Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110150 articles
Browse latest View live

TANZIA: SPIKA MSTAAFU WA BUNGE MH. SAMUEL SITTA AFARIKI DUNIA, RAIS DKT MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI

$
0
0
Taarifa iliyoigikia Globu ya Jamii asubuhi hii, inaeleza kwamba Aliyekuwa Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri Mwandamizi Mhe. Samuel Sitta amefariki dunia usiku wa kuamkia leo huko nchini Ujerumani alikokuwa katika matibabu... taarifa rasmi itawajia baadae kidogo. Globu ya Jamii inatoa Pole kwa ndugu , jamaa na marafiki wote na Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahala pema peponi" 


VOA Swahili: Zulia Jekundu S1 Ep 99: Hillary Duff, Drake, Taylor Swift, Kim Kardashian and Ciara

$
0
0
Zulia Jekundu ni kipindi cha televisheni cha kila wiki ambacho hukuletea habari mbalimbali za burudani zinazotamba. Humu utapata kujua juu ya habari za mastaa zinazogonga vichwa vya habari, kujua baadhi ya wanaosherehekea siku zao za kuzaliwa wiki husika na hata filamu 5 zilizoongoza kwa mauzo katika wiki hiyo.
KARIBU


SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

VITUKO KUTOKA UWANJA WA SOKOINE KABLA NA BAADA YA MCHEZO WA YANGA NA TANZANIA PRISON

$
0
0
Hiki ni moja ya Kituko kilichofanya na Timu Ya Kutoka Mbozi Mbeya Jina La Timu Limehifadhiwa Kituko cha Kubadilishana Jezi Uwanjani wakati mpira ukiendelea Ikiwa ni Mechi Ya Utangulizi Dhidi ya Prison "B" na Timu ya Kutoka Mbozi jina la Timu Limehifadhiwa kabla ya Mtanange wa Yanga na Prison Kuanza..
Chukuwa Yangu Nipe Yako huku kocha kulia wa Timu ya kutoka Mbozi Akiendelea na Kazi Kama Kawaida..
Kituko kingine Ni hiki Cha Marafiki Hawa Walio Kuwa wakipigana Picha mara Baada ya Mtanange wa Yanga Na Prison Kumalizika Ndipo Wadau Hawa Walijipatia Fursa Yakupata Taswira Golini Mwa Uwanja Wa Sokoine Jijini Mbeya.
Kumbu kumbu Zikiendelea Kuchukuliwa kwa Mapozi Mbalimbali ya Bi Dada aliyokuwa akipewa na Mpiga picha aliepigwa picha akimpiga picha Rafiki yake.

TAARIFA KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

$
0
0
LIGI YA WANAWAKE MCHEZO MMOJA TU
Raundi ya Pili ya Duru la Kwanza ya Ligi Kuu ya Taifa ya Wanawake itaendela kesho Jumanne kwa mchezo mmoja tu, wa Panama ya Iringa kuwa wageni wa timu ya Marsh Academy kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. 
Lakini, wakati mchezo huo Na. 5 wa Kundi B, ukifanyika michezo mingine mitano ya raundi ya pili ikiwamo mitatu ya Kundi A, imebidi iahirishwe na itapangiwa tarehe nyingine. Sababu kubwa ya kuahirishwa kwa michezo hiyo ni uwingi wa wachezaji kutoka timu zinazoshiriki ligi hiyo kujumuishwa kwenye timu ya taifa ya Wanawake – Twiga Stars. 
Kwa mujibu wa ratiba ya ligi hiyo, michezo ya Kundi B iliyoahirishwa ni kati ya Majengo Women ya Singida iliyokuwa icheza na Baobab ya Dpdoma kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida wakati mechi nyingine ni kati ya Victoria Queens ya Kegera iliyokuwa icheze na Sisters ya Kigoma – mchezo ulipangwa kufanyika Uwanja wa Katiba mjini Bukoba. 
Michezo ya Kundi A iliyoahirishwa ni kati ya Fair Play ya Tanga iliyokuwa iikaribishe Mburahati Queens ya Dar es Salaam kesho Novemba 8, 2016 kwenye Uwanja wa Mkwakwani ilihali michezo mingine iliyoahirishwa ni ya Novemba 9, ambako JKT Queens ya Dar es Salaam ilikuwa icheze na Viva Queens kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam wakati Evergreen Queens na Mlandizi zilikuwa zitumie Uwanja wa Karume, Ilala kucheza mechi yao hiyo.  
MECHI TATU ZA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA
 Zile mechi tatu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara za raundi ya Nane Duru la Kwanza, sasa zitafanyika Jumatano. 
Michezo hiyo inahusisha timu za Mwadui ya Shinyanga na Azam FC ambayo ilipewa jina la Mechi Na. 57 itachezwa Uwanja wa CCM Kambarage wakati Simba itasafiri hadi Mbeya kucheza na Tanzania Prisons katika mchezon Na. 60 Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine ilihali Young Africans ya Dar es Salaam itakuwa mwenyeji wa Ruvu Shooting Uwanja wa Uhuru jijini katika mchezo Na.59. 
Mechi zilipangiwa ratiba, lakini tarehe zake hazikupangwa (TBA). Tayari Bodi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), imewasiliana na wahusika kuhusu mabadiliko hayo. Sababu ya kuvuta nyuma michezo hiyo ni kutoa nafasi ya maandalizi ya kambi ya timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayotarajiwa kusafiri Ijumaa wiki hii kwenda Harare Zimbabwe kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa unaotarajiwa kufanyika Novemba 13, maka huu.

MUSEUM ART EXPLOSION NOVEMBER 2016

Klabu ya Azam FC yamlilia mwenyekiti wake, kuzikwa kesho makaburi ya kisutu jijini Dar es salaam

$
0
0

Uongozi wa Klabu ya Azam FC kwa masikitiko makubwa, unatangaza kifo cha mwenyekiti wake, Mzee Said Mohamed Abeid (pichani), kilichotokea alasir ya leo Novemba 7, 2016, katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam.

Mzee Said Mohamed, atakumbukwa kama mmoja wa nguzo muhimu kwenye mafanikio ya klabu ya Azam FC tangu kuanzishwa kwake miaka takribani nane iliyopita.
Chini ya uongozi wake kama mwenyekiti wa Azam FC, aliiongoza klabu hii kunyakuwa mataji mbalimbali makubwa na kwa mafanikio, ikiwemo taji la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe la Mapinduzi mara mbili pamoja na Ngao ya Jamii.

Si hivyo tu, mchango wake Mzee Said Mohamed hauku-ishia nyumbani kwake Azam FC tu, bali hata kwenye familia ya soka la Tanzania kwa ujumla wake ambapo hadi umauti unamkuta alikuwa ni makamu mwenyekiti wa bodi ya ligi kuu Tanzania bara na mjumbe wa kamati mbalimbali za shirikisho la soka Tanzania.

Sisi Azam FC, tutamkumbuka Mzee Said Mohamed kwa ucheshi wake, ukarimu na uchapakazi wake kwa ujumla.

Marehemu alizaliwa tarehe 20 Machi 1940 visiwani Zanzibar na anatarajiwa kuzikwa Jumanne ya tarehe 8 Novemba, 2016 kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam baada ya swala ya Alasir. Mwili wake utaswaliwa kwenye msikiti wa Maamour Upanga.
Mwenyezi Mungu ailaze roho yake Said Mohamed Abeid mahali pema peponi, Amiin,
Innalilah Wa-inna-ilaih Rajioun.

Nassor Idrisa,
Makamu Mwenyekiti,
Azam Football Club.

CCM YAOMBOLEZA KIFO CHA MZEE SAMWEL JOHN SITTA


BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU 07.11.2016

MKATABA WA UBIA KATI YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI NA UMOJA WA ULAYA WAWASILISHWA BUNGENI KUJADILIWA

MKURUGENZI WA CLOUDS MEDIA GROUP JOSEPH KUSAGA ATEMBELEA WCB WASAFI

Madaktari Bingwa kutoka ubeligiji wahudumia wagonjwa zaidi ya 400 wa meno na zaidi 390 wa macho

ARUSHA WAZINDUA SIKU YA USALAMA BARABARANI, TWAKIMU ZAONYESHA AJALI ZA PIKIPIKI ZINAONGEZEKA

$
0
0
  Askari wa usalama barabarani koplo Atilio Choga akiwa anatoa maelezo mafupi ya barabara zilizopo mkoani Arusha na jinsi magari yanavyoingia na kutoka  katika siku ya uzinduzi wa wiki ya usalama barabarani ilianza Jana katika viwanja vya sheikh Amri Abeid ,mbele ni mkuu wa wawilaya ya Arusha Fabian Daqarro ambapo alikuwa mgeni rasmi
 Askari polisi wa kikosi cha usalama barabarani akimuonyesha mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa wilaya ya Arusha jinsi kifaa chakupimia ulevi kwa madereva kinavyo fanya kazi.
 kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Nuru Selemani  akiwa anasoma risala
Mkuu wa wilaya ya Arusha Mhe. Fabian Daqaro katikati akiwa anaandika baadhi ya changamoto alizotajiwa.
Kwa taarifa kamili na picha zaidi BOFYA HAPA


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akutana na Kamati Tendaji ya Milade Nabii

$
0
0
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kati kati akizungumza na Ujumbe wa Kamati Tendaji ya Milade Nabii iliyofika Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar kumualika Sherehe za Maulidi ya uzawa wa Mtume Muhammad {SAW } yanayotarajiwa kufanyika Tarehe 11 Disemba.
Kushoto ya Balozi Seif ni Mwenyekiti wa Kamati Tendaji hiyo ya Milade Nabii Sheikh Sheraly Shamsi na wa kwanza kutoka kulia ni Sheikh Hamad.
Wa kwanza kutoka kushoto ni Wajumbe wa Kamati hiyo Sheikh Ali na Sheikh Kassim Haidar.
Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Milade Nabii Sheikh Sheraly Shamsi akifafanua jambo wakati Kamati yake ilipofika kwa Balozi Seif kumualika ushiriki wa sherehe za Maulidi ya Uzawa wa Mtume Muhammad (SAW). Picha na OMPR – ZNZ.

TYPF yatoa huduma ya upimaji afya kwa akina mama

$
0
0
Taasisi ya Tanzania Yemeni Professional Foundation (TYPF), Jumamosi ya Novemba 5 mwaka huu iliendesha huduma ya upimaji wa afya kwa akina mama wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa udhamini wa Ofisi ya Ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania.
Shughuli iliyopewa jina la Women’s Health Day, ilikuwa na lengo la taasisi hiyo kutoa huduma bora kwa akina mama kama sehemu ya kuangalia namna ya kusogeza huduma karibu na wananchi sambamba na kuhamasisha suala zima la upimaji wa afya ya akina mama.
Akizungumza katika shughuli hiyo ya upimaji afya kwa wanawake, Mwenyekiti wa Tanzania Yemen Professional Foundation (TYPF), Dr Ameir Binzoo, alisema huduma hiyo ya upimaji afya ilikuwa na dhamira ya kuwasaidia akina mama kufahamu afya zao.
Alisema Siku hiyo ya afya ya wanawake ilidhaminiwa na Ubalozi wa Kuwait, ikiwa ni hatua bora ya kushirikiana na wadau wa afya kuwasaidia wanawake wote wa jijini Dar es Salaam, wakiwamo wale waliohudhuria katika upimaji huo.
“Tunashukuru kwa kufanikiwa kumaliza salama tukio letu kwa sababu limefanyika vizuri na kusudio letu tulilotaka limefika kwa wahusika, wakiwamo akina mama wa jijini Dar es Salaam ambao ndio walengwa haswa.
“Tunawapongeza pia wenzetu wa Ubalozi wa Kuwait kwa kuguswa kwenye suala la afya ya wanawake hali iliyowasukuma kuingia kwenye tukio letu la kutoa huduma ya bure ya afya ya wanawake,” alisema Dr Binzoo.

Kwa mujibu wa Dr Binzoo, mbali na kuwapima wanawake hao waliohudhuria, pia walikuwa wakitoa elimu na mbinu ya kukabiliana na magonjwa ikiwamo kujiwekea utaratibu wa kupima afya zao mara kwa mara.
Mwenyekiti wa Tanzania Yemen Professional Foundation (TYPF), Dr Ameir Binzoo (kushoto) akimpatia zawadi Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Mheshimiwa Jasem Al Najem kwa udhamini wa siku ya afya ya mwanamke iliyoandaliwa na taasisi hiyo nchini na kudhaminiwa na Ubalozi wa Kuwait kwa ajili ya kuboresha afya ya mwanamke jijini Dar es Salaam.


Balozi wa Kuwait akipata picha ya pamoja na wadau wa taasisi hiyo baada ya kumalizika shughuli ya upimaji afya kwa akina mama.

Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Jasem Al Najem akipewa maelekezo aliposhiriki katika shughuli ya upimaji afya kwa wanawake jijini Dar es Salaam iliyoandaliwa na Tanzania Yemen Professional Foundation (TYPF).



DKT. POSSI AIPONGEZA UNESCO KUPUNGUA KWA UKATILI DHIDI YA ALBINO

$
0
0
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini, Zulmira Rodrigues akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Mhe. Dkt Abdallah Possi kutoa hotuba kwenye mkutano wa UNESCO unaoangalia tathmini ya watu wenye ulemavu wa ngozi uliofanyika leo katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. (Habari picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
Mwenyekiti wa Jumuiya ya watu wenye Alibinism Tanzania (TAS) Nemes Temba akitoa neno kwenye mkutano wa UNESCO unaoangalia tathmini ya watu wenye ulemavu wa ngozi uliofanyika leo katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kiongozi mkuu wa tathmini hiyo, Dkt. Nandera Mhando akiainisha mambo muhimu yaliyobainika kwenye tathmini wakati mkutano wa UNESCO unaoangalia tathmini ya watu wenye ulemavu wa ngozi uliofanyika leo katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

MAMA MWANAMWEMA SHEIN AZUNGUMZA NA WAUMINI WA DINI YA KIKRISTO PEMBA, AZINDUA ALBAM YA KWAYA YA R G C

$
0
0
 MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na Viongozi wa Dini wakati akiwasili katika ukumbi wa Chuo cha Amali Vitongoji Pemba, kuzungumza na Waumini wa Dini na kuzindua Albam la Kwaya ya R.G.C, ya Chakechake, Pemba.
 MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiangalia bidhaa zinazotengenezwa na Kikundi cha Wawanawake cha Nia Njema  cha Wete Pemba wakati wa mkutano huo na Viongozi wa Dini Kisiwani Pemba uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Amali Vitongoji
 MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akizungumza na Waumini wa Dini wa madhehebu mbalimbali ya Kikristo kisiwani Pemba wakati wa mkutano wake wa kuwashukuru kwa ushirikiano katika shughuli za maendeleo na kudumisha amani na kuwazinduliwa  Albam ya Kwaya ya Kanisa la R.G.C Chakechake, uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Amali Vitongoji Pemba. kulia Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman na Mchungaji wa Kanisha la Anglikana Zanzibar Emanuel Masoud.
 BAADHI ya Waumini wa madhehebu mbalimbali wa Dini ya Kikristo kisiwani Pemba wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar akitowa nasaha zake kwa waumini hao katika ukumbi wa Chuo cha Mafunzo ya Amali Vitongoji Pemba
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akionesha Albam ya Kwaya ya R.G.C ya Chakechake baada ya kuinduwa ikiwa na nyimbo za kuitakia Amani Zanzibar uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mafunzo ya Amali Vitongoji Pemba.(Picha zote na Othman Maulid)
Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI YAPOKEA MSAADA WA MASHINE KUBWA YA UTRASOUND YENYE UWEZO MKUBWA WA KUNG’AMUA MAGONJWA YA FIGO.

$
0
0
Hospitali ya Taifa Muhimbili imepokea msaada wa mashine kubwa na ya kisasa ya Utra Sound maalum kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wenye matatizo ya Figo. Msaada huo umetolewa na Hospitali ya Chuo Kikuu cha Haukeland cha nchini Norway ambapo pamoja na mambo mengine wameahidi kuendelea kutoa ushirikiano katika maeneo ya elimu , utafiti pamoja na vifaa tiba. 
Daktari Bingwa wa magonjwa ya Figo ambaye pia Mhadhiri kutoka MUHAS Paschal Ruggajo amesema mashine hiyo itasaidia kuchukua sampuli ya figo kwa ajili ya kugundua magonjwa ya Figo, kuweka vifaa kwenye mishipa damu kwa wagonjwa wanaoanzishiwa matibabu ya uchujaji wa damu na kugundua matatizo mbalimbali ya Figo. 
“ Kwa muda mrefu sasa tumekua na ushirikiano wa karibu kati ya Hospitali hiyo , MUHAS na MNH na wametusaidia kufundisha Madaktari sita wa Figo , wameshatoa mashine za kusafisha Figo na sasa wametupatia mashine hii kubwa ya Utra Sound kwakweli tunawashukuru kwa msaada wao.” amesema Dk. Ruggajo. 
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili , Dk . Hedwiga Swai ambaye ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba ameishukuru Hospitali hiyo ya Haukeland na kusisitiza kuwa msaada huo umekuja wakati muafaka kwakua mashine hiyo itasaidia sana katika kitengo cha Figo.
 :   Profesa Einar Svastard ( kulia)   akimkabidhi  msaada wa mashine kubwa ya kisasa ya Utrasound  Mkurugenzi wa huduma za tiba  MNH Dk. Hedwiga Swai  .

 Dk. Hedwiga Swai ( kushoto ) akimshukuru Profesa  Svastard kwa msaada walioutoa kwa niaba ya Mkurugenzi  Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru.
 Hii ndio mashine  ya  Utrasound ambayo itatumika kuchukua sampuli ya figo kwa ajili ya kugundua magonjwa  ya Figo , kuweka vifaa kwenye mishipa damu kwa wagonjwa wanaoanzishiwa matibabu ya uchujaji wa damu na kugundua matatizo mbalimbali ya Figo.

Profesa Einar Svastard akimfanyia uchunguzi mgonjwa kwa kutumia mashine hiyo 

TANZIA: HUSNA HALID KILUVIA MSHAMI AFARIKI DUNIA

$
0
0
Kwa masikitiko makubwa Captain  Denis Mshami wa wakala wa ndege za serikali anasikitika kutangaza kifo cha mke wake mpenzi HUSNA HALID KILUVIA MSHAMI (pichani) kilichotokea leo tarehe  7.11.2016.
Msiba upo nyumbani kwa Capt. Mshami huko Ukonga Kipunguni Matembele.
Habari ziwafikie ndugu jamaa na marafiki popote walipo.

Raha ya milele umpe eee Bwana 
Na mwanga wa milele umwangazie apumzike kwa amani - Amina.

Article 7

Viewing all 110150 articles
Browse latest View live




Latest Images