Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1426 | 1427 | (Page 1428) | 1429 | 1430 | .... | 3270 | newer

  0 0

  VOTING LINES OFFICIALLY OPEN. The voting lines for the Abryanz Style & Fashion Awards 2016 are officially open. 
  HOW TO VOTE. 
  The voting process is being done via two official lines; online at there website, www.abryanzstyleandfashionawards.com, and on social media( Instagram and twitter), by use of the hash tags provided ( #Asfas2016Nomines, #Asfa2016) The public voting carried a 40% power and the 60% is held by our panel of esteemed judges from the ASFAS Academy. #Asfa2016 #Asfahappeningagain #BringFashionToTheAsfas #CirocUg4Asfas 9.12.2016 KAMPALA SERENA HOTEL. 
  "Dress To Inspire" VOTE VOTE VOTE! 
  Vote for Sheria Ngowi as Fashion Designer of the Year 2016! To vote @sheriangowi for the Fashion Designer of the year(East Africa) 2016, Post this voting banner or image of Sheria Ngowi and caption it with the name of the category, and the hashtags, #IvoteSheriaNgowi #Asfa2016Nominee #Asfa2016 OR Visit there official site for the Abryanz Style & Fashion Awards, at www.abryanzstyle

  0 0


  0 0
 • 11/11/16--21:10: MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 12
 • 0 0


  0 0

  UONGOZI wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, unayofuraha kuwaataarifu wapenzi wa soka kuwa jioni ya leo umefanikiwa kuingia mkataba wa miaka mitatu na kiungo mshambuliaji kutoka Ghana, Enock Atta Agyei.
  Agosti mwaka huu, Azam FC tuliingia makubaliano maalumu na Medeama ya Ghana juu ya kumsajili kinda huyo anayetimiza umri wa miaka 18 mwakani baada ya benchi la ufundi kuridhishwa na uwezo wake na sasa amejiunga rasmi kwenye viunga vya Azam Complex.

  Agyei anasaini mkataba tayari kabisa kuanza kuitumikia Azam FC katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) mwakani pamoja na michuano mingine ikiwemo Kombe la Shirikisho Afrika.
  Tunaamini ya kuwa ujio wa nyota huyo wa timu ya Taifa ya Vijana ya Ghana chini ya miaka 17, utazidi kuipa nguvu timu yetu kuelekea kwenye michuano inayotukabili mbeleni, hivyo tunapenda kumtakia mafanikio mema kwa kipindi chote atakachokuwa akiipigania jezi ya Azam FC.
  Azam FC tunapenda kuwafahamisha mashabiki wetu kuwa tutaendelea kukifanyia marekebisho kikosi chetu kuelekea usajili wa dirisha dogo, lengo ni kukipa nguvu kikosi hicho ili kifanye vizuri zaidi katika michuano ya hapa nchini pamoja na ile ya Kimataifa.

  Lengo kubwa la Azam FC ni kuendelea kuwafurahisha mashabiki wetu kwa kupata matokeo bora uwanjani, na tunaamini ya kuwa, benchi zuri la ufundi tulilokuwa nalo, wachezaji wazuri walioko kikosini na wengine watakaokuja kuongeza nguvu, wote kwa pamoja wataweza kutuvusha kuelekea safari ya mafanikio msimu huu.
  Hivyo, tunawaomba mashabiki wetu kuvuta subira na kuendelea kuisapoti timu kwani tunaamini ya kuwa nyie ndio nguzo muhimu ya 12 uwanjani katika kuwapa hamasa wachezaji ya kupata matokeo bora pamoja na kuijenga timu kiujumla.
  Wakati huo huo, leo tumewapokea wachezaji saba waliokuja kwenye majaribio ya kujiunga na Azam FC, ambao ni mabeki wa kati Mbimbe Aaron Nkot (Cameroon), Kone Nabil Ibrahim (Ivory Coast), kiungo mkabaji Kingue Mpondo Stephane (Cameroon),


  Wengine ni washambuliaji Yaya Awaba Joel (Cameroon), Samuel Afful, Benard Ofori (wote Ghana) na Konan Oussou kutoka Ivory Coast.
   Mshambuliaji kutoka Ghana Enock Atta Agyei akimwaga wino kuchezea Azam FC  mbele ya viongozi wa klabu hiyo jijini Dar es salaam
   Kiungo mshambuliaji kutoka Ghana Enock Atta Agyei akiweka dole tayari kuchezea Azam FC  mbele ya viongozi wa klabu hiyo jijini Dar es salaam
  Mshambuliaji kutoka Ghana Enock Atta Agyei akimwaga wino kuchezea Azam FC  mbele ya viongozi wa klabu hiyo jijini Dar es salaam

  0 0
 • 11/12/16--00:59: MAPITIO YA MAGAZETINI LEO

 • 0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. Justin Ntalikwa leo amefanya ziara ya kutembelea Miradi mbalimbali ya Kuboresha Miundombinu ya Usambazaji umeme jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuangalia maendeleo ya utekelezaji wa miradi hiyo inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

  Miongoni mwa miradi aliyoitembelea ni Kituo cha Usambazaji Umeme Ilala kinachojengwa chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), Mradi wa Kuboresha Huduma ya Umeme Katikati ya Jiji la Dar es Saalam katika Kituo cha Dar es Salaam City Centre na Mradi wa Kituo cha Kudhibiti Mifumo ya Usambazaji umeme, kilichopo eneo la Mikocheni Jijini Dar es Salaam.

  Mara baada ya kutembelea miradi hiyo, Prof. Ntalikwa amesema kuwa, kukamilika kwake kutaimarisha miundombinu ya usambazaji umeme Jijini Dar es Saalam na hivyo kuwezesha Jiji la Dar es Salaam kupata umeme wa uhakika.

  Akizungumzia kituo cha Kudhibiti Mifumo wa Usambazaji Umeme cha Mikocheni, kilichojengwa na Serikali ya Finland na Tanzania ameeleza kuwa, kituo hicho kimefungwa mashine za kisasa zinazotumia teknolojia za hali ya juu kama zinazotumiwa katika nchi zilizoendelea na hivyo, kukamilika kwake kutawezesha kuondoa tatizo la kukatika kwa umeme jijini Dar es Salaam ikiwemo kubaini kwa haraka na moja kwa moja eneo lolote lenye hitilafu kupitia mitambo hiyo na hivyo kuwezesha tatizo kushughulikiwa kwa haraka.

  “ Kwa ujumla nimeridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi ya kuboresha miundombinu ya umeme inayotekelezwa jijini Dar es Salaam. Mradi wa Kuboresha Huduma ya Umeme Katikati ya Jiji la Dar es Saalam, unatarajiwa kuzinduliwa tarehe 16 Novemba,2016 na Mhe. Rais Dkt.John Magufuli. Kukamilika kwake kutakuwa na manufaa makubwa kwa upatikanaji umeme jijini Dar es Salaam,” ameongeza Prof. Ntalikwa.
  Mkurugenzi Mtendaji wa (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba (kulia), akimwongoza Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. Justin Ntalikwa na ujumbe wake kutembelea maeneo mbalimbali katika Kituo cha Ilala, jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara yake. 
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. Justin Ntalikwa (wa kwanza kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba (katikati) wakati alipotembelea Mradi wa Kituo cha Kuboresha Miundombinu ya Umeme cha Ilala, jijini Dar es Saalam. Wa kwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. Justin Ntalikwa na ujumbe aliofuatana nao, wakisikiliza maelezo ya kuhusu namna kituo cha Kudhibiti Mifumo wa Usambazaji Umeme cha Mikocheni, kinavyofanya kazi


  0 0

  Na Woinde Shizza,Arusha.

  Wananchi wa Kata ya Engutoto jijini Arusha wamelalamikia uuzaji holela wa maeneo ya wazi ya serikali hali inayopelekea uhaba wa maeneo ya kujenga huduma za kijamii kama zahanati na shule huduma ambazo hazipatikani katika kata hiyo hivyo wameiomba serikali itatue tatizo hilo ili wananchi wapate huduma bora za kijamii.
  Wakitioa malalamiko yao mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo wamesema kuwa licha ya uuzaji holela wa ardhi kuna migogoro ya ardhi katika kata hiyo na wananchi wengi wanaomiliki ardhi bado hawajapatiwa hati jambo ambalo linawapa wasiwasi kuwa huenda ardhi zao zikamegwa na wawekezaji.
  Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Joseph Kamete alisema kuwa wameomba sana hati za maeneo ambayo wanaishi lakini wamekuwa awapewi na wanazungushwa zungushwa kitu ambacho kinawatia mashaka makubwa.
  “Mkuu wa mkoa kinachotuuma zaidi sisi tumekaa hapa tangu kipindi cha mikonge lakini tukiomba hati hatupewi lakini akija muwekezaji anapatiwa hati kwa wakati sasa tunajiuliza inamaana sisi atuna haki ya kukaa katika viwanja hivi watuambie tu ili na sisi tujue sio wanafanya kazi ya kutuzungusha zungusha kwakweli tumekuwa tunaishi kama ndege katika maeneo yetu na atuna amani kabisa maana kama wanatunyima hati wanania gani kweli tunaomba mkuu wa mkoa utusaidie kwa hili “alisema Zaituni Marunda.
  Aidha wananchi hao pia wanasumbuliwa na kero za maji na umeme kwa kipindi kirefu hivyo wameiomba serikali iwasaidie kutatua kero hiyo inayowaathiri zaidi kinamama ambao hutembea umbali mrefu wakitafuta huduma za maji.
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ambaye alifika katika kata hiyo katika shughuli ya uzinduzi wa daraja  lililojengwa na mwekezaji Hans Paul ameagiza ofisi ya Mkurugenzi kumkabidhi ripoti ya maeneo ya wazi ya jiji yaliyouzwa kienyeji ili aweze kushughulikia kero hiyo pia ameshukuru kampuni ya Hanspaul kwa kujitoa kusaidia jamii jambo ambao linapaswa kuigwa na wawekezaji wengine.
  Alisema kuwa wao kama serikali wapo tayari kushirikiana na wawekezaji ambao wanalipa kodi kama ipasavyo na wale ambao wanajishuhulisha katika kusaidia jamii inayowazunguka.Mkuu wa Mkoa wa Arusha amefanya mkutano wa kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi pamoja na kuzindua daraja ambalo limegharimu kiasi cha shilingi milioni 67.
  Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akizindua daraja katika Kata ya Engutoto ambalo limejengwa na wawekezaji daraja hilo limegharimu zaidi ya shilingi milioni 65 za kitanzania
  Mkuu wamkoa wa Arusha akiwa anaongea na wananchi wa kata ya Engutoto ilipo ndani ya jiji la Arusha
  Wa kwanza kulia ni muwekezaji Hans Paul katikati ni mkuu wa mkoa wa Arusha mrisho Gambo kushoto ni mkurugenzi wa jiji la ArushaAthuman Kiamia wakipiga magofi mara baada ya kuzindua daraja


  0 0

  Na Beatrice Lyimo-MAELEZO-Dar es Salaam.

  NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Nuru Millao ametoa wito kwa vijana wa kitanzania kutumia fursa ya ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na China katika taaluma za masomo ikiwemo kusoma na kujifunza lugha ya kichina ili kuharakisha shughuli za maendeleo nchini.

  Aliyasema hay oleo Jijini Dar es salaam wakati wa sherehe za ufunguzi wa maadhimisho na maonesho ya utamaduni wa china yaliyolenga kuenzi mchango wa waandisi wa vitabu wa zamani William Shakespeare wa Uingereza na Tang Xianzu wa China.Bibi Nuru alisema kuwa kwa sasa Nchi ya China ipo mbali kimaendeleo hivyo wanafunzi wa wakitanzania hawana budi kutumia fursa hiyo katika kujifunza masuala mbalimbali ikiwemo lugha ya kichina. mbalimbali.

  Aidha, Bibi Nuru aliwaasa watanzania kuiga tamaduni zinazofanywa na watu wa wachina katika kuenzi kazi za waandishi mbalimbali wa mashairi, vitabu, tamthilia na maigizo ili kuweza kufaidika katika nyanya tofauti za maendeleo nchini.“Tanzania itafaidika vizuri zaidi wa kuiga mifano chanya ya wenzetu kwa kuenzi kazi za waandishi wa vitabu mbalimbali nchini, kwa mfano Mwalimu Nyerere aliandika vitabu vilivyochochea maendeleo ya Taifa” alifafanua Bibi Nuru.

  Kwa upande wake Balozi wa China Nchini, Dkt. Lu Youqing alisema China itaendeleza ushirikiano uliopo baina yao na Tanzania katika sekta mbalimbali ili kuweza kuleta manufaa baina ya wananchi wa pande zote mbili.Balozi Youqing alisema, kumekuwa na ushirikiano mzuri baina ya Tanzania na China hasa katika sekta ya utamaduni ambapo kwa sasa takribani vyuo vikuu Vinne nchini China vinafundisha lugha ya Kiswahili.

  Aidha Dkt. Youqing alisema shule sita za Sekondari nchini Tanzania zina programu ya kufundisha lugha ya kichina ikiwemo Chuo Kikuu cha Dar es salaam, tawi la Mlimani na pamoja na Chuo Kikuu cha Dodoma.Aidha Balozi Youqing alisema kuwa, nchi ya nchina imekuwa ikitafsiri vitabu vya lugha Kiswahili kwenda kwenye lugha ya kichina ambapo wameweza kutafsiri vitabu vya Mwalimu Nyerere vinavyowasaidia katika ujenzi wa Taifa lao.

  Maonyesho hayo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 400 ya waandishi wa vitabu vya riwaya, tamthilia na filamu wakiwemo William Shakespeare wa Uingereza na Tang Xianzu wa China.
  Balozi wa China nchini, Dkt. Lu Youqing akizungumza na wageni waalikwa katika maadhimisho ya miaka 400 ya kuwaenzi waaandishi wa vitabu vya zamani Tang Xianzu wa China na William Shakespeare wa nchini Uingereza. Maadhimisho hayo yalifanyika leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Kaitbu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Nuru Millao.
  Balozi wa China nchini, Dkt. Lu Youqing akimkabidhi zawadi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo, Bi. Nuru Millao katika maadhimisho ya miaka 400 ya kuwaenzi waaandishi wa vitabu vya zamani Tang Xianzu wa China na William Shakespeare wa nchini Uingereza. Maadhimisho hayo yalifanyika leo Jijini Dar es Salaam.
  Balozi wa China nchini, Dkt. Lu Youqing akimpa maelezo ya ufafanuzi ya vazi la asili, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Nuru Millao katika maadhimisho ya miaka 400 ya kuwaenzi waaandishi wa vitabu vya zamani Tang Xianzu wa China na William Shakespeare wa nchini Uingereza. Maadhimisho hayo yalifanyika leo Jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Wimbo: Inuka- Dudu baya Mamba ft Tid
  Producer: Mgwabati Classic & Nice P
  Studio: Tawanyika Studios

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa akifungua Kikao Kazi kilichowakutanisha Wataalam wa masuala ya takwimu ambao ni Wawakilishi kutoka nchi 24 Barani Afrika kujadili juu ya njia bora na mahususi katika kulisaidia Bara la Afrika katika utoaji bora wa takwimu.
  Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa pamoja na Wataalam wa masuala ya takwimu ambao ni Wawakilishi kutoka nchi 24 Barani Afrika wakijadiliana masuala muhimu kuhusu namna bora ya kulisaidia Bara la Afrika katika utoaji bora wa takwimu.
  Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa (aliyevaa gauni jekundu) pamoja na Wataalam wa masuala ya takwimu ambao ni Wawakilishi kutoka nchi 24 Barani Afrika wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa Kikao Kazi kuhusu namna bora ya kulisaidia Bara la Afrika katika utoaji bora wa takwimu. PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA

  0 0

  VIJANA saba wenye umri chini ya miaka 17, wamepenya kwenye majaribio ya wazi ya mwisho katika mkoa wa Dar es Salaam, yaliyoendeshwa na Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC leo Jumamosi.Huo ni mwendelezo wa mpango wa mabingwa hao wa kutengeneza timu bora ya vijana wa umri huo kwa ajili ya kuwatumia kwa miaka ijayo na wengine kunufaika nao kwa kuwauza.
  Katika majaribio hayo walijitokeza vijana 433 wenye umri tofauti kuanzia chini ya umri wa miaka 10, 12, 14 na 17, ambapo waliweza kuchaguliwa saba pekee na wengine 33 kuorodheshwa.
  Mpaka sasa mpango huo umeshahusisha mikoa maeneo matano tofauti nchini katika mkoa wa Dar es Salaam, Tanga, Morogoro, Dodoma na Visiwani Zanzibar, ambako kote kumefanya idadi ya vijana waliofanyiwa usaili kufikia 2,593, kati ya hao 50 pekee ndio waliochaguliwa kushiriki fainali ya mwisho itakayofanyika Uwanja wa Azam Complex mwezi ujao.

  0 0
 • 11/12/16--09:49: mambo ya Gado
 • Nov 13 16 Trump calls President Uhuru (Kenya)

  0 0


   Taswira za mazoezi ya Taifa Stars mjini Harare kujiandaa kupambana na timu ya taifa ya Zimbabwe
   Taswira za mazoezi ya Taifa Stars mjini Harare kujiandaa kupambana na timu ya taifa ya Zimbabwe
   Taswira za mazoezi ya Taifa Stars mjini Harare kujiandaa kupambana na timu ya taifa ya Zimbabwe
  Taswira za mazoezi ya Taifa Stars mjini Harare kujiandaa kupambana na timu ya taifa ya Zimbabwe

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.  Zainab Telack amefanya ziara wilayani Kishapu na kukagua mradi wa nyumba za watumishi wa Idara ya Afya zilizojengwa kwa msaada wa Mfuko wa Benjamin William Mkapa.

  Katika ziara hiyo Mhe. Telack akiwa ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, alitembelea nyumba hizo katika kata za Shagihilu, Mwakipoya na Idukilo ambazo tayari zimekamilika kwa ajili ya makazi.

  Mkuu huyo wa mkoa aliiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kuhakikisha kuwa changamoto zote zinazoikabili miradi hiyo na sekta ya afya kwa ujumla zitatuliwe ziwe zimetatuliwa.

  Aliitaka Idara ya Afya kushirikisha Idara ya Ujenzi katika kutekeleza miradi inayohusu ujenzi wa mindombinu mbalimbali katika sekta hiyo muhimu kwa kuwa ndiyo wataalamu.

  Awali wakati akisoma taarifa ya halmashauri hiyo, Mkurugenzi Mtendaji, Stephen Magoiga alisema jumla ya zahanati 22 zinajengwa na Serikali kwa kushirikiana na wadau.

  Magoiga aliongeza kwa kusema kuwa kukamilika kwa zahanati hizo katika kata mbalimbali kutasaidia kutatua changamoto ya vifo vya wajawazito na watoto.

  Alibainisha kuwa hivi sasa halmashauri ina magari ya wagonjwa (ambulance) manne ambapo matatu kati yake yalitolewa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNFPA) wakati moja lilinuliwa na halmashauri.

  Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (mbele) akikagua moja ya nyumba za watumishi wa Afya kata ya Shagihilu zilizojengwa kwa ufadhili wa Mfuko wa Benjamin William Mkapa. Wengine pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga (mwenye tai) na Mganga Mkuu wa Mkoa, Mwita Ngutunyi (mwenye suti).

  Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji mara baada ya kuwasili katika nyumba ya mtumishi wa Zahanati ya Kata ya Idukilo wakati wa ziara yake wilayani humo.

  Mkuu wa Mkoa akifungua mlango wa moja ya nyumba kujionea mradi huo uliofadhiliwa na Mfuko wa Benjamin William Mkapa wakati wa ziara yake.

  Mkuu wa Mkoa akiwasili katika zahanati ya Badi iliyopo Kata ya Mwakipoya wilayani Kishapu kukagua miradi ya nyumba za watumishi wa Afya. Wengine pichani kuanzia kushoto Afisa Mipango Wilaya, Mang’era Mang’era, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya, Stephen Magoiga (mwenye tai) na Mganga Mkuu wa Mkoa, Mwita Ngutunyi (mwenye suti).

  Ukaguzi wa nyumba unaendelea huku Mhandisi Ujenzi Wilaya, Samson Pamphil (kushoto) akichukua taarifa muhimu.


  0 0

  Wadau mbalimbali wa shuguli za usafiri wa anga nchini, wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya usfiri wa anga Tanzania, Bw. Hamza Johari,(wa nne kutoka kulia) wakimsikilza kwa makini mhandisi wa  mitambo ya kuongozea ndege ya  DVOR+DME , Kelvin Mwakalobo wakati walipofanya ziara  kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA)  jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho siku ya wataalam wa mitambo ya kuongoza  ndege (AIR TRAFFIC SAFETY ELECTRONICS PERSONNEL'S DAY - ATSEP- )
   Mkurugenzi Mkuu wa Mamalaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Hamza Johari  ( kushoto) pamoja na wadau mbalimbali wa usafiri a anga nchini   wakimsikiliza  mhandisi wa mtambo wa kuongozea ndege wa Rada  Marco Omari ,wakati walipofanya ziara   kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA)  jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho siku ya wataalam wa mitambo ya kuongoza  ndege.
   ya uhandisi.
   Mkurugenzi Mkuu wa Mamalaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Hamza Johari  (wapili kushoto) pamoja na wadau mbalimbali wa usafiri a anga nchini   wakimsikiliza  mhandisi wa mitambo ya kuongea ndege  ili iweze kutua kwa usalama( AWOS) James Mjema ,wakati walipofanya ziara   kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA)  jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho siku ya wataalam wa mitambo ya kuongoza  ndege.
  Wadau wa shuguli za usafiri wa anga nchini katika picha ya pamoja wakati wa  maadhimisho siku ya wataalam wa mitambo ya kuongoza  ndege.

  0 0


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mwakilishi wa Ubalozi wa Norwaya Bw. Victor Mlundo wakati wa kuzindua majengo mapya ya Wodi ya Watoto Kinamama katika Hospitali ya Mnazi mmjoja uliofanyika leo .
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Chumba cha kulelea Watoto wachanga wakati alipotembelea majengo mapya ya Wodi ya Kinamama na Watoto katika Hospitali ya Mnazi Mmoja baada ya uzinduzi rasmi leo,(wa pili kulia) mwakilishi wa Ubalozi wa Uholanzi Teresia Mcha 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya Chuo Kikuu cha Hauklend Bw.Eivend Hansen wakikata utepe kuzindua jengo la Wodi ya Watoto wakati wa uzinduzi wa majengo mapya ya Wodi ya Kinamama na Watoto uliofanyika leo katika Hospitali ya Mnazi Mmoja.


  0 0
  0 0


  Nteghenjwa Hosseah - Arusha

  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo amezinduzaa daraja la Mto Kijenge linalounganisha kata za Engutoto na Moshono ambalo limejengwa kwa ufadhili wa Kampuni ya Dharam Singh Hanspaul.

  Akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa amesema daraja hilo ni ukombozi na msaada kwa wananchi wengi ambao walikua wakipata adha kubwa ya kuvuka haswa wakati wa mvua kutokana na kukosa kivuko cha uhakika na kivuko kilichokuwepo awali kiliashiria hali ya hatari kubwa kwa watoto, wazee, waendesha pikipiki, waenda kwa miguu wote na zaidi hakuna Gari lililokuwa na uwezo wa kupita hapo.

  Hii ndio tunayoita kurudisha kwa jamii “Community Social Responsibility”, kampuni hii ya Hanspaul imetoa msaada ambao utatoa mchango mkubwa sana kwa jamii na sisi kama Serikali tunafarijika kwa kuona wadau wanaunga mkono jitihada za Serikaili kwa kiwango hiki hili ni jambo la kuigwa na Kampuni nyingine wajifunze katika hili.

  Katika uzinduzi wa daraja hili Rc Gambo alitumia fursa hiyo alisikiliza kero za wananchi waliohudhuria na ambao wamelalamikia uuzaji holela wa maeneo ya wazi ya Serikali hali inayopelekea uhaba wa maeneo ya kujenga huduma za kijamii kama zahanati na shule huduma ambazo hazipatikani katika kata ya Engutoto hiyo hivyo wameiomba serikali itatue tatizo hilo ili wananchi wapate huduma bora za ijamii. 
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akizindua Daraja la Mto Kijenge.
  Hili ndilo Daraja lililojengwa na wafadhili chini ya Bw. Hans Paul lina upana wa Mita 20, uwezo wa kupitisha magari yenye uzito wa Tani 3, urefu kwenda juu Mita 2.2 na uwezo wa kudumu kwa miaka 50. 
   Daraja walilokuwa wanatumia wananchi wa Engutoto na Moshono kabla ya kujengewa Daraja la kiwango na Kampuni ya Dharam Sign Hanspaul .

  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo(kwanza kulia) akipokea Kero kutoka kwa mwananchi kama zilivyowasilishwa na Mama Debora wakati wa  Unzinduzi wa Daraja la Mto Kijenge 


older | 1 | .... | 1426 | 1427 | (Page 1428) | 1429 | 1430 | .... | 3270 | newer