Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1437 | 1438 | (Page 1439) | 1440 | 1441 | .... | 3282 | newer

  0 0  Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipozungumza nao, kusikiliza na kutatua kero zao katika eneo la Keko Dar es Salaam leo, akiwa katika ziara ya kikazi wlayani Temeke. Mh.Paul Makonda yuko kwenye ziara ya siku kumi ya kuijenda upya Dar Es Salaam.PICHA NA BASHIR NKOROMO

  0 0


  BAADA YA KUPIGA SHOW AKIWA NA WANAMUZIKI SAUTI SOL KUTOKA KENYA NA KUACHA ZOGO KUBWA NDANI YA MARYLAND MALAIKA SASA KUWARARUA  HOUSTON TEXAS IJUMAA HII YA THANKS GIVING ! FOR BOOKING PIGA NAMBA ZASIMU !

  0 0

  For inquiries Call +255 766 411441

  0 0


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh.Amos Makalla akihutubia mamia ya wananchi katika  sherehe ya maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama, Sherehe iliyo fanyika kimkoa katika Uwanja wa CCM Rwanda Nzovwe jiji la Mbeya. Sherehe hii iliyo wagusa wadau mbalimbali ikiwepo, Jeshi la Polisi, Wanafunzi, Mashirika ya kiserikali na Mashirika binafsi Pamoja na wananchi wote kwa ujumla katika jukumu la Kuzuia na Kupinga ajali za barabarani kwa kutii sheria Bila Shuruti.
  Picha zote na Mr.Pengo wa Mmg Mbeya.


   Bendi ya Magereza ikiongoza maandamano ya sherehe ya wiki ya nenda kwa usalama yaliyo anzia maeneo ya Soweto mpaka uwanjani Rwanda Nzovwe.

   Baadhi ya madereva wa  bodaboda wakiwa wamepozi kwa utulivu.
   Mkuu wa mkoa wa Mbeya na mgeni rasmi wa sherehe ya maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama Mhe. Amos Makalla akipata picha ya pamoja na wadau wa Usalama Barabarani.


  0 0

  Familia ya Kiluvia inasikitika kutangaza kifo cha baba yao mpenzi Mzee Hamadi Kiluvia (pichani) kilichotokea jana  alfajiri jijini Dar es salaam. Habari ziwafikie ndugu, jamaa, majirani na marafiki popote pale walipo.
  Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Regent Estate mtaa wa Migombani nyumba namba 72 ambapo ndipo ulipo msiba.

   Msibani hapo ni hatua chache kutoka kituo cha mafuta cha Oil Com Victoria house, ila ili kufika unafuata barabara ya Mikocheni kwa Kairuki hadi njia panda ambapo unakata kulia na mbele tena unakutana na barabara inayotoka kwa JK  ambapo unakata tena kulia. Hatua chache mbele  utakuwa umefika.

  Marehemu Mzee kiluvia atakumbukwa kama mmoja wa viongozi wa zamani serikalini na michezoni, ambapo katika uhai wake aliwahi kuwa mkuu wa Wilaya, mmoja wa viongozi wa chama cha mpira wa miguu cha FAT enzi hizo pamoja na kuwa kiongozi aliyeheshimika sana katika klabu ya Yanga.

  UPDATES:  Mwili wa marehemu utapelekwa msikiti wa Regent Estate Ijumaa  sita kamili mchana kwa ajili ya kuswaliwa baada ya swalat'Jumaa. Kisha utapelekwa nyumbani kwake kwa ajili ya taratibu za mwisho kabla ya  kuanza safari ya kupelekwa Usangi, Same, mkoani Kilimanjaro kwa mazishi ambayo yanayotarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi saa saba mchana.

  Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu baba yetu mahala pema peponi - Amin.

  Matokeo ya Utafutaji
  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa jiji la Dar,Paul Makonda amepiga marufuku biashara ya samaki kandokando ya barabara inayoelekea kivukoni na soko la samaki la feri baada ya wafanyabishara wa feri kulalamika kwa mkuu wa mkoa huyo kuwa wafanyabiashara hao wamekuwa wakwepa kodi.

  Awali Makonda aliambiwa na wafanyabiashara hao kuwa soko hilo linakosa wateja kutokana na kushindwa kufikiwa na wateja ambao hununua samaki au bidhaa nyengine kandokando ya barabara na kusababisha wateja kutofika sokoni humo.

  Wakati huo huo Makonda amesikitishwa na kitendo cha wakuu wa idara mbalimbali kushindwa kukamilisha miradi kwa wakati kwa kisingizo cha kutopata fedha za bajeti ya serikali kuu ikiwa wangeweza kubuni miradi itakayowaingizia fedha.

  RC Makonda alisema kuwa hatakubaliana na watendaji wa namna hiyo kwani hurudisha maendeleo nyuma.

   Mnada wa samaki katika Soko la Feri ulipokuwa ukiendelea mapema jana jioni. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
   Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza na viongozi na watendaji wa wilaya ya Ilala katika ukumbi wa Anatoglo jana jijini Dar es salaam.
   Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala,Edward Mpogolo akizungumza machache katika ukumbi wa Anatoglo jana jijini Dar es salaam.
   Viongozi na watendaji wa wilaya ya Ilala wakimsikiliza  Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda katika ukumbi wa Anatoglo jana  jijini Dar es salaam.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0
  0 0

  Kundi la Muziki wa kizazi kipya(Bongo Flavour) Wasafi limemuomba Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye   kusaidia wasanii wa muziki huo kujivunia kazi yao kwa kupata maslahi ya kazi hiyo kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

  Akizungumza wakati Waziri huyo alipotembelea Studio za Wasafi na kujionea utendaji kazi wa studio hiyo, Mmiliki wa studio hizo Naseeb Abdul (Diamond Platinumz) amesema, kumekuwa na changamoto nyingi katika tasnia ya muziki hasa wizi wa kazi zao ambazo zimekuwa zikirudufiwa na kuuzwa kiholela ndani na nje ya nchi bila wao kufaidika na uuzwaji wa kazi hizo.

  Changamoto nyingine alizozitaja  msanii Diamond ni pamoja na kupunjwa mapato yatokanayo na Miito ya Simu (Caller tunes) , kukosekana kwa ukumbi wa kisasa kwa ajj ili ya kufanyia maonesho makubwa ya muziki nchini, kuongezeka kwa uwiano wa nyimbo za kitanzania zinazopigwa redioni dhidi ya nyimbo za kigeni hasa kutoka Afrika ya Magharibi.

  Aidha wamemuomba Waziri Nape Moses Nnauye kuwasaidia kupata Elimu juu ya ulipaji kodi ili tasnia ya Muziki nayo iweze kuwa kati ya tasnia zenye mchango mkubwa kwa pato la taifa kwa maendeleo ya wasanii na taifa kwa ujumla.

  Kwa upande wake Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye  amehaidi kuzifanyia kazi changamoto hizo na kuifanya tasnia ya muziki kuwa ajira kubwa kwa vijana wengi kwa kuongeza vipato vyao na pato la taifa kwa ujumla.


  Wasafi Classic ni kundi la Muziki wa kizazi kipya(Bongo Flavour) Tanzania linalomilikiwa na Msanii Naseeb Abdul (Diamond Platinumz) na mpaka sasa lina wasanii wapatao 16 na linaongozwa na mameneja Babu Tale, Said Fella na Sallam SK.
  wasf
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye  akizungumza na  Mmiliki wa Wasafi Classic Msanii Naseeb Abdul (Diamond Platinumz) wakati alipotembelea Studio za Wasafi Classic kujionea utendaji kazi wa studio hiyo Novemba 23,2016.
  wasf2
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na Mmiliki wa Wasafi Classic Msanii Naseeb Abdul (Diamond Platinumz) na wasanii harmonize na Rich Mavoko.

  0 0

  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Kanda ya Kaskazini ,Elizabeth Mushi akizungmza walipkkutana na wanahabari mkoani Kilimanjaro.
  Wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya siku 16 za kupinga ukatili kutoka Mtandao wa Jinsia wa jeshi la Polisi (TPF Network) , Grace Lyimo (Kushoto) na Theresia Nyangasa.(Kulia).
  Meneja Programu wa Shirika lisililo la Kiserikali linalojishughulisha na kupinga ukeketaji (NAFGEM) Honorata Nasuwa akizungumza mbele ya wanahabri juu ya uzinduzi rasmi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia .
  Wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Kanda ya Kaskazini walipokutana na wanahabri mkoa Kilimanjaro kuzungumzia tukio la uzinduzi litakalo fanyika kesho Ijumaa katika viwanja vya kituo kikuu cha Mabasi mjini Moshi.


  0 0

  Na Evelyn Mkokoi

  Hifadhi ya Taifa ya Msitu wa Ukwemi uliyopo katika wilaya ya Kahama upo hatarini kutoweka kutokana na shughili za kibinadamu zinazofanywa ndani ya hifadhi hiyo zinazochangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira.

  Hayo yameelezwa na Meneja kutoka wakala wa Taifa wa Misitu Bw. Mohamed Dosa wakati wa Ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina alipotembelea HIfadhi hiyo iliyopo ndani ya Halmashauri ya Kahama inayopakana na Halmashauri ya Mbongwe Mmkoani geita.

  Katika Ziara yake ya Ukaguzi wa Mazingira katika Hifadhi ya Msitu Huo, Naibu Waziri Mpina alielezwa kuwa shughuli kubwa zinazotegemewa na wakazi wa vijiji vya jirani na msitu huo ni, ukataji miti kwa uchomaji wa mikaa na ukataji wa magogo kwa shunghuli mbali mbali ikiwa ni pamoja na shughuli na ujenzi na utengenezaji wa samani za majumbani.

  Meneja Dosa Amemuelezea Naiubu Waziri Mpina kuwa (generation) kizazi cha kwanza cha aina na miti ndani ya hifadhi hiyo kilishakwisha na miti inayoota na kuonekana sasa ni ya kizazi cha pili.

  “changamoto kubwa tunayokumbana nayo katika kulinda hifadhi hii ni magari ya doria kuzunguka ndani ya msitu kwani ni mkubwa sana na hakuna skari wa kutosha kufanya doria. “ Alisisitiza Bw. Dosa.

  Akiwa katikati ya Msitu huo Naibu Waziri Mpina alijionea Uharibifu mkubwa wa uchomaji mkaa na kushuhudia mhalifu Bw John Abdalah Sanga makazi wa kijiji cha jirani cha mwendakulima aliyekuwa akimaliza kuchoma mkaa katikati ya msitu huo na kueleza kuwa amekuwa akifanya kazi hiyo kwa takribani miaka mitatu sasa hali iliyompelekea Naibu Waziri Mpina na timu yake kutekekeza baadhi ya matanuru ya mkaa ndani yam situ huo.

  Kwa upande wake Mratibu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na usimamizi wa Mazingira NEMC kanda ya ziwa Bw. Jamal Baruti alieleza kuwa hali ya uharibifu wa misitu nchini bado ni kubwa na suala la mkaa bado ni changamoto, hivyo wanaanchi washiriki katika kuhifadhi misitu na kutafuta mbadala wa mkaa na misitu ni muhimu kwa kutunza baiyonuwai., wakati katibu tawala wa wilaya ya kahama Bw. Thomas Nganya akitoa Rai kwa wananchi waone kuwa suala la utunzaji wa mazingira ni jukumu la kila mmoja na siyo kuiachia seriali peke yake. 
  Sehemu ya Hifadhi ya Msitu wa Mkwemu iliyoharibiwa vibaya na shughuli za binadamu ikiwa na pamoja na uchomaji wa mkaa, na baadhi ni magogo yanayoonekana pichani yaliyokuwa yamekatwa na wahalifu wa mazingira.
  Katikati Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akishiriki katika kuteketeza tanuru la mkaaa katikati ya hifadhi ya m situ ya Mkwemu Wilayani Kahama.
  Aliyeshika kiuno, Naibu Waziri Ofisi Ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akiangalia Tanuru la Mkaa likitekea baada ya kushiriki kuteketeza ndani ya Msitu wa Mkwemu wilayani Kahama. (Picha na Evelyn Mkokoi wa OMR)

  0 0

  Mwenyekiti Wa Serikali Ya Mtaa Wa Gongolamboto, Bakari Shingo akiwa chini ya ulinzi baada ya kuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akamatwe kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo ya kughushi nyaraka za serikali. 

  Malalamiko kuhusiana na kutosoma taarifa ya mapato na matumizi na kukusanya mapato kutoka kwa wananchi kinyume ana taratibu za makusanyo ya fedha za umma.

  RC Makonda anaendelea na ziaraa yake ya siku 10 katika jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kusikiliza kero za wanachi ambapo leo amefanya ziara katika Wilaya ya  Ilala.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
   Mwenyekiti Wa Serikali ya Mtaa wa Gongolamboto, Bakari Shingo alipokuwa akitoa hotuba fupi kabla ya kuwekwa chini ya ulinzi wa polisi
   Mwenyekiti Wa Serikali ya Mtaa wa Gongolamboto, Bakari Shingo akiwa  chini ya ulinzi wa Polisi.
    Mwenyekiti Wa Serikali ya Mtaa wa Gongolamboto, Bakari Shingo akiwa  chini ya ulinzi wa Polisi akipakizwa kwenye gari kwa hatua zaidi za kisheria


  0 0
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais mstaafu wa awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais mstaafu wa awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi Ikulu jijini Dar es Salaam. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais mstaafu wa awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na  Waziri wa Ardhi  Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi kabla ya kuanza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

  0 0

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amekutana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke alipotembelea katika ofisi za Wizara hiyo.

  Balozi Sarah alipongeza mafanikio makubwa yaliyofikiwa na Serikali ya Tanzania katika sekta ya Ardhi kwa kipindi kifupi. Miongoni mwa mafanikio hayo ni pamoja na Mpango wa Serikali kupanga, Kupima na Kumilikisha kila kipande cha ardhi nchini pamoja na Mfumo Unganishi wa Taarifa za Ardhi (ILMIS) ambao unalinga kutoa huduma za ardhi kwa wananchi kielektroniki pamoja na utoaji hati za kielektroniki.

  Aidha, Balozi huyo amepongeza mchakato wa kuandaa Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 2016 na jinsi ulivyo shirikisha wananchi na wadau wote wa sekta ya ardhi nchini.

  Mhe. William Lukuvi alimueleza Balozi huyo ambaye alifurahishwa zaidi na juhudi za Serikali za kuwawezesha wananchi kumiliki ardhi katika kujiletea maendeleo yao, pamoja na juhudi za kuwawezesha wananchi wanaoishi katika makazi holela kupimiwa na kumilikishwa makazi yao pamoja na kupatiwa hati miliki za ardhi.
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimkaribisha Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke katika ofisi za Wizara hiyo jijini Dar es salaam.
  Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke akielezea kufurahishwa kwake na mafanikio makubwa yaliyofikiwa na Serikali ya Tanzania katika sekta ya Ardhi.
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akisalimiana na Afisa Maendeleo kutoka ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania wakati akimuaga Balozi wa Uingereza nchini Tanzania.

  0 0
 • 11/23/16--23:28: Article 11


 • 0 0

   Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC), Clifford Tandari (kulia) akifurahi jambo na Balozi wa Australia mwenye makazi yake Jijini Nairobi, Nchini Kenya, John Feakes aliemtembelea ofisini kwake Jijini Dar es salaam leo, ambapo walizungumzia fursa mbalimbali za uwekezaji zinazopatikana nchini Tanzania.
  Balozi wa Australia mwenye makazi yake Jijini Nairobi, Nchini Kenya, John Feakes (kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC), Clifford Tandari (kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na Meneja Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania, Pendo Gondwe pamoja na Afisa Mwandamizi wa Huduma kwa Wawekezaji wa TIC, George Mkono.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mh. Amos Makalla ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe za wiki ya nenda kwa usalama akipokea maelekezo kutoka kwa Meneja wa Kampuni ya Fleet Track, Bwana Taufiq, Fleet Track ni Kampuni inayo jishughulisha na Uuzaji wa Vifaa vya kisasa vitumikavyo kwenye vyombo mbalimbali ikiwemo Magari, Ndege, Pikipiki pia hata nyumbani ambavyo husaidia kwa kiasi kikubwa kuweka ulinzi na usalama wa chombo chako chochote na mahali popote kwa kutumia GPS Sattelite moja kwa moja, 

  Pia vifaa hivyo vya kisasa Hukupatia matokeo halisi ya kifaa au chombo chako kwa kukuonyesha moja kwa moja kupitia simu ya mkononi au kompyuta, Kwenye vyombo vya usafili pia kazi ni hiyo hiyo kukupatia matokeo ya picha na sauti kwenye gari lako au chombo chochote cha usafiri pia, Kifaa hicho kinakupa uhuru wa mmiliki wa gari kuzioma gari lako popote duniani ikiwa Dereva anaendesha kinyume na utaratibu, Kipimo cha Spidi, Kujuwa matumizi ya Mafuta, Dereva ameanza safari muda gani na anaendesha au anakudanganya inakupa taarifa, gari ikiama njia alama inakujuza, Epuka kukamatwa na tochi kwani inarekodi mwendo kasi wa gari, Kuweka ulinzi kwenye gari yako mtu mwengine yoyote asiliwashe bila idhini yako,na Vitu vingine vingi kwa vyombo vya usafiri na Pia Kampuni ya Fleet Track imefunga mitambo ya vifaa hivi kwenye magari mengi ya miziogo, mabasi ya mikoani na magari mengi nchini, Imefanikiwa kukamata magari manne yaliyo ibiwa yakiwa yamefungwa vyombo hivyo.
  Kwa maelezo zaidi wasiliana nao kwa mawasiliano yafuatyayo.

  Magore Street, P.O.Box 2115, Dar es salaam, Tanzania.
  Mobile:+255 784 911 786 Hotline:+255 774 786 911
  taufiq@fleettracktz.com,  www.fleettracktz.com.
  Mkuu wa mkoa wa mbeya mh.Amos Makalla akishuhudia kwa vitendo utendaji kazi wa vifaa hivyo kutoka katika kampuni ya Fleet Track Tanzania wanao patikana Jijini Dar es salaam.

  Picha ya pamoja ya watendaji wa kampuni hiyo ya Fleet Track Ikiongozwa na Meneja Taufiq (katikati).  0 0

  The Federal Republic of Germany,  KfW Development Bank  and the East African Community (EAC) today signed Financing Agreement of 40 million euros in total, to support regional immunization programme and establishment and operations of the Regional Laboratory Network for Communicable Diseases.

  The Secretary General of the East African Community, Amb. Liberat Mfumukeko signed on behalf of the Community while His Excellency Egon Kochanke, Ambassador of the Federal Republic of Germany to the United Republic of Tanzania and also accredited to the East African Community initialled on behalf the Germany Government and Dr. Helmut Schon, on behalf of KfW.
  Secretary General of the EAC, Amb. Liberat Mfumukeko and Ambassador of the Federal Republic of Germany His Excellency Egon Kochanke signs the agreement as Ms Lena Thiede, Counsellor / Head of Regional Cooperation at the German Embassy in Dar es Salaam; Director of KfW Development Bank Dr. Helmut Schon and EAC Deputy Secretary General (Productive and Social Sector) Hon Bazivamo looks on.

  ·         30 million euros in financial assistance will be invested in Immunization programmes in the EAC in collaboration with GAVI

  ·         Another 10 million euros in financial assistance will be used in  the operation of the Regional Laboratory Network for Communicable Diseases consisting of mobile laboratory units located at national reference laboratories.

  This new commitment will bring Germany’s contribution to fight child mortality through immunisation programmes to 90 million euros since 2013. So far about 50 million of Rota Virus Vaccines, Pneumococcal Vaccines and Pentavalent Vaccines have been financed in the EAC Partner States. Implicitly, an equal number of children have been vaccinated against the biggest killers of children, namely diarrhea and pneumonia.
   
  The Secretary General of the East African Community, Amb. Liberat Mfumukeko having a chat with His Excellency Egon Kochanke, Ambassador of the Federal Republic of Germany to the United Republic of Tanzania and Accredited to the EAC.

  Speaking during the signing ceremony, the  EAC  Secretary General, Amb. Liberat Mfumukeko, thanked the Government of the Federal Republic of Germany for its support to the EAC. ‘’We have truly benefited from the German support which has catalysed other development Partners to support our projects and programmes.


  0 0
  0 0

  Waziri wa Rasilimali za Maji na Umwagiliaji wa Misri, Prof. Dkt. Mohammed Abdel Aty na Waziri wa Maji na Umwagiliaji nchini, Inj. Gerson Lwenge, pamoja na Balozi wa Misri nchini, Yasser Ahmed Al Eldin Elshawaf wakimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali za Maji, Grace Nsanya mara baada ya kuzindua mradi wa maji wa visima 30 kwa ajili ya uboreshaji wa huduma ya majisafi kwa wilaya za Same, Mwanga, Kiteto, Bariadi na Itilima.
  Waziri wa Rasilimali za Maji na Umwagiliaji wa Misri, Prof. Dkt. Mohammed Abdel Aty na Waziri wa Maji na Umwagiliaji nchini Inj. Gerson Lwenge, wakifungua maji yaliyotokana na moja ya visima 8 vilichochimbwa mkoani Kilimanjaro katika Kijiji cha Kasapo, Kata ya Mkuyuni, Wilayani Same.
  Waziri wa Rasilimali za Maji na Umwagiliaji wa Misri, Prof. Dkt. Mohammed Abdel Aty na Waziri wa Maji na Umwagiliaji nchini, Inj. Gerson Lwenge wakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mecky Sadick na Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Senyamule.


older | 1 | .... | 1437 | 1438 | (Page 1439) | 1440 | 1441 | .... | 3282 | newer