Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

BAYPORT TANZANIA YAADHIMISHA MIAKA 10 TANGU KUANZISHWA KWAKE NCHINI

$
0
0
Na Dotto Mwaibale

TAASISI ya Kifedha ya Bayport Tanzania juzi iliadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwake na kuelezea mafanikio makubwa iliyopata ndani ya kipindi hicho.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Hyatt Regency Hotel jijini Dar es Salaam juzi, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bayport Tanzania, John Mbaga alisema ndani ya miaka 10 wameweza kupiga hatua kubwa kwa kuwafikia wananchi wengi.

"Tumepiga hatua kubwa kwa kuwafikia wananchi wengi ambao wamenufaika na huduma zetu" alisema Mbaga.Alisema kupitia taasisi hiyo wananchi wameweza kuanzisha biashara na kujenga nyumba ikiwa ni pamoja na kusomesha watoto.

Mgeni rasmi wa hafla hiyo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki alisema Serikali inaipongeza taasisi hiyo kwa huduma za mikopo inayotoa kwa wananchi hivyo kusaidia kuinua pato la taifa na mtu mmoja mmoja.

"Changamoto kubwa iliyopo ambayo mnapaswa kuiangalia ni riba kubwa katika mikopo yenu jaribuni kuliangalia jambo hilo kwa karibu" alisema Kairuki.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki akihutubia katika hafla ya kutimiza miaka 10 ya Taasisi ya kifedha ya Bayport Tanzania iliyofanyika Hyatt Regency Hotel jijini Dar es Salaam juzi.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bayport Tanzania, John Mbaga akizungumza kwenye hafla hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki (kulia), Mjumbe wa Bodi ya Bayport Tanzania, Mama Anna Mkapa (katikati) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bayport Tanzania, John Mbaga, wakikata keki katika maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Bayport Tanzania yaliyofanyika Hyatt Regency Hotel Dar es Salaam juzi.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bayport Tanzania, John Mbaga (kushoto), akimlisha keki Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi.


AZAM FC KUSUKA KIKOSI CHA NGUVU RAUNDI YA PILI

$
0
0


UONGOZI wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, kwa kushirikiana na benchi la ufundi la timu hiyo hivi sasa upo kwenye mchakato wa kukiongezea nguvu kikosi hicho.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni nia ya dhati kabisa ya Azam FC kutaka kufanya vizuri zaidi kwenye mzunguko wa pili wa ligi, Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) na michuano ya Kimataifa inayokuja kuanzia mwezi ujao na mwakani (Kombe la Kagame na lile la Shirikisho Afrika).


Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli aruhusiwa hospitali awashukuru madaktari

$
0
0


Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli aliyekuwa amelazwa katika wodi ya Sewahaji ya Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam ameruhusiwa na kurejea nyumbani leo tarehe 11 Novemba, 2016 baada ya afya yake kuimarika.

Kabla ya kuondoka katika wodi ya Sewahaji alikokuwa amelazwa Mama Janeth Magufuli amewashukuru Madaktari na Wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu mazuri aliyoyapata na pia amewashukuru Watanzania wote kwa kumuombea afya njema.

"Namshukuru sana Mungu kwamba afya yangu imeimarika, pia napenda kuwashukuru Madaktari na Wauguzi, nimepata huduma nzuri sana maana siku nilipoletwa hapa nilikuwa sina fahamu na hali yangu ilikuwa mbaya lakini mmenipigania na leo narudi nyumbani nikiwa na afya imara.

"Naomba pia niwashukuru Watanzania wote kwa kuniombea, nawahakikishie kuwa sasa nipo vizuri na madaktari wameniruhusu nirudi nyumbani ambako nitamalizia matibabu yangu" amesema Mama Janeth Magufuli. 

Mama Janeth Magufuli alilazwa hospitalini hapo tangu Juzi tarehe 09 Novemba, 2016 baada ya kuugua ghafla na kupoteza fahamu.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam


11 Novemba, 2016

 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa anatoka kwenye  Wodi ya Sewahaji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kurejea nyumbani  mara baada ya kuruhusiwa baada ya kupata nafuu. Mama Janeth Magufuli alikuwa amelazwa hospitalini hapo tangu tarehe 9 Novemba 2016.

 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimshukuru Dkt. Raymond Mwenesano, Mkuu wa Idara ya Wagonjwa wa nje na Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili mara baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini hapo na kurejea nyumbani baada ya kupata nafuu.
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimshukuru Dkt. Edward Ngwalle, Daktari wa Rais mara baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini hapo na kurejea nyumbani baada ya kupata nafuu.






Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimshukuru Dkt. Benard Kepha ambaye Daktari Bingwa wa Magonjwa ya dharura na ajali katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili mara baada ya kuruhusiwa kutoka na kurejea nyumbani mara baada ya kupata nafuu. Picha na IKULU

Eatv watangaza makundi mengine matatu yatakayo wania tuzo 2016

$
0
0


Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

KITUO cha televisheni cha Eatv leo kimetangaza makundi mapya matatu yatakayoshindaniwa katika tuzo za Eatv Awards zinazotaraji kufanyika Desemba 10 mwaka huu.

Makundi hayo ambayo yametangazwa leo mapema jijini Dar es Salaam na Meneja masoko wa kampuni hiyo Roy Mbowe katika mkutano wa waandishi wa habari na waandaaji wa tuzo hiyo katika hoteli ya Sleepway .

“tuzo hizi zenye vipenfgele 10 ambazo dhamira yake ni kuwatunza wanamuziki na wasanii wa filamu zilianza kwa kuwaomba wasanii wajipendekeze wenyewe kwa kujaza fomu maalum za kuwania tuzo ambapo wanaotajwa leo ndio waliofuta utaratibu kupitia mchujo wa awali”amesema Roy.
Amesema kuwa makundi yaliyotanjwa leo ni wimbo bora wa mwaka ambapo wanaoshindania ni , John Makini na wimbo wa Don’t Bother ,Lady Jaydee na wimbo wake wa Ndindindi, Navy Kenzo na wimbo wa wao wa kamatia chini, Ali Kiba na wimbo wake wa Aje na Ben Paul ambae ameingia na wimbo wa Moyo Mashine.Kundi la pili ni mwanamuziki bora wa kiume ambapo wanaoshindania George Sixtius  (G nako )na wimbo wa Arosto, Nurdin Billal(Shettah) na wimbo wa Namjua, Beanard Paul(Ben Paul) na wimbo wa Moyo Mashine, Hamis Mwijuma (Mwana Fa) na wimbo wa asanteni kwa kuja na wa mwisho ni Ally Kiba na wimbo wake wa Aje.

Alimaliza kwa kutaja kundi la mwisho litakalo shindaniwa kuwa ni mwanamuziki bora wa kike ambapo wanaotajwa kuwania tuzo hiyo ni Lilian Mbabazi na wimbo wa Yoola,Ruby na wimbo wa Forever sijuti, Linah Sanga na wimbo wa No Stress, Vannesa Mdee na wimbo wa Never Ever na lady Jaydee na wimbo wake wa Ndindindi.

Kwa upande wake katibu mkuu wa baraza la sanaa nchini Tanzania (BASATA), Godfrey Mwingereza, amesema kuwa tuzo hizo zimefata vigezo vyote kwa kuwa wasanii wote ambao wameshiriki katika tuzo hizo wamesajiliwa na basata hivyo wale wote waliojipendekeza lakini awakusajiliwa walikuwa wanajiondoa wenyewe kwenye mashindano kwa kukosa sifa.
Meneja masoko wa Kituo cha televisheni cha EATV, Roy Mbowe akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, wakati wa kutangaza makundi mapya matatu yatakayoshindaniwa katika tuzo za Eatv (EatvAwards) zinazotaraji kufanyika Desemba 10 mwaka huu.

YANGA YAONGOZA MAPATO TIKETI ZA ELECTRONIKI

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

KLABU ya soka ya Dar es Salaam Young Africa (Yanga) imeongoza kwa kuingiza fedha nyingi kwa kupitia mapato ya mlangoni tangu kuanza kutumika kwa mfumo wa tiketi za kielectronic.

Hayo yamesemwa leo na Meneja Masoko wa Selcom nchini, Juma Mgori alipokuwa katika mahojiano maalum na Globu ya jamii jijini Dar es Salaam.

Mgori amesema kuwa licha ya kuwepo kwa changamoto ya uelewa wa kutumia kadi hizo kwa mashabiki mpaka sasa Yanga ndio klabu inayoongoza kuingiza fedha nyingi ikifuatiwa na klabu ya Simba.

“mfumo huu umeweza kuzinufaisha sana timu hizi kwa namna moja au nyingine kwani zimeweza kuingiza fedha moja kwa moja kwenye akaunti zao bila ya kuwepo na utata wowote huku timu kama Toto Afrika ya Mwanza ikiwa imenufaika maradufu kwa kupata kiasi cha shilingi milioni tisa katika mechi moja tofauti na mechi za nyuma kabla ya mfumo wa electroniki ulivyoanza kutumika” amesema Mgori.

Mgori ameongeza kuwa ni muda sasa wa shirikisho la soko nchini TFF na Vilabu vya soka nchini kuanza kutoa elimu ya kutosha juu ya matumizi ya kadi hizo hili waweze kujiongezea kipato katika michezo mbalimbali itakayochezwa nchini.

Amesema wapo viongozi wakubwa tu wa vilabu vya soka hapa nchini ambao wamewapigia simu kwa jinsi gani walivyoweza kunufaika na mpango huu wa tiketi za electroniki.

TAASISI YA HASSAN MAAJAR KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA ELIMU NCHINI

$
0
0
Taasisi ya Hassan Maajar (HMT) ambayo hivi karibuni ilitimiza miaka 5 imeendelea na juhudi zake za kuboresha mazingira ya elimu hapa nchini. Katika kipindi cha miaka mitano, taasisi hiyo imefanya kazi kwa kushirikiana na Bank M kama Mdhamini Mkuu hasa katika mradi wa HMT uitwao “Dawati kwa Kila Mtoto”.

Mwaka huu, Hassan Maajar Trust kwa kushirikiana na Bank M wanaandaa hafla ya kuchangisha fedha itakayofanyika tarehe 25 Novemba 2016 katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam. Mgeni rasmi katika hafla hiyo atakuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Kassim Majiliwa.

Akiongea na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchangishaji Fedha ya taasisi hiyo, Bw, Daniel Mwasandube alisema kuwa Hassan Maajar Trust wanafurahi  kushirikiana tena na Bank M na kuongeza kuwa ushirikiano wanaoupata kutoka Bank M tangu kuanzishwa kwa Taasisi yao mwaka 2011 umechangia kwa kiasi kikubwa sana kufanikisha miradi wanayoitekeleza.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchangishaji Fedha ya taasisi ya Hassan Maajar, Bw, Daniel Mwasandube akiongea na wanahabari jana jijini kuhusiana na hafla ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ununuzi wa madawati iliyoandaliwa na taasisi hiyo kwa kushirikiana na Benki M itakayofanyika 05th November 2016 hapa Dar es salaam. Kushoto ni Ofisa wa program wa taasisi hiyo Bi. Kaymarie Bukila.

“Tumetimiza miaka mitano hivi karibuni, hadi sasa HMT imeweza kutoa madawati 9,000 ambayo yamenufaisha zaidi ya wanafunzi 30,000 katika mikoa 13 hapa nchini. Mikoa hiyo ni Rukwa, Njombe, Singida Mwanza, Pwani, Shinyanga, Kigoma, Lindi, Mbeya, Iringa, Mtwara, Dar es Salaam, and Kilimanjaro.”

Taasisi yetu inatambua adha inayowakabili wanafunzi wanapojifunza kusoma na kuandika wakiwa wameketi sakafuni. Aidha HMT imefanikiwa kuhamasisha umma nchini Tanzania na kwingine kuunga mkono jitihada zetu katika kutatua tatizo la upungufu wa madawati nchini chini ya kauli mbiu; “Dawati kwa Kila Mtoto”. 

Tunawashukuru sana wadhamini wetu wote” alisema Mwenyekiti huyo na kuongeza kuwa uamuzi wa Bank M kushirikiana na HMT umeonesha jinsi benki hiyo inavyojali kukuza maendeleo ya elimu hapa nchini. Serikali pia imeonesha kutambua jitihada hizi zinazofanywa na taasisi yetu kwa kushiriana na Bank M”, alisema Mwasandube.
Mojawapo ya hafla za makabidhiano ya madawati yaliyotolewa na taasisi ya Hassan Maajar kwa kushirikiana na Benki M iliyofanyika katika mkoa wa kigoma mwaka jana. Taasisi ya Hassan Maajar imeweza kutoa madawati 9,000 ambayo yamenufaisha zaidi ya wanafunzi 30,000 katika mikoa 13 hapa nchini. Mikoa hiyo ni Rukwa, Njombe, Singida Mwanza, Pwani, Shinyanga, Kigoma, Lindi, Mbeya, Iringa, Mtwara, Dar es Salaam, na Kilimanjaro.

Mwasandube pia alieleza kuwa kupitia fedha zitakazochangishwa kwenye hafla ya mwaka huu, HMT itaendelea na mradi wa madawati kwa kuwa upungufu wa madawati umeongezeka licha ya jitihada za Serikali kwa kuwa idadi ya wanafunzi nayo imeongezeka. Hata hivyo, HMT itaangalia zaidi samani na vifaa kwa ajili shule kwa Wanafunzi wenye mahitaji maalum pamoja na Waalimu. Kubwa zaidi, HMT itawasha mshumaa kuangazia tatizo sugu la uhaba wa huduma ya vyoo  katika shule.

Kwa kuongezea, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Dk. Yusuph Sinare, alielezea jinsi walivyoridhishwa na hali ya uchangiaji kupitia kampeni mbalimbali zinazofanywa na HMT, na kwamba hadi kufikia mwezi Juni mwaka huu, wamefanikiwa kuchangisha Shilingi za Kitanzania Bilioni 1.7 fedha taslimu na Shilingi za Kitanzania Milioni 140 ikiwa ni michango mali.

Hivi karibuni, Afisa Mtendaji Mkuu (Mtarajiwa) wa Bank M, Bi Jacqueline Woiso, alisema kuwa Benki yao inajivunia kushirikiana na Taasisi ya Hassan Maajar Trust katika mpango huu na aliipongeza taasisi hiyo kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa miaka 5 hadi sasa. “Kuwezesha wanafunzi zaidi ya 30,000 kukaa kwenye madawati ndani ya miaka 5 ni mafanikio ambayo tunayatambua na yanaashiria juhudi endelevu”.

TANZANIA YAANDAA KONGAMANO LA UWEKEZAJI BAINA YAKE NA UBELGIJI

MAGARI MANNE YAGONGANA KONGOWE TEMEKE JIJINI DAR LEO MCHANA, WATU KADHAA WAJERUHIWA

$
0
0
 Wananchi wakiangalia ajali iliyohusisha magari manne na pikipiki iliyotokea daraja la Mzinga Kongowe, Temeke jijini Dar es Salaam leo mchana. Katika ajali hiyo watu kadhaa walijeruhiwa.

Na  Dotto Mwaibale

WATU kadhaa wamejeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha magari manne na pikipiki iliyotokea daraja la Mzinga Kongowe Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Ajali hiyo ilitokea saa sita mchana na kuhusisha magari hayo lori la mafuta aina ya Scania lenye namba T 617 AQQ, Coster ya abiria namba T 415 DCC inayofanya safari zake kati ya Kilwa Masoko na Mbagala, Prado yenye namba  T 177 AHH, pikipiki na lori jingine. 

Ofisa wa Polisi aliyekuwepo eneo la ajali ambaye alitambulika kwa jina moja la Emanuel alisema chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika.

"Nimefika sasa hivi bado hatujajua chanzo cha ajali wala watu waliopoteza maisha na kujeruhiwa" alisema ofisa huyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Gilles Muroto alipopigiwa simu ili kuthibitisha ajali hiyo alikiri kutokea  hata hivyo alisema alikuwa hajapata taarifa kamili kutoka kwa Mkuu wa Kikosi cha Usalama wa Wilaya hiyo ambaye alikuwepo eneo la tukio.

Kwa mujibu wa mashuhuda walioshuhudia ajali hiyo walisema majeruhi walikimbizwa Hospitali ya Manispaa ya Temeke kwa matibabu.
 Wananchi wakiangali basi dogo aina ya Coster ya abiria namba T 415 DCC ikiwa imeharibika vibaya baada ya kugongwa.
 Wananchi wakiwa eneo la ajali.
 Ofisa wa Jeshi la Polisi akiwa eneo la ajali akichukua taarifa.
Prado yenye namba  T 177 AHH iliyohusika katika ajali hiyo.

MAREHEMU SAMWEL JOHN SITTA AAGWA KWA HESHIMA ZOTE BUNGENI

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai pamoja na viongozi wengine wakiusubiri mwili wa Spika mstaafu, Samuel Sitta uteremshwe kwenye ndege ya ATC katika uwanja wa ndege wa Dodoma Novemba 11, 2016.
 Mwili wa Spika Mstaafu Samuel Sitta ukiteremshwa kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Novemba 11, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika kikao maalum cha bunge cha kumuenzi Spika Mstaafu, Samuel Sitta, bungeni mjini Dodoma Novemba 11, 2016. 
 Waziri Mkuu Mstaafu, Samuel Malecela akimpa pole mjane wa Spika Mstaafu, Margareth Sitta bungeni mjini Dodoma Novemba 11, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa Spika Mstaafu, Samuel Sitta, bungeni mjini Dodoma, Novemba 11, 2016.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA




RPC KINONDONI AWAASA WANAFUNZI VYUO VIKUU KUEPUKA MIGOMO NA MAANDAMANO YASIYO NA TIJA

TTCL yapeleka intaneti bure Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)

$
0
0
    KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) leo imefunga huduma za mawasiliano ya intaneti bure katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) itakayowawezesha madaktari, wafanyakazi wengine, wagonjwa pamoja na wananchi wanaofika katika kituo hicho kupata huduma ya mawasiliano ya intaneti bure yenye kasi ya hali ya juu. 

 Akikabidhi huduma hiyo, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Wazir W. Kindamba alisema kampuni hiyo imetumia jumla ya shilingi milioni 120 kufunga huduma bure ya intaneti katika kituo hicho na itatolewa kwa muda wa mwaka mmoja ikiwa ni kuiwezesha taasisi hiyo kuendesha shughuli zake kwa ufanisi.

 Akifafanua zaidi Bw. Kindamba alisema huduma hiyo ambayo itagharimu shilingi milioni 10 kwa kila mwezi ambazo zitakuwa zikilipwa na TTCL ikiwa ni mchango wake kwa jamii na hasa kwa matibabu yanayofanyika katika kituo hicho itakuwa ikitolewa kwa teknolojia ya Wi-Fi bure kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Novemba 10, 2016 hadi Novemba 10, 2017.

 "Kwa kuzingatia umuhimu wa sekta ya afya na kazi kubwa inayofanywa na Taasisi hii, TTCL tumetoa intaneti yenye kasi hadi kufikia spidi ya 100Mbps, spidi hii itasaidia kuongeza uwajibikaji katika kutoa huduma kwa wananchi, kuimarisha mawasiliano miongoni watumishi wa JKCI na nje ya Taasisi, kupashana habari za kitabibu na kubadilishana taarifa za kitabibu miongoni mwa wataalamu kutoka hospitali za ndani na hospital za nje ya mipaka ya Tanzania," alisema Kindamba. 
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Wazir W. Kindamba (kulia) akimkabidhi kibao cha kuashiria huduma bure ya intaneti ya teknolojia ya Wi-Fi kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi (kushoto) leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya Kampuni ya TTCL kukabidhi huduma hiyo. Huduma hiyo ina itakayotolewa kwa mwaka mmoja inagharimu shilingi milioni 120.Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Wazir W. Kindamba (kulia) akimkabidhi kibao cha kuashiria huduma bure ya intaneti ya teknolojia ya Wi-Fi kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo  ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi (kushoto) leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya Kampuni ya TTCL kukabidhi huduma hiyo. Huduma hiyo ina itakayotolewa kwa mwaka mmoja inagharimu shilingi milioni 120.Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Wazir W. Kindamba (kulia) akimkabidhi kibao cha kuashiria huduma bure ya intaneti ya teknolojia ya Wi-Fi kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi (kushoto) leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya Kampuni ya TTCL kukabidhi huduma hiyo. Huduma hiyo ina itakayotolewa kwa mwaka mmoja inagharimu shilingi milioni 120.Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Wazir W. Kindamba (kulia) akimkabidhi kibao cha kuashiria huduma bure ya intaneti ya teknolojia ya Wi-Fi kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo  ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi (kushoto) leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya Kampuni ya TTCL kukabidhi huduma hiyo. Huduma hiyo ina itakayotolewa kwa mwaka mmoja inagharimu shilingi milioni 120.Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi akizungumza katika hafla ya Kampuni ya TTCL kukabidhi huduma ya bure ya intaneti ya teknolojia ya Wi-Fi kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Huduma hiyo itakayotolewa kwa mwaka mmoja inagharimu shilingi milioni 120.Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi akizungumza katika hafla ya Kampuni ya TTCL kukabidhi huduma ya bure ya intaneti ya teknolojia ya Wi-Fi kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Huduma hiyo itakayotolewa kwa mwaka mmoja inagharimu shilingi milioni 120.Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Wazir W. Kindamba (kulia) akizungumza katika hafla ya kampuni ya TTCL kukabidhi huduma bure ya intaneti ya teknolojia ya Wi-Fi kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi akifuatilia.   Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Wazir W. Kindamba (kulia) akizungumza katika hafla ya kampuni ya TTCL kukabidhi huduma bure ya intaneti ya teknolojia ya Wi-Fi kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi akifuatilia. 
Picha ya pamoja mara baada ya zoezi la makabiadhiano. Picha ya pamoja mara baada ya zoezi la makabiadhiano.

VIJANA WAKITANZANIA WAASWA KUTUMIA MAWAZO YAO KUJIKWAMUA KIUCHUMI

$
0
0

Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii

YALI Regional Leadership Centre ya Nchini imedhamiria kutoa elimu ya ujasiriamali kwa vijana Tanzania Bara na Visiwani kwa kumualika moja ya waandamizi wa masuala ya ujasiriamali kutoka nchini Jordan Laith Al Qassam ili kutoa mafunzo mbalimbali kwa kuhakikisha wanapata nafasi za kujiajiri na kuongeza pato la taifa.

Akizugumza kabla ya kuanza semina hiyo,Muàndaaji wa Semina hiyo Fabian Shayo amesema kuwa mafunzo hayo yajulikanayo kama Blue Ocean Strategy yatahusisha zaidi masuala ya ujasiriamali hususani kwa vijana na mkufunzi Al Qassama ambaye amebobea katika masuala hayo atatoa elimu kwa vijana waliojitokeza.

Shayo amesema Blue Ocean Strategy imeweza kusaidia watu wengi hususani vijana katika masuala ya ujasiriamali na hata kuanzisha makampuni duniani kote pia imeweza kutengeneza soko la kibiashafa na kukuza faida.

Mkufunzi wa mafunzo hayo, Al Qassama ambaye ni mmoja ya waandamizi wa kiwanda cha Jordan ICT na kukiwezesha kuwa moja ya makampuni makubwa duniani amesena kuwa vijana wengi wanaamini kuwa fedha ndiyo kila kitu na kushindwa kuelewa kuwa mawazo yanaweza kuwa msaada kwao.

Blue Ocean Strategy itaendeshwa katika vipindi vitatu tofauti kwa bara na visiwani kwa ajili ya kuwapatia elimu vijana kwa watakaoleta mabadiliko na maendeleo kwenye sekta ya ujasiriamali kupata fursa za ajira na kukuza kiwango cha maendeleo ya kiuchumi katika taifa.

Katika ukanda wa Afrika Mashariki, Vijana waliowahi kushiriki semina hiyo(Alumni) wametumia fursa hii kuwasaidia vijana wenzao ili kuweza kuangalia wanakwamuka vipi kiuchumi kwa kupitia njia ya ujasiriamali.
Mwenyekiti wa kamati ya uandaaji wa mafunzo hayo, Fabian Shayo akizungumza na waandishi wa habari juu ya mikakati yao ya kusaidia vijana kujikwamua kiuchumi kwa kutumia sera ya ujasiriamali. Kulia ni Mkufunzi Laith Al Qassam na kushoto ni Mwenyekiti wa kamati ya fedha Fortunatus Eklklesiah.
Mkufunzi Laith Al Qassam akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mafunzo hayo ya ujasiriamali kwa vijana na nini wanatakiwa kufanya ili kuondoa dhana ya kuajiriwa au kuamini fedha zinaweza kufanya kila kitu. Kulia ni Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano, Khalila Mbowe na kushoto ni Mwenyekiti wa kamati ya uandaaji wa mafunzo hayo, Fabian Shayo.
Mkufunzi wa Semina hiyo Laith Al Qassam akitoa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana waliojitokeza yaliyoendeshwa na YALI Regional Leadership Centre kwa ukanda wa Afrika Mashariki. 

Extended Services Limited latest offers

DKT SHEIN UZINDUA MAJENGO MAPYA YA WODI YA WATOTO NA KINAMAMA

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mwakilishi wa Ubalozi wa Norwaya Bw. Victor Mlundo wakati wa kuzindua majengo mapya ya Wodi ya Watoto Kinamama katika Hospitali ya Mnazi mmjoja uliofanyika leo .
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Chumba cha kulelea Watoto wachanga wakati alipotembelea majengo mapya ya Wodi ya Kinamama na Watoto katika Hospitali ya Mnazi Mmoja baada ya uzinduzi rasmi leo,(wa pili kulia) mwakilishi wa Ubalozi wa Uholanzi Teresia Mcha 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya Chuo Kikuu cha Hauklend Bw.Eivend Hansen wakikata utepe kuzindua jengo la Wodi ya Watoto wakati wa uzinduzi wa majengo mapya ya Wodi ya Kinamama na Watoto uliofanyika leo katika Hospitali ya Mnazi Mmoja.

DKT MGWATU AAHIDI KUTOA VITENDEA KAZI KWA TEMESA NJOMBE

$
0
0
Na Theresia Mwami TEMESA Njombe.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu ameahidi kuwapatia makasha yenye vitendea kazi vya karakana pamoja na mashine ya kucharge betri za magari kwa wafanyakazi wa kituo cha TEMESA Mkoani Njombe.

Dk Mgwatu amesema kuwa ameamua kuleta mabadiliko katika ufanyaji kazi kwa kuhakikisha wafanyakazi wanapata vitendea kazi kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

“Nitaleta vifaa vinavyohitajika nataka kila mmoja atimize wajibu wake, tufanye kazi kwa kuzingatia uadilifu sababu tunabeba dhamana kubwa ya kutengeneza magari ya viongozi mbali mbali wa serikali” alisema Dkt Mgwatu.

,Mtendani huyo ameongeza kuwa atokuwa na msamaha na mtumishi yeyote atakayeshindwa kuwa muadilifu na kutoimiza wajibu wake ipasavyo. Aidha Dkt Mgwatu aliwaagiza watumishi wa kituo hicho kufanya kazi kwa weledi na kwa ubora zaidi ili karakana iweze kuvuta wateja wengi zaidi na kuongeza pato la kituo.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa TEMESA Njombe Mhandisi John Rubaga alimueleza kuwa kituo kinakabiliwa na tatizo la madeni kinayodai wateja wake pamoja na madeni kinayodaiwa na wazabuni mbali mbali.

Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Musaa Mgwatu yupo katika ziara ya kikazi kutembelea vituo vya TEMESA vilivyopo nyanda za juu Kusini ili kubaini changamoto mbali mbali zilizo kwenye vituo hivyo na kuzitafutia ufumbuzi.



Watumishi wa TEMESA Njombe wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa  Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu (Mwenye shati la rangi ya bluu) alipotembelea kituoni hapo kujionea utendaji wa kazi wa kituo hicho. Picha zote na Theresia Mwami TEMESA Njombe.Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu (kushoto), akimsikiliza Meneja wa TEMESA Njombe Mhandisi John Rubaga (kulia) wakati alipotembelea kituoni hapo kujionea utendaji wa kazi wa kituo hicho. 


Rais Magufuli aongoza waombolezaji kumuaga Samuel Sitta, atuma rambirambi kifo cha Mbunge Hafidh Ali Tahir

$
0
0
 

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 11 Novemba, 2016 amewaongoza viongozi na wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kuuaga mwili wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samuel John Sitta aliyefariki dunia tarehe 07 Novemba, 2016 katika hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujerumani.
Mwili wa Marehemu Samuel John Sitta umeagwa katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam ambapo Viongozi wengine waliojumuika kuuaga mwili huo ni pamoja na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zubeir Ali Maulid, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Mawaziri wakuu wastaafu Jaji Joseph Sinde Warioba na Frederick Tluway Sumaye, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Jaji Kiongozi Mhe. Ferdinand Katipwa Wambali na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.
Baada ya kuagwa katika viwanja vya Karimjee, mwili wa Marehemu Samuel John Sitta umesafirishwa kwenda Dodoma ambako Wabunge, Viongozi wa Mkoa na wananchi watapata fursa ya kuuaga katika Viwanja vya Bunge na baadaye jioni utasafirishwa kwenda Tabora ambako maziko yatafanyika kesho Jumamosi huko Urambo.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai kufuatia kifo cha Mbunge wa Jimbo la Dimani Zanzibar Mhe. Hafidh Ali Tahir kilichotokea majira ya saa 9 usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.Mhe. Hafidh Ali Tahir amefariki dunia muda mfupi alipofikishwa hospitali baada ya kuugua ghafla.

"Nimeshtushwa sana na kifo cha Mhe. Hafidh Ali Tahir na ninakuomba Mhe. Spika Job Ndugai unifikishie salamu za pole kwa Familia ya Marehemu, Wabunge, Wananchi wa Jimbo la Dimani, Ndugu, Jamaa na Marafiki wote walioguswa na msiba huu.
"Tutamkumbuka Mhe. Hafidh Ali Tahir kwa mchango wake mkubwa alioutoa katika utumishi wa umma, katika michezo na akiwa mwakilishi wa wananchi, kwa hakika tumepoteza mtu muhimu sana" amesema Rais Magufuli na kumuombea Marehemu apumzishwe mahali pema peponi. Amina.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
11 Novemba, 2016


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli akitoa heshima zake za mwisho kwa aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa kiongozi huyo mkongwe katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam  leo Novemba 11, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli akimfariji Mama Margareth Sitta, Mjane wa aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa kiongozi huyo mkongwe katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam  leo Novemba 11, 2016.
 Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe Benjamin William Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa wakitoa heshima  za mwisho kwa aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa kiongozi huyo mkongwe katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam  leo Novemba 11, 2016
  Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa kiongozi huyo mkongwe katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam  leo Novemba 11, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli akimpa pole Mhe. John Sitta, mtoto wa  aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa kiongozi huyo mkongwe katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam  leo Novemba 11, 2016.

MKE WA RAIS MAMA JANETH MAGUFULI ARUHUSIWA KUTOKA KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI ALIPOKUWA AMELAZWA

$
0
0
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa anatoka kwenye  Wodi ya Sewahaji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kurejea nyumbani  mara baada ya kuruhusiwa baada ya kupata nafuu. Mama Janeth Magufuli alikuwa amelazwa hospitalini hapo tangu tarehe 9 Novemba 2016.
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimshukuru Dkt. Edward Ngwalle, Daktari wa Rais mara baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini hapo na kurejea nyumbani baada ya kupata nafuu.
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimshukuru Dkt. Benard Kepha ambaye Daktari Bingwa wa Magonjwa ya dharura na ajali katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili mara baada ya kuruhusiwa kutoka na kurejea nyumbani mara baada ya kupata nafuu.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimshukuru Dkt. Raymond Mwenesano, Mkuu wa Idara ya Wagonjwa wa nje na Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili mara baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini hapo na kurejea nyumbani baada ya kupata nafuu.
Picha na IKULU

Rais Magufuli aongoza waombolezaji kumuaga Samuel Sitta, atuma rambirambi kifo cha Mbunge Hafidh Ali Tahir

$
0
0
 

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 11 Novemba, 2016 amewaongoza viongozi na wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kuuaga mwili wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samuel John Sitta aliyefariki dunia tarehe 07 Novemba, 2016 katika hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujerumani.
Mwili wa Marehemu Samuel John Sitta umeagwa katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam ambapo Viongozi wengine waliojumuika kuuaga mwili huo ni pamoja na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zubeir Ali Maulid, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Mawaziri wakuu wastaafu Jaji Joseph Sinde Warioba na Frederick Tluway Sumaye, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Jaji Kiongozi Mhe. Ferdinand Katipwa Wambali na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.
Baada ya kuagwa katika viwanja vya Karimjee, mwili wa Marehemu Samuel John Sitta umesafirishwa kwenda Dodoma ambako Wabunge, Viongozi wa Mkoa na wananchi watapata fursa ya kuuaga katika Viwanja vya Bunge na baadaye jioni utasafirishwa kwenda Tabora ambako maziko yatafanyika kesho Jumamosi huko Urambo.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai kufuatia kifo cha Mbunge wa Jimbo la Dimani Zanzibar Mhe. Hafidh Ali Tahir kilichotokea majira ya saa 9 usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.Mhe. Hafidh Ali Tahir amefariki dunia muda mfupi alipofikishwa hospitali baada ya kuugua ghafla.

"Nimeshtushwa sana na kifo cha Mhe. Hafidh Ali Tahir na ninakuomba Mhe. Spika Job Ndugai unifikishie salamu za pole kwa Familia ya Marehemu, Wabunge, Wananchi wa Jimbo la Dimani, Ndugu, Jamaa na Marafiki wote walioguswa na msiba huu.
"Tutamkumbuka Mhe. Hafidh Ali Tahir kwa mchango wake mkubwa alioutoa katika utumishi wa umma, katika michezo na akiwa mwakilishi wa wananchi, kwa hakika tumepoteza mtu muhimu sana" amesema Rais Magufuli na kumuombea Marehemu apumzishwe mahali pema peponi. Amina.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
11 Novemba, 2016


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli akitoa heshima zake za mwisho kwa aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa kiongozi huyo mkongwe katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam  leo Novemba 11, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli akimfariji Mama Margareth Sitta, Mjane wa aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa kiongozi huyo mkongwe katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam  leo Novemba 11, 2016.
 Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe Benjamin William Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa wakitoa heshima  za mwisho kwa aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa kiongozi huyo mkongwe katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam  leo Novemba 11, 2016
  Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa kiongozi huyo mkongwe katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam  leo Novemba 11, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli akimpa pole Mhe. John Sitta, mtoto wa  aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa kiongozi huyo mkongwe katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam  leo Novemba 11, 2016.

WAZIRI MKUU AONGOZA MAMIA KUAGA MWILI WA MHE. SITTA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameongoza mamia ya wabunge, viongozi wa kitaifa na watumishi wa Ofisi ya Bunge kuuaga mwili wa Spika Mstaafu, Samwel Sitta.

Bw. Sitta alifariki dunia usiku wa kuamkia Novemba 7 katika hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujerumani.Akizungumza  wakati wa kuuaga mwili huo Bungeni mjini Dodoma leo (Ijumaa, Novemba 11, 2016), Waziri Mkuu ametoa pole kwa Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai, mke wa marehemu Mheshimiwa Magreth Sitta, mama wa marehemu Hajat Zuena Fundikila na familia ya marehemu na wabunge wote.

“Nitumie fursa hii pia kukupa pole Mheshimiwa Spika kwa pigo ambalo Bunge lako tukufu imelipata kwa kumpoteza mmoja wa viongozi mahiri wa Bunge hili katika historia ya nchi yetu. Msiba uliotupata wa Spika Mstaafu wa Bunge la Tisa (2005-2010) na Mbunge Mstaafu wa jimbo la Urambo mkoani Tabora ni mzito.”

Amesema Bw. Sitta alikuwa mtu muhimu aliyetoa mchango mkubwa katika uongozi na maendeleo.  “Serikali imepokea taarifa za msiba huu kwa mshtuko mkubwa. Historia ya Mzee Sitta ni pana sana. Tunatambua utumishi uliotukuka katika nyadhifa mbalimbali alizozitumikia. Tutamkumbuka kwa utumishi wake,” amesema.

Waziri Mkuu ameongeza kuwa: “Tuzidi kumuomba Mwenyezi Mungu kila mtu kwa imani yake ili tuweze kufikia japo mema machache aliyoyatenda katika enzi za uhai wake.”

Enzi za uhai wake Mhe. Sitta alibahatika kufanya kazi na Marais wa awamu nne zilizopita tangu ya kwanza ya Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, akiwa mbunge kwa miaka 30.

Nyadhifa nyingine alizowahi kushika ni pamoja na Mkuu wa Mikoa ya Iringa na Kilimanjaro, Waziri wa Ujenzi, Waziri anayesimamia Ustawishaji Makao Makuu, Waziri wa Katiba na Sheria, Waziri wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba.
Mwili wa Spika Mstaafu, Samuel Sitta ukiingizwa bungeni mjini Dodoma Novemba 11, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
1A2358 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka shada la maua kwenye jeneza la Spika Mstaafu Samwel Sitta, bungeni mjini Dodoma Novemba 11, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa Spika Mstaafu, Samuel Sitta, bungeni mjini Dodoma, Novemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)​

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 11.11.2016

Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images