Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110089 articles
Browse latest View live

ANGALIA HAPA MOJA KWA MOJA TUKIO LA RAIS DKT. MAGUFULI KUTUNUKU KAMISHELI KWA MAAFISA WA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli atawanuku Kamisheli Maafisa Wanafunzi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, leo katika Viwanja vya Ikulu Jijini Dar es salaam.

Kamisheni hii inatolewa kwa mara ya kwanza ndani ya Ikulu, na pia nje ya Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli Mkoani Arusha tangu kihamishwe kutoka Dar es Salaam kwenda Arusha mwaka 1976.
Nyote mnakaribishwa.

BOFYA LINK HIYO HAPO CHINI KUONA TUKIO HILO MOJA KWA MOJA

WAMILIKI WA LESENI ZA UCHIMBAJI MDOGO WA MADINI MKOANI SINGIDA WATOZWA FAINI YA SHILINGI MILIONI 20 KWA UHARIBIFU WA MAZINGIRA

$
0
0
Na Evelyn Mkokoi-Singida

Wamilki wa Leseni za uchimaji mdogo wa madini wa Joshua Mine na Sekeknke one mine wa Sekenke Mkoani Singida, wametozwa faini ya shilingi milioni 10 kila moja kwa kosa la uchafuzi wa mazingira wa kutumia vibaya madini ya zebaki, hivyo kuhatarisha maisha ya viumbe hai.

Baraza la taifa la Hifadhi na usimamizi wa Mazingira limeitoza faini hiyo kupitia mratibuwa wa Barazakanda a Ziwa Bw. Jamali Baruti na kiwataka wamiliki hao kulipa faini hiyo ndani ya siku 14.

Adhabu hiyo inatokana na makelele katika eneo la uchimbaji, kusambaa kwa vumbi lisilovumilika, kukosekana kwa vyoo pia na matumizi mabaya ya miti katika uchimbaji wao ambao huenda sambamba na uharifu wa misitu.

Aidha Baraza limewataka wachimbaji hao kuwa na vyeti vya tathmini ya athari ya mazingira pamoja na leseni ya uchimbaji.
Kwa Upande wake Mkuu wa Wiaya ya Mkalama Injinia Joakim Masakala  akimuwaklisha mkuu wawiaya ya Iramba, alisema kuwa ni vizuri wakazi wa maeneo hayo wanavyojibidisha katika kazi lakini ni muhimu sana kuzingatia afya kwani uchimbaji wa kutumia madini aina ya zebaki bila vifaa salama kazini unaweza kuleta maradhi hususan ya saratani kwani madini hayo upenya kirahisi katika mwili wa binadamu.

Awali Katika Kikao na uongozi wa Mkoa pamoja na wadau wa Mazingira Naibu Waziri Mpina alitolea ufafanuzi masuala mbalimbali ya Mazingira ikiwemo matumizi ya Mifuko ya plastic na kuwashauri wakazi wa singida kutunza mazingira akitolea mfano wa ziwa Kitangiri lililoo Hatarini kutoweka kabisa.
Mratibu wa Baraza la Taifa na Usimamizi wa Mazingira NEMC kanda ya ziwa,Jamal Baruti (katikati) akitoa adhabu kwa wamiliki wa leseni za uchimbaji mdogo wa madini wa kampuni ya Jushua Mine na Sekenke one Mine wa Sekenke, mkoani Singida, kwa kosa la uharibifu wa mazingira kwa kutumia vibaya madini aina ya zebaki katika uchimbaji wao, pembeni yake ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akimsikiliza Bwana Baruti.
Naibu Waziri ofisi ya Makamu wa Rais Mungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akinyooshea kidole sehemu inayoonekana kuwa na maji katika ziwa Kitangiri Wilayani Iramba wakati kwa hali halisi ziwa hilo limepotea kabisa, hii ni kutokana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Sehemu ya viongozi wa Mkoa wa Singida Pamoja na wadau , Wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina hayupo Pichani katika kikao cha pamoja cha kupokea ripoti ya Mazingira ya Mkoa na kutolea ufafanunuzi baadhi ya masuala ya swala zima la usimamizi wa mazingira nchini. (Picha na Evelyn Mkokoi OMR)

SERIKALI KUENDELEA KUVIFUTIA USAJILI VYUO AMBAVYO HAVINA SIFA NCHINI

$
0
0
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Profesa Shadrack Mwakalila (kushoto), Naibu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala, Dk. Magreth Shawa na Naibu Ktibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dk. Leonard Akwilapo (kulia), wakiteta jambo kabla ya maandamano ya kuelekea eneo maalumu lililotengwa kwa ajili ya mahafali ya 11 ya chuo hicho yaliyofanyika Dar es Salaam jana.

Taswira meza kuu. Kutoka kulia ni Naibu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala, Dk. Magreth Shawa, Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, Mkurugenzi wa Elimu ya Ufunzi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhandisi Thomas Katebalirwe, Naibu Ktibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dk. Leonard Akwilapo, Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Profesa Shadrack Mwakalila, Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma, Dk. Thomas Ndaluka na Katibu Tawala Wilaya ya Kigamboni, Rahel Mhando.
Naibu Ktibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dk. Leonard Akwilapo (kulia), akitoa cheti kwa mmoja wa wahitimu.

Wazazi, walezi na ndugu jamaa wa wahitimu hao pamoja na wafanyakazi wa chuo hicho wakijumuika kwenye ahafali hayo.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Rais wa Zanzibar Dkt. Shein azindua Hospitali ya Abdalla Mzee Pemba

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Balozi wa China Nchini Tanzania Mhe. Lu Youqing wakikata utepe kuizindua Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba leo,iliyojengwa na Kampuni ya Kichina Jiang SU Ltd.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Balozi wa China Nchini Tanzania Mhe,Lu Youqing (kushoto) na Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd wakati  akitembelea sehemu mbali mbali za Jengo la Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba baada ya kuizindua rasmi leo. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiangalia mashine za kuchunguzia maradhi mbalimbali wakati alipotembelea Chumba cha Maabara katika Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba baada ya kuizindua rasmi leo akiwa na Balozi wa China Nchini Tanzania Mhe,Lu Youqing (katikati) na Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipaa maelezo kutoka kwa Dk.Mariuma Abdalla Salum (kushoto)alipotembelea katika wodi ya wazazi baada ua kuizindua leo,ambayo imejengwa na Kampuni ya Kichina Jiang SU Ltd,(katikati) balozi wa China Nchini Tanzania Lu Younqing.
Wananchi waliohudhuria katika uzinduzi wa Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba iliyozinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo,ambayo imejengwa na Kampuni ya Kichina Jiang SU Ltd. Picha na Ikulu, Zanzibar. 

WAMILIKI WA LESENI ZA UCHIMBAJI MDOGO WA MADINI MKOANI SINGIDA WAMETOZWA FAINI YA SHILINGI MILIONI 20 KWA UHARIBIFU WA MAZINGIRA

$
0
0

Na Evelyn Mkokoi-Singida

Wamilki wa Leseni za uchimaji mdogo wa madini wa Joshua Mine na Sekeknke one mine wa Sekenke Mkoani Singida, wametozwa faini ya shilingi milioni 10 kila moja kwa kosa la uchafuzi wa mazingira wa kutumia vibaya madini ya zebaki, hivyo kuhatarisha maisha ya viumbe hai.

Baraza la taifa la Hifadhi na usimamizi wa Mazingira limeitoza faini hiyo kupitia mratibuwa wa Barazakanda a Ziwa Bw. Jamali Baruti na kiwataka wamiliki hao kulipa faini hiyo ndani ya siku 14.

Adhabu hiyo inatokana na makelele katika eneo la uchimbaji, kusambaa kwa vumbi lisilovumilika, kukosekana kwa vyoo pia na matumizi mabaya ya miti katika uchimbaji wao ambao huenda sambamba na uharifu wa misitu.Aidha Baraza limewataka wachimbaji hao kuwa na vyeti vya tathmini ya athari ya mazingira pamoja na leseni ya uchimbaji.

Kwa Upande wake Mkuu wa Wiaya ya Mkalama Injinia Joakim Masakala akimuwaklisha mkuu wawiaya ya Iramba, alisema kuwa ni vizuri wakazi wa maeneo hayo wanavyojibidisha katika kazi lakini ni muhimu sana kuzingatia afya kwani uchimbaji wa kutumia madini aina ya zebaki bila vifaa salama kazini unaweza kuleta maradhi hususan ya saratani kwani madini hayo upenya kirahisi katika mwili wa binadamu.

Awali Katika Kikao na uongozi wa Mkoa pamoja na wadau wa Mazingira Naibu Waziri Mpina alitolea ufafanuzi masuala mbalimbali ya Mazingira ikiwemo matumizi ya Mifuko ya plastic na kuwashauri wakazi wa singida kutunza mazingira akitolea mfano wa ziwa Kitangiri lililoo Hatarini kutoweka kabisa. 

Katikati Bwana Jamal Baruti Mratibu wa Baraza la Taifa na Usimamizi wa Mazingira NEMC kanda ya ziwa, akitoa adhabu kwa wamiliki wa leseni za uchimbaji mdogo wa madini wa kampuni ya Jushua Mine na Sekenke one Mine wa Sekenke, mkoani Singida, kwa kosa la uharibifu wa mazingira kwa kutumia vibaya madini aina ya zebaki katika uchimbaji wao, pembeni yake ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akimsikiliza Bwana Baruti.
Naibu Waziri ofisi ya Makamu wa Rais Mungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akinyooshea kidole sehemu inayoonekana kuwa na maji katika ziwa Kitangiri Wilayani Iramba wakati kwa hali halisi ziwa hilo limepotea kabisa, hii ni kutokana na athari za mabadiliko ya tabia nchi. 
Sehemu ya viongozi wa Mkoa wa Singida Pamoja na wadau , Wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina hayupo Pichani katika kikao cha pamoja cha kupokea ripoti ya Mazingira ya Mkoa na kutolea ufafanunuzi baadhi ya masuala ya swala zima la usimamizi wa mazingira nchini. (Picha na Evelyn Mkokoi OMR) 

DC TUNDURU JUMA HOMELA AELEZA MAFANIKIO YA MPANGO WA KUTOKOMEZA MIMBA MASHULENI KATIKA WILAYA YAKE SEHEMU YA KWANZA.

$
0
0
MKUU wa wilaya ya Tunduru JUMA HOMELA akizungumza na mwandishi wa RUVUMA TV on line ambaye hayupo pichani mafanikio ya kupambana na utoro mashuleni pamoja na kutokomeza mimba mashuleni. Kwa undani wa habari hii bonyeza hiyo video.

KIWANDA CHA SARUJI SIMBA CEMENT YAIPIGA JEKI SHULE YA MSINGI YA KANGE , TANGA

$
0
0
Tanga, KIWANDA Cha Saruji Cha Simba Cement kimeijengea shule ya Msingi ya Kange vyumba viwili vya madara na madawati 50 pamoja na matundu mawili vya vyoo vyote vikiwa na thamani zaidi ya shilingi milioni 76.
Msaada huo umekuja kupunguza kero ya wanafunzi kurundikana darasa moja na wengine kukaa chini jambo ambalo hupunguza ufahamu wa wanafunzi darasani.
 
Akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano, Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwailapwa, alisema msaada huo uwe mfano kwa makampuni mengine na wadau wa elimu lengo likiwa ni kuondokana na changamoto ya  baadhi ya shule inazokabiliana nazo.
 
Kwa upande wake, Mkuu wa Rasilimali watu kiwanda cha Saruji cha Simba Cment, Anna Malambugi, alisema kiwanda hicho moja ya sera zake ni kusaidia  jamii ikiwemo, Elimu, Afya na Mazingira.
 
Nae Mwalimu mkuu wa Shule hiyo, Debora Danniel, alisema awali walikuwa wakiwaweka wanafunzi 120 darasa moja kufuatia uhaba wa madarasa.
Alisema kwa msaada huo utaondosha kero ya wanafunzi kurundikana darasa moja na kuwaomba wadau wa elimu kuisaidia shule hiyo katika Nyanja mbalimbali ikiwemo miundombinu yamaji na uchakavu wa majengo.
 Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias  Mwailapwa akifungua moja milango ya vyumba viwili ya madarasa shule ya msingi Kange Tanga, anaemtazama ni Afisa Fedha Pitter De Jagger na kulia ni Mkurugenzi wa jiji la Tanga, Daudi Mayeji.
 Afisa Uhusiano kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga, Noor Mtanga, akiwakabidhi madawati 50 wanafunzi wa shule ya msingi ya Kange pamoja na majengo mawili na vyoo vyenye matundu mawili vyote vikiwa na thamani zaidi ya shilingi milioni 76, nyuma kulia ni Mwenyekiti wa mtaa wa Kasera, Aidan Munis na kulia ni mwalimu mkuu wa shule hiyo, Debora Mzava.

Mkuu Rasiliwamali watu kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga,  Anna Mwalambuji akiwakabidhi madawati 50 wanafunzi wa shule ya msingi ya Kange kufuatia uhaba wa madawati shule hiyo pompja na kuwakabidhi jengo la vyumba viwili na vyoo vyenye matundu mawili vyote vikiwa na thamani zaidi ya shilingi milioni 76.

SINGIDA YATEKELEZA AGIZO LA RAIS LA USAFI WA MAZINGIRA KIKAMILIFU

$
0
0
Na Evelyn Mkokoi – Singida.

Katika kutekeleza agizo la Serikali la usafi wa mazingira kila Jumamosi ya Mwisho wa Mwezi, wananchi wa Mkoa wa Singida wamejitokeza kwa kwingi katika zoezi hilo lililofanyika kitaifa mwezi huu mkoani humo.

Akishiriki zoezi hilo  Mkoani Singida kitaifa, Naibu waziri Ofisi ya Makamu w Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Singida na wana  singida kwa ujumla kwa jitihada walizoonyesha kwani kila eneo la Singida Jumamosi ya leo Limeonekana kuwa nadhifu kabla hata ya muda wa kuanza kufanya usafi tofauti na mikoa mingine ambayo amewahi kushiriki zoeZi hilo.

Akiongea na Hadhara iliyojitokeza katika siku ya usafi Mjini Singida Leo, Mpina alisema kuwa usafi wa mazingira  unapunguza magonjwa yatokanayo na uchafu akitolea mfano ugonjwa wa kipindu pindu na hivyo taifa likiwa safi litaweza kuokoa ngumukazi yake, na kupunguza gharama ambazo zingetumika kutibu maradhi hayo.

“Ukiona Msichana mzuri barabarani ujue kagharamiwa ukiona kijana mtanashati vilevile ujue kagharamiwa Mkiona taifa zuri na safi ujue limegharamiwa na wananchi wake wamejipanga vizuri, hivyo wana singida Muendelee kujitahidi katika suala zima la usafiwa mazingira.” Alisisitiza Mpina.

Zoezi la usafi wa Mazingira Mkoani Singida lilienda sambamba na zoezi la upandaji miti ambapo, Naibu Waziri Mpina Pia alishiriki  na wananchi katika zoezi la kupanda miti mkoani Singida ambapo alipanda mti aina ya mpararachichi katika eneo la stand mpya ya Misuna.
 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina Pamoja na wananchi wa Mji wa Singida wakikusanya uchafu katika siku ya Usafi Kitaifa Mjini Singida.

 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muugano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akipeleka uchafu katika kizimba cha uchafu cha soko  kuu la Singida lililoko katika Mtaa wa Ipembe.

 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akiandaa mche wa mti kitalam kabla ya kuupanda katika zoezi la usafi na upandaji miti mjini Singida leo.



Naibu Wazir Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina Akipanda Mti aina ya Mparachichi katika eneo la Misuna Stand Mpya Mjini Singida leo katika Zezi la usafi wa mazingira Kitaifa. (Picha na Evelyn Mkokoi wa OMR)


Mkurugenzi wa Mifumo Ofisi ya Rais (TAMISEMI) ATAKA MALENGO 17 YA SDGs KUFIKISHWA NGAZI ZA CHINI ZA UTEKELEZAJI

$
0
0
Mkurugenzi wa Mifumo Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Henry Katabwa ametaka Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) kuhusishwa kwenye michakato ya maendeleo ya serikali za mitaa, hasa kwenye programu zinazotekelezwa kwenye ngazi za chini kabisa ambapo ndiko wananchi wenye hali duni kimaendeleo wanapatikana. 
 
Kauli hiyo aliitoa wakati akifunga warsha ya malengo ya maendeleo endelevu kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na Mipango kutoka mikoa saba ya kanda ya ziwa. Alisema malengo 17 ya maendeleo endelevu (SDGs) yamehusishwa kwenye mpango wa maendeleo wa miaka mitano hivyo ni vyema kuhakikisha hata katika ngazi za chini utekelezaji wa program unazingatia malengo hayo.
 
 “Kuna haja ya kuhakikisha kwamba, shabaha ya malengo haya inahusishwa kwenye michakato ya maendeleo ya serikali za mitaa na hasa kwenye miradi ya program zinazotekelezwa kwenye ngazi za chini kabisa, ambako ndiko wananchi wenye hali duni ya kimaendeleo wanapatikana” alisema .
Mwenyekiti wa warsha ya siku tatu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na Mipango nchini ambaye pia ni Katibu Tawala Msaidizi idara ya Mipango na Uratibu mkoa wa Mara, Eldom Anyosisye akitoa neno la ukaribisho wakati wa kufunga warsha ya siku tatu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na Mipango nchini iliyomalizika mwishoni wa juma mjini Dodoma chini ya ufadhili wa Shirika UNDP.

Pia alisema serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na mradi wa uimarishaji wa wa sekta ya umma inaendelea kuboresha mfumo wa ukusanyaji takwimu ili uweze kukusanya takwimu katika ngazi zote za serikali za mitaa ili zitumike kuandaa mipango ya maendeleo. 
 
Akisoma maazimio kwa niaba ya washiriki wa warsha hiyo, Afisa Mipango wa wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera, Innocent Maduhu alisema sheria ya Bajeti ya mwaka 2015 izingatiwe na kila mhusika atekeleze wajibu na majukumu yake. Pia yafanyike mapitio ya mgawanyo na matumizi ya fedha za mapato ya ndani kwa lengo la kupata uhalisia sambamba na kuweka mkazo katika kutafuta rasilimali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya Maendeleo.
Mkurugenzi wa Kupunguza Umaskini na Kuinua Uchumi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Anna Mwasha akizungumza jambo kabla ya mgeni rasmi kufunga warsha hiyo iliyomalizika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.

Aidha wajumbe hao waliazimia kila sekta iwezeshwe vitendea kazi na rasilimali muhimu ili ziweze kutimiza majukumu yake pia mifumo ya upangaji mipango na utoaji taarifa ihuishwe ili iendane na Malengo ya Maendeleo Endelevu. Pia wametaka yafanyike mafunzo rejea ya mifumo kwa watumishi na kwa wakati na rasilimali katika sekta ya Kilimo ziongezwe kwa lengo la kuongeza na kuboresha uzalishaji na kupata malighafi kwa ajili ya viwanda. 
 
Sambamba na halmashauri zote kuboresha mifumo ya ukusanyaji mapato na kubuni vyanzo vipya pamoja na kudhibiti mapato na matumizi, uwepo mpango au mkakati maalumu wa kuendeleza Mikoa na Halmashauri zilizopo nyuma kimaendeleo. “Mbinu za uibuaji na upangaji wa miradi ya maendeleo kutoka ngazi ya chini ufanyike upya katika halmashauri zote” alisema Maduhu.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Mifumo Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Henry Katabwa akitoa hotuba ya kufunga warsha ya siku tatu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na Mipango nchini iliyomalizika mwishoni wa juma mjini Dodoma chini ya ufadhili wa Shirika UNDP.

RC MAKONDA AWATAKA WATENDAJI WOTE WA KATA KUWA NA TAARIFA ZOTE ZA MIRADI YA MAENDELEO

$
0
0
Ikiwa ni muendelezo wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ambapo leo ni siku ya nane tangu aanze ziara hiyo, akiwa katika ziara yake ndani ya Wilaya ya Ubungo Kata ya Msigani mtaa wa Temboni RC Makonda ametoa agizo kwa Watendaji Kata wote katika Mkoa wake.

RC Makonda amewataka watendaji wote wa Kata kuwa na taarifa zote za miradi ya maendeleo vinginevyo atawachukulia hatua stahiki.
"Sitaki Kumkuta Mtendaji yeyote wa Kata ambaye hajui jambo lolote kwenye kata yake" Alisema RC Makonda. 

Ambapo amemtolea mfano mzuri Mkuu wa Wilaya hiyo Humphrey Polepole kwa kuwa na taarifa mbalimbali kuhusu miradi ya maendeo na kuwaomba waige kutoka kwake.

Pia RC Makonda amemuagiza RPC Mkoa wa kipolisi Kinondoni Suzan Kaganda kwa kushirikiana na TAKUKURU kumshikilia na kumfanyia uchunguzi aliyekuwa Mtendaji wa Kata hiyo Neema Kalumbe ambaye kwa sasa ni Mtendaji wa Kata ya Makongo kujibu tuhuma za ubadhirifu wa fedha za mradi wa Barabara ya kutokea Msuguri na Msingwa ambao ulitengewa milioni 17 na hakuna barabara iliyojengwa. 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza na wananchi wa Kata ya Msigani mtaa wa Temboni juu ya watendaji wote wa Kata kuwa na taarifa zote za miradi ya maendeleo vinginevyo atawachukulia hatua stahiki leo jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akimsikila Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Humphrey Polepole  alipokuwa akitolea ufafanuzi kuhusu mradi wa maji huo
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikangua mradi wa maji ambao ulikuwa ukiratibiwa na kamati ya maji ya Mtaa ambapo ulionesha mapungufu na kwasasa mradi huo unasimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka DAWASCO
Mkazi wa Mtaa wa Temboni, Moroen Goube akifafanua jambo katika ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.
Wananchi wa Mtaa wa Temboni wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo jijini Dar es Salaam.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI KAIRUKI AKABIDHI VYETI KWA WAHITIMU WA MAFUNZO YA UCHUNGUZI

$
0
0
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Angella Kairuki akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya uchunguzi Afisa Uchunguzi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa umma Edson Kamugisha. Hafla hiyo ilifanyika katika Chuo cha maafisa wa Jeshi la Polisi Kidatu, Mkoani Morogoro jana.

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Angella Kairuki akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya uchunguzi Katibu Msaidizi  wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa umma Evodia Pangani. Hafla hiyo ilifanyika katika Chuo cha maafisa wa Jeshi la Polisi Kidatu, Mkoani Morogoro jana. 

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Angella Kairuki akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya uchunguzi Katibu Msaidizi  Kanda ya Mashariki wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa umma Eritrudi Cyliacus Ishengoma. Hafla hiyo ilifanyika katika Chuo cha maafisa wa Jeshi la Polisi Kidatu, Mkoani Morogoro jana.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Angella Kairuki akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya uchunguzi Katibu Msaidizi  Kanda ya Mashariki wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa umma Eritrudi Cyliacus Ishengoma. Hafla hiyo ilifanyika katika Chuo cha maafisa wa Jeshi la Polisi Kidatu, Mkoani Morogoro jana. 

Voda Stars yainyuka Jipange Venture FC 1-0 Gymkhana Club

$
0
0
Wachezaji wa timu ya soka ya Vodacom Tanzania, Voda Stars, Mbisso Ephram (kushoto), Gabby Magori na Astrid Mapunda (kulia),wakimbana mchezaji wa timu ya  Jipange Venture,Rajabu Juma ( wa pili kulia) kwenye mechi ya kirafiki katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam leo Novemba 26, 2016. Voda Stars ilishinda 1-0.
 Mshambuliaji wa Jipange Venture, Rajabu Juma ( kulia) akijaribu kuiwatoka wachezaji wa timu ya soka ya Vodacoma Tanzania, Voda Stars, Mbisso Ephram (kushoto) na Gabby Magori kwenye mechi ya kirafiki katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam leo Novemba 26, 2016. Voda Stars ilishinda 1-0.
 Mchezaji wa timu ya soka ya Vodacom Tanzania, Voda Stars,  Gabby Magori (kushoto)  akichuana na Shaaban  Abdi wa  timu ya  Jipange Venture, kwenye mechi ya kirafiki katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam leo Novemba 26, 2016. Voda Stars ilishinda 1-0. 
 Mfungaji wa goli pekee la timu ya soka ya Vodacom Tanzania, Voda Stars, Astrid  Mapunda akishangilia bao lake wakati timu yake ilipocheza na timu  Jipange Venture, kwenye mechi ya kirafiki katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam leo Novemba 26, 2016. Voda Stars ilishinda 1-0.
Wakiwa katika picha ya pamoja ni kikosi cha timu ya soka ya Vodacom Tanzania, Voda Stars iliyocheza kwenye mechi za kirafiki katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam leo Novemba 26, 2016.

MKAPA AMPONGEZA JK KWA UJENZI WA CHUO CHA UDOM.

$
0
0
RAIS mstaafu katika serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, amempongeza Rais wa Awamu iliyopita, Jakaya Kikwete, kwa kuthubutu na kuwezesha ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom). 

Akizungumza katika mahafali ya saba ya chuo hicho, alisema Maono ya chuo hicho yalianza na serikali zote tatu ikiwamo aliyoiongoza lakini hakuweza kuthubutu.

“Nampongeza mzee Kikwete kwa kuweza kuthubutu na kufanikisha ujenzi wake na leo tupo hapa.Mradi wa ujenzi wa chuo hichi, uliafikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) tangu utawala wa Rais wa Awamu ya Kwanza, Hayati Julius Nyerere, Ali Hassan Mwinyi (awamu ya pili) na kisha mimi lakini wote hatukuweza kuthubutu,”alisema Mkapa.

Kadhalika, Rais Mkapa alishauri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ikutane na kufanya mazungumzo na Vyuo Vikuu vinavyomilikiwa na Serikali ili kuchambua matatizo yanayotokea mara kwa mara. Alisema ni vyema uwepo mkutano wa wenyeviti wa vyuo hivyo ili kufahamu gharama wanzotumia kwa ajili ya uendeshaji wake.

Hata hivyo alibainisha idadi ya wanachuo kila kukicha inaongezeka na nakusababisha vyuo hivyo kushindwa kujiendesha, hivyo jambo bora ni kukutana kwa wenyeviti hao na kujadiliana kuhusu gharama za uendeshaji wake. Hata hivyo alisema kutoa amri na maagizo kwa wanachuo kila wakati, si suluhisho la kumaliza migogoro vyuoni, lakini pale wenyeviti wa Vyuo Vikuu vyote wakikutana pamoja na kufahamu gharama zao za uendeshaji, kuna uwezekano wa kutatua kero zote.

Naye makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof, Idris Kikula, alisema wahitimu hao wanakabiliwa na changamoto ya upatikanaji ajira ambayo kwa sasa imekuwa tishio duniani huku akiwashauri kujiajiri na kuacha kutegemea ajira serikalini kutokana na tatizo hilo kuwa la kidunia.

 
 Mkuu wa Chuo UDOM ambaye ni Rais Mstaafu Benjamin Mkapa akitunuku Shahada ya Uzamivu(PHD)Ombeni Msuya katika mahafali ya saba ya chuo hicho.
 Mkuu wa Chuo UDOM ambaye ni Rais Mstaafu Benjamin Mkapa akitunuku Shahada mbalimbali katika mahafali ya saba ya chuo hicho.
 Wahitimu wa Mahafali ya saba ya Chuo cha Udom.
Wahitimu wa Shahada ya Uzamili katika Chuo cha Udom wakiwa katika nyuso za furaha baada ya kuhitimu.

MASAUNI AZINDUA KAMPENI YA ABIRIA PAZA SAUTI KITUO KUU CHA MABASI, UBUNGO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni amewaasa abiria kutoa taarifa pale wanapoona dereva anahatarisha maisha yao katika vyombo vya usafiri.

Masauni ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Paza Sauti iliyoratibiwa na Mabalozi wa Usalama Babarani RSA Tanzania katika Kituo cha mabasi ya Mikoani na Nchi Jirani cha ubungo jijini Dar es Salaam, amesema kila mtu anawajibu wa kutoa taarifa dhidi ya dereva anayehatarisha maisha katika vyombo vya usafiri.

Amesema dereva kutojua sheria za usalama barabarani isiwe kigezo cha kuvunja sheria zilizowekwa kutokana na waathirika wa ajali ni watanzania ambao ndio nguvu kazi ya taifa.

Amesema kampeni hiyo iweze kuleta matokeo chanya ambayo yataonyesha kupungua kwa ajali au kutokuwepo kwa ajali na kufanya watanzania kuwa salama katika vyombo vya usafiri.

Nae Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishina wa Jeshi la Polisi (DCP), Mohamed Mpinga amesema kampeni iliyozinduliwa ni jitihada za kikosi cha usalama barabarani katika kupambana na ajali pamoja na kuongeza askari kila sehemu ambayo dereva wamekuwa wakikiuka sheria za usalama barabarani.

Amesema abiria wanatakiwa kuwa chachu ya kutoa taarifa za uvunjifu wa sheria za usalama barabarani kwa madereva ili waweze kuchukulia hatua.

Mjumbe Usalama barabarani Mkoa Dar es Salaam, Idd Azzan amesema kampeni hiyo ni italeta mageuzi katika kupunguza ajali.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto) akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua Kampeni ya Abiria Paza Sauti ndani ya basi la Machame Express katika Kituo Kikuu cha Mabasi, Ubungo jijini Dar es Salaam leo. Kampeni hiyo iliandaliwa na Mabalozi wa RSA kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali nchini. Kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na abiria mara baada ya kuzindua Kampeni ya Abiria Paza Sauti katika Kituo Kikuu cha Mabasi, Ubungo jijini Dar es Salaam. Masauni aliwataka abiria nchini kutoa taarifa kwa haraka pindi wanapoona dereva anavunja sheria na pia kila abiria ni wajibu wake kujua haki zake. Kushoto ni Mlezi wa RSA Taifa ambaye pia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia) akimsikiliza Katibu wa Mabalozi wa Usalama Barabarani (RSA) Taifa, Asina Omary alipokuwa anatoa historia ya RSA pamoja na majukumu yake kabla ya Naibu Waziri huyo kuzindua Kampeni ya Abiria Paza Sauti katika Kituo Kikuu cha Mabasi, Ubungo jijini Dar es Salaam leo. Kampeni hiyo iliratibiwa na Mabalozi wa RSA kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali nchini.

AKINAMAMA ZANZIBAR WAFANYIWA UCHUNGUZI WA SARATANI YA MATITI BILA MALIPO

$
0
0
Zaidi ya wanawake 500 wamefanyiwa uchunguzi wa saratani ya matiti iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Jumuiya ya watu wanaoishi na maradhi hayo (ZCA), Ilala Afya Centre ya Dar es salaam na Wizara ya Afya Zanzibar.

Kampeni hiyo ya siku moja iliyofanyika Hospitali kuu ya Mnazimmoja iliwashirikisha akinamama wenye umri kuanzia miaka 25 ilikuwa na lengo la kuweza kuwagundua mapema akinamama wenye tatizo la maradhi hayo ambayo dalili zake zinachelewa kujitokeza.

Daktari bingwa wa uchunguzi wa maradhi ya saratani Zanzibar ambae pia ni Mwenyekiti wa ZCA Dkt. Msafiri Marijani amesema kampeni hiyo ilihusisha uchunguzi wa Utrasound na uchunguzi wa sindano na waliopatikana na dalili watafanyiwa vipimo ili kujua kama ni saratani ama matatizo mengine.

Dkt. Marijani amekumbusha kuwa saratani hadi hivi sasa haina tiba na kitu muhimu ni kuigundua mapema ili kuidhibiti kabla haijaleta athari kubwa hivyo amewashauri wananchi kupima afya zao mara kwa mara.

“Saratani ni maradhi yanayouwa watu wengi duniani kutokana na kuchelewa kugundulika mapema, kitu muhimu ni wananchi kujenga utamaduni wa kuchunguza afya zao,” alisisiti Dkt. Marijani.Amesema Hosipitali zote za Wiala na vituo vingi vya Afya vya vijijini vinatoa huduma ya uchunguzi wa saratani hivyo amewashauri wananchi kuvitumia.

Kiongozi wa Jumuiya ya watu wanaoishi na maradhi ya saratani Zanzibar Bi. Zakia Mohd amesema kufuatia uchunguzi huo ambapo zaidi ya wanawake 100 wamebainika kuwa na dalili za saratani, wamegundua kuwa tatizo ni kubwa kinyume na walivyo fikiria awali.Amesema kutokana na hali hiyo ZCA itafikiria kununua chombo maalumu cha uchunguzi ‘mamography’ ambacho kinauwezo wa kugundua dalili za awali kabisa za maradhi hayo.

Ameongeza kuwa Jumuiya imeazimia kufanya uchunguzi mwengine wa saratani ya shingo ya kizazi na saratani ya tenzi dume katika siku zijazo kwa vile ni miongoni mwa maradhi yanayowasumbuwa wananchi wengi wa Zanzibar. Mwisho

Baadhi ya akinamama waliofika Hospitali ya Mnazimmoja kufanyiwa uchunguzi wa saratani ya matiti wakipata maelekezo kutoka kwa mhudumu wa hospitali hiyo.

Mkurugenzi wa Ilala Afya Centre ya Dar es salaam Jaffer Dharsee (kulia) akibadilishana mawazo na viongozi wa Jumuiya ya watu wanaoishi na saratani Zanzibar (ZCA) ambapo taasisi hizo mbili kwa kushirikiana na Wizara ya Afya zimeandaa kampeni hiyo.

Dak. Nalvis Dominguez Torres akimfanyia uchunguzi wa maradhi ya saratani ya matiti mmoja wa akinamama waliofika Hospitali ya Mnazimmoja kwa ajili ya uchunguzi wa maradhi hayo.

Daktari bingwa wa uchunguzi wa maradhi ya saratani Zanzibar Msafiri Marijani akichukua sampuli kutoka kwa mmoja wa akinamama waliofika Hospitalini hapo kwa ajili ya uchunguzi wa saratani.

Mkurugenzi wa Ilala Afya Centre ya Dar es salaam Jaffer Dharsee akitoa maelekezo kwa akinamama waliofanyiwa uchunguzi wa saratani ya matiti katika kampeni iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa kituo hicho, Wizara ya Afya na ZCA. icha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar .
IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR.

WAZIRI MAKAMBA MGENI RASMI UZINDUZI WA BARAZA LA VIJANA WILAYA YA MAGHARIBI “A”- ZANZIBAR

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba amewataka vijana wasisite kuleta mabadiliko chanya katika Nchi mana Vijana ndiyo tegemeo la Taifa. 

Ameyasema hayo mjini Unguja alipokua akizindua Baraza la Vijana la Wilaya ya Magharibi A mjini Kisiwani Zanziba.  Amewasishi Vijana watumie baraza hilo kama tanuri ya kutengenezea mbinu za uongozi na pia kama daraja la kuanzishia vikundi vya ujasiriamali na uzalshaji mali na kutengeneza njia mbalimbali za kuinua uchumi na kutowafanya kuwa tegemezi.

Akijibu risala ya Vijana hao ambayo imesomwa na Mwenyekiti wa Baraza hilo la Vijana Bi Farida Juma ambapo walitaja changamoto zinazowakabili ni pamoja na uhaba wa fedha, Waziri Makamba amelitaka Baraza hilo kufungua akaunti na yeye atawapatia mchango wake wa shilingi milioni mbili.

Awali akimkaribisha Mheshimwa Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Magaharibi A, Mheshimiwa Mwinyiusi Hassan amewataka vijana kuwa nguvu kazi ya Taifa na pia wahakikishe wanalinda na kuheshimu na kuulinda utamaduni wa Nchi yetu.

Wakitoa shukrani zao kwa Mgeni Rasmi Mwakilishi wa Baraza hilo la Vijana walimshukuru Mheshimiwa Waziri kwa kuitikia wito wao wa kumuomba awe mgeni Rasmi katika siku yao hiyo adhimu.
Waziri Wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akihutubia wakati wa uzinduzi wa Baraza la Vijana la Wilaya ya Magharibi ‘A’ mjini kisiwani Zanzibar ambapo alkua Mgeni Rasmi.
Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Baraza la Vijana Wialaya Magharibi A, Waziri Wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akionyesha cheti kama ishara ya uzinduzi wa Baraza la Vijana wilaya ya Magharibi A.
Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Baraza la Vijana Wialaya Magharibi A, Waziri Wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akifurahia jambo pamoja na Mbunge wa Jimbo la Magharibi A, Mh Saada Mkuya, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Bi. Farida Juma na Mkuu wa Wilaya ya Magaharibi ‘A” Mh Mwinyiusi Hassan.

TUMETOA KIPAUMBELE KIKUBWA KATIKA SEKTA YA ELIMU: MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema  Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais Dk. John Magufuli imetoa  kipaumbele kikubwa katika kuboresha sekta ya elimu nchini.

Amesema hatua imejidhihirisha kwenye bajeti ya mwaka 2016/2017 ambapo Serikali imetenga sh. trilioni 1.3 kwa ajili ya Sekta hiyo.

Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo jana usiku (Ijumaa, Novemba 25,2016) kwenye harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya uboreshaji wa shule nchini iliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Saalam.

Akizungumza katika harambee hiyo iliyoandaliwa na Taasisi ya Hassan Maajar Trust,  Waziri Mkuu aliwahakikishia wananchi kwamba bajeti ya Sekta ya elimu itaendelea kuongezeka kadri uwezo wa Serikali utakavyokuwa unaimarika.

“Kama mnavyofahamu, Serikali iliamua kuanza mara moja, utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 ambayo inaelekeza Serikali kutoa elimu bure kwa watanzania wote kuanzia shule ya Msingi hadi Sekondari,” alisema.

Alisema uamuzi huo ulikuja na changamoto mbalimbali, ikiwemo upungufu wa madawati kufuatia ongezeko kubwa la wanafunzi waliodahiliwa.

Alisema kufuatia hali hiyo, tarehe 15 Machi, 2016 Serikali iliwaagiza Wakuu wa Wilaya na Mikoa kuhakikisha tatizo la madawati linatafutiwa ufumbuzi wa kudumu kwa kuwashirikisha wananchi na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi.

“Napenda kuwaarifu kwamba, jitihada hizo zimeanza kuzaa matunda kwani baadhi ya mikoa tayari imemaliza tatizo hilo kwa shule za msingi na sekondari, wakati Mikoa mingine ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji,”.

“Hadi sasa Mikoa ambayo imekamilisha zoezi hilo kwa shule za msingi na sekondari na kubaki na madawati ya ziada ni Arusha, Iringa, Kilimanjaro, Manyara, Mbeya, Mtwara, Njombe, Pwani, Shinyanga, Singida na Tabora,” alisema.

Waziri mkuu alitumia fursa hiyo kuwapongeza viongozi na wananchi wa Mikoa hiyo kwa kushiriki kikamilifu katika kumaliza kadhia hiyo kwa wanafunzi ambao walikuwa wanakaa chini. “Huo ndio uongozi tunaoutaka, uongozi wa kusimama bega kwa bega na wananchi na kutatua kero zao”,.

Wakati huo huo aliipongeza taasisi hiyo kwa kutoa mchango mkubwa katika kumaliza upungufu wa madawati katika baadhi ya Mikoa nchini  kupitia harambee mbalimbali.

Alisema kati ya mikoa 13 iliyopata ufadhili kutoka ya Taasisi ya Hassan Maajar Trust, mikoa 10 kati yake imefanikiwa kumaliza tatizo la madawati kwa shule zote za msingi na sekondari.

Mikoa hiyo ni pamoja na Njombe, Rukwa, Singida, Pwani, Shinyanga, Lindi, Mbeya, Iringa, Mtwara, na Kilimanjaro.

“Hii inathibitisha kwamba jitihada za pamoja kati ya Serikali na asasi zisizokuwa za Kiserikali zinaweza kuleta ufumbuzi wa changamoto nyingi zinazolikabili Taifa letu,” alisema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa taasisi ya Hassan Maajar Trust Fund,    Balozi Mwanaidi Maajar, alisema tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo miaka mitano iliyopita  imefanikiwa kuwainua watoto takribani 30,000 kutoka sakafuni kufuatia kampeni ya Dawati kwa Kila Mtoto.

Huawei, Clara Boutique wazindua duka kubwa Kanda ya Ziwa

$
0
0
Kampuni ya Teknolojia ya Mawasiliano ya Huawei Tanzania kwa kushirikiana na Mfanyabiashara maarufu jijini Mwanza, Clara Salon & Boutique imefungua duka kubwa liitwalo “Clara Smartphone Shop” katika Jiji la Mwanza. Hatua hiyo ni mwendelezo wa Huawei katika kutekeleza moja ya mikakati yake ya kujitanua kibiashara nchini.

Huawei imeona kuwepo wa Duka hili kubwa la Clara, katika Jiji la Mwanza kunatokana na kukua mahitaji ya bidhaa za Huawei nchini na hivyo kutoa fursa ya watumiaji kupata huduma kwa karibu zaidi.

“Tunafahamu watanzania walio wengi wanachohitaji, ndiyo maana leo hii tuko Mwanza. Tunaamini kuwa hii ni fursa pekee kwa wakazi wa Mwanza na miji ya jirani kupata bidhaa zetu zenye ubora na viwango vya hali ya juu. Tunaamini kuwa Clara Salon & Boutique wana jina kubwa katika Jiji la Mwanza na hivyo itatusaidia sisi kutimiza lengo letu, anasema Mkurugenzi huyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Huawei Tanzania, Bruce Zhang(kulia) na Mkurugenzi wa Clara Huawei Smartphone Brand Shop, Clara Mwasa wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Duka hilo uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Mwanza.

Huawei inampango wa kukuza teknolojia ya mawasiliano nchini Tanzania na sasa imeanza kushirikiaba kwa karibu na wazawa kama Clara. Milango iko wazi kwa yeyote anayetaka kutuunga mkono kiabiashara.

Wakati Huawei inazindua duka hilo katika Ukanda wa Kanda ya Ziwa, Mkurugenzi huyo alitangaza uwepo wa simu mpya ya kisasa, Huawei Y3II na nyinginezo, katika soko la simu nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Huawei Tanzania, Bruce Zhang(katikati) akiwaonyesha wateja walihudhuria uzinduzi wa Duka la Clara Huawei Smartphone Brand Shop lililozinduliwa rasmi mwishoni mwa wiki jijini Mwanza.Kulia ni Mkurugenzi wa Duka hilo, Clara Mwasa.

Alisema kuwa simu hiyo ina ubora na kuwataka watanzania kutumia, akifafanua zaidi kuwa ni simu yenye ubora, lakini gharama yake sio kubwa, ikilinganishwa na simu za makampuni mengine.Pia bidhaa nyingine zitaambatana na simu hiyo kama matoleo mangine tofauti Huawei P9, Y3c, Y5II ,Y6II, Y3lite na nyingine nyingi.

Hizi ndizo faida za kuwa na duka kubwa katika Jiji la Mwanza. Kuanzia sasa wanunuzi wa bidhaa zetu wana fursa ya kupata bidhaa zetu zote kwa wakati. Tunaanza na simu hii ya Huawei Y3II ambayo kwa hakika kila atakayeamua kuitumia ataipenda kwa ubora wake.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, Kampuni ya Huawei inaendelea na mchakato wake wa kusogeza huduma zake kwa wateja wake, kwa lengo la kutimiza malengo yake ili kupambana na soko la mawasiliano.

DKT MABULA AHAMASISHA MASUALA YA ELIMU JIMBONI KWAKE ILEMELA

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu waziri wa Ardhi Dkt .Angeline Mabula akigawa Chaki zinazotengenezwa na kiwanda cha vijana- Maswa Chalk kilichopo Mkoani Simiyu,Dkt.Mabula yupo ziara jimboni kwake akihamasisha masuala ya kielimu kwa kugawa vitabu na Katoni za Chaki kwenye shule zake za msingi na sekondari.

RAIS MSTAAFU ALI HASSAN MWINYI AONGOZA MAHAFALI YA CHUO KIKUU CHA KAMPALA JIJINI DAR ES SALAM

$
0
0

RAIS mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi amewataka wahitimu wa vyuo vikuu nchini kuacha tabia ya kuchagua kazi za kufanya mara baada ya kuhitimu elimu yao. Mwinyi alisema tabia hiyo imepitwa cha wakati hasa katika dunia ya sasa yenye changamoto kubwa ya ajira.

Rais Mwinyi alitoa kauli hiyo juzi wakati akizungumza na wahitimu wa kozi mbalimbali kwenye sherehe za mahafali ya nne ya Chuo Kikuu cha Kampala (KIU) cha jijini Dar es Salaam.


Alisema kitendo cha baadhi ya wahitimu hasa wa vyuo vikuu kupendelea kuchagua kazi za kufanya kimekuwa kikiwapotezea muda na fursa anuai, hivyo kuwataka kuacha tabia hiyo ambayo kwa kipindi hiki imepitwa na wakati.Alisema wahitimu hawana budi kuanza kufanya kazi zozote zinazojitokeza mbele yao na kutumia fursa hiyo kuelekea kwenye mafanikio kadri walivyojipangia katika  maisha yao. 

"...Nawapongeza wahitimu kwa hatua hii, sasa mnaingia katika maisha mapya na ya vitendo msiende kuchagua kazi za kufanya, anza na kazi yoyote inayojitokeza mbele  yako kisha uitumie kutimiza ndoto zako," alisema katika hotuba yake kwa wahitimu hao.
 Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi akiwatunuku wahitimu wa kozi mbalimbali katika mahafali ya Chuo Kikuu cha Kampala cha jijini Dar es Salaam kwenye sherehe za mahafali.
 Baadhi ya waadhiri wa chuo hicho wakiwa kwenye mahafali hayo.
 Baadhi  ya wahitimu wa ngazi ya digree kozi ya afya wakila kiapo cha kuhitimu fani hiyo.
 Sehemu ya wahitimu wakiwa katika mahafali hayo.
Msafara wa mahafali ukiongozwa na Rais msaafu wa Awamu ya Pili, Mwinyi mara baada ya sherehe za mahafali ya nne ya Chuo Kikuu cha Kampala (KIU) cha jijini Dar es Salaam.kumalizika.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Viewing all 110089 articles
Browse latest View live




Latest Images