Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

Kampuni ya Mbolea yaanza kusambaza Mbolea ya Ruzuku kwenda kwa Wakulima

$
0
0
Wakati msimu mpya wa kilimo ukiwa unatarajiwa kuanza, Kampuni ya Mbolea Tanzania (Tanzania Fertilizer Company – TFC) imeanza zoezi la kusambaza mbolea ya ruzuku kwenda katika mikoa inayotarajia kuanza msimu wa kilimo wa 2016/2017.

Akiongea na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali, Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mbolea Tanzania, Bwana Salum Mkumba amewataka wakulima kujiandaa kupokea mbolea ya ruzuku ambayo imeanza kusafirisha tangu jana tarehe 7/11/2016 kutoka kwenye maghala ya Kampuni hiyo yaliyopo Jijini Dar es Salaam kwenda Mikoa 20 ya Tanzania Bara.

Bwana Mkumba amesema kuwa kwa zoezi la kusambaza mbolea hiyo ya ruzuku, litahusisha kiasi cha tani 32,300 (Tani elfu thelasini na mbili na mia tatu) ambazo zinaigharimu Serikali fedha kiasi cha shilingi bilioni 12 ambapo mkulima atapaswa kununua mfuko wa mbolea ya kupandia au kukuzia wa kilo 50 kwa shilingi 30,000.

Bwana Mkumba aliongeza kuwa mbolea hiyo imeanza kupelekwa katika Mkoa wa Katavi na Mikoa minginge ya Nyanda za Juu Kusini, Mikoa hiyo matumizi ya mbolea yapo juu na kwamba zaoezi hilo litaendelea kwenda Mikoa mingine kwa kutumia usafiri wa Reli na Barabara mpaka kukamilisha zaidi ya tani 32,000 zilizokusudiwa.

Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Pembejeo, Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, Bwana Shanil Nyoni amesema, lengo la Serikali ni kuiwezesha Mikoa 20 kupata mbolea hiyo na ndivyo itakavyokuwa na kwamba Mkoa wa Katavi na Rukwa inaanza kupata mbolea hiyo kwa sababu, msimu wa kilimo unaanza hivyo itawafikia kwa wakati.

Bwana Shanil ameongeza kuwa lengo la Serikali ni kuwasaidia wakulima wasio na uwezo wa kumudu kununua mbolea na kwa utaratibu unaanza kwa kuwatambua wakulima kuanzia katika  ngazi ya Kijiji wenye sifa ya ukaazi wa eneo hilo, mwenye eneo la kulimia mahindi kuanzia ekari moja, na awe mkulima aliyetayari kupokea utaalam wa matumizi ya pembejeo hizo, ikiwemo mbolea na mbegu bora na awe tayari kuchangia gharama kidogo na kuongeza kuwa kwa kuanzia mpango huu umelenga kuwafikia wakulima laki tatu.

Aidha Bwana Nyoni amewataka wakulima kuondoa hofu ya kuwa mbolea hizo zinadumaza mazao na badala yake zinaongeza tija na uzalishaji kwa kuwa zimefanyiwa utafiti kabla ya kuwafikia wakulima kulingana na udongo na aina ya mazao.  

 Mkurungezi Msaidizi wa Pembejeo za Kilimo Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvvi Bwana Shanil Nyoni akizungumza na Waandishi wa Habari 

 Meneja Mkuu wa Kampuni  ya Mbolea Tanzania Bwana Salum Mkumba akisema jambo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari.

Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Mbolea  Tanzania (TFC) wakipakia mifuko ya mbolea ya ruzuku tayari kwa kusafirishwa


AZAM TV NA BBC SWAHILI WAONGEA NA WATANZANIA WASHINGTON, DC KUHUSU UCHAGUZI WA MAREKANI

$
0
0
Mtagazaji wa BBC Swahili Zuhra Yunus (kushoto) akifanya mahojiano na mkazi wa DMV Asha Hariz Siku ya Jumanne Novemba 8, 2016 ya uchaguzi wa rais wa Marekani katika mgahawa wa Swahili Village.
 Kulia ni Mtangazaji wa luniga wa Azam Tv Charles Hillary akifanya mahojiano na Iddi Ligongo (kushoto) na Mzee Boaz siku ya Jumanne Novemba 8, 2016 ya uchaguzi wa rais wa Marekani katika mgahawa wa Swahili Village.
Kutoka kushoto ni Nambai mkazi wa DMV akifanyiwa mahojiano na mtangazaji wa siku nyingi ambaye kwa sasa yupo Azam TV Charles Hillary (kulia) siku ya Jumanne Novemba 8, 2016 ya uchaguzi wa rais wa Marekani katika Studio za Kilimanjaro zilizopo Beltsville, Maryland, Kati ni Mtagazaji aliyobobea na maswala ua utangazaji na DMV Mubelwa Bandio.
 aliyobobea na maswala ua utangazaji na DMV Mubelwa Bandio.
 Kushoto ni Mashaka akipata picha na John Mbele
 kushoto ni Dotto Haruba mkazi wa DMV Alawi akifanyiwa mahojiano na mtangazaji wa siku nyingi ambaye kwa sasa yupo Azam TV Charles Hillary (kulia) siku ya Jumanne Novemba 8, 2016 ya uchaguzi wa rais wa Marekani katika Studio za Kilimanjaro zilizopo Beltsville, Maryland, Kati ni Mtagazaji aliyobobea na maswala ua utangazaji na DMV Mubelwa Bandio.



Zifahamu Sifa za kuwa Mpiga Kura

$
0
0
 Mwanasheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  Bi. Fausta Mahenge akitoa Elimu ya Mpiga Kura kwa wananchi wa Shule ya Sekondari ya Kidinda ya mjini Bariadi mkoani Simiyu.
Afisa Uchaguzi wa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw.  Stephen Elisante akiwaonesha wananchi wa Shule ya Sekondari ya Kidinda iliyopo mjini Bariadi mkoani Simuyu. 


WIMBO MPYA WA KABAGO AKIWA NA HARDMAD-TANZANIA WATOKA RASMI.

$
0
0
Mkongwe wa Hip Hop nchini Kabago ameachia rasmi hii leo wimbo wake uitwao Tanzania akiwa na mkongwe mwenzake Hardmad, wimbo unaitwa Tanzania. Kupitia BMG sikiliza wimbo huo maana ni wimbo bora.
Bonyeza HAPA Kuupakua au bonyeza Play hapo chini kusikiliza.

WABUNGE WASAINI MAAZIMIO YA TB CAUCUS YA KUTOKOMEZA KIFUA KIKUU

$
0
0
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akisaini Maazimio ya Wabunge wa Tanzania yenye dhamira ya kutokomeza ugonjwa wa kifua kikuu" TB Caucus ",mtandao huo ulianzishwa jijini Barcelona,Hispania Oktoba 2014 na kuitwa Mtandao wa Wabunge duniani "The Global TB Caucus
 Mjumbe wa Mtandao wa wabunge duniani,Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akisaini maazimio hayo
 Mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii, Mhe. Peter Serukamba akisaini maazimio hayo ya wabunge wa Tanzania.nchini Tanzania takribani wagonjwa 160,000 huugua kifua kikuu  kila mwaka.

 Naibu Mratibu wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua kikuu na ukoma Dkt. Liberate Mleoh akijibu maswali yaliyoulizwa na waheshimiwa wabunge wakati wa semina ya wabunge kuhusu kifua kikuu iliyofanyika kwenye ukumbi wa wabunge jijini Dodoma.
Afisa mpango  toka mpango wa taifa wa kudhibiti kifua kikuu na ukoma Dkt.  Deus Kamala akijibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na wabunge.
(Picha zote na Catherine Sungura-Dodoma)
Kupata hotuba ya Mhe Ummy Mwalimu BOFYA HAPA

WIKI YA NENDA KWA USALAMA YAZINDULIWA DARES SALAAM/ARUSHA

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mhe. Gabriel Daqarro(kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Vodacom Tanzania kanda ya kaskazini Bw. Henry Tzamburakis cheti cha kutambua mchango mkubwa wa udhamini unaotolewa na kampuni hiyo  katika kuadhimisha wiki ya  Usalama barabarani jijini Arusha.

Baadhi ya Askari wa Usalama Barabarani wakitazama bidhaa za Vodacom katika  banda la Vodacom Tanzania kwenye wiki ya Usalama barabarabani inayoadhimishwa jijini Arusha.
 Mgeni rasmi, Mkuu wa Wilayaya Temeke jijini Dar es Salaam Mhe. Felix Lyaviva akisalimiana na makamanda wa polisi, Uhamiaji, Magereza, Zimamoto, viongozi wa dini na wajumbe wa Baraza la Usalama Barabarani mkoa wa Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama katika viwanja vya Mwembe Yanga.

 Kamanda wa polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Temeke, (RTO) ASP Solomon Mwangamilo akitoa maelekezo.
 Wanafunzi  wa sekondari wakishiriki maandamano ya ufunguzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke.




MAGAZETI YA LEO JUMATANO NOVEMBA 9, 2016

PMAYA 2016 AWARDS LAUNCHED, NON MEMBERS TO ALSO PARTICIPATE

$
0
0
THE Confederation of Tanzania Industries (CTI) in partnership with Bank M launched the President’s Manufacturer of the Year Awards (PMAYA) 2016 competition in Dar es Salaam yesterday and invited for the first time ever, non-members to also participate.

While announcing this year’s competition, the CTI Executive Director Mr. Leodegar Tenga said that CTI, in order to accommodate the advice given by its Patron the  President of the United Republic of Tanzania H E John Pombe Magufuli, during the last PMAYA, has decided to widen participation by allowing non-members to participate in the competition.“It’s our belief that inviting non- members to participate in this year’s PMAYA competition will increase the number of participants and make the contest more competitive” he said.
“The Confederation of Tanzania Industries (CTI) Executive Director Leodegar Tenga giving a brief to the press yesterday in Dsm during the launch of President’s Manufacturer of the year awards 2016 (PMAYA) which is organized by CTI in partnership with Bank M. He is flanked by ISHARA Consulting Director Mr. Isaac Saburi (left), Bank M’s CEO-Designate Ms.Jacqueline Woiso and GIZ Energy program manager Mr. Sven Emadel."

PMAYA competition is an annual event organised by CTI to award outstanding industries of the preceding year. The awards were first presented to the winners in 2005 when CTI organised the first ever Competition among its members countrywide. 

This year’ Competition has been improved by including Energy Efficiency Award. The award will also act as an opportunity to publicise the industrial energy efficiency actions across the country. CTI, DANIDA and GIZ are actively involved in promoting energy management and efficiency in industries  e.g energy audits in industries recently done throughout Tanzania.
“GIZ Energy program manager Mr. Sven Emadel speaking during the launch of President’s Manufacturer of the year awards 2016 (PMAYA). Others from his right are Bank M’s CEO-Designate Ms.Jacqueline Woiso, CTI Executive Director Leodegar Tenga and ISHARA Consulting Director Mr. Isaac Saburi.

READ MORE HERE

TAKE ADVANTAGE OF OPPORTUNITIES IN THE REGION – EALA SPEAKER TELLS OBONGI RESIDENTS

$
0
0
Speaker of EALA, Rt Hon Daniel F. Kidega yesterday challenged residents of Obongi County, Moyo District in Northern Uganda to take advantage of the integration process and tap in to available opportunities. Addressing residents at the Obongi Day Festivities 2016 at the Obongi Primary School grounds, the Speaker said the evolution of the Common market agenda would be meaningful for so long as EAC citizens embraced the transformation agenda.

“The transformation agenda must start from oneself,” he said.  We must change our individual mindsets initially, if we are to fully embrace and appreciate integration”, he added.

The Speaker who was the chief guest at the occasion anchored on the theme: Connecting Obongi to Arusha through Good Roads, Rail and Internet connections, called on the Obongi inhabitants to enhance productivity by trading in their commodities as a way of fully engaging in the free market.
 
The Speaker of EALA, Rt Hon Daniel F. Kidega (left) is received by the Obongi County MP, Hon Kaps Fungaroo Hassan to the celebrations

He informed participants that the EAC was committed to enhancing inter-connectivity by improving infrastructure. “The EAC road and rail network as well as enhancement in ICTs will play a key role in opening up the region”, the EALA Speaker said.

“It is important for authorities in Obongi to see how to open up the hinterland to the main region would benefit from the inter-connectivity of infrastructure”, he added.Rt Hon Kidega hailed the Government for ensuring peace and stability in Northern Uganda and said it was a pre-requisite for development.

The Leader of Official Opposition in Parliament, Hon Winifred Kiiza, called for enhancement of infrastructure and said all regions, devoid of their affiliations, were deserving.  “All citizens of Uganda pay taxes and Government of the day must ensure the services are equally distributed”, Hon Kiiza said.
 
The boat race commemorating the Obongi Day Festivities 2016

The Minister for Information Communication Technology, Hon Richard Tumwebaze said Government would expand and improve infrastructure for mobile telephony. He said Government would honour the pledges of President Yoweri Kaguta Museveni on enhancing infrastructure in the area.

He remarked that NRM Government would ensure equal services are rendered to all citizens.  The Minister of State for East African Community Affairs, Hon Julius Wandera Maganda said the location of Moyo district and the West Nile generally was strategic and it would open up the entire region.  He pledged to ensure the Ministry for EAC Affairs undertakes sensitization in the area.

The Party Leader of the Forum for Democratic Change (FDC), Major Gen Mugisha Muntu urged the EAC region to ensure peace and security prevails.  
 
the Band leads the celebrations of the day.

“Conflict is costly. We have all seen what is happening in the neighbouring countries of South Sudan, Burundi and the Democratic Republic of Congo. It is important for us to build strong institutions and adhere to the fully commiting to democracy”, he said.  On his part, the Deputy Secretary General of NRM, Richard Todwong rallied the region to stay united so as to ensure progress is realized.

The Member of Parliament of Obongi County and host, Hon Kaps Fungaroo, Hassan said the region needed better infrastructure and appealed to Government to provide the essential services to the people.   He challenged Government authorities to rehabilitate and upgrade the Lomuunga Airstrip to enable the aviation industry to link the County to other parts of the country and the region.  The legislator also called for faster internet connectivity to the region and installation of electricity for faster development.

A number of activities were held during that climaxed in the celebrations.  The activities included key workshops, sporting activities and cultural events.

Waombolezaji wajitokeza kwa wingi kuomboleza msiba wa marehemu Samwel Sitta, mwili kuwasili Alhamisi

$
0
0

Waombolezaji na viongozi mbalimbali wameendelea kujitokeza kutoa salam za pole kwa familia ya aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samweli Sitta aliyefariki ujerumani juzi kwa Maradhi ya Tezi Dume.
Msemaji wa familia, Bw. Gerlad Mongella amesema mwili wa marehemu unatarajiwa kuwasili Dar es salaam siku ya Alhamisi majira ya saa nane na kupelekwa nyumbani. Siku ya ujumaa mwili wa marehemu utaagwa kuanzia majira ya saa tatu hadi saa sita katika viwanja vya Karimjee, kabla ya kuelekea mkoani Dodoma kwa ajili kuagwa rasmi na waheshimiwa wabunge.

Bw. Mongella amesema kuwa ratiba ikienda kama wanavyotarajia, mazishi ya kiongozi huyo yatafanyika siku ya Jumamosi huko nyumbani kwake Urambo mkoani Tabora.

Amesema wanafamilia wanashukuru ndugu jamaa na marafiki  kwa kuendelea kwao kufika hapo nyumbani na kuwafariji katika kipindi kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.
 mmoja wa waombolezaji akiwa ameinama kwa uchungu baada ya kusaini  katika daftari la maombolezo nyumbani kwa Marehemu mtaa wa Rufiji Masaki jijini Dar es salaam leo


Waziri wa zamani Profesa Philemon Sarungi akitoa mpole kwa mtoto wa Marehemu,Agnes Sitta katika msiba wa aliykuwa spika wa zamani Samuel Sitta.

 Dkt Emmanuel Nchimbi akisaini kitabu cha Maombolezo 
 Wabunge wastaafu wakiwa kwenye maombolezo ya Marehemu Samwel Sitta
Mbunge wa Afrika Mashariki Mhe. Shyrose Banji,akimpa pole Meya wa Kinondoni Benjamini Sitta. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. paul Makonda. Picha zote na Humphrey Shao wa Globu ya Jamii.

ANGALIA UCHAGUZI WA MAREKANI LIVE

MWALIKO KWA WENYE NIA YA KUNUNUA HISA NA KUWEKEZA MTAJI KWENYE BENKI YA TWIGA/INVITATION TO EXPRESS INTEREST TO ACQUIRE SHARES AND PUT IN NEW CAPITAL INTO TWIGA BANCORP LIMITED

Wakala wa Bima ya Biashara Afrika (ATI) KUTUMIA DOLA ZA KIMAREKANI BILIONI 1.2 KUIMARISHA SEKTA YA NISHATI

$
0
0
Wakala wa Bima ya Biashara Afrika (ATI) umeitaka serikali ya Tanzania kuimarisha ushirikiano uliopo baina yake ili kuwekeza dola za Marekani bilioni 1.2 (2.6tr/-) katika sekta ya nishati utakaoongeza megawati 1,200 katika gridi ya taifa.  
Tanzania ni mmoja wa wajumbe waliasisi ATI wakala ambao ulianzishwa ili kutoa bima kwa wawekezaji pamoja na kufanya shughuli nyingine za kibiashara miongoni mwa nchi za Afrika ambazo ni wanachama. Chini ya ubia ambao ulisainiwa na Rais Mstaafu Mheshimiwa Benjamini William Mkapa mwaka 2001, Tanzania na nchi nyingine zilikubaliana kutoa upendeleo wa kupata mkopo katika miradi yote inayoungwea mkono na ATI. 
Ahadi hiyo ambayo inatoa uhakika kwa nchi mwanachama ambao utaiepusha na madai yoyote katika miradi inayoungwa mkono na ATI, kuwapatia wawekezaji, wagavi na na nafasi nyingine muhimu katika kuzindua miradi Tanzania. 
“Lengo letu ni kuisaidia Tanzania kwa kuuleta nchini uwekezaji unaohitajika sana na kupunguza gharama za kukopa. Sisi ni watu wakimya lakini ni sehemu muhimu sana ya fumbo kwa sababu tumesimama nyuma ya uwekezaji na biashara ambayo inakadiriwa kufikia dola bilioni (2tr/-) nchini Tanzania tangu kuanza kwa biashara mwaka 2004”, alibainisha Ofisa Mtendaji Mkuu wa ATI George Otieno. Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Bima ya Biashara Afrika (ATI) George Otieno akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) wakati wa mkutano maalum uliofanyika Jijini Dar es salaam kwa lengo la kuwaeleza wanatazania juu ya kinachojadiliwa katika mkutano wa jukwaa la kimataifa la sekta ya nishati ambalo likiwa na kauli “Kufungua uwekezaji kutawezesha ongezeko kubwa la Nishati Tanzania” ambalo limeitishwa na ATI mkutano ambao unafanyika Jijini Dar es salaam. Tusekile Kibonde ambaye ni Underwriter Responsible for Tanzania Kutoka ATI akieleza maswala mbalimbali mbele ya wanahabari juu ya Mkutano huo ambao unafanyika Jijini Dar es salaam ambapo Jukwaa hilo linawakutanisha pamoja wadau kutoka Nyanja binafasi za umma katika kutafuta masuluhisho ambayo yataondoa hatari zinazoikabili sekta ya nishati ili kuvutia uwekezaji unaohitajika sana.
Kamishna msaidizi wa Umeme wa wizara, mhandisi Innocent Luoga akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) wakati wa mkutano maalum uliofanyika Jijini Dar es salaam kwa lengo la kuwaeleza wanatazania juu ya kinachojadiliwa katika mkutano wa jukwaa la kimataifa la sekta ya nishati ambalo likiwa na kauli “Kufungua uwekezaji kutawezesha ongezeko kubwa la Nishati Tanzania” ambalo limeitishwa na ATI mkutano ambao unafanyika Jijini Dar es Salaam.
Viongozi wakiwa katika picha ya pamoja. Tanzania inaweza kunufaika zaidi kutokana na ubia wake na ATI kirahisi kwa kurudia utekelezaji wa ahadi zake kwa kusaidia miradi inayoungwa mkono na ATI ndani ya Tanzania. Chini ya masharti ya ubia, Tanzania inaweza kuwepo kiwango mbadala wa vipimo vya viwango kwa kipimo cha uwekezaji cha ATI daraja A mara tutakaposaini manunuzi yanayoungwa mkono na ATI.
Chini ya kanuni za Basel, ambazo zinasimamia mabenki mengi ya kimataifa, ynaweza kuikopesha nchi kama Tanzania ikiwa inaungwa mkono katika bima na taasisi kama ATI, ambayo ni taasisi inayoheshimika na inayoaminiwa na masoko ya kimataifa ya fedha. Bima ya ATI inaiwezesha benki kupunguza kiwango cha mwisho cha malipo ya bima, ambacho kwa kiwango kikubwa kinapunguza gharama za kukopa kwa Tanznaia na nchi nyingine za Afrika ambazo ni wanachama. 
Kushindwa kutumia kikamilifu fursa hii, Tanzania inaweza kukosa uwekeza wenye thamani ya mamilioni ya fedha. “ATI inaweza kuisaidia nchi kuwa inavutia kuwekeza kifedha kwa kuvutia uwekezaji zaidi. Hili ni muhimu hususani katika sekta ya nishati ambayo kwa hivi sasa ina ushindani mkubwa,” alisema Mdhamini Mkazi wa ATI nchini Tanzania Tusekile Kibonde.

TUME YA JUMUIYA YA MADOLA KUZINDUA MAKABURI MAPYA YA ASKARI WA KIHINDI TANGA WALIOKUWA KWENYE VITA YA KWANZA YA DUNIA

$
0
0
TUME ya Jumuiya ya Madola inayosimamia Makaburi ya Vita vya Kwanza vya Dunia (CWGC) inatarajiwa kuzindua hapa makaburi mapya ya askari wa Kihindi waliokufa katika vita hivyo vya kwanza vya dunia. 

Akizungumza na waandishi habari jijini Tanga jana , Ofisa ufundi wa Jumuiya hiyo, Daniel Achini, alisema uzinduzi huo utafanyika mwezi Novemba 11, 2016.Achini alisema uzinduzi huo utafanywa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo ya CWGC, Victoria Wallace ukishuhudiwa na Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cook na Balozi wa India, Sandeep Arya. 

Sherehe hizo pia zitahudhuriwa na Balozi wa Ujerumani, Egon Konchake na viongozi wa Mkoa na Halmashauri ya Jiji la Tanga.Alisema makaburi hayo mapya yapatayo 62 yamezikwa miili ya askari wa Kihindi waliokufa vitani katika eneo la Jasin kati ya Januari na Julai, 1915.Makaburi hayo yamejengwa maeneo ya Usagara na Jasin, karibu na jiji.

Kumbukumbu ya makaburi ya Wahindi na yale ya Usagara yaliyoko hapa Tanga ni sehemu tu ya makaburi mengi yanayohudumiwa na Tume hiyo ya CWGC.Ofisa huyo alieleza kuwa makumbusho ya Jasin, ulikuwa ni mji wa mbele wa kujihami katika pwani ya kaskazini ya mji wa Tanga na ambao ulichukuliwa na Wajerumani mwezi Januari, 1915. 

Alisema vikosi vya Jind na Kashmiri ndivyo vilivyoulinda mji, ambao ulitekwa na kuchukuliwa tena na vikosi vya wanajeshi 2,000 wa Kijerumani tarehe 18 Januari, 1915. Makumbusho ya makaburi ya Tanga ambayo yapo katika eneo la Usagara, yanahifadhi kumbukumbu ya vifo 394 vilivyotokea katika vita vikali vilivyopiganwa katika mji wa Tanga kati 1914 na 1916 baina ya mataifa makubwa ya Uingereza na Ujerumani. 

Achini alifafanua kwamba moja ya kazi muhimu ya Tume hiyo barani Afrika ni pamoja na kutunza makaburi na kumbukumbu za vifo zaidi 190,000 vilivyotokea katika vita vya kwanza na pili vya dunia katika nchi zaidi ya 40 zilizopo Afrika.

"Nchini Tanzania, tunavikumbuka vifo zaidi ya 55,000 vilivyotokea katika vita vyote katika viwanja 12 vya makaburi", alidokeza Achini.Alitaja baadhi ya maeneo ya makaburi yanayohudumiwa na CWGC yanapatikana Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma, Iringa na Moshi Zanzibar.

Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.
Wakazi wa Usagara Tanga, Joseph Kimani, Martin Kiarie na Ali Hamis wakiangalia majina ya askari wa Uingereza na India waliouwawa Tanga wakati wa vita ya kwanza ya Dunia mwaka 1914, jumla ya askari 270 waliuwawa na majina yao kuwekwa na tume ya Jumuiya ya Madola (CWGC).
Mkazi Usagara Tanga, Joseph Kimani, akiangalia majina ya askari wa Uingereza na India waliouwawa wakati wa vita ya kwanza ya Dunia ambapo jumla ya askari 270 waliuwawa Tanga wakati wa vita hivyo vilivyopiganwa mwaka 1914.Majina hayo yamehifadhiwa na tume ya Jumuiya ya Madola (Commonwealth War Graves Cammission) (CWGC)

CCM YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA MHE. MUNGAI

$
0
0


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg. Abdulrahman Kinana amemtumia salamu za rambi rambi Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Ndg. Jesca Msambatavangu kufuatia kifo cha Mhe Joseph Mungai, Mbunge mstaafu wa Jimbo la Mufindi kilichotokea jana tarehe 08 Novemba, 2016 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.
Mhe. Mungai, ameshika nyadhifa mbalimbali za uongozi na utumishi katika Chama na Serikali. Alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Mkuu wa Mkoa, Mbunge kuanzia miaka ya 1970 hadi 2010, na amekuwa Waziri katika wizara mbalimbali za Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuanzia Awamu ya kwanza mpaka ya nne.
Mhe. Mungai, atakumbukwa na wanaCCM, na wananchi wa Mkoa wa Iringa na Tanzania kwa kuasisi na kuendeleza shamba kubwa la miti la SAOHILL na kwamba mchango wake huo tutaendelea kuuenzi na kuuthamini.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe. 
Imetolewa na:- 

Christopher Ole Sendeka (MNEC)
MSEMAJI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

MAOFISA wawili wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wapandishwa kizimbani kwa tuhuma za rushwa

$
0
0
MAOFISA wawili wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka ya kujihusisha na rushwa ya Sh milioni 25 kwa ajili ya kupanga matokeo.
Washtakiwa hao Kaimu Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Martin Chacha (picha ya juu) na Msaidizi wa Rais wa shirikisho hilo, Juma Matandika (picha ya chini), walifikishwa mahakamani hapo jana.
Walisomewa mashtaka yao na Wakili kutoka Taasaisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Leonard Swai pamoja na Wakili wa Serikali Odesa Horombe mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Wakili Horombe alidai kuwa Februari 4, mwaka huu katika ofisi za Makao Makuu ya TFF, washtakiwa hao waliomba rushwa ya Sh milioni 25 kutoka kwa Salum Kalunge na Ofisa wa Shirikisho la Soka mkoani Geita na Klabu ya Mpira wa Miguu ya Geita, Constantine Morandi.
Inadaiwa waliomba fedha hizo kwa ajili ya kuishinikiza na kuishawishi TFF na Idara ya Uhamiaji kupanga uamuzi wa matokeowa mechi ya Klabu ya Mpira wa Miguu ya Tabora ili kuisaidia klabu ya Geita Gold  iweze kupanda daraja na kucheza Ligi Kuu ya Soka Tanzania, jambo ambalo ni kinyume cha sheria za mwajiri wao.
Washtakiwa walikana mashtaka na Wakili Horombe alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kumba tarehe nyingine kwa ajili ya kuanza kusikilizwa, pia hana pingamizi na dhamana.

Washtakiwa hao waliachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili waaminifu wenye vitambulisho, waliosaini hati ya Sh milioni tano kwa kila mmoja.
Hakimu Shaidi aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 30, mwaka huu, kwa ajili ya kuanza kusikilizwa.

Taasisi ya TradeMark East Africa, itatumia mabilioni ya shilingi kuwajengea uwezo wafanyabiasha wanawake kutumia fursa za soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki

$
0
0

Mkurugenzi wa TradeMark East Africa, John Ulanga akifungua warsha ya Chama cha Wafanya Biashara, Wanawake wa Tanzania, Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCCIA) kuhusu namna ya kufanya biashara kwenye soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyohudhuriwa na wanawake wafanyabiashara wa mipakani jijini Dar es salaam
  Sehemu ya washiriki wa warsha ya Chama cha Wafanya Biashara Wanawake wa Tanzania Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCCIA)
Mkurugenzi wa TradeMark East Africa, John Ulanga, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam le, baada ya kufungua warsha ya Chama cha Wafanya Biashara, Wanawake wa Tanzania, Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCCIA) kuhusu namna ya kufanya biashara kwenye soko la Jumuiya ya Afrika, Mashariki iliyohudhuriwa na wanawake wafanyabiashara wa mipakani. Kushoto ni Mwenyekiti wa TWCCIA, Mama Jacline Mneney Maleko.
Picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa warsha hiyo

Hospitali ya Kairuki yaboresha huduma zake

$
0
0

Hospitali ya Kairuki katika kuboresha huduma zake kwa wagonjwa imeanza kutumia kitengo kipya kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wa kutwa  hususani wale wanachama wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

Kitengo hicho kipya (OPD 3)  kilichopo nyuma ya Jengo kuu la hospital mkabala na kitengo cha magonjwa ya viungo (Physiotherapy Unit) kina sehemu kubwa ya mapokezi, vyumba  mbalimbali  vikiwemo  vyumba 10 via madaktari, maabara,Duma la dawa,sehemu ya sindano na kufunga vidonda,chumba cha ultrasound,mapokezi , huduma za chanjo ya watoto (RCH),chumba cha wauguzi na duka dogo la vinywaji na vitafunwa nk.

Kitengo hicho kipya kitaiwezesha hospitali hiyo kutoa huduma kwa haraka na ufanisi zaidi kwa wagonjwa wasiopungua 120,000 kwa mwaka hivyo kupunguza kero ya  foleni na msongamano iliokuwepo siku za nyuma.


Imetolewa na Afisa 

Mahusiano, Arafa Mohamed
Wagonjwa wakisubiri kupata matibabu.
Wagonjwa wakisubiri kupata matibabu.
Vyumba vya madaktari.

BAADHI YA WABUNGE WAKICHANGIA TAARIFA YA KAMATI ZA BUNGE ZA HESABU ZA SERIKALI KUU NA SERIKALI ZA MITAA

TAASISI YA DARWIN YASAIDIA KUWATAFUTIA VIJANA 50 ELIMU YA JUU NJE YA NCHI

$
0
0
Na Dac Popo wa Globu ya Jamii
 Katika harakati za Taasisi zisizo za kiserekali za kusaidia vijana kuweza kupata elimu ili kujenga maisha yao ya baadaye, taasisi ijulikanayo kwa jina la Darwin imesaidia vijana wapatao 50 kupata nafasi katika  vyuo vya juu nje ya nchi.
 Taasisi hiyo iliyoanzishwa miezi 6 iliyopita imefanikisha kuwapatia vijana hao kupata elimu hiyo katika nchi za China, India, Malaysia, Canada na Australia. 
 Akieleza hayo katika hafla fupi ya kuwaaga baadhi ya vijana hayo kwenye uwaja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa taasisi hiyo Bw. Makungu J. Malando amesema taasisi yake ambayo inatambuliwa na T.C.U.  na inasaidia vijana kupata visa, malazi, usafiri na scholarship. 
 Naye mmoja wa wazazi ambaye mtoto wake amebahatika kupata nafasi hiyo Bw. Hamis Suleimani ameishukuru Darwin kwa kufanikisha safari hiyo kwa kijana wake na kusisitiza kuwa taasisi hiyo inaangalia zaidi ubora wa vyuo wanavyo watafutia nafasi vijana wa Tanzania.
 Mkurugenzi wa taasisi ya Darwin Bw. Makungu Joseph Malando akizungumza katika hafla ya kuwaaga vijana wanaokwenda kujiunga na vyuo vikuu nje ya nchi kwenye uwanja wa ndege jijini Dar es salaam leo.
 Mzee Hamis Suleiman ambaye ni mzazi wa mmoja wa vijana wanaokwenda kusoma katika moja ya vyuo vikuu nje ya nchi akiongea katika hafla ya kuwaaga vijana wanaokwenda kujiunga na vyuo vikuu nje ya nchi kwenye uwanja wa ndege jijini Dar es salaam leo.
Mkurugenzi wa taasisi ya Darwin Bw. Makungu Joseph Malando akiwa katika picha ya pamoja na wazazi na baadhi ya vijana wanaokwenda masomoni nje ya nchi katika hafla ya kuwaaga vijana wanaokwenda kujiunga na vyuo vikuu nje ya nchi kwenye uwanja wa ndege jijini Dar es salaam leo.picha  na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images