Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1439 | 1440 | (Page 1441) | 1442 | 1443 | .... | 3278 | newer

  0 0

  Leo ukiwa unatimiza miaka 10 tangu ututoke machoni mwetu, tunanaendelea kusema tunakupenda zaidi tukikumbuka na kuitafakari historia ya maisha yako ambayo kwa hakika Mungu alituzawadia kwa upendo. Bwana alitoa na kutwaa tena jina lake libarikiwe! 

  Kutakuwa na Misa ya Kumuombea Marehemu Mama yetu mpendwa, Siku ya Jumapili Novemba 27, katika Kanisa la St Martha, Mikocheni B Jijini Dar es salaam, Kuanzia Saa tatu asubuhi. Karibuni sana tumuombee Mama yetu.

  0 0
 • 11/25/16--01:36: Article 9


 • 0 0

   Mbunifu wa Shirika la kuhudumia Viwanda vidogo Sido, Zacharia Maziku, akiwaonyesha baadhi ya vijana wajasiliamali jinsi ya kuandaa na kutengeneza Jora la Kitambaa wakati Vijana hao walipotembelea kujionea kazi na uzalishaji wa Shirika hilo jana Nov 24, 2016, wakiwa katika zaiara ya mafuzo yaliyoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la The Foundation for Civil Cociety kwa kushirikiana na Tanzania Women Chambers of Commerce (TWCC). Mafunzo hayo yanamalizika rasmi hii leo kwenye Hoteli ya Blue Pearl Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.  Picha na Mafoto Blog
   Mbunifu wa Shirika la kuhudumia Viwanda vidogo Sido, Zacharia Maziku, akiwaonyesha baadhi ya vijana wajasiliamali jinsi ya kuandaa na kutengeneza Jora la Kitambaa wakati Vijana hao walipotembelea kujionea kazi na uzalishaji wa Shirika hilo jana Nov 24, 2016, wakiwa katika zaiara ya mafuzo yaliyoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la The Foundation for Civil Cociety kwa kushirikiana na Tanzania Women Chambers of Commerce (TWCC). Mafunzo hayo yanamalizika rasmi hii leo kwenye Hoteli ya Blue Pearl Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. 
   Vujana wakimsikiliza Mkurugenzi wa Kampuni ya EFA Production Solutions Ombeni Selestine, wakati wakilitembelea Ofisi yake jana.
   Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya EFA Production wakijaza Lotion katika makopo kwa kutumia mikono tayari kwa kupaki katika maboksi na kuuzwa.
   Baadhi ya vijana wakiangalia jinsi Jora linavyotengenezwa.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Na Beatrice Lyimo-MAELEZO.

  SERIKALI imedhamiria kuimarisha mtandao wa usafirishaji na usambazaji umeme nchini ili kufikia malengo ya taifa ya asilimia 75 ya watanzania wanaonufaika na huduma ya umeme ifikapo 2025.

  Katika kutimiza azma hiyo, hivi karibuni Serikali kupitia Shirika la ugavi la umeme Tanzania (TANESCO) imezindua mradi wa uboreshaji wa huduma za umeme jijini Dar es salaamu uliobuniwa kwa lengo la kuboresha Miundombunu ya Usafirishaji na usambazaji umeme katika jiji la Dar es salaam.

  Mradi huo umetokana na ongezeko la wahitaji wa huduma ya umeme katika Jiji la Dar es Salaam ambapo mradi huo utasaidia katika kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika na hivyo ku0vutia wawekezaji wapya katyika sekta za viwanda.

  Akizindua Mradi huo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema kuwa Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) imekuwa katika jitihada mbalimbali za kuboresha miundombinu yake ili iweze kuwafikia wananchi wengi na katika ubora unaohitajika.

  “Mradi huu wa kuboresha miundombinu ya umeme unalenga kuimarisha upatikanaji wa huduma ya umeme wa uhakika katika jiji la Dar es Salaam” anasema Majaliwa.Anasema mradi huo utafungua fursa nyingi za uzalishaji na kupelekea upatikanaji wa fursa za ajira za uhakika kwa wananchi.


  0 0

  Mfuko wa Pensheni wa LAPF wakabidhi vifaa vya umwagiliaji maji kwa kikundi cha watu wenye Ulemavu cha Buigiri, Dodoma. Pichani ni Afisa Masoko Mwandamizi wa LAPF Rehema Mkamba akikabidhi baadhi ya vifaa hivyo kwa viongozi wa kikundi hicho. Vifaa hivyo vitawasaidia kuendesha shughuli za kilimo cha mboga mboga cha umwagiliaji ili kujipatia kipato.

  0 0


  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  MAKAMU Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Clement Sanga amemtambulisha rasmi kocha mkuu wa timu hiyo Mzambia George Lwandamina, aliyechukua nafasi ya Mholanzi  Hans Van De Pluijm aliyevikwa viatu vya Mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo.

  Lwandamina anachukua mikoba ya Mholanzi Hans Van De Pluijm aliyebadilishiwa majukumu na kuwa mkurugenzi wa ufundi ili kumsaidia Mzambia huyo katika masuala mbali mbali ya maendeleo ya klabu hiyo, na moja kwa moja Mzambia huyo huku mzambia huyo akafunguka juu ya kikosi atakachoingia nacho vitani.

  Sanga ameweka wazi kuwa ujio wa kocha huyo sasa ni rasmi na wamempa kandarasi ya miaka miwili,lengo kubwa ikiwa ni kuongeza nguvu kwenye kikosi cha wanajangwani hao katika kutetea Ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom na michuano ya kimataifa. 

  "Uongozi wa Yanga leo hii unayo furaha kuwatambulisha kocha mkuu George Lwandamina na Mkurugenzi wa ufundi Hans Van De Pluijm, tunaamini kwa pamoja wataweza kuipa mafanikio zaidi timu yetu kutoka hapa ilipo na kusonga mbele zaidi" amesema Sanga.

  Baada ya utambulisho huo, Kocha mkuu Lwandamina akafunguka na kusema kuwa ni changamoto mpya kwake kwani anajua Yanga ni klabu kubwa na amepewa nafasi hiyo na kwa kushirikiana na benchi la ufundi kwa ujumla na wachezaji kwa pamoja atahakikisha anatumia kila kinachowezekana kuhakikisha Yanga inafanya vizuri kuanzia kwenye ligi ya nyumbani hadi klabu Bingwa Afrika. 

  Akaeleza kuwa kuna habari zinazoenea kuwa anakuja na wachezaji wapya kutoka Zesco, akasisitiza zaidi kuwa "Nasikia tetesi kuhusu wachezaji wapya kutoka Zesco kusajiliwa Yanga mimi kama kocha mkuu sijui chochote labda michakato hiyo inafanyika bila mimi kushirikishwa kikosi kilichopo ndicho nitaendelea nacho". 

  Mkurugenzi wa ufundi wa klabu hiyo Pluijm akawa na yake ya kusema na kueleza kuwa hana shida na kubadilishiwa majukumu na zaidi ataendelea kushirikiana na benchi la ufundi kwa ujumla katika kuhakikisha wanaendelea kutetea ubingwa wao na kufanya vizuri kwenye kombe la Klabu Bingwa Afrika.
  Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Clement Sanga akimkabidhi jezi ya timu hiyo Kocha Mkuu George Lwandamina leo Jijini Dar es salaam.
  Kocha Mkuu George Lwandamina akisalimiana Mkurugenzi wa benchi la Ufundi Hans Van De Pluijm ambaye awali alikuwa ndiye kocha Mkuu.
  Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Clement Sanga akizungumza na waandishi wa habari wakati wa utambulisho wa kocha mkuu  Mzambia George Lwandamina (kulia) pamoja na nafasi ya Mholanzi Hans Van De Pluijm aliyechukua nafasi ya mkurugenzi wa ufundi. 


  0 0

  Na Bakari Madjeshi,Globu ya Jamii

  Baada ya kuanza safari zake Octoba 14 2016,Shirika la Ndege la ATCL limekili kuwepo kwa changamoto mbalimbali zikiwemo ucheleweshaji wa ndege na kutoa huduma katika maeneo ambayo yalipaswa kuhudumiwa.

  Akitoa changamoto hizo,Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo,Mhandisi Emmanuel Korosso amekili kuwepo kwa changamoto ya Marubani katika Shirika hilo ikizingatiwa mpaka sasa Shirika hilo linatarajiwa kumaliza mafunzo ya Marubani 13 katikati ya mwezi Desemba.

  Amesema kuhusu Wafanyakazi Bodi yake imeagiza Menejimenti ya Shirika kusimamisha kwa muda mkataba wa hiari ambao unatoa mwanya kwa wafanyakazi kutumia vibaya ruhusa za matumizi ya tiketi za bure.

  "Katokana na haja ya kuboresha Utendaji, ATCL iliamuliwa Wakurugenzi wote katika Menejimenti ya ATCL isipokuwa Mkurugenzi Mtendaji,na baadhi ya Menejimenti waondolewe katika nafasi zao Mara moja kutokana na Utendaji dhaifu na viwango vya Elimu visivyokidhi matakwa ya nafasi zao",amesema Mhandisi Korosso

  "Tumeamua wakurugenzi wanaokaimu nafasi zao warudishwe katika nafasi zao za chini ambazo siyo za Menejimenti au wahamishiwe katika vituo vya mikoani",ameeleza Mhandisi Korosso.Aidha,Wakurugenzi na Menejimenti waliokuwa wamethibitishwa tumeagiza waondolewe ATCL ili wapangiwe majukumu mengine kulingana na sifa zao.

  Aidha Bodi imemuagiza Mtendaji Mkuu kutangaza mara moja nafasi zote za Wakurugenzi na pia nafasi za Mameneja zilizo wazi kwa kufuata muundo wa muda uliopitishwa na Bodi (Interim Organization Structure).Pia Mtendaji Mkuu ameagizwa kutangaza nafasi zozote ambazo anaona kuna umuhimu wa kuajiri watu wengine kutokana na utendaji usioridhisha wa wafanyakazi wanaoshikiria nafasi hizo kwa sasa.
  Mwenyekiti wa Bodi ya ATCL,Mhandisi Emmanuel Korosso(katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari leo katika Ofisi za Shirika hilo,Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika,Ladislaus Matindi,kulia ni Mjumbe wa Bodi,Dkt. Mussa Mgwata.

  0 0


  Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii

  Serikali imejipanga kufanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa na jukwaa la usafirishaji nchini ,ili kuboresha hali ya usafiri hapa nchini kutoka bandarini kutoka nchini jirani.

  Hayo yamesemwa na Katibu mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na uchukuzi,Profesa Faustine Kamuzora alipokuwa akifungua jukwaa hilo lililoasisiwa na tasisi ya Trade Mark East Afrika.

  "Hivyo serikali imejipanga na kuakikisha kuwa bandari ya Dar es Salaam inakuwa sehemu rafiki kwa wafanyabiashara kutoka nchi zinazotunguka kwa kupunguza urasimu unaochangia kuchelewa kwa kutoa mzigo bandarini"amesema Prof Kamuzora.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa hilo la usafirishaji ,Angelina Ngalula , amesema kuwa serikali inatakiwa kuanza kuandaa mazingira ya upatikanaji wa mzigo wa tani milioni 10 katika reli ya Standard Geji inayo taraji kujengwa hapa nchini .

  Amesema kuwa wazo la serikali la kujenga reli ya kisasa ni zuri hivyo tunaiomba serikali inahakikisha inaandaa mazingira ya upatikanaji wa mizigo hili tusije tukaiona reli hiyo kama pambo tu.
    Mkurugenzi mkazi wa Trademark East Afrika,John Ulanga akizungumza na wadau wa usafirishaji wakati uzinduzi wa jukwaa lamusafirishaji.
   Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF ,Godfrey Simbeye  akito maelezo jinsi tasisi yake inavyofanya kazi bega kwa bega na wawekezaji ususani katika swala la usafirishaji.
   Mwenyekiti wa Jukwaa la Usafirishaji ,Angelina Ngalula akizungumza na wadau wa usafirishaji wakati uzinduzi wa jukwaaa hilo.
   Katibu mkuu wa wizara ya Uchukuzi,Prof Faustine Kamuzora akitoa hotuba ya ufunguzi wa jukwaa la usafirishaji jijini Dar es Salaam
  Wadau wa usafirishaji wakisikiliza kwa makini wakati wa uzinduzi wa jukwaa hilo.
   Picha ya pamoja ya wadau wa usafirishaji na mgeni rasmi.

  0 0

  Serikali imewataka maafisa elimu kupanga muda wa kusikiliza kero za walimu na kuzitafutia ufumbuzi ili kuongeza morali ya walimu kufundisha. Agizo hilo lilitolewa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe.Seleman Said Jafo alipokuwa akiongea na walimu wa shule ya sekondari Segera iliyopo wilayani Handeni, wakati wa ziara ya kiserikali Wilayani Handeni na Mkoa wa Tanga. 

  Mhe.Jafo alisema kuwa wapo baadhi ya Maafisa elimu ambao wanajifanya kuwa ni Miungu watu linapokuja suala la kusikiliza na kutatua kero za walimu. Waziri Jafo alisema “Wapo walimu wanaotembea umbali mrefu kufuata huduma makao makuu ya Halmashauri kwa wakubwa wao mara nyingi wameshindwa kutatuliwa kero zao hali inayopelekea usumbufu, Kuanzia leo 24/11/2016 napiga marufuku tabia hiyo”. 
   
  Aliongeza msisitizo kuwa Maafisa elimu wapo kwa lengo la kuwasikiliza walimu na kuwasaidia kutatua kero zao ili waweze kujikita katika ufundishaji wa wanafunzi. Alisema kuwa walimu ni watu muhimu sana nchini ila wamekuwa wakikatishwa tamaa na utendaji wa baadhi ya maafisa elimu. Aliongeza kuwa kero kubwa ya walimu ni kutokupanda madaraja kwa wakati na kutopata stahiki zao ikiwa ni pamoja na posho za likizo,uhamisho na madai mengine.

  Wakati huohuo, Naibu Waziri aliiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kukamilisha miradi yote ya SEDP-II ambayo haijakamilika kuhakikisha inakamilika kabla au ifikapo tarehe 20/12/2016. Alisema kuwa katika kusimamia miradi hiyo na miradi ya maendeleo kwa ujumla kila mtu lazima atimize wajibu wake na kuhakikisha fedha iliyotengwa na kutolewa inatumika vizuri na thamani yake kuonekana kwa muda mrefu (value for money).

  Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Said Jafo akisaini kitabu cha wageni shule ya sekondari Segera, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. Wiliam Makufwe na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe.
  Picha ya pamoja ya Mhe. Selemani Said Jafo na waalimu wa shule ya sekondari ya Segera. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni akitoa utambulisho mfupi kwenye ukumbi wa Halmashauri. 
  Baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.
  Viongozi wakisikiliza kwa makini maagizo ya Naibu Waziri ikiwa ni pamoja na kuwa na usimamizi bora wa rasilimali fedha.  0 0

  Hayo yamesemwa jana na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi wakati akihojiwa na kipindi maalumu cha TUNATEKELEZA kinachorushwa hewani na kituo cha Televisheni ya Taifa (TBC1).


  Meja Jenerali Milanzi anasema Serikali imeweka mfumo maalumkatika kulinda hifadhi zilizopo na ili kuweza kukabiliana na ujangili unaojitokeza katika hifadhi mbalimbali nchini.

  “Sekta ya Utalii nchini inachangia pato la taifa kwa takribani asilimia 17.5 na kutoa ajira kwa zaidi ya watumishi milioni 3 katika sekta mbali mbali ya utalii nchini, hivyo ni vyema tukaweka mikakati madhubuti katika kulinda vyanzo vilivyopo” alisema Meja Milanzi.

  Aidha, alisema kuwa Serikali itaendelea kuwachukulia hatua kali za kisheria watu wote watakaobainika kujihusisha na ujangili pamoja na biashara ya magogo ili kulinda hifadhi za Taifa na kuweza kuvutia watalii nchini.Aidha Meja Jenerali Milanzi aliitaka jamii kwa ujumla kuona umuhimu wa kutumia nishati mbadala ili kulinda misitu iliyopo kwa kutunza mazingira na hifadhi za taifa.

  Mbali na hayo Meja Jenerali Milanzi alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazovutia watalii wengi kutoka Marekani na Uingereza hivyo kuwataka wananchi kuzingatia sheria na kanuni zinazosimamimia Hifadhi za Taifa ili kuzudi kuvutia watalii nchini.

  0 0


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema serikali itaendelea kuviimarisha vyuo vya ufundi stadi nchini –VETA- ili viweze kutoa wahitimu bora ambao watakidhi katika soko la ajira hasa kwenye viwanda vilivyopo na vitajengwa nchini.
  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo leo wakati anazungumza na uongozi wa kiwanda cha A to Z kilichopo mkoani Arusha katika ziara yake ambayo imeingia siku ya Pili ya kutembelea viwanda mbalimbali mkoani humo ili kujua changamoto zinazokabili viwanda hivyo na serikali kuzitafutia ufumbuzi.
  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali imetenga fedha za kutosha zitakazotumika kuviimarisha vyuo vya Veta ili viweze kutoa mafunzo bora yatakayosidia vijana kufanya kazi zao kwa ufanisi wa hali ya juu pindi watakapoajiriwa au kujiajiri wenyewe.
  Kuhusu maslahi kwa wafanyakazi wa Kiwanda cha A to Z,Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameutaka uongozi wa kiwanda hicho kulinda na kutetea haki za wafanyakazi kwa kutoa maslahi mazuri ambayo yatawezesha wafanyakazi hao kufanya kazi kwa bidii.
  Makamu wa Rais pia amesisitiza usawa katika ulipaji wa mishahara kwa wafanyakazi wa ndani na wa nje ya nchi walioajiriwa kwenye kiwanda hicho ili kuondoa tofauti za mishahara hali ambayo ijenga motisha kwa wafanyakazi.Kiwanda cha A to Z kilichopo eneo la Kisongo mkoani Arusha ambacho kinatengeneza vyandarua, nguo na mifuko mbalimbali ikiwemo ya saruji kimeajiri zaidi ya wafanyakazi 7500 ambapo asilimia 80 ya wafanyakazi wote ni wanawake.
  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewahimiza wawekezaji kote nchi walipe kodi za serikali mapema kodi ambazo zitatumika kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
  Amewahakikishia wawekezaji kuwa Tanzania itaendelea kujenga na kuimarisha mazingira bora kwa wawekezaji ili kuhakikisha wawekezaji wanafanyakazi zao vizuri kwa ajili ya manufaa ya taifa na ya wawekezaji. 

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akiangalia nguo zinazotengenezwa na Kiwanda cha A to Z. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa kiwanda hicho Bw. Kalpesh Shah, na kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo. Makamu wa Rais amefanya  ziara kwenye kiwanda hicho ikiwa sehemu ya kutambua mchango wa wawekezaji wa ndani na changamoto wanazokutana nazo ili kupata majibu ya kurahisisha kufanikisha Tanzania mpya ya Viwanda. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akitembezwa  
  Mkurugenzi wa kiwanda hicho Bw. Kalpesh Shahkatika,

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mkurugenzi wa kiwanda hicho Bw. Kalpesh Shah akipata maelezo ya namna kiwanda cha A to Z kinavyofanya utafiti wa kupambana na wadudu wanaoharibu mahindi kutoka kwa Mkurugenzi wa kituo cha utafiti cha Africa Technical Research Centre Dkt.Johson Ouma Odera. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo.

  0 0


  Na Dotto Mwaibale

  SHILINGI milioni 10 zinazodaiwa kutolewa na Halmshauri ya Manisaa ya Temeke kwa ajili ya ujenzi wa choo katika  Soko la Madenge hazijulikani zilipo hivyo kuzua tafrani kwa wananchi.

  Wananchi hao wamelalamikia kukosa choo katika soko hilo kwa zaidi ya miaka mitano licha ya kutengwa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya ujenzi wa choo hicho.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mtandao wa www.habari za jamii.com wananchi hao walisema wanalazimika kutumia choo cha kulipia baada ya choo cha soko hilo kilichoanza kujengwa kushindwa kumalizika.

  Mmoja wa wafanyabiashara wa soko hilo ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe alisema Manispaa ya Temeke ilitenga  fedha hizo kwa ajili ya ujenzi wa choo hicho lakini kwa muda wa miaka mitano ujenzi wake haujakamilika.Hali hiyo inaleta adha kwa wafanyabiashara kwa kuendelea kulipia huduma za choo kilichopo sokoni hapo kinyume cha matarajio yao.

  " Hii ni hujuma au matumizi mabaya ya fedha  kwa nini ujenzi wa choo umeishia njiani licha ya fedha kutolewa na Manispaa na kibaya zaidi baadhi  ya miundombinu kama milango imeng'olewa hivyo kubaki kama gofu" alihoji.

  Akitoa ufafanuzi wa malalamiko hayo Ofisa Masoko wa Wilaya ya Temeke, Johnson Makalanga alikiri kuwepo kwa jambo hilo na kuwa limetokana na mkandarasi aliyepewa tenda ya ujenzi wa choo hicho kukomea njiani kwa kuwa fedha zake hakumaliziwa."Ninachofahamu mimi Changamoto kubwa iliyosababisha kutokamilika kwa ujenzi huo ni mkandarasi kucheleweshewa fedha zake kwani anadai sh.milioni 4" alisema Makalanga.

  Makalanga aliongeza kuwa ujenzi wa vyoo hivyo ilikuwa ni kwa baadhi ya masoko ya wilaya hiyo ambapo yeye alisimamia kujenga choo kilichopo kwa Urasa Kigamboni ambacho kinatoa huduma na kuingiza mapato yanayotokana na wananchi kuchangia fedha baada ya kupata huduma za choo hicho.

  Makalanga alisema hawezi kulizungumzia suala hilo kwa mapana kwa vile ni hayupo kwa muda mrefu katika kata hiyo badala yake aliomba atafutwe ofisa Mtendaji au Diwani wa Kata ya Temeke kwa ufafanuzi zaidi.

  Jitihada za gazeti hili kumpata mtendaji wa kata hiyo ziligonga mwamba baada ya kufika ofisini kwake jana na kuambiwa alikuwa kwenye kikao na watendaji wake.
   Choo cha Soko la Madenge katika Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam kikiwa kimeng'olewa milango kutokana na kutokamilika ujenzi wake licha ya manispaa hiyo kutenga sh.milioni 10 za ujenzi. 
   Mkazi wa Temeke akipita mbele ya choo hicho.

  Mwonekano wa moja ya tundu la choo hicho ambacho hakina miundombinu ya mifereji.

  0 0  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa sherehe fupi za ufunguzi wa jengo la ofisi za Umoja wa Mataifa litakalotumika kutunza kumbukumbu mbalimbali za Mahakama ya Umoja wa Mataifa Kuhusu Mauaji ya Rwanda (MICT) katika eneo la Laki Laki nje kidogo ya mji wa Arusha.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la ufunguzi wa jengo la ofisi za Umoja wa Mataifa litakalotumika kutunza kumbukumbu mbalimbali za Mahakama ya Umoja wa Mataifa Kuhusu Mauaji ya Rwanda (MICT) katika eneo la Laki Laki nje kidogo ya mji wa Arusha.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Mahakama hiyo wakati ufunguzi wa jengo la ofisi za Umoja wa Mataifa litakalotumika kutunza kumbukumbu mbalimbali za Mahakama ya Umoja wa Mataifa Kuhusu Mauaji ya Rwanda (MICT) katika eneo la Laki Laki nje kidogo ya mji wa Arusha, kutoka kushoto ni John Hocking (Msajili MICT ), Theodor Meron (Rais wa MICT ) , Miguel de Serpa Suares (Msaidizi wa katibu mkuu wa Umoja wa Taifa katika masuala ya kisheria ) ,kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga, Mkuu wa mkoa wa Arusha mhe. Mrisho Gambo,Serge Brammertz (Mwendesha Mashitaka wa MICT ) na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman (kulia)

  .......................................................................

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan amezindua majengo ya ofisi za Umoja wa Mataifa zitakazotumika kutunza kumbukumbu mbalimbali za Mahakama ya Umoja wa Mataifa Kuhusu Mauaji ya Rwanda (MICT) katika eneo la Laki Laki nje kidogo ya mji wa Arusha.

  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amezindua majengo hayo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta John Pombe Magufuli na kusisitiza kuwa Tanzania itaendelea kudumisha mahusiano

  Majengo hayo yamejengwa katika eneo la Laki laki mkoani Arusha baada ya Serikali ya Tanzania kuipatia Umoja wa Mataifa eneo lenye ukubwa wa ekari 16.17 bure kwa ajili ya kujenga hayo ya kihistoria hapa nchini.

  Tanzania inaomba nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kusaidia kupatikana kwa wote waliohusika na mauaji hayo ya kimbari ili kuhakikisha haki inapatikana kwa wahanga wa mauaji hayo.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Fadhili Nkurlu amezindua kifaa cha kubaini moto ukiwa katika hatua ya moshi (smoke detector) wilayani humo. Tukio hili limefanyika katika shule ya sekondari Dakama ambapo Mhe. Nkurlu amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri zote tatu  za wilaya ya Kahama kuhakikisha kwamba kifaa hicho kinafungwa kwenye shule na mabweni yote ili kutekeleza agizo la serikali la kupambana na moto mashuleni.
  Wanafunzi wa shule ya sekondari Dakama wakijifunza namna ya kutumia  kifaa cha kubaini moto ukiwa katika hatua ya moshi (smoke detector)
   Wanafunzi wa shule ya sekondari Dakama wakioneshwa  namna ya   kifaa cha kubaini moto ukiwa katika hatua ya moshi (smoke detector) kinavyofanya kazi
    Wanafunzi wa shule ya sekondari Dakama wakiwasha moto kukijaribu  kifaa cha kubaini moto ukiwa katika hatua ya moshi (smoke detector)
   Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Fadhili Nkurlu akiwa na Wanafunzi wa shule ya sekondari Dakama wakati wa kujifunza namna ya kutumia kifaa cha kubaini moto ukiwa katika hatua ya moshi (smoke detector)
   Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Fadhili Nkurlu akielekeza wanafunzi wa shule ya sekondari Dakama wakati wa kujifunza namna ya kutumia kifaa cha kubaini moto ukiwa katika hatua ya moshi (smoke detector)

  0 0


  SIMU.TV: Tanzania imeungana na jamii ya kimataifa kuadhimisha siku kumi na sita za kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na kuahidi kufanyia marekebisho ya sheria ya ndoa ili kuondokana na ndoa za utotoni. https://youtu.be/DzBTeSQ8eP0

  SIMU.TV: Wenyeviti wa mitaa pamoja na watendaji wa jiji la Dar es Salaam wameendelea kujikuta matatani baada ya kubainika kuuza viwanja kinyume na sheria. https://youtu.be/Fq-pg8LgL6w

  SIMU.TV: Bodi ya wakurugenzi wa shirika la ndege ATCL imewaondoa baadhi ya wakurugenzi baada ya kugundulika kuwa na kiwango dhaifu vya elimu. https://youtu.be/0G_igIwZ8VE

  SIMU.TV: Mgogoro wa mwekezaji wa kampuni ya Tanzanite one na wakazi wa kata ya Naisinyai wilayani Simanjiro umemalizika baada ya mwekezaji huyo kutimiza madai ya wananchi. https://youtu.be/2CzUTW7vUOc

  SIMU.TV: Wakala wa majengo nchini TBA umekabidhi majengo mawili yaliyopo Ocean Road kwa ofisi ya mpango wa kurasimisha biashara za wanyonge Tanzania MKURABITA baada ya kuwa na uhaba wa ofisi za kutosha kwa muda mrefu. https://youtu.be/7jCFL-9NX7Y

  SIMU.TV: Watanzania wametakiwa kuchangamkia fursa za kibiashara katika masoko ya nchi za kiarabu ili kuweza  kujikwamua kiuchumi. https://youtu.be/H4q3A4_eY1g

  SIMU.TV: Makamu wa pili wa rais wa serikali ya mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ali Idd ameitaka serikali kutafsiri vitabu vinavyoelezea utalii kwa lugha mbalimbali ili kupata wageni kutoka nchi mbalimbali. https://youtu.be/npXn22n0XXQ

  SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ametoa rai kwa wawekezaji kuwekeza eneo la Kogamboni ambako kuna viwanja vingi kwa ajili ya uwekezaji. https://youtu.be/6vLz5YWnQX8

  SIMU.TV: Ligi ya vijana nchini imeendelea leo wakati timu ya vijana ya Azam Fc imetoshana nguvu na Timu ya vijana ya African Lyon. https://youtu.be/2ptC8rBY0xI

  SIMU.TV: Klabu ya Soka ya Yanga leo imemtambulisha rasmi kocha mpya George Lwandamina ambapo ameahidi kushirikiana bega kwa began a uongozi wa timu hiyo ili kupata matokeo mazuri. https://youtu.be/BKJdOkBdYqY

  0 0


  0 0

  Taarifa zilizoripotiwa na Kituo cha Televisheni ya Taifa ya nchi ya Cuba,  na kutangazwa moja kwa moja na Rais wa nchi hiyo, Raul Castro, zinaeleza kuwa Raiswa zamani wa nchi hiyo, Fidel Castro aliyekuwa na umri wa Miaka 90 na ambaye aliiongoza Cuba kwa zaidi ya miaka 30 kabla ya kuachia kijiti kwa mdogo wake Raul Castro (Rais wa sasa) mwaka 2008 amefariki Dunia ikiwa ni siku moja tu kuwaaga wajumbe wa Chama Cha Kikomunisti Cuba na kuwaambia atafariki siku si nyingi lakini mapinduzi yataishi, ikiwa ni baada ya kuugua kwa muda mrefu.

  Fidel Castro ambaye aliwahi kuiongoza nchi ya Cuba kama Waziri Mkuu kwa kipindi cha miaka 18 (kuanzia mwaka 1959 hadi mwaka 1976) kabla ya kushika nafasi ya Urais aliyodumu nayo kuanzia mwaka 1976 hadi mwaka 2008.

  Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

  0 0

  Uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kanda ya kaskazini ulitanguliwa na maandamano yaliyopita katika barabara mbalimbali za mji wa Moshi na kuhitimishwa katika viwanja vya kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadiki akizungumza wakati wa uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ,uzinduzi iliofanyika katika viwanja wa vya kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi.Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi katika Shule ya Polisi Theresia Nyangasa  akisoma taarifa juu ya vitendo vya kuutali na njia zilizoanza kuchukuliwa katika kukabiliana navyo wakati wa uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili kanda ya Kaskazini .
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadiki pamoja na Mkuu wa wilaya ya Moshi Kippi Warioba wakifuatilia taarifa juu ya ukatili wa kijinsia iliyokuwa ikitolewa na viongozi wa Asasi mbalimbali .


  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (mwenye kofia nyekundu), ambaye pia alikua ni mgeni rasmi katika Mahafali ya 42 ya chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) akiwa na Mkuu Wa Chuo hicho Profesa Taadeo Andrew Satta, (mwenye kofia nyeusi) wakiwa wako tayari kwaajili ya kuanza msafara wa kuelekea katika viwanja vya Karemjee jijini Dar es Salaam kwaajili ya ufunguzi wa mahafali hayo ya achuo hicho.
  Mgeni rasmi katika katika Mahafali ya 42 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) nchini, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akizungumza na wahitimu wa ngazi mbalimbali wa chuo hicho (hawako pichani) katika viwanja vya Karemjee jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii.
  Mgeni rasmi katika Mahafali ya 42 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) nchini, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimpongeza Rehema Sibuga mhitimu mmoja kati ya wahitimu wengine waliofanya vizuri zaidi katika miaka yote masomo yao chuoni hapo.


older | 1 | .... | 1439 | 1440 | (Page 1441) | 1442 | 1443 | .... | 3278 | newer