Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1436 | 1437 | (Page 1438) | 1439 | 1440 | .... | 3285 | newer

  0 0


  Mtu mmoja aliye fahamika kwa jina moja la Mwita na  mfanyabiashara wa nyama ya ng'ombe afanyae bishara zake eneo la Mwanjelwa, amekutwa amefariki dunia asubuhi hii  katika eneo la Mafiati jijini Mbeya akiwa ametokwa na damu nyingi kichwani ikisemekana kuwa "alivamiwa na kupigwa na watu wasio julikana". Pichani Mwili wa marehemu Mwita ukiingizwa kwenye Gari ya Polisi.


  Huzuni ikiwa imetawala kwa ndugu jamaa na marafiki  eneo hilo la tukio huku wakipeana taarifa kuwajuza wengineo juu ya tyukio hilo lililo Tokea asubuhi hii eneo la Mafiati Jijini Mbeya.
  Jeshi la Poli likiondoka na mwili wa marehemu 
  PICHA NA MR.PENGO WA MMG. 

  0 0
 • 11/20/16--21:09: TIBA YENYE NGUVU ZA AJABU!
 • Tiba hii inaitwa JIKO. Kila mwanaume anae itumia, INAMPONYESHA KABISA tatizo la UKOSEFU na UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME. Imethibitishwa na MKEMIA MKUU WA SERIKALI YA TANZANIA

  Kufahamu jinsi tiba hii inavyo fanya kazi, bofya link hii hapa chini :


  Kwa mahitaji yako ya tiba hii, wasiliana na duka la NEEMA HERBALIST & NUTRITIONAL FOODS CLINIC kwa simu namba 0766 53 83 84.

  Tunapatikana UBUNGO jijini DAR ES SALAAM, jirani na SHULE YA MSINGI UBUNGO NATIONAL HOUSING nyuma ya jengo la UBUNGO PLAZA. · Kwa wateja waliopo DAR ES SALAAM, wasio na nafasi ya kufika ofisini kwetu, watapelekewa dawa mahali walipo ( HOME & OFFICE DELIVERY ).

  · Kwa wateja waliopo mikoani, watatumiwa dawa kwa njia ya mabasi mbalimbali.

  · Kwa wateja waliopo Zanzibar, watatumiwa dawa kwa njia ya usafiri wa boti.

  · Kwa wateja wa Mombasa, watatumiwa dawa kwa basi la TAHMEED COACH.

  · Kwa wateja wa NAIROBI watatumiwa dawa kwa basi la DAR EXPRESS.

  · Na kwa wateja wa UGHAIBUNI ( DIASPORA), watatumiwa dawa kwa njia ya POSTA au DHL.

  · Kwa taarifa zaidi kuhusu huduma zetu, tembelea kila siku website yetu www.neemaherbalist.com


  0 0

  10
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe: Paul Makonda akijibu kero za wananchi aliposimama na msafara wake eneo la Kibada Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.
  11
  Mkazi wa Kibada, Bi Siwazuri Abdalah akimuelezea Makonda kero anazozipata katika Hospital ya kibada.
  12
  Mkuu wa Idara ya Uifadhi wa Mazingira na Usimamizi wa Taka Ngumu, Fanuel Kibera akimuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda (katikati), mchoro wa dampo la kisasa  litakalojengwa eneo la Kisarawe II Kigamboni.
  14
  Msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ukiwa eneo la Kisarawe II.
  16
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe: Paul Makonda (katikati), akiwa amefuatana na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa, na   Mkurugenzi wa Kiwanda cha maji na maziwa (MILKCOM), Said Nahdi  (mwenye kanzu) wakiwa ndani ya kiwanda hicho wakikagua shughuli za kiwanda hicho.
  18
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe: Paul Makonda akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa shule ya msingi Tunduwi Songani.
  19
  Wananchi wa Tunduwi Songani wakishuhudia uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa shule ya msingi .


  0 0  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza wakati wa uzinduzi wa magari mapya ya F12 kutoka kampuni yas Yutong katika hafla iliyofanyika katika Hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiakta utepe kuashiria uzinduzi wa magari mapya ya F12 kutoka kampuni yas Yutong katika hafla iliyofanyika katika Hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa kampuni ya Yutong mara baada ya uzinduzi wa magari mapya ya F12 kutoka kampuni ya hiyo katika hafla iliyofanyika katika Hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam.

  Picha na kitengo cha Mawasiliano Serikali WHUSM

  0 0

  Timu ya Boko Beach Veterans (BBV) imeeendeleza ubabe wake baada ya kuichapa Timu ya Veterans ya Bunju kwa jumla ya magoli 6-1 na kuendeleza kuweka rekodi ya kutofungwa katika michezo mitano. BBV imeshazitadika Timu za Tabora Veterans, BOT Veterans, Mbezi Veterans na Veteran ya Jeshi Lugalo, na kufanya kuwa tishio kwa timu zingine ambazo zinatafakari ni namna gani wataikabili timu hiyo vinara wa Maveterans.

  Dalili za mvua hiyo zilianza mapema katika kipindi cha kwanza baada ya kazi nzuri ya kiungo Lazaro Ngimba kuihadaa beki ya Bunju na kutoa pasi nzuri kwa Bruce Mwile ambaye bila ajizi alitupia kambani, baada ya goli hilo BBV waliendelea kuishambulia ngome ya BUNJU kama nyuki na kufanikiwa  kufunga magoli mengine kupitia kwa Lazaro Ngimba, Holombe Jr, Hebron Malakasuka na Bruce Mwile aliefunga hat trick. 
  Katika mchezo huo uliotawaliwa na BBV ambayo ilionyesha uwezo mkubwa iliwakilishwa na golikipa Dihile, Mabeki Mango, Msaki, Robert, Kairuki, viungo Lazaro, Rodric Mwambene, Deo Ringia, Horombe Jr, Mawinga Ole aka Aguerro, Richard, Chief Ndabile na striker Bruce, Edwin aka Mavugo na Wengine waliotokea Katika bench.


  0 0

  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu)Mhe. Dkt. Abdallah Possi akipokea mafuta maalumu ya ngozi kwa watu wenye ualbino kutoka kwa Mkuu wa Kituo cha kuhudumia watoto wenye Ualbino cha Lamadi Bi. Hellen Ntambulwa ikiwa ni sehemu ya zawadi kwa ziara yake kituoni hapo. Novemba 20, 2016
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto wenye ualbino wanaolelewa na Kituo cha Lamadi Wilayani Busega Mkoa wa Simiyu.
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akimsikiliza Mwandishi wa habari wa ITV Bw. Berensi China wakati wa ziara yake Kituo cha kulelea watoto wenye Ualbino cha Lamadi Simiyu. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akiwasalimiana na viongozi wa Wilaya katika eneo la mapokezi wakati wa ziara yake Wilayani hapo.

  Nteghenjwa Hosseah , Monduli.

  Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ameuagiza uongozi wa wilaya ya Monduli Mkoani Arusha pamoja na baraza la madiwani la wilaya hiyo kuhakikisha wanabadilisha umiliki wa shamba la Manyara ranch lenye ukubwa wa ekari 44,930 kutoka kwa taasisi ya Tanzania Land Conservation Trust{TLCT} kwenda kwa wananchi wa vijiji viwili kama Rais wa awamu ya tatu Mhe. Benjamini William Mkapa alivyoagiza.

  Rc Gambo alitoa agizo hilo katika mikutano ya hadhara iliyofanyika katika kata ya Elesilalei na Makuyuni baada ya kutembelea miradi  ya mamilioni ya fedha iliyopo ndani ya shamba hilo inayofadhiliwa na African Wildlife Foundation{AWF} na kuelezwa kero na changamoto zilizopo juu ya umiliki wa shamba hilo kwa taasisi ya TLCT.
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha akitoa maelekezo ya kubadilisha Hati ya Umiliki wa shamba kutoka kwa TLCT kwenda kwa wananchi wa vijiji vya Elesilalei na Ortukai.

  Alisema nyaraka zinaonyesha wazi kuwa Shamba hilo lilitolewa kwa wananchi wa vijiji vya Elesilalei na Ortukai na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu  mwaka 1999   kwa ajili ya kilimo na ufugaji lakini hilo halikufanyika badala yake  taasisi ya TLCT ikajimilikisha shamba hilo kinyume na maagizo.

  Mkuu huyo wa Mkoa  alisema kutokana na hali hiyo ninawaagiza viongozi wote wa wilaya ya Monduli wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo pamoja na baraza la madiwani kuhakikisha ndani ya muda mfupi wanabadilisha umilikiwa wa shamba hilo kutoka taasisi hiyo kwenda katika vijiji hivyo.

  Gambo alisema serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt John  Magufuli iko madarakani kwa ajili ya kuwahudumia wanyonge na watu wa hali ya chini na kamwe haiwezi kuona baadhi ya watu fulani wananufaika na rasilimali ya nchi kwa manufaa yao.
  Meneja wa Ranch hiyo Ndg. Fidelis Ole Kashe akiwasilisha taarifa ya Shamba hilo kwenye Kikao maalum na Mkuu wa Mkoa wa Arusha pamoja na viongozi wa Wilaya.


  0 0

  Na Benny Mwaipaja, Msemaji Wizara ya Fedhana Mipango

  SERIKALI imesema kuwa itaendelea na utaratibu wa kuwalipa wastaafu wanaohudumiwa na Wizara ya Fedha na Mipango, pensheni yao kila mwezi kwa mujibu wa sharia ya mafao ya wastaafu Na. 371 badala ya kuwalipa malipo hayo kila baada ya miezi mitatu

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. DOTTO JAMES amesema kuwa uamuzi huo umetolewa baada ya kupitia na kujadili mapendekezo ya baadhi ya wastaafu waliofika Makao Makao Makuu ya Wizara ya Fedha Jijini Da ers salaam mwezi uliopita wakitaka serikali irejeshe utaratibu wa kuwalipa kila baada ya miezi mitatu mitatu ili waweze kujikimu kimaisha.

  James amesema kuwa Wizara imepokea maombi kutoka kwa baadhi ya wastaafu kutaka kulipwa kila baada ya kipindi hicho huku wengine wakitaka kulipwa kila mwezi hatua ambayo imeifanya Serikali kuamua kulifanyia kazi suala hilo kwa kina na kuahidi kulitolea uamuzi hapo baadae.

  0 0

  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya
  Taifa ya Uchaguzi (NEC)
  Bw. Kailima Ramadhani
  Na Margareth Chambiri – Dar es salaam.

  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani amesema jambo kubwa ambalo watanzania wanapaswa kujifunza kutokana na Uchaguzi wa Marekani uliomalizika hivi karibuni ni kwa wananchi kuheshimi mifumo ya Uchaguzi.

   Mkurugenzi Kailima ametoa kauli hiyo ikiwa ni tathimi yake kuhusu uchaguzi huo wa Marekani na namna ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakihoji kuhusu ucheleweshaji wa kutangaza matokeo ya uchaguzi unaofanywa na Tume ikilinganishwa na ilivyofanyika nchini Marekani.

  Akizungumza mwishoni mwa wiki katika kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa na Kituo cha Redio cha Clouds FM, Kailima amesema siyo sahihi kulinganisha uchaguzi wa Marekani na Tanzania, akitolea mfano sekta ya mawasiliano ambayo ni muhimu katika kusafirisha vifaa na taarifa mbalimbali za uchaguzi inavyokabiliwa na changamoto.

  Amesema watanzania na hasa Wapiga kura wengi wanaishi maeneo ya vijijini ambayo baadhi yake hayafikiki kwa urahisi na kwamba haiwezekani Tume ikatangaza matokeo bila kuhakikisha kuwa kila kura imehesabiwa ikiwemo ya yule mwananchi wa kijijini.

  Amebainisha kuwa yapo mambo ya msingi ambayo watanzania wanapaswa kujifunza kutokana na Uchaguzi wa Marekani, kubwa ikiwa ni hatua ya kuheshimu mifumo ya Uchaguzi sambamba na Mamlaka zinazosimamia chaguzi hizo.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0

   Hivi ni baadhi ya picha za muonekekano wa sehemu ya vikwangua anga vinavyolipendezesha Jiji la Dar es salaam kutokea upende wa Baharini.


  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Eda Sanga (katikati) na msomaji wa taarifa ya pamoja ya Mtandao wa wadau kutoka asasi za kiraia unaotetea marekebisho ya sheria na sera ihusuyo usalama barabarani Tanzania akizungumza katika Siku ya Kimataifa Kuwakumbuka Wahanga wa Ajali za Barabarani inayoadhimishwa kila Novemba 20, 2016. Kulia ni Jones John kutoka Taasisi ya Jukwaa la Haki za Watoto Tanzania na Mwakilishi kutoka TAWLA, Nasieku Kisamby (kushoto). Taasisi ya Jukwaa la Haki za Watoto Tanzania, Jones John (katikati) akizungumza katika Siku ya Kimataifa Kuwakumbuka Wahanga wa Ajali za Barabarani inayoadhimishwa kila Novemba 20, 2016 iliyofanyika Ofisi za TAMWA jijini Dar es Salaam. Kulia ni Bi. Gladness Munuo kutoka TAMWA.

  MTANDAO WA WADAU KUTOKA ASASI ZA KIRAIA UNAOTETEA MAREKEBISHO YA SHERIA NA SERA IHUSUYO USALAMA BARABARANI TANZANIA. SIKU YA KIMATAIFA KUWAKUMBUKA WAHANGA WA AJALI ZA BARABARANI 20 NOVEMBA, 2016.

  Matukio ya ajali za barabarani yamekuwa na athari nyingi hapa nchini kiuchumi na kijamii. Vilevile matukio haya ya ajali za barabarani yamekuwa yakiwasababishia wananchi madhara makubwa yakiwemo kupoteza maisha, majeraha makubwa, ulemavu wa kudumu, mali kuharibika ikiwa ni pamoja na kuacha familia nyingi zikiwa tegemezi baada ya kuondokewa na watu wanaowategemea.

  Takwimu zinaonyesha kuwa takribani watu milioni 1.24 duniani hufariki kila mwaka kutokana na ajali za barabarani, aidha, watu milioni 20 mpaka 50 hupata ulemavu. (Hii ni kutokana na takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO). Kadhalika sehemu kubwa ya vifo na madhara ya ajali hizi zimetokea Kusini mwa Jangwa la Sahara , Tanzania ikiwa moja ya nchi hizo. 


  0 0  Meneja Mawasiliano wa Barclays Tanzania, Hellen Siria, akihojiwa na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari, wakati wa uzinduzi rasmi wa maabara ya kompyuta inayotembea itakayohudumia shule nne za sekondari katika wilaya hiyo. Mradi wa kompyuta unawezeshwa kwa kushirikiana na asasi ya PEN Tanzania. Hafla hiyo ilifanyika katika Shule ya Sekondari Kijitonyama, Dar es Salaam .
  Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Barclays Tanzania, Aron Luhanga (wa tatu kulia), Meneja Teknolojia wa benki hiyo, Dakshit Pandya (katikati mwenye miwani), na Mkurugenzi wa asasi ya PEN Tanzania, Sharnel Deo (wa nne kulia), wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa maabara ya kompyuta inayotembea itakayohudumia shule nne za sekondari katika wilaya hiyo. Mradi wa kompyuta unawezeshwa kwa kushirikiana na asasi ya PEN Tanzania. Hafla hiyo ilifanyika katika Shule ya Sekondari Kijitonyama, Dar es Salaam .
  Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Barclays Tanzania, Aron Luhanga (wa pili kulia) akikabidhi pedi za kike kwa baadhi ya wanafunzi wa shule za sekondari za Wilaya ya Kinondoni mara baada ya uzinduzi wa maabara ya kompyuta inayotembea itakayohudumia shule nne za sekondari katika wilaya hiyo. Mradi wa kompyuta unawezeshwa kwa kushirikiana na asasi ya PEN Tanzania. Hafla hiyo ilifanyika katika Shule ya Sekondari Kijitonyama, Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Teknolojia wa benki hiyo, Dakshit Pandya.
  Ofisa Masoko wa Benki ya Barclays, Nasikiwa Berya (wa tano kushoto), akitoa maelekezo kwa baadhi ya wanafunzi waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa maabara ya kompyuta inayotembea itakayohudumia shule nne za sekondari katika wilaya ya Kinondoni. Mradi wa kompyuta unawezeshwa kwa kushirikiana na asasi ya PEN Tanzania. Hafla hiyo ilifanyika katika Shule ya Sekondari Kijitonyama, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wengine kutoka kushoto ni Meneja Mawasiliano wa PEN Tanzania, Nancy Kataraihya, Meneja Mawasliano wa Barclays, Hellen Siria na Meneja Teknolojia wa benki hiyo, Dakshit Pandya. 


  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Eda Sanga na msomaji wa taarifa ya pamoja ya Mtandao wa wadau kutoka asasi za kiraia unaotetea marekebisho ya sheria na sera ihusuyo usalama barabarani Tanzania akizungumza katika Siku ya Kimataifa Kuwakumbuka Wahanga wa Ajali za Barabarani inayoadhimishwa kila Novemba 20, 2016Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Eda Sanga (katikati) na msomaji wa taarifa ya pamoja ya Mtandao wa wadau kutoka asasi za kiraia unaotetea marekebisho ya sheria na sera ihusuyo usalama barabarani Tanzania akizungumza katika Siku ya Kimataifa Kuwakumbuka Wahanga wa Ajali za Barabarani inayoadhimishwa kila Novemba 20, 2016. Kulia ni Jones John kutoka Taasisi ya Jukwaa la Haki za Watoto Tanzania na Mwakilishi kutoka TAWLA, Nasieku Kisamby (kushoto).Taasisi ya Jukwaa la Haki za Watoto Tanzania, Jones John (katikati) akizungumza katika Siku ya Kimataifa Kuwakumbuka Wahanga wa Ajali za Barabarani inayoadhimishwa kila Novemba 20, 2016 iliyofanyika Ofisi za TAMWA jijini Dar es Salaam. Kulia ni Bi. Gladness Munuo kutoka TAMWA 
  Mkutano kati ya wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari pamoja ya Mtandao wa wadau kutoka asasi za kiraia unaotetea marekebisho ya sheria na sera ihusuyo ukiendelea.


  0 0

  Imeelezwa kuwa uchumi wa wananchi wa Mikoa ya Njombe, Mbeya na Ruvuma utaimarika kwa kasi kama watatumia vizuri fursa ya uwepo wa meli za mizigo na abiria katika ziwa Nyasa.   Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani amesema kukamilika kwa meli mbili za mizigo za Mv. Njombe na Mv. Ruvuma na ujenzi wa meli ya abiria ya Mv. Mbeya ni fursa mpya ya kiuchumi kwa wakazi wa mikoa hiyo. 

  “Tumejipanga kuhakikisha tunafungua ukanda huu wa nyanda za juu kusini kiuchumi hivyo ni jukumu la wananchi kuchangamkia fursa za kibiashara zinazoweza kusafirishwa ndani na nje ya nchi ili kukuza uchumi”.amesema Eng. Ngonyani. 

  Naibu Waziri Ngonyani ameelezea kuridhishwa kwake na hatua ya ujenzi wa meli za Mv.Njombe na Ruvuma ambao umefikia asilimia tisini na tisa na kusisitiza kuwa Serikali itaendelea kuwaamini makandarasi wazawa wanaofanya kazi kwa ubunifu, uadilifu na uaminifu ili kutoa fursa nyingi za ajira kwa watanzania. 

  Kaimu Meneja wa bandari ya Itungi na Kiwira Eng. Juma Kisavara amemhakikishia Naibu Waziri Ngonyani kuwa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) imejipanga kuhaikikisha bandari zote kumi na tano zilizopo katika ziwa Nyasa kwa upande wa Tanzania zinafufuliwa na kutumika kupakia na kushusha mizigi ikiwemo vifaa vya ujenzi, makaa ya mawe,mbolea na mazao ambayo yana soko ndani na nchi za jirani. 

  Eng. Kisavara amemhakishia Naibu wa Ujenzi kuwa tayari wametafuta soko la kutosha la kusafirisha mizigo hivyo kuiomba Serikali kuendelea na kasi ya ujenzi wa meli nyingine zitakazotumika katika ziwa Nyasa. 

  Zaidi ya shilingi bilioni 11 zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa Meli ya Mv.Ruvuma na Mv. Njombe zinazojengwa na kampuni ya Songoro Marine Transport ya hapa nchini na meli hizo zinatarajiwa kukabidhiwa kwa Serikali mwezi Januari mwakani. 

  Katika hatua nyingine Naibu Waziri Ngonyani amekagua ujenzi wa barabara ya Kikusya-Ipinda hadi Matema KM 34.6 wilayani Kyela inayojengwa kwa kiwango cha lami na kusisitiza kuwa Serikali italipa fedha kwa mkandarasi anayejenga barabara hiyo ili kuiwezesha kukamilika kwa muda uliopangwa. 

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. 

   Muonekano wa Meli za Mv. Njombe na Mv.Ruvuma ambazo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 99, meli hizo zipo katika hatua za majaribio kabla ya kuanza kutoa huduma.


   Mkurugenzi wa Kampuni ya Songoro Marine Transport Bw. Salehe Songoro akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (katikati) ripoti ya ukaguzi wa ujenzi wa meli mbili za mizigo katika bandari ya Itungi ziwa Nyasa.

   Kaimu Meneja  wa bandari ya Itungi na Kiwira Eng. Juma Kisavara (wa kwanza kushoto) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (katikati) kuhusu namna ya kuondoa mchanga katika kingo za ziwa Nyasa ili kuwezesha meli zinazotengenezwa kuingizwa katika maji kwa urahisi.


   Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akikagua mfumo wa uendeshaji wa Meli ya Mv. Njombe ambao ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 99.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Waziri wa Viwanda na biashara Mhesimiwa Charles Mwijage amewapongeza watengenezaji wa vifaa vya kuhifadhia maji kwa kuendelea kuyaunga mkono malengo ya serikali ya kuanzisha viwanda nchini. 

  Hayo aliyasema katika hafla ya kuitimisha kampeni ya miezi mitatu ya uza SIMTANK na ushinde na kutoa zawadi kwa mawakala wauzaji wa SIMTANK Bi. Fatina Said na Bw. Rama Jurijs ambao walijishia gari kila mmoja iliyofanyika jijini Dar es Salaam. 

  “Nawaomba SILAFRICA waendelee kuibua na kufikia masoko mapya na kutengeneza bidhaa zinazokidhi mahitaji ya wateja wao ikiwa ni pamoja na matumizi ya viwandani na majumbani” alisema Mh. Mwijage. 

  Viwanda vingi vitakavyoanzishwa nchini vitahitaji kwa kiasi kikubwa vifungashio vya bidhaa zake hivyo pamoja na SILAFRICA kuzalisha matangi ya kuhifadhia maji kuna fursa kubwa ya kiwanda hiki kutumia plastiki kuzalisha hivyo vifungashio. Pia Mh. Mwijage aliwataka mawakala wa SIMTANK kuhakikisha wakaazi wa vijijini wanafikiwa na huduma hii ya vifaa vya kutunzia maji vilivyobora ukilinganisha na vile vya asili yaani mitungi inayowezavunjika wakati wowote. 

  Pamoja na hayo waziri aliwaomba SIALFRICA kuanzisha mpango wa elimu ya kukusanya na kuhifadhi maji wakati wa mvua ili kuwaepusha wananchi na usumbufu wa kukosa maji kipindi cha kiangazi. 

  Mkurugenzi mkuu wa SILAFRICA TANZANIA LTD, Bw. Alpesh Patel alimuhakikishia waziri kuwa wako tayari kutoa elimu kwa wananchi juu ya uhifadhi wa maji na kusema kuwa kampeni ya mwaka huu imekuwa na vipengele saba vilivyoshindaniwa hii yote ni kuonyesha jinsi kampuni inavyowajali mawakala wake na wateje wake kwa ujumla. 
  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage wa pili kulia akimkabidhi funguo za gari mmiliki wa duka la vifaa vya ujenzi la FMJ, Fatima Said baada ya kuibuka mshindi wa mauzo ya bidhaa za tangi la maji aina ya Simtank, kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Simtank, Alpesh Patel na kulia ni mshindi mwengine wa shindano hilo Ramadhani Sakalani
  Mh. Mwijage akisalimiana na mshindi wa gari katika kampeni ya uza SIMTANK na ushinde Bw. Ramadhani Sakalani. Wakitazama kushoto ni Bw. Alpesh Patel na Bi. Fatina Said.
  Bw. Ramadhani Sakalani akionyesha ufunguo wa gari aliloshinda baada ya kukabidhiwa na Mh. waziri.
  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage wa nne kulia akifafanua jambo mara baada ya kukabidhi funguo za gari kwa mmiliki wa duka la vifaa vya ujenzi la FMJ, Fatima Said baada ya kuibuka mshindi wa mauzo ya bidhaa za tangi la maji aina ya Simtank.


  0 0

   Meya wa jiji la Arusha Kalisti Lazaro akizungumza katika Mahafali ya Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji  Arusha (AJTC) ,Kulia ni Mkurugenzi wa Mafunzo katika Chuo hicho Joseph Mayagila, kushoto ni Diwani wa kata ya Themi, Melans Kinabo. 
  Wahitimu wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji  Arusha (AJTC) wakirusha kofia juu ishara ya kuonyesha kutunukiwa vyeti vya Shahada na Stashahada. Picha na Mahmoud Ahmad, Arusha

  0 0


  The Bank of Tanzania will hold a two-day Conference of Financial Institutions from 24th to 25th November 2016, at the Arusha International Conference Centre (AICC), Arusha. The Conference will be officiated by Hon. Dr. Philip Mpango, Minister for Finance and Planning.

  The Conference of Financial Institutions is a forum created in 1980 under the auspices of the Bank of Tanzania for exchanging views and experiences on issues pertaining to the financial sector and the economy in general. The Conference is held biennially and brings together heads of financial institutions and other stakeholders. The theme for this years’ Conference is: “Harnessing Tanzania’s Geographical Advantage: The Role of the Financial Sector”.


  Eight thematic papers will be presented by experts from within and outside Tanzania.  The topics include:


  1)      Exploiting Geographical Advantage: Lessons from Emerging Market Economies.

  2)      The Challenges of Industrialization in Tanzania: A Comparative Perspective.

  3)      Pursuing Manufacturing-Based Export-Led Growth in Tanzania: Opportunities and Challenges.

  4)      Leveraging Transit Trade for Tanzania.

  5)      Accelerating Corridor Development for Rapid Economic Growth.

  6)      Extending Tanzania’s Financial Frontiers: The Role of Technology.

  7)      Extending Tanzania’s Financial Frontiers: Experience, Lessons and Way Forward.

  8)      Financial Development in Tanzania: Challenges for Industrial Development and Job Creation.  Public Relations and Protocol Department


  November 21, 2016


  0 0

  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Juma Assad.
  Soko la Mwanjelwa jijini Mbeya 


  Na JamiiMojaBlog,Mbeya 

  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesanu za serikali(CAG), anatarajia kuanza kufanya kazi ya ukaguzi maalum katika halmashauri ya Jiji la Mbeya baada ya kudaiwa kuwepo kwa viashiria vya ubadhilifu wa fedha zilizotumika kukamilisha ujenzi wa soko la Mwanjelwa.

  Awali, Agosti 9 mwaka huu, Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa akiwa katika ziara yake Mkoani Mbeya, alifanikiwa kutembelea mradi huo wa soko ambao inasemekana umetumia kiasi cha shilingi Bilioni 26, tofauti na matarajio ya serikali.

  Serikali, ilikuwa ikiamini mradi huo utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 16 lakini kutokana na utendaji kazi wa hovyo unaodaiwa kufanywa na baadhi ya watendaji tena kwa maslahi yao binafsi ulisababisha soko hilo kutumia kiasi cha shilingi bilioni 26.

  Hatua hiyo ndio iliyomfanya waziri Mkuu, kumuagiza Mkaguzi Mkuu wa Hsabu za serikali kwenda Mbeya na kufanya ukaguzi wa mradi huo ili kuondoa utata uliopo juu ya kiasi sahihi cha fedha kilichotumika kwenye mradi huo.
  Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya, David Mwashilindi 

  Akizungumzia hilo, Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya, David Mwashilindi amesema kuwa baada ya agizo la waziri mkuu kutolewa, halmashauri ilianza mchakato wa kumuita mkaguzi huyo ili kufika kufanya ukaguzi.

  Amesema, kinachofanyika sasa ni kamati ya fedha kuketi kwa ajili ya kupitisha matumizi hayo ya fedha na kazi kuanza kufanyika ikiwa na kutekeleza agizo la Waziri Mkuu. Amesema Kamati ya fedha inataraji kukaa November 22 mwaka huu, na kutoa maamuzi na kupitisha kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kutumika kwa kazi ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ya kufanya ukaguzi wa fedha katika soko la Mwanjelwa.

  Aidha, Meya huyo aliwaomba wafanya biashara wote ambao tayari waliingia mikataba na halmashauri ya Jiji, kuanza kuendesha biashara zao kama makubaliano ya mkataba yanavyoelekeza.Hata hivyo, aliongeza kuwa tayari halmashauri imeingia mkataba na wakala atakayendesha zoezi la kuwaondoa wafanyabiashara wote ambao wamekiuka makubaliano ya mkataba kwa kushindwa kuendesha biashara kwa kipindi husika.

  0 0


  Napenda kuutaarifu umma wa Watanzania kupitia kwenu waandishi wa habari kwamba ni jambo la ajabu na aibu kwa watu makini na wenye kuhitaji mabadiliko ya kweli Kuacha kuunga Mkono juhudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano chini Uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli bila kusahau utendaji makini wa Waziri Mkuu wake Mhe. Majaliwa Kasim Majaliwa (Mb) pamoja na mawaziri mbalimbali wameonesha kutaka kufuata mwenendo wa Rais Magufuli na Waziri Mkuu wake.

  Mimi Moses Joseph Machali niliyefanya sana siasa za Upinzani hapa nchini na niliyepiga kelele na kupinga siasa za kifisadi zilizoitawala nchi hii; niliyepinga pia ufisadi uliokuwa umeitawala serikali huko nyuma kwa nguvu na uwezo wangu wote nikishirikiana na wapinzani wenzangu, ninaamua kujiunga na watu wanaonesha dhamira safi ya kuiendeleza nchi yetu Tanzania. Watu wenye mwelekeo na dhamira ya kuijenga nchi yetu kwa maendeleo enedelevu ni jamii ya akina Magufuli, Kasim Majaliwa, nk.

  Mwaka mmoja wa Uongozi wa Rais Magufuli na baadhi ya wasaidizi wake kupitia hatua mbalimbali zilizochukuliwa dhidi ya ufisadi uliokuwa umeigubika nchi yetu, inatosha kabisa kwa mtu yeyote makini kufanya uamuzi wa kumuunga mkono au kutokumuunga mkono Rais Magufuli.

  Mimi nimechagua kumuunga Mkono Rais kwa vitendo, kwa sababu ninaposoma Rekodi yangu ya enzi nikiwa Mbunge (Hansard) na kabla ya kuwa mbunge ni kwamba nilipinga mnoo wizi na ufisadi wa kila aina; Nilipinga Matumizi ya fedha serikalini yasiyo ya lazima na yasiyo na tija kwa taifa (Rejeeni hotuba yangu ya Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi, nikiwa Waziri Kivuli wa wizara hiyo ya mwaka 2014/2015 na 2015/2016), vilevile bila kusahau hotuba zangu mbalimbali Bungeni na nje ya Bunge.

  Kwa kushirikiana na wapinzania wenzangu enzi hizo tulishauri na kupinga ufisadi wa kila aina, tuliitaka serikali kufanya mambo yenye tija kwa taifa na sasa kila mwenye macho anaona hatua zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya tano. Miradi kama ya Ujenzi wa Reli, Ununuzi wa ndege mbili na mipango ya kununua ndege zaidi kama namna ya kulifufua shirikia la ATCL ni mambo tuliyoyahitaji kuyaona wapinzani; sasa yanafanyika. Wale wenye dhamira ya dhati ya kuona nchi yetu ikipiga hatua, kamwe hatuwezi kubeza mambo hayo bali kuyaunga mkono.

  Wale tuliosema na kupiga kelele kwamba Serikali ni dhaifu ktk kuwachukulia hatua watu mbalimbali wenye dhamana serikalini walioonekana kufanya vibaya serikalini ktk nafasi zao, leo tunaona kumekuwepo na kasi nzuri ktk kuwachukulia hatua watu hao. Hata hivyo leo hii upinzani umepiteza mwelekeo kwa sababu unapingana na kile ulichokihubiri nchini.

  Agenda ya kupinga ufisadi siyo ya upinzani tena bali ya JPM na CCM yake au yao. Wapinzani wamegeuka kuwa watu wanaokataa yale waliyoyasimamia na kuyahubiri huko nyuma. Hakika huo siyo uungwana bali aina mpya ya ufisadi nchini na usaliti kwa agenda zao.

  Kama kweli sisi tumekuwa wapinzani na tulioonesha kupinga kwa nguvu zote ufisadi ulioiumiza nchi hii tulimaanisha yale tuliyoyahubiri na kuwaaminisha watu basi tunao wajibu wa kuacha tabia ya kuwa vigeugeu kwa mambo tuliyoyaamini na kuyahubiri. Kutofanya hivyo basi ni mwendelezo wa ufisadi kwa maslahi binafsi.


  0 0

   Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu, Mhe. Dkt. Abdallah Possi amezitaka Halmashauri zote nchini kutekeleza agizo la kuunda Kamati za Watu Wenye Ulemavu kuanzi ngazi ya Vijiji, Kata, Wilaya hadi Mkoa.

  Mhe. Possi ametoa maagizo hayo kwa nyakati tofauti wakati wa ziara yake katika mikoa ya Mwanza na Simiyu hivi karibuni ambapo alitembelea makazi ya watu wenye mahitaji maalum ya Bukumbi, Shule ya watu wenye mahitaji maalum ya Mitindo na kituo cha kulelea watoto wenye ualbino cha Lamadi.


  Kauli ya Dkt. Possi imekuja kufuatia maagizo yaliyolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu mwezi Machi mwaka huu kwa kuziandikia Halmashauri zote kutekeleza uundwaji wa kamati za Watu wenye Ulemavu ikiwa ni sehemu ya kutatua changamoto wanazokabiliana nazo.


  “Ni muhimu sana kutekeleza agizo lililotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu mwanzoni mwa mwaka huu ambalo limeeleza wazi kuundwa kwa Kamati za Watu wenye Ulemavu na ikumbukwe kuwa, suala hii lipo kisheria na lina miongozo yake katika utekelezaji wake”. Alisema Waziri Possi.


  Waziri Possi alisisitiza kuwa maagizo ya kuundwa kwa kamati za watu wenye ulemavu yalitolewa na Ofisi hiyo ili kusaidia upatikanaji sahihi wa taarifa za watu wenye ulemavu ili kupata namna bora ya kutatua changamoto zinazowakabili.


  “Ofisi ya Waziri Mkuu ilitoa agizo hilo ili kusaidia kujua mahitaji ya watu wenye ulemavu na kuwa na njia nzuri za utatuzi wa changamoto zao kwa kuzingatia takwimu sahihi zitakazo toa picha halisi ya hali zao katika nyanja zote.”Alisema Dkt.Possi


  Aliongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kutoa vipaumbele kwa watu wenye ulemavu na mahitaji maalum kwa kuwapa nafasi za ushiriki katika mipango yote ya maendeleo ikiwemo; elimu, huduma za afya na uchumi ikiwa ni sehemu ya kuwawezesha katika jamii.


  Nae Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe. Juma Sweda alimpongeza Mhe. Possi kwa juhudi za kuhakikisha sauti za watu wenye ulemavu zinasikika katika ngazi zote kwa kuudwa kwa kamati hizo zitazotatua na kutibu changamoto za watu wenye ulemavu.


  ”Nikupongeze Mhe. Waziri kwa kutembelea Wilaya yetu na kuona umuhimu wa kuweka msisitizo wa uundwaji wa Kamati hizi, nasi tunakuhaidi kulitekeleza hilo kama Ofisi yako ilivyoekeza ili kufikia malengo ya Serikali katika kuhakikisha Haki na Usawa unakuwepo kwa watu wote bila kujali hali zao”.Alisema Mhe.Sweda.


   Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi (wa kwanza kushoto) akizungumza jambo na Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe. Juma Sweda wakati wa ziara yake katika shule ya Mitindo yenye kuhudumia watu wenye mahitaji maalum Jijini Mwanza. 
    Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akizungumza jambo wakati wa ziara yake katika Shule ya wenye mahitaji maalumu ya Mitindo Wilayani Misungwi Mkoa wa Mwanza.
   Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akisalimiana na Mwalimu wa wasioona Bw. Mika Sholla wakati wa ziara yake katika shule ya Mitindo Wilayani Misungwi Mwanza. 
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akizungumza na baadhi ya Watendaji wa Serikali katika Ofisi ya Kituo cha Kulelea Watu wenye mahitaji maalum cha Bukumbi Wilayani Misungwi mkoa wa Mwanza wakati ya ziara yake.

  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi (katikati mwenye miwani) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Mitindo pamoja na baadhi ya Watendaji wa Serikali wakati wa ziara yake shuleni hapo Jijini Mwanza. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU).

older | 1 | .... | 1436 | 1437 | (Page 1438) | 1439 | 1440 | .... | 3285 | newer