Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1441 | 1442 | (Page 1443) | 1444 | 1445 | .... | 3272 | newer

  0 0


  Na Mathias Canal, Bukoba
  Kukosekana kwa huduma bora na msingi kwa wazee nchini imetajwa kuwa changamoto kubwa kwa Wazee waishio katika kambi mbalimbali za serikali na zile za binafsi.

  Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Asasi isiyokuwa ya Kiserikali ya METDO Tanzania (Mining and Environmental Transformation for Development  Organization) Bw Ashraf Omary wakati akikabidhi mahitaji kwa wazee wa kituo cha KIILIMA kilichopo Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera.

  Bw Omary alisema kuwa Asasi hiyo yenye usajili No. ooNGO/08317 inajishughulisha na kutoa Elimu ya Mazingira kwa wananchi wanozunguka migodi pamoja na wafanyakazi wa migodini ambapo pia imejikita kuwasaidia wazee waishio katika kambi mbalimbali nchini katika huduma za kuwapatia mahitaji ya msingi ya kila siku kama vile (Chakula, na Mavazi) sambamba na kutoa huduma ya upimaji wa afya zao kupitia wataalamu wa tiba na kuwapatia dawa kwa ajili ya matibabu ya magonjwa mbalimbali.

  Alisema kuwa kumekuwa na wimbi kubwa la wazee kutopatiwa huduma bora ikiwemo chakula na matibabu jambo ambalo kwa kiasi kikubwa linachangia wazee wengi kufariki pasina huduma yoyote ya kitabibu sambamba na kukosa Lishe Bora.

  Bw Omary ameushukuru uongozi wa kampuni ya ZONGII PUMBLING LTD ya Jijini Mwanza kwa kushirikiana na METDO Tanzania kufanikisha kupatikana mahitaji mbalimbali kwa ajili ya wazee wa kambi ya KIILIMA sambamba na kuupongeza uongozi wa Mkoa wa Kagera kwa ushirikiano ulioonyesha ikiwa ni pamoja na kuruhusu madaktari kwa ajili ya kwenda kuwapima afya wazee hao.

  Kwa upande wake Meneja Mradi wa METDO Tanzania Bw Hussein Sungura amebainisha kadhia zinazowakumba wazee katika kituo cha KIILIMA sambamba na vituo vingine nchini kuwa ni pamoja na ukosefu wa huduma za usafiri ili kurahisisha wazee kufikishwa haraka hospitalini pindi wauguapo, Ufinyu wa Bajeti, Ukosefu wa vitendea kazi kama vile vifaa vya usafi na ucheleweshaji wa Ruzuku ya serikali.

  Sungura alisema kuwa Mpaka sasa Asasi hii ya METDO Tanzania imesaidia katika maeneo mbalimbali ikiwemo tukio la Agosti 13, 2016 la kumuenzi Mwl Julius Kambarage Nyerere katika Makao ya wazee wasiojiweza BUKUMBI Mwanza, Tukio la Octoba Mosi 2016 SIKU YA WAZEE DUNIANI katika wilaya ya Shinyanga ambapo jamii ilishirikishwa kutambua changamoto zilizopo katika kituo cha Wakoma na Wazee wasiojiweza cha KOLANDOTO pamoja na Kituo cha Wakoma na  Wazee wasiojiweza cha NYABANGE BUTIAMA  na kuwa sehemu ya kuzitatua changamoto hizo.
  Mratibu wa Asasi isiyokuwa ya kiserikali ya METDO Tanzania  Mathias Canal akimkabidhi Kaimu Mkuu wa Kituo cha Wazee KIILIMA Bi Gladness Lwiza baadhi ya mahitaji kwa ajili ya wazee waishio kituoni hapo.
  Kushoto ni Mkurugenzi wa Asasi isiyokuwa ya Kiserikali ya METDO Tanzania (Mining and Environmental Transformation for Development  Organization) Bw Ashraf Omary akimsikiliza kwa makini mzee aliyelala kutokana na homa kali inayomsumbua
  Pichani katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salum Kijuu, Kushoto kwake ni Mathias Canal Mratibu wa Asasi isiyokuwa ya kiserikali ya METDO Tanzania, Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Kagera Ndg Charles  Mafimbo, Kulia kwa Mkuu wa Mkoa ni Hussein Sungura Meneja Mradi METDO Tanzania na Mkurugenzi wa METDO Tanzania Ndg Ashrafu Omary
  Mkurugenzi wa METDO Tanzania Bw Ashraf Omary mwenye Jembe akimsaidia kazi Mzee Wilson Ziraimani, Mzee huyu alikuwa anafanya kazi za kilimo katika mashamba mbalimbali nchini, yeye ni mkazi wa Ngara na wakati akiwa mtoto alikuwa analelewa na Mama wa kambo.
  Aliwasili katika kituo cha kulelea Wazee cha KIILIMA Mwaka 1986 hapo alipo anatambaa kwani alivunjika kiuno enzi za ujana wake baada ya kuanguka mtini wakati alipokuwa anakata kuni kwa ajili kupikia.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Peter Mavunde akiwa pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla ya kukabidhi madawati 20 yaliyotolewa na Mtandao wa Wapenda soka wa Kandanda kwa shule hiyo. Hafla hiyo imefanyika Novemba 26, 2016 jijini Dar es salaam.
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Peter Mavunde akifurahi jambo na wanfunzi hao mara baada ya kukabidhi madawati.
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Peter Mavunde akizungumza kabla ya kukabidhi madawati 20 yaliyotolewa na Vijana wa Mtandao wa Kandanda.
  Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Ubungo Plaza,Renatus Pathi akizungumza wakati wa hafla ya kupokea madawati iliyofanyika shuleni hapo .


  0 0

  Rais Mstaafu awamu ya nne,Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa njiani kurejea kijijini kwake Msoga, alisimama Ruaha Mkuu mkoani Iringa na kununua vitunguu na kuwaungisha vijana hao wanaojishughulisha na kilimo cha vitunguu.
  Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa na vijana wajasiliamali hao ambao ni maarufu kwa ulimaji na uuzaji wa vitunguu

  0 0

  Wakazi wa Kibamba Wilayani Ubungo wamezuia msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda huku wakiwa wamebeba mabango yanayoonesha kero zao mbalimbali ikiwemo na kero ya kudhulimiwa maeneo yao ya.

  Akizungumza na wakazi hao waliokuwa wamesimamisha msafara huo, Mkuu wa Wilaya hiyo Humphrey Polepole aliwataka wakazi hao kufuata utaratibu Kwani madai yao yamefika mezani kwake na baadhi yameanza kushughulikiwa kwa watu kulipwa fidia zao kutokana na kupisha eneo la chuo na hospitali ya MUHAS .

  DC Polepole amesisitiza kuwa serikali ipo pamoja na wananchi hao ambao wengine wanadai fidia ya eneo la kwembe na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete aliahidi kuwa watalipwa, vilevile Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliwahidi kuwa serikali itazifanyia kazi ahadi zote zilizoachwa na serikali iliyopita. 

  DC Polepole ameongeza kuwa kwa wale wakazi waliopo maeneo ya hifadhi ya barabara serikali itaendelea na msimamo wake wa upanuzi wa barabara kama alivyohaidi Rais Magufuli jana kwenye Mkutano wa hadhara wa RC Makonda uliofanyika Maramba Mawili.

  Kwa upande wake RC Makonda ambaye alishuka baada ya wakazi hao kuonekana kugoma kupisha msafara hu na kuwaambia kufuata utaratibu kutokana na majibu ya awali ya DC Polepole.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza na wananchi wa Kibamba Wilayani Ubungo huku wakiwa wamebeba mabango yanayoonesha kuwa wamedhulumiwa ardhi yao.
  Mkuu wa Wilaya ya Ubungo,Humphrey Polepole akizungumza na wananchi wa Kibamba Wilayani Ubungo huku wakiwa wamebeba mabango yanayoonesha kero zao mbalimbali wanazotaka zipatiwe majibu
  wananchi wa Kibamba Wilayani Ubungo wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda alipokuwa akizungumza nao kwenye ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero za Wananchi.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii


  0 0  Afisa Mradi, Kitengo cha Kujenga Uwezo kutoka shirika lisilo la Kiserikali la 'The Foundation For Civil Society' Nasim Losai, akizungumza na Vijana wajasiliamali kutoka Mikoa mbalimbali ya Tanzania walioshiriki Mafunzo ya Siku tano ya Ujasiliamali, Fursa na Taratibu za kufanya biashara kuelekea Soko la Jumuiya ya Afrika Mashari. Nasimi alifunga mafunzo hayo yaliyomalizika juzi Nov 25, 2016 kwenye Hoteli ya Blue Pearl Ubungo Plaza.
  Afisa Mradi, Kitengo cha Kujenga Uwezo kutoka shirika lisilo la Kiserikali la 'The Foundation For Civil Society' Nasim Losai, akizungumza na Vijana wajasiliamali kutoka Mikoa mbalimbali ya Tanzania walioshiriki Mafunzo ya Siku tano ya Ujasiliamali, Fursa na Taratibu za kufanya biashara kuelekea Soko la Jumuiya ya Afrika Mashari. Nasimi alifunga mafunzo hayo yaliyomalizika juzi Nov 25, 2016 kwenye Hoteli ya Blue Pearl Ubungo Plaza.
  Afisa Mradi, Kitengo cha Kujenga Uwezo kutoka shirika lisilo la Kiserikali la 'The Foundation For Civil Society' Nasim Losai, akizungumza na Vijana wajasiliamali kutoka Mikoa mbalimbali ya Tanzania walioshiriki Mafunzo ya Siku tano ya Ujasiliamali, Fursa na Taratibu za kufanya biashara kuelekea Soko la Jumuiya ya Afrika Mashari. Nasimi alifunga mafunzo hayo yaliyomalizika juzi Nov 25, 2016 kwenye Hoteli ya Blue Pearl Ubungo Plaza.
  Afisa Mradi, Kitengo cha Kujenga Uwezo kutoka shirika lisilo la Kiserikali la 'The Foundation For Civil Society' Nasim Losai, akifurahia na Vijana hao wakati wakiimba wimbo maalum.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo amehitimisha ziara yake Mkoani Tanga huku akionesha kuchukizwa na kitendo cha Wahandisi wa ujenzi Katika Halmashauri za mkoa huo kwa kutozingatia mahitaji ya wanafunzi wenye ulemavu.

  Jafo alifanikisha ziara yake ya siku tatu kwa kutembelea Halmashauri zote za mkoa wa Tanga. Katika ziara yake mkoani huo, Jafo alikagua ujenzi wa vyoo vinavyo jengwa katika shule mbalimbali za sekondari mkoani Tanga kupitia mradi wa SEDEP II.

  Akizungumza mara baada ya ziara yake, Jafo alisema amegundua vyoo vyote vilivyo kamilika na vinavyo endelea kukamikishwa mkoani huo havijazingatia kuweka miundombinu ya watu wenye ulemavu.

  “Katika kila shule niliyopita nimekuta vyoo vizuri sana vimejengwa lakini vina kasoro ya kukosa hata tundu moja kwa maeneo yote ya wasichana na wavulana yaliyo andaliwa kwaajili ya watoto walemavu,”alisema Jafo

  Aliwaagiza wakurugenzi wote kuhakikisha hitaji hilo la msingi kwa watoto walemavu linazingatiwa kwa kufanya marekebisho kwa upande wa vyoo vya wavulana na wasichana ili kupata tundu moja kwa lengo la kuwasaidia watoto wenye ulemavu.

  Jafo mara baada ya kuhitimisha ziara yake mkoani Tanga anaelekea kuanza ziara nyingine katika mkoa wa Ruvuma, Mtwara, Lindi na Pwani.   Waatumishi wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo katika ziara yake aliyoifanya mkoani Tanga.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizungumza katika kikao cha watumishi wilaya ya Handeni.Pichai kati ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni.Mh.Godwin Gondwe. 

  0 0


  Friday 2nd Dec 2016 from 2100hrs till dawn
  Entrance Tshs 30,000/= |VIP Single Tshs 100,000/=  VIP Table for 6 People 500,000 Inclusive a bottle of Whisky and Mixers| plus Performance by  @Christianbella1, @BarnabaClassic @officialnandy and @cassotz Plus CEO @rosendauka as Elegant Night Ambassador.
  "Dress Code Classic" @hartmanntrader
  Limited Seats are available get your Ticket Now.. 

  0 0  0 0

   Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi akiwatunuku wahitimu wa kozi mbalimbali katika mahafali ya Chuo Kikuu cha Kampala (KIU) cha jijini Dar es Salaam kwenye sherehe za mahafali.
   Baadhi ya wahadhiri wa chuo hicho wakiwa kwenye mahafali hayo.
   Baadhi  ya wahitimu wa ngazi ya digrii  kozi ya afya wakila kiapo cha uadilifu baada ya kuhitimu fani hiyo.
   Sehemu ya wahitimu wakiwa katika mahafali hayo.  0 0

  Naibu Msajili wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni(BRELA)(Sheria za Biashara), Bw.Andrew Mkapa akiwasilisha mada kwenye semena elekezi juu ya ujasiriamali na urasimishaji biashara kwa vijana wa jijini Dar es Salaam. semina hiyo imeandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kwa lengo la kuwaelimisha vijana juu ya ujasiriamali ili waweze kuachana na dhana ya kuajiriwa na kufikiria kujiajiri zaidi kutokana na fursa zilizopo katika maeneo yao.
  Washiriki wa semina ya ujasiriamali wakifatilia kwa makini mada inayowasilishwa na Naibu Msajili wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni(BRELA)(Sheria za Biashara), Bw.Andrew Mkapa (hayupo pichani) juu ya umuhimu wa kurasimisha biashara zao ili waweze kupata fursa ya kufanya kazi na kutambulika na Serikali. Semina hiyo imeandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni yenye lengo la kuwaelimisha vijana juu ya ujasiriamali ili waweze kuachana na dhana ya kuajiriwa na kufikiria kujiajiri zaidi kutokana na fursa zilizopo katika maeneo yao.

  Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

  WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) umetoa wito  kwa vijana nchini kutumia fursa mbalimbali  za mafunzo ya ujasiriamali na biashara ili kujingea uwezo  wa kujiamini pale wanapoamua kujihusisha na biashara.

   Naibu Msajili  wa Wakala (Sheria za Biashara), Bw.Andrew Mkapa amesema mafunzo ya ujasiriamali na biashara ni nguzo muhimu kwa vijana hasa wanapokuwa na malengo ya kujiajiri kwani mafunzo hutoa mwongozo.  “Ni Muhimu  sana  nawashauri vijana  nchini kujitokeza kwenye mafunzo ya ujasiriamali na biashara muweze kujijengea uwezo na kujua umuhimu kurasimisha biashara zao ili  kutambulike na mamlaka husika,” Bw. Mkapa alitoa wito huo mwishoni mwa wiki  mara baada ya kutoa mada kwenye semina ya ujasiriamali kwa vijana iliyoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana wa kujiajiri.

   Bw. Mkapa alisema, Vijana waondokane na dhan ya kusubiri kuajiliwa pindi wanapomaliza shule  badala yake wajikite  zaidi kwenye kujiajiri wenyewe kwenye biashara na shughuli nyingine za kijamii.  “BRELA imeamua kujikita zaidi katika kutoa elimu ya mafunzo ya kurasimisha biashara kwa vijana ili  kuwahamasisha wapate ufahamu wa jinsi gani wanaweza kuanzisha makampuni na majina ya biashara ili waweze kutambulika kisheria,” alisisitiza.

   Bw. Mkapa ambaye pia alitoa mada iliyowasisimua zaidi vijana, alimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Kindoni, Bw.Hapi kwa jitihada za kuwakutanisha vijana pamoja na kutoa mafuzo ya ujasiriamali na biashara. “Kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu na Msajili wa  Makampuni, nachukua fursa kumpongeza mkuu wa wilaya, wawezeshaji na washiriki wote kwenye mafunzo haya,” alisema na kuongeza kuwa BRELA  ipo tayari muda wote kutoa elimu  jinsi ya ya kusajili makampuni, jinsi ya kusajili majina ya biashara na faida zake.

  Haya mafunzo yana maana na yatawasaidia sana vijana pindi watakapoanza kuunganishwa na fursa mbalimbali zinazotolewa kama vile ya mikopo kwani tayari watakuwa na uwelewa mkubwa wa kuzitumia fursa.  “sio tuu kwa vijana hawa waliohudhuria leo hapa lakini ni kwa watu wote kwa ujumla nchi nzima ni muhimu katika karne hii ya sasa kufanya biashara zilizo rasmi,” alisisitiza Mkapa

  Mshiriki wa mafunzo, Bw. Medson Moshi ni miongoni mwa vijana waliohudhuria semina hiyo na aliwataka na kuwahimiza vijana wengine kuchangamkia fursa kama hizo na kuachana na mtazamo wa kusubiri  kulipwa fedha ili kuweza kudhuria semina za mafunzo kama hiyo.  “mimi nitoe tu mwito kwa vijana wezangu siyo mpaka upewe fedha ndio uje kwenye mafunzo kama haya, ni vizuri kuangalia elimu kwanza na fedha itakuja baada ya miundombinu  kwanza” alisema, Bw. Moshi.

  Semina hiyo  ambayo iliandaliwa  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kwa lengo la kuwabadilisha kifikra na mtazamo  vijana  kuachana na dhana ya  kupenda kuajiriwa tu ni vizuri wakaanza  kufikiria kujiajiri zaidi kutokana na fursa zilizopo katika maeneo yao.

  0 0
  0 0

   Mtaalamu wa Usalama wa Mtandao nchini  Bw. Yusuph Kileo akipokea tuzo kama  Mtaalamu wa Usalama Mtandao wa Mwaka (Cybersecurity expert of the year) ikiwa ni katika kutambua mchango wake  katika mataifa ya Afrika. Mgeni rasmi kwenye hafla hiyo iliyofanyika jana jijini Nairobi alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya mipango na Majimbo (Ugatuzi)  wa  Kenya Mhe. Saitoti Torome. Jumla  tuzo 31 category tofauti zilitotela.
   Mtaalamu wa Usalama Mtandao  nchini  Bw. Yusuph Kileo akipokea tuzo kama  Mtaalamu wa Usalama Mtandao wa Mwaka (Cybersecurity expert of the year)  akishukuru baada ya kukabodhiwa tuzo hiyo.
    
   Mtaalamu wa Usalama Mtandao  nchini Bw. Yusuph Kileo baada ya kupokea  tuzo kama  Mtaalamu wa Usalama Mtandao wa Mwaka (Cybersecurity expert of the year).
  Globu ya Jamii inampongeza Mzalendo huyu ambaye amekuwa akihaha usiku na mchana kuhakikisha ujumbe wa umuhimu wa kuwekeza katika mapambano uhalifu mtandao na usalama mtandao katika kila nyanja.

  0 0


  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) na Mkurugenzi wa huduma za Hospitali Mohamed Dahoma na Viongozi wengine wakiwa katika chumba cha uchunguzi wa matatizo ya uti wa mgongo baada ya kuizindua rasmi Hospitali ya Abdalla Mzee iliyopo Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba leo ,[Picha na Ikulu.] 26/11/2016.

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) na katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt.Juma Malik Akil wakifuatana na Viongozi wengine wakati alipotembelea Hospitali ya Abdalla Mzee iliyopo Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba baada ya kuizindua rasmi leo (kulia) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe, Mwanajuma Majid hospitali hii imejengwa na Kampuni ya Kichina Jiang SU Ltd,

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono wananchi mara baada ya kutembelea sehemu mbali mbali za Hospitali ya Abdalla Mzee iliyopo Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba baada ya kuizindua rasmi leo (kulia) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe, Mwanajuma Majid hospitali hii imejengwa na Kampuni ya Kichina Jiang SU Ltd,
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake kwa wananchi wa Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba na Viongozi mbali mbali baada ya kuizindua Hospitali ya Abdalla Mzee leo ambayo imejengwa na Kampuni ya Kichina Jiang SU Ltd

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 26 Novemba, 2016 ametunuku Kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi 194 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)  kundi la 59/15 katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.

  Hii ni mara ya kwanza kwa Maafisa Wanafunzi wa JWTZ kutunukiwa Kamisheni nje ya Chuo Cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli kilichopo mkoani Arusha, na ni mara ya kwanza kwa Maafisa Wanafunzi wa JWTZ kutunukiwa Kamisheni ndani ya  Ikulu.


  Maafisa hao ambao 168 ni wanaume na 26 ni wanawake, wametunukiwa Kamisheni katika cheo cha Luteni Usu na sasa wamekuwa Maafisa Wapya wa JWTZ.


  Kabla ya kutunuku Kamisheni, Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli amekagua gwaride rasmi lililoandaliwa na Maafisa wanafunzi wa JWTZ na baadaye akashuhudia uhodari wa askari kutoka kikosi cha maadhimisho cha JWTZ waliofanya onesho la gwaride la kimyakimya.


  Akizungumza baada ya chakula cha mchana katika ukumbi wa Ikulu, Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli amempongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange, Makamanda na Askari wote wa JWTZ kwa jukumu kubwa wanalolitekeleza la kuhakikisha nchi ipo salama na amesema Serikali itahakikisha inaboresha zaidi maslai na mazingira ya kazi kwa Jeshi hilo na vyombo vingine vya ulinzi na usalama.


  Aidha, Rais Magufuli amesema ameamua tukio hili la kutunuku Kamisheni lifanyike Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kutoa heshima kwa Maafisa wa JWTZ kama ambavyo Viongozi wengine Serikalini wamekuwa wakipata heshima ya kuapishiwa Ikulu.


  "Kwamba Mawaziri tunapotaka kuwaapisha tunawaapishia hapa, Wakuu wa Mikoa tunawaapishia hapahapa, Makatibu Wakuu tunawaapishia hapahapa, kwa nini hawa Maafisa wa Jeshi tusiwaapishie hapahapa kwenye nyumba yao? Nyinyi ndio mnalinda nchi, nyinyi ndio mnasimamia usalama wa nchi hii, lakini nikiuliza hapa inawezekana wengine mpaka wamekuwa Mabrigedia Jenerali hawajawahi kukanyaga Ikulu, wakati hapa ni kwenu" amesema Rais Magufuli.


  Sherehe za kutunuku Kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi hao zimehudhuriwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi na Wakuu wa Jeshi la Ulinzi wastaafu na Majenerali wastaafu wa JWTZ.


  Gerson Msigwa

  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

  Dar es Salaam


  26 Novemba, 2016
    Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitunuku kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam  Novemba 26, 2016
   :Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akikagua gwaride la heshima linaloundwa na Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) kabla hajawatunuku kamisheni katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es  salaam  Novemba 26, 2016


   Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiweka saini kwenye hati  ya  kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) kabla hajawatunuku katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 2016
   Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiweka saini kwenye hati  ya  kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) kabla hajawatunuku katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 2016
   Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea baada ya kutunuku  kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 2016
   Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea baada ya kutunuku  kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 2016. PICHA NA IKULU


  0 0

  Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania imetangaza dhamira yake ya kuuza hisa kwa umma itakayofuatiwa na kujiunga kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) ikiwa ni utekelezaji wa sheria ya  Elektroniki na Mawasiliano ya Posta (EPOCA) na sheria ya Fedha ya mwaka 2016 ambayo inaelekeza makampuni ya simu  kumilikisha  asilimia 25 ya hisa zake kwa wananchi kwa kujiunga na Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).

  Akizungumzia  hatua hiyo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom, Bwana Ian Ferrao alisema “Tunayo furaha kutangaza kuwa tumeanza rasmi mchakato wa kuuza hisa kwa umma kwa mujibu wa matakwa ya sheria na  tumewasilisha maombi na utaratibu mzima utakaotumika kuuza hisa zetu na ratiba yetu nzima kuhusiana mchakato huu kwenye Mamlaka ya Usimamiaji wa  Masoko ya Mitaji  na Dhamana (CMSA) na Soko la Hisa  (DSE).   

  Hatua hii ni kubwa na inadhihirisha kuwa Vodacom ipo mstari wa mbele katika kutekeleza agizo la kuuza hisa zake kwa umma  na inadhihirisha jinsi ilivyojipanga  kuendelea kuboresha na kukuza sekta ya mawasiliano nchini Tanzania katika siku za usoni”.

  Uuzaji wa hisa kwa umma  na kujiunga na Soko la Hisa kunapitia  hatua mbalimbali za  kupata vibali kutoka taasisi za serikali zenye mamlaka ya kupitia maombi na kutoa  vibali vya utekelezaji wake.Ferrao aliendelea kueleza “Tunaamini uuzaji wa hisa zetu kwa umma utazidi kukuza shughuli za Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE),kunufaisha watanzania kiuchumi na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla.Kampuni yetu haitajulikana kwa jina la mwanzo la Vodacom Tanzania Limited bali imekuwa na jina la Vodacom Tanzania Public Limited Company (Plc) ikiwa ni hatua ya awali ya kujiandaa kuingia sokoni. 

  Tunawahakikishia kuwa mchakato wa kuingia kwenye hatua hii umeanza vizuri kwa mafanikio na tunaendelea kuwashirikisha wadau mbalimbali kutoka serikalini kuhakikisha tunatimiza dhamira ya kuanza  kuuza hisa kwa wananchi yenye dira ya kuleta manufaa kwa wote.”

  Ferrao alitoa msisitizo kuwa Vodacom inalo jukumu kubwa kuhakikisha hatua hii inaleta manufaa kwa pande zote zinatazohusika kuanzia  wanunuaji wa hisa, kuendelea kuwekeza , kuendelea kuleta mapinduzi ya ubunifu wa kiteknolojia na kuimarisha ubora wa huduma za kampuni kwa wateja wake “Tutaendelea kutoa mchango mkubwa wa ufanikishaji wa sera ya nchi ya miaka 5 ya kukuza sekta ya mawasiliano.Tutaendelea pia kuwaletea taarifa mbalimbali kuhusiana na mchakato wa kuuza hisa kwa umma unavyoendelea”Alisema Ferrao.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao,(watatu kushoto) akimkabidhi hati ya maombi ya kuijiunga na soko la hisa la Dar es Salaam,(DSE) Mkurugenzi wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji na Dhamana(CMSA) Nicodemus Mkama wapili (kushoto) wakati wa hafla fupi iliyofanyike mwishoni mwa wiki katika ofisi za CMSA jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni Meneja Uhusiano wa CMSA, Charles Shirima , wanaoshuhudia kutoka Kulia ni Mkurugenzi wa Ushauri wa kutoka huduma za Orbit Securities Company Ltd. Gerase Kamugisha, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (wapili kulia) na Mkuu wa fedha wa kampuni ya Orbit Securities Company Ltd, Godfrey Gabriel (watatu kutoka kulia).
  Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao,(kulia) akimkabidi hati ya maombi ya kujiunga na soko la hisa la Dar es Salaam,(DSE) Mkurugenzi wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji na Dhamana (CMSA) Nicodemus Mkama(wapili kushoto) wakati wa hafla fupi iliyofanyike mwishoni mwa wiki katika ofisi za CMSA jijini Dar es Saalaam,Kushoto ni Meneja Uhusiano wa CMSA, Charles Shirima.
  Mkurugenzi wa Ushauri wa kutoka huduma za Orbit Securities Company Ltd. Gerase Kamugisha(kushoto)Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao, Mkurugenzi Mtendaji wa DSE,Moremi Marwa, Mkuu wa masuala ya kifedha wa Orbit Securities Company Ltd, Godfrey Gabriel, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia,wakionyesha hati za maombi ya kuijiunga na soko la hisa la Dar es Salaam,(DSE) mwishoni mwa wiki.

  0 0

  Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania Bw, Deus Kibamba akitoa elimu kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba pamoja na historia ya mchakato huo kwa vijana wa  wilaya zote za jiji la Dar Es Salaam.
  Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Bw. Hebron Mwakagenda akitoa mafunzo kuhusu katiba ya zamani pamoja na katiba mpya kwa vijana kutoka wilaya zote za jiji la Dar es Salaam leo. (Picha na Geofrey Adroph)
  Baadhi ya Vijana wa wilaya ya mbalimbali za jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye mafunzo kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba yaliyofanyika leo ambao wameazimia kuendelea kwa mchakato wa kupatikana kwa katiba mpya.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akisalimiana na baadhi ya walimu wa shule ya sekondari ya Songea Boys wakati wa ziara yake shuleni hapo ili kuona hali halisi ya wanafunzi wenye mahitaji maalum Novemba 26, 2016 Mkoani Ruvuma.
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akizungumza jambo na baadhi ya Watendaji wa Serikali katika Ofisi ya Shule ya Sekondari ya Songea Boys alipotembelea kwa lengo la kuangalia vituo na shule zinazohudumia watu wenye ulemavua Wilayani Songea mkoa wa Ruvuma.
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akizungumza na baadhi ya wanafunzi ya shule ya Sekondari ya Songea Boys wakati wa ziara yake shuleni hapo Novemba 26, 2016.


  0 0  Dkt. Ringo Tenga wa Chuo Kikuu Dar es salaam akishiriki kutoa maoni kuhusu marekebisho ya Sera mpya ya Ardhi ya Mwaka 2016 Ukumbi wa VETA Mkoani Morogoro.

  “Pamoja na kuwaalika wawekezaji Tulinde maeneo ambayo ni Vyanzo vya chakula” hayo ni baadhi ya Maoni ya Dr Ringo Tenga kutoka Chuo kikuu cha Dar es salaam, aliyo wasilisha wakati wa zoezi la kukusanya maoni ya wadau kuhusu Sera Mpya ya ardhi ya mwaka 2016 katika ukumbi wa VETA Mkoani Morogoro.

  Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi Dkt Yamungu Kayandabila Akiwahakikishia wadau kwamba Maoni yao yatafanyiwa kazi.Dkt kayandabila ameyasema hayo wakati wa zoezi la kukusanya maoni kutoka kwa Wadau Ukumbi wa VETA Mkoani Morogoro.

  0 0


   Rais Mstaafu wa Cuba Mhe. Fidel Castro enzi za uhai wake
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Magufuli, amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Jamhuri ya Cuba Mhe. Raul Castro kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa Cuba Mhe. Fidel Castro kilichotokea tarehe 25 Novemba, 2016.

  Katika Salamu hizo Rais Magufuli amesema;


  "Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Cuba Mhe. Fidel Castro. Kwa niaba ya Serikali, Wananchi wa Tanzania na kwa niaba yangu mwenyewe natoa pole nyingi kwako, familia, Serikali ya Cuba na wananchi wa Cuba kwa kumpoteza mtu muhimu.


  Fidel Castro alikuwa kiongozi shupavu wa karne, atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika na pia kwa misaada mikubwa aliyoitoa katika kuboresha huduma za kijamii kwa wananchi.


  Alikuwa rafiki wa Tanzania na Afrika nzima, historia ya Tanzania na Afrika haziwezi kukamilika bila kumtaja Fidel Castro, hakika kifo chake sio tu ni pigo kwa Cuba bali pia kwa Tanzania na Afrika.

  Naungana nawe na wananchi wa Cuba katika kipindi hiki kigumu cha majonzi, na pia nakuombea kwa Mwenyezi Mungu wewe, familia na wananchi wote wa Cuba muwe na nguvu, subira na ustahimilivu kutokana na kuondokewa na mpendwa wenu."


  Pia Rais Magufuli amemuombea marehemu Fidel Castro apumzishwe mahali pema peponi, Amina.


  Gerson Msigwa

  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

  Dar es Salaam


  26 Novemba, 2016


  0 0

     Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameendelea na ziara yake ya siku ya  leo ni zamu ya wilaya ya Kinondoni.

  Akizungumza na watumishi wa Manispaa ya Kinondoni RC Makonda ametoa agizo kwa Wakuu wote wa wilaya wa Mkoa wa Dar es Salaam kusimamia agizo lake la kupiga marufuku wenyeviti wote wa Mtaa kutembea na mihuri kwani wamekuwa wanaitumia kinyume na utaratibu kwa kudhulumu haki za wanyonge ikiwemo kuuza viwanja kinyume na utaratibu, huku akisisitiza kuwa watendaji wa mtaa ndiyo inabidi wakae na mihuri hiyo.

  Pia RC Makonda amewataka wakuu wa wilaya wote kuanzisha kitengo maalum cha kisheria kitakacho tumika kutoa elimu kuhusu migogoro ya ardhi na kuwashauri wananchi kabla ya kuipeleka mahakamani na kuwaweka wazi kama kuna dalili ya kushinda au vinginevyo na kuwapa suluhisho la kudumu.

  Katika hatua nyingine RC Makonda amemtaka DC Hapi na Meya wa Kinondoni Bernard Sita kufuatilia suala la vibali vya ujenzi na kuhakikisha vinatoka kwa wakati ili kuharakisha maendeleo.

  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni DC Hapi amehaidi kuwashughukia watendaji wote watakao bainika kutowajibika kikamilifu ili kuchochea maendeleo.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati) akizungumza na watumishi wa Manispaa ya Kinondoni ambapo  ametoa agizo kwa Wakuu wote wa wilaya wa Mkoa wa Dar es Salaam kusimamia agizo lake la kupiga marufuku wenyeviti wote wa Mtaa kutembea na mihuri kwani wanaitumia kinyume na utaratibu, leo jijini Dar es Salaam kushoto ni Mkuu  wa wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi na (kulia) ni Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro
  .Mkuu  wa wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi akizungumza machache na watumishi wa Manispaa ya Kinondoni leo jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akipokea ripoti ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda  akiwasili kwenye ukumbi wa Police Officer’s Mess akiambatana na Mkuu  wa wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi leo jijini Dar es Salaam.
  Watumishi wa Manispaa ya Kinondoni wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda leo jijini Dar es Salaam.

older | 1 | .... | 1441 | 1442 | (Page 1443) | 1444 | 1445 | .... | 3272 | newer