Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

Article 6


MAGAZETI YA LEO JUMANNE OKTOBA 8, 2016

Mbeya wahimizwa kurasimisha biashara zao

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, Mbeya
Wafanyabiashara mkoani hapa wametakiwa kuchangamkia fursa mbali mbali pamoja na kurasimisha biashara zao ili kutambuliwa  na serikali na taasisi za fedha.
Hatua hiyo, imesemekana, itawasaidia kuingia katika ushindani wa kutafuta masoko na kukua kimitaji.
 
Ushauri huo umetolewa jana wakati wa ufunguzi wa semina ya siku tano kwa wafanyabiashara mkoani Mbeya jana na Katibu Tawala mkoa wa Mbeya, Bi. Mariam Mtunguja.
 
Mafunzo hayo yanayotolewa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni  (BRELA),  yanalenga kuwajengea uwezo wa namna ya kurasimisha biashara zao na kuzisajili ili kutambuliwa na mamlaka zinazohusika.
 
“Hii ni fursa kwenu wafanyabiashara muitumie vizuri,” alisema Bi. Mtunguja.
 
Alisema wafanyabiashara katika mkoa wake wana wajibu wa kusajili biashara na kuzirasimisha ili kufanya biashara kisasa na sio kwa mtindo wanaoutumia sasa wa kufanya biashara bila kutambuliwa.
 
“Nawapongeza sana Brela kwa hatua hii, kwa kweli mmetufanyia jambo kubwa katika mkoa wetu,” aliongeza.
 
Aliwaambia wafanyabiashara hao kuwa wakishatambuliwa na taasisi za fedha na vyombo vingine ni rahisi kupiga hatua na kusisitiza kutekeleza ushauri watakaopata katika semina hiyo.
 
Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Brela, Bw. Frank Kanyusi alisema suala la kusajili jina la biashara ni la lazima kwa mujibu wa sheria.
 
“Tumeshatoa maelekezo kwa wafanyabiashara wote nchini kusajili majina ya biashara zao,” alisema Kanyusi na kusisitiza kuwa sheria kali zitachukuliwa dhidi ya wote watakaokaidi agizo hilo.  
 
Alisema serikali inapoteza mapato mengi kwa kutowatambua wafanyabiashara, hivyo ni wajibu wa kila mfanyabiashara kuisaidia serikali katika hilo.
 
Akizungumza kwa niaba ya wafanyabishara wa mkoa wa Mbeya,  Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa mkoa huo, Bw. Emile Malinza  alisifu hatua ya wakala huo.
 
“Hii ni namna ya kutujenga kifikra na ni muhimu wafanyabiashara wa Mbeya wakalitambua hili,” alisema Malinza ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa TCCIA mkoani humo.
 
Alisema mkoa wa Mbeya una wafanyabiashara wengi, lakini hawatambuliki katika mamlaka husika, na kuongeza kuwa hii ni fursa kwao kujisali na kutambuliwa.
 Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Bi.Mariam Mtunguja, (kulia)  akisindikizwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni ( Brela) Bw. Frank Kanyus, (katikati), katika Ukumbi wa mikutano wa Benjamini Mkapa, ambapo alifungua mafunzo ya siku tano kwa wafanyabiashara wa mkoa huo, mafunzo yanayotolewa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni  ( BRELA),  yanalenga kuwajengea uwezo wa namna ya kurasimisha  na kusajili biashara zao, (kushoto) ni Mkurugenzi wa Idara ya Miliki Bunifu kutoka Brela, Bi. Loy Mhando.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni ( Brela) Bw. Frank Kanyus ( kushoto) akisisitiza jambo wakati wa mafunzo ya siku tano kwa wafanyabiashara wa Mkoa Mbeya, mafunzo yanayotolewa na  BRELA, yanalenga kuwajengea uwezo wa namna ya kurasimisha  na kusajili biashara zao, (katikati) ni Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Bi.Mariam Mtunguja, (kulia) ni Mkurugenzi wa Idara ya Miliki Bunifu kutoka Brela, Bi. Loy Mhando.
Baadhi ya wafanyabiashara wa Mkoa wa Mbeya wakisikiliza kwa makini mafunzo katika ukumbi wa Benjamini Mkapa, mafunzo hayo ya siku tano yalifunguliwa na Katibu Tawala Mkoa wa huo Bi.Mariam Mtunguja,  mafunzo yanayotolewa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni  ( BRELA),  yanayolenga kuwajengea uwezo wa namna ya kurasimisha  na kusajili biashara zao

Jamii yatakiwa kushirikiana ili kuleta maendeleo yao binafsi na taifa kwa ujumla

$
0
0
Mwenyekiti wa UWASMA,Peter Thadeo akiongea na wana Kikundi kuhusiana na swala zima la kujikwamua katika lindi la  umaskini jijini Dar jana.
Katibu mkuu ,Aron Kashaija akiongea na wanakikundi kuhusu maswala mbalimbali yanayoweza kusaidia katika swala zima la kupambana na Umasikini.
Baadhi ya Wanakikundi cha UWASMA Wakiwasikiliza viongozi kujadili maswala mbalimbali ya kimaendeleo jijini Dar es salaam.
Wanakikundi cha UWASMA wakiwa katika picha ya Pamoja


Jamii imetakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano ili kutatua changamoto zinazowazunguka ili kuweza kunyanyuka kiuchumi na kunyanyua pato la Taifa.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa chama cha Umoja wa wanafunzi wa St. Matthew UWASMA,Peter Thadeo na kueleza kuwa changamoto kubwa iliyopo ni suala la umaskini ambalo linapelekea jamii kubwa kutofikia malengo yao na kushindwa kupata mahitaji muhimu.

Thadeo ameongeza kuwa lengo kubwa la kuanzisha chama hicho ni kusaidiana na kunyanyua vipato vyao kupitia uwekezaji kwenye kilimo kwa kuunganisha elimu na nguvu walizonazo.Uwekezaji katika kilimo ni njia bora ya kunyanyua na muhimili mkuu wa kupambana na umaskini.alisema thadeo.

UWASMA ni chama kilichoanzishwa na wanafunzi waliomaliza kidato cha sita katika shule ya sekondari ya st.matthew iliyoko jijini dar es salaam lengo likiwa ni kusaidiana katika masuala mbalimbali ya kiuchumi kwa kupitia uwekezaji.

VIWANJA VINAUZWA

$
0
0
Mahali Vilipo - Mbweni Jijini Dar es Salaam Sifa:- - Vimepimwa, Vina Hati ya Umiliki -Viko sehemu nzuri - Vinafaa kwa matumizi ya Makazi -Kimoja kina Sqmt 1400, Kingine Sqmt 700 Bei- Maelewano Mawasiliano - 0653 917000

MKUU WA WILAYA YA ARUSHA AZINDUA WIKI YA USALAMA BARABARANI MKOANI HUMO JANA CHINI YA VODACOM TANZANIA

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqarro(kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Vodacom Tanzania kanda ya kaskazini, Henry Tzamburakis cheti cha kutambua mchango mkubwa wa udhamini unaotolewa na kampuni hiyo katika kuadhimisha wiki ya Usalama barabarani jijini Arusha. Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro(kushoto) akipatiwa maelezo kuhusiana na chama cha msalaba mwekundu unavyofanya kazi wakati wa kuadhimisha wiki ya Usalama barabarani jijini Arusha na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania katika viwanja vya shekhe Abed Karume. Baadhi ya Askari wa Usalama Barabarani wakitazama bidhaa za Vodacom katika banda la Vodacom Tanzania kwenye wiki ya Usalama barabarabani inayoadhimishwa jijini Arusha.

PPF YAANDIKISHA MAMIA YA WAPANDA BODABODA KUWA WANACHAMA WA MFUKO HUO KUPITIA MPANGO WA WOTE SCHEME

$
0
0
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
MFUKO wa Pensheni wa PPF umeendelea na kampeni yake ya kuandikisha wanachama wapya kupitia mpango wa “Wote Scheme”, unaohusisha wafanyakazi walio katika sekta rasmi na wale waliojiajiri wenyewe ambapo katika uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama mkoani Dar es Salaam, zaidi ya waendesha bodaboda 250, kutoka wilaya ya Temeke, walijiunga na mpango huo.
Katika uzinduzi huo uliofanyika viwanja vya Mwembe-Yanga, wilayani humo Novemba 7, 2016, Mkuu wa wilaya ya Temeke, Bw. Felix Jackson Lyaviva, ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, aliwakabidhi kadi za uanachama wa Mfuko huo baadhi ya waendesha bodaboda hao.
Akizungumza baada ya zoezi hilo la kuwakabidhi kadi hizo, Meneja Uhusiano wa PPF, Bi. Lulu Mengele alisema, zoezi la kuandikisha wanachama wapya wakiwemo hao wa bodaboda, litakwenda sambamba na maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa usalama ambayo itafanyika kwenye wilaya za Ilala, na Kionondoni pia.
“Tunatoa wito kwa, wananchi wote, wakiwemo wajasiriamali, mama lishe, bodaboda, machinga, kujiunga na mpango huo ambao una faida nyingi ikiwemo kujipatia bima ya afya, mikopo ya elimu na mafao mengine mengi.” Alifafanua.
 Baadhi ya wapanda boda boda kati ya 250 waliojiunga na Mfuko wa Pnsheni wa PPF kupitia mpango wa "Wote Scheme wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, wakionyesha mfano wa kadi za kujiunga na mpango huo baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa wilaya ya Temeke, Bw. Felix Jackson Lyaviva, wakati wa uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama mkoani Dar es Salaam, Novemba 7, 2016.
 Bw. Lyaviva, akimkabidhi mfano wa kadi ya uanachama wa PPF, mpanda bodaboda, Mkemwa William Faustin.
 Bw. Lyaviva, akimkabidhi mfano wa kadi ya uanachama wa PPF, mpanda bodaboda, Lowowa Emmanuel Julius.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

UNDUGU,URAFIKI,RUSHWA VINAUA NGUMI ZA KULIPWA - BIGRIGHT

$
0
0
Na Ibrahim Kamwe "Bigright"
Hivi karibuni kumetokea na migongano ya kisheria na fitna ndani ya ngumi za kulipwa na baadhi ya wavamizi  kuitumia nafasi hiyo kuisambaratisha kama sio kuua kabisa tasnia ya ngumi za kulipwa.kwa kujaribu kufanya mapinduzi.
 Ukweli ni kuwa kwa muda mrefu sana ngumi za kulipwa hapa nchini zilikuwa zikiendeshwa na kuongozwa na  makampuni hasa PST na TPBO huku TPBC nayo ikijikokota kwa nyuma yao likisimamia jina bila kuwa na mapambano mengi ya kueleweka. 
Huku mapambano yote makubwa na ya ubingwa  yakisimamiwa na makampuni hayo na mawaziri  wenye dhamana husika wakiwa ndio wageni rasmi na kutoa michango yao, kwa TPBO au PST au TPBC ltd, sasa iweje leo hawakubaliki? Kusoma zaidi BOFYA HAPA

KABAGO, MKONGWE KWENYE MUZIKI WA KUCHANA NCHINI KUACHIA WIMBO MPYA

$
0
0
Kupitia vyombo mbalimbali vya redio, kesho jumatano Novemba 09, 2016 mkongwe wa muziki wa kuchana nchini, Filbert Kabago "Kabago", ataachia wimbo wake mpya uitwao Tanzania akiwa amemshirikisha Hardmad

Kabago anatambulika kama mmoja wa watu waliowezesha hiphop nchini kusonga mbele tangu akiwa mkoani Arusha na hata alipohamia Mwanza, akiwa kama msanii na mtangazaji wa redio (kwa sasa Passion Fm Mwanza).
Atakumbukwa namna alivyosaidia kwenye harakati za kimaendeleo Jijini Mwanza kupitia kazi zake za muziki na hata namna wimbo wa tatizo la umeme ulivyoleta nafuu kwa wakazi wa Jiji la Mwanza.
Kama hiyo haitoshi, mchango wake redioni ni mkubwa kwa wasanii mbalimbali hususani wanaochipukia ambapo wengi wao ambao sasa ni wanavuma akiwemo Baraka Da Prince na Young Killer, wamepitia mikononi mwake. 
Kaa tayari kuusubiri wimbo wa Kabago uitwao Tanzania ambao umetengenezwa kwenye studio yake iitwayo K-Records chini ya produza Sam Music.

MFUMUKO WA BEI WA TAIFA KWA MWEZI OKTOBA 2016, UMEBAKI KUWA ASILIMIA 4.5

$
0
0
Na Dotto Mwaibale
MFUMUKO wa bei wa Taifa kwa mwezi Oktoba, 2016 umebaki kuwa ni asilimia 4.5 kama ilivyo mwezi Septemba 2016.
Hayo yamebainishwa na Meneja wa Takwimu za Ajira na Bei wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Ruth Minja wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo.
"Hii inaamanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2016 imekuwa sawa na kasi ya upandaji wa bei ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba 2016" alisema Minja.
Minja alisema fahirisi za bei zimeongeza hadi 103.17 mwezi Oktoba, 2016 kutoka 98.72 mwezi Oktoba 2015 ambapo mfumuko wa bei za bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Oktoba 2016 umebaki kuwa asilimia 6.0 kama ilivyokuwa mwezi Septemba 2016.
Alisema mfumuko wa bei wa mwezi Oktoba umechangiwa na kuongezeka kwa kasi ya bei za bidhaa za vyakula na zisizi za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Oktoba 2016 zikilinganishwa na bei za mwezi Oktoba 2015.
Akizungumzia uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia shilingi 96 na senti 92 mwezi Oktoba 2016 ikilinganishwa na shilingi 97 na senti 04 ilivyokuwa mwezi Septemba 2015.
Aidha akizungumzia hali ya mfumuko wa bei kwa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki alisema nchini Kenya mfumuko wa bei wa mwezi Oktoba 2016 umeongezeka kidogo hadi asilimia 6.47 kutoka asilimia 6.34 mwezi Septemba 2016.
Alisema nchini Uganda mfumuko wa bei wa mwezi Oktoba 2016 umepungua hadi asilimia 4.1 kutoka asilimia 4.2 mwezi Septemba 2016.
 Meneja wa Takwimu za Ajira na Bei wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Ruth Minja (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwa ke Dar es Salaam leo, wakati akitoa taarifa kuhusu mfumuko wa bei wa taifa wa mwezi Oktoba 2016. Kushoto ni Mtakwimu, Philbert Mrema.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

TANESCO YATOA TAARIFA KUFAFANUA KUHUSU BEI YA UMEME

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, 
(TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

YALIYOJIRI BUNGENI MJINI DODOMA LEO November 8, 2016.

$
0
0


SIMU.tv: Ni lini serikali itaanza ujenzi wa barabra ya kilimita 10 ndani ya mji wa Nzega? Swali kutoka kwa mbunge wa Nzega Mhe. Bashe. https://youtu.be/W_4h6Lwn_3c

SIMU.tv: Kwanini serikali ya  jamhuri China isichangie gharama za matibabu kwa wananchi wanaopata ajali za bodaboda? Haya majibu ya serikali; https://youtu.be/2IQQaxie1hk

SIMU.tv: Je,serikali imeandaa utaratibu gani wa kukagua watoto wa umri chini ya miaka 5 ili kufahamu kama wamekeketwa? Haya hapa majibu ya serikali. https://youtu.be/5Aq-auXFpeU

SIMU.tv: Serikali yatolea ufafanuzi kuhusu wachimbaji wadogo wa dhahabu jimbo la Mbongwe kupewa maeneo ya kuchimba. https://youtu.be/aMXU-GjpOqU

SIMU.tv: Je,serikali imefikia hatua gani kuhusu kuwatafutia soko wakulima wa mazao mbalimbali nchini? Hapa waziri Charles Mwijage anafafanua. https://youtu.be/FhCQ-QU4Fns

SIMU.tv: Je, serikali ina mpango gani wa kuhalalisha viwanda vya kutengeneza kinywaji cha Gongo ili kuchochea uchumi wa kati? Haya hapa majibu. https://youtu.be/TzosIy7YMrI

SIMU.tv: Je, ni nini umuhimu wa kuwa na mabaraza ya ardhi nchini? Hapa naibu waziri wizara ya ardhi Mhe. Mabula anatoa ufafanuzi; https://youtu.be/gNPkuCYpXGg

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AHUDHURIA MSIBA WA NAIBU KATIBU MKUU MSTAAFU WA CCM ZANZIBAR

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa pole mke wa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Zanzibar, Marehemu Ferouz Bi. Shara Ferouz nyumbani kwake Mtaa wa Mbweni Zanzibar.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amejumuika kwenye na ndugu na jamaa msibani kwa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Zanzibar, Marehemu Salehe Ramadhan Ferouz nyumbani kwake Mtaa wa Mbweni
Zanzibar.

Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Zanzibar, Marehemu Salehe Ramadhan Ferouz likitolewa nyumbani kwake Mtaa wa Mbweni Zanzibar tayari kwenda kuswaliwa.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA TAREHE 08.11.2016 - ASKARI WAWILI MBARONI KWA KUDHLILISHA WANAFUNZI WA KIKE

$
0
0
Mnamo tarehe 04.11.2016 majira ya saa 23:30 usiku huko katika Shule ya Sekondari Isuto iliyopo Kijiji na Kata ya Isuto, Tarafa ya Isangati, Wilaya ya Kipolisi Mbalizi, Mkoa wa Mbeya, askari wawili wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya waliofahamika kwa majina ya 1. H.4925 PC PETROOSCAR MAGANA wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Mbeya na 2. J.1422 PC LUKASJOSEPH NG’WEINA wa Wilaya ya Kipolisi Mbalizi walituhumiwa kuwafanyia vitendo vibaya kinyume na maadili wanafunzi wa kike wa kidato cha nne wa Shule hiyo. 
Inadaiwa kuwa, askari hao kwa pamoja wakiwa kwenye ulinzi wa mitihani ya kitaifa ya kidato cha nne 2016 waliwatoa kwenye Hostel wanafunzi wa kike kwa kile walichodai kupiga kelele. 
Baada ya kuwatoa wanafunzi hao, waliwapeleka eneo la kufoleni na kuanza kuwapa adhabu mbalimbali ambazo ni kupiga push up, kuruka kichura, kushika masikio na kuwachapa viboko sehemu za makalio vitendo vilivyowasababishia maumivu makali na kupelekea baadhi ya wanafunzi hao wa kike kuondoa na kuelekea nyumbani kwao. 

Kufuatia vitendo hivyo, Mkuu wa Shule hiyo aitwaye ROSE MZEE DIHEMBE alitoa taarifa kwa uongozi wa Wilaya ambapo taarifa zilifika kwa uongozi wa Mkoa ambao mara moja walifika eneo la tukio na kuchukua hatua za awali ikiwemo kusikiliza malalamikio hayo ya tukio na kuwaondoa askari waliolalamikiwa na mwisho kuchukua hatua za kinidhamu zilizopelekea kufukuzwa kazi askari hao. 
Hata hivyo, kutokana na vitendo walivyovifanya askari hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika.  
WITO: 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishna wa Polisi DHAHIRI A. KIDAVASHARI anatoa wito wananchi waendelee kuliamini Jeshi la Polisi kwamba halitafumbia macho vitendo vya askari vinavyokwenda kinyume na maadili ya kazi yao. Pia vitendo vinavyokwenda kinyume na sheria za nchi. Aidha Kamanda KIDAVASHARI anaomba wananchi kuendelea kutoa taarifa ya vitendo vyote vya uhalifu vinavyotendwa bila kujali vinatendwa na askari au wananchi wa kawaida ili hatua kali za kisheria ziweze kuchukuliwa. 

Imesainiwa na:

[DHAHIRI A. KIDAVASHARI - DCP]


KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


MKUU WA MKOA WA DODOMA MHE. JORDAN RUGIMBANA AKUTANA NA BALOZI WA UINGEREZA NCHINI MHE. SARAH COOKE

$
0
0
Balozi wa Uingereza hapa nchini Mheshimiwa Sarah Cooke (kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana mara baada ya kumaliza mazungumzo yao mapema leo hapa mjini Dodoma, wengine ni Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Ndg. Rehema Madenge na Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Dodoma Mwl. Eliud Njogera.

BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 08.11.2016

KATIBU TAWALA MKOA WA DAR ES SALAAM, AFUNGUA MAFUNZO YA AWAMU YA TATU YA KAMPENI YA 'TUNAWEZA' JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Katibu Tawala wa Mko wa Dar es Salaam, Theresia Mbando, akizungumza wakati akifungua rasmi Mafunzo ya Kampeni ya awamu ya tatu ya 'TUNAWEZA' lenye lengo la kuondoa aina zote za Ukatili wa kijinsia dhidi ya Wanawake, yaliyofanyika leo Nov 8, 2016 kwenye Hoteli ya Jamirex iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam,leo.  Kushoto ni Mratibu wa Mafunzo hayo, Rehema Msami, kutoka Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC).
 Mratibu wa Mafunzo hayo, kutoka Kituo cha Msaada wa sheria kwa Wanawake (WLAC) Rehema Msami, akifafanua jambo kuhusu mafunzo hayo wakati wa ufunguzi huo.
 Mwanasheria wa Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake, Karilo Karilo, akizungumza kabla ya mgeni rasmi kufungua mafunzo hayo.




TANZIA: MZEE JOSEPH MUNGAI AFARIKI DUNIA, RAIS DKT MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI

$
0
0
 Aliyewahi kuwa Waziri wa elimu na Utamaduni katika Serikali ya awamu ya tatu  Mhe. Joseph Mungai (pichani), amefariki dunia leo majira ya saa 11 jioni. 

Akithibitisha taarifa hizo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Aminiel Aligaesha, alisema kuwa marehemu Mungai amefikishwa katika hospitali hiyo akiwa tayari amekwisha fariki na kwamba kwa upande wao hawajatoa matibabu yoyote zaidi ya huduma ya chumba cha kuhifadhia maiti (Mochwari)
"Ni kweli tumempokea Mungai, lakini alikuwa tayari amekwisha fariki, tunachosaidia sisi ni mochwari tu, kwahiyo kusema kuwa amefia Muhimbili siyo sahihi" Amesema Eligaesha.


Kuhusu chanzo cha kifo chake, Eligaesha amesema hadi sasa bado hakijafahamika, hadi uchunguzi utakapofanyika kwa kuwa hakufia katika hospitali hiyo. "Hatuwezi kusema nini chanzo hilo ni jukumu la familia, na pia kwa kuwa hajafia hapa hatuwezi kujua hadi postmoterm ifanyike, kwa sasa amehifadhiwa hapa" Alimalizia Eligaisha.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa Chumba cha maiti katika Hospitali hiyo ya Taifa ya Muhimbili. Habari kamili ya msiba huo zitawajia kadri zitakavyokuwa zikitufikia. Mtandao huu unatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki.  
Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina la Bwana lihimidiwe.  Mungu ilaze roho ya Marehemu mahala pema peponi, Amina



RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA MWENYEKITI WA BODI YA TANAPA JENERALI GEORGE WAITARA NA MKUU WA JKT BRIGEDIA JENERALI MICHAEL ISAMUHYO

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TANAPA 
Jenerali George Waitara alipokutana naye kwa mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Oktoba 8, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Brigedia Jenerali Michael Isamuhyo alipokutana naye kwa mazungumzo  Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Oktoba 8, 2016.Picha na IKULU.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images