Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

NEWS ALERT: Salim zagar achaguliwa kuwa mwenyekiti wa klabu ya Pan African, Makamu wake Shabani Kessi Mtambo

$
0
0
 Katibu wa kamati ya uchaguzi  Bw. Peter Mushi akisoma matokeo ya uchaguzi wa uongozi wa Pan African uliosimamiwa na kamati ya uchaguzi  pembeni yake ambayo ni toka kushoto  Sunday Manara "Computer:, Mzee Chombinga, Mzee Muhidini Ndolanga na Mzee Mtulia
 Katibu kamati ya uchaguzi Bw. Peter Mushi  akifafanua jambo baada ya uchaguzi katika mkutano mkuu wa klabu ya Pan African uliofanyika hoteli ya Falcon Mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam leo.Nyuma yake kutoka kulia ni viongozi hao wapya ambao ni Salim Zagar (Mwenyekiti) Shabani Kessi Mtambo (Makamu Mwenyekiti) na wajumbe Kepteni Davis Malikita, Salum Carlos Mwinyimkuu na Mohamed Mkweche
 Sehemu ya wanachama wakiwa katika mkutano mkuu uliofanyika hoteli ya Falcon Mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam leo.
  katika mkutano mkuu uliofanyika hoteli ya Falcon Mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam leo. kwa picha zaidi BOFYA HAPA

FULL TIME: KAGERA SUGAR 2 vs 1 RUVU SHOOTING, TEMI FELIX, MANGOMA NA MBARAKA WAIPANDISHA KAGERA NAFASI YA TATU!

$
0
0
Mbaraka Yusuf alikunjuka zikiwa zimebaki dakika chache mpira kumalizika na kumchambua beki wa Ruvu Shooting na kuziona nyavu za Ruvu Rooting ambapo mpaka wakati huo Kipa hakuwepo langoni mwake. Ushindi huo wa Kagera Sugar umewapandisha juu nafasi ya tatu wakiwa na pointi 24. Ligi hii ya Vodacom sasa inaenda mapumziko ya msimu wa kwanza wa 2016/2017. Kipindi cha pili Temu Felix aliisawazishia bao Kagera Sugar na Kisha baadae Seleman Mangoma akapachika bao la pili na kufanya Kagera Sugar waongoze kwa bao 2-1 dhidi ya Timu ya Ruvu Shooting.
Seleman Mangoma Kulia baada ya kuziona nyavu za Ruvu Shooting leo
Said Dunga dakika ya 45 kipindi cha kwanza aliifungia bao RUVU SHOOTING na kwenda mapumziko wakiongoza bao 1-0 dhidi ya wenyeji Kagera Sugar. 

Waamuzi wa Mtanange  kati ya Kagera Sugar v/s  Ruvu Shooting wakati wa mapumziko wakitoka Nje ya Uwanja kwenda kwenye mapumziko ya dakika chache kujiandaa na dakika 45 za kipindi cha pili. 

MAFUNDISHO YA MCHUNGAJI DANIEL KULOLA KUONESHWA KWENYE KING'AMUZI CHA CONTINENTAL

$
0
0
Usikose kufuatilia mahubiri na mafundisho ya Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza, Dkt.Daniel Moses Kulola (kulia), kwenye runinga ya STAR RELIGION kupitia king'amuzi cha CONTINENTAL. Ni kila jumapili saa moja jioni hadi saa mbili usiku na jumanne saa tina na nusu alasiri hadi saa kumi na nusu jioni kupitia kipindi cha Mlipuko wa Injili.
Na BMG
Maandalizi ya kipindi cha Mlipuko wa Injili yakiendelea ambapo kulia ni Mchungaji Dkt.Daniel Kulola na kushoto ni mwongozaji George Binagi
Kipindi hiki hukuletea mahubiri na mafundisho ya neno la Mungu yenye mwanga bora katika maisha yako
Ungana nasi kila jumapili saa moja jioni hadi saa mbili usiku na jumanne saa tina na nusu alasiri hadi saa kumi na nusu jioni kupitia kipindi cha Mlipuko wa Injili.

KUELEKEA NOVEMBA 14 WIZARA YA AFYA ZANZIBAR YAANDAA MICHUANO YA MPIRA WA MIGUU KUADHIMISHA SIKU YA KISUKARI DUNIANI

$
0
0
Na Ramadhani Ali, Maelezo           
Waandaaji wa michuano ya maadhimisho ya siku ya kisukari Duniani kwa Zanzibar Timu ya Wizara ya Afya imeyaaga mashindano hayo katika mchezo  wa ufunguzi baada ya kufungwa na timu ya Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na watoto kwa mikwajuni ya penelti katika kiwanja cha Amani nje.
Michezo hiyo inayoshirikisha Timu  nane za Wizara za Serikali ya Mapnduzi ya Zanzibar  inachezwa kwa mtindo wa mtoano na fainali itachezwa tarehe 13 mwezi huu, siku moja kabla ya kilele cha maadhimisho hayo yanayofanyika kili ifikapo 14 Novemba, ya kila mwaka.
Timu hizo zilimaliza dakika 90 zikiwa zimefungana bao 1-1 mabao yote yakipatikana kipindi cha kwanza . Wizara ya Kazi ilipata bao lake dakika ya 26 kupitia kwa mchezaji wao Ali Seif na  Wizara ya Afya ilisawazisha kwa njia ya penelti iliychongwa na Ahmed Rashid dakika ya 35.
Muda wa penelti tano-tano ulipowadia kila timu ilipoteza mbili na hatua ya kupigiana penelti moja moja ikaendelea na ndipo wenyeji wakajikuta wanapoteza penelti yao muhimu na kuipa michuano hiyo mkono wa kwaheri kwa masikitiko.
Akizindua michuano hiyo, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Juma Malik Akili alisema lengo la maadhimisho ya siku ya kisukari duniani ni kuunga mkono jitihada za Kimataifa katika kupambana na maradhi hayo yanayoongezeka  kwa kasi duniani kote.
Alisema asilimia 3.7 ya Wazanzibari wanaugua maradhi ya kisukari na wengine wengi wako katika hatari ya kupata maradhi hayo iwapo hawatafanya juhudi za kujikinga.
Hata hivyo alisema tiba kubwa ya maradhi ya kisukari ni  watu kuweka utaratibu wa  kufanya mazoezi na kuweka utaratibu mzuri wa vyakula kwani ndiyo vinavyochangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la maradhi hayo.
Katibu Mkuu aliwashauri wafanyakazi wa Mawizara maidara taasisi za Serikali na binafsi na jamii kwa jumla kuhamasisha katika kufanya mzaoezi na kutenga wakati wa mapumziko ili kuweka mzunguruko mzuri wa damu na kupunguza uzito.
Timu zinazoshiriki michuano hiyo ni Wizara ya Afya, Wizara ya Kazi, Wizara ya Habari, Utalii Utamaduni na Michezo, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko, Wizara ya Kilimo Maliasili Uvuvi na Mifugo na Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. 
 Mratibu wa michuano ya maadhimisho ya siku ya Kisukari Duniani  Waziri Mohamed Ngwangwa akimuomba katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Juma Malik  Akili kuzikagua timu ya Wizara ya Kazi na Wizara ya Afya katika ufunguzi wa michuano hiyo inayoendelea Kiwanja cha Amani nje Mjini Zanzibar.
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Juma Malik Akili akikagua timu ya Wizara ya Kazi na Wizara ya Afya kabla ya kuanza mechi ya ufunguzi wa mashindano ya maadhimisho ya siku ya kisukari Duniani katika  kiwanja cha Amani nje.
 Kikosi cha Timu ya Wizara ya Afya Zanziabar kabla ya pambano lao la ufunguzi.
 Kikosi cha Timu ya Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Juma Malik Akili akitoa nasaha kwa wachaezaji wa timu ya Wizara ya Afya na Wizara ya Kazi  kabla ya kuanza mechi ya ufunguzi wa mashindano ya maadhimisho ya siku ya kisukari Duniani katika kiwanja cha Amani nje.
Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

KAMPENI YA BINTI WA KITAA YAFIKA WILAYA YA TEMEKE JIJINI DAR, WAKAZI WAPATA ELIMU JUU YA KUZUIA MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI.

$
0
0
 Mkazi wa Mtaa wa Mvomero Tandika Bi. Rauva Maulid akieleza namna akina baba walivyo na tabia ya kuwarubuni mabinti wenye chini ya umri wa miaka 18 na kuwababishia Mimba,na kuongeza kuwa kwa tandika watoto wengi wanapata mimba wakiwa na miaka kuanzia miaka 12.
 Mkazi wa Mtaa wa Mvomero Said Mgeni akisisitiza kuwa wazazi wanatakiwa kuwa jirani na watoto wao ili waweze kuwa rafiki na kuwaeleza matatizo wanayoyapata kwa sababu kwa kufanya hivyo mabinti watakuwa huru kueleza matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na tatizo la mimba.
 Aisha mkazi wa Tandika akieleza namna vijana wanavyowarubuni na kuwasumbua ili waweze kushiriki nao katika ngono uzembe.
 Kampeni ya Binti wa Kitaa huwakutanisha Mabinti pamoja na watu wa rika zote, hapa Msema chochote Steven Mfuko  maarufu kwa Jina la Zero akiwa na Bibi Zakia Seif akiwafunda mabinti wenye umri chini ya Miaka 18 kutokuwa na papara ya kukimbilia katika ngono.
 Mmoja ya wageni waliofika katika kampeni ya Binti wa Kitaa Jesca Kitomary alishauri kuwa wazazi wanatakiwa kuwaelimisha mabinti wao juu ya athari za mimba za utotoni  na kuolewa mapema, kwa kufanya hivyo itawasaidia kupata mimba na kuolewa kwa muda.

Mkurugenzi mtarajiwa wa Mtandao wa Fullshangweblog aendelea na safari ya kusaka nondozzzz

$
0
0
iv1
Bwana John Bukuku Mkurugenzi wa Mtandao wa Fullshangweblog na Mama Mkurugenzi wakimpongeza Mkurugenzi Mtarajiwa wa Fullshangwe Ivone John Bukuku mara baada ya kuhitimu mafunzo ya awali ngazi ya cheti kwenye chuo cha Saint Glory College Of Health and Allied Sciences jijini Dar es salaam katika ndoto yake ya Uuguzi kabla ya kuendelea na hatua nyingine ya mafunzo hayo.
iv3
Mkurugenzi John Bukuku na Mkurugenzi mtarajiwa Ivone wakipozi kwa picha.
iv4
Mkurugenzi mtarajiwa akipokea pongezi kwa simu mkurugenzi mwenza wa Fullshangwe ambaye yuko shule Kilimanjaro na hakuhudhuria mahafali ya dada yake.
iv5
Mkurugenzi mweza Diana John wa pili kutoka kulia yeye amempongeza mkubwa wake kwa hatua hiyo japo walipongezana kwa njia ya simu tu akiwa shuleni.


Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela azindua mradi wa maji kijijini Lupalama

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela amezindua mradi wa maji katika kijiji cha Lupalama kilichopo katika Tarafa ya kalenga Wilayani Iringa uliodhaminiwa na  Shirika la E.P.I.C (Everyday People Initiate Changes) la Marekani liloanzishwa na Mwanamuziki wa Marekani Tinara Moore. ambaye aliwahi kutembelea Tanzania na baadae kuamua kutoa misaada mbalimbali. 
Wanakijiji wa Lupalama kwa muda mrefu wamekuwa wakitembea umbali mrefu kutafuta maji, “Tulikuwa tukilazimika kutembea saa zima kufata maji mtoni nabado maji haya kuwa ya uhakika kwa maana kipindi cha kiangazi mto ulikuwa una kauka jambo lililopelekea kupata shida kubwa sana katika upatikanaji wa maji”  anaeleza Bi Theobadina Ngailo mkazi wa Lupalama anaongeza kuwa “Tulikuwa tunatumia hata maji ya kwenye vidimbwi ambayo sio salama kwa matumizi ya binadamu kwani muda mungine tulikuwa tukichangia maji hayo na mifugo jambo lilipolekea kulipuka kwa magonjwa kama kuhara”. 
Akizungumza wakati wa kukabidhi mradi huo Muwakilishi wa E.P.I.C Tanzania Bwana Johnson Mkini Kisinda amsema kuwa mradi huo umeghalimu pesa zaidi ya milioni therasini na tano hadi kukamilika “Hiki ni kisima cha pili kwa urefu katika visima vyote tulivyo chimba kwani Lengo lilikuwa kuchimba mita sabini tu ila tulikosa maji tukalazimika kuchimba mita mia moja na themanini kwenda chini hadi kuyafikia maji”, pia ame waasa wanakijiji wa Lupalama kuwa walinzi wa miundo mbinu hiyo ya maji kwani ni kwa faida yao wenyewe. 
Akikabidhi Mradi huo kwa wanakijiji wa lupalama mkuu wa wilaya ya Iringa amewaomba  wana kijiji hao kuusimamia vema mradi huo kwani Ofisi yake ina mpango wa kuhakikisha maji hayo yana sambazwa katika Maeneo Yote ya kijiji hicho ili kuhakikisha upatikanaji wa maji kwa wingi “Ni ndoto yangu kuona Maji haya yana wafikia wanakijiji wote wa lupalama ikibidi na maeneo ya Jirani wapate pia maji haya nitoe agizo kwa serikali ya kijiji kuunda kamati ya kusimamia na kutunza mradi huu ili uendelee kufanya kazi na kunufaisha wengi wakati mimi niki hangaika kuona jinsi gani tunapata pampu ya Umeme ikishindikana hata ya kutumia nguvu ya jua ili tusambaze maji haya sehemu nyingi zaidi”. 
Pia ameagiza Serikali ya kijiji Kuanza mara moja Mchakato wa ujenzi wa kituo cha afya kijijini hapo kwani ni kero ya muda mrefu hasa kwa akina mama kwani wana lazimika kutembea kilomita saba kufuata huduma ya afya “Nawaombeni Zoezi hili  lianze mapema sana na ikibidi kila mwanakijiji ashiriki kukusanya mawe ya ujenzi na pindi mkiwa tayali ujenzi uanze mara moja”. 
Katika hotuba yake Mkuu wa wilaya pia amehimiza watu kutunza chakula “ mvua mwaka huu sio za kuridhisha hivyo basi ipo hofu ya kukosekana chakula ni muhimu wananchi wakatunza chakula na kulima mazao yenye kuhimili ukame”

 Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela akikata utepe kuzindua mradi wa maji katika kijiji cha Lupalama kilichopo katika Tarafa ya Kalenga Wilayani Iringa. Kulia kwake ni bwana Johnson Kisinda muwakilishi wa E.P.I.C Tanzania Kushoto ni Diwania wa Lupalama.
  Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela akichota maji baada ya  kuzindua mradi  huo katika kijiji cha Lupalama kilichopo katika Tarafa ya Kalenga Wilayani Iringa
 Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela akimtiwka Bi. Theobadina Sengailo ndoo ya maji baada ya  kuzindua mradi  huo katika kijiji cha Lupalama kilichopo katika Tarafa ya Kalenga Wilayani Iringa
 Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela katika hafla ya  kuzindua mradi wa maji  katika kijiji cha Lupalama kilichopo katika Tarafa ya Kalenga Wilayani Iringa

SHIRIKISHO LA WANAFUNZI WA VYUO VYA ELIMU YA JUU WAPONGEZWA KWA KUWA NA UBUNIFU

$
0
0
 Katibu Msaidizi Mkuu wa Idara ya Utawala ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Bw. Kirumbe Ng’enda akisisitiza jambo mbele ya wanachama wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu wa Chama hicho(hawapo pichani) wakati wa Kongamano la kutathmini sekta ya elimu kwa kipindi cha siku 365 za uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli jana Jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Bw. Hamid Saleh Mhina na Katibu Msaidizi wa Shirikisho Bw. Daniel Zenda.
 Baadhi ya wanachama wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania wakichangia mada wakati wa Kongamano la kutathmini sekta ya elimu kwa kipindi cha siku 365 za uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli jana Jijini Dar es Salaam.

 Baadhi ya wanachama wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania wakichangia mada wakati wa Kongamano la kutathmini sekta ya elimu kwa kipindi cha siku 365 za uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli jana Jijini Dar es Salaam.
Kutoka kushoto ni Mtendaji wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Taifa, Bi. Deborah Charles, Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Imani Matabula na Mgeni rasmi (Mnec) Kirumbe Ng’emba wakiandika hoja zilizoibuliwa na washiriki wa Kongamano la kutathmini sekta ya elimu kwa kipindi cha siku 365 za uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli lililofanyika Jijini Dar es Salaam jana.


SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

TAARIFA KWA UMMA: BENKI YA TWIGA BANCORP LTD. KUANZA KUTOA HUDUMA NOVEMBA 8, 2016

$
0
0
Kwa mamlaka iliyopewa kisheria kupitia kifungu namba 58(2) (a) na (b) cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006, Benki Kuu inapenda kuutarifu umma kwamba zoezi la tathmini ya hali ya kifedha ya Twiga Bancorp Ltd (Twiga) limekamilika; kwa mantiki hiyo, Twiga itaanza kutoa baadhi ya huduma za kibenki kwa umma kuanzia Jumanne tarehe 8 Novemba 2016. Huduma hizo ni pamoja na ukusanyaji wa marejesho ya mikopo ya wateja. Meneja Msimamizi wa benki hiyo atawajulisha wateja huduma zitakazotolewa na taratibu za kuzingatia. 

Benki Kuu ipo katika mchakato wa kupitia na kuchambua njia mbadala za kutatua tatizo la mtaji linaloikabili Twiga Bancorp. Njia inayopewa kipaumbele ni kutafuta mtaji kutoka kwa wawekezaji wapya, mchakato utakaowahitaji kuchambua hali halisi ya taarifa za hesabu za Twiga (due diligence). Zoezi hili linatarajiwa kuchukua takribani wiki tatu na litakapokamilika, Benki Kuu itaingia makubaliano na wawekezaji wapya kuhakikisha wanaingiza mtaji unaohitajika haraka iwezekanavyo ili shughuli za kawaida za kibenki ziweze kuendelea.

Benki ya Twiga itaendelea kuwa chini ya usimamizi wa Benki Kuu hadi hapo utaratibu wa kuwamilikisha wawekezaji wapya utakapokamilika. 
Benki Kuu ya Tanzania ilitangaza kuiweka Twiga Bancorp Ltd chini ya usimamizi wake kuanzia tarehe 28 Oktoba 2016 kutoka na upungufu mkubwa wa mtaji unaoikabili.
Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuuhakikishia umma kuwa itaendelea kulinda maslahi ya wenye amana katika mabenki kwa lengo la kuleta ustahimilivu katika sekta ya fedha. 

BENKI KUU YA TANZANIA
6 Novemba, 2016

Ziara ya Mama Shein Kisiwani Pemba Kuzungumza na Wanawake wa UWT

$
0
0
 MKE wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman akitowa nasaha zake kwa Wanawake wa UWT Wilaya ya Micheweni Pemba wakati wa Mkutano wa Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, kutowa shukrani kwao
 MKE wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Muasisi wa Umoja wa Wanawake Mama Fatma Karume akizungumza wakati wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Kityuo cha Walimu Wingwi Micheweni Pemba kutowa shukrani kwa Wanawake wa Pemba.
 MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akizungumza na Wanawake wa UWT Wilaya ya Micheweni kutowa shukraza kwa kuwapigia kura Wagombea wa CCM katika Uchaguzi Mkuu uliopita, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Kituo cha Walimu Skuli ya Wingwi Micheweni.  
 MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akizungumza na Wanawake wa UWT Wilaya ya Micheweni kutowa shukraza kwa kuwapigia kura Wagombea wa CCM katika Uchaguzi Mkuu uliopita, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Kituo cha Walimu Skuli ya Wingwi Micheweni
MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akizungumza na Wanawake wa UWT Wilaya ya Micheweni kutowa shukraza kwa kuwapigia kura Wagombea wa CCM katika Uchaguzi Mkuu uliopita, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Kituo cha Walimu Skuli ya Wingwi Micheweni.(Picha zote na Othman Maulid)  

Serikali yaipongeza Kampuni ya MultiChoice Tanzania kwa kuanzisha Chaneli inayorusha Filamu zinazotumia lugha ya Kiswahili

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya MNET, Yalisa Phawe akitoa hutuba fupi katika uzinduzi huo. Kulia ni Mkuu wa Chaneli ya Maisha  Magic Bongo, Barbara Kambogi.
 Mkuu wa Chaneli ya Maisha  Magic Bongo, Barbara Kambogi akizungumza kwenye hafla ya maadhimisho ya mwaka mmoja na uzinduzi rasmi wa Chaneli hiyo iliyoambatana na uzinduzi wa filamu za Harusi, Mirindimo ya Pwani, Huba na nyingine  mapema wikiendi hii.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akipeana mkono wa pongezi na Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Innocenty Mungy (kushoto) mara baada ya kumaliza kusoma hotuba wakati wa hafla ya kusherehekea maadhimisho ya mwaka mmoja na uzinduzi rasmi wa Channel ya Maisha Magic Bongo inayopatika kupitia Dstv 160 iliyoambatana na uzinduzi wa Filamu za Harusi, Huba Mirindimo ya Pwani na n.k. Channel hii ni kwa ajili ya kuonyesha filamu na vipindi vinavyotumia rafudhi ya lugha ya Kiswahili.Katikati ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo.
 Baadhi ya wasanii wa Filamu nchini wakifuatilia maadhimisho ya mwaka mmoja wa Channel ya Maisha Magic Bongo ulionda sambamba na uzinduzi wa filamu za Harusi, Mirindimo ya Pwani, Huba na Mzooka. Kulia ni Baraka Shelukindo wa MultiChoice.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akiwaongoza baadhi ya viongozi wakati akizindua rasmi Chaneli ya Maisha Magic Bongo mapema wikiendi hii,Wa kwanza kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo na wapili ni Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Simon Mwakifamba. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

WABUNGE WAPEWA SEMINA YA EPA BUNGENI MJINI DODOMA LEO

$
0
0
                                Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Dodoma.
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamepewa semina kuhusu Mkataba wa Makubaliano ya Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Ulaya (EPA) ili wapate uelewa na hatimaye kuishauri Serikali juu ya suala hilo.
Semina hiyo imetolewa kwa Wabunge leo mjini Dodoma na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Saalam akiwemo Prof. Palamagamba Kabudi, Dkt. Ng’waza Kamata na Dkt. John Jingu pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda. 
Akifungua semina hiyo, Spika Mhe. Job Ndugai amesema kuwa anatambua umuhimu wa mkataba huo ni vema Wabunge watumie fursa ya semina hiyo ili watakapofika kwenye mjadala wenyewe ndani ya Bunge wawe na uelewa mpana kwa manufaa ya nchi.
“Natambua kwamba majadiliano haya yamefanyika sana hasa katika vikao vya Bunge lililopita, lakini kwa kuwa wabunge wengi ni wapya tumeona kuna umuhimu wa kuandaa Semina hii ili tuweze kupata elimu na kuongeza uelewa wa jambo hili kabla ya kuujadili rasmi ndani ya Bunge letu”, alisema Mhe. Ndugai.
Ameongeza kuwa semina hii pia itawapa wabunge nafasi ya kuuliza maswali na kufanya majadiliano ya jumla ili kupata ufafanuzi wa kina juu ya mambo mbalimbali yanayohusu mkataba huo, hiyo yote ikiwa ni njia ya kuwaelimisha ili siku ya majadiliano rasmi watoe mapendekezo yatakayoleta tija na manufaa kwa nchi yetu.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda alipokuwa akiwasilisha mada juu ya chimbuko, mustakabali na uchambuzi wa EPA amesema hiyo ni namna bora ya kuwashirikisha na kuwapa uelewa Wabunge ili waweze kujadili mkataba huo kwa manufaa ya taifa. 
Nao wataalam kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wamewashauri wabunge kutumia semina hiyo kama muongozo utakaowawezesha kuboresha mjadala wao wakati wa kutoa michango yao ndani ya Bunge ili waweze kutoa majibu sahihi siku ya kuujadili mkataba huo.
Mswada huo unatarajiwa kuwasililishwa Bungeni Novemba 10 mwaka huu ambapo mjadala huo utapelekea kuishauri Serikali kuhusu hatma ya mkataba huo.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge, Job Ndugai (kulia kwake) na wabunge wengine wakimsikiliza Profesa Paramgamba Kabudi, Mhadhiri  wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (kulia) wakati alipotoa mada kuhusu Mkataba wa EPA kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Novemba 6, 2016. 
Profesa Paramgamba Kabudi, Mhadhiri  wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (kulia) akiendelea kutoa  mada kuhusu Mkataba wa EPA kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Novemba 6, 2016. (Picha na Ofifi ya Waziri Mkuu)

RAIS WA ZANZIBAR AFUNGUA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KISIWANI PEMBA

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Nd,Nassor Ali Nassor Mchoraji wa ramani katika kampuni ya United Construction LTD,(katikati) wakati alipotembelea jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni leo akiwa katika ziara ya kuzindua miradi ya maendeleo katika Mikoa ya Pemba,(kushoto)Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe,Haji Omar Kheir,
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia kama ishara ya uzinduzi wa madarasa mapya ya Maandalizi katika Skuli ya Gando Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba akiwa katika ziara ya kufungua miradi mbali mbali ya Maendeleo.
 Wanafunzi wa Maandalizi wakiimba wimbo maalum wa kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein mara baada ya kuyazindua madarasa yao leo katika Skuli ya Gando Wilaya yaWete Mkoa wa Kaskazini Pemba,akiwa katika ziara ya kufungua miradi mbali mbali ya Maendeleo Kisiwani Pemba,
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe,Riziki Pembe Juma,hati maalum ya kukamilisha Ujenzi wa madarasa mapya ya Maandalizi yaliyojengwa kwa kupitia Tassaf katika Skuli ya Gando Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba leo wakati wa Uzinduzi wa Rasmi wa Madarasa hayo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba ya ufunguzi wa jengo la madarasa mapya ya Maandalizi yaliyojengwa kwa kupitia Tassaf katika Skuli ya Gando Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba leo,(kulia)  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe,Riziki Pembe Juma,na (katikati) Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mhe. Mohamed Aboud Mohamed.


SIMBA YASHINDWA KUTAMBA KWA AFRICAN LYON LEO, YACHAPWA BAO 1-0

$
0
0
 
Mshambuliaji wa Timu ya African Lyon  Omary Abdallah akiwatoka mabeki wa Timu ya Simba, Novality LUfunga na Jonas Mkude, katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa jioni ya leo katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. African Lyon imeshinda bao 1-0.

Timu ya African Lyon imefanikiwa kuondoka na alama tatu katika Uwanja wa Uhuru baada ya kuifunga Simba goli dakika ya 96 na kuweka rekodi ya kuwafunga wekundu hao wa Msimbazi toka ligi ianze.
African Lyon waliweza kucheza kwa makini na waliweza kutumiawaliitumia kwenye kipindi cha kwanza, ilizaa matunda kutokana na kuibana Simba ambayo ilionekana kushindwa kabisa kupenya safu ya ulinzi ya Lyon.

Pamoja na kujitahidi kutengeneza nafasi za mabao na kupata kona tatu kwenye kipindi cha kwanza, mashambulizi mengi ya Simba yaliishia mikononi mwa kipa Youthe Rostand wa Lyon ambaye alikuwa kikwazo kwenye mchezo huo.
Dakika nne za nyongeza kwenye mchezo huo, zilikuwa chungu kwa Simba baada ya mshambuliaji Abdallah Msuhi kuitumia vyema krosi Ya Rahidhan Hafidh na kuifungia bao Lyon ambalo limevunja rekodi ya Simba kucheza mechi 13 za ligi bila kupoteza.
Kufungwa kwa bao hilo kuliwachochea mashabiki wa Simba ambao walianza kurusha makopo ya maji uwanjani wakionyesha kutoridhishwa na mwamuzi wa pembeni Frank Komba wakidai kuwa mpigaji wa krosi alikuwa ameotea. 
 Mshambuliaji wa Timu ya African Lyon, Abdullah Msuhi akiachia shuti lililoingia moja kwa moja wavuni na kuiandikia timu yake bao la kuongoza dhidi ya Timu ya Simba, katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa jioni ya leo katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. African Lyon imeshinda bao 1-0.
 Mshambuliaji wa Timu ya African Lyon, Abdullah Msuhi akiruka juu kushandilia goli lake dhidi ya Wekundu wa Msimbazi, katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa jioni ya leo katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. African Lyon imeshinda bao 1-0.
 
Mshambuliaji wa Simba, Laudit Mavugo akiichachafya ngome ya African Lyon. 


PENATI YAWAPA USHINDI YANGA WA GOLI 1-0 DHIDI YA TANZANIA PRISON MBEYA

$
0
0
TIMU ya Yanga imefanikiwa kutoka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya askari magereza wa mkoani Mbeya Tanzania Prisons na kufikisha jumla ya alama 30 wakiwa nyuma ya alama tano dhdi ya mahasimu wao wakubwa Simba ambao wamepoteza mchezo wao wa leo. 
Mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine ulikuwa wa kasi na kila upande ukicheza kwa umakini uliweza kumaliza dakika 45 za kipindi cha kwanza huku kila timu ikiwa haijaona lango la mwenzake. 
Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kufanya mabadiliko na kuanza kulisakama lango la Tanzania Prisons lakini makosa ya washambuliaji wa timu hiyo walishindwa kutumia nafasi hizo na kukosa magoli, lakini makosa ya mabeki wa Yanga yalisabababisha Prisons kupata penati lakini uwezo wa golikipa Beno Kakolanya aliweza kuokoa mkwaju huo.
Mnamo dakika ya 74 mwamuzi wa kati Hance Mabena kutoka Tanga aliipatia Yanga penati inayopigwa na Simon Msuva na kuiandikia Yanga goli la kuongoza na mpaka dakika 90 za kumalizika kwa mchezaji huo.


Saimon Msuva Akitimuwa Vumbi kwa shuti kali wakati akipiga penati katika lango la Tanzania Prison na kuipatia yanga goli moja kwa bila katika mchezo ulio chezwa katika Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya Ikiwa ni muendelezo wa Ligi Kuu Ya Soka Vodacom Tanzania Bara.

Haruna Niyonzima wa Timu ya Yanga Akimuomba Radhi Mchezaji Mwenzie Wa Timu ya Yanga Saimon Msuva  alipokuwa Akijibizana Na Muamuzi. 
Victor Hangaya Shoto Akimpoteza Deus Kaseke.
Kutoka Shoto ni Benjamin Asukile akichuana Vikali na Mwinyi Haji katika mtanange wa Yanga na Tanzania Prison ulio chezwa Katika Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
PICHA NA MR.PENGO MAELEZO ZAINAB NYAMKA MMG.

TTCL yaichapa NSSF, kwenye mashindano ya Taasisi za Umma

$
0
0
Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) imeendelea kuonesha ubabe  kwa timu mbalimbali zinazoshiriki katika mashindano ya yanayoshirikisha Taasisi za Umma, baada ya kuichapa NSSF  kwa magoli 2-1 katika mchezo uliochezwa katika kiwanja cha TPDC, Mikocheni.  
Kutokana na matokeo hayo, TTCL inaongoza kundi B baada ya kuvuna  pointi Tisa (9), katika michezo hiyo inayochezwa kila wikiendi. 

Ushindi huo dhidi ya NSSF ulishuhudiwa  pia Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu,Waziri Kindamba aliyefika katika viwanja hivyo ili kuongeza nguvu kwa vijana wake wa TTCL. 

Mchezo ulikuwa Mkali kwa pande zote mbili, uku wakishambuliana kwa zamu, mpaka kipindi cha  kwanza kinakamilika timu zote zilikuwa bado hazijafungana. 

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi  kwa pande zote mbili, magoli ya TTCL yalifungwa na  Peter Ntwala  na Raphael Ntila, uku bao machozi la NSSF lilifungwa na Iddi Rajibu.

Nahodha  wa TTCL, Samuel Uwiso na kocha Julius Kilenga wamesema kuwa siri ya ushindi unatokana na juhudi za wachezaji kuzingatia mazoezi na maelekezo kutoka kwa viongozi wao. 

Naye, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Bw Waziri Waziri Kindamba amewapongeza wachezaji wa TTCL  kwa kazi nzuri wanayoifanya kwa kuongoza kundi B, na kuwasihi wachezaji wasibwete na matokeo hayo bali iwe chachu ya kujiandaa na michezo mingine. 


TTCL inaongoza katika kundi B, ikifuatiwa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali (NAOT) 
   Wachezaji wa TTCL na NSSF wakipeana mikono kabla ya mchezo huo kuanza, katika kiwanja cha TPDC

  Timu ya TTCl wakiwa katika picha ya pamoja

 Hatari katika lango la NSSF wakati TTCL wakipiga kona
 Walinzi wa TTCL wakithibiti mashambulizi ya NSSF

1.       Kaimu Afsa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Bw Waziri Waziri Kindamba (fulana nyeusi) akiwapongeza na wachezaji wa TTCL baada ya mechi kumalizika na ushindi wa Magoli 2 dhidi ya NSSF, katika kiwanja cha TPDC. 

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM ATEMBELEA VITUO VYA POLISI JIJINI, APANGA KUJENGA VINGINE 20

MDAU AJADILI MADA YA URAIA PACHA

MAGAZETI YA LEO JUMATATU NOVEMBA 7, 2016

Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>