Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

SERENGETI BOYS WAKWAA PIPA KUELEKEA KOREA YA KUSINI

$
0
0
Na Dac Popo wa Globu ya jamii
Kikosi cha wachezaji 19 wa timu ya vijana walio chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys na viongozi 8 wameondoka jijini Dar es salaam leo kuelekea nchini Korea ya Kusini kushiriki mashindano maalumu ya vijana walio katika umri huo. 
Akizungumza baada ya kuwaaga wachezaji hao katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa J.K.Nyerere afisa habari wa shirikisho la kabumbu Tanzania TFF Alfred Lucas alisema kuwa mashindano hayo yanayojumuisha mataifa manne yameandaliwa na shirikisho la kandanda la Korea ya Kusini na kupewa baraka na FIFA. 
Amesema kuwa hiyo ni nafasi nzuri ya mazoezi kwa timu hiyo kwani iwapo rufaa iliyokatwa na TFF kuhusu timu ya taifa ya Congo ya umri huo kumchezesha mchezaji aliyezidi umri timu hizo zilipopambana kuwania kushiriki mashindano ya Afrika itafaulu basi timu yetu itakuwa imepata mafunzo ya kutosha na kujiweka vizuri zaidi kwa fainali hizo zitakazofanyika Madagascar. 
Wakati huo huo Alfred Lucas amesema kuwa timu yoyote iliyo katika Ligi Kuu ya kandanda nchini VPL ambayo haitapeleka timu yake ya vijana wa chini ya umri wa miaka 20 katika mashindano yake yatakayofanyika katika vituo vya Kagera na Dar es salaam itakumbwa na adhabu ya faini na kunyang’anywa pointi. 
Ametanabaisha kuwa kutokana na kanuni ya 42 kifungu cha 27 ya kanuni za ligi timu ikikosa mchezo wa kwanza itapokwa pointi 3 na faini ya sh.2,000,000/ na kama haitapeleka timu basi timu yake kubwa itapokwa pointi 12 kutoka katika pointi ilizonazo kwenye msimamo wa ligi ulivyo sasa. Ametoa kauli hiyo kufuatia klabu za Yanga na African Lion kutishia kutopeleka timu zao za vijana katika kituo cha Kagera ambazo wamepangiwa,mashindano hayo yamepangwa kuanza tarehe 16 ya mwezi huu.
 Afisa Habari wa Shirikisho la Kabumbu Tanzania TFF Alfred Lucas akizungumza na waandishi wa habari juu ya  timu ya vijana  walio chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys na viongozi 8 kuondoka jijini Dar es salaam leo kuelekea nchini Korea ya Kusini kushiriki mashindano maalumu ya vijana walio katika umri huo.
Serengeti Boys wakiwasili katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa J.K.Nyerere tayari kwa safari kuelekea nchini Korea ya Kusini kushiriki mashindano maalumu ya vijana walio katika umri huo.
Vijana  wa Serengeti Boys wakiingia kwenye eneo la ukaguzi katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa J.K.Nyerere tayari kwa safari kuelekea nchini Korea ya Kusini kushiriki mashindano maalumu ya vijana walio katika umri huo. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

mkataba wa kutunga nyimbo kwa washindi wa klabu raha leo show yaTBC1 wasainiwa

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa shirika la habari Tanzania TBC1 Dr Ayub Ryoba Chacha akiingia makubaliano Na C.E.O wa High Table Sound Bw.  Elias Barnaba kwa ajili ya kuimba na kuwatungia nyimbo moja moja kila mshindi wa kwanza na mshindi wa pili wa CLUB RAHA LEO SHOW msimu wa Tatu. Kulia kwa Barnaba ni mshindi wa jumla  Rajab Saidi na  kushoto KWA Dr Ryoba ni Amiri Amidu.
  Mkurugenzi Mkuu wa shirika la habari Tanzania TBC1 Dr Ayub Ryoba Chacha baada ya kuingia makubaliano Na C.E.O wa High Table Sound Bw.  Elias Barnaba kwa ajili ya kuimba na kuwatungia nyimbo moja moja mshindi wa kwanza na mshindi wa pili wa CLUB RAHA LEO SHOW msimu wa Tatu. Kulia kwa Barnaba ni mshindi wa jumla  Rajab Saidi na  kushoto KWA Dr Ryoba ni Amiri Amidu.
 Mkurugenzi Mkuu wa shirika la habari Tanzania TBC1 Dr Ayub Ryoba Chacha akifurahia makubaliano Na C.E.O wa High Table Sound Elias Barnaba kwa ajili ya kuimba na kuwatungia nyimbo moja moja  mshindi wa kwanza na mshindi wa pili wa CLUB RAHA LEO SHOW msimu wa Tatu. Kulia kwa Barnaba ni mshindi wa jumla  Rajab Saidi na  kushoto KWA Dr Ryoba ni Amiri Amidu.

Invitation for Tenders at State University of Zanzibar (SUZA)

Bayport yakabidhi madarasa matatu yenye thamani ya shilingi m 200/- kwa kituo cha KCVC

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Kibaha Mh AsumtaMshama, akishuhudia uzinduzi wa moja ya madarasa ya kituo cha watoto yatima cha KCVC uliofanywa na mlezi kituo hicho mama Anna Mkapa na mwenyekitiwabodiya Bayport Tanzania Dkt. Ken Kwaku hafla iliyofanyika kijiji cha Simbani wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani 
Afisa Mtendaji Mkuu wa Bayport Tanzania, John Mbaga akiongea na wageni waalikwa katika hafla ya uzinduzi wa kituo cha KCVC.
Mlezi kituo hicho mama Anna Mkapa akitoa hotuba kwa wageni waalikwa 
Viongozi wa Bayport Tanzania wakiwa katika picha ya pamojana Mkuu wa wilaya ya Kibaha Mh Asumpta Mshama, Mama Anna Mkapa, mtoto Esther Furaha pamoja na wasimamizi wa kituo cha Kibaha Children’s village centre.

TTCL YAWAFUATA WATEJA MITAANI

$
0
0
KAMPUNI ya Simu Tanzania TTCL, leo imeanza Kampeni ya kuwafuata wateja wake mitaani ili kuzungumza nao, kuwapa taarifa za huduma zinazotolewa na kuwaunganisha wateja hao katika huduma mbali mbali za TTCL. 
Kampeni hiyo imeongozwa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Bw Waziri W. Kindamba na kusaidiwa na Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na Wafanyakazi wa TTCL waliosambaa katika maeneo mbali mbali ya Jiji la Dar Es Salaam. "Huu utakuwa ni utamaduni wetu, tutawafuata Wateja popote walipo, tutawapa taarifa za huduma zetu bora na nafuu, tutawasikiliza na kufanyia kazi maoni yao. 
Tunataka kuwahakikishia Wananchi kuwa, hii ni TTCL Mpya, Shirika lao la kizalendo limerejea katika nafasi ya mhimili mkuu wa Mawasiliano nchini Tanzania. Watumie huduma zetu, waone tofauti, wapate ubora na viwango vya juu kabisa", amesema Bw Kindamba. 
Kwa upande wake Afisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa TTCL Bw Peter Ngota amesema, TTCL inawaletea wateja wake Ofa MPYA kabambe kwa ajili ya Simu ya Mezani inayotoa uhakika wa mawasiliano kati ya Wanafamilia. Kwa Mteja atakayeongeza salio la shilingi 23,000/- atapata ofa ya Simu Bure pamoja na ofa kupiga simu TTCL kwenda TTCL bure.
 Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania TTCL, Bw. Waziri W. Kindamba (kushoto) akiwaelezea wananchi mitaani juu ya ofa mpya ya huduma ya Simu za Mezani katika eneo la Posta Mpya leo jijini Dar es Salaam, pembezoni mwa mtaa wa Azikiwe Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania TTCL, Bw. Waziri W. Kindamba (wa kwanza kushoto) pamoja na baadhi ya wakuu wa Idara na Vitengo na Wafanyakazi wa TTCL wakizunguka baadhi ya mitaani wakielezea hudumba mbalimbali za kampuni hiyo kwa wakazi wa Jiji la Dar Es Salaam Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania TTCL, Bw. Waziri W. Kindamba (kushoto) akiwaelezea wananchi mitaani juu ya ofa mpya ya huduma ya Simu za Mezani katika eneo la Posta Mpya leo jijini Dar es Salaam, pembezoni mwa mtaa wa Azikiwe. Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania TTCL, Bw. Waziri W. Kindamba akigawa vipeperushi kwa mmoja wa wananchi vinavyoelezea ofa mpya ya huduma ya Simu za Mezani katika eneo la Posta Mpya leo jijini Dar es Salaam, pembezoni mwa mtaa wa Azikiwe. Hapa baadhi ya wafanyakazi pamoja na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania TTCL, Bw. Kindamba na baadhi ya wakuu wa Idara na Vitengo wakionesha alama ya T mara baada ya kampeni yao.

BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 09.11.2016

SIMBA YASHINDWA KUUNGURUMA MBELE YA TANZANIA PRISON,YAFUNGWA GOLI 2-1

$
0
0
Mtanange wa Simba Dhidi ya Tanzania Prison Ulimalizika kwa Kishindo uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya Ambapo Timu Ya wekundu wa msimbasi Simba Fc Ilipokea kichapo Cha Goli 2-1 Kutoka kwa wajelajela Tanzania Prison kama ambavyo Taswira Hapo juu ikionyesha mchezaji wa Simba Shoto, Jonas Mkude akichuwana Vikali na Salum Kimenya Katika Mtanange Ulio Malizika Katika Uwanja Wa Sokoine Ikiwa Jamal Mnyate Dk.43 Kipindi cha Kwanza Aliipatia Goli Timu Ya Simba, Huku Victor Hangaya kutoka Prison alisawazisha na kuongeza bao la Pili kwa Timu Yake Ya Tanzania Prison Mbeya.
Baadhi ya mashabiki kinazi wa Timu ya Wekundu wa Msimbazi wakiwa Katika Eneo lao.

 Kushoto Ni Kocha wa Timu ya Simba Joseph Omog akisalimiana na Kocha Wa Timu ya Prison Abdul Mingange kabla ya Mchezo kuanza..






 Jonas Mkude shoto akimtoka mchezaji wa Prison Victor Hangaya.
PICHA ZOTE NA MR.PENGO MMG MBEYA.

TANZANIA UHURU NIGHT COLUMBUS, OHIO

$
0
0

NUNUA TIKETI MAPEMA KWA NUSU BEI MWISHO NI NOVEMBA 30,2016

kuwait yachngia dola za kimarekani 33,000 kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera

$
0
0
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akipokea mfano wa hundi ya dola za Kimarekani 33,000  kutoka kwa balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Al-Najem zikiwa ni mchango wa nchi hiyo kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera, ofisini kwake bungeni mjini Dodoma November 9, 2016.

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI NOVEMBA 10, 2016

UMOJA WA MATAIFA WAISHUKURU SERIKALI YA TANZANIA

$
0
0

Na Mwandishi Maalum, New York


Umoja wa Mataifa kwa mara nyingine tena, umeishukuru Serikali ya Tanzania kwa kusaidia kwa hali na mali ujenzi na hatimaye kuelekea ukamilishwaji wa Majengo mapya ambayo yatatumika kwa shughuli za iliyokuwa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda ( ICTR) ambayo ilihitimisha majukumu yake mwaka jana.

Shukrani hizo zimetolewa siku ya jumatano na Bw.Theodor Meron, ambaye ni Rais wa Mahakama za Kimataifa za Kesi za Masalia na Utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka zote muhimu za zilizokuwa Mahakama za Kimataifa zilizoshughulikia mauaji ya halaiki yaliyotokea Rwanda na Yugoslavia ya zamani ( IRMCT).

Bw. Theodor Meron alikuwa akiwasilisha Ripoti yake ya Nne kuhusu IRMCT mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa . Ripoti ambayo imeanisha maendeleo ya kipindi cha mpito kutoka ICTR na ICTY kwenda IRMCT kazi ambayo amesema inakwenda vizuri ingawa kumekuwapo na changamoto kadhaa.

“Wakati ninapowasilisha ripoti hii, nichukue fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati kabisa kwa mchango mkubwa na ushirikiano ambao tumeupata kutoka serikali ya Tanzania, takribani wiki tatu zijazo majengo hayo yatazinduliwa rasmi baada ya kuwa yamekamilika”. Akasema Bw. Meroe

Baadhi ya changamoto hizo kwa upande wa iliyokuwa ICTR ni pamoja na kutokamatwa hadi sasa kwa watuhumiwa watatu ambao inaelezwa wapo mafichoni. Ni pili ni mahali pa kuwapeleka watu ambao ama wamekwisha maliza kutumikia vifungo vyao na kuachiwa huru. Watu hao wamekosa nchi ya kuwapokea na hadi sasa bado wanaendelea kuishi nchini Tanzania.

Na kwa sababu hiyo, Rais wa IRMCT ametoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kutoa ushirikiano wa kuwachukua watu hao ambao hawana mahali pa kwenda na kwa wale walioko mafichoni nchi ambazo wamejificha watoe ushirikiano kwa kuwafichua na kuwakamata ili hatimaye sheria iweze kuchukua mkondo wake

Kwa upande wake, Tanzania kupitia Mwakilishi wake katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, amesema Tanzania inakaribisha kuhitimishwa kwa ujenzi kwa ujenzi wa makazo mapya ya iliyokuwa ICTR katika eneo la Lakilaki ndani ya wakati na kwa bajeti iliyopangwa.

“Kwa namna ya pekee tunampongeza Msajili wa Mahakama, Bw. John Hopkins kwa uongozi wake na ushirikiano wake ambao umewezesha kukamilisha hatua hii muhimu sana”. Akasisiza Balozi.

Rais wa IRMCT, Bw. Theodor Meron akiwasilisha mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, hapo siku ya jumatano, Ripoti ya utendaji kazi wa Matawi ya Mahakama za Kimataifa za Kesi za Masalia zinachokua nafasi ya iliyokuwa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda ( ICTR) na Mauaji ya halaiki yaliyotokea katika iliyokuwa Yugoslavia ya zamani ( ICTY. Bw. Meron alitumia pia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano wa hali na mali katika ujenzi wa majengo yanayochokua nafasi ya ICTR majengo hayo yamejengwa katika eneo la Lakilaki Mkoani Arusha.
.Mwakilishi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi akizungumza wakati wa uwasilishwaji wa Ripoti ya utendaji kazi wa IRMCT ambapo alimshukuru kwa namna ya pekee Msajili wa IRMCT Bw. John Hopkins kwa uongozi wake na ushirikiano ambao ameonyesha katika ujenzi wa majengo mapya huko Lakilaki lakini pia katika kusimamia kipindi cha mpito na makabidhiano kutoka ICTR kwenda IRMCT.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MSHINDI WA MILIONI 100

$
0
0
Mshindi wa Milioni Mia kupitia promosheni ya Jiongeze na M-pawa iliyokuwa ikiendeshwa na Vodacom Tanzania,Mkazi wa Mwanza Paulina Kulwa akifurahi baada ya kupokea mfano wa hundi yake, kwenye hafla iliyofanyika jijini Mwanza.
Mshindi wa Milioni Mia ya Jiongeze na M-pawa mkazi wa Mwanza Paulina Kulwa(kulia) akipokea mfano wa hundi yake kutoka kwa Mkuu wa Kanda ya Ziwa wa Vodacom Tanzania, Ayubu Kalufya(kushoto), kwenye hafla iliyofanyika jijini Mwanza, akishuhudia katikati ni Mkuu wa kitengo cha Masoko wa CBA Benki, Solomon Kawiche.
Mshindi wa Milioni Mia kupitia promosheni ya”Jiongeze na M-pawa”iliyokuwa ikiendeshwa na Vodacom Tanzania, Mkazi wa Mwanza Paulina Kulwa(katikati) akifurahi baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi na Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya Ziwa,Ayubu Kalufya kwenye hafla fupi iliyofanyika jijini Mwanza jana, kushoto ni Meneja Masoko wa huduma za kifedha wa kampuni hiyo Noel Mazoya.

YALIYOJIRI MAGAZETINI LEO November 10, 2016

KIWANDA CHA SUKARI MAHONDA CHAHITAJI ENEO ZAIDI LA ARDHI KUFANIKISHA UZALISHAJI

$
0
0
Kiwanda cha Sukari Mahonda.

Na Mwashungi Tahir Maelezo Zanzibar 9-11-2016

Meneja wa Biashara wa Kiwanda cha sukari Mahonda Bw Pronav Shah amekumbushia ombi lao kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar la kukipatia Kiwanda maeneo zaidi ya ardhi ili kuimarisha uzalishaji wa sukari katika kiwanda hicho.

Amesema kiwanda hulazimika kusitisha uzalishaji wa sukari kutokana na upungufu wa miwa na huku ikwalipa mishahara wafanyakazi bila ya kuzalisha na kukipelekea kiwanda kuingia katika hasara.

Ameeleza hayo Ofisini kwake Mahonda wakati Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi ilipofanya ziara ya kutembelea kiwanda hicho kuangalia mafanikio na changamoto zinazowakabili . 

Bw Pronav Shah ameieleza Kamati hiyo ya Baraza la Wawakilishi kuwa sehemu kubwa ya mashamba ya kiwanda imevamiwa na wananchi wa kawaida kwa shughuli zao ikiwemo ujenzi wa nyumba huku wakijua kuwa ni sehemu ya kiwanda na kupunguza ukubwa wa shamba hilo. 

“Sehemu kubwa ya shamba la miwa hivi sasa limevamiwa na watu wa kawaida na inasemekana wanaungwa mkono na baadhi ya viongozi wa shehia,” amelalamika Meneja huyo.

Katika hatua nyengine Meneja huyo wa Biashara ameiomba serikali kuwapatia bima ili inapotokea ajali waweze kufidiwa gharama za ajali hiyo. 

Amesema iwapo serikali itawapatia bima itawasaidia hasa kwa vile mara kwa mara mashamba ya miwa hushambuliwa na moto ambao haujulikani chanzo chake licha ya juhudi za uchunguzi zinazofanwa na jeshi la Polisi. 

Bw. Pronav Shah ameshauri kuruhusiwa kupanua soko la kuuza sukari katika soko la Tanzania Bara ambalo hivi sasa bei ni tafauti na Zanzibar ama kuuza sukari yao Zanzibar kwa bei ya soko la Tanzania Bara.

Nae mwenyekiti wa Kamati ya Fedha , Biashara na Kilimo Yussuf Hassan ameutaka uongozi wa Kiwanda hicho kuendeleza uzalishaji wa sukari ili kuwasaidia vijana kupata ajira na kufikia lengo la kujitosheleza kwa bidhaa hiyo.

Ameuhakikishia uongozi wa kiwanda hicho kuwa ombi lao la kupata ardhi zaidi kwa ajili ya kuongeza mashamba ya miwa watalifikisha katika ngazi za juu ili liweze kupatiwa ufumbuzi.

Amesema Serikali inafahamu kuwa kufanikiwa kwa Kiwanda cha sukari cha Mahonda itakuwa ni kivutio kwa wawekezaji wengine kuja kuwekeza Zanzibar.

IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR 

RC GAMBO AONGOZA KIKAO CHA KWANZA CHA KAMATI YA AMANI

$
0
0
Nteghenjwa Hosseah – Arusha 

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Mashaka Gambo amekutana na kamati ya Amani ya Mkoa ambayo inajumuisha viongozi wa dini mbalimbali zilizoko katoka Mkoa huu kuzungumzia mustakabali wa Amani na namna viongozi hawa wa dini watashirikiana na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuleta maendeleo kwa wananchi ambao ni waumini wao.

Akizungumza katika Kikao hicho Mhe. Gambo alisema kazi ya Ulinzi wa Amani itakua rahisi sana kupitia viongozi wa dini ambao wana karama ya kuongea na kubadilisha maisha ya watu bila kutumia nguvu ama kuwashurutisha isipokua kwa chakula cha roho ambacho hujenga misingi imara ya imani na tabia njema.

Maendeleo ya wananchi hayawezi kupatikana bila Amani kuwepo katika Mkoa wetu ni lazima tusaidiane katika hili dhamira yetu ifanikiwe kwa wepesi zaidi tuna Imani kubwa sana Na viongozi wetu wa dini na ndio maana nikaona ni vyema tukakutana ili tusikie kutoka kwenu ninyi ambao mnawakilisha kundi kubwa la wananchi na pia kufahamu kero mbalimbali zinazowakwaza wananchi katika maeneo yenu alisema Gambo.
 
Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini Kati KKKT Solomon Masangwa akichangia kuhusu masuala yanayoweza kuhatarisha amani alisema kundi ambalo linatakiwa kuangaliwa kwa jicho la Tatu na litasaidia sana katika ulinzi wa Amani ni waendesha boda boda pamoja na wanachinga ambao kwa sasa wanaonekana kutopewa kipaumbele au hatuwajali kwa kiasi kinachostahili.

Tunapaswa kuangalia namna gani watu wanaofanya shughuli hizi wanakua rasmi kwa kupatiwa maeneo maalumu pamoja na utambulisho utakaowawezesha kufanya kazi zao kwa Amani na kujipatia kipato cha kuendesha maisha yao na si kama walivyo sasa wanafanya kazi hizo katika maeneo yasiyo rasmi na kuhama kila siku hali hii ina wafanya wajihisi kama si sehemu ya Taifa hili hivyo wanaweza kutumika kiurahisi kuhatarisha amani ya Nchi yetu alisema Masangwa.


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo(katikati) katika Picha ya pamoja na Viongozi wa Dini waliohudhuria Kikao cha Kamati ya Amani.


baadhi ya Madaktari Bingwa watakaowasili Tanzania Nov 11 kutoka Saudi Arabia

$
0
0


Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Mheshimiwa Hemed Mgaza kushoto, akishuhudia Viongozi wa Madaktari Bingwa wa Jumuiya ya WAMY nchini hapa wakisoma ramani ya Tanzania katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania mjini Riyadh, ili kuifahamu vizuri Tanzania na maeneo watakayofikia katika msafara wao wa kwenda Visiwani Zanzibar kwa ajili ya kutoa huduma za afya bure kwa siku 10 kwenye Hospitali za Chake Chake na Wete. Picha na Mpiga Picha Wetu, Riyadh.
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza akiwa na viongozi wa Madaktari Bingwa wa Jumuiya ya WAMY ambao walifika Ubalozini mjini Riyadh kujitambulisha na kukamilisha taratibu za safari kuingia Tanzania. Madaktari hao wanatarajiwa kuwasili nchini Tanzania Novemba 11.

YANGA YAIADHIBU RUVU SHOOTING UWANJA WA UHURU LEO, YASHINDA BAO 2-1

$
0
0
MABINGWA watetezi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, Yanga leo wameendeleza ubabe wao baada ya kuwadidimiza Maafande wa Ruvu Shooting goli 2-1 na kufikia alama 33 nyuma ya mahasimu wao Simba wenye alama 35.

Dakika ya 6 ya mchezo, Ruvu walianza kufungua pazia la magoli kupitia kwa mshambuliaji wake Abraham Mussa baada ya kufanya shambulio la kushtukiza langoni kwa Yanga.

Yanga walianza kulisakama lango la Ruvu shooting na katika dakika ya 32, Simon Msuva akaisawazishia timu yake goli na kufanya matokeo kuwa 1-1 mpaka mapumziko.

Kabla ya kipindi cha pili kuanza kocha wa Yanga, Hans Van De Pluijm anatolewa nje kwa amri ya mwamuzi wa mchezo huo, Mathew Akram kutoka jijini Mwanza baada ya kumzonga na kwenda kushuhudia kipindi cha pili cha mchezo huo akiwa jukwaani na mashabiki.

Ukiwa umeanza kwa kasi kwa kila upande kutafuta goli la kuongoza na katika dakika ya 56 juhudi za Donald Ngoma zinaisaidia Yanga ambapo Haruna Niyonzima anaachia shuti kali lililotinga kimiani na kuiandikia Yanga goli 2.

Kila upande wakiwa wanashambuliana kwa zamu mpaka dakika 90 zinamalizika Yanga anatoka kifua mbele kwa ushindi wa goli 2-1.
Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva akiiandikia timu yake bao la kusawazisha katika mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara, uliopogwa katika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es salaam leo. Yanga imeshinda bao 2-1.
Kiungo Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Thaban Kamusoko akichuana vikali na Beki wa Ruvu Shooting, Shaibu Nayopa, wakati wa Mchezo wa ligi kuu Tanzania bara, uliochezwa katika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es salaam leo. Yanga imeshinda bao 2-1.

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

$
0
0

SIMU.TV: Rais Dr John Pombe Magufuli ameongoza mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam katika kuaga mwili wa aliyewahi kuwa waziri wa elimu Marehemu Joseph Mungai. https://youtu.be/yxiPYXzDKUw

SIMU.TV: Vikosi vya zima moto kwa kushirikiana na jeshi la polisi limefanikiwa kuthibiti moto uliozuka katika ghala la kuhifadhia vipuri vya pikipiki na baiskeli la Saba General lililopo jijini Dar es Salaam. https://youtu.be/W8Hx1xqMZGw

SIMU.TV: Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto amekishauri chama madaktari hapa nchini kujadili na kutoa mapendekezo namna ya kufanya mgawanyo kwa rasilimali watu katika sekta hiyo. https://youtu.be/JoWNFgRugQE

SIMU.TV: Serikali imewataka wenyeviti na waratibu wa uwezeshaji nchini kujipanga vyema na kufanikisha utekelezaji wa sera ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ya mwaka 2004. https://youtu.be/eIPZG7C_Uzc

SIMU.TV: Kampuni hodhi ya rasilimali za reli nchini imeanza utekelezaji wa mradi mkubwa wa ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha standard Gauge. https://youtu.be/MMFAG-Pop50

SIMU.TV: Wakazi wa kijiji cha Naisinyai mkoani Manyara  wamezuia lango la mgodi wa Tanzanite one kwa madai kuwa mwekezaji amekiuka makubaliano. https://youtu.be/-KnXz4yzFIs

SIMU.TV: Serikali imezindua kampeni ya kuelimisha na kuhamasisha wananchi na watumishi wa umma kufanya kazi kwa kuzingatia maadili bora. https://youtu.be/fxM02gUGjL8

SIMU.TV: Maonesho ya taasisi za kifedha yamezinduliwa jijini Dar es Salaam ili kutoa elimu kwa umma inayohusiana na huduma za kifedha kwa pamoja. https://youtu.be/VE0EXZYqoBg

SIMU.TV: Viongozi wa vyama vya ushirika na watunza maghala ya vyama vya ushirika mkoani Mtwara wametakiwa kuhakikisha wanunuzi wa zao la korosho wanatoa korosho kwenye maghala mara wanapo lipia. https://youtu.be/tOMRrjGDSSY

SIMU.TV: Maboresho ya uwanja wa gofu Lugalo yameendelea kwa ajili ya mashindano ya kumuenzi muanzilishi wa klabu ya gofu ya Lugalo Jenerali George Waitara. https://youtu.be/i279nc6Z8aA

SIMU.TV: Mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara timu ya Yanga wamejiweka katika nafasi nzuri ya kuutetea ubingwa huo baada ya kuifunga Ruvu Shooting mabao mawili kwa moja. https://youtu.be/iiyytgaXYes

majaribio ya wazi ya Azam FC (U-17) yaliyofanyika Zanzibar mwishoni mwa wikiendi iliyopita, Zoezi lijalo litafanyika Dar es Salaam Keshokutwa

$
0
0
KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, inatarajia kuendelea na mpango wake wa Kitaifa wa kusaka wachezaji chini ya umri wa miaka 17 (U-17) Jumamosi ijayo Novemba 12 mwaka huu kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 9.00 alasiri ndani ya Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Baada ya wikiendi iliyopita kufanya majaribio ya wazi visiwani Zanzibar, ambako walichaguliwa wachezaji watano, sasa tunarudisha mkazo wetu Tanzania Bara na kufanya majaribio ya mwisho katika jiji la Dar es Salaam.
Kwa majaribio mengine ya wazi katika maeneo mengine kuzunguka Tanzania yatatangazwa hivi karibuni.
 Msimamizi wa majaribio hayo akitoa maelekezo kwa mmoja ya wachezaji katika uwanja wa Amaan Zanzibar
 Wachezaji wakionesha uwezo wao katika uwanja wa Amaan Zanzibar
 Wachezaji katika uwanja wa Amaan Zanzibar.


Introducing new song "NIJUE" by Weusi ft Christian bella

Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images