huku miongoni mwa kero yao kubwa ni kutozwa fedha nyingi na wamiliki wa boda boda hizo.

  Akiongea na waendesha boda boda Rc Gambo alisema ninaona jinsi mnavyojituma katika kujitafutia riziki lakini hamthaminiki na kazi hii imekua ikidharaulika, sasa muda umefika kwa kazi hii kuwa ya heshima mbele ya Jamii, kila kijana aliyepo katika biashara hii ataweza kumiliki Pikipiki yake na sio kuendesha Pikipiki za watu ambao wamekuwa wakiwanyonya kila siku kwa kuwatoza Fedha nyingi na wao kuzidi kuneemeka wakati ninyi mnazidi kuwa masikini.
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (Katikati) akiwasili kwenye Kikao na waendesha bodaboda wa Jiji la Arusha.

  “Kundi hili limekuwa likitumiwa kwa maslahi ya watu wachache kwa kuwa wamekuwa wakipewa Pikipiki hizo kwa faidi kubwa na mmiliki anapokea Fedha zaidi yya mara mbili ya bei ya kununulia Pikipiki hiyo ndipo aamue kummilikisha kijana pikipiki hiyo au aamue kuendelea kupokea Fedha kwa kipindi chote wakati ninyi mnapata tabu barabarani huko na mnaambulia Fedha kidogo kiasi ambacho hamuwezi fikia hatua ya kumiliki Pikipiki zenu” Alisema Gambo.


  0 0  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Rais wa Chad, Idriss Deby kwenye uwanja wa ndege wa Julius kambarage Nyerere jijini Dar es salaam kabla ya Rais huyo kuondoka nchini Novemba 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Rais wa Chad, Idriss Deby  kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam wakati Rais huyo alipoondoka nchini Novemba 28, 2016.
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Rais wa Chad, Idriss Deby  kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere wakati Rais huyo alpoondoka nchini Novemba 28, 2016. 
   Rais wa Chad, Idriss Deby akiwapungia wananchi kwenye uwanja wa ndege wa Dar es salaam wakati alipoondoka nchini Novemba 28, 2016. Kulia ni  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  ambaye alimsindikiza na kushoto ni mke wa Rais wa Chad, Hinda Deby.
   Rais wa Chad, Idriss Deby akipokea heshima kwenye uwnja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere wakati alipoondoka nchini Novemb 28, 2016.  Kushoto kwake ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye alimsindikiza. 

  0 0


  Na Dotto Mwaibale

  UJUMBE wa watu sita kutoka Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) umewasili nchini kwa ziara ya siku saba kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM)

  Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ramadhani Madabida alisema ujumbe huo umeongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Mahusiano ya Kimataifa, Maendeleo na Mafunzo wa Chuo cha Viongozi wa chama hicho, Jia Bo.

  Madabida alisema ziara ya ujumbe huo hapa nchini ni kudumisha ushirikiano baina ya Tanzania na China ulioasisiwa na Hayati Baba wa Taifa na kiongozi wa Taifa hilo Hayati Mao  Tse-Tung.

  Alisema ujumbe huo ambao utatembelea Wilaya ya Temeke na Zanzibar umewasili nchini kufuatia ziara ya baadhi ya makada wa CCM walipokwenda nchini China ambapo walijifunza mambo mbalimbali ambayo ujumbe huo utapenda kujua kama wameyafanyia kazi.

  Mratibu wa Masuala ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Pindi Chana alisema ujio wa viongozi wa chama hicho kutoka China ni matunda ya ushirikiano wa Tanzania na nchi mbalimbali duniani.

  " Ujio wa wenzetu hawa kutoka China ni matunda ya ushirikiano kati yetu na nchi nyingine kama Zimbabwe, Afrika Kusini, Angola, Cuba,  Ulaya hasa katika siasa za kijamaa" alisema Chana.

  Alisema wenzetu wa China wapo karibu bilioni moja na wamepiga hatua katika maeneo mbalimbali hivyo ujio wao hapa nchini ni fursa kwao kujifunza mambo yetu na sisi kujifunza kwao kutokana na hatua ya kiuchumi waliyonayo.
   Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),  Mkoa wa Dar es Salaam Ramadhani Madabida (kushoto), akimkabidhi Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015,  Mkurugenzi wa Idara ya Mahusiano ya Kimataifa, Maendeleo na Mafunzo wa Chuo cha Viongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China, Jia Bo,  Dar es Salaam leo asubuhi, ambaye yupo nchini na wajumbe wenzake sita kwa zaiara ya siku saba ya kichama kukitembelea Chama Cha Mapinduzi (CCM).
   Mkutano ukiendelea.
   Wajumbe hao wakisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida.
   Makada wa CCM wakijumuika na wajumbe wenzao kutoka china.

  0 0

  Vyombo vya baadhi ya wakazi wa nyumba za Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam vikitolewa nje baada ya wamiliki wa nyumba kushindwa kulipia nyumba hizo kwa mujibu mikataba waliyokubaliana na Shirika hilo. (Picha na Francis Dande).
  SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), limeendelea na kazi ya kuwaondoa wadaiwa sugu. 

  Wadaiwa hao ni wale walionunua nyumba na kushindwa kulipa deni lililobaki kwa muda uliopangwa.

  Akizungumza jjijini Dar es Salaam, Kaimu Meneja Mipango na Uwekezaji wa NSSF, Radhia Tambwe, alisema kwamba nyumba hizo ni za Mtoni Kijichi ambapo alisema kwamba kazi hiyo itafanyika kwa wadaiwa  saba.

  “Wakazi wa nyumba zote hizo walitolewa na kampuni ya udalali ya Majembe Action Mart kwa kushirikiana na NSSF,”alisema.

  Aidha alisema kwamba wadaiwa hao waliondolewa katika nyumba hizo baada ya taratibu za kisheria kufuatwa hivyo nyumba hizo zitauzwa kwa watu wengine.

  Aidha alisema kwamba kazi hiyo ni endelevu kwa wale watakaoshindwa kulipa madeni yao kama mikataba inavyosema.

  Shirika la NSSF limewataka walionunua ama kupanga nyumba kulipa kwa mujibu wa mikataba yao ili kuepuka adha ya kutolewa vyombo vyao nje na kupata hasara.


  0 0


    Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Homa ya Ini na Matumbo wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk John Lwegasha akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu kuanza kwa uchunguzi na tiba ya homa ya INI (Hepatitis B) katika hospitali hiyo. Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba, Dk Hedwiga Swani na Dk Eva Owisso wa Muhimbili wakifuatilia mkutano huo.
   Mkurugenzi wa Huduma za Tiba, Dk Hedwiga Swai akifafanua jambo kwenye mkutano huo leo.
  “Hatua hiyo kuifanya Tanzania kuwa nchi ya pili Ukanda wa Afrika Mashariki katika udhibiti na tiba ya ugonjwa huo”
  Hospitali ya Taifa Muhimbili  (MNH), Disemba Mosi mwaka huu inatarajia kuanza kufanya uchunguzi wa Virusi vya Homa ya Ini (Hepatitis B) na kutoa tiba bure ya  ugonjwa huo kwa kutumia dawa ya Tenofovir na hivyo kuifanya Tanzania kuwa nchi ya pili Ukanda wa Afrika Mashariki baada ya Rwanda katika udhibiti na kutoa tiba ya ugonjwa huo.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ini na Matumbo, John Lwegasha amesema ni wakati muafaka wa watu kujitokeza na kupima afya zao kwa ujumla na kwa wale waliothirika na ugonjwa huo wajitokeze ili kufanyiwa uchunguzi zaidi na kupata nafasi ya tiba kulingana na miongozo ya tiba inavyoelekeza.

  “Utaratibu mwingine wa uchangiaji wa gharama za matibabu katika maeneo mengine ya uchunguzi na tiba ikiwa ni pamoja na uchangiaji wa gharama za kumuona Daktari utabaki kama ulivyo,” amesema Dk. Lwegasha.

  Tatizo la ugonjwa huo Tanzania, kwa mujibu wa Dk . Lwegasha inakadiriwa kuwa watu wanane kati ya watu mia moja wana maambukizi ya ugonjwa huo na kwamba kiwango hicho ni kikubwa zaidi ya kile kinachokadiriwa kwenye maambukizi ya Ukimwi kitaifa ambacho ni asilimia pungufu ya sita.
  “Katika Hospitali ya Taifa Muhimbili asilimia 60 ya wagonjwa wanaokutwa na Saratani ya Ini mara nyingi imetokana na maambukizi ya virusi hivyo,” amesema Dk. Lwegasha.

  Kuhusu tiba amesema kama ilivyo kwa ugonjwa wa Ukimwi , ugonjwa huo sugu wa Homa ya Ini hauna tiba ya kuponya isipokua dawa zilizopatikana hadi sasa zinaweza kupunguza kasi ya maambukizi mwilini na kuzuia madhara kwenye Ini.

  Ugonjwa wa Homa ya Ini ( Hepatitis) unasababishwa na Virusi viitwavyo Hepatitis B na maambukizi yaugonjwa huo yanashahabiana na njia ya maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi kama vile kufanya ngono zisizo salama , kuchangia sindano au vikatio, kupewa damu isiyopimwa , kupitia uzazi wa mama na mtoto hasa wakati wa kujifungua.

  0 0

   Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo akikagua ujenzi wa barabara ya lami ya Sango katika eneo la Soko kuu la majengo, Manispaa ya Dodoma.
    Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo akipokea maelezo ya ujenzi wa barabara ya lami ya Sango katika eneo la Soko kuu la majengo, Manispaa ya Dodoma.
   Dampo la kisasa lilojengwa katika eneo la Chidaye Manispaa ya Dodoma.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, Godwin Kunambi kuhusu mtaro uliopo katika Dampo la kisasa eneo la Chidaye.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

older | 1 | .... | 1442 | 1443 | (Page 1444) | 1445 | 1446 | .... | 3284 | newer